Mazungumzo Mafupi Kuhusu “Ufalme wa Milenia Umefika”
Mnayaonaje maono ya Ufalme wa Milenia? Baadhi ya watu hutafakari sana kuuhusu na kusema kuwa Ufalme wa Milenia utadumu duniani kwa miaka elfu moja, hivyo basi ikiwa waumini wazee katika kanisa hawajaoa, je, wanapaswa kuoa? Familia yangu haina pesa, je napaswa nianze kutafuta pesa? … Ufalme wa Milenia ni nini? Je, mnajua? Watu ni nusu vipofu na wanapitia mateso mengi. Kwa hakika, Ufalme wa Milenia bado haujafika rasmi. Katika hatua ya kuwafanya wanadamu wakuwe wakamilifu, Ufalme wa Milenia bado hauna uzoefu; katika kipindi cha Ufalme wa Milenia uliozungumziwa na Mungu, mwanadamu atakuwa amefanywa mkamilifu. Hapo nyuma, ilisemekana kwamba watu wangekuwa kama watakatifu na kusimama imara katika nchi ya Sinimu. Ni pale tu watu watakapofanywa wakamilifu—watakapokuwa watakatifu walionenwa na Mungu—ndipo Ufalme wa Milenia utakapokuwa umefika. Mungu anapowafanya watu kuwa wakamilifu, anawatakasa, na kadiri walivyo wasafi ndivyo wanavyofanywa wakamilifu na Mungu. Uchafu, uasi, upinzani na mambo ya kimwili yakitokomezwa kutoka kwako, ukishatakaswa, basi utakuwa mpendwa wa Mungu (na kwa maneno mengine, utakuwa mtakatifu); ukifanywa mkamilifu na Mungu na kuwa mtakatifu, utakuwemo katika Ufalme wa Milenia. Sasa ni Enzi ya Ufalme. Katika Enzi ya Ufalme wa Milenia, watu watategemea maneno ya Mungu kuishi, na mataifa yote yatakuja chini ya jina la Mungu, na wote watapata kusoma maneno ya Mungu. Wakati huo, wengine watapiga simu, na wengine watatuma faksi … watatumia kila njia kuyafikia maneno ya Mungu, nanyi, vilevile, pia, mtakuja chini ya maneno ya Mungu. Haya yote ni maswala yanayofanyika baada ya watu kufanywa wakamilifu. Leo hii, watu wanafanywa wakamilifu, wanasafishwa, wanapata nuru, na kuongozwa kupitia kwa maneno; hii ni Enzi ya Ufalme, ni hatua ya watu kufanywa wakamilifu na haina uhusiano na Enzi ya Ufalme wa Milenia. Wakati wa Enzi ya Ufalme wa Milenia, watu tayari watakuwa wamefanywa wakamilifu, na tabia mbovu ndani yao zitakuwa zimetakaswa. Wakati huo, maneno yasemwayo na Mungu yatawaongoza wanadamu hatua kwa hatua, na kufichua siri za kazi ya Mungu tangu uumbaji hadi leo, na maneno Yake yatawaambia watu kuhusu matendo ya Mungu katika kila enzi na kila siku, jinsi Anavyowaongoza watu ndani, kazi Aifanyayo katika ufalme wa kiroho, na yatawaambia kuhusu mienendo ya ufalme wa kiroho. Hapo tu ndipo itakuwa Enzi ya kikweli ya Neno; kwa sasa iko tu katika hali isiyo na uzoefu tu. Iwapo watu hawatafanywa wakamilifu na kutakaswa, hawatakuwa na njia ya kuishi miaka elfu moja duniani, na miili yao pasi kuzuia itaoza; iwapo watu watatakaswa kwa ndani, na kamwe wasiwe wa Shetani na wa kimwili, basi watabaki hai duniani. Katika hatua hii, bado uko nusu kipofu na yote unayoyapitia ni Mungu wa upendo na kuwa na ushuhuda Kwake kila siku mnayoishi duniani.
“Ufalme wa Milenia Umefika” ni unabii, ni mfano wa utabiri wa nabii ambao kwao Mungu anatabiri kitakachofanyika hapo mbeleni. Maneno anenayo Mungu siku za usoni na yale Anayoyanena leo hii si sawa: Maneno ya siku za usoni yataiongoza enzi, ilhali maneno anenayo leo hii yanawafanya watu kuwa wakamilifu, kuwasafisha na kuwashughulikia. Enzi ya Neno katika siku zijazo ni tofauti na Enzi ya Neno leo. Leo, maneno yote yanenwayo na Mungu—bila kujali Ameyanena kwa namna gani—kwa ujumla, ni kwa ajili ya kuwafanya watu kuwa wakamilifu, kutakasa kile kilicho kichafu ndani yao, na kuwafanya watakatifu na wenye haki mbele ya Mungu. Maneno yanenwayo leo na maneno yatakayonenwa katika siku za usoni ni vitu viwili tofauti. Maneno yanenwayo katika Enzi ya Ufalme ni ya kuwafanya watu waingie katika mafunzo yote, kuwafanya watu waingie katika njia sahihi kwa kila kitu, kukitokomeza chochote kilicho kichafu ndani yao. Hayo ndiyo Mungu Anayofanya katika enzi hii: Anajenga msingi wa maneno Yake kwa kila mtu, Anayafanya maneno Yake kuwa uzima wa kila mtu na Anayatumia maneno Yake kuwapatia nuru watu na kuwaongoza ndani kila wakati, na wasipoyajali mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu yatakuwa ndani yao kuwakemea na kuwafundisha nidhamu. Maneno ya leo yanafaa kuwa uzima wa mwanadamu, yanatoa moja kwa moja kila anachokihitaji mwanadamu, kila unachokikosa kwa ndani kinatolewa na maneno ya Mungu, na wale wote wanaoyakubali maneno ya Mungu wanapata nuru kwa kula na kunywa maneno Yake. Maneno yanenwayo na Mungu katika siku za usoni huwaongoza watu wa ulimwengu mzima; leo hii, maneno haya yanazungumzwa Uchina pekee, na hayawakilishi yale yanenwayo ulimwenguni kote. Mungu Atazungumza tu na ulimwengu mzima Ufalme wa Milenia ukija. Fahamu kuwa maneno yanenwayo na Mungu leo hii ni kuwafanya watu kuwa wakamilifu; maneno yanenwayo na Mungu katika hatua hii ni ya kuwapa watu mahitaji yao, si ya kukufanya ujue siri au kuiona miujiza ya Mungu. Kunena kwake kwa namna nyingi ni ili awapatie watu mahitaji yao. Enzi ya Ufalme wa Milenia haujafika bado—Enzi ya Ufalme wa Milenia inayozungumziwa ni siku ya utukufu wa Mungu. Baada ya kazi ya Yesu kule Uyahudi kukamilika, Mungu Aliihamishia kazi yake barani Uchina na kutengeneza mpango mwingine. Anaifanyia sehemu nyingine ya kazi Yake ndani yenu, Anafanya kazi ya kuwafanya watu wakamilifu kwa maneno, na kutumia maneno kuwafanya watu wapitie maumivu makali sana na pia kupata neema ya Mungu. Hii hatua ya kazi itaunda kundi la washindi na baada ya kuliunda kundi hili la washindi, wataweza kushuhudia matendo Yake, wataweza kuishi kwa kudhihirisha uhalisia, na kumtosheleza na kuwa waaminifu Kwake hadi kifo, na kwa njia hii Mungu Atatukuzwa. Mungu anapotukuzwa Atakapolifanya hili kundi la watu kuwa wakamilifu, itakuwa Enzi ya Ufalme wa Milenia.
Yesu Alikuwa duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, Alikuja kufanya kazi ya usulubisho na kupitia usulubisho, Mungu Alipata sehemu moja ya utukufu. Mungu Alipokuja katika mwili, Aliweza kunyenyekea na kujificha, na Aliweza kustahimili mateso makubwa. Japokuwa Alikuwa Mungu Mwenyewe, bado Alipitia kila aina ya fedheha, na kila aina ya matusi, na Alipitia uchungu mkubwa kwa kuangikwa msalabani ili kukamilisha kazi ya ukombozi. Baada ya hatua hii ya kazi kutamatishwa, japokuwa watu waliona kuwa Mungu Alikuwa Amepata utukufu mkubwa, huu haukuwa ukamilifu wa utukufu Wake; ilikuwa tu sehemu moja ya utukufu Wake ambao Alikuwa Amepata kutoka kwa Yesu. Japokuwa Yesu Aliweza kupitia magumu ya kila aina, kuwa Mnyenyekevu na kujificha, kusulubishwa kwa ajili ya Mungu, Mungu Alipata tu sehemu moja ya utukufu Wake, na utukufu Wake ulipatikana Israeli. Mungu bado Ana sehemu nyingine ya utukufu: kuja duniani kufanya kazi na kufanya kundi la watu kuwa wakamilifu. Wakati wa hatua ya kazi ya Yesu, Alifanya baadhi ya mambo ambayo si ya kawaida, ila ile hatua ya kazi kwa yoyote ile haikuwa tu ili kufanya ishara na maajabu. Kimsingi ilikuwa kuonyesha kuwa Yesu Angeweza kuteseka na kusulubishwa kwa ajili ya Mungu, kwamba Yesu Angeweza kupitia uchungu mkubwa kwa kuwa Alimpenda Mungu, na kwamba japokuwa Mungu Alimtelekeza, bado Alikuwa radhi kuyatoa maisha Yake kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Baada ya Mungu kukamilisha kazi Yake Israeli na Yesu Kuangikwa msalabani, Mungu Alitukuzwa, na Mungu Alikuwa na ushuhuda mbele ya Shetani. Hamjui na wala hamjaona jinsi Mungu Amekuwa mwili nchini Uchina, basi mnaonaje kuwa Mungu Ametukuzwa? Mungu Anapofanya kazi nyingi ya ushindi kwenu, na mnasimama imara, basi hii hatua ya kazi ya Mungu inakuwa ya mafanikio, na hii ni sehemu ya utukufu wa Mungu. Mnaliona hili tu na bado hamjafanywa na Mungu kuwa wakamilifu, bado hamjaitoa roho yenu kwa Mungu kikamilifu. Bado hamjauona huu utukufu kwa ukamilifu; mnaona tu kwamba Mungu Ameushinda moyo wenu tayari, kwamba hammuachi kamwe na kwamba mtamfuata Mungu mpaka mwisho na moyo wenu hautabadilika, na huo ndio utukufu wa Mungu. Ni katika kitu gani mnauona utukufu wa Mungu? Kwenye athari za kazi Yake kwa wanadamu. Watu huona kuwa Mungu anapendeza sana, wana Mungu mioyoni mwao, na hawako radhi kumuacha, na huu ni utukufu wa Mungu. Wakati ambapo uthabiti wa ndugu na dada wa makanisa unapotokea, na wanaweza kumpenda Mungu kutoka mioyoni mwao, na kuuona ukuu wa kazi inayofanywa na Mungu, ukuu usiomithilika wa maneno Yake, waonapo kwamba maneno yake yanabeba mamlaka na kwamba anaweza kuanzisha kazi Yake katika miji iliyohamwa katika bara ya Uchina, wakati ambapo, japo watu ni wanyonge, mioyo yao inasujudu mbele ya Mungu na wako radhi kuyakubali maneno ya Mungu, na wakati ambapo, japo ni wanyonge na wasiofaa, wanaweza kuona kuwa maneno ya Mungu ni ya kupendeza sana na yastahili utunzaji wao basi huu ndio utukufu wa Mungu. Siku ikija ambayo watu watafanywa wakamilifu na Mungu, na wanaweza kujisalimisha mbele Yake, na kuweza kumtii Mungu kabisa, na kuyawacha matarajio na majaliwa yao mikononi mwa Mungu, basi sehemu ya pili ya utukufu wa Mungu itakuwa imepatikana kikamilifu. Hii ni kusema kuwa wakati ambapo kazi ya Mungu wa vitendo itakapokuwa imekamilishwa kabisa, kazi Yake katika bara ya Uchina itafika kikomo; kwa maneno mengine, wakati wale walioamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu watakapokuwa wamefanywa wakamilifu, Mungu Atatukuzwa. Mungu Alisema kwamba Ameleta sehemu ya pili ya utukufu Wake Mashariki, na bado hili halionekani kwa macho. Mungu Ameleta kazi Yake Mashariki: tayari Amekuja Mashariki, na huu ni utukufu wa Mungu. Leo ingawa kazi yake haijakamilika bado, kwa sababu Mungu Ameamua kufanya kazi, bila shaka itakamilika. Mungu Ameamua kuwa Ataikamilishia kazi yake Uchina, na Ameamua kuwafanya kuwa wakamilifu. Hivyo Hawapatii njia nyingine—tayari Ameishinda mioyo yenu, na lazima utaendelea upende usipende, na mnapokubaliwa na Mungu, Mungu Anatukuzwa. Leo hii bado Mungu Hajatukuzwa kikamilifu, kwa sababu bado hujafanywa kuwa wakamilifu. Ingawa moyo wako umerudi kwa Mungu, bado kuna udhaifu mwingi katika mwili wako, hauna uwezo wa kumridhisha Mungu, huwezi kushughulishwa na mapenzi ya Mungu, na bado mna vitu vingi hasi ambavyo ni sharti muondokane navyo nab ado lazima mpitie majaribu na usafishaji mwingi. Ni kwa njia hiyo tu ndiyo tabia zenu za maisha zinaweza kubadilika na mnaweza kupatwa na Mungu.