Njia … (8)
Haijakuwa tu siku moja au mbili tangu Mungu aje duniani kushirikiana na wanadamu, kuishi na watu. Pengine, wakati huu wote watu wamemjua Mungu kwa kiwango fulani, na labda wamepata utambuzi muhimu wa kumhudumia Mungu, na wamepata uzoefu sana katika imani yao katika Mungu. Hata iweje, watu wanaelewa vizuri sana tabia ya Mungu, na maonyesho ya kila aina ya tabia za binadamu yanatofautiana kwa kweli. Jinsi Nionavyo, maonyesho tofautitofauti ya watu yanatosha kwa Mungu kuyatumia kama sampuli, na shughuli zao za fikira zinatosha kwa Yeye kurejelea. Labda hii ni hali moja ambayo kwayo wanadamu hushirikiana na Mungu, ni ushirikiano usiokusudiwa wa mwanadamu na Mungu, ili utekelezaji huu unaoelekezwa na Mungu uwe wa kupendeza na wenye uhai, dhahiri sana. Ninasema mambo haya kwa ndugu zangu kama mwelekezaji mkuu wa mchezo huu wa kuigiza—kila mmoja wetu anaweza kunena na fikira na hisia zake baada ya kuliigiza hili, na kuzungumza kuhusu vile kila mmoja wetu anayapitia maisha yake ndani ya mchezo huu wa kuigiza. Huenda ikawa vyema kwa sisi kuwa na aina mpya kabisa ya kongamano ili kuifungua mioyo yetu na kuzungumza kuhusu sanaa yetu ya maonyesho, tuone vile Mungu atamwongoza kila mtu ili katika utambaji unaofuata tuweze kuonyesha kiwango cha juu zaidi cha sanaa yetu na kila mtu aweze kuigiza sehemu yake mwenyewe kwa kiasi kikuu zaidi iwezekanavyo, bila kutomridhisha Mungu. Natumai kwamba ndugu Zangu wataweza kulitilia hili maanani—hakuna anayeweza kulipuuza kwa sababu kuigiza sehemu fulani vizuri si jambo linaloweza kutimizwa katika siku moja au mbili. Linahitaji tuyapitie maisha na kuingia ndani kabisa katika maisha yetu halisi kwa kipindi kirefu, na kuwa na uzoefu wa utendaji wa aina mbalimbali za maisha. Ni wakati huo tu ndipo tunaweza kwenda juu ya jukwaa. Nimejawa tumaini kwa ajili ya ndugu Zangu, na Naamini kwamba hamjavunjika moyo wala kukata tamaa, na haijalishi kile ambacho Mungu anafanya, ninyi ni kama chungu chenye moto—huwa hamna uvuguvugu kamwe na mnaweza kushikilia mpaka mwisho, mpaka kazi ya Mungu ifichuliwe kwa ukamilifu, na mpaka mchezo wa kuigiza ambao Mungu anaelekeza ufike katika hitimisho la mwisho wake. Sina matakwa mengine kwenu. Kila Ninachotumai ni kwamba muweze kuendelea kushikilia, kwamba musiwe na wasiwasi kwa ajili ya matokeo, kwamba mshirikiane na Mimi ili kazi Ninayopaswa kufanya ifanyike vizuri, na kwamba hakuna atakayesababisha pingamizi au usumbufu. Sehemu hii ya kazi ikishatimizwa, Mungu atawafichulia ninyi kila kitu. Baada ya kazi Yangu kutimizwa, Nitawasilisha sifa njema yenu mbele ya Mungu kutoa maelezo Kwake. Je, hilo si bora? Tunaweza kusaidiana kutimiza malengo yetu wenyewe. Je, hili si suluhisho kamili kwa kila mtu? Huu ni wakati mgumu unaowahitaji mlipe gharama. Kwa sababu Mimi ndiye mwelekezi sasa, Natumai kwamba hakuna mmoja wenu aliyekerwa. Hii ndiyo kazi ambayo Ninafanya. Labda kutakuweko na siku moja ambapo Nitahamia kwa “kitengo cha kazi” cha kufaa na Nisifanye tena mambo yawe magumu kwenu. Nitawaonyesha ninyi chochote mnachopenda kuona, na pia Nitawakamilisha ninyi katika chochote mnachopenda kusikia. Lakini sio sasa—hii ni kazi ya leo na siwezi kuwapa uhuru kwa hulka zenu na kuwaruhusu kufanya chochote mnachotaka kufanya. Hivyo, kazi Yangu haingekuwa rahisi kufanya. Kusema kweli, hilo halingezaa matunda yoyote na halingekuwa la manufaa kwenu. Kwa hiyo sasa mnahitaji “kupitia magumu,” na siku ifikapo ambapo hatua hii ya kazi Yangu itakuwa imetimizwa Nitakuwa huru. Sitaubeba mzigo mzito kama huu, na Nitakubali chochote mtakachoomba kutoka Kwangu; maadamu tu ni cha manufaa kwa maisha yenu Nitatimiza maombi yenu. Nimechukua sasa jukumu zito. Siwezi kwenda kinyume cha amri za Mungu Baba, na Siwezi kuvuruga mipango ya kazi Yangu. Siwezi kusimamia mambo Yangu binafsi kupitia kwa mambo ya biashara Yangu. Natumai nyote mnaweza kunielewa na kunisamehe Mimi kwa sababu kila kitu Nifanyacho kinalingana na kusudi la Mungu Baba. Nafanya chochote Atakacho Nifanye haijalishi Anachotaka, na Siko radhi kuchochea hasira Yake au ghadhabu Yake. Mimi hufanya tu Ninachopaswa kufanya. Kwa hiyo kwa niaba ya Mungu Baba, Ninawashauri ninyi mvumilie tu kwa muda mrefu kidogo. Mtu yeyote asiwe na wasiwasi. Baada ya Mimi kutimiza Ninachotaka kufanya, mnaweza kufanya chochote mtakacho na kuona chochote mpendacho, lakini lazima Nitimize kazi Ninayohitaji kutimiza.
Katika hatua hii ya kazi sisi tunatakiwa kuwa na imani kuu na upendo mkuu. Huenda tukajikwaa kutokana na uzembe kidogo kabisa kwa sababu hatua hii ya kazi ni tofauti na zile zote za awali. Kile ambacho Mungu anakamilisha ni imani ya wanadamu—mtu hawezi kuiona au kuigusa. Kile ambacho Mungu anafanya ni kuyageuza maneno kuwa imani, kuwa upendo, na kuwa uzima. Watu lazima wafikie kiwango ambacho wamestahimili mamia ya kusafisha na wawe na imani iliyo kuu zaidi kuliko ya Ayubu. Wanatakiwa kustahimili taabu ya ajabu sana na aina zote za mateso bila kuondoka kwa Mungu wakati wowote. Wanapokuwa watiifu hadi kufa, na wawe na imani kuu katika Mungu, basi hatua hii ya kazi ya Mungu imetimizwa. Ni kazi hii ndiyo Nimekubali kuifanya, kwa hiyo Natumai kwamba ndugu Zangu wanaweza kuelewa matatizo Yangu na hawana matakwa yoyote zaidi Kwangu. Haya ni matakwa ya Mungu Baba Kwangu na Siwezi kuepuka uhalisi huu. Lazima Nifanye kazi Ninayopaswa kufanya. Yote Ninayotumai ni kwamba msiwe bila busara, kwamba mpate utambuzi zaidi na msiyatazame masuala kwa urahisi sana. Fikira zenu ni za kitoto sana, za kijinga sana. Kazi ya Mungu sio rahisi kama mnavyoweza kufikiri, kwamba Anafanya tu chochote Atakacho kufanya. Ingekuwa hali ni hiyo mpango Wake ungeangamizwa. Hamngesema hivyo? Ninafanya kazi ya Mungu. Siwafanyii tu watu kazi zisizo za kawaida, kufanya chochote Ninachohisi kufanya na kupanga binafsi iwapo Nitafanya kitu au la. Sio rahisi vile sasa hivi. Nimetumwa na Baba kutenda kama mwelekezi—mnafikiri kwamba Nilipanga na kuchagua hili Mwenyewe? Maoni ya mwanadamu wakati mwingi yanaelekea kukatiza kazi ya Mungu, ndiyo maana, baada ya Mimi kufanya kazi kwa kipindi cha muda fulani, kuna maombi mengi kutoka kwa watu ambayo Sijaweza kutimiza na watu wote wamebadilisha mawazo yao kunihusu Mimi. Nyote mnapaswa kuelewa mawazo haya mliyonayo—Sina haja ya kuyataja moja kwa moja. Siwezi kufanya chochote ila kufafanua kazi Niifanyayo; hisia Zangu haziumizwi na hili katu. Mara tu mkishaelewa hilo, mnaweza kulichukulia vyovyote mtakavyo. Sitatoa pingamizi zozote kwa sababu hivi ndivyo Mungu hufanya kazi. Sishurutishwi kueleza yote. Nimekuja tu kutekeleza kazi ya maneno, kufanya kazi na kuruhusu uigizaji huu uendelee kwa mwelekeo wa maneno. Sihitaji kusema mengi kuhusu mengine, na Siwezi kufanya jambo lingine lolote. Nimeeleza kila kitu Ninachotakiwa kusema. Chochote mnachofikiria kukihusu ni sawa, na haijalishi Kwangu. Lakini bado Ningependa kuwakumbusha ninyi kwamba kazi ya Mungu si rahisi kama mnavyoifikiria kuwa. Kadri isivyolingana na fikira za watu ndivyo umuhimu wake ulivyo wa kina, na kadri inavyolingana na fikira za watu, ndivyo isivyokuwa na thamani, na bila umuhimu halisi. Fikirieni maneno haya kwa makini—Nasema tu kitu hiki kimoja kuhusu hilo, na ninyi wenyewe mnaweza kuchambua mengine. Sitafanya ufafanuzi wowote.
Watu hufikiri kwamba Mungu hufanya mambo kwa njia fulani, lakini kwa mwaka huu uliopita au zaidi, je, kile ambacho tumeona na kupitia kuhusu kazi ya Mungu kimelingana kweli na fikira za binadamu? Tangu uumbaji wa ulimwengu mpaka sasa, hakuna hata mtu mmoja ambaye ameweza kugundua hatua au sheria za kazi ya Mungu. Ikiwa wangeweza, ni kwa nini wale viongozi wa kidini hawatambui kwamba Mungu wakati wa sasa anafanya kazi kwa njia hii? Ni kwa nini watu wachache sana wanaelewa uhalisi wa leo? Kutokana na hili tunaweza kuona kwamba hakuna anayeielewa kazi ya Mungu—watu wanaweza tu kufanya mambo kulingana na uongozi wa Roho Wake, lakini hawawezi tu kutumia sheria kwa imara kwa kazi Yake. Ukichukua mfano na kazi ya Yesu na kuilinganisha na kazi ya Mungu ya sasa, ni kama vile watu wa Kiyahudi wakijaribu kumlinganisha Yesu na Yehova. Je, huku sio kupata hasara? Hata Yesu hakujua kazi ya Mungu katika siku za mwisho ingekuwa ipi; yote Aliyojua ni kwamba kile Alichohitaji kutimiza kilikuwa ni kazi ya kusulubiwa, kwa hiyo wengine wangejuaje? Wangejuaje ni kazi gani ambayo Mungu angeifanya katika siku za usoni? Mungu angefichuaje mipango Yake kwa wanadamu, ambao wamemilikiwa na Shetani? Je, huo si upumbavu? Kile ambacho Mungu anakuruhusu kujua na kuelewa ni mapenzi Yake. Hakuruhusu wewe ufikirie juu ya kazi Yake ya siku za usoni. Tunahitaji kujishughulisha tu na imani ndani ya Mungu, kutenda kwa mwongozo Wake kuwa wenye vitendo kwa utatuzi wa matatizo halisi na, na kutofanya mambo kuwa magumu kwa Mungu au kumletea Yeye matatizo. Tunapaswa tu kwenda kufanya tunachopaswa kufanya—maadamu tunaweza kuwa katika kazi ya Mungu ya wakati uliopo hiyo inatosha! Hii ni njia Ninayowaongoza nyinyi kwayo. Tunapaswa kuendelea mbele, na Mungu hatamtesa yeyote kati yetu. Katika mwaka huu uliopita wa uzoefu wenu wa ajabu mmepata mambo mengi sana; Naamini kwamba hamtafadhaishwa sana. Njia Ninayowaelekeza kwayo ni kazi Yangu, wajibu Wangu, na iliamriwa na Mungu kitambo sana ili tuweze kuamuliwa kabla kufika umbali huu, hadi leo—kwamba tumeweza kufanya hili ni baraka yetu kubwa, na ingawa haijakuwa njia rahisi, urafiki wetu ni wa milele, na utapitishwa moja kwa moja katika enzi. Kama zilikuwa nderemo na kicheko au huzuni na machozi, acha zote ziwe kumbukumbu nzuri! Yawezekana unajua kwamba siku za kazi Yangu ni chache. Nina miradi mingi sana ya kazi, na Siwezi kuandamana nanyi mara kwa mara. Natumai mnaweza kunielewa Mimi—kwa sababu urafiki wetu wa asili bado uko vilevile. Labda siku moja Nitaonekana kwa mara nyingine mbele yenu, na Natumai kwamba hamtafanya mambo yawe magumu Kwangu. Hata hivyo, Mimi ni tofauti nanyi. Nasafiri kwenda kote kwa ajili ya kazi Yangu, na Siishi maisha Yangu kwa kupumzika tu kivivu katika hoteli nyingi. Bila kujali vile mlivyo, Mimi hufanya tu Ninachopaswa kufanya. Natumai kwamba mambo tuliyoshirikiana hapa awali yatakuwa kipeo cha uzuri wa urafiki wetu.
Inaweza kusemwa kwamba hii njia ilifunguliwa na Mimi, na kama ni chungu au tamu, Nimeiongoza njia. Kuweza kwetu kuendelea mpaka wakati wa sasa yote imekuwa ni kwa sababu ya neema ya Mungu. Huenda kukawa na wengine wanaonishukuru Mimi, na huenda kukawa na wengine wanaolalamika dhidi Yangu, lakini hakuna lililo muhimu kati ya hayo. Yote Nitakayo kuona ni kwamba kinachopaswa kutimizwa katika kundi hili la watu kimetimizwa. Hili linapaswa kusherehekewa. Kwa hiyo, sina kisasi dhidi ya wale wanaolalamika dhidi Yangu; yote Nitakayo ni kutimiza kazi Yangu haraka iwezekanavyo ili moyo wa Mungu uweze kuwa na raha hivi punde. Wakati huo Sitaubeba mzigo wowote mzito, na hakutakuwa na wasiwasi ndani ya moyo wa Mungu. Je, mko radhi kushirikiana kwa njia iliyo bora? Je, kufanya kazi ya Mungu vizuri sio lengo bora kwa ajili ya mapambano yetu? Inaweza kusemwa kweli kwamba tumepitia taabu nyingi na kupitia furaha na huzuni yote katika kipindi hiki cha wakati, na kwa jumla, utendaji wa kila mtu umekuwa takriban wa wastani. Labda, siku zijazo kutakuwa na kazi bora mtakayotakiwa kufanya, lakini msikawie katika kuwaza juu Yangu; fanyeni tu mnachopaswa. Ninachohitaji kufanya kinakaribia kufika mwisho, na Natumai kwamba mtakuwa waaminifu wakati wote na kwamba hamtakuwa wenye hamu ya mambo yaliyozoewa kuhusu kazi Yangu. Mnapaswa kujua kwamba Nimekuja tu kutimiza hatua moja ya kazi, bila shaka sio kufanya kazi yote ya Mungu. Hili ni jambo mnalotakiwa kuelewa. Msiwe na maoni mengine kulihusu. Kazi ya Mungu inahitaji njia nyingi zaidi ili iweze kukamilika; hamwezi kunitegemea Mimi kila mara. Labda mliona zamani sana kwamba Ninachofanya ni sehemu moja tu ya kazi hiyo; haimwakilishi Yehova au Yesu. Kazi ya Mungu imegawanywa katika hatua nyingi, kwa hivyo msiwe wagumu sana. Wakati Ninapofanya kazi lazima mnisikilize Mimi. Kazi ya Mungu imekuwa tofauti katika kila enzi moja; haibaki vilevile, na sio tu wimbo ule ule wa zamani unaoimbwa. Kuna kazi Yake ambayo ni ya kufaa kwa kila hatua na hubadilika pamoja na hatua hizo. Kwa vile umezaliwa katika enzi hii, lazima ule na kunywa maneno ya Mungu na kuyasoma maneno Yake. Siku huenda ikaja ambapo kazi Yangu itabadilika, ambapo kutokana nayo ni lazima mwendelee kwenda mbele jinsi mnavyopaswa kufanya. Kazi ya Mungu kamwe haiwezi kuwa na dosari. Ustilie maanani jinsi ulimwengu wa nje unavyobadilika; Mungu hawezi kuwa mwenye makosa na kazi Yake haiwezi kuwa yenye makosa. Ni kwamba tu wakati mwingine kazi ya Mungu ya zamani hupita na kazi Yake mpya huanza; hata hivyo, haiwezi kusemwa kwamba kwa vile kazi mpya imekuja kazi ya zamani ni yenye makosa. Hiyo ni hoja ya uwongo! Kazi ya Mungu haiwezi kusemekana kuwa ni sahihi au yenye kosa, inaweza tu kusemekana kuwa ya mwanzoni au ya baadaye. Huu ni mwongozo wa imani ya watu katika Mungu na hauwezi bila shaka kupuuzwa.