Sura ya 4
Ili kuwazuia watu wote kutiwa kiburi na kujisahau baada ya mabadiliko yao kutoka kwa ubaya hadi kwa uzuri, katika sura ya maneno la mwisho la matamshi ya Mungu, mara tu Mungu akishazungumza kuhusu matakwa yake ya juu zaidi kwa watu Wake—mara tu Mungu akishawaambia watu kuhusu mapenzi Yake katika hatua hii ya mpango wa usimamizi Wake—Mungu huwapa nafasi ya kuyatafakari maneno Yake, kuwasaidia kufanya uamuzi wa kuridhisha mapenzi ya Mungu mwishowe. Wakati ambapo hali za watu ni nzuri, Mungu huanza mara moja kuwauliza watu maswali kuhusu upande mwingine wa suala. Yeye huuliza mfululizo wa maswali ambayo ni magumu kwa watu kuyaelewa: “Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu? Je, uaminifu wenu Kwangu ulikuwa safi na wa moyo wako wote? Je, ufahamu wenu kunihusu ulikuwa wa kweli? Je, Nilikuwa na nafasi kiasi gani katika nyoyo zenu?” Na kadhalika. Katika nusu ya kwanza ya aya hii, isipokuwa kemeo mbili, yaliyobaki yote ni maswali. Hasa, “Je, matamshi Yangu yamewagonga katika sehemu yenu ya udhaifu?” ni swali la kufaa sana, na lile linalogonga kweli mambo ya siri kabisa ndani ya vina vya mioyo ya watu, kuwafanya kujiuliza wenyewe bila kufahamu: Je, mimi ni mwaminifu kweli katika upendo wangu kwa Mungu? Ndani ya mioyo yao, watu hukumbuka bila kufahamu uzoefu wao wa wakati uliopita katika kuhudumu: Waliharibiwa na kujisamehe, kujidai, kujiona, majisifu, ridhaa kupita kiasi, na kiburi. Walikuwa kama samaki mkubwa aliyenaswa ndani ya wavu—na baada ya kuingia ndani ya nyavu hizi, haikuwa rahisi kwao kujinasua. Na zaidi ya hayo, walikuwa wasiozuiwa mara kwa mara, walidanganya mara kwa mara ubinadamu wa kawaida wa Mungu, na wakajithamini wenyewe katika yote waliyofanya. Kabla ya kuitwa “watendaji huduma,” walikuwa kama mtoto wa chui mkubwa mwenye milia aliyezaliwa, aliyejawa nguvu. Ingawa kwa kiasi walilenga uangalifu wao kwa uzima, wakati mwingine walifanya mambo kwa namna isiyo ya dhati; kama mtumwa, walikuwa wazembe kwa Mungu. Katika wakati wa kufichuliwa kama watendaji huduma, walikuwa wabaya, walibaki nyuma, walijawa na huzuni, walilalamika kuhusu Mungu, waliinamisha vichwa vyao kwa huzuni, na kadhalika. Kila hatua ya hadithi zao wenyewe za ajabu, na za kugusa moyo hukawia ndani ya fikira zao. Hata inakuwa vigumu kwao kulala, na wao hushinda mchana katika mzubao. Wanaonekana kwamba wameondolewa mara ya pili na Mungu, wameanguka Kuzimu, na hawana uwezo wa kutoroka. Ingawa Mungu hakufanya chochote ila kuuliza maswali machache magumu katika aya ya kwanza, soma kwa makini, yanaonyesha kwamba lengo la Mungu ni zaidi ya kuuliza tu haya maswali kwa ajili ya wao wenyewe; ndani yao kuna kiwango cha kina cha maana, kile ambacho ni lazima kielezwe kwa utondoti mkuu zaidi.
Ni kwa nini Mungu alisema wakati fulani kwamba leo, hata hivyo, ni leo, na kwa vile jana tayari imepita, hakuna wito wa kiu ya mambo yaliyozoewa, na ilihali katika sentensi ya kwanza hapa, Anawauliza watu maswali, na kuwasababisha wakumbuke wakati uliopita? Hebu fikiria: Ni kwa nini Mungu anasema kwamba watu wasiwe na kiu ya mambo yaliyozoewa kuhusu wakati uliopita, lakini pia wayakumbuke? Inawezekana kwamba kuna makosa katika maneno ya Mungu? Inawezekana kwamba asili ya maneno haya ina makosa? Kwa kawaida, wale wasiozingatia maneno ya Mungu hawangeweza kuuliza maswali ya kina kama hayo. Lakini kwa wakati huu, hakuna haja ya kulizungumzia hili. Kwanza, wacha Nieleze “kwa nini” ya hapo juu. Bila shaka, kila mtu anafahamu kwamba Mungu amesema Yeye haneni maneno matupu. Maneno yakitamkwa kutoka kinywani mwa Mungu, basi kuna lengo na umuhimu kwayo—na hili linagusa kiini cha suala. Kasoro kubwa zaidi ya watu ni kutoweza kwao kubadilisha njia zao za uovu na utatanishi wa asili yao ya zamani. Kuwakubalia watu wote kujijua kabisa na kwa uhalisi, Mungu kwanza anawaongoza kukumbuka wakati uliopita, ili waweze kufikiri juu yao wenyewe kwa kina, na hivyo waje kujua kwamba hakuna hata neno moja la Mungu lililo tupu, na kwamba maneno yote ya Mungu hutimizwa katika watu tofautitofauti kwa viwango tofautitofauti. Katika wakati uliopita, namna ambayo Mungu aliwashughulikia watu iliwapa ufahamu kidogo wa Mungu na kusababisha uaminifu wao kwa Mungu kuwa wa dhati zaidi kidogo. Neno “Mungu” linachukua asili mia 0.1 pekee ndani ya watu na mioyo yao. Kutimiza hili kunaonyesha Mungu ametekeleza kiasi kikubwa mno cha wokovu. Ni haki kusema kwamba kutimiza kwa Mungu kwa kiasi hiki katika kundi hili la watu—kundi linalonyonywa na joka kuu jekundu na kutawaliwa na Shetani—ili wasithubutu kufanya wapendavyo. Hiyo ni kwa sababu haiwezekani kwa Mungu kumiliki asilimia mia moja ya mioyo ya wale ambao wametawaliwa na Shetani. Ili kuongeza ufahamu wa watu kuhusu Mungu wakati wa hatua inayofuata, Mungu analinganisha hali za watendaji huduma wa zamani na zile za watu wa Mungu wa leo, hivyo kuunda tofauti wazi inayoongeza hisi ya watu ya aibu. Kama alivyosema tu Mungu, “hamna mahali pa kuficha aibu yenu?”
Kwa hiyo, mbona Nilisema kwamba Mungu haulizi tu maswali kwa ajili ya hayo yenyewe? Kusoma kwa makini kuanzia mwanzo hadi mwisho kunaonyesha kwamba, ingawa maswali yanayoulizwa na Mungu hayajaelezwa kabisa, yote yanahusu kiasi cha uaminifu wa watu kwa Mungu na ufahamu wa Mungu; yanahusu, kwa maneno mengine, hali halisi za watu, ambazo ni za kusikitisha, na ngumu kwao kueleza wazi kuzihusu. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba kimo cha watu ni cha kimbaombao sana, kwamba ufahamu wao wa Mungu ni wa juujuu sana, na uaminifu wao Kwake ni wa mawaa na najisi sana. Kama alivyosema Mungu, karibu watu wote hufanya mambo magumu ili kujinufaisha na wako pale tu kuongeza idadi. Mungu anaposema “Je, mnaamini kwa kweli kuwa hamjafuzu kuwa watu Wangu?” maana ya kweli ya maneno haya ni kwamba miongoni mwa watu wote, hakuna wanaofaa kuwa watu wa Mungu. Lakini ili kutimiza athari kubwa zaidi, Mungu hutumia mbinu ya kuuliza maswali. Mbinu hii ni ya kufaa zaidi kuliko maneno ya wakati uliopita, ambayo kwa kikatili yalishambulia, yakakatakata, na kuwaua watu, kiasi cha kuumiza mioyo yao. Tuseme Mungu angekuwa amesema moja kwa moja jambo la kuchosha na lisilo na ladha kama “Ninyi si waaminifu Kwangu, na uaminifu wenu ni wa mawaa, na Sishikilii mahali halisi ndani ya mioyo yenu…. Sitakuachia mahali pa wewe kujificha kutoka kwako mwenyewe, kwani hakuna kati yenu anayetosha kuwa watu Wangu.” Mnaweza kulinganisha mawili: Maudhui yake ni sawa, lakini toni ya kila moja ni tofauti. Kutumia maswali ni kwa kufaa zaidi. Hivyo, Mungu mwenye hekima anatumia toni ya kwanza, ambayo inaonyesha ustadi Anaotumia kuzungumza. Hili haliwezi kutimizwa na mwanadamu, na hivyo sio ajabu kwamba Mungu alisema, “Watu ni vyombo tu wanaotumiwa na Mimi, tofauti pekee iliyoko kati yao ni kwamba wengine ni duni, na wengine ni wa thamani.”
Endeleeni kusoma. Maneno ya Mungu huja kwa idadi kubwa na haraka, na kuwapa watu nafasi ya kupumua kwa shida, kwani Mungu hawi mwangalifu kwa mwanadamu kamwe. Watu wanapohisi majuto makubwa sana, Mungu huwaonya kwa mara nyingine: “Iwapo hutambui kabisa maswali haya, basi hii inaashiria kuwa unafanya kazi gizani, kwamba uko tu pale kuongeza idadi, na kwamba katika muda ulioamuliwa na Mimi kabla ya siku hii, kwa hakika utaangamizwa na kutupwa katika shimo lisilo na mwisho kwa mara ya pili. Haya ni maneno Yangu ya onyo, na yeyote anayeyachukulia kwa wepesi atapigwa na hukumu Yangu, na, kwa wakati ulioteuliwa atapatwa na janga.” Kuyasoma maneno hayo, watu hawawezi kufanya lolote ila kufikiria juu ya wakati ambapo walitupwa ndani ya shimo lisilo na mwisho: Kwa kutishwa na msiba mkuu, kutawaliwa na amri za usimamizi za Mungu, mwisho wao wenyewe ukiwangoja, kwa muda mrefu wakihisi kusikitishwa, wenye huzuni, wasiotulia, wasioweza kumwambia yeyote kuhusu ghamu iliyo ndani ya mioyo yao—yakilinganishwa na hili, ingekuwa heri kwao ikiwa wangeacha miili yao itakaswe…. Wakilifikiria hili, hawana la kufanya ila kuhisi kusikitishwa. Wakifikiria kuhusu vile walikuwa wakati uliopita, vile walivyo leo, na vile watakavyokuwa kesho, huzuni ndani ya mioyo yao hukua, wao huanza kutetemeka bila kufahamu, na hivyo wao huogopa zaidi amri za usimamizi za Mungu. Inavyotokea kwao kwamba neno “Watu wa Mungu” linaweza pia kuwa njia ya kuzungumza, furaha ndani ya mioyo yao hugeuka mara moja kuwa sikitiko. Mungu anatumia udhaifu wao wa mauti kuwapiga, na wakati huu, Anaanza hatua inayofuata ya kazi Yake, akisababisha hisia za uchangamfu kuzidi kuamshwa, na kuongeza hisi yao kwamba matendo ya Mungu ni yasioeleweka, kwamba Mungu hafikiki, kwamba Mungu ni mtakatifu na safi, na kwamba hawastahili kuwa sehemu ya watu wa Mungu. Kutokana na hilo, wanaongeza maradufu juhudi zao za kujiendeleza wenyewe, hawathubutu kubaki nyuma.
Linalofuata, ili kuwafunza watu funzo, na kuwafanya wajijue wenyewe, kumcha Mungu, na kumwogopa Mungu, Mungu huanza mpango Wake mpya: “Tangu wakati wa uumbaji mpaka sasa, watu wengi wamekosa kutii maneno Yangu na hivyo wametupwa nje na kutolewa katika mtiririko wa urejesho Wangu; hatimaye, miili yao inaangamia na roho zao zinatupwa kuzimu, na mpaka wa leo bado wanapitia adhabu kali. Watu wengi wameyafuata maneno Yangu, lakini wameenda kinyume na nuru na mwanga Wangu … na wengine….” Hii ni mifano halisi. Katika maneno haya, Mungu hawapi tu watu wote wa Mungu onyo halisi la kuwafanya wayajue matendo ya Mungu kotekote katika enzi, bali pia hutoa ufafanuzi usio wazi wa sehemu ya kile kinachofanyika katika ulimwengu wa kiroho. Hili linawakubalia watu kujua kwamba hakuna kizuri kinachoweza kutokana na wao kutomtii Mungu. Watakuwa alama ya milele ya aibu, na watakuwa mfano halisi wa Shetani, na nakala ya Shetani. Ndani ya moyo wa Mungu, hali hii ya maana ni ya umuhimu wa baadaye, kwani maneno haya tayari yamewaacha watu wakitetemeka na wakiwa na hasara. Uzuri wa hili ni kwamba, watu wanapotetemeka kwa woga, wao pia hupata kiasi fulani cha tondoti za ulimwengu wa kiroho—lakini kiasi fulani tu, kwa hiyo lazima Nitoe ufafanuzi kidogo. Kutoka kwa mlango wa ulimwengu wa kiroho inaweza kuonekana kwamba kuna aina zote za pepo. Wengine, hata hivyo, wako Kuzimu, wengine wako jehanamu, wengine wako katika ziwa la moto, na wengine wako ndani ya shimo lisilo na mwisho. Nina kitu fulani cha kuongeza hapa. Kuzungumza kwa kijuujuu, pepo hawa wanaweza kugawanywa kulingana na mahali; kuzungumza kwa dhahiri, hata hivyo, wengine wanashughulikiwa moja kwa moja na kuadibu kwa Mungu, na wengine wako katika kifungo cha Shetani, anayetumiwa na Mungu. Kwa dhahiri zaidi, a kwao kunatofautiana kulingana na uzito wa hali zao. Wakati huu, wacha Nieleze zaidi kidogo. Wale wanaoadhibiwa moja kwa moja kwa mkono wa Mungu hawana roho duniani, kumaanisha hawana nafasi ya kuzaliwa upya. Roho wanaomilikiwa na Shetani—maadui ambao Mungu huzungumzia Anaposema “kuwa adui Zangu”—wameunganishwa kwa mambo ya kidunia. Pepo wabaya mbalimbali walio duniani wote ni maadui wa Mungu, watumishi wa Shetani, na sababu yao ya kuwepo kwao kutoa huduma ili kuwa yenye upinzani kwa matendo ya Mungu. Hivyo, Mungu husema, “Watu hawa hawajafanywa tu wafungwa na Shetani, bali wamekuwa watenda dhambi wa milele na kuwa adui Zangu, na wananipinga moja kwa moja.” Linalofuata, Mungu huwaambia watu kuhusu mwisho wa aina hii ya pepo: “Watu wa aina hii ndio viumbe Nitakaohukumu wakati wa ghadhabu Yangu kali,” Mungu pia hubainisha hali zao za wakati huu: “leo hii wao bado ni vipofu, wakiwa bado ndani ya jela zenye giza.”
Ili kuwaonyesha watu ukweli wa maneno ya Mungu, Mungu hutumia mfano halisi kama thibitisho (suala la Paulo ambalo Anazungumzia) ili onyo Lake liweze kuacha kwa watu alama ya kina zaidi. Ili kuwakomesha watu kuchukulia kama hadithi kile kinachosemwa kuhusu Paulo, na kuwazuia kujifikiria kama watazamaji—na, zaidi ya hayo, ili kuwakomesha kwenda huku na huko wakijivunia mambo yaliyofanyika maelfu ya miaka iliyopita waliyojifunza kutoka kwa Mungu, Mungu hamakinikii matukio aliyopitia Paulo katika maisha yake yote. Badala yake, Mungu analenga juu ya matokeo na mwisho wa Paulo, sababu ambayo Paulo alimpinga Mungu, na vile Paulo aliishia kama alivyoishia. Kile ambacho Mungu analenga ni kusisitiza kanusho Lake la matumaini ya utukufu ya Paulo hapo mwisho, na kuweka wazi moja kwa moja hali yake katika uwanja wa kiroho: “Paulo anaadhibiwa moja kwa moja na Mungu.” Kwa sababu watu ni wasiosikia na hawana uwezo wa kuelewa chochote cha maneno ya Mungu, Mungu anaongeza ufafanuzi (sehemu inayofuata ya matamshi), na kuanza kuzungumza kuhusu suala la eneo lingine: “yeyote anayeniasi (na sio kuuasi tu mwili Wangu lakini la muhimu zaidi, maneno Yangu na Roho Wangu, ambayo ni kusema uungu Wangu), anapata hukumu Yangu katika mwili wake.” Ingawa, kwa kuzungumza kijuujuu, maneno haya yanaonekana kutokuwa na uhusiano na yale yaliyo hapo juu, na inaonekana hakuna uhusiano wowote kati ya hayo mawili, msiwe na hofu: Mungu ana malengo Yake mwenyewe; maneno rahisi ya “mfano ulio hapo juu yanathibitisha kwamba” yanaunganisha kimfumo masuala mawili yanayoonekana kutohusiana—ambayo ni ustadi wa maneno ya Mungu. Hivyo, watu wanapata nuru kupitia kwa maelezo ya Paulo, na kwa hiyo, kwa sababu ya uhusiano ulioko kati ya maneno halisi yaliyo hapo juu na hapa chini, ufuatiliaji wao wa kumjua Mungu huongezwa kupitia kwa somo la Paulo, ambalo hasa ni athari ambayo Mungu alitaka kutimiza katika kuyazungumza maneno hayo. Linalofuata, Mungu anazungumza maneno mengine yanayotoa usaidizi na kupata nuru kwa kuingia kwa watu katika maisha. Haina haja ya Mimi kuingia katika hilo. Mtahisi kwamba ni rahisi kuyaelewa. Kila ambacho lazima Nieleze, hata hivyo, ni wakati ambapo Mungu anasema, “Nilipofanya kazi katika ubinadamu wa kawaida, watu wengi walikuwa tayari wamejipima dhidi ya ghadhabu Yangu na uadhama Wangu, na tayari walijua kiasi kidogo kuhusu hekima na tabia Yangu. Leo hii, Ninazungumza na kutenda moja kwa moja katika uungu, na bado kuna baadhi ya watu ambao wanaona ghadhabu na hukumu Yangu kwa macho yao wenyewe; zaidi ya hayo, kazi muhimu ya sehemu ya pili ya enzi ya hukumu ni kuwafanya watu Wangu wote wajue matendo Yangu katika mwili moja kwa moja, na kuwafanya ninyi nyote mtazame tabia Yangu moja kwa moja.” Maneno haya machache yanahitimisha kazi ya Mungu katika ubinadamu wa kawaida na kuanzisha rasmi sehemu ya pili ya kazi ya Mungu ya enzi ya hukumu, inayotekelezwa katika uungu, na kutabiri mwisho wa sehemu ya watu. Wakati huu, inastahili kueleza kwamba Mungu hakuwaambia watu kwamba hii ilikuwa sehemu ya pili ya enzi ya hukumu walipokuwa watu wa Mungu. Badala yake, baada tu ya kuwaambia watu kuhusu mapenzi ya Mungu na malengo ambayo Mungu hutamani kutimiza wakati wa kipindi hiki, na kuhusu hatua ya mwisho ya Mungu ya kazi duniani ndipo Anaeleza kwamba hii ni sehemu ya pili ya enzi ya hukumu. Ni wazi kwamba, pia kuna hekima ya Mungu katika hili. Watu wakishaamka tu kutoka kwa vitanda vyao vya wagonjwa, kitu cha pekee ambacho wanajali ni kama watakufa au la, au kama ugonjwa wao unaweza kuondolewa ndani yao au la. Hawatilii maanani kama wataongeza uzito, au kama wanavalia nguo sawa. Hivyo, ni wakati tu ambapo watu wanaamini kabisa kwamba wao ni sehemu ya watu wa Mungu ndipo Mungu huzungumza juu ya matakwa Yake, hatua kwa hatua, na Huwaambia watu enzi ya leo ni gani. Hiyo ni kwa sababu watu huwa tu na nguvu za kutilia maanani hatua za usimamizi wa Mungu siku chache baada ya wao kupata nafuu, na kwa hiyo huu ni wakati wa kufaa zaidi wa kuwaambia. Ni baada tu ya watu kuelewa ndipo wanaanza kuchambua: Kwa vile hii ni sehemu ya pili ya enzi ya hukumu, matakwa ya Mungu yamekuwa makali zaidi, na Nimekuwa mmoja wa watu wa Mungu. Ni sawa kuchambua hivyo, linafikika na mwanadamu, na hivyo Mungu hutumia mbinu hii ya kuzungumza.
Mara tu watu wanapoelewa kidogo, Mungu mara tena huingia katika ufalme wa kiroho kuzungumza, na hivyo wao mara tena huingia katika uvamizi. Wakati wa mfululizo huu wa maswali, kila mtu hujikuna kichwa chake, akichanganyikiwa, asijue mapenzi ya Mungu yako wapi, asijue ni maswali gani ya Mungu atayajibu, na, aidha, asijue ni lugha gani ya kutumia kuyajibu maswali ya Mungu. Mtu hushangaa kama atacheka au atalia. Kwa watu, maneno haya yanaonekana kama kwamba yanaweza kuwa na mafumbo makubwa sana—lakini ukweli ni kinyume kabisa. Huenda hata Nikakuongezea ufafanuzi kidogo hapa- hii itaipa akili yako pumziko, na utahisi ya kuwa hiki ni kitu rahisi na hakuna haja ya kulifikiria juu yake. Kwa kweli, ingawa kuna maneno mengi, yana lengo moja tu la Mungu: kuupata uaminifu wa watu kupitia maswali haya. Lakini si la kufaa kusema hili moja kwa moja, kwa hiyo Mungu anatumia maswali mara nyingine tena. Toni, hata hivyo, ni nyororo hasa, tofauti kabisa na hapo mwanzo. Ingawa wanaulizwa maswali na Mungu, aina hii ya utofautishaji huwaletea watu kiwango fulani cha tulizo. Waweza basi ukasoma kila swali moja kwa moja; je, mambo haya hayakuwa yakitajwa mara kwa mara wakati uliopita? Kaika maswali haya machache rahisi, kuna maudhui mengi. Mengine ni maelezo ya fikira za watu: “Je, uko radhi kuyafurahia maisha hapa duniani ambayo yanafanana na yale yaliyo mbinguni?” Mengine ni “kiapo cha askari wa vita” cha watu mbele ya Mungu: “Je, kweli mna uwezo wa kujiruhusu kuuwawa na Mimi, na kuongozwa na Mimi, kama kondoo?” Na mengine ni matakwa ya Mungu kwa mwanadamu: “Kama Singezungumza moja kwa moja, je, ungewacha kila kitu kilicho karibu na wewe na ukubali kutumiwa na Mimi? Je, hii siyo hali halisi Ninayohitaji …?” Au ushawishi na uthibitisho za Mungu kwa mwanadamu: “Ilhali Ninauliza kuwa msishushwe na wasiwasi tena, kwamba muwe msitari wa mbele katika kuingia kwenu na muelewe kiini cha maneno Yangu. Hii itazuia hali ya nyinyi kutoelewa maneno Yangu, na hali ya kutokuwa na uwazi kuhusu maana Yangu, na hivyo kukiuka amri Zangu za utawala.” Hatimaye, Mungu anazungumza kuhusu matumaini yake kwa mwanadamu: “Natumaini kuwa mtaelewa Nia Yangu kwenu katika maneno Yangu. Msifikiri juu ya matarajio yenu tena, na mtende vile ambavyo mmeamua mbele Yangu kutii mipango ya Mungu katika kila kitu.” Swali la mwisho lina maana ya kina. Ni la kuchochea akili, linaathiri mioyo ya watu na ni gumu kulisahau, linalia bila kukoma kama kengele inayoning’inia karibu na masikio yao …
Yaliyo hapo juu ni maneno machache ya ufafanuzi kwa wewe kutumia kama rejeleo.