Sura ya 70

Kwamba siri Zangu zinafichuliwa na zinadhihirika wazi, na hazifichiki tena, ni kwa sababu ya neema na rehema Zangu kabisa. Zaidi ya hayo, kwamba neno Langu linaonekana kati ya wanadamu, na halifichiki tena, nako pia ni kwa sababu ya neema na rehema Zangu. Ninawapenda wote wanaojitumia na kujitoa wenyewe kwa dhati kwa ajili Yangu. Nawachukia wale wote waliozaliwa kutoka Kwangu ila bado hawanijui Mimi, na hata wananipinga Mimi. Sitamwacha yeyote ambaye kwa dhati yuko kwa ajili Yangu; badala yake, baraka zake Nitazifanya ziwe mara dufu. Nitawaadhibu mara dufu wale wasio na shukrani na wanaokiuka fadhila Zangu, na sitawaachilia kwa urahisi. Katika ufalme Wangu hakuna upotovu au udanganyifu, na hakuna udunia; yaani, hakuna harufu ya wafu. Badala yake, yote ni unyofu na haki; yote ni usafi na uwazi, bila kuwa na chochote kilichofichika au kisicho wazi. Kila kitu ni kipya, kila kitu ni starehe, na kila kitu ni cha kujenga. Yeyote ambaye bado ananuka wafu hawezi kamwe kubakia katika ufalme Wangu, na badala yake atatawaliwa na fimbo Yangu ya chuma. Siri zote zisizo na mwisho, tangu zamani sana hadi sasa, zinafichuliwa kikamilifu kwenu—kundi la watu ambao wanapatwa na mimi katika siku za mwisho. Je, hamhisi kuwa mmebarikiwa? Zaidi ya hayo, siku ambazo yote yanafunuliwa wazi, ni siku ambazo mtashiriki utawala Wangu.

Kundi la watu ambao kwa kweli hutawala kama wafalme hutegemea majaliwa na uchaguzi Wangu, na kamwe hakuna mapenzi ya mwanadamu ndani yake. Yeyote anayethubutu kushiriki katika hili lazima apate pigo kutoka kwa mkono Wangu, na watu kama hao watakabiliwa na moto Wangu mkali; huu ni upande mwingine wa haki na uadhama Wangu. Nimeshasema kwamba ninatawala vitu vyote, mimi ndiye Mungu mwenye hekima ambaye ana mamlaka kamili, na Sina huruma kwa mtu yeyote; Mimi ni katili kabisa, sina hisia za kibinafsi kamwe. Ninamtendea mtu yeyote (haijalishi anaongea vizuri namna gani, Sitamwachilia) kwa haki, uadilifu na uadhama Wangu, wakati huohuo Nikimwezesha kila mtu kuona maajabu ya matendo Yangu vizuri zaidi, na vilevile maana ya matendo Yangu. Mmoja baada ya mwingine, Niliwaadhibu pepo wabaya kwa kila aina ya matendo wanayotenda, nikiwatupa kila mmoja ndani ya shimo lisilo na mwisho. Kazi hii Niliimaliza kabla ya wakati kuanza, nikawaacha bila nafasi, nikiwaacha bila mahali pa kufanya kazi yao. Hakuna hata mmoja wa watu Wangu wateule—wale waliojaliwa na kuchaguliwa na Mimi—anayeweza kupagawa kamwe na roho waovu, na badala yake atakuwa mtakatifu daima. Lakini kwa wale ambao Sijawajalia na kuwachagua, Nitawakabidhi kwa Shetani, na sitaruhusu wabakie tena. Katika vipengele vyote, amri Zangu za kiutawala zinajumuisha haki Yangu na uadhama Wangu. Sitamwachilia hata mmoja wa wale ambao Shetani anatenda kazi kwao, lakini nitawatupa pamoja na miili yao kuzimuni, kwa maana namchukia Shetani. Sitamwachilia kwa urahisi hata kidogo, lakini nitamwangamiza kabisa, nisimruhusu hata fursa ndogo kabisa kufanya kazi yake. Wale ambao Shetani amewapotosha kwa kiwango fulani (yaani, wale ambao watakabiliwa na maafa) wako chini ya mpangilio wa hekima wa mkono Wangu. Msidhani kwamba hili limetokea kwa sababu ya ukali wa Shetani; jueni kuwa Mimi ni Mwenyezi Mungu anayetawala ulimwengu na vitu vyote! Kwangu Mimi, hakuna matatizo ambayo hayawezi kutatuliwa, sembuse kitu ambacho hakiwezi kukamilishwa au neno lolote ambalo haliwezi kusemwa. Wanadamu hawapaswi kutenda kama washauri Wangu. Jihadharini na kuangushwa na mkono Wangu na kutupwa kuzimuni. Nakuambia hili! Wale ambao wanashirikiana na Mimi leo kwa vitendo ndio werevu kupita wote, na wataepuka hasara na kukwepa maumivu ya hukumu. Yote haya ni mipangilio Yangu, iliyojaliwa na Mimi. Usitoe matamshi yasiyo na busara na usizungumze maneno matupu, ukidhani wewe ni mkuu sana. Je, yote haya hayatokani na majaliwa Yangu? Ninyi, ambao mnataka kuwa washauri Wangu, hamwoni aibu! Hamjui kimo chenu wenyewe; jinsi kilivyo kidogo kiasi cha kusikitisha! Hata hivyo, mnafikiri hili silo jambo kubwa, na hamjijui wenyewe. Tena na tena, mnayapuuza maneno Yangu, na kusababisha juhudi Zangu kubwa kuwa za bure na hamgundui hata kidogo kuwa ni udhihirisho wa neema na rehema Zangu. Badala yake, mnajaribu kuonyesha ujanja wenu tena na tena. Mnakumbuka hili? Je, ni adhabu gani ambayo watu ambao wanafikiri ni wajanja sana wanapaswa kupokea? Mkiwa wasiojali na wasio waaminifu kwa maneno Yangu, na msioyaandika mioyoni mwenu, mnanitumia Mimi kama kisingizio cha kufanya hivi na vile. Watenda mabaya! Je, ni lini ambapo mtaweza kuufikiria moyo Wangu kikamilifu? Hamuuzingatii, kwa hivyo kuwaita “watenda maovu” sio kuwatendea vibaya. Inawastahili kabisa!

Leo Ninawaonyesha, moja baada ya jingine, mambo ambayo zamani yalikuwa yamefichika. Joka kubwa jekundu limetupwa ndani ya shimo lisilo na mwisho na kuangamizwa kabisa, maana kuendelea kuliweka hakutakuwa na faida kabisa; hii inamaanisha kuwa haliwezi kumhudumia Kristo. Baada ya hapa, vitu vya rangi nyekundu havitakuwapo tena; hatua kwa hatua, lazima vipotee kabisa. Ninatenda kile Ninachosema; huku ndiko kukamilika kwa kazi Yangu. Ondoeni fikira za kibinadamu; kila kitu ambacho Nimesema, nimefanya. Yeyote anayejaribu kuwa mjanja hujiletea uangamizi na dharau, na hataki kuishi. Kwa hivyo, Nitakuridhisha, na hakika sitawaweka watu kama hao. Baada ya hapa, idadi ya watu itaongezeka katika ubora, ilhali wote ambao hawashirikiana na Mimi kwa vitendo wataangamizwa kabisa. Wale ambao Nimewaidhinisha ndio ambao Nitawakamilisha, na sitamtupa hata mmoja. Hakuna ukinzani katika kile Ninachosema. Wale ambao hawashirikiani na Mimi kwa vitendo watapata adhabu zaidi, ingawa mwishowe, hakika nitawaokoa. Hata hivyo, kufikia wakati huo, kiwango cha maisha yao kitakuwa tofauti kabisa. Je, wewe unataka kuwa mtu kama huyo? Inuka na ushirikiane na Mimi! Hakika Sitamtendea vibaya yeyote anayejitumia kwa dhati kwa ajili Yangu. Kwa wale wanaojitolea Kwangu kwa bidii, Nitawapa baraka Zangu zote. Jitoe kikamilifu Kwangu! Kile unachokula, kile unachovaa, na siku zako zijazo vyote viko mikononi Mwangu; Nitapangilia kila kitu sawasawa, ili uwe na starehe isiyo na mwisho, ambayo hutaimaliza kamwe. Hii ni kwa sababu Nimesema, “Kwa wale ambao wanatumia rasilmali zao kwa ajili Yangu kwa dhati, hakika Nitakubariki sana.” Baraka zote zitakuja kwa kila mtu anayejitumia kwa dhati kwa ajili Yangu.

Iliyotangulia: Sura ya 69

Inayofuata: Sura ya 71

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp