Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu
Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu. Ingawa ni uamuzi wa watu kama hawa kumfuata Mungu, hawafaidi chochote. Wale wote wasiopata chochote kwenye mkondo huu ndio watakaoondolewa—wao wote hawana kazi. Haijalishi ni hatua gani ya kazi ya Mungu unayopitia, lazima uandamane na maono makuu. Bila maono kama haya, itakuwa vigumu kwako kukubali kila hatua ya kazi mpya, kwa maana mwanadamu hana uwezo wa kuwaza kuhusu kazi mpya ya Mungu, ni kuu kushinda mawazo ya mwanadamu. Kwa hivyo bila mchungaji kumlinda mwanadamu, bila mchungaji kushirikiana na mwanadamu kuhusu maono hayo, mwanadamu hana uwezo kukubali kazi hii mpya. Iwapo mwanadamu hawezi kupokea maono haya, basi hawezi kupata kazi mpya ya Mungu, na iwapo mwanadamu hawezi kutii kazi mpya ya Mungu, basi mwanadamu hana uwezo wa kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na hivyo ufahamu wake wa Mungu ni bure. Kabla mwanadamu atimilize maneno ya Mungu, lazima ayajue maneno ya Mungu, hivyo ni kusema, aelewe mapenzi ya Mungu; ni kwa njia hii tu ndiyo maneno ya Mungu yanaweza kutekelezwa kwa usahihi na kulingana na moyo wa Mungu. Hili lazima liwe na kila mmoja anayetafuta ukweli, na ndiyo njia ambayo lazima kila mmoja anayejaribu kumjua Mungu aipitie. Njia ya kuyajua maneno ya Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na pia njia ya kuijua kazi ya Mungu. Na hivyo, kujua maono hakuashirii tu kuujua ubinadamu wa Mungu mwenye mwili, lakini pia kunajumuisha kujua maneno na kazi ya Mungu. Kutokana na maneno ya Mungu wanadamu wanapata kuelewa mapenzi ya Mungu, na kutokana na maneno ya Mungu wanapata kuelewa tabia ya Mungu na pia kujua kile Mungu alicho. Imani katika Mungu ndiyo hatua ya kwanza katika kumjua Mungu. Harakati ya kusonga kutoka katika imani ya mwanzo katika Mungu mpaka imani kuu kwa Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na harakati ya kuipitia kazi ya Mungu. Iwapo unaamini kwa Mungu kwa ajili tu ya kuamini kwa Mungu, na huamini kwa Mungu kwa ajili ya kumjua Mungu, basi hakuna ukweli katika imani yako, na haiwezi kuwa safi—kuhusu hili hakuna tashwishi. Iwapo, wakati wa harakati anapopata uzoefu wa kazi ya Mungu mwanadamu anapata kumjua Mungu polepole, basi hatua kwa hatua tabia yake itabadilika pia, na imani yake itaongezeka kuwa ya kweli zaidi. Kwa njia hii, wakati mwanadamu anafaulu katika imani yake kwa Mungu, ataweza kumpata Mungu kwa ukamilifu. Mungu alijitoa pakubwa kuingia katika mwili mara ya pili na kufanya kazi Yake binafsi ili mwanadamu apate kumjua Yeye, na ili mwanadamu aweze kumwona. Kumjua Mungu[a] ndiyo matokeo ya mwisho yanayofikiwa katika mwisho wa kazi ya Mungu; ndilo hitaji la mwisho la Mungu kwa mwanadamu. Anafanya hili kwa ajili ya ushuhuda Wake wa mwisho, na ili kwamba mwanadamu mwishowe na kwa kikamilifu aweze kumgeukia Yeye. Mwanadamu anaweza tu kumpenda Mungu kwa kumjua Mungu, na ili ampende Mungu lazima amjue Mungu. Haijalishi vile anavyotafuta, au kile anachotafuta kupata, lazima aweze kupata ufahamu wa Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumridhisha Mungu. Ni kwa kumjua Mungu tu ndio mwanadamu anaweza kumwamini Mungu kwa ukweli, na ni kwa kumjua Mungu tu ndio anaweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Wale wasiomjua Mungu hawataweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Kumjua Mungu kunahusisha kujua tabia ya Mungu, kuelewa mapenzi ya Mungu, na kujua kile Mungu alicho. Na haijalishi ni kipengee gani cha kumjua Mungu, kila mojawapo kinamhitaji mwanadamu alipe gharama, na kinahitaji nia ya kutii, ambapo bila hivi hakuna atakayeweza kufuata mpaka mwisho. Kazi ya Mungu hailingani na mawazo ya mwanadamu hata kidogo, tabia ya Mungu na kile Mungu alicho ni vitu vigumu sana kwa mwanadamu kufahamu, na yote Anayosema na kufanya Mungu ni makuu sana yasiyoeleweka na mwanadamu; iwapo mwanadamu anatamani kumfuata Mungu, na hana nia ya kumtii Mungu, basi mwanadamu hatafaidi chochote. Tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa, Mungu Amefanya kazi nyingi ambayo haieleweki na mwanadamu na ambayo mwanadamu amepata ugumu kuikubali, na Mungu amesema mengi yanayofanya mawazo ya mwanadamu magumu kupona. Ilhali Hajawahi kukomesha kazi Yake kwa sababu mwanadamu ana ugumu mwingi; Ameendelea kufanya kazi na kuzungumza, na hata ingawa idadi kubwa ya “wanajeshi” wameangamia njiani, Yeye bado Anaendelea na kazi Yake, na bado anateua kundi baada ya kundi la watu walio tayari kukubali kazi Yake mpya. Yeye hawahurumii wale “mashujaa” walioangamia, na badala yake anawathamini wale wanaoikubali kazi Yake mpya na maneno. Lakini ni kwa sababu gani ndiyo Anafanya kazi kwa njia hii, hatua kwa hatua? Ni kwa nini Yeye kila mara huwaondoa na kuchagua watu wengine? Ni kwa nini Yeye hutumia mbinu za aina hii kila mara? Kusudi la kazi Yake ni ile wanadamu wapate kumjua, na ili waweze kutwaliwa na Yeye. Kanuni ya kazi Yake ni kufanya kazi kwa wale wanaoweza kutii kazi Anayofanya leo, na sio kufanya kazi kwa wale wanaotii kazi Yake ya zamani, na wanaipinga kazi Yake ya leo. Hii ndiyo sababu hasa Amewafuta na kuwaangamiza watu wengi.
Matokeo ya funzo la kumjua Mungu haliwezi kufikiwa kwa siku moja au mbili: Mwanadamu lazima apate uzoefu wa matukio mengi, apitie mateso, na awe na utiifu wa kweli. Kwanza kabisa, anza na kazi na maneno ya Mungu. Lazima uelewe kumjua Mungu kunajumuisha nini, jinsi ya kupata maarifa kuhusu Mungu, na jinsi ya kumwona Mungu katika matukio yako. Hili ndilo kila mtu lazima afanye wakiwa bado hawajamjua Mungu. Hakuna anayeweza kushika kazi na maneno ya Mungu kwa mara moja, na hakuna anayeweza kupata maarifa ya ukamilifu wa Mungu kwa muda mfupi. Kinachohitajika ni harakati mahususi ya matukio, na bila haya hakuna mwanadamu atakayeweza kumjua au kumfuata Mungu kwa kweli. Mungu Anapofanya kazi zaidi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kumjua. Zaidi kazi ya Mungu inavyokinzana na mawazo ya mwanadamu, ndivyo ufahamu wa mwanadamu Kwake unavyofanywa upya na wenye kina kirefu. Iwapo kazi ya Mungu ingebaki milele bila kubadilika, basi mwanadamu angekuwa tu na ufahamu mdogo wa Mungu. Kati ya uumbaji na wakati wa sasa, vitu ambavyo Mungu alifanya wakati wa Enzi ya Sheria, Alichofanya wakati wa Enzi ya Neema, na kile Afanyacho wakati wa Enzi ya Ufalme: lazima ujue vizuri sana maono haya. Lazima mjue kazi ya Mungu. Ni baada tu ya kumfuata Yesu ndio Petro alipata kujua polepole kuhusu kazi ambayo Roho alifanya ndani ya Yesu. Alisema, “Kutegemea matukio ya mwanadamu hakutoshi kufukia ufahamu kamili wa Mungu; Lazima kuwe na mambo mengi kutoka kwa kazi ya Mungu ya kutusaidia kumjua Mungu.” Mwanzoni, Petro aliamini kuwa Yesu alitumwa na Mungu, kama mtume, na hakumwona Yesu kama Kristo. Wakati huu, alipoanza kumfuata Yesu, Yesu Alimuuliza, “Simoni, mwana wa Yona, je, utanifuata?” Petro alisema, “Ni lazima nimfuate yule aliyetumwa na Baba wa mbinguni. Lazima nimtambue yule aliyechaguliwa na Roho Mtakatifu. Nitakufuata Wewe.” Kutoka kwa maneno Yake, inaonekana wazi kuwa Petro hakuwa na ufahamu kumhusu Yesu; alikuwa ameyapitia maneno ya Mungu, alikuwa amejikabili mwenyewe, na pia alikuwa amepitia ugumu kwa ajili ya Mungu, ilhali hakujua kazi ya Mungu. Baada ya muda wa uzoefu, Petro aliona ndani ya Yesu matendo mengi ya Mungu, aliona vile Mungu anavyopendeza, na aliona uwepo wa Mungu ndani ya Yesu. Vilevile, aliona kuwa maneno ya Yesu hayangeweza kuzungumzwa na mwanadamu, na kwamba kazi Aliyofanya Yesu haingefanyika na mwanadamu. Katika maneno ya Yesu na matendo Yake, zaidi ya hayo, Petro aliona wingi wa hekima ya Mungu, na kazi nyingi ya uungu. Wakati wa matukio yake, hakupata kujijua mwenyewe tu, ila alitilia maanani matendo ya Yesu, ambayo kutokana nayo aligundua mambo mengi mapya; kama vile, kwamba kulikuwa na maonyesho mengi ya Mungu wa matendo katika kazi ya Aliyofanya Mungu kupitia kwa Yesu, na kwamba maneno ya Yesu, matendo Yake, na jinsi Alivyoyachunga makanisa na kazi Aliyofanya ilitofautiana kabisa na mwanadamu wa kawaida. Hivyo, kutoka kwa Yesu Petro alijifunza mafunzo mengi aliyopaswa kusoma, na kufikia wakati Yesu Alikuwa karibu kusulubiwa, alikuwa amepata ufahamu kiasi kuhusu Yesu—ufahamu ambao ulikuwa msingi wa uaminifu wake wa maisha katika Yesu, na kusulubiwa kwake kichwa kikiwa chini ambako alipitia kwa ajili ya Bwana. Ingawa yeye alikuwa na fikira fulani na hakuwa na ufahamu kamili kuhusu Yesu mwanzoni, mambo kama haya bila shaka yanapatikana ndani ya wanadamu wapotovu. Alipokuwa karibu Anaondoka, Yesu Alimwambia Petro kwamba kusulubiwa Kwake ndiyo kazi Aliyokuja kufanya; Lazima Akataliwe na enzi hiyo, enzi hii nzee yenye uchafu lazima imsulubishe msalabani, na Alikuwa Amekuja kukamilisha kazi ya ukombozi, na, kwa kuwa Alikuwa ameikamilisha kazi hii, huduma Yake ilikuwa imekamilika. Aliposikia haya, Petro alipatwa na huzuni, na akampenda Yesu sana hata zaidi. Yesu Aliposulubiwa msalabani, Petro alilia kwa uchungu akiwa peke yake. Kabla ya hili, alikuwa amemuuliza Yesu, “Ee Bwana! Unasema kwamba unaenda kusulubiwa. Baada ya Wewe kwenda, tutakuona tena lini?” Je, hakuna mchanganyiko katika maneno Aliyozungumza? Je, hakuna fikira zake pale ndani? Moyoni mwake, alijua kuwa Yesu Alikuja kukamilisha sehemu ya kazi ya Mungu, na kwamba baada ya Yesu kuondoka, Roho angekuwa pamoja naye; ingawa Angesulubiwa na Apae mbinguni, Roho wa Mungu Angekuwa pamoja naye. Wakati huo, alikuwa na ufahamu kiasi kumhusu Yesu, na kujua kwamba Alitumwa na Roho wa Mungu, kwamba Roho wa Mungu Alikuwa ndani Yake, na kwamba Yesu Alikuwa Mungu Mwenyewe, Alikuwa Kristo. Lakini kwa sababu ya upendo wake kwa Yesu, na kwa sababu ya udhaifu wa mwanadamu, bado Petro alisema maneno hayo. Ikiwa unaweza kutilia maanani na kupitia matukio ya hali ya juu katika kila hatua ya kazi ya Mungu, basi utaweza kuutambua uzuri wa Mungu hatua kwa hatua. Na maono ya Paulo yalikuwa yapi? Yesu Alipomwonekania, Paulo alisema, “Wewe ni nani, Bwana?” Yesu Akasema, “Mimi ndimi Yesu ambaye wewe unamtesa.” Haya ndiyo yalikuwa maono ya Paulo. Petro alitumia kufufuka kwa Yesu na kuonekana Kwake kwa siku arubaini, na mafunzo ya Yesu wakati wa maisha Yake, kama maono yake mpaka alipofika mwisho wa safari yake.
Mwanadamu hutambua kazi ya Mungu, hupata kujijua mwenyewe, hujitoa katika tabia yake potovu, na kutafuta kukua katika maisha yote kwa ajili ya kumjua Mungu. Ukitafuta kujijua mwenyewe tu na kujishughulisha tu na tabia yako potovu, na huna ufahamu ni kazi gani Mungu Anafanya kwa mwanadamu, kuhusu jinsi wokovu Wake ulivyo mkuu, au jinsi unavyojua kazi ya Mungu na kushuhudia matendo Yake, basi matukio yako hayana maana. Iwapo unafikiri kuwa kuweza kuuweka ukweli katika matendo, na kuwa na uwezo wa kuvumilia kunamaanisha maisha ya mtu yamekua, basi hii ina maana kuwa bado huelewi maana kamili ya Maisha au huelewi kusudi la Mungu la Kufanya kazi ya kumkamilisha mwanadamu. Siku moja, ukiwa katika makanisa ya kidini, miongoni mwa wanachama wa Kanisa la Toba au Kanisa la Uzima, utakutana na watu wengi wenye imani ambao maombi yao yana maono, na wanaohisi kuguzwa na walio na maneno ya kuwaongoza katika kuendelea kwao na maisha. Aidha, kwa mambo mengi wanaweza kuvumilia, na kujitelekeza wenyewe, bila kuongozwa na mwili. Wakati huo, hutaweza kujua tofauti: Utaamini kuwa kila wanachofanya ni sawa, kuwa ni udhihirisho wa kawaida wa maisha, lakini ni jambo la kusikitisha kweli kuwa jina wanaloamini si sahihi. Je imani kama hizi si pumbavu? Ni kwa nini inasemekana kuwa watu wengi hawana maisha? Ni kwa sababu hawamjui Mungu, na hivyo inasemekana kuwa hawana Mungu mioyoni mwao, na hawana uhai. Iwapo imani yako kwa Mungu imefikia kiwango fulani ambapo unaweza kwa kikamilifu kuyafahamu matendo ya Mungu, ukweli wa Mungu, na kila hatua ya kazi ya Mungu, basi umejawa na ukweli. Iwapo hujui kazi na tabia ya Mungu, basi uzoefu wako bado ni wa chini. Jinsi Yesu Aliifanya hatua ile ya kazi Yake, jinsi hatua hii inavyoendelezwa, jinsi Mungu Alifanya kazi Yake katika enzi ya Neema na ni kazi ipi iliyofanywa, ni kazi ipi inafanyika katika hatua hii—iwapo huna ufahamu kamilifu wa mambo haya, basi hutawahi kuondokewa na wasiwasi na utakuwa na shaka. Iwapo, baada ya kipindi cha uzoefu, wewe unaweza kujua kazi inayofanywa na Mungu na kila hatua ya kazi ya Mungu, na unao ufahamu mkuu wa malengo ya maneno ya Mungu, na ni kwa nini maneno mengi yaliyozungumzwa na Yeye hayajatimika bado, basi unaweza kutulia na kuendelea katika safari iliyo mbele yako, ukiwa huru kutokana na wasiwasi na kusafishwa. Mnapaswa kuona kile Mungu anatumia wingi wa kazi Yake. Yeye hutumia maneno Anayozungumza, akimsafisha mwanadamu na kuyabadilisha mawazo ya mwanadamu kupitia maneno mengi tofauti. Mateso yote ambayo mmestahimili, kusafishwa kote ambako mmepitia, kushughulikiwa ambako mmekukubali ndani yenu, kupata nuru ambako mmeona—yote yamefanikishwa kutumia maneno Aliyozungumza Mungu. Ni kwa sababu ya nini ndio mwanadamu anamfuata Mungu. Ni kwa sababu ya maneno ya Mungu! Maneno ya Mungu ni yenye mafumbo makuu, na yanaweza kuuguza moyo wa mwanadamu, kufunua vitu vilivyo ndani ya moyo wa mwanadamu, yanaweza kumfanya ajue vitu vilivyotendeka zamani, na kumruhusu kuona katika siku za usoni. Na kwa hivyo mwanadamu anavumilia mateso kwa sababu ya maneno ya Mungu, na anafanywa mkamilifu kwa sababu ya maneno ya Mungu, na ni baada ya hapo tu ndipo mwanadamu anamfuata Mungu. Anachostahili kufanya mwanadamu katika hatua hii ni kukubali maneno ya Mungu, na haijalishi kama amefanywa mkamilifu, au kusafishwa, kilicho cha muhimu ni maneno ya Mungu; hii ni kazi ya Mungu, na ni maono ambayo mwanadamu lazima ayajue leo hii.
Mungu Anamfanyaje mwanadamu kuwa kamili? Tabia ya Mungu ni gani? Na ni nini kilicho ndani ya tabia Yake? Ili kuyabainisha mambo haya yote: mtu huliita kusambaza jina la Mungu, mtu huliita kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na mtu huliita kumtukuza na kumsifu Mungu, na bila shaka mwanadamu atafikia mabadiliko katika tabia ya maisha yake kwa msingi wa kumjua Mungu. Kadri mwanadamu anavyopitia kushughulikiwa na kusafishwa, ndivyo nguvu yake inavyoongezeka zaidi, na hatua za Mungu zinavyozidi kuwa nyingi, ndivyo mwanadamu anavyofanywa kamili. Leo, katika uzoefu wa mwanadamu, kila hatua ya kazi ya Mungu inayagonga mawazo ya mwanadamu, na kila hatua haiwezi kuwazwa na akili ya mwanadamu, na kuzidi matarajio ya mwanadamu. Mungu Anakimu mahitaji yote ya mwanadamu, na kwa kila njia yote huwa yanakinzana na mawazo ya mwanadamu, na ukiwa mdhaifu, Mungu Ananena maneno Yake. Ni kwa njia hii tu ndio Anaweza kukupa uhai wako. Kwa kuzigonga fikira zako, unakuja kukubali kazi ya Mungu, na kwa njia hii pekee ndio unaweza kuondoa upotovu wako. Leo hii, kwa upande mmoja Mungu mwenye mwili Anafanya kazi katika uungu, na kwa upande mwingine Anafanya kazi katika ubinadamu wa kawaida. Unapoacha kuweza kukana kazi yoyote ya Mungu, unapoweza kutii bila kujali lolote Analosema Mungu au kufanya katika hali ya ubinadamu wa kawaida, unapoweza kutii na kuelewa bila kujali ni ukawaida wa aina gani Anadhihirisha: ni wakati huo tu ndio unaweza kuwa na uhakika kwamba Yeye ni Mungu, na ni hapo tu utakoma kuwa na dhana, na ni hapo tu ndio utaweza kumfuata mpaka mwisho. Kuna hekima katika kazi ya Mungu, na Anajua jinsi mwanadamu Anaweza kuwa na ushuhuda Kwake. Anajua pale ambapo udhaifu wa uhai wa mwanadamu upo, na maneno Anayozungumza yanaweza kukugonga pale penye udhaifu wako upo, lakini pia Anatumia maneno Yake makuu na yenye busara kukufanya uwe na ushuhuda Kwake. Hayo ndiyo matendo ya kimiujiza ya Mungu. Kazi inayofanywa na Mungu haiwezi kufikiriwa na akili ya mwanadamu. Hukumu ya Mungu inafunua aina za upotovu ambazo mwanadamu, kwa kuwa ni mwili, amejawa nao, na vitu vipi ndivyo umuhimu wa mwanadamu, na humwacha mwanadamu bila mahali pa kujificha aibu yake.
Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake ya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu kosa lolote, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu wa hadharani. Mabadiliko yanafanikishwa kwa tabia ya mwanadamu kupitia njia tofauti ya kazi ya Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangekuwa wa kuupendeza moyo wa Mungu. Mabadiliko katika tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amejiweka huru kutokana na minyororo ya Shetani, amejiweka huru kutokana na ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kifaa cha kujaribiwa cha kazi ya Mungu, amekuwa shahidi wa kweli wa Mungu na mtu aliye wa kuupendeza moyo wa Mungu. Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja kufanya kazi Yake duniani, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, aweze kumtii, awe na ushuhuda Kwake—aweze kujua kazi Yake ya matendo na ya kawaida, atii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote ya kumwokoa mwanadamu, na matendo yote Anayofanya ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni aina hii tu ya ushuhuda ndio ulio sahihi, na wa kweli, na ni aina hii tu ya ushuhuda ndio unaoweza kumpa Shetani aibu. Mungu Anawatumia wale waliomjua baada ya kupitia hukumu Yake na kuadibu, ushughulikiaji na upogoaji, kuwa na ushuhuda Kwake. Anawatumia wale waliopotoshwa na Shetani kumtolea Yeye ushuhuda, na vilevile Anawatumia wale ambao tabia yao imebadilika, na wale basi ambao wamepokea baraka Zake, kumtolea ushuhuda. Yeye hana haja na mwanadamu kumsifu kwa maneno tu, wala hana hitaji lolote la sifa na ushuhuda kutoka kwa namna ya Shetani, ambao hawajaokolewa na Yeye. Ni wale tu wanaomjua Mungu ndio wanaohitimu kumtolea Mungu ushuhuda, na ni wale tu ambao tabia zao zimebadilika ndio wanaofaa kumshuhudia Mungu, na Mungu hatamruhusu mwanadamu kwa makusudi aliletee jina Lake aibu.
Tanbihi:
a. Nakala ya kwanza inasema “Kazi ya kumjua Mungu.”