Sura ya 90

Wale wote ambao ni vipofu lazima waondoke kutoka Kwangu na hawapaswi kubaki kwa dakika moja zaidi, kwani wale Ninaowataka ni wale wanaoweza kunijua, wanaoweza kuniona na wanaoweza kupata vitu vyote kutoka Kwangu. Na wanaoweza kweli kupata vitu vyote kutoka Kwangu ni nani? Kwa hakika kuna watu wachache sana wa aina hii na hakika watapokea baraka Zangu. Nawapenda watu hawa na Nitawachukua mmoja baada ya mwingine kuwa wasaidizi Wangu wakuu, kuwa maonyesho Yangu, na Nitayafanya mataifa yote na watu wote wanisifu bila kukoma, wakishangilia bila kukoma kwa sababu ya watu hawa. Ee, Mlima Sayuni! Inua bango la ushindi na unishangilie! Kwa maana Mimi naenda ulimwenguni kote na hadi miisho ya dunia, Nikienda katika kila kona ya milima, mito na vitu vyote, kisha kurudi hapa tena. Narudi kwa ushindi na haki, hukumu, ghadhabu na kuchoma, na hata zaidi na wazaliwa Wangu wa kwanza. Vitu vyote ninavyovichukia na watu wote, mambo, na vitu vyote ninavyovichukia navitupa mbali. Mimi ni mshindi na Nimekamilisha yote ambayo Nataka kufanya. Nani anayethubutu kusema Sijakamilisha kazi Yangu? Nani anayethubutu kusema Sijawapata wazaliwa Wangu wa kwanza? Nani anayethubutu kusema kwamba Sijarudi kwa ushindi? Bila shaka wao ni aina ya Shetani, na ni wale wanaoona vigumu kupata msamaha Wangu. Wao ni vipofu, wao ni pepo wabaya na Ninawachukia zaidi. Juu ya mambo haya Nitaanza kufichua ghadhabu Yangu na ukamilifu wa hukumu Yangu, na, kupitia moto Wangu uwakao, kuwasha ulimwengu na dunia kutoka mwisho mmoja hadi mwingine, Nikiangaza kila kona—hii ni amri Yangu ya utawala.

Mara tu mnapoelewa maneno Yangu, mnapaswa kupata faraja kutoka kwayo; hampaswi kuyaacha yapite bila kuyasikiza. Matamshi ya hukumu yanakuja kila siku, kwa hiyo mbona ninyi ni wapumbavu na msiojali hivyo? Mbona hamshirikiani na Mimi? Je, mko tayari sana kwenda kuzimu? Nasema Mimi ni Mungu wa huruma kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, wanangu na watu Wangu, hivyo mnalielewaje hili? Hii si kauli rahisi, na inapaswa kueleweka kutoka kwa mtazamo mzuri. Ee wanadamu vipofu! Nimewaokoa mara nyingi, nikiwatoa kutoka kwa mikono ya Shetani na kutoka kwa kuadhibu ili mpate ahadi Yangu, basi kwa nini ninyi msionyeshe huruma kwa moyo Wangu? Je, yeyote kati yenu anaweza kuokolewa kwa njia hii? Haki yangu, uadhama na hukumu yangu havionyeshi huruma kwa Shetani. Lakini kwa ajili yenu, vipo ili kuwaokoa, lakini ninyi hamna uwezo wa kuelewa tabia Yangu, wala hamjui kanuni zilizo nyuma ya matendo Yangu. Mlifikiri kuwa Natenda bila kujua ukali wa vitendo Vyangu, au kujua malengo yao—wapumbavu mlioje! Naweza kuona wazi watu wote, matukio, na vitu. Ninaelewa kwa uwazi kabisa kiini cha kila mtu, ambayo ni kusema, Ninang’amua kabisa mambo ambayo mtu anashikilia ndani yake mwenyewe. Ninaweza kuona wazi ikiwa mtu ni Yezebeli au mzinzi, na Ninajua ni nani anayefanya nini kwa siri. Usijivunie hirizi zako mbele Yangu—wewe mnyonge! Ondoka hapa sasa! Ili kuepuka kuleta aibu kwa jina Langu, Sina matumizi kwa aina hiyo ya mtu! Hawawezi kulishuhudia jina Langu, lakini badala yake wanatenda kinyume na maendeleo na wanaleta fedheha kwa familia Yangu! Watatolewa nje ya nyumba yangu mara moja. Siwataki. Sitavumilia kuchelewa kwa hata sekunde moja! Kwa watu hao ni bure bila kujali jinsi wanavyotafuta, kwani katika ufalme Wangu wote ni watakatifu na hawana dosari yoyote. Ikiwa ni pamoja na watu Wangu, NIkisema simtaki mtu fulani basi Namaanisha hilo; usisubiri Nibadili mawazo Yangu. Sijali jinsi ulikuwa mzuri Kwangu hapo awali!

Ninawafunulia mafumbo kila siku. Je, mnajua mbinu Yangu ya kuzungumza? Je, ninafichua siri Zangu kwa mujibu wa nini? Je, mnajua? Mara nyingi ninyi husema kwamba Mimi ni Mungu ambaye huwapa riziki kwa wakati ufaao, kwa hivyo mnaelewaje vipengele hivi? Ninafichua siri Zangu kwenu moja baada ya nyingine kwa mujibu wa hatua za kazi Yangu, na Ninawaruzuku kwa mujibu wa mpango Wangu, na hata zaidi kwa mujibu wa vimo vyenu halisi (kuruzuku kunatajwa kwa kurejelea kila mtu katika ufalme). Mbinu Yangu ya kuzungumza ni hivi: Kwa watu walio nyumbani Mwangu Nawapa faraja, Nawaruzuku na Ninawahukumu; kwa Shetani Sionyeshi huruma, na yote ni hasira na uchomaji. Nitatumia amri Zangu za utawala ili kuwatoa nje ya nyumba Yangu mmoja baada ya mwingine wale ambao Sijawaamulia kabla au kuwachagua. Hakuna haja ya kuhisi wasiwasi. Baada ya kuwafanya wafichue maumbo yao ya asili (baada ya wao kutoa huduma kwa wanangu mwishowe), watarudi kwenye shimo lisilo na mwisho, la sivyo Sitawahi kulipumzisha jambo hili na Sitaliacha kamwe. Mara nyingi watu hutaja kuzimu na jahanamu. Lakini maneno haya mawili yanarejelea nini, na tofauti kati yao ni ipi? Je, kweli yanarejelea pembe fulani ya baridi, ya giza? Akili ya binadamu daima inakatiza usimamizi Wangu, wakifikiria kwamba kutafakari kwao kusiko na mpango maalumu ni kuzuri sana. Lakini haya yote ni mawazo yao wenyewe. Kuzimu na jahanamu zote zinarejelea hekalu la uchafu ambalo limeishiwa na Shetani awali au na roho wabaya. Hiyo ni kusema, yeyote ambaye amemilikiwa na Shetani au roho wabaya awali, ni wao ambao ni Kuzimu na wao ndio jahanamu—hakuna kosa kuhusu hilo! Hii ndiyo sababu Nimesisitiza kwa kurudia katika siku za nyuma kwamba Siishi katika hekalu la uchafu. Je, Mimi (Mungu Mwenyewe) Ninaweza kuishi Kuzimu, au jahanamu? Je, huo hauwezi kuwa upuuzi usio na maana? Nimesema hili mara kadhaa lakini ninyi bado hamwelewi Ninachomaanisha. Ikilinganishwa na jahanamu, Kuzimu imepotoshwa zaidi na Shetani. Wale ambao ni wa Kuzimu ndio walio katika hali mbaya sana, na Sijawaamulia kabla watu hawa kabisa; wale walio wa jahanamu ni wale Niliowaamulia kabla, lakini kisha wameondolewa. Kwa maneno rahisi, Sijamchagua hata mmoja wa watu hawa.

Watu mara nyingi hujionyesha kuwa wataalam katika kutoelewa maneno Yangu. Kama Singeonyesha wazi wazi na kufafanua mambo kidogo kidogo, nani kati yenu angeelewa? Ninyi mnaamini tu nusu hata ya maneno Ninayozungumza, sembuse mambo ambayo hayajatajwa hapo awali. Sasa, migogoro ya ndani imeanza ndani ya mataifa yote: Wafanyakazi wakibishana na viongozi, wanafunzi na walimu, wananchi na maofisa wa jeshi wa serikali, na shughuli zote kama hizi zinazosababisha vurugu kwanza zinaibuka katika kila taifa, na yote ni sehemu moja tu inayotoa huduma Kwangu. Na kwa nini Nasema inanitolea huduma? Je, Ninafurahia bahati mbaya ya watu? Je, Ninakaa bila kusikiza? Bila shaka hapana! Kwa maana huyu ni Shetani anayepiga kelele katika maumivu yake ya mwisho ya kifo na kutoka kwa upande hasi, hii inafanya kazi kama foili[a] kwa mamlaka Yangu na kama foili kwa matendo Yangu ya ajabu. Yote ni ushuhuda wa nguvu ambao unanishuhudia Mimi, na ni silaha ambayo inatumika kumshambulia Shetani. Wakati tu mataifa yote ya dunia yanapigania ardhi na ushawishi, wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi tunatawala kama wafalme pamoja na kuyashughulikia, na inazidi kabisa mawazo yao kwamba chini ya mazingira haya mabaya, ufalme Wangu unafanikishwa kabisa kati ya mwanadamu. Zaidi ya hayo, wanapong’ang’ania mamlaka na kutaka kuwahukumu wengine, wengine wanawahukumu na wanachomwa na ghadhabu Yangu—ni huzuni iliyoje! Ni huzuni iliyoje! Ufalme Wangu unatimizwa miongoni mwa wanadamu—hili ni tukio tukufu kweli!

Kuwa mwanadamu (iwe ni watu wa ufalme Wangu au uzao wa Shetani), lazima nyote muone matendo Yangu ya ajabu, vinginevyo Sitalipumzisha jambo hili kamwe. Hata kama uko tayari kukubali hukumu Yangu, bado haitakubalika kama hujaona matendo Yangu ya ajabu. Watu wote lazima washawishike kwa moyo, kwa neno na kwa kuona, na hakuna mtu anayeweza kuruhusiwa kupenyeza tu. Watu wote lazima wanipe Mimi utukufu. Mwishowe, Nitalifanya hata joka kubwa jekundu liinuke na kunisifu kwa ajili ya ushindi Wangu. Hii ni amri Yangu ya utawala—je, utaikumbuka? Watu wote lazima wanisifu bila kukoma na kunipa utukufu!

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Sura ya 89

Inayofuata: Sura ya 91

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp