Sura ya 61

Ukiwa na ufahamu wa hali yako mwenyewe basi utafanikisha mapenzi Yangu. Kwa kweli, mapenzi Yangu si magumu kushika, ni kwamba tu katika siku zilizopita hukuweza kutafuta kulingana na lengo Langu. Ninachotaka si dhana wala fikira za binadamu, sembuse pesa zako wala mali yako. Ninachotaka ni moyo wako, unaelewa? Haya ni mapenzi Yangu, na hata zaidi ni kitu ambacho Nataka kupata. Watu daima hutumia dhana zilizo akilini mwao kunifanyia maamuzi, na kuhakiki kimo Changu wakitumia Vipimo vyao. Kwa binadamu, hiki ni kitu kigumu sana kujihusisha nacho, na ndicho Ninachokichukia na kusinywa nacho zaidi, mnaona? Kwa sababu hii ndiyo tabia ya Shetani inayoonekana zaidi. Na vimo vyenu ni vidogo, hivyo kila mara mnaanguka katika njama za kijanja za Shetani. Hamuwezi hata kuzitambua! Nimewaambia mara nyingi muwe waangalifu kila wakati na kwa kila namna, kwamba msidanganywe na Shetani. Lakini hamskilizi na kwa wepesi wa moyo mnapuuza Ninayoyasema, hivyo mnaishia kupoteza maishani mwenu na majuto huja yakiwa yamechelewa mno. Vyovyote vile, si itakuwa vizuri kwako kuchukua hili kama funzo kwa ajili ya kutafuta kwako kwa baadaye. Nakwambia, kuwa hasi kwa urahisi kutaleta hasara kwa maisha yako na itakuwa yenye ukali mwingi zaidi. Kwa kujua hili, unafaa uamke, sivyo?

Watu wana pupa ya matokeo ya haraka na wanaona tu yalio mbele ya macho yao. Ninaposema Nimeanza kuwaadhibu walio mamlakani, mnakuwa hata wenye wasiwasi zaidi, na mnauliza: “Mbona watu hao bado wako mamlakani? Si Mungu amezungumza maneno matupu?” Dhana za binadamu zimekita mizizi sana! Hamwelewi maana ya yale Nisemayo. Wale ambao Nawaadhibu ni wale waovu, wale ambao wananidharau, wale ambao hawanifahamu, na Nawapuuza wale wanaoniamini lakini hawatafuti ukweli. Nyinyi ni wapumbavu sana! Hamjaelewa yale ambayo Nimesema hata kidogo! Ingawa hii ndiyo hali, bado mnajisifu mkifikiri kwamba mmekomaa, kuwa mnaelewa mambo na kuwa mnaweza kufahamu mapenzi Yangu. Mara kwa mara Mimi husema vitu vyote na mambo yote yanamtumikia Kristo, lakini kwa kweli mnayaelewa maneno haya? Mnayajua maneno haya kweli? Nimesema awali kuwa Simwadhibu mtu yeyote bila subira. Kila mtu katika ulimwengu dunia hufuata mipango Yangu inayofaa: Wale ambao ni walengwa wa adhabu Yangu, wale wanaomtumikia Kristo (hawa Sitawaokoa), wale ambao wameteuliwa na Mimi, na wale ambao wamechaguliwa nami lakini baadaye wanakuwa walengwa wa kuondolewa, wote hawa Ninawashika mkononi Mwangu, bila hata kukutaja wewe—ambaye Nimemchagua—ambaye Ninamwelewa hata zaidi. Vitu Nifanyavyo katika awamu hii na vitu Nitakavyovifanya katika awamu ijayo vyote vinafuata mipango Yangu ya busara. Huhitaji kupanga lolote kwa ajili Yangu kabla; ngoja tu starehe yako! Hiki ni kitu ambacho unastahili. Natawala vitu vilivyo Vyangu na Sitawahurumia kwa wepesi wale watakaothubutu kunung’unika ama watakaothubutu kuwa na maoni mengine kunihusu. Mara kwa mara siku hizi Ninalipuka kwa hasira, kwa kuwa mpango wa amri za utawala ambazo Nimepanga zimeendelea hadi katika hatua hii. Usifikiri kuwa Sina hisia. Kwa kuwa Nimesema awali hakuna mtu hata mmoja, tukio ama kitu kinachothubutu kuzuia hatua Zangu za kuendelea. Natenda Nisemayo, na hiki ndicho Mimi nilicho, na hata zaidi ni dalili inayoonekana sana ya tabia Yangu. Nawatendea watu wote kwa usawa, kwani nyote ni wana Wangu, na Nawapenda nyote. Ni baba yupi asiyechukua wajibu wa maisha ya mwanawe? Ni baba yupi hafanyi bidii usiku na mchana kwa ajili ya siku za baadaye za mwanawe? Na nani kati yenu anaweza kujua? Nani anaweza kuuonyesha moyo Wangu huruma? Daima mnapanga mipango na utaratibu wa anasa zenu za kimwili na hamna utambuzi wowote wa moyo Wangu. Ninauhangaisha moyo Wangu hadi unavunjika kwa sababu yenu, lakini daima mnazitamani anasa za kimwili, kula na kunywa, kulala, jinsi mnavyovaa—hamna dhamiri hata kidogo? Kama hii ndiyo hali, basi ninyi ni wanyama waliovalia nguo za binadamu. Ninayosema si yasiyostahili na lazima muweze kuyastahimili. Hii ndiyo njia nzuri kabisa ya kuwaokoa na hata zaidi ni pahali ambapo hekima Yangu ipo—kuupiga udhaifu wa nguvu za Shetani, kumshinda kabisa na kumwangamiza kabisa. Mradi tu mtubu na kuhakikisha kuwa mnaweza kunitegemea Mimi kuindoa asili ya zamani na kuishi kwa kudhihirisha umbo la mtu mpya, moyo Wangu utaridhika kikamilifu, kwani huku ni kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, kuwa na ushuhuda kwa jina Langu, na ndicho kinachonifurahisa zaidi.

Kila wakati lazima uwe karibu na Mimi, na inaweza kuonekana kuwa mwendo Wangu unaongeza kasi siku kwa siku. Kama wakati wowote unakosa ushirika wa kiroho, basi hukumu Yangu italetwa juu yako mara moja. Kwa hoja hii una ufafanuzi wa kina. Sio kwa sababu Sikupendi ndiyo Nakuadibu, bali Nakufunza nidhamu kwa sababu ya upendo Wangu kwako. Vinginevyo hungekua na daima ungepotoshwa bila kuzuiwa na Roho Mtakatifu. Hii hata zaidi ni uso wa hekima Yangu.

Iliyotangulia: Sura ya 60

Inayofuata: Sura ya 62

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp