Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Kasi

Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Uzima wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii kumefanyika kulingana na hali zinazozunguka ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova hakuwa amepanga bado awamu ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; awamu ya pili ya kazi, ile ya neema; au awamu ya tatu ya kazi, ile ya kushinda, ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi vya Moabu, na kuanzia hapa Angeweza kushinda ulimwengu mzima. Hakuyaongea maneno haya baada ya kuumba ulimwengu; Hakuyaongea maneno haya baada ya Moabu, wala hata kabla ya Lutu. Kazi yake yote ilifanywa bila kupangwa. Hivi ndivyo hasa kazi Yake nzima ya usimamizi ya miaka elfu sita imeendelea; kwa vyovyote vile, Hakuwa ameandika mpango kama huo kama Chati ya Muhtasari wa Maendeleo ya Binadamu kabla ya kuumba ulimwengu. Katika kazi ya Mungu, Anaeleza moja kwa moja kile Alicho; Hachemshi bongo kuunda mpango. Bila shaka, manabii wengi wameongelea unabii mwingi, lakini bado haiwezi kusemekana kwamba kazi ya Mungu siku zote imekuwa ya upangaji mpango wa dhati; unabii ulitolewa kulingana na kazi halisi ya Mungu. Kazi zake zote ni kazi halisi zaidi. Hutekeleza kazi Yake kulingana na maendeleo ya nyakati, na Anatekeleza kazi Yake nyingi zaidi halisi kulingana na mabadiliko ya mambo Kwake Yeye, kutekeleza kazi ni sawa na kutoa dawa kwa ugonjwa; Anafanya uangalizi wakati akifanya kazi Yake; Anafanya kazi kulingana na uangalizi Wake. Katika kila awamu ya kazi Yake, Anaweza kuelezea hekima Yake tosha na kuelezea uwezo Wake tosha; Anafichua hekima Yake tosha na mamlaka Yake tosha kulingana na kazi ya enzi hiyo husika na kuruhusu watu wowote wale waliorudishwa na Yeye wakati wa enzi hizo kuweza kuiona tabia Yake nzima. Anawaruzuku watu na kutekeleza kazi Anayofaa kufanya kulingana na kazi ambayo lazima ifanywe katika enzi husika; Anawaruzuku watu kulingana na kiwango ambacho Shetani amewapotosha. Ilikuwa ni njia hii wakati Yehova aliweza kuwaumba mwanzo Adamu na Hawa ili kuwaruhusu kumdhihirisha Mungu katika nchi na kuwa na mashahidi wa Mungu miongoni mwa uumbaji, lakini Hawa alitenda dhambi baada ya kujaribiwa na nyoka; Adamu alifanya vivyo hivyo, na kwa pamoja wakiwa kwenye bustani wakalila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Na hivyo basi, Yehova alikuwa na kazi ya ziada ya kutenda miongoni mwao. Aliuona uchi wao na kuifunika mili yao kwa nguo ziliyotengenezwa kutoka kwenye ngozi za wanyama. Kufuatia haya, Alimwambia Adamu “Kwa sababu umesikiliza sauti ya mkeo, na umekula kutoka kwa mti ule, ambao Nilikuamuru, nikisema, usile kutoka kwa mti huo: udongo umelaaniwa kwa sababu yako … mpaka urudi udongoni, kwani ulitolewa hapo: kwa kuwa wewe ni mavumbi, na utarudi mavumbini.” Kwa mwanamke Akasema, “Nitazidisha mara dufu maumivu yako na kupata kwako watoto; kwa maumivu utazaa wana; na tamaa yako itakuwa kwa mume wako, na yeye atatawala juu yako.” Kuanzia hapo aliwafukuza kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuwafanya kuishi nje ya bustani, kama vile binadamu wa kisasa afanyavyo sasa nchini. Wakati Mungu alipomwumba mwanadamu mwanzoni kabisa, Hakupanga kumfanya binadamu kujaribiwa na nyoka baada ya kuumbwa na kisha kuwalaani binadamu na nyoka. Kwa hakika hakuwa na mpango wa aina hii; ilikuwa tu maendeleo ya mambo yaliyompa kazi hii mpya miongoni mwa uumbaji Wake. Baada ya Yehova kutekeleza kazi Yake miongoni mwa Adamu na Hawa kwenye ardhi, binadamu waliendelea kuimarika kwa miaka elfu kadhaa mpaka “Yehova akaona ya kwamba uovu wa mwanadamu ni mkuu ulimwenguni, na kuwa kila wazo la fikira za moyo wake ni ovu pekee daima. Na ikamghairi Yehova kwa sababu alikuwa amemfanya mwanadamu ulimwenguni, na ikamhuzunisha moyoni. Ila Nuhu alipata neema katika macho ya Yehova.” Wakati huu Yehova alikuwa na kazi mpya zaidi, kwa ajili binadamu Aliowaumba ulikuwa umezidisha dhambi baada ya kujaribiwa na nyoka. Kwa mujibu wa hali hizi, Yehova aliichagua familia ya Nuhu kutoka miongoni mwa watu hawa na kuwanusuru, na kutekeleza kazi Yake ya kuuangamiza ulimwengu kwa gharika. Binadamu wameendelea kukua kwa njia hii mpaka siku ya leo, wakiendelea kupotoka pakubwa, na wakati maendeleo ya binadamu yafikapo kilele, utakuwa ndio mwisho wa binadamu. Kuanzia mwanzo kabisa hadi mwisho wa ulimwengu, ukweli wa ndani wa kazi Yake siku zote umekuwa hivi. Itakuwa sawa na namna ambavyo binadamu atakavyoainisha kulingana na aina yake; mbali na kila mtu anayeamuliwa kabla kwa kundi kinachomfaa mwanzoni kabisa, watu wanawekwa kwenye kategoria kwa utaratibu baada ya kupitia mchakato wa maendeleo. Mwishowe, yeyote ambaye hawezi kuokolewa kwa uzima atarudishwa kwa mababu zake. Hamna kati ya kazi za Mungu miongoni mwa binadamu iliyokuwa tayari imetayarishwa wakati wa uumbaji wa ulimwengu; badala yake, ilikuwa ni maendeleo ya mambo yaliyomruhusu Mungu kutekeleza kazi Yake hatua kwa hatua kwa uhalisia zaidi na kwa kimatendo zaidi miongoni mwa binadamu. Hivi ni kama ambavyo Yehova Mungu hakumwumba nyoka ili kumjaribu mwanamke. Haukuwa mpango Wake mahususi, wala halikuwa jambo ambalo alikuwa ameliamulia kimakusudi awali; mtu anaweza kusema kwamba hali hii haikutarajiwa. Hivyo basi ilikuwa ni kwa sababu ya haya ndiyo Yehova aliwatimua Adamu na Hawa kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuapa kutowahi kumwumba binadamu tena. Lakini hekima ya Mungu inagunduliwa tu na watu kwenye msingi huu, kama tu ile hoja Niliyotaja awali. “Hekima Yangu hutumika kutokana na njama za Shetani.” Haikujalisha ni vipi ambavyo binadamu walizidi kupotoka au vipi nyoka alivyowajaribu, Yehova bado alikuwa na hekima Yake; kwa hivyo, Amekuwa Akijihusisha katika kazi mpya tangu Alipouumba ulimwengu, na hamna hatua zozote za kazi hii zimewahi kurudiwa. Shetani ameendelea kutekeleza njama zake; binadamu wamekuwa wakipotoshwa siku zote na Shetani, na Yehova Mungu pia ameendelea kutekeleza kazi Yake ya hekima siku zote. Hajawahi kushindwa, na Hajawahi kusita kufanya kazi Yake kuanzia uumbaji wa ulimwengu mpaka sasa. Baada ya binadamu kupotoshwa na Shetani, Aliendelea siku zote kufanya kazi miongoni mwa watu ili kumshinda adui Wake anayepotosha binadamu. Vita hivi vitaendelea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ulimwengu. Kwa kufanya kazi hii yote, Hajauruhusu tu binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani, kupokea wokovu Wake mkubwa, lakini pia amewaruhusu kuiona hekima Yake, uweza na mamlaka, na hatimaye Atawaruhusu binadamu kuiona tabia Yake ya haki—huku Akiwaadhibu wenye maovu na kuwatuza wenye wema. Amepigana na Shetani hadi siku hii ya leo na Hajawahi kushindwa, kwani Yeye ni Mungu mwenye hekima, na hekima Yake hutumika kutokana na njama za Shetani. Na kwa hivyo basi mbali na kufanya tu kila kitu mbinguni kunyenyekea kwa mamlaka Yake; pia Hufanya kila kitu nchini kupumzika chini ya kigonda Chake, na pia Huwafanya wale watenda maovu wanaoshambulia na kunyanyasa binadamu kujipata katika kuadibu Kwake. Matokeo yote ya kazi yanaletwa kutokana na hekima Yake. Alikuwa hajawahi kufichua hekima Yake kabla ya uwepo wa binadamu, kwani Hakuwa na maadui kule mbinguni, juu ya nchi, au kwenye ulimwengu kwa ujumla, na hakukuwa na nguvu za giza zilizoshambulia chochote katika maumbile. Baada ya malaika mkuu kumsaliti Yeye, Aliwaumba binadamu kwenye nchi, na ilikuwa ni kwa sababu ya binadamu ndiyo Alianza rasmi vita Vyake vya milenia nzima dhidi ya Shetani, malaika mkuu, vita ambavyo vilizidi kushamiri kwa kila hatua iliyopigwa. Uweza Wake na hekima vinapatikana katika kila mojawapo ya awamu hizi. Ni katika muda huu tu ndipo kila kitu kule mbinguni na nchini huweza kushuhudia hekima ya Mungu, uweza Wake, na hasa uhalisi wa Mungu. Angali anatekeleza kazi Yake kwa njia ile ya kihalisi leo; aidha, Anapoendelea kutekeleza kazi Yake anafichua pia uweza Wake na hekima Yake; Anawaruhusu kuona ule ukweli wa ndani katika kila awamu ya kazi, kuweza kuona hasa ni vipi unaweza kuelezea ule uweza wa Mungu na hasa ni vipi unavyoweza kuelezea ule uhalisia wa Mungu.

Je, watu hawaamini kwamba ilipangwa awali kabla ya uumbaji kwamba Yuda angeweza kumwuza Yesu? Kwa hakika, Roho Mtakatifu alikuwa amepanga haya kulingana na uhalisia wakati huo. Ilifanyika tu kwamba kulikuwepo mtu kwa jina la Yuda ambaye siku zote angebadhiri fedha. Hivyo basi alichaguliwa kutekeleza wajibu huu na kuwa mwenye huduma katika njia hii. Huu ni mfano halisi wa kutumia rasilimali za mahali palepale. Yesu hakujua hili kwanza; Alilijua hili tu Yuda alipolifichuliwa baadaye. Kama mtu mwingine angeweza kutekeleza wajibu huu, basi mtu mwingine angeweza kufanya hivi badala ya Yuda. Kile ambacho kiliamuliwa awali kiliweza hasa kufanywa wakati mmoja na Roho Mtakatifu. Kazi ya Roho Mtakatifu siku zote inafanywa kwa hiari; wakati wowote Anapopanga kazi Yake, Roho Mtakatifu ataitekeleza. Kwa nini sikuzote Nasema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni ya uhalisi? Kwamba siku zote ni mpya na haijawahi kuwa zee, na siku zote inakuwa na uhai zaidi? Kazi ya Mungu ilikuwa bado haijawahi kupangwa wakati ulimwengu ulipoumbwa; hivi sivyo kamwe ilivyofanyika! Kila hatua ya kazi hufikia athari yake bora kwa wakati wake mwafaka, nazo haziingiliani kati. Kunao wakati mwingi ambapo mipango katika akili zako hazilingani kamwe na kazi ya hivi punde ya Roho Mtakatifu. Kazi Yake si rahisi kama wanavyofikiria watu, wala si ngumu kama watu wengi wanavyofikiria; inajumuisha kuwaruzuku watu wakati wowote na mahali popote kulingana na mahitaji yao ya sasa. Hakuna aliye wazi zaidi kuhusu kiini halisi cha watu kama Yeye, na ni kwa sababu hii mahususi ndiposa hakuna kinachoweza kufaa mahitaji ya kihalisi ya watu kama vile ambavyo kazi Yake inavyofanya. Hivyo basi, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kazi Yake ilipangiwa milenia kadha mbele. Anavyofanya kazi miongoni mwenu sasa, kulingana na hali yenu, Yeye pia Anafanya kazi na kuongea wakati wowote na mahali popote. Wakati watu wako katika hali fulani, Yeye huongea maneno hayo ambayo hasa ndiyo wanayohitaji ndani yao. Ni kama hatua ya kwanza ya kazi Yake ya nyakati za kuadibu. Baada ya nyakati za kuadibu, watu walionyesha tabia fulani, walikuwa na mienendo ya kuasi katika njia fulani, hali fulani nzuri ziliibuka, hali fulani mbaya pia ziliibuka, na mipaka ya juu ya hali hii ya ubaya ikafikia kiwango fulani. Mungu alifanya kazi Yake kutokana na mambo haya yote, na hivyo basi Alichukua haya yote ili kuweza kutimiza athari bora zaidi kwa ajili ya kazi Yake. Anatekeleza tu kazi Yake ya kuruzuku miongoni mwa watu kulingana na hali zao za sasa. Yeye Hutekeleza kila hatua ya kazi Yake kulingana na hali halisi za watu. Uumbaji wote umo mikononi Mwake; Angekosa kuujua? Kwa mujibu wa hali za watu, Kazi hii haikupangwa maelfu ya miaka kabla; hii ni dhana ya kibinadamu tu! Yeye hufanya kazi kwa kadri Anavyoangalia athari ya kazi Yake, na kazi Yake inaendelea kuwa ya kina na kukuzwa; kwa kadri Anavyoendelea kuangalia matokeo ya kazi Yake, ndipo Anapotekeleza hatua inayofuata ya kazi Yake. Yeye hutumia mambo mengi ili kuingia kwenye mpito hatua kwa hatua na kufanya kazi Yake mpya kuonekana na watu baada ya muda. Aina hii ya kazi inaweza kuruzuku mahitaji ya watu, kwani Mungu anawajua watu vizuri mno. Hivi ndivyo Anavyotekeleza kazi Yake kutoka mbinguni. Vilevile, Mungu mwenye mwili anafanya kazi Yake kwa njia iyo hiyo, Akipangilia kulingana na uhalisia na utendakazi miongoni mwa binadamu. Hakuna yoyote kati ya kazi Zake iliyopangwa kabla ya ulimwengu kuumbwa, wala kupangwa kwa umakinifu kabla ya wakati. Miaka 2,000 baada ya ulimwengu kuumbwa, Yehova aliona binadamu walikuwa wamepotoka sana kiasi cha kwamba Alikitumia kinywa cha nabii Isaya kutabiri kwamba baada ya Enzi ya Sheria kukamilika, Angetekeleza kazi Yake ya kukomboa binadamu katika Enzi ya Neema. Huu ulikuwa mpango wa Yehova, bila shaka, lakini mpango huu uliweza pia kufanywa kulingana na hali ambazo Aliangalia wakati huo; bila shaka Yeye hakuufikiria mara moja baada ya kumwumba Mwanadamu. Isaya alitabiri tu, lakini Yehova hakuandaa matayarisho mara moja wakati wa Enzi ya Sheria; badala yake, Alianza kazi hii katika mwanzo wa Enzi ya Neema, wakati mjumbe alipojitokeza katika ndoto ya Yusufu na kumpa yeye nuru, wakimwambia kwamba Mungu angekuwa mwili, na hivyo kazi Yake ya kupata mwili ikaanza. Kama watu wanavyofikiria Mungu hakujitayarishia kazi Yake ya kuwa mwili baada ya kuumba ulimwengu; jambo hili liliamuliwa tu kulingana na kiwango cha maendeleo ya binadamu na hadhi ya vita Vyake na Shetani.

Wakati Mungu anapokuwa mwili, Roho Wake anamwingia binadamu; kwa maneno mengine, Roho wa Mungu anauvaa mwili. Anafanya kazi Yake nchini, na badala ya kuleta naye hatua mbalimbali zilizozuiliwa kazi hii haina mipaka kamwe. Kazi ambayo Roho Mtakatifu hufanya katika mwili bado inaamuliwa na athari ya kazi Yake, na Yeye hutumia mambo haya kuamua urefu wa muda ambao Atafanya kazi akiwa mwili. Roho Mtakatifu hufichua moja kwa moja kila hatua ya kazi Yake; Yeye huchunguza kazi Yake anapozidi kuendelea; si jambo ambalo linazidi maumbile kiasi cha kupanua ile mipaka ya kufikiriwa na binadamu. Hii ni kama kazi ya Yehova katika kuumba mbingu na nchi na vitu vyote; Aliweza kupanga na kufanya kazi wakati huo huo Alitenga nuru kutoka kwenye giza, na asubuhi pamoja na jioni vyote vikawa—hii ilichukua siku moja. Siku ya pili Aliumba mbingu, ambayo pia ilichukua siku moja na kisha Akaiumba nchi, bahari na viumbe vilivyojaa ndani, pia ikichukua siku nyingine moja. Hali hii iliendelea hivyo hadi siku ya sita, wakati Mungu alipomwumba binadamu na kumwacha asimamie viumbe hivi vyote juu ya nchi, mpaka siku ya saba, Alipokuwa amemaliza kuumba viumbe vyote, na akapumzika. Mungu Alibariki siku ya saba na kuitenga kuwa siku takatifu. Aliiamulia siku hii takatifu baada ya kuviumba viumbe vyote, na wala si kabla ya kuviumba. Kazi hii iliweza pia kutekeleza kwa hiari; kabla ya kuviumba viumbe vyote, Hakuamua kuumba ulimwengu kwa siku sita na kuamua kupumzika siku ya saba; hoja hizi haziko hivi kamwe. Hakusema hivyo, wala Hakupanga hivi. Kwa vyovyote vile Hakusema kwamba uumbaji wa viumbe vyote ungekamilishwa katika siku ya sita na kwamba Angepumzika siku ya saba; badala yake, Aliumba kulingana na kile kilichokuwa kikionekana kizuri Kwake. Punde Alipomaliza kuumba kila kitu, tayari ilikuwa ni siku ya sita. Kama ingekuwa ni siku ya tano alipomaliza kuumba kila kitu, Angepangilia basi siku ya sita kuwa siku takatifu; hata hivyo, Alimaliza kuumba kila kitu katika siku ya sita, na hivyo basi siku ya saba ikawa siku takatifu, ambayo imepangiwa kuwa hivyo hadi siku ya leo. Hivyo basi, kazi Yake ya sasa inatekelezwa kwa njia sawa na hiyo. Yeye huongea na kuwaruzuku kulingana na hali zenu. Yaani, Roho huongea na kufanya kazi kulingana na hali za watu; Roho huangalia kila kitu na kufanya kazi wakati wowote na mahali popote. Kile Ninachofanya, kwa mfano, kuwawekea na kuwapatia bila kiwazo ni kile mnachohitaji. Ndiyo maana Nasema kwamba hakuna kazi Yangu iliyo tofauti na uhalisia; yote ni halisi, kwani nyinyi nyote mnajua ya kwamba “Roho wa Mungu hulinda vyote.” Kama haya yote yalikuwa yameamuliwa kabla ya wakati, huoni kwamba mambo yangekuwa yamekwisha amuliwa? Unafikiri kwamba Mungu alifanya kazi kwa milenia nzima sita na kisha kuamulia kabla binadamu kama waasi, wapingaji, waongo na wasio aminifu, kama kuwa na mwili, tabia za kishetani zilizopotoka, ashiki za macho na kujihusisha kwao kwa mambo yasiyofaa. Haya yote hayakupangwa awali, lakini yalitokana na upotovu wa kishetani. Baadhi watasema, “Shetani naye hakuwa ndani ya mashiko ya Mungu? Mungu naye alikuwa amepanga awali kwamba Shetani angepotosha binadamu kwa njia hii, na baada ya hapo akatekeleza kazi Yake miongoni mwa binadamu.” Je, Mungu angepanga awali Shetani hasa ili kuwapotosha binadamu? Anayo hamu mno ya kuwaruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida na kibinadamu; Angenyanyasa maisha ya binadamu? Basi kumshinda Shetani na kuokoa binadamu si kungekuwa jitihada za bure bilashi? Je, uasi wa binadamu ungeamuliwa vipi kabla? Ulitokana na kunyanyaswa na Shetani kwa hali halisi; ungepangwa vipi awali na Mungu? Shetani aliye ndani ya mashiko ya Mungu ambaye mnamwelewa na Shetani ndani ya mashiko ya Mungu ambaye Ninamzungumzia ni tofauti sana. Kulingana na kauli zenu kwamba “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake,” Shetani asingemsaliti Yeye. Je, wewe hujasema kwamba Mungu ni mwenyezi? Maarifa yenu ni ya kidhahania mno na hayaambatani na uhalisia; hayaeleweki wala hayana urazini na hayafanyi kazi! Mungu ni mwenyezi; huu si uwongo kamwe. Malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa sababu Mungu alimpa sehemu ya mamlaka awali. Bila shaka, tukio hili halikutarajiwa, kama vile Hawa kukabiliwa na jaribio la nyoka. Hata hivyo, bila kujali ni vipi ambavyo Shetani hutekeleza usaliti wake, tofauti na Mungu, yeye si mwenyezi. Kama vile mlivyosema, Shetani ni mwenye nguvu; haijalishi ni nini atafanya, mamlaka ya Mungu humshinda siku zote. Hii ndiyo maana ya kweli katika ule msemo “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake.” Hivyo basi, vita Vyake na Shetani lazima vitekelezwe hatua moja baada ya nyingine; aidha, Yeye hupanga kazi Yake katika kuitikia ujanja wa Shetani. Hivi ni kusema, kulingana na enzi, Anawaokoa watu na kufichua hekima na uweza Wake. Vilevile, kazi katika siku za mwisho haikuamuliwa awali kabla ya enzi ya Neema; haikuamuliwa awali katika mpangilio unaofuatana kama huu: Kwanza, fanya tabia ya nje ya binadamu kubadilika; pili, fanya binadamu kupokea kuadibu na majaribio yake; tatu, fanya binadamu kupitia kifo; nne, fanya binadamu kupitia zile nyakati za kumpenda Mungu na kuelezea uamuzi wa kiumbe kilichoumbwa; tano, fanya binadamu kuyaona mapenzi ya Mungu na kujua Mungu kabisa, kisha kumkamilisha binadamu. Hakupanga mambo haya wakati wa Enzi ya Neema; badala yake, Alianza kupanga mambo haya katika enzi ya sasa. Shetani yumo kazini, kama vile alivyo Mungu. Shetani huonyesha tabia yake potovu, huku naye Mungu huongea moja kwa moja na kufichua baadhi ya mambo muhimu. Hii ndiyo kazi inayofanywa leo, na hii ndiyo kanuni sawa inayofanya kazi na iliyotumika kwenye siku za kale baada ya ulimwengu kuumbwa.

Kwanza Mungu alimwumba Adamu na Hawa, na pia Alimwumba nyoka. Miongoni mwa mambo haya yote, nyoka ndiye aliyekuwa mwenye sumu zaidi; mwili wake ulikuwa na sumu, na Shetani aliitumia sumu hiyo ili kufaidika. Ni nyoka aliyemjaribu Hawa hadi akatenda dhambi. Adamu alitenda dhambi baada ya Hawa kutenda, na wawili hawa waliweza kutofautisha kati ya mema na maovu. Kama Yehova Alikuwa Amejua kwamba nyoka angemjaribu Hawa, na kwamba Hawa angemjaribu Adamu, kwa nini Akawaweka wote pale katika bustani? Kama Aliweza kutabiri mambo haya kwa nini Akamwumba nyoka na kumweka ndani ya Bustani ya Edeni? Kwa nini Bustani ya Edeni ilikuwa na tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Alinuia wao walile hilo tunda? Wakati Yehova alipokuja, Adamu wala Hawa hawakuthubutu kumkabili Yeye, na ulikuwa tu wakati huu ambapo Yehova alijua kwamba walikuwa wamelila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya na kujipata katika ujanja wa yule nyoka. Hatimaye Alimlaani nyoka, na Akamlaani Adamu na Hawa. Yehova hakuwa na habari wakati wawili hawa walipolila tunda lile la mti. Binadamu walipotoka hadi kufikia kiwango cha kuwa na uovu na uasherati wa kimapenzi, hadi kufikia awamu ya mambo haya yote waliyoyahifadhi katika mioyo yao yakawa maovu na yasiyo ya haki; yote yalikuwa machafu. Yehova hivyo basi alijutia kwa kuumba binadamu. Baadaye Alitekeleza kazi Yake ya kuharibu ulimwengu kwa gharika, ambayo Nuhu na watoto wake wa kiume walinusurika. Baadhi ya mambo kwa hakika hayajaendelea na kuzidi maumbile ya kawaida kama vile watu wanavyoweza kufikiria. Baadhi wanauliza: Kwa sababu Mungu alijua malaika mkuu angemsaliti Yeye, kwa nini alimwumba? Hizi ndizo hoja: Wakati nchi haikuwepo, malaika mkuu ndiye aliyekuwa malaika mkuu zaidi mbinguni. Alikuwa na mamlaka juu ya malaika wote kule mbinguni; haya ndiyo yaliyokuwa mamlaka ambayo Mungu alimpa. Kando na Mungu, ndiye aliyekuwa malaika mkubwa zaidi mbinguni. Wakati Mungu alipouumba binadamu baadaye, malaika mkuu alitekeleza usaliti mkuu zaidi dhidi ya Mungu nchini. Nasema kwamba alimsaliti Mungu kwa sababu alitaka kuwasimamia binadamu na kumzidi Mungu katika mamlaka. Ni malaika mkuu ambaye alimjaribu Hawa hadi akatenda dhambi; alifanya hivyo kwa sababu alipenda kuanzisha ufalme wake nchini na kuwafanya binadamu kumsaliti Mungu na kumtii badala yake. Aliona kwamba kulikuwa na vitu vingi ambavyo vilimtii; malaika walimtii sawa na vile ambavyo watu walivyomtii duniani. Ndege na wanyama, miti, misitu, milima, mito na viumbe vyote vilivyo nchini vilikuwa katika utunzaji wa binadamu—yaani, Adamu na Hawa—huku nao Adamu na Hawa wakimtii. Malaika mkuu hivyo basi alitamani kuzidi mamlaka ya Mungu na kumsaliti Mungu. Baadaye aliwaongoza malaika wengi kumsaliti Mungu, ambao baadaye walikuja kuwa pepo wachafu mbalimbali. Je, huoni kwamba maendeleo ya binadamu hadi siku ya leo yamesababishwa na upotoshaji wa malaika mkuu? Binadamu wako tu namna walivyo leo kwa sababu malaika mkuu alimsaliti Mungu na kuwapotosha binadamu. Kazi hii ya hatua kwa hatua haipo popote pale karibu na dhahania na nyepesi kama vile watu wanavyofikiria. Shetani alitekeleza usaliti wake kwa sababu fulani, ilhali watu hawawezi kufahamu kitu chepesi kama hicho. Kwa nini Mungu akaiumba mbingu na nchi na viumbe vyote, na pia kumwumba Shetani? Kwa sababu Mungu anamdharau Shetani sana, naye Shetani ni adui Wake, kwa nini akamwumba Shetani? Kwa kumwumba Shetani, hakuwa anamwumba adui? Mungu kwa hakika hakuumba adui; badala yake, Alimwumba malaika, na baadaye malaika akamsaliti Yeye. Hadhi yake ilikuwa kubwa mno kiasi cha kwamba alitaka kumsaliti Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba hali hii ilikuwa ya sadfa, lakini ulikuwa pia mtindo usiokwepeka. Ni sawa na vile ambavyo mtu atakufa akiwa na umri fulani bila uwezo wa kuzuia hali hiyo; mambo yamefikia tayari katika awamu fulani. Kunao hata baadhi ya wale wa kipumbavu wanaosema: “Kwa sababu Shetani ni adui Yako, kwa nini Ukamwumba? Kwani hukujua kuwa malaika huyu mkuu angekusaliti Wewe? Kwani Huwezi kukazia macho kutoka kwa milele moja hadi nyingine? Kwani Wewe huijui asili yake? Kwa sababu ulijua waziwazi kuwa angekusaliti Wewe, basi kwa nini ukamfanya kuwa malaika mkuu? Hata kama mtu atapuuza suala la usaliti wake, aliweza bado kuwaongoza malaika wengi na akashuka hadi kwa ulimwengu wa binadamu wasiodumu ili kuwapotosha binadamu; hadi siku ya leo umeshindwa kukamilisha mpango Wako wa usimamizi wa miaka elfu sita.” Hayo ni kweli? Je, huoni kwamba unajiweka kwenye matatizo mengi zaidi kuliko inavyohitajika? Wengine bado husema: Kama Shetani asingewapotosha binadamu hadi siku ya leo, Mungu asingewaokoa binadamu kwa njia hii. Katika mfano huu, hekima na uweza wa Mungu vyote vingekuwa havionekani; hekima Yake ingewezaje kujionyesha? Hivyo basi Mungu alikiumba kizazi cha binadamu kwa minajili ya Shetani; katika siku za usoni, Mungu angefichua uweza Wake—vinginevyo, binadamu angewezaje kugundua hekima Yake? Kama binadamu asingempinga Yeye na kuchukua hatua ya kumwasi Yeye, isingehitajika kwa vitendo Vyake kujionyesha. Kama uumbaji wote ungemwabudu Yeye na kumtii Yeye, Asingekuwa na kazi ya kufanya. Hali hii nayo ni mbali zaidi na uhalisia wa mambo, kwani hakuna uchafu wowote kuhusu Mungu, na hivyo basi Hawezi kuumba uchafu. Yeye hufichua tu vitendo Vyake ili kuweza kuwashinda kabisa adui Zake, ili kuokoa binadamu, ambao aliuumba, ili kuyashinda mapepo na Shetani, ambao wanamchukia, wanamsaliti Yeye na wanampinga Yeye, ambao walikuwa katika utawala Wake na walimilikiwa na Yeye mwanzo kabisa; Anataka kuwashinda hawa mapepo na katika kufanya hivyo kuufichua uweza Wake kwa viumbe vyote. Binadamu na viumbe vyote vilivyomo nchini sasa hivi vimemilikiwa na Shetani na katika utawala wa waovu. Mungu anataka kuvifichua vitendo Vyake kwa viumbe vyote ili watu waweze kumjua Yeye, na hivyo kuishia kumshinda Shetani na kuangamiza kabisa adui Zake. Viumbe Vyake vyote vimemilikiwa na Shetani, na hivyo basi Anapenda kuufichua uweza Wake kwa viumbe hivyo, kwa hivyo kumshinda Shetani. Kama Shetani asingekuwepo, Asingehitaji kuvifichua matendo Yake Kama usingekuwa unyanyasaji wa Shetani, angewaumba binadamu na kuuongoza kuishi katika Bustani ya Edeni. Kwa nini Hakuwahi kufichua vitendo Vyake vyote kwa malaika au malaika mkuu kabla ya kusalitiwa na Shetani? Kama malaika na malaika mkuu wangalimjua Yeye, na pia kumtii Yeye pale mwanzoni, basi Asingewahi kutekeleza vile vitendo vya kazi visivyo na maana. Kwa sababu ya uwepo wa Shetani na mapepo, watu humpinga na wanajazwa hadi pomoni na tabia ya uasi, na hivyo basi Mungu angependa kufichua vitendo Vyake. Kwa sababu Angependa kupigana vita na Shetani, lazima Atumie mamlaka Yake kumshinda Shetani na kutumia vitendo Vyake vyote kumshinda Shetani; kwa njia hii, kazi Yake ya wokovu Anayotekeleza miongoni mwa binadamu itawafanya watu waone hekima na uwezo Wake. Kazi anayofanya Mungu leo ni yenye maana na haifanani kwa vyovyote vile na ile baadhi watu wanayoisema: “Je, kazi hii Unayofanya haihitilafiani? Je, huu mfuatano wa kazi si mazoezi ya kujitatiza Wewe tu? Ulimwumba Shetani, kisha baadaye ukamruhusu Akakusaliti na kukupinga Wewe. Uliwaumba binadamu, na kisha ukamkabidhi Shetani, na Ukaruhusu Adamu na Hawa kujaribiwa. Kwa sababu uliyafanya mambo haya yote kimakusudi, kwa nini Unawachukia binadamu? Kwa nini Unachukia Shetani? Mambo haya si ya kujitungia Wewe? Ni nini kipo cha Wewe kuchukia?” Watu wengi wa kipumbavu watasema hayo. Wanatamani kumpenda Mungu, lakini mioyoni mwao wanalalamika kumhusu Mungu—ukinzani jinsi gani! Wewe huelewi ukweli, unazo fikira nyingi sana za kimiujiza, na pia unadai kwamba hili ni kosa la Mungu—wewe ni mpumbavu kiasi kipi! Ni wewe unayecheza na ukweli; si kosa la Mungu! Baadhi ya watu wataweza hata kulalamika na kulalamika: Ni wewe uliyemwumba Shetani, na ni Wewe uliyempa Shetani binadamu. Binadamu wanamiliki tabia ya kishetani; badala ya kuwasamehe, Unauchukia kwa kiwango fulani. Mwanzo Uliupenda binadamu kwa kiwango fulani. Ulimtimua Shetani hadi ulimwenguni mwa binadamu, na sasa Unawachukia binadamu. Ni wewe unayewachukia na kuwapenda binadamu—maelezo ya kauli hii ni yapi? Je, huu si ukinzani? Bila kujali ni vipi mnavyoangalia suala hili, hivi ndivyo ilivyofanyika mbinguni; malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa njia hii, nao binadamu wakapotoshwa kwa njia hii, na ukaendelea mpaka leo kwa njia hii. Bila kujali ni vipi mnavyopangilia kauli hizi, hii ndiyo hadithi yote. Hata hivyo, lazima muelewe kwamba Mungu anaifanya kazi ya leo ili kuwaokoa nyinyi, na ili kumshinda Shetani.

Kwa sababu malaika hasa alikuwa mnyonge na hakumiliki uwezo wowote, alikuwa mwenye kiburi wakati alipewa mamlaka, hasa malaika mkuu, ambaye hadhi yake ilikuwa ya juu zaidi kuliko ile ya wale malaika wengine. Malaika mkuu alikuwa ndiye mfalme wa malaika wote. Aliwaongoza mamilioni ya malaika, na kwa usimamizi wa Yehova mamlaka yake yalizidi yale ya malaika yeyote mwingine. Alitaka kufanya hivi na vile, na kuwaongoza malaika hadi ulimwenguni mwa binadamu ili kuutawala ulimwengu. Mungu alisema kwamba Yeye huutawala ulimwengu; malaika mkuu akasema kwamba ulimwengu ulikuwa wake wa kutawala, na kuanzia hapo akamsaliti Mungu. Mbinguni, Mungu alikuwa ameuumba ulimwengu mwingine. Malaika mkuu akataka kuutawala ulimwengu huu na pia kushuka chini kwenye himaya ya binadamu. Je, Mungu angemruhusu kufanya hivi? Hivyo basi, Alimtimua hadi chini na akawa angani. Tangu hapo alipowapotosha binadamu, Mungu amefanya vita dhidi yake ili kuwaokoa binadamu; Ametumia milenia hizi sita kumshinda. Dhana yenu ya Mwenyezi Mungu hailingani na kazi ambayo Mungu anatekeleza sasa; haifanyi kazi katika kutenda na ni ya upumbavu ajabu! Kwa hakika, Mungu alitangaza malaika mkuu kuwa adui Yake baada tu ya malaika mkuu kumsaliti Yeye. Ilikuwa kutokana tu na kusaliti kwake Mungu ndiposa aliwadhalilisha binadamu baada ya kuwasili katika ulimwengu wa binadamu, na ilikuwa kwa sababu hii ndiposa binadamu waliendelea hadi kiwango hiki. Kufuatia haya, Mungu alikula kiapo na Shetani: Nitakushinda wewe na kuwaokoa binadamu, uumbaji Wangu. Shetani hakushawishika wakati wa mwanzo na akasema, ni nini kwa hakika unachoweza kunifanyia mimi? Wewe unaweza kunifukuza hadi katika anga kweli? Wewe unaweza kwa kweli kunishinda mimi? Baada ya Mungu kumtimua hadi angani, Hakumtilia maanani tena na kisha Alianza kuwaokoa binadamu na kufanya kazi Yake mwenyewe, licha ya unyanyasaji ulioendelea kutoka kwa Shetani. Kila kitu ambacho Shetani angeweza kufanya kilitokana na nguvu alizopewa na Mungu; alichukua vitu hivi pamoja naye hadi angani na amevihifadhi vitu hivi hadi leo. Mungu alimtimua hadi angani lakini hakuchukua mamlaka yake, na hivyo basi aliendelea kuwapotosha binadamu. Mungu, kwa mkono mwingine, Alianza kuwaokoa binadamu, ambao Shetani alikuwa amepotosha baada ya kuumbwa kwao. Mungu hakufichua vitendo Vyake wakati akiwa mbinguni; hata hivyo, kabla ya kuiumba dunia, Aliwaruhusu watu katika ulimwengu Aliouumba mbinguni kuona vitendo Vyake na hivyo kuwaongoza watu juu mbinguni. Aliwapa hekima na busara, na kuwaongoza watu hao kuishi kwenye ulimwengu huo. Kiasili, hakuna kati yenu ambaye amewahi kusikia haya awali. Baadaye, baada ya Mungu kuumba binadamu, malaika mkuu alianza kuwapotosha binadamu; duniani, binadamu wote walikuwa katika fujo. Ulikuwa ni wakati huu tu ambapo Alianza vita Vyake dhidi ya Shetani, na ulikuwa ni katika wakati huu tu ambapo watu waliona vitendo Vyake. Mwanzo vitendo Vyake vilifichwa kutoka kwa binadamu. Baada ya Shetani kutimuliwa hadi angani, alijishughulisha na masuala yake, naye Mungu akajishughulisha Mwenyewe na kazi Yake binafsi, mara kwa mara Akifanya vita dhidi ya Shetani, kila wakati mpaka siku za mwisho. Sasa ndio wakati ambao Shetani anafaa kuangamizwa. Mwanzoni Mungu alimpa mamlaka, na baadaye Mungu alimtimua hadi angani, lakini Shetani alibaki mwasi. Baadaye, alipofika nchini, aliwapotosha binadamu, lakini Mungu alikuwa kwa hakika ulimwenguni akiwasimamia binadamu. Mungu hutumia usimamizi Wake wa watu kumshinda Shetani. Kwa kuwapotosha watu, Shetani huleta hutamatisha hatima ya watu na kuinyanyasa kazi ya Mungu. Kwa upande mwingine, kazi ya Mungu ndiyo wokovu wa binadamu. Ni hatua gani ya kazi yenyewe ya Mungu ambayo hainuii kuwaokoa binadamu? Ni hatua gani hainuii kutakasa watu, ili kuwafanya kuwa wenye haki na kuwafanya kuishi kwa njia ambayo huunda taswira inayoweza kupendwa? Shetani, hata hivyo, hafanyi hivi. Yeye huwapotosha binadamu; siku zote anatekeleza kazi zake za kuwapotosha binadamu kote ulimwenguni. Bila shaka, Mungu pia hufanya kazi Yake. Hamtilii maanani Shetani. Haijalishi ni mamlaka kiasi kipi Shetani anayo, mamlaka yake bado yalitoka kwa Mungu; Mungu kwa hakika hakumpa mamlaka Yake yote tu, na hivyo basi haijalishi ni nini afanyacho Shetani, hawezi kuzidi Mungu na siku zote huwa kwenye udhibiti wa Mungu. Mungu hakufichua vitendo Vyake vyovyote akiwa mbinguni. Alimpa Shetani kiwango kidogo tu cha mamlaka ili kumruhusu kutekeleza udhibiti wake dhidi ya malaika. Hivyo basi, haijalishi ni nini hufanya, hawezi kuzidi mamlaka ya Mungu kwa sababu mamlaka ambayo Mungu alimpa awali ni finyu. Huku Mungu akifanya kazi, Shetani hunyanyasa. Katika siku za mwisho, atamaliza unyanyasaji wake; vilevile, kazi ya Mungu itakamilika, na aina ya mtu ambaye Mungu angependa kumkamilisha atakuwa amekamilika. Mungu huwaelekeza watu kwa njia nzuri; maisha Yake ni maji yenye uzima, yasiyopimika na yasiyo na mipaka. Shetani amepotosha binadamu hadi kiwango fulani; hatimaye, yale maji hai ya uzima yatamkamilisha binadamu, na haitawezekana kwa Shetani kuingilia kati na kutekeleza kazi yake. Hivyo basi, Mungu ataweza kuwapata kabisa watu wake. Shetani angali anakataa kukubali haya sasa; siku zote hupambana na Mungu, lakini Mungu hamtilii maanani. Amesema, Nitakuwa mshindi dhidi ya nguvu zote za giza za Shetani na dhidi ya ushawishi wote wa giza. Hii ndiyo kazi ambayo lazima ifanywe kwa mwili, na ndiyo pia maana ya kupata mwili kwa Yesu Kristo. Ni kukamilisha awamu ya kazi ya kumshinda Shetani katika siku za mwisho, kuondoa vitu vyote vinavyomilikiwa na Shetani. Ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani ni mtindo usioepukika! Shetani kwa hakika alishindwa kitambo sana. Wakati injili ilipoanza kuenezwa kote nchini mwa joka kubwa jekundu, yaani, wakati Mungu mwenye mwili alipoanza kufanya kazi na kazi hii ikafanywa kuendelea, Shetani aliweza kushindwa kabisa, kwani kupata mwili wa Kristo kulimaanisha kumshinda Shetani. Shetani aliona kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili na alikuwa ameanza kutekeleza kazi Yake, na akaona kwamba hakuna nguvu ambazo zingeweza kukomesha kazi hii. Hivyo basi, alipigwa na bumbuazi alipoona kazi hii na hakuthubutu kufanya kazi yoyote nyingine zaidi. Kwanza Shetani alifikiria kwamba pia alimiliki hekima nyingi, na akaingilia kati na kunyanyasa kazi ya Mungu; hata hivyo, hakutarajia kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili, na kwamba katika kazi Yake, Mungu alikuwa ametumia uasi Wake kuhudumu kama ufunuo na hukumu kwa binadamu; na hivyo basi kushinda binadamu na kumshinda Shetani. Mungu ni mwerevu kumshinda, na kazi Yake inamzidi Shetani. Hivyo basi, Niliwahi kutaja awali kwamba: Kazi Ninayoifanya inatekelezwa kutokana na ujanja wa Shetani. Mwishowe Nitafichua uweza Wangu na hali ya kutoweza kwa Shetani. Wakati Mungu anapofanya kazi Yake, Shetani anamfuata unyo kwa unyo kutoka nyuma mpaka mwishowe anaangamizwa—hatajua hata kilichomgonga! Ataweza kutambua tu ukweli baada ya kuvunjwa na kupondwapondwa; na wakati huo atakuwa tayari amechomwa kwenye ziwa la moto. Hatakuwa ameshawishika kabisa wakati huo? Kwani hatakuwa na njama zozote zingine za kutumia!

Ni kazi hii ya kihalisi ya hatua kwa hatua ambayo mara nyingi inalemea moyo wa Mungu kwa huzuni ya binadamu, ili vita Vyake na Shetani vimedumu kwa sasa miaka 6,000. Hivyo basi Mungu alisema hivi: Sitawahi tena kuumba binadamu, wala kuwahi tena kuwapa malaika mamlaka. Kuanzia hapo, wakati malaika walipokuja kazini duniani, walimfuata tu Mungu ili kufanya kazi fulani. Hakuwahi kuwapatia malaika mamlaka. Je, malaika ambao Waisraeli waliwaona walitekeleza vipi kazi yao? Walijifichua katika ndoto na kupitisha maneno ya Yehova. Wakati Yesu alipofufuka siku tatu baada ya kusulubishwa, ni malaika ndio waliolisukuma jiwe kando; Roho wa Mungu hakufanya kazi hii yeye binafsi. Malaika waliweza kufanya tu kazi ya aina hii; waliweza kuwa na wajibu wa usaidizi na hawakuwa na mamlaka, kwani Mungu hatawahi tena kuwapatia mamlaka. Baada ya kufanya kazi kwa muda fulani, watu ambao Mungu alitumia hapa duniani walichukua nafasi ya Mungu na kusema, Nataka kuzidi ulimwengu! Nataka kusimama kwenye mbingu ya tatu! Tunataka hatamu za nguvu ya ukuu! Wangekuwa na kiburi baada ya siku kadhaa za kazi; walitaka nguvu ya ukuu duniani, walitaka kuanzisha taifa jingine, walitaka vitu vyote katika utawala wao na walitaka kusimama katika mbingu ya tatu. Je, kwani hujui kwamba wewe ni binadamu tu unayetumiwa na Mungu? Unawezaje kupaa hadi kwenye mbingu ya tatu? Mungu huja duniani kufanya kazi, kimyakimya na bila ya kujitangaza, na Huondoka kimyakimya baada ya kukamilisha kazi Yake. Hajitangazi kama vile binadamu wanavyofanya, lakini badala yake Anatekeleza kwa kiuhalisia kazi Yake. Wala haingii kanisani na kujitangaza, Nitawamaliza nyinyi nyote! Nitawalaani na kuwaadibu! Anatekeleza tu kazi Yake binafsi, na kuondoka mara Anapomaliza. Wale wachungaji wa kidini wanaowaponya wagonjwa na kupunga mapepo, wanawasomea wengine kutoka kwenye madhabahu, na kutoa hotuba ndefu na zenye makuu na kuzungumzia masuala yasiyo ya kihalisi, wana kiburi hadi moyoni! Wao ni vizazi vya malaika mkuu!

Baada ya kutekeleza kazi Yake ya miaka 6,000 hadi leo, Mungu tayari amefichua vitendo Vyake vingi, kimsingi kumshinda Shetani na kuwaokoa binadamu wote. Anatumia fursa hii kuruhusu kila kitu mbinguni, kila kitu kilicho duniani, kila kitu kinachopatikana baharini pamoja na kila kifaa cha mwisho ambacho Mungu aliumba ulimwenguni kuweza kuona uweza wa Mungu na kushuhudia vitendo vyote vya Mungu. Huchukua fursa ya kumshinda Shetani ili kufichua vitendo Vyake kwa binadamu na kuwaruhusu watu kuweza kumsifu Yeye na kuitukuza hekima Yake kwa kumshinda Shetani. Kila kitu nchini, mbinguni na ndani ya bahari humletea utukufu, huusifu uweza Wake, kinasifu vitendo Vyake vyote na kutamka kwa sauti jina Lake takatifu. Hii ni ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani; hii ni ithibati ya Yeye kumshinda Shetani; na la muhimu zaidi, ni ithibati ya wokovu Wake kwa binadamu. Uumbaji wote wa Mungu humletea utukufu, humsifu Yeye kwa kumshinda adui Wake na kurudi kwa ushindi na humsifu Yeye kama Mfalme mkubwa mwenye ushindi. Kusudio lake si kumshinda Shetani tu, na hivyo basi kazi Yake imeendelea kwa miaka 6,000. Anatumia kushindwa kwa Shetani kuwaokoa binadamu; Anakutumia kushindwa kwa Shetani kufichua vitendo Vyake vyote na kufichua utukufu Wake wote. Atapata utukufu, na umati wote wa malaika utaweza pia kushuhudia utukufu Wake wote. Wajumbe walio mbinguni, wanadamu walio nchini na uumbaji wote ulio nchini utauona utukufu wa Muumba. Hii ndiyo kazi Aifanyayo. Viumbe vyake kule mbinguni na nchini wote utauona utukufu Wake, na atarudi kwa vifijo na nderemo baada ya kumshinda Shetani kabisa na kuruhusu binadamu kumsifu Yeye. Ataweza hivyo basi kutimiza kwa ufanisi vipengele hivi viwili. Mwishowe binadamu wote watashindwa na Yeye, na atamwondoa yeyote yule anayepinga au kuasi, hivi ni kusema, Atawaondoa wale wote wanaomilikiwa na Shetani. Unaviona vitendo hivi vyote vya Mungu sasa, ilhali ungali unapinga na unakuwa mwasi na hutaki kunyenyekea; unayahifadhi mambo mengi ndani yako na unafanya utakacho; unafuata ashiki zako, na kile upendacho—huu ni uasi; huu ni upingaji. Kusadiki Mungu ambako kunatekelezwa kwa ajili ya mwili, kwa ajili ya ashiki za mtu, na kwa ajili ya kile anachopenda mtu, kwa ajili ya ulimwengu, na kwa ajili ya Shetani ni kuchafu; ni upinzani na uasi. Kunazo aina zote tofauti za kusadiki sasa: Baadhi hutafuta hifadhi dhidi ya janga, na wengine hutafuta kupokea baraka, huku baadhi wakitamani kuelewa mafumbo na bado wengine hujaribu kupata pesa. Hiyo yote ni mifumo ya upinzani; hiyo yote ni kukufuru! Kusema kwamba mtu anapinga au anaasi—huku si kwa mujibu wa mambo haya? Watu wengi sasa hivi wanalalamika, wanatamka manung'uniko au kutoa hukumu. Mambo haya yote yanafanywa na waovu; wao ni binadamu wapinzani na waasi; watu kama hao wamemilikiwa na kujawa na Shetani. Watu ambao Mungu huwapata ni wale wanaonyenyekea Kwake kabisa, wale waliopotoshwa na Shetani lakini kuokolewa na kushindwa na kazi Yake sasa, wale waliovumilia majaribu na hatimaye wamepokelewa kabisa na Mungu na hawaishi tena katika utawala wa Shetani na wamevunja minyororo ya udhalimu, walio radhi kuishi kwa kudhihirisha utakatifu—hawa ndio watu watakatifu zaidi; hawa ndio wale watakatifu. Kama matendo yako ya sasa hayalingani na sehemu moja ya mahitaji ya Mungu utaondolewa. Hii haipingiki. Kila kitu kinafanywa kulingana na leo; ingawa Amekuamulia awali na kukuchagua wewe, hatua zako leo bado zitaamua matokeo yako. Kama huwezi kuendelea kwa mwendo sawa sasa, utaondolewa. Kama huwezi kuendelea kwa mwendo sawa sasa, hata unawezaje kutumaini[a] kuendelea kwa mwendo sawa baadaye? Vile sasa muujiza mkubwa kama huo umekufanyikia wewe, bado huamini. Hebu Niambie, utamwamini vipi baadaye wakati Atakapomaliza kazi Yake na Hafanyi tena kazi kama hiyo? Wakati huo itakuwa vigumu zaidi kwako wewe kumfuata Yeye! Baadaye Mungu atategemea mwelekeo na maarifa yako katika kazi ya Mungu kuwa mwili na kile ulichopitia wewe ili kuamua kama wewe ni mwenye dhambi au mwenye haki, au kuamua kama wewe ndiwe uliyefanywa kuwa mtimilifu ama wewe ni yule aliyeondolewa. Lazima uweze kuona wazi sasa. Roho Mtakatifu hufanya kazi hivyo: Yeye huamua matokeo yako kulingana na tabia yako leo. Nani huongea maneno ya leo? Nani hufanya kazi ya leo? Nani huamua kama utaondolewa leo? Nani huamua kukufanya kuwa mtimilifu? Hivi sivyo Ninavyofanya Mimi mwenyewe? Mimi Ndimi ninayeongea maneno haya; Mimi Ndimi ninayetekeleza kazi hii. Kulaani, kuadibu na kuhukumu watu vyote ni sehemu ya kazi Yangu mimi binafsi. Hatimaye, kukuondoa kutakuwa pia kazi Yangu binafsi. Yote ni kazi Yangu binafsi! Kukufanya kuwa mtimilifu ni shughuli Yangu binafsi, na kukuruhusu kufurahia baraka ni shughuli Yangu binafsi pia. Hii yote ni kazi Yangu binafsi. Matokeo yako hayakuamuliwa awali na Yehova; yanaamuliwa leo na Mungu wa leo. Yanaamuliwa sasa; hayakuamuliwa kabla ya ulimwengu kuumbwa. Baadhi ya watu wapumbavu husema, Pengine kuna jambo mbaya na macho Yako, na Hunioni mimi kama vile Unavyofaa kuniona. Hatimaye mtaona namna Roho atakavyoonyesha kila kitu! Yesu kwanza Alimchagua Yuda kama mwanafunzi Wake. Watu hufikiria kwamba Yesu alikuwa amefanya kosa kwa kumchagua yeye. Angewezaje kumchagua mwanafunzi ambaye angemsaliti? Mwanzo Yuda hakuwa na nia ya kumsaliti Yesu. Hili jambo lilifanyika tu baadaye. Wakati huo Yesu alikuwa amemchukua Yuda kwa upendo; Alimfanya mwanamume huyo kumfuata Yeye na kumfanya kuwajibikia masuala yao ya kifedha. Kama Angejua kwamba Yuda angebadhiri pesa, Asingemwacha kusimamia pesa hizo. Mtu anaweza kusema kwamba Yesu hakujua mwanzo kwamba mwanamume huyu alikuwa asiye mwaminifu na mdanganyifu, na kwamba aliwadanganya ndugu zake. Baadaye Yuda alipokwisha kumfuata kwa muda fulani, Yesu alimwona akiwadanganya ndugu zake na akidanganya Mungu. Watu waligundua pia kwamba siku zote angetumia pesa kutoka kwenye mfuko wa fedha na kisha wakamwambia Yesu. Yesu alipata habari tu kuhusu haya yote wakati huu. Kwa sababu Yesu alikuwa atekeleze kazi ya kusulubishwa na Alihitaji mtu wa kumsaliti Yeye, na Yuda alitokea tu kuwa mhusika mzuri wa wajibu huu, Yesu akasema, kutakuwepo miongoni mwenu ambaye atanisaliti Mimi. Mwana wa adamu atatumia usaliti huu kuweza kusulubishwa na baada ya siku tatu atafufuka. Wakati huo Yesu hakuchagua hasa Yuda ili aweze kumsaliti Yeye; kinyume cha mambo ni kwamba, Alipenda kwamba Yuda awe mwanafunzi mtiifu. Kwa mshangao Wake, Yuda aligeuka kuwa mlafi na mwenye sifa mbaya aliyemsaliti Bwana, na akatumia hali hii kumchagua Yuda kwa kazi hii. Kama wanafunzi wote kumi na wawili wa Yesu wangekuwa watiifu, na hakuna mtu kama Yuda angekuwa miongoni mwao, yule mtu wa kumsaliti Yesu angekuwa hatimaye mtu kutoka nje ya wale wanafunzi. Hata hivyo, wakati huo ilifanyika tu kwamba kulikuwa na mmoja miongoni mwao aliyefurahia kuchukua hongo—Yuda. Yesu kwa hivyo basi alimtumia mwanamume huyu kukamilisha kazi Yake. Jambo hili liweje rahisi hivyo! Yesu hakuliamua awali mwanzoni mwa kazi Yake; alifanya tu uamuzi huu punde tu mambo yalipoimarika hadi hatua fulani. Huu ulikuwa ni uamuzi wa Yesu, yaani, uamuzi wa Roho wa Mungu Mwenyewe. Wakati huo ni Yesu aliyemchagua Yuda; wakati Yuda alipomsaliti Yesu baadaye, haya yalikuwa ni matendo ya Roho Mtakatifu ili kuhudumu hatima Zake mwenyewe; ilikuwa ni kazi ya Roho Mtakatifu wakati huo. Wakati Yesu alipomchagua Yuda, Hakuwa na wazo lolote kwamba Angemsaliti. Alijua tu kwamba alikuwa Yuda Iskariote. Matokeo yenu yanaamuliwa pia kulingana na kiwango chenu cha kunyenyekea leo na kulingana na kiwango chenu cha ukuzi wa maisha, na wala si kulingana na wazo miongoni mwa dhana za binadamu kwamba ilikuwa imepangiwa awali katika uumbaji wa ulimwengu. Lazima uelewe mambo haya waziwazi. Kazi hii nzima haitekelezwi kulingana na kufikiria kwako.

Tanbihi:

a. Maandishi asilia yameacha "hata unawezaje kutumaini."

Iliyotangulia:Maneno kwa Vijana na Wazee

Inayofuata:Kuhusu Majina na Utambulisho

Unaweza Pia Kupenda