Sura ya 69
Mapenzi Yangu yanapoenenda, yeyote anayethubutu kupinga na yeyote anayethubutu kuhukumu au kuwa na shaka, Nitamfukuza mara moja. Leo, yeyote ambaye hatendi kulingana na mapenzi Yangu, au yeyote anayeyafikiria mapenzi Yangu visivyo, ni lazima atupwe nje na kuondolewa kutoka kwa ufalme Wangu. Katika ufalme Wangu hakuna mwingine—wote ni wana Wangu, wale Niwapendao na wanaonifikiria Mimi. Zaidi ya hayo, ndio ambao hutenda kulingana na neno Langu na ambao wana uwezo wa kutawala katika uongozi kwa niaba Yangu kuhukumu mataifa yote na watu wote. Aidha, wao ni kundi la wana wa kiume wazaliwa wa kwanza, wasio na hatia na wachangamfu; sahili na wazi; waaminifu na wenye hekima. Mapenzi Yangu yameridhika ndani yenu, na kile ambacho Nataka kufanya kimetimia ndani yenu, bila makosa, wazi kabisa na kufichuliwa. Wale ambao wana nia na madhumuni mabaya—Nimeanza kuwaacha, na Nitafanya waanguke mmoja mmoja. Nitawaangamiza mmoja baada ya mwingine kufingia hatua ambapo wasiweze kuendelea kuishi—na haya yote yanarejelea roho zao, nafsi zao na miili yao.
Elewa kwamba kile ambacho mkono Wangu unafanya—kuwaruzuku maskini, kuwatunza na kuwalinda wale wanaonipenda Mimi, kuwaokoa wajinga na wenye bidii ambao hawaingilii usimamizi Wangu, kuwaadhibu wale ambao hunipinga Mimi na wale ambao hawashirikiani Nami kikamilifu—mambo haya yote yatathibitishwa moja baada ya jingine kulingana na yale niliyosema. Je, wewe ni mtu ambaye kweli unanipenda Mimi? Je, wewe ni mtu ambaye unajitoa kwa ajili Yangu kwa uaminifu? Je, wewe ni mtu ambaye husikiliza neno Langu na kutenda ipasavyo? Je, wewe ni mtu ambaye unanipinga, au unalingana na Mimi? Je, akili yako iko wazi juu ya mambo haya? Je, wewe ni mtu ambaye husikiliza neno Langu na kutenda ipasavyo? Je, wewe ni mtu ambaye hunipinga Mimi, au wewe ni mtu unayelingana na Mimi? Je, mawazo yako mwenye yako wazi juu ya mambo haya? Je, unaweza kujibu kwa mambo haya Niliyoyasema moja baada ya jingine? Kama huwezi, wewe ni mtu ambaye hufuata kwa shauku, lakini hayaelewi mapenzi Yangu. Aina hii ya mtu kwa urahisi zaidi ataingilia usimamizi Wangu na kufikiria mapenzi Yangu visivyo. Iwapo mtu kama huyo kwa muda ana nia mbaya, yeye atakabiliwa na kufukuzwa na kuangamizwa na Mimi.
Ndani Yangu kuna mafumbo yasiyo na mwisho, yasiyoweza kueleweka. Nitayafichua kwa watu moja baada lingine kulingana na mpango Wangu. Yaani, Nitawafunulia wana Wangu wa kwanza. Kwa wale wasioamini na ambao hunipinga Mimi, Nitawaruhusu kwenda na mkondo, lakini mwishowe lazima Niwafanye waelewe kwamba Mimi ni hukumu na uadhama. Watu wasioamini wa leo wanajua tu kinachotokea mbele ya macho yao, lakini hawajui mapenzi Yangu. Ni Wanangu tu, Ninaowapenda, wanaojua na kuyaelewa mapenzi Yangu. Kwa Wanangu, Nimefichuliwa wazi wazi, lakini kwa Shetani Mimi ni hukumu na uadhama, sijafichwa hata kidogo. Leo ni wanangu wazaliwa wa kwanza tu ambao wanastahili kujua mapenzi Yangu—hakuna mtu mwingine anayestahili—na hili ndilo Nililopanga kabla ya uumbaji. Ni nani amebarikiwa na ni nani amepigwa mijeledi wote walikuwa wamepangwa vizuri nami mapema, Nilikuwa wazi kuhusu hili, na kwa sasa tayari limedhihirika kikamilifu: Wale waliobarikiwa wameanza kufurahia baraka zao, ilhali wale ambao wamechapwa viboko pia wameanza kuteseka kwa maafa. Wale ambao hawataki kuteseka na baa hata hivyo watateseka kwa sababu hili ndilo Nimeamua na hili ndilo mikono Yangu ya amri za kiutawala imepanga. Hasa ni aina gani ya mtu amebarikiwa na ni aina gani ya mtu amepigwa viboko? Tayari Nimefichua mambo haya; hili si siri kwenu, lakini limejitokeza waziwazi: Wale wanaonikubali Mimi lakini ambao nia zao ni mbaya; wale wanaonikubali Mimi lakini hawafuatilii; wale wanaonijua Mimi lakini si watiifu; wale wanaojiingiza katika uhalifu na udanganyifu kunihadaa Mimi; wale wanaosoma maneno Yangu lakini hutapika uhasi; wale ambao hawajijui wenyewe, ambao hawajui wao ni nini, ambao wanajidhani kuwa wao wenyewe ni wakubwa, na ambao wanadhani kwamba wamefikia ukomavu (mfano wa Shetani), hawa ni vifaa vya baa. Wale ambao hunikubali Mimi na ambao nia yao ni kunielekea Mimi (na kama wakisababisha matatizo Mimi sitakumbuka makosa yao, lakini nia zao ni lazima ziwe za haki na ni lazima daima wawe na tahadhari, wawe makini na wasiwe wapotovu, na lazima daima waweke mioyoni mwao kunisikiliza Mimi na kunitii); wale ambao ni wasafi; wale ambao wako wazi; wale ambao ni waaminifu, wale ambao hawadhibitiwi na mtu yeyote, kitu, au jambo; watu walio kama watoto kwa kuonekana ingawa wao ni wakomavu katika maisha, hawa ndio wapendwa Wangu, vifaa vya baraka Yangu. Sasa, kila mmoja atachukua nafasi yake sahihi kwa mujibu wa hali yake. Na wewe utajua kama umebarikiwa au umepigwa viboko—hakuna haja Kwangu kusema dhahiri. Wale waliobarikiwa lazima washangilie na kuwa na furaha, huku wale ambao watafikwa na baa hawapaswi kuhuzunika. Yote mawili yamepangwa na mkono Wangu, lakini Mimi si wa kulaumiwa: Ni ukosefu wako mwenyewe wa ushirikiano hai na Mimi, na kushindwa kwako kuelewa kwamba Mimi ni Mungu anayetafuta ndani kabisa ya moyo wa binadamu; ni kile ambacho Nimeamua kabla, na ni kwa hila yako ndogo ambapo umejidhuru mwenyewe; ni kujiumiza mwenyewe! Kwamba lazima utumbukie Kuzimu si kutendewa vibaya! Huu ni mwisho wako; haya ni matokeo yako!
Wabarikiwa wana wazaliwa kwa kwanza! Inukeni upesi kushangilia! Inukeni upesi kutoa sifa! Kuanzia sasa na kuendelea, hakutakuwa na uchungu tena, hakuna mateso tena, na kila kitu kiko mikononi mwetu. Yeyote aliye na nia moja na Mimi ni yule Ninayempenda, na hatapatwa na mateso ya maafa. Chochote ambacho ni hamu ya moyo wako, Nitakitimiza (lakini haiwezi kuwa ya kiholela), hii ni kazi Yangu.