Sura ya 71

Mimi wote Nimejiweka dhahiri kwenu, lakini kwa nini mnashindwa kutafakari maneno Yangu kwa mioyo na nafsi zenu zote? Kwa nini mnachukua maneno Yangu kama takataka? Je,yote Ninayosema ni makosefu? Je, maneno Yangu yamekupiga katika sehemu ya uzima? Daima kuchelewesha, daima kusita, kwa nini mnafanya mambo hivi? Je, Mimi sijaongea wazi? Nimesema mara nyingi sana kwamba maneno Yangu lazima yatafakariwe kwa makini, na lazima yazingatiwe kwa makini. Je, kuna wowote kati yenu ambao ni watoto watiifu na wanyenyekevu? Je, Nimeongea bure? Je, hakuna matokeo kabisa? Ni kiasi gani cha yale yaliyo ndani yako yanayoweza kukidhi mapenzi Yangu? Kama kwa muda hukaripiwi, wewe huwa mpotovu na asiyedhibitika. Nisipoeleza wazi jinsi ya kutenda, au jinsi ya kuzungumza, je, inawezekana kwamba wewe huna wazo katika moyo wako? Nakuambia! Anayepata hasara ni yule ambaye ni mkaidi, ambaye hanyenyekei, ambaye anaamini kwa upofu! Kama mtu hawi makini kwa yale Ninayoyasema, kama hawezi kung'amua kila kitu, basi hataweza kuelewa nia Zangu, na hataweza kunitumikia Mimi. Mtu wa aina hii atashughulikiwa na Mimi, na atapambana na hukumu Yangu. Kutoelewa kila kitu ni kuwa fidhuli sana na kuwa na pupa kwa makusudi. Kwa hivyo Namchukia mtu wa aina hii, na Sina upole hata kidogo kwake, Nikimtendea bila heshima, uadhama wote na hukumu; ona kama bado unathubutu kunidanganya Mimi. Mimi ni Mungu ambaye huchunguza ndani kabisa ya moyo wa binadamu. Sehemu hii yapaswa kuwa wazi kwa kila mtu; vinginevyo, wataendesha shughuli zao kwa njia ya kawaida wakinilaghai Mimi. Hii ndiyo sababu baadhi ya watu bila kujua hupigwa nami. Nimesema kwamba Sitamshughulikia mtu yeyote bila ya haki, kwamba Sitafanya mambo maovu, kwamba kila kitu Nifanyacho ni kwa mujibu wa mipango ya busara ya mkono Wangu.

Hukumu Yangu imeshuka juu ya watu wote wasionipenda kwa dhati, wakati ambapo itakuwa wazi ni nani Niliyemjaalia na kumchagua, na ni nani ambaye ameondolewa na Mimi. Haya sharti yawekwe wazi moja moja, bila kuficha chochote. Watu wote, matukio, na mambo yameasisiwa na yapo ili kuleta maneno Yangu kwa ukamilisho; kila kitu kimetumiwa katika kufanya kweli maneno yaliyonenwa kwa kinywa Changu. Mkono Wangu huidhibiti miisho ya ulimwengu wote. Nitampiga yeyote anayethubutu kutoyatii maneno Yangu, au kutofanya kama Ninavyosema. Hivyo mtu huyo atazama kuzimu na hataishi. Maneno Yangu yote yanafaa na sahihi bila uchafu wowote. Je, kuzungumza kwenu kunaweza kufanana na Kwangu? Yote ni marefu na ya kuchosha, haueleweki na hauelezi kwa dhahiri, na bado unafikiri umepata baadhi ya mambo, kwamba uko karibu sana, Nakwambia! Jinsi mtu alivyo mwenye kiburi, ndivyo anavyokuwa mbali na viwango Vyangu. Haonyeshi nadhari kwa mapenzi Yangu, naye hunidanganya Mimi na kuliaibisha Jina Langu kwa ukali sana! Hana haya! Huangalii kimo chako mwenyewe. Wewe ni mpumbavu na ya mjinga kiasi kilichoje!

Maneno Yangu husizitiza mambo wakati wote na katika sehemu zote. Je, inaweza kuwa kwamba bado huelewi, na bado huna uhakika? Je, unataka kunisikitisha Mimi? Jikakamue, na utayarishe ujasiri wako. Simtendei kwa njia isiyo ya haki mtu yeyote ambaye ananipenda Mimi. Mimi huchunguza ndani kabisa ya moyo wa binadamu na Ninajua yote ya yaliyo katika moyo wa kila mtu. Haya yote yatadhihirishwa moja moja, na yote yatapitia uchunguzi Wangu. Sitakosa kamwe kutotilia maanani mtu yeyote ambaye kwa kweli ananipenda Mimi. Wao wote ni wapokeaji wa baraka; wao ni kundi la wana wa kiume wazaliwa wa kwanza ambao Nimewajaalia kuwa wafalme. Na kwa wale ambao hawanipendi Mimi, wao ni madango ya hila zao wenyewe, na ni wapokeaji wa baa, na pia imejaaliwa na Mimi. Usihangaike. Nitawafichua mmoja mmoja. Nimetayarisha kazi hii mapema sana, na Nimeanza kufanya kazi hii. Yote ni kwa mujibu wa mpango wa mfuatano, si machafuko kamwe. Tayari Nimemaliza kazi ya kuamua ni nani mteule na ni nani ameondolewa. Mmoja kwa mmoja watafichuliwa kwenu muone. Katika kipindi cha nyakati hizi mtaona kile mkono Wangu unachokifanya, watu wote wataona kwamba haki Yangu na uadhama Wangu hauruhusu kosa au upinzani kutoka kwa mtu yeyote, na kwamba mtu yeyote ambaye anakosea ataadhibiwa vikali.

Mimi Ndiye ambaye daima hukagua ndani kabisa ya moyo wa kila mtu. Msinione Mimi kutoka kwa nje tu. Wanadamu vipofu! Hamsikilizi maneno ambayo Nimeyazungumza wazi, na kabisa nyinyi hamuniamini Mimi, ambaye ni Mungu Mwenyewe kamili. Bila shaka Sitamvumilia yeyote ambaye huthubutu kufanya ulaghai au udanganyifu.

Unakumbuka yale yote ambayo Nimeyasema? "Kuniona Mimi ni sawa na kuona kila moja ya siri iliyofichwa tangu milele hata milele." Je, umeitafakaria kwa makini taarifa hii? Mimi ni Mungu. Siri Yangu imeonyeshwa kwa ajili yenu. Je, hamjaiona? Kwa nini hamnizingatii Mimi? Na mbona unamwabudu Mungu asiye yakini ambaye yuko katika mawazo yako? Ningewezaje Mimi—Mungu mmoja wa kweli—kufanya kosa lolote? Angalia hili kwa udhahiri! Kuwa na uhakika kwalo! Kila neno Langu na amali, kila tendo Langu na kila mwendo, kutabasamu Kwangu, kula Kwangu, na mavazi Yangu, kila kitu Changu hufanywa na Mungu Mwenyewe. Mnanihukumu Mimi, je, yawezekana kuwa kwamba tayari mlimuona Mungu kabla ya ujio Wangu? Hivyo kwa nini siku zote wewe hunilinganisha Mimi na Mungu wako katika moyo wako? Zote ni dhana za wanadamu! Vitendo Vyangu na tabia haviambatani na mawazo yako, ni kweli? Huwa Simruhusu mtu yeyote kutoa maoni kama vitendo Vyangu na tabia ni sahihi au la. Mimi ndiye Mungu mmoja wa kweli. Huu ni ukweli usioweza kubadilishwa, na sahihi kabisa! Usidanganywe na hila zako mwenyewe. Maneno Yangu yamelisema kwa uwazi kabisa. Hakuna doa la ubinadamu ndani Yangu, na Mimi wote ni Mungu Mwenyewe, Aliyedhihirishwa kikamilifu kwenu, bila kitu fiche!

Iliyotangulia: Sura ya 70

Inayofuata: Sura ya 72

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Kazi na Kuingia (5)

Leo wote mnajua kwamba Mungu anawaongoza watu katika njia sahihi ya uzima, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuchukua hatua inayofuata kuingia...

Shida Kubwa Sana: Usaliti (2)

Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu, kwa sababu asili potovu ya mwanadamu hutoka kwa Shetani kabisa; asili ya mwanadamu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki