Kwenye Hatua za Kazi ya Mungu

Kutoka nje, inaonekana kwamba hatua za kazi ya sasa ya Mungu tayari zimekamilika, na mwanadamu tayari amehukumiwa, kuadibiwa, kuangamizwa na kusafishwa na maneno ya Mungu, na amepitia hatua hizi kama majaribio ya watendaji huduma, usafishaji wa wakati wa kuadibu, majaribio ya kifo, majaribio ya foili[a], na wakati wa kumpenda Mungu. Bado licha ya kupitia mateso makubwa katika kila hatua, watu wamebaki kutojua mapenzi ya Mungu. Kwa mfano, fikiria majaribio ya watendaji huduma: Bado hawaelewi kile walichopata, kile walichokuja kujua, na matokeo ambayo Mungu alitaka kutimiza. Tukiangalia kasi ya kazi ya Mungu, mwanadamu anaonekana hawezi kabisa kuwa sambamba na kasi ya leo. Inaweza kuonekana kwamba Mungu kwanza anamfichulia mwanadamu hatua hizi za kazi Yake leo, na kwamba badala ya kutimiza kiwango ambacho mwanadamu anafikiria kinawezekana katika zozote kati ya sehemu hizi, Anaangazia suala fulani. Kwa Mungu kumkamilisha mtu ili aweze kupatwa na Yeye kwa kweli, lazima Atekeleze hatua hizi zote zilizotajwa juu. Lengo la kufanya kazi hii ni kuonyesha ni hatua zipi ambazo Mungu lazima atekeleze ili Akamilishe kikundi cha watu. Hivyo, tukiangalia kutoka nje, hatua za kazi ya Mungu zimekamilika—lakini kimsingi, ndipo Ameanza tu rasmi kuwakamilisha wanadamu. Watu wanapaswa kuelewa hili: Ni hatua za kazi Yake ambazo zimekamilika, lakini kazi yenyewe bado haijahitimika. Lakini katika dhana zao, watu huamini kwamba mwanadamu amefichuliwa hatua zote za kazi ya Mungu, na kwa hiyo hakuwezi kuwa na shaka kwamba kazi ya Mungu imekamilika. Njia hii ya kuyachukulia mambo ni yenye makosa kabisa. Kazi ya Mungu huenda kinyume na dhana za mwanadamu na huzipiga dhana kama hizi katika kila suala; hatua za kazi ya Mungu hasa ni tofauti na dhana za mwanadamu. Haya yote yanaonyesha hekima ya Mungu. Inaweza kuonekana kwamba dhana za mwanadamu zinasababisha vurugu mara kwa mara, na Mungu hukabili kila kitu ambacho mwanadamu hufikiria, jambo linalokuwa dhahiri wakati wa uzoefu halisi. Kila mtu hufikiri kwamba Mungu hufanya kazi haraka mno, na kwamba kazi ya Mungu hukamilika kabla ya wao kujua, kabla ya wao kupata ufahamu wowote na wakati ambapo bado wako katika hali ya kukanganywa. Hivyo ndivyo ilivyo katika kila hatua ya kazi Yake. Watu wengi sana huamini kwamba Mungu anawachezea watu—lakini hilo silo kusudi la kazi Yake. Mbinu Yake ya kufanya kazi ni ya kutafakari: kwanza kwa kuyakagua mambo kwa juu juu, kisha kuyachunguza kwa utondoti, na baada ya hapo kurekebisha maelezo haya kikamilifu—jambo ambalo huwapata watu wasipotarajia. Watu hujaribu kumdanganya Mungu, wakifikiri kwamba wakiendelea tu kuishi hadi kiwango fulani, Mungu ataridhishwa. Kwa kweli, Mungu anawezaje kuridhishwa na majaribu ya mwanadamu ya kuendelea kuishi? Ili kutimiza matokeo bora kabisa, Mungu hufanya kazi kwa kuwafumania watu, kwa kuchukua hatua wakati ambapo hawajui; hili huwapa ufahamu mkubwa zaidi wa hekima Yake, na ufahamu mkubwa zaidi wa haki na uadhama Wake na tabia Yake isiyokosewa.

Leo, Mungu ameanza rasmi kumkamilisha mwanadamu. Ili wafanywe wakamilifu, lazima watu wapitie ufunuo, hukumu na kuadibiwa na maneno Yake, lazima wajaribiwe na kusafishwa na maneno Yake (kama vile majaribio ya watendaji huduma), na lazima waweze kuvumilia majaribio ya kifo. Maana ya hili ni kwamba wakiwa katikati ya hukumu, kuadibu na majaribio ya Mungu, mtu anayetenda mapenzi ya Mungu kweli anaweza kutoa sifa kutoka katika kina cha moyo wake katikati ya hukumu, kuadibu na majaribu ya Mungu, mtu mkamilifu yuko hivi, na hii hasa ndiyo kazi ambayo Mungu ananuia kufanya, na kazi ambayo Atakamilisha. Watu hawapaswi kufanya uamuzi kuhusu mbinu ambazo kwazo Mungu hufanya kazi bila kufikiria. Wanapaswa tu kufuatilia kuingia katika maisha. Hili ni jambo la muhimu. Usichunguze mbinu ya kazi ya Mungu daima; hili litazuia tu matarajio yako ya baadaye. Umeona kiasi kipi cha mbinu ambayo kwayo Mungu anafanya kazi? Umekuwa mtiifu kiasi kipi? Umepata kiasi kipi kutoka kila kwa mbinu ya kazi Yake? Je, uko radhi kukamilishwa na Mungu? Je, ungetaka kukamilishwa? Haya yote ni mambo ambayo unapaswa kuyaelewa vizuri na kuyaingia.

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini

Inayofuata: Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp