Sura ya 89
Sio rahisi kuwa sawa na makusudi Yangu kwa kila kitu unachofanya; si suala la kujilazimisha kujifanya, lakini inategemea kama Nilikujalia ubora Wangu kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, ambayo ilikuwa juu Yangu. Hiki si kitu ambacho watu wanaweza kufanya. Ninampenda yeyote ninayetaka kumpenda, na yeyote Ninayesema ni mzaliwa wa kwanza hakika ni mzaliwa wa kwanza, hii ni sahihi kabisa. Unaweza kutaka kudanganya, lakini huku kutakuwa bure tu! Unadhani Sikutambui? Je, kuwa na tabia nzuri mbele Yangu inatosha? Je, ni rahisi hivyo? La hasha. Lazima uwe na ahadi Yangu, majaliwa Yangu. Je, unafikiri sijui unachokifanya nyuma Yangu? Umepotoshwa! Rudi haraka kwenye ziwa la moto na kiberiti mara tu huduma yako Kwangu itakapokamilika! Nimechukizwa, Ninajawa na chuki kwa kukuona. Wote walio katika huduma Kwangu ambao hawatumii kwa uaminifu kwa ajili Yangu, ni walegevu na wasiozuiliwa, na hawafikirii nia Zangu, baada ya huduma yako kufanyika, ondokeni mbele ya macho Yangu! Vinginevyo, Nitakufukuza! Watu hawa hawawezi kuishi katika nyumba Yangu (yaani, kanisa) kwa muda zaidi. Lazima waondoke hapa ili kuzuia kutia jina Langu aibu, kuharibu sifa Yangu. Watu hawa wote ni wa ukoo wa joka kuu jekundu, wametumwa na joka kuu jekundu kuvuruga usimamizi Wangu. Wamebobea katika udanganyifu kuvuruga kazi Yangu. Mwanangu! Ni lazima muone hili! Msishirikiane na watu hawa. Unapowaona watu wa aina hii nenda mbali nao kwa haraka ili kuzuia kutiwa kwenye mtego na hao na kuleta madhara katika maisha yako! Ninawachukia zaidi watu ambao huongea ovyo ovyo, wanaotenda bila kufikiria, wanaofanya mzaha na kucheka tu, wanaojihusisha na mazungumzo yasiyofaa. Siwataki watu hawa, wote ni wa namna ya Shetani! Kutania bila sababu hata kidogo, je, hao ni nini? Kuongea na kufanya upuuzi, je, bado hawaoni aibu? Kwa uhalisi, mtu wa aina hii anachukuliwa kuwa wa thamani ya chini zaidi, kwa muda mrefu Nimewatazama, kwa muda mrefu Nimewatelekeza. La sivyo, kwa nini wanaongea upuuzi mara kwa mara bila ya Mimi kuwaadhibu? Wao kweli ni wa ukoo wa joka kuu jekundu! Sasa Nimeanza kuvitoa vitu hivi kimoja baada ya kingine. Je, Ninaweza kutumia kizazi cha Shetani kama wana Wangu wazaliwa wa kwanza, kama wana Wangu na watu Wangu? Basi Sitakuwa nimechanganyikiwa? Hakika sitafanya hivyo. Je, mnaelewa hili kwa uwazi?
Kila kitu mnachokumbana nacho leo, kiwe kizuri au kibaya, vyote vimepangwa kwa mikono Yangu yenye hekima: vyote vimepangwa, vimedhibitiwa na Mimi. Hakika hiki sio kitu ambacho mwanadamu anaweza kuwa tayari kukifanya. Watu wengine bado wanatokwa jasho kwenye viganja vyao, wakiwa na wasiwasi kunihusu; kweli hawafai kuwa na wasiwasi! Wanaisahau kazi yao kuu, kutoingia katika roho ilhali wanataka kukua katika maisha; wanatumaini bure! Hawana wasiwasi kabisa, lakini bado wanataka kuridhisha makusudi Yangu! Una wasiwasi kwa niaba Yangu, lakini Mimi sina wasiwasi. Je, una wasiwasi ya nini? Una uzembe katika kazi yako Kwangu, huku ukidanganya wazi wazi. Ninakwambia! Nitamwondoa mtu wa aina hii kutoka kwenye nyumba Yangu kuanzia sasa. Hafai kunitumikia katika nyumba Yangu. Namchukia mtu wa aina hii kwa sababu ananikufuru kwa matendo yake. Iliposemekana “kukufuru dhidi Yangu ni dhambi isiyosameheka,” hii ilikuwa inamuashiria nani? Je, mnaelewa hili? Mtu wa aina hii anaamini kwamba hiyo shida bado haijawa mbaya sana ingawa ameshatenda dhambi. Kweli mtu huyu aliyechanganyikiwa ni kipofu, mjinga, na roho yake imetiwa kizuizi! Nitakutupa nje! (kwa sababu hili ni jaribu la Shetani Kwangu, Ninalichukia kiasi hiki na jambo hili limetajwa mara kwa mara, kila wakati linanikasirisha. Siwezi kuizuia, hakuna anayeweza kuisimamisha. Isingekuwa ni suala la wakati bado haujafika, Ningekuwa nimeshughulikia kitambo.) (Hii ni kuhusu ukweli kwamba kwa wakati huu kuna watu wengi ambao bado hawaamini kwamba wageni watatafuta kuja nchini China; hata sasa bado hawaamini, kuifanya hasira Yangu kuvurugika na kuchemka.)
Je, ni mtu wa aina gani anayeupendeza moyo Wangu katika nyumba Yangu? Hiyo ni kusema, kabla ya uumbaji, ni watu wa aina gani Niliowajalia ili waishi milele katika nyumba Yangu? Je, mnajua? Je, mmefikiria ni aina gani ya watu Ninaopenda na aina gani ya watu Ninaowachukia? Nyumba Yangu ni ya watu walio na mawazo sawa na Mimi, wanaoshiriki nyakati nzuri na ngumu pamoja nami, huku ni kusema, watu wanaoshiriki katika baraka na magumu. Hawa watu wote wanaweza kupenda Ninachopenda na kuchukia Ninachochukia. Wanaweza kukiacha kile Ninachochukia. Nikisema hawataweza kula, wako tayari kushinda njaa ili kuridhisha makusudi Yangu. Mtu wa aina hii yuko tayari kusalia mwaminifu Kwangu na kujitumia kwa ajili Yangu, wanaweza kufikiria kuhusu jitihada Zangu za bidii, daima wakinifanyia kazi kwa bidii. Kwa hivyo, kwa mtu wa aina hii, Ninampa cheo cha mzaliwa wa kwanza, Nikimpa kila kitu Nilicho nacho: Nina uwezo wa kuongoza makanisa yote, hili Ninawapa; Nina hekima, hii pia Ninawapa; Ninaweza kuteseka kwa kutenda ukweli, na pia Nitawapa watu hawa nia, kuwafanya wawe na uwezo wa kuteseka kwa kila kitu kwa ajili Yangu; Nina ubora mzuri wa tabia na hii pia Nitawapa, kuwafanya kuwa kama Mimi kabisa, bila tofauti hata kidogo, ili kwamba wengine wataniona watakapowaona watu hawa. Sasa, Nauweka uungu Wangu wote ndani ya watu hawa kuwawezesha kuishi kulingana na kipengele kimoja cha uungu Wangu kamili, kuwa ufunuo Wangu kamili; hili ndilo kusudi Langu. Usitafute kuwa kama Mimi kwa vitu vya nje (kula kama Mimi, kuvaa nguo sawa na kama Mimi), haya yote hayana maana, na mtajiangamiza tu mkivitafuta vitu hivi. Hii ni kwa sababu wale wanaotafuta kuniiga kwa nje ni vikaragosi wa Shetani, na bidii hii ni mbinu ya Shetani, ni lengo la Shetani. Unatafuta kuwa sawa na Mimi lakini unastahili? Nitakukanyaga mpaka ufe! Kazi Yangu inaendelea daima, ikienea kwa kila taifa duniani. Zifuate hatua Zangu kwa haraka!