Sura ya 113

Hekima Yangu iko ndani ya kila kitendo Ninachokifanya, lakini mwanadamu hawezi kabisa kuelewa hekima hii; mwanadamu anaweza tu kuona matendo Yangu na maneno Yangu, si utukufu Wangu au kuonekana kwa nafsi Yangu, kwa kuwa mwanadamu kimsingi hana uwezo huu. Hivyo, bila Mimi kumbadilisha mwanadamu, wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi tutarejea Sayuni na kubadili sura, ili mwanadamu aweze kuiona hekima Yangu na nguvu Yangu yote. Hekima na kudura Yangu yote ambayo mwanadamu anaiona sasa, ni sehemu tu moja ndogo ya utukufu Wangu, isiyostahili kutajwa kamwe. Kutoka kwahili, inaweza kuonekana kwamba hekima Yangu na utukufu Wangu havina kikomo—yenye kina sana—ina akili ya mwanadamu kimsingi haina uwezo wa kuuzingatia au kuuelewa. Kuujenga ufalme ni wajibu wa wazaliwa wa kwanza, na hii ni kazi Yangu pia. Hiyo ni kusema, ni kipengele cha mpango Wangu wa usimamizi. Ujenzi wa ufalme si sawa na ujenzi wa kanisa; kwa kuwa wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi ni nafsi Yangu na ufalme, basi wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi tutakapoingia katika Mlima Sayuni, ujenzi wa ufalme utakuwa umetimia. Kusema kwa njia nyingine, ujenzi wa ufalme ni hatua katika kazi—hatua ya kuingia katika ulimwengu wa kiroho. (Hata hivyo, yote ambayo Nimefanya tangu kuiumba dunia yamekuwa kwa ajili ya hatua hii. Ingawa Nasema ni hatua, kwa kweli si hatua kabisa.) Hivyo, Nawatumia watendaji huduma wote wa hatua hii, na kwa sababu hiyo, katika siku za mwisho, idadi kubwa za watu itajiondoa; wote wanatoa huduma kwa wazaliwa wa kwanza. Yeyote anayetoa wema kwa watendaji huduma hawa ataaga kutokana na laana Zangu. (Watendaji huduma wote wanawakilisha njama za joka kubwa jekundu, na wote ni watumishi wa Shetani, kwa hiyo wale ambao wanaeneza wema kwa watu hawa ni vikaragosi wa joka kubwa jekundu nao ni wa Shetani.) Napenda yote ambayo Ninapenda, na Nachukia walengwa wote wa laana Zangu na kuteketezwa. Je, ninyi pia mnaweza kufanya hivi? Bila shaka Sitamsamehe Yeyote anayesimama dhidi Yangu, wala kumwachilia huru! Kwa kufanya kila tendo, Ninapanga kwa idadi kubwa ya watendaji huduma kunihudumia Mimi. Hivyo inaweza kuonekana kwamba katika historia nzima, imekuwa kwa ajili ya hatua hii ya leo ambapo manabii na mitume wote wametoa huduma, na hawajishughulishi na kuutafuta moyo Wangu, hawatoki Kwangu. (Ingawa wengi wao ni waaminifu Kwangu, hakuna aliye Wangu. Hivyo, kukimbia kwao huku na kule ni kuunda msingi wa hatua hii ya mwisho kwa ajili Yangu, lakini jitihada zao zote ni bure kuhusiana na wao wenyewe). Kwa hiyo, katika siku za mwisho hata zaidi kutakuwa na idadi kubwa za watu wa kujiondoa. (Sababu Ninasema “idadi kubwa” ni kwamba mpango Wangu wa uongozi umefikia kilele, ujenzi wa ufalme Wangu umefanikiwa, na wazaliwa wa kwanza wameketi juu ya kiti cha enzi.) Yote hayo ni kutokana na kuonekana kwa wazaliwa wa kwanza. Kwa sababu wazaliwa wa kwanza wameonekana, joka kubwa jekundu hujaribu kila njia iwezekanayo kutekeleza uharibifu na kutumia njia zote. Linatuma kila aina ya pepo wabaya ambao huja kufanya huduma kwa ajili Yangu, ambao wamebainisha tabia zao halisi zilivyo katika wakati wa sasa, na ambao wamejaribu kukatiza usimamizi Wangu. Haya hayawezi kuonekana kwa macho; yote ni mambo ya ulimwengu wa kiroho. Hivyo, watu hawaamini kwamba kutakuwa na idadi kubwa za watu ambao hurudi nyuma, ilihali Najua yale Ninayofanya, Ninaelewa usimamizi Wangu; hii ndiyo sababu ya kutomruhusu mwanadamu kuingilia kati. (Kutakuja siku ambapo kila aina ya pepo mbaya asiyefaa atafichua nafsi yake ya kweli, na watu wote wataridhika kwa dhati.)

Nawapenda wazaliwa Wangu wa kwanza, lakini wale ambao ni ukoo wa joka kubwa jekundu na wanaonipenda kwa uaminifu mkubwa, Siwapendi kabisa; kwa kweli Nawadharau hata zaidi. (Watu hawa si Wangu, na ingawa wanadhihirisha nia nzuri, na kunena maneno ya kufurahisha, hii yote ni njama ya joka kubwa jekundu, na hivyo Nawachukia hadi kwa moyo Wangu wote.) Hii ni tabia Yangu, na huu ni ukamilifu Wangu kwa ukamilifu. Mwanadamu hawezi kuelewa kabisa. Kwa nini ukamilifu wa haki Yangu unafichuliwa hapa? Kutokana na hili, mtu anaweza kutambua tabia Yangu takatifu na isiyoruhusu kosa lolote. Naweza kuwapenda wazaliwa Wangu wa kwanza na kuwadharau wale wote ambao si wazaliwa Wangu wa kwanza (hata ikiwa wao ni watu waaminifu). Hii ni tabia Yangu. Je, hamwezi kuona? Katika fikira za watu, Mimi daima ni Mungu mwenye huruma, nami Nawapenda wote wanaonipenda; je, tafsiri hii si kukufuru dhidi Yangu Mimi? Naweza kuwapenda wanyama na fahali? Naweza kumchukua Shetani kama mzaliwa Wangu wa kwanza na kufurahia hilo? Upuuzi! Kazi Yangu inatekelezwa kuwahusu wazaliwa Wangu wa kwanza, na mbali na wazaliwa Wangu wa kwanza, Sina kitu kingine cha kupenda. (Wana na watu ni nyongeza, lakini si muhimu.) Watu wanasema kwamba hapo awali, Nilifanya kazi nyingi sana isiyo na maana, lakini kwa maoni Yangu, kwa kweli kazi hiyo ilikuwa ya thamani sana, na yenye maana sana. (Hii inarejelea kikamilifu kazi yote iliyofanyika wakati wa kuupata mwili kuwili; kwa sababu Nataka kufichua nguvu Zangu, lazima Niwe mwili ili Niikamilishe kazi Yangu.) Sababu Ninasema Roho Wangu huja kufanya kazi yeye binafsi, ni kwamba kazi Yangu ikamilishwe katika mwili. Hiyo ni kusema, wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi sasa tunaanza kuingia katika mapumziko. Vita na Shetani katika mwili ni vikali zaidi kuliko vita na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, vinaweza kuonekana na watu wote, hivyo hata ukoo wa Shetani pia wnaweza kutoa ushuhuda mzuri kwa ajili Yangu, na huna nia ya kuondoka; hii ndiyo maana yenyewe ya kufanya Kwangu kazi katika mwili. Ni hasa ili kuufanya ukoo wa ibilisi umuaibishe ibilisi mwenyewe; hii ni aibu kubwa sana kwa ibilisi Shetani, kubwa sana kiasi kwamba hana mahali pa kuficha aibu yake, na kuomba rehema mbele Zangu kwa kurudia rudia. Nimeshinda, Nimeshinda juu ya kila kitu, Nimeipenya mbingu ya tatu na kuufikia Mlima Sayuni, kufurahia neema ya kifamilia pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza, milele kufurahia sanakatika karamu kubwa ya ufalme wa mbinguni!

Kwa wazaliwa wa kwanza, Nimelipa kila gharama na kuchukua maumivu yote kwa juhudi zangu. (Mwanadamu hajui kabisa kwamba yote Nimefanya, yote Nimesema, ukweli kwamba Nabaini kila aina ya pepo mbaya, na kwamba Nimemfukuza kila aina ya mtendaji huduma, —hii yote imekuwa kwa sababu ya wazaliwa wa kwanza.) Lakini ndani ya kazi nyingi, mpango Wangu ni wenye utaratibu; kazi hii haifanywi ovyo. Katika matamshi Yangu kila siku, mnapaswa kuweza kuona mbinu na hatua za kazi Yangu na hatua zake; katika matendo Yangu kila siku mnapaswa kuona hekima Yangu na kanuni Zangu katika kukabiliana na mambo. Kama Nilivyosema, Shetani amewatuma wale ambao wananifanyia huduma kwa nia ya kukatiza usimamizi Wangu. Hawa watendaji huduma ni magugu, lakini neno “ngano” hairejelei wazaliwa wa kwanza, lakini kwa wana wote na watu ambao si wazaliwa wa kwanza. “Siku zote ngano itakuwa ngano, siku zote magugu yatakuwa magugu”; hii ina maana asili ya wale ambao ni wa Shetani haiwezi kubadilika kamwe. Kwa hiyo, kwa ufupi, wao wanabaki Shetani. “Ngano” linarejelea wana na watu, kwa sababu Niliweka ubora Wangu ndani ya watu hawa kabla ya kuumbwa ulimwengu. Kwa sababu Nimeshasema tayari kwamba asili ya mwanadamu haibadiliki, na hiyo ndiyo maana ngano siku zote itakuwa ngano. Basi, wazaliwa wa kwanza ni nini? Wazaliwa wa kwanza wanatoka Kwangu, hawaumbwi nami, hivyo hawawezi kuitwa ngano (kwa sababu kutajwa kwa aina yoyote kwa ngano, daima kumeunganishwa na maneno “kupanda,” na “kupanda” maana yake ni “kuumba”; magugu yote yamepandwa na Shetani kisiri, ili kutenda kama watendaji huduma). Mtu anaweza tu kusema kwamba wazaliwa wa kwanza ni onyesho kamili na karimu la nafsi Yangu, wanapaswa kuwakilishwa na dhahabu na fedha, na vito vya thamani. Hili linagusia ukweli kwamba kuja Kwangu ni kama kule kwa mwizi, nami Nimekuja kuiba dhahabu na fedha na vito vya thamani (kwa sababu hii dhahabu na fedha na vito vya thamani vyote vilikuwa Vyangu, nami Nataka kuvirudisha nyumbani Kwangu). Wakati ambapo wazaliwa wa kwanza nami tutarudi Sayuni pamoja, hii dhahabu, hii fedha na vito vya thamani vitakuwa vimeibiwa na Mimi. Wakati huu, kutakuwa na vizuizi na vurugu ya Shetani, na hivyo Nitazichukua dhahabu, fedha na vito vya thamani na kuzindua vita vya maamuzi na Shetani. (Hapa, bila shaka sisemi hadithi; hili ni tukio katika ulimwengu wa kiroho, hivyo watu hawana uwazi kabisa kulihusu, na wanaweza tu kulisikia kama hadithi. Lakini ni jukumu lenu kuona kutoka katika maneno Yangu kile ambacho mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita unahusu, na ni sharti msilichukulie kama utani kabisa. Vinginevyo, Roho Wangu Ataondoka kutoka ndani ya wanadamu wote.) Leo, vita hivi vimekamilika kabisa, nami Nitawaleta wazaliwa Wangu wa kwanza (Nikizileta dhahabu, fedha na vito vya thamani ambavyo ni Vyangu) pamoja nami Mlimani Kwangu Sayuni. Kutokana na uhaba wa dhahabu, fedha na vito vya thamani, na kwa sababu ya thamani yao, Shetani hujaribu kila namna iwezekanayo kuvipokonya, lakini Nasema tena na tena kwamba kile kitokacho Kwangu lazima kinirudie, maana yake ambayo imetajwa hapo juu. Msemo Wangu kwamba wazaliwa wa kwanza wanatoka Kwangu na ni Wangu ni tangazo kwa Shetani. Hakuna mtu anayeelewa hili, na kwa ukamilifu ni jambo ambalo hutokea katika ulimwengu wa kiroho. Hivyo, mwanadamu haelewi kwa nini Narudia kusisitiza kwa kurudia kwamba wazaliwa wa kwanza ni Wangu; leo, mnapaswa kuelewa! Nimesema kwamba maneno Yangu yana kusudi na hekima, lakini mnaelewa hili kwa nje—hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuona hili wazi katika roho.

Nasema zaidi na zaidi, na zaidi Ninavyosema ndivyo makali zaidi maneno Yangu yanavyokuwa. Inapofika kiwango fulani, Nitayatumia maneno Yangu kuwafinyanga watu kwa kiwango fulani, kuwafanya watu wasiridhishwe moyoni na kwa neno tu, lakini zaidi ya hayo kuwafanya wakaribie kifo; hii ni mbinu Yangu ya kazi na jinsi kazi Yangu inavyoendelea kwa hatua zake. Lazima iwe hivyo; ni hivyo tu ndivyo inavyoweza kumwaibisha Shetani na kuwakamilisha wazaliwa wa kwanza (kuyatumia maneno Yangu ili hatimaye kuwafanya wazaliwa wa kwanza kamili, ili kuwaruhusu kujitenga na mwili na kuingia katika ulimwengu wa kiroho). Mwanadamu haelewi mbinu na sauti ya maneno Yangu. Utambuzi kiasi unafaa kuwajia nyote kutokana na maelezo Yangu na mnapaswa kufuata maneno Yangu ili muikamilishe kazi ambayo mnapaswa kuifanya. Hiki ndicho ambacho Nimewaaminia. Lazima mfahamu hili, na si tu kutoka ulimwengu ya nje, lakini muhimu zaidi, kutoka katika ulimwengu ya kiroho.

Iliyotangulia: Sura ya 112

Inayofuata: Sura ya 114

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp