Sura ya 62

Kuyaelewa mapenzi Yangu hakufanywi ili tu kwamba uweze kujua, ila pia kwamba uweze kutenda kulingana na nia Yangu. Watu hawauelewi moyo Wangu. Ninaposema huku ni mashariki, wanalazimika kuenda na kutafakari, wakijiuliza, “Kweli ni mashariki? Pengine sio. Siwezi kuamini kwa urahisi hivyo. Nahitaji kujionea mwenyewe.” Ninyi watu ni wagumu sana kushughulikia, na hamjui utii wa kweli ni nini. Mnapoijua nia Yangu kisha mwende kuitenda kwa kusita—hakuna haja ya kuifikiria! Daima unashuku Ninachokisema na kukielewa kwa upuuzi, hivyo basi unawezaje kuwa na utambuzi wowote wa kweli? Kamwe hutafuti kuingia katika maneno Yangu. Kama ambavyo Nimesema awali, Ninachotamani ni wachache waliochaguliwa, sio watu wengi sana. Wale wasioweka umuhimu kwa kuingia katika maneno Yangu hawastahili kuwa askari wazuri wa Kristo, ila badala yake wanatenda kama vikaragosi vya Shetani na kuingilia kazi Yangu. Usifikiri hili ni suala dogo. Yeyote anayeingilia kazi Yangu anazikosea amri Zangu za utawala, na bila shaka Nitamfundisha nidhamu kwa ukali. Yaani, kuanzia sasa kuendelea, ukigeuka kutoka Kwangu kwa muda basi hukumu Yangu itakufikia. Usipoyaamini maneno Yangu basi jaribu ujionee, uone ni hali gani uliyo katika ukiishi katika mwanga wa uso Wangu, na uko katika hali gani unaponiacha.

Siogopi kwamba huishi katika roho. Kazi Yangu imeendelea hadi kwa hatua ya sasa, hivyo unaweza kufanya nini? Nafanya vitu kwa hatua, hivyo hakuna haja ya wewe kuwa na wasiwasi. Nitafanya kazi Yangu Mimi mwenyewe. Ninapofanya kitu watu wote wanaridhishwa kabisa, vinginevyo Nitawashughulikia kwa kuwaadibu kwa ukali zaidi. Hili linahusisha amri Zangu za utawala zaidi. Inaweza kuonekana kwamba amri Zangu za utawala tayari zimeanza sasa kutangazwa na kutekelezwa, zisifichwe tena. Ni lazima uone hili kwa uwazi! Sasa heshima zote zinahusu amri Zangu za utawala na yeyote anayezikosea lazima apate hasara. Hili bila shaka si suala dogo. Kweli mnatambua hili? Mnaelewa kipengele hiki vizuri kabisa? Sasa Naanza kushiriki: Mataifa yote na watu wote wa dunia wanaongozwa mikononi Mwangu na, bila kujali dini yao, wote lazima waje kwa kiti Changu cha enzi. Bila shaka, wengine wanaopokea hukumu watatupwa katika shimo la kina kirefu (ni walengwa wa uangamizi ambao watateketezwa kabisa na hawatabaki tena), na wengine wanaokubali jina Langu baada ya kuhukumiwa watageuka watu wa ufalme Wangu (watafurahia kwa miaka 1,000 pekee). Wale kati yenu watakaoshikilia ufalme na Mimi milele baadaye, na kwa vile awali mliteseka kwa ajili Yangu, Nitabadilisha mateso yenu na baraka Nitakazowapa bila kikomo; wale kati ya watu Wangu watabaki tu wakitoa huduma kwa Kristo. Hiyo raha hairejelei tu raha, ila badala yake kwamba wale watu wanawekwa mbali na kupitia maafa. Hii ndiyo maana ya ndani ya matakwa Yangu kwenu sasa kuwa makali zaidi, na kuhusu kila kitu sasa kugusa amri Zangu za utawala. Kwa maana iwapo hamkukubali mafundisho Yangu basi hakungekuwa na njia ya Mimi kuwapa kile mnachopaswa kurithi. Ingawa hali iko hivi, bado mnaogopa kuteseka, mnaogopa majeraha yafikie roho zenu, daima mkifikiri kuhusu mwili na daima mkipanga na kuratibu kwa ajili yenu wenyewe. Je, Sijawafanyia mipango ya kuwafaa ninyi? Hivyo kwa nini tena na tena unajifanyia mipango yako mwenyewe? Unanitukana! Sivyo? Ninakupangia kitu lakini unakikana kabisa na kufanya mipango yako mwenyewe.

Mnaweza kuzungumza vyema, lakini kwa hakika hamtii mapenzi Yangu hata kidogo. Nakuambia, Sitasema kabisa kwamba kuna yeyote miongoni mwenu ambaye anaweza kuyafikiria mapenzi Yangu kwa kweli. Ingawa vitendo vyako vinaweza kukubaliana na mapenzi Yangu Sitakusifu hata kidogo. Hii ni njia Yangu ya wokovu. Ingawa hali iko hivi, bado mnaridhika wakati mwingine, mkijiona kuwa wa kushangaza na kuwadharau wengine wote. Hiki ni kipengele kimoja cha tabia potovu ya mwanadamu. Nyote mnakubali hoja hii Ninayotoa, lakini juu juu pekee. Ili kuweza kubadilika kwa kweli unahitaji kunikaribia; kushiriki na Mimi na Nitakupa neema. Watu wengine wanafikiri kukaa kwa kutulia tu na kuvuna kile ambacho wengine wamekipanda, wakihisi kwamba ili kuvaa mavazi, wanahitaji tu kunyoosha mikono yao, na ili kula, wanahitaji tu kufungua midomo yao, hata wakingojea wengine wawatafunie chakula chao kabla wawe radhi kukimeza. Watu kama wao ni wapumbavu zaidi, wanaopenda kula kile ambacho wengine wamekila tayari, na hili ni dhihirisho la kipengele kizembe zaidi cha mwanadamu. Kwa kusikia haya maneno Yangu, ni lazima usiyapuuze tena. Kutahadhari kabisa ndio njia sahihi pekee. Kisha mapenzi Yangu yanaweza kuridhishwa, na huu ni utii wa aina bora zaidi.

Iliyotangulia: Sura ya 61

Inayofuata: Sura ya 63

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp