Kuhusu Biblia (3)

Si kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana nyingi za kibinadamu, upendelevu wa binadamu, na ufahamu wa ajabu wa binadamu. Ni kweli, maneno mengi ni matokeo ya kupatiwa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, na ni ufahamu sahihi—lakini haiwezi kusemwa kuwa ni udhihirishaji sahihi kabisa wa ukweli. Maoni yao juu ya vitu fulani si chochote zaidi ya maarifa yaliyotokana na uzoefu binafsi, au kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Utabiri wa manabii ulikuwa umeagizwa na Mungu binafsi: Unabii wa mifano ya Isaya, Danieli, Ezra, Yeremia, na Ezekieli, ulitoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu; watu hawa walikuwa ni waonaji maono, walipokea Roho ya Unabii, wote walikuwa ni manabii wa Agano la Kale. Wakati wa Enzi ya Sheria watu hawa, ambao walikuwa wamepokea ufunuo wa Yehova, walizungumza unabii mwingi, ambao ulisemwa na Yehova moja kwa moja. Na kwa nini Yehova alifanya kazi ndani yao? Kwa sababu watu wa Israeli walikuwa ni wateule wa Mungu: Kazi ya manabii ilipaswa kufanyika miongoni mwao, na walikuwa wamefuzu kupokea maono hayo. Kimsingi, wao wenyewe hawakuelewa ufunuo wa Mungu kwao. Roho Mtakatifu Alizungumza maneno hayo kupitia vinywa vyao ili watu wa baadaye waweze kuelewa mambo hayo, na kuona kwamba ni kweli ilikuwa ni kazi ya Roho wa Mungu, ya Roho Mtakatifu, na haikutoka kwa mwanadamu, na kuweza kuwathibitishia kazi ya Roho Mtakatifu. Wakati wa Enzi ya Neema, Yesu Mwenyewe Alifanya kazi hii yote badala yao, na hivyo watu hawakuzungumza tena unabii. Kwa hivyo Yesu alikuwa nabii? Yesu, kimsingi alikuwa ni nabii, lakini pia Alikuwa na uwezo wa kufanya kazi ya mitume—: Aliweza kusema unabii na kuhubiri na kufundisha watu katika nchi yote. Bado kazi Aliyoifanya na utambulisho Aliouwakilisha haukuwa unafanana. Alikuja kuwakomboa binadamu wote, kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini; Alikuwa nabii, na mtume, lakini zaidi ya hapo Alikuwa Kristo. Nabii Anaweza kuzungumza unabii, lakini haiwezi kusemwa kwamba yeye ni Kristo. Wakati huo, Yesu alizungumza unabii mwingi, na hivyo inaweza kusemwa kwamba Alikuwa nabii, lakini haiwezi kusemwa kwamba Alikuwa nabii na hivyo sio Kristo. Hiyo ni kwa sababu Alimwakilisha Mungu Mwenyewe katika kutekeleza hatua ya kazi, na utambulisho Wake ulikuwa tofauti na ule wa Isaya: Alikuja kukamilisha kazi ya ukombozi, na hivyo Alitoa maisha ya mwanadamu, na Roho wa Mungu Alikuja Kwake moja kwa moja. Katika kazi Aliyoifanya, hakukuwa na uvuvio wa kutoka kwa Roho wa Mungu au maelekezo kutoka kwa Yehova. Badala yake, Roho alifanya kazi moja kwa moja—kitu ambacho kinatosha kuthibitisha kwamba Yesu Hakuwa sawa na nabii. Kazi Aliyoifanya ilikuwa ni kazi ya ukombozi, kazi iliyoifuatia ilikuwa ni kuzungumza unabii. Alikuwa ni nabii, mtume, na zaidi ya hapo Alikuwa ni Mkombozi. Wakati huo, watabiri, wangeweza tu kuzungumza unabii, na walikuwa hawana uwezo wa kumwakilisha Roho wa Mungu katika kufanya kazi nyingine yoyote. Kwa sababu Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haijawahi kufanywa na binadamu, na Alifanya kazi ya kumkomboa mwanadamu, kwa hiyo Alikuwa tofauti na manabii wengine kama Isaya. Kwamba watu wengine hawakubali mkondo wa leo ni kwa sababu hii imetengeneza kizuizi kwao. Wanasema: “Katika Agano Jipya manabii wengi pia walisema maneno mengi—sasa, kwa nini hawakuwa Mungu katika mwili? Mungu wa leo Anazungumza maneno—je, hii inatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu mwenye mwili? Huipatii Biblia umuhimu mkubwa, wala huichunguzi, sasa una msingi gani wa kusema kwamba Yeye ni Mungu aliyepata mwili? Unasema kwamba wameongozwa na Roho Mtakatifu, na unaamini kwamba hatua hii ya kazi ni kazi ambayo imefanywa na Mungu Mwenyewe—lakini msingi wako kwa hili ni nini? Umetilia mkazo katika maneno ya Mungu leo, inaonekana kana kwamba umeikana Biblia, na kuiweka katika upande mmoja.” Na hivyo wanasema kwamba unaamini uzushi, na imani mbalimbali.

Ikiwa unatamani kuwa na ushuhuda kwa kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho, basi unapaswa kuelewa kisa cha ndani cha Biblia, muundo wa Biblia, na hulka ya Biblia. Leo, watu wanaamini kwamba Biblia ni Mungu, na kwamba Mungu ni Biblia. Na hivyo pia, wanaamini kwamba maneno yote ya Biblia ni maneno pekee ambayo Mungu alizungumza, na kwamba yote yalizungumzwa na Mungu. Wale wanaomwamini Mungu hata wanafikia hatua ya kufikiri kwamba ingawa vitabu vyote sitini na sita vya Agano la Kale na Agano Jipya viliandikwa na watu, vyote viliandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na ni rekodi ya matamshi ya Roho Mtakatifu. Huu ni ufahamu wenye makosa wa mwanadamu, na hauafikiani kabisa na kweli. Kimsingi, mbali na vitabu vya unabii, sehemu kubwa ya Agano la Kale ni rekodi ya kihistoria. Baadhi ya nyaraka za Agano Jipya zinatokana na uzoefu wa watu, na baadhi zinatokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu; nyaraka za Paulo, kwa mfano, zilitokana na kazi ya mwanadamu, zote zilitokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, na ziliandikwa kwa ajili ya makanisa, yalikuwa ni maneno ya kushawishi na kutia moyo kwa kaka na dada wa makanisa. Hayakuwa maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu—Paulo asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu, na wala hakuwa nabii, sembuse kuona maono ambayo Yohana aliona. Nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya makanisa ya Efeso, Filadefia, Galatia, na makanisa mengineyo. Na hivyo, nyaraka za Paulo za Agano Jipya ni nyaraka ambazo Paulo aliandika kwa ajili ya makanisa, na sio uvuvio wa Roho Mtakatifu, wala sio matamshi ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu. Ni maneno tu ya kushawishi, faraja, na kutia moyo ambayo aliyaandika kwa ajili ya makanisa wakati wa kazi yake. Na hivyo pia, ni rekodi zaidi ya kazi na muda ya Paulo. Ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada wote katika Bwana, na zilikuwa ni kwa ajili ya kuwafanya kaka na dada wa makani yote ya wakati huo kufuata ushauri wake na kudumu siku zote katika njia zote za Bwana Yesu. Kwa namna yoyote ile Paulo hakusema kuwa, iwe ni kwa makanisa ya wakati huo au makanisa ya wakati ujao, yote yanapaswa kula na kunywa vitu alivyoandika, wala hakusema kwamba maneno yake yote yalitoka kwa Mungu. Kulingana na mazingira ya kanisa wakati huo, aliwasiliana tu na kaka na dada, na aliwashawishi, na akawaimarisha imani kwao; na aliwahubiria na kuwakumbusha watu na kuwashawishi. Maneno yake yalijikita katika mzigo wake mwenyewe, na aliwasaidia watu kupitia maneno haya. Alifanya kazi ya mitume wa kanisa wa wakati huo, alikuwa mfanyakazi ambaye alitumiwa na Bwana Yesu, na kwa hivyo lazima achukue jukumu kwa ajili ya makanisa, na lazima afanye kazi ya makanisa, alipaswa kujifunza kuhusu hali za ndugu—na kwa sababu hii, aliandika nyaraka kwa kaka na dada wote katika Bwana. Yote aliyoyasema ambayo yaliyokuwa ni ya kuadilisha na mazuri kwa watu yalikuwa sahihi, lakini hayakuwa yanawakilisha matamshi ya Roho Mtakatifu, na hayakuweza kumwakilisha Mungu. Ni uelewa mbaya kupita kiasi, na makufuru makubwa sana kwa watu kuchukulia rekodi za uzoefu wa mwanadamu na nyaraka za mwanadamu kama maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu kwa makanisa! Hiyo ni kweli kabisa tunapokuja katika nyaraka ambazo Paulo aliziandika kwa ajili ya makanisa, kwani nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada kulingana na mazingira na hali ya kila kanisa kwa wakati huo, na yalikuwa ni kwa ajili ya kuwashawishi kaka na dada katika Bwana, ili waweze kupokea neema ya Bwana Yesu. Nyaraka zake zilikuwa ni kwa ajili ya kuwaamsha kaka na dada wa wakati huo. Inaweza kusemwa kuwa huu ulikuwa ni mzigo wake mwenyewe, na pia ulikuwa ni mzigo aliopewa na Roho Mtakatifu; hata hivyo, alikuwa ni mtume aliyeyaongoza makanisa ya wakati huo, ambaye aliandika nyaraka kwa ajili ya makanisa na kuwashawishi, huo ulikuwa wajibu wake. Utambulisho wake ulikuwa tu ni mtume anayefanya kazi, na alikuwa ni mtume tu aliyetumwa na Mungu; hakuwa mtabiri, wala mtoa unabii. Kwake, kazi yake mwenyewe na maisha ya kaka na dada yalikuwa na umuhimu mkubwa sana. Hivyo, asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu. Maneno yake hayakuwa maneno ya Roho Mtakatifu, wala yasingesemwa kuwa ni maneno ya Mungu, maana Paulo hakuwa chochote zaidi ya kiumbe wa Mungu, na hakika hakuwa Mungu aliyepata mwili. Utambulisho wake haukuwa sawa na ule wa Yesu. Maneno ya Yesu yalikuwa ni maneno ya Roho Mtakatifu, yalikuwa ni maneno ya Mungu, maana utambulisho wake ulikuwa ule wa Kristo—Mwana wa Mungu. Inawezekanaje Awe sawa na Paulo? Ikiwa watu wanaona nyaraka au maneno kama ya Paulo kama matamshi ya Roho Mtakatifu, na kuwaabudu kama Mungu, basi inaweza kusemwa tu kuwa ni watu wasiochagua kwa busara. Tukisema kwa ukali zaidi, haya sio makufuru? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na inawezekanaje watu wapigie magoti rekodi za nyaraka zake na maneno aliyoyazungumza kana kwamba yalikuwa ni kitabu kitakatifu, au kitabu cha mbinguni? Je, inawezekana maneno ya Mungu kutamkwa kwa kawaida na mwanadamu? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na hivyo, unasemaje—kwamba nyaraka alizoandika kwa ajili ya makanisa haziwezi kutiwa doa na mawazo yake mwenyewe? Inawezekanaje zisitiwe doa na mawazo ya kibinadamu? Aliandika nyaraka kwa makanisa kulingana na uzoefu wake binafsi, na maarifa yake binafsi. Kwa mfano, Paulo aliandika waraka kwa kanisa la Wagalatia ambao ulikuwa na maoni fulani, na Petro aliandika waraka mwingine, ambao ulikuwa na mtazamo mwingine. Ni upi kati ya hizo ulitoka kwa Roho Mtakatifu? Hakuna anayeweza kutoa jibu, hakika. Hivyo inaweza kusemwa tu kwamba wote wanawiwa na mzigo kwa makanisa, lakini barua zao zinawakilisha kimo chao, zinawakilisha vile wanavyowapatia na kuwasaidia kaka na dada, na vile wanavyowiwa na makanisa, na zinawakilisha tu kazi ya binadamu; hayakuwa ya Roho Mtakatifu kabisa. Ikiwa unasema kwamba nyaraka zake ni maneno ya Roho Mtakatifu, basi wewe ni mpumbavu, na unafanya makufuru! Nyaraka za Paulo na nyaraka nyingine za Agano Jipya ni sawa na kumbukumbu za viongozi mashuhuri wa kiroho wa hivi karibuni. Zipo sawa na vitabu vya Watchman Nee au uzoefu wa Lawrence, na kadhalika. Ni vile tu vitabu vya viongozi mashuhuri wa kiroho wa hivi karibuni havijajumuishwa katika Agano Jipya, lakini hulka ya watu hawa ni sawa: Kulikuwa na watu ambao walitumiwa na Roho Mtakatifu wakati fulani, na hawakuweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja.

Injili ya Mathayo ya Agano Jipya inaandika ukoo wa Yesu. Mwanzoni, inasema kwamba Yesu alikuwa mzao wa Abrahamu na wa Daudi, na mwana wa Yusufu; sehemu inayofuata inasema kwamba Yesu alizaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, na kuzaliwa na bikira—kitu kinachomaanisha kwamba Hakuwa mwana wa Yusufu au mzao wa Abrahamu na wa Daudi. Hata hivyo, orodha ya ukoo inasisitiza kumhusisha Yesu na Yusufu. Sehemu inayofuata, orodha ya ukoo inaanza kurekodi mchakato ambao kwa huo Yesu alizaliwa. Inasema mimba ya Yesu ilitungwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, kwamba Alizaliwa na bikira, na sio mwana wa Yusufu. Lakini katika orodha ya ukoo imeandikwa waziwazi kwamba Yesu alikuwa mwana wa Yusufu, na kwa kuwa orodha ya ukoo iliandikwa kwa ajili ya Yesu, inaandika vizazi arobaini na mbili. Inapokwenda katika ukoo wa Yusufu, inasema kwa haraka kwamba Yusufu alikuwa mume wa Mariamu, haya ni maneno kwa ajili ya kuthibitisha kwamba Yesu alikuwa mzao wa Abrahamu. Je, huu si mkanganyiko? Orodha hii ya ukoo inaonyesha waziwazi chimbuko la Yusufu, ni wazi kwamba hii ni orodha ya ukoo wa Yusufu, lakini Mathayo anasisitiza kwamba ni orodha ya ukoo wa Yesu. Je, hii haipingi ukweli kwamba Yesu alizaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu? Hivyo, orodha ya ukoo iliyoandikwa na Mathayo sio mawazo ya kibinadamu? Hii ni dhihaka! Kwa namna hii, unaweza kujua kwamba kitabu hiki sio chote kimetoka kwa Roho Mtakatifu. Pengine, kuna baadhi ya watu wanaodhani kwamba Mungu lazima atakuwa na orodha ya ukoo duniani, na matokeo yake ni kwamba wanampachika Yesu kama kizazi cha arobaini na viwili cha Abrahamu. Hii ni dhihaka kabisa! Baada ya kuja duniani, Mungu angewezaje kuwa na orodha ya ukoo? Ikiwa unasema kwamba Mungu ana ukoo, je, humweki katika madaraja sawa miongoni mwa viumbe wa Mungu? Maana Mungu si wa ulimwengu, Yeye ni Bwana wa uumbaji, na ingawa yeye ni wa mwili, hana asili sawa na mwanadamu. Unawezaje kumweka Mungu katika daraja sawa na viumbe wa Mungu? Abrahamu hawezi kumwakilisha Mungu; alikuwa ni mhusika wa kazi ya Yehova wakati huo, alikuwa ni mtumishi mwaminifu tu aliyethibitishwa na Yehova, na alikuwa mmoja wa watu wa Israeli. Inawezekanaje awe babu wa Yesu?

Ni nani aliandika orodha ya ukoo wa Yesu? Ni Yesu Mwenyewe ndiye aliyeandika? Je, ni Yesu Mwenyewe ndiye Alisema, “Andika orodha Yangu ya ukoo”? Iliandikwa na Mathayo baada ya Yesu kuangikwa msalabani. Wakati huo, Yesu alikuwa amefanya kazi kubwa ambayo ilikuwa haifahamiki kwa mitume, na Hakutoa maelezo yoyote. Baada ya Yeye kuondoka, mitume walianza kuhubiri na kufanya kazi kila mahali, na kwa ajili ya hatua hiyo ya kazi, walianza kuandika nyaraka na vitabu vya injili. Vitabu vya injili ya Agano Jipya vilirekodiwa miaka ishirini hadi thelathini baada ya Yesu kusulubiwa msalabani. Kabla ya hapo, watu wa Israeli walisoma tu Agano la Kale. Hiyo ni sawa na kusema, mwanzoni mwa Enzi ya Neema watu walisoma Agano la Kale. Agano Jipya lilionekana tu wakati wa Enzi ya Neema. Agano Jipya halikuwepo wakati wa kazi ya Yesu; watu waliandika kazi Yake baada ya kuwa amefufuka na kupaa mbinguni. Baada ya hapo kulikuwa na Injili Nne, katika nyongeza hiyo pia kulikuwa na nyaraka za Paulo na Petro, na vile vile kitabu cha Ufunuo. Ni baada tu ya zaidi ya miaka mia tatu baada ya Yesu kupaa mbinguni, wakati vizazi vilivyofuata viliweka pamoja rekodi zao, ndipo kulikuwa na Agano Jipya. Ni baada tu ya kazi hii kukamilika ndipo kukapatikana Agano Jipya; halikuwepo hapo kabla. Mungu alikuwa amefanya kazi yote hiyo, mtume Paulo alifanya kazi yote hiyo, na baadaye nyaraka za Paulo na Petro ziliunganishwa, na njozi kuu zaidi iliyorekodiwa na Yohana katika kisiwa cha Patmo iliwekwa mwishoni, maana ilikuwa inatoa unabii wa kazi ya siku za mwisho. Hii yote ilikuwa ni mipango ya vizazi vilivyofuata na ni tofauti na matamshi ya leo. Kile kilichorekodiwa leo ni kulingana na hatua za kazi ya Mungu; kile ambacho watu wanashughulika nacho leo ni kazi ambayo imefanywa na Mungu Mwenyewe, na maneno yaliyotamkwa na Mungu Mwenyewe. Wewe—mwanadamu—hupaswi kuingilia; maneno, ambayo yanatoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, yamepangwa hatua kwa hatua, na ni tofauti na mpangilio wa rekodi za wanadamu. Inaweza kusemwa kuwa, kile walichorekodi kilikuwa ni kulingana na kiwango chao cha elimu na tabia. Kile walichokirekodi kilikuwa ni uzoefu wa wanadamu, na kila mmoja alikuwa na namna yake ya kurekodi na kuelewa, na kila rekodi ilikuwa tofauti. Hivyo, ikiwa unaiabudu Biblia kama Mungu wewe ni mjinga na mpumbavu wa kutupwa! Kwa nini usitafute kazi ya Mungu wa leo? Ni kazi ya Mungu tu ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu. Biblia haiwezi kuwaokoa wanadamu, wanaweza kuisoma kwa maelfu kadhaa ya miaka na bado hakutakuwa na mabadiliko hata kidogo ndani yao, na kama unaiabudu Biblia hutaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hatua mbili za kazi ya Mungu katika Israeli zote zimerekodiwa katika Biblia, na hivyo miongoni mwa rekodi hizi majina yote ni ya Israeli, na matukio yote ni ya Israeli; na hata jina “Yesu” ni jina la Kiisraeli. Ikiwa unaendelea kusoma Biblia leo, huoni unafungamanishwa kwa maagano? Yale yaliyorekodiwa katika Agano Jipya la Biblia ni masuala ya Yudea. Matini ya awali yalikuwa katika Kiyunani na Kiebrania, na maneno ya Yesu, na jina ambalo kwalo Aliitwa wakati huo ambapo yote yalikuwa katika lugha ya mwanadamu. Aliposulubiwa msalabani, Yesu Alisema: “Eloi, Eloi, lama sabakthani” Je, hiki sio Kiebrania? Hii tu ni kwa sababu Yesu alipata mwili Yudea, lakini haithibitishi kwamba Mungu ni Myahudi. Leo, Mungu amefanyika mwili China, na hivyo kila kitu Anachokisema bila shaka ni katika lugha ya Kichina. Lakini hakiwezi kulinganishwa na Kichina kilichotafsiriwa kutoka katika Biblia, maana chanzo cha maneno haya ni tofauti. Moja inatoka kwa Kiebrania kilichorekodiwa na watu, na moja inatoka katika matamshi ya moja kwa moja ya Roho. Kunawezaje kutokuwa na tofauti hata kidogo?

Iliyotangulia: Kuhusu Biblia (2)

Inayofuata: Kuhusu Biblia (4)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp