Sura ya 88

Watu hawawezi tu kuwaza kiasi ambacho mwendo Wangu umezidisha kasi: Haya ni maajabu ambayo yametokea isiyoeleweka kwa mwanadamu. Kasi Yangu imeendelea tangu uumbaji wa dunia, na kazi Yangu haijawahi kusimama. Ulimwengu wote hubadilika siku kwa siku na watu, pia, wanabadilika mara kwa mara. Hizi zote ni sehemu ya kazi Zangu, zote ni sehemu ya mipango Yangu na, aidha, zote ni za usimamizi Wangu, na hakuna binadamu anayejua au kuelewa hivi vitu. Wakati tu Mimi Mwenyewe Ninapowaambia, wakati tu Ninapowasiliana nanyi uso kwa uso, ndipo mnajua hata kiasi kidogo kabisa; vinginevyo, hakuna kabisa yeyote anayeweza kujua kuhusu mpango makini wa mpango Wangu wa usimamizi. Hii ndiyo nguvu Yangu kuu, na aidha, haya ndiyo matendo Yangu ya ajabu. Hivi ndivyo vitu ambavyo hakuna anayeweza kuvibadilisha. Kwa hivyo, kile Ninachosema leo ndicho kinachofanyika, na hii haiwezi kubadilika tu. Dhana za binadamu hazina hata ufahamu kidogo juu Yangu—zote ni kuropoka kwa upuuzi! Usifikiri kwamba umepata ya kutosha au kwamba umeridhika! Ninakwambia hivi: Wewe bado una mbali pa kwenda! Kwa mpango Wangu wote wa usimamizi, mnajua kidogo tu, kwa hivyo lazima msikize kile Ninachosema na mfanye chochote Ninachowaambia mfanye. Tendeni kulingana na mapenzi Yangu katika kila kitu, na hakika mtapata na baraka Zangu; yeyote aaminiye anaweza kupokea, ilhali yeyote asiyeamini atakuwa na hiyo “hakuna” ambayo alidhania imetimizwa ndani yake. Hii ni haki Yangu, na, hata zaidi ni uadhama Wangu, hasira Yangu na kuadibu Kwangu. Sitamwacha yeyote aepuke na hata wazo au kitendo kimoja.

Baada ya kuyasikia maneno Yangu, watu wengi huogopa na kutetemeka, nyuso zao zikijikunja kwa wasiwasi. Je, Nimekukosea kwa kweli? Je, inawezekana kuwa kwamba wewe si mtoto wa joka kuu jekundu? Unajifanya hata kuwa mzuri! Unajifanya hata kuwa mwana Wangu mzaliwa wa kwanza! Je, unafikiri Mimi ni kipofu? Je, unafikiri Siwezi kutofautisha kati ya watu? Mimi ndiye Mungu anayechunguza mioyo ya ndani ya watu: Hili ndilo Ninalowaambia wana Wangu, na ndilo Ninalowaambia ninyi pia, watoto wa joka kuu jekundu. Ninaona kila kitu kwa wazi, bila kufanya hata kosa dogo kabisa. Ningekosaje kujua kile Ninachokifanya? Niko wazi kabisa kuhusu kile Ninachofanya! Kwa nini Nasema kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe, Muumbaji wa ulimwenguni na vitu vyote? Kwa nini Nasema kwamba Mimi ndiye Mungu anayechunguza mioyo ya ndani ya watu? Ninajua vyema hali ya kila mtu. Je, mnafikiri Sijui cha kufanya au cha kusema? Hili haliwahusu. Iweni makini msiuwawe kwa mkono Wangu; mtapoteza kwa njia hiyo. Amri Zangu za utawala hazina msamaha. Je, mnaelewa? Haya yote yaliyo hapa juu ni sehemu za amri Zangu za utawala. Kuanzia siku ile Ninayowaambia kuzihusu, mkitenda dhambi zozote zaidi, kutakuwa na adhabu, kwa sababu awali hamkuelewa.

Sasa Nawatangazia rasmi amri Zangu za utawala (zinaanza kazi kuanzia siku zilipotangazwa rasmi, kutoa kuadibu tofauti kwa watu tofauti):

Natimiza ahadi Zangu, na kila kitu kiko mikononi Mwangu: Yeyote aliye na shaka hakika atauwawa. Hakuna nafasi ya huruma yoyote; wataangamizwa mara moja, hivyo kuondoa chuki kutoka moyoni Mwangu. (Kuanzia sasa inathibitika kwamba yeyote anayeuwawa lazima asiwe mshiriki wa ufalme Wangu, na lazima awe wa ukoo wa Shetani.)

Kama wazaliwa wa kwanza wa kiume, ni sharti mtunze nafasi zenu na mtimize wajibu wenu vema, na msiwe wadadisi. Ni sharti mjitolee kwa mpango Wangu wa usimamizi, na popote muendapo, ni sharti muwe na ushuhuda mzuri Kwangu na mlitukuze jina Langu. Msitende vitu vya aibu; kuweni mfano kwa wana Wangu wote na watu Wangu. Msiwe waasherati hata kwa muda kidogo: Lazima muonekane kila mara mbele ya kila mtu mkiwa na utambulisho wa wazaliwa wa kwanza wa kiume, na msiwe watumwa; badala yake, mnapaswa kutembea kwenda mbele kwa kujiamini. Nawaomba mlitukuze jina Langu, sio kulitia aibu jina Langu. Wale ambao ni wazaliwa wa kwanza wa kiume kila mmoja wao ana kazi yake binafsi, na hawawezi kufanya kila kitu. Hili ndilo jukumu Nililowapa, na halipaswi kuepukwa. Lazima mjitolee kwa mioyo yenu yote, kwa akili zenu zote na nguvu zenu zote, kwa kutimiza kile ambacho Nimewaaminia.

Kuanzia leo kuendelea, katika Ulimwengu wote, jukumu la kuongoza wana Wangu wote na watu Wangu wote litakabidhiwa wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume walitimize, na Nitamwadibu yeyote asiyeweza kuutoa moyo wake wote na akili katika kulitimiza. Hii ni haki Yangu. Sitawasamehe au kuwabembeleza hata wazaliwa Wangu wa kiume wa kwanza.

Ikiwa kuna yeyote kati ya wana Wangu wote au kati ya watu Wangu wote anayemdhihaki na kumtusi mmoja wa wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume, Nitamwadhibu vikali, kwa sababu wana Wangu wazaliwa wa kwanza wananiwakilisha Mimi Mwenyewe; kile ambacho mtu anawafanyia, ananifanyia Mimi pia. Hii ndiyo kali zaidi kati ya amri Zangu za utawala. Nitawaruhusu wazaliwa Wangu wa kwanza, kulingana na matamanio yao, watoe haki Yangu dhidi ya yeyote kati ya wana Wangu wote na watu Wangu anayeikiuka amri hii.

Taratibu Nitamtenga yeyote anayenitazama kipuuzi na anayelenga tu chakula Changu, mavazi na usingizi anayeshughulikia tu mambo Yangu ya nje na haudhukuru mzigo Wangu, na hatilii maanani kutimiza kazi zake inavyostahili. Hili linaelekezwa kwa wote walio na masikio.

Yeyote amalizaye kunifanyia huduma lazima aondoke kwa utiifu bila vurugu yoyote. Kuwa makini, la sivyo Nitakushughulikia. (Hii ni amri ya ziada).

Wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume watachukua fimbo ya chuma kuanzia sasa na kuendelea na kuanza kutekeleza mamlaka Yangu kutawala mataifa na watu wote, kutembea kati ya mataifa na watu wote na kuzitekeleza hukumu Zangu, haki, na uadhama kati ya mataifa yote na watu. Wana Wangu wote na watu Wangu wote wataniogopa, watanipa sifa, watanishangilia, na kunitukuza bila kukoma kwa sababu mpango wangu wa usimamizi umekamilika na wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume wanaweza kutawala nami.

Hii ni sehemu ya amri Zangu za utawala; baada ya hili, Nitawaambia kuyahusu kazi inapoendelea. Kutokana na amri za utawala zilizoko hapo juu, mtaona kasi ambayo kwayo Nafanya kazi Yangu, na vile vile ni hatua ipi ambayo kazi Yangu imefika. Hili litakuwa thibitisho.

Nimeshamhukumu Shetani. Kwa sababu mapenzi Yangu hayapingwi na kwa sababu wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume wametukuzwa pamoja na Mimi, tayari Nimetumia haki Yangu na uadhama juu ya dunia na vitu vyote ambavyo ni mali ya Shetani. Sikiinui kidole wala kumsikiliza Shetani kabisa (kwa sababu hastahili hata kuzungumza na Mimi). Nazidi tu kufanya kile Ninachotaka kufanya. Kazi Yangu inaendelea kwa ulaini, hatua kwa hatua, na mapenzi Yangu hayapingwi duniani kote. Hili limemwaibisha Shetani kwa kiwango na ameangamizwa kabisa, lakini hili peke yake halijatimiza mapenzi Yangu. Naruhusu pia wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume kutekeleza amri Zangu za utawala juu ya mambo yote yaliyo ya Shetani. Kwa upande mmoja, kile Ninachomruhusu Shetani aone ni hasira Yangu kuelekea kwake; kwa upande, mwingine Namruhusu auone utukufu Wangu (kuona kwamba wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume ndio mashahidi wakubwa sana kwa udhalilishaji wa shetani). Simwadhibu Mimi mwenyewe; badala yake, bali Naruhusu wazaliwa wangu wa kwanza wa kiume kutekeleza haki Yangu na uadhama. Kwa sababu Shetani alikuwa anawanyanyasa wana Wangu, kuwatesa wana Wangu na kuwaonea wana Wangu, leo, baada ya huduma yake kuisha, Nitawaruhusu wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume waliokomaa washughulike nalo. Shetani amekuwa hana nguvu dhidi ya maangamizi. Kiharusi cha mataifa yote duniani ndio ushuhuda mzuri zaidi; watu kupigana na nchi zikiwa vitani ni onyesho la wazi kabisa la kuanguka kwa ufalme wa Shetani. Sababu iliyofanya Sikuonyesha ishara na maajabu yoyote hapo zamani ilikuwa ili kumletea Shetani fedheha na kulitukuza jina Langu hatua kwa hatua. Wakati shetani ameangamizwa kabisa Naanza kuonyesha nguvu Zangu: kile Ninachosema kinatokea, na vitu vya kuvuka mipaka ambavyo havina usawa na fikira za kibinadamu vitatimia (hivi vinarejelea baraka zinazokuja karibuni). Kwa sababu Mimi ndimi Mungu Mwenyewe wa vitendo na Sina amri, na kwa sababu Nazungumza kulingana na mabadiliko katika mpango Wangu wa usimamizi, kwa hivyo kile Nilichosema zamani si lazima kiwe cha kutumika sasa. Msishikilie mawazo yenu wenyewe! Mimi siye Mungu anayezingatia amri; Kwangu, kila kitu ni huru, cha kuvuka mipaka, na kimeachiliwa kabisa. Labda kilichosemwa jana kimepitwa na wakati leo, au huenda kikawekwa kando leo (hata hivyo, amri Zangu za utawala, kwa sababu zimetangazwa rasmi hazitabadilika kamwe). Hizi ndizo hatua katika mpango Wangu wa usimamizi. Msishikilie kanuni. Kila siku kuna mwanga mpya na kuna ufunuo mpya, na huo ndio mpango Wangu. Kila siku mwanga wangu utafichuliwa kwako na sauti Yangu itaachiliwa kwa ulimwengu dunia. Je, unaelewa? Huu ni wajibu wako, jukumu ambalo Nimekuaminia. Ni lazima usilipuuze hata kidogo. Nitawatumia mpaka mwisho watu Ninaowaidhinisha, na hili halitabadilika kamwe. Kwa sababu Mimi ni mwenyezi Mungu, Najua ni mtu wa aina gani anayepaswa kufanya kitu kipi, na vile vile ni mtu wa aina gani anaweza kufanya kitu kipi. Huu ndio uweza Wangu.

Iliyotangulia: Sura ya 87

Inayofuata: Sura ya 89

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp