Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 114

Niliumba ulimwengu; Nilitengeneza milima, mito, na vitu vyote; Niliunda miisho ya mifumo ya sayari; Niliwaongoza wana Wangu na watu Wangu; Niliamuru vitu na mambo yote. Sasa, Nitawaongoza wana Wangu wazaliwa wa kwanza warudi kwenye Mlima Wangu Sayuni, kurudi mahali ambapo Naishi, ambayo itakuwa hatua ya mwisho katika kazi Yangu. Yote ambayo Nimeyatenda (kila kitu kilichofanyika kutoka uumbaji mpaka sasa) yalikuwa kwa sababu ya hatua ya leo ya kazi Yangu, na zaidi ni kwa sababu ya utawala wa kesho, ufalme wa kesho, na kwa ajili ya Mimi na wana Wangu wazaliwa wa kwanza kuwa na furaha ya milele. Hii imekuwa lengo Langu katika kuumba vitu vyote na itakuwa mafanikio Yangu ya mwisho ya uumbaji. Kuna kusudi katika kile Ninachosema na kufanya; kila kitu kina mpango na hakifanyiki ovyoovyo. Ingawa Ninasema kuwa na Mimi yote ni uhuru na haki ya kujiamulia la kufanya, hata hivyo kila kitu Ninachofanya ni kulingana na kanuni, yote Ninayofanya ni yamewekwa kwa msingi wa hekima na tabia Yangu. Je, mmeona chochote kuhusu hili? Kuanzia uumbaji mpaka leo, kando na wana Wangu wazaliwa wa kwanza, hawapo ambao wamenijua Mimi na hawapo ambao wameuona uso Wangu wa kweli. Upekee Nilioufanya kwa wana Wangu wazaliwa wa kwanza ni kwa sababu wao kimsingi ni sehemu ya nafsi Yangu.

Nilipouumba ulimwengu, Nilimtengeneza mwanadamu katika makundi manne ya safu kwa mujibu wa mahitaji Yangu, ambayo ni: wana Wangu, watu Wangu, wale wanaotoa huduma, na wale ambao wataangamizwa. Ni kwa nini wana Wangu wazaliwa wa kwanza hawako kati ya orodha hii? Ni kwa sababu wana Wangu wazaliwa wa kwanza sio wa asili ya uumbaji; wao ni kutoka Kwangu na sio wa wanadamu. Nilifanya mipango kwa ajili ya wana Wangu wazaliwa wa kwanza kabla Sijapata mwili; ni kaya gani ambayo wangezaliwa kwayo na ni nani wangekuwa huko kuwahudumia—vitu vyote hivi vilipangwa na mimi. Nilipanga pia ni wakati upi ambapo ni yupi kati yao angepatikana tena na Mimi na mwishoni tutarudi Sayuni pamoja. Hii yote ilipangwa kabla ya uumbaji, kwa hivyo hakuna mtu anayejua jambo hilo na halijaandikwa katika kitabu chochote kwa sababu hayo ni mambo ya Sayuni. Zaidi ya hayo, Nilipopata mwili, Sikumpa mwanadamu welekevu huu, kwa hiyo hakuna mtu aliyejua mambo hayo. Mtakaporejea Sayuni, mtajua vile mlivyofanana zamani, vile mnavyofanana sasa, na kile ambacho mmefanya katika maisha haya. Hivi sasa ni tu kuwa Ninawaambieni mambo haya kwa wazi na kidogo kidogo, vinginevyo hamngeelewa hata mfanye bidii namna gani, na mngezuia usimamizi Wangu. Leo, ingawa Nimejitenganisha kutokana na miili ya wana wangu wengi wazaliwa wa kwanza, sisi tu wa Roho mmoja, na ingawa maumbo yetu ya mwili yanaweza kuwa tofauti, sisi, tangu mwanzo hadi mwisho, tu Roho mmoja. Hata hivyo, wazao wa Shetani hawatatumia hii kama nafasi ya kunyonya. Haijalishi jinsi unavyojificha mwenyewe, inabakia ya juu juu, na sitaiafiki. Kwa hiyo mtu anaweza kuona kutoka kwa hili kuwa wale ambao wanasisitiza mambo ya juu juu na kutafuta kuniiga kwa nje wana uhakika asilimia mia moja kuwa ni Shetani. Kwa sababu roho yao ni tofauti na wao si wa wapendwa Wangu, haijalishi wataniiga namna gani hawafanani na Mimi. Zaidi ya hayo, kwa kuwa Wana wangu wazaliwa wa kwanza kimsingi ni wa Roho moja pamoja nami, hata kama hawaniigi, wanasema na kutenda sawasawa na Mimi, na wote ni waaminifu, safi, na wazi (kwa wale ambao hawana hekima ni kwa sababu tu ya uzoefu wao mdogo ulimwenguni, na hivyo kukosa hekima sio dosari ya wana Wangu wazaliwa wa kwanza, wakati ambapo watarudi katika mwili yote yatakuwa sawa). Kwa hiyo ni kwa sababu iliyoelezwa hapo juu kuwa watu wengi bado hawabadili asili yao ya kale bila kujali namna Ninavyowashughulikia. Lakini kwa wana Wangu wazaliwa wa kwanza, wanakubaliana na makusudi Yangu bila mimi kulazimika kuwashughulikia na hii ni kwa sababu sisi ni wa Roho mmoja. Wanahisi ndani ya roho yao nia ya kujitumia kabisa kwa ajili Yangu. Kwa hiyo, mbali na wana Wangu wazaliwa wa kwanza, hakuna mtu ambaye anajali kwa kweli na kwa dhati makusudi Yangu; ni baada ya mimi kumshinda Shetani tu ndiyo wako tayari kunifanyia huduma.

Hekima Yangu na wana Wangu wazaliwa wa kwanza husimama juu ya yote, hushinda yote, na hakuna kitu au mtu au jambo linalothubutu kuwazuia. Zaidi ya hayo, hakuna mtu, jambo, au kitu ambacho kinaweza kuwashinda, na badala yake yote yanajisalimisha kwa utii mbele ya nafsi Yangu. Huu ni ukweli ambao unatokea mbele ya macho ya mtu na ukweli ambao tayari nimekwisha kuutimiza. Mtu yeyote anayeendelea kuishi katika kutotii (wale wasiotii bado wanamtaja Shetani na wale wametwaliwa na Shetani bila shaka ni Shetani), kwa hakika Nitawaangamiza mzizi na tawi ili kusiwe na shida ya baadaye; watakufa mara moja kutokana na kuadibu Kwangu. Aina hii ya Shetani ni wale ambao hawana nia ya kutoa huduma Kwangu na vitu hivi daima vimenipinga kwa ukaidi tangu uumbaji, na leo wanaendelea kuishi kwa kutonitii (watu hawawezi kuona hili kwa sababu ni jambo tu la kuhusu roho. Mtu wa aina hii anawakilisha Shetani wa aina hii). Nitawaangamiza kwanza kabla ya kitu chochote kiwe tayari, na kuwafanya wapokee adhabu kali milele ("kuwaangamiza" hapa hakumaanishi kutokuwepo tena, lakini badala yake kunamaanisha kiwango cha ukatili ambacho watagandamizwa nao, na neno "kuangamiza" hapa ni tofauti na neno "kuangamiza" linalotumika kwa wale ambao wataangamizwa), na watalia na kusaga meno milele na milele, bila kikomo. Mwanadamu hawezi kufikiria mandhari hii kwa vyovyote. Kwa mawazo ya wanadamu yenye kufa, hawawezi kufahamu mambo ya kiroho, kwa hivyo, mtaelewa vitu vingi zaidi baada ya kurudi Sayuni tu.

Katika nyumba yangu itakayokuja, hakutakuwa na yeyote isipokuwa wana Wangu wa kwanza kuzaliwa na Mimi na wakati huo tu ndipo lengo Langu litafikiwa na mpango Wangu utakuja kuzaa matunda, kwa kuwa yote yatarejeshwa kwa hali yake ya awali na kila kitu kitaainishwa kulingana na aina yake. Wana wangu wazaliwa wa kwanza watarudi Kwangu, wana na watu Wangu watarejea katika ufalme wa viumbe na watendaji huduma na wale walioangamizwa watarudi kwa Shetani. Baada ya kuuhukumu ulimwengu, Mimi na wana Wangu wa kwanza kuzaliwa tutaanza tena maisha ya kiungu na hawataniacha kamwe na daima watakuwa pamoja na Mimi. Siri zote ambazo zinaweza kueleweka na akili za kibinadamu zitafichuliwa kwenu kidogo kidogo. Katika historia yote, kumekuwa na watu wengi ambao wameuawa kishahidi kwa sababu Yangu, wakijitolea kikamilifu Kwangu, lakini wanadamu ni viumbe hata hivyo na haijalishi ni wazuri namna gani, hawawezi kuainishwa kama Mungu; huu ni mwenendo usioepukika na hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote. Hata hivyo, ni Mungu ambaye anaumba vitu vyote na watu ni viumbe, na Shetani daima ni lengo Langu la uharibifu na adui Wangu wa kuchukiwa—ni maana ya kweli zaidi ya "chui hawezi kubadilisha madoadoa yake." Kuwa katika hali hii na hatua hii sasa ni ishara kwamba mimi na wana wangu wa kwanza kuzaliwa tutaingia katika raha. Hii ni kwa sababu kazi Yangu katika ulimwengu imekamilika kabisa na hatua inayofuata ya kazi Yangu itanihitaji nirudi kwenye mwili kuikamilisha. Hizi ni hatua za kazi Yangu na Nilizipanga vizuri sana zamani. Jambo hili linapaswa kuonekana wazi, vinginevyo watu wengi watavunja amri Zangu za kiutawala.

Iliyotangulia:Sura ya 113

Inayofuata:Sura ya 115

Unaweza Pia Kupenda