Sura ya 63

Zielewe hali zako mwenyewe, na zaidi ya hayo, kuwa wazi kuhusu njia unayohitaji kutembea; usubiri tena Mimi niyainue masikio yako na kukuonyesha mambo. Mimi ni Mungu ninayeangalia moyo wa ndani kabisa wa mwanadamu nami najua kila fikra na wazo lako, hata zaidi Naelewa matendo na tabia yako. Lakini matendo yako na tabia yana ahadi Yangu? Je, yana mapenzi Yangu? Umetafuta haya kwa kweli? Je, kweli umetumia wakati wowote kuhusu suala hili? Je, kweli umefanya jitihada yoyote? Mimi sikukosoi. Ninyi mnapuuza tu kipengele hiki! Siku zote mmechanganyikiwa na hamwezi kuona chochote kwa uwazi. Je, mnafahamu sababu ya hili ni nini? Je, ni kwa sababu mawazo yenu hayako wazi na dhana zenu zina msingi madhubuti sana, na kuongeza kwamba ukweli kwamba hamuonyeshi fikira zozote kuhusu mapenzi Yangu. Baadhi ya watu watasema: “Unawezaje kusema hatuonyeshi fikira zozote kuhusu mapenzi Yako? Mara kwa mara tunajaribu kuelewa mapenzi Yako, lakini hatuwezi kuyaelewa, hivyo tunaweza kufanya nini? Je, kweli Unaweza kusema kwamba sisi hatufanyi jitihada yoyote?” Acha nikuulize: Je, unathubutu kusema kwamba kweli wewe ni mwaminifu Kwangu? Na nani anathubutu kusema kwamba anajitoa Kwangu katika uaminifu kamili? Nina hofu kwamba hakuna mmoja kati yenu anayeweza kusema hivi. Kwa sababu, ni wazi Mimi kusema, kila mmoja wenu ana uwezo wake wa kuchagua na mambo yake mwenyewe anayoyapenda, na hata zaidi nia zenu wenyewe. Msiwe wadanganyifu! Nilielewa kabisa zamani sana yote mnayoyafikiria mioyoni mwenu; bado Nahitaji kufafanua hili? Lazima uchunguze zaidi kutoka katika kila kipengele (mawazo na dhana zako, kila kitu unachosema, kila neno, kila nia na motisha katika kila hatua unayoichukua); kwa njia hii utapata kufikia kuingia kila kipengele, na hata zaidi utakuwa na uwezo wa kujiandaa na ukweli kamili.

Kama Singewaambia hivi bado mngekuwa mmechanganyikiwa, mkitamani anasa za mwili kwa siku nzima, bila ya hamu yoyote ya kuonyesha mapenzi Yangu nadhari yoyote. Daima Nautumia mkono Wangu wenye upendo kuwaokoa, mnajua hivyo? Je, mmekuja kutambua hili? Nakupenda kwa dhati; unathubutu kusema unanipenda kwa dhati? Jiulize, unaweza kweli kuja mbele zangu kupokea ukaguzi Wangu kuhusu kila tendo lako? Je, unaweza kweli kuniruhusu Nichunguze kila mwenendo wako? Nasema umepotoka nawe uko tayari kujitetea. Hukumu Yangu inakujia; sasa lazima uamke katika ukweli! Yote Nisemayo ni ukweli, na yanaonyesha hali halisi ndani yako. Aa, wanadamu! Ninyi ni wagumu sana kuwashughulikia. Ni wakati tu Ninapokuonyesha hali yako halisi ndipo mnaamini katika mioyo na kwa neno. Nisipofanya hivi, basi kila mara mnashikilia mawazo yenu ya zamani na kushikamana na njia zenu za kufikiri, mkifikiri kwamba hakuna mtu yeyote duniani aliye mwerevu zaidi yenu. Je, hivi si wewe ni mwenye kujidai? Je, si ni wewe kujiingiza katika majisifu na kuridhika, na majivuno? Sasa unapaswa kutambua hili! Usijidhani mwerevu au wa ajabu, lakini badala yake ni lazima uwe daima na ufahamu wa mapungufu yako mwenyewe na tabia zako mwenyewe yenye udhaifu. Kwa njia hii, azimio lako la kunipenda halitapungua, lakini litakuwa imara zaidi na zaidi, na hali zako mwenyewe zitakuwa bora na bora zaidi; muhimu zaidi maisha yako yataendelea zaidi milele, siku baada ya siku.

Utakapofahamu mapenzi Yangu basi utajijua, na hivyo kunijua Mimi bora zaidi na kuendelea zaidi katika uhakika wako kunihusu Mimi. Katika wakati wa sasa, kama mtu hawezi kufikia asilimia tisini wa uhakika kunihusu Mimi, lakini badala yake anaendelea kuwa juu dakika moja na chini dakika ya pili, akiwa moto na baridi, basi Nasema mtu huyo kwa hakika ni kitu cha kuachwa. Asilimia kumi iliyobaki hutegemea kabisa nuru na mwangaza Wangu, hivyo kufikia asilimia mia moja ya uhakika kunihusu. Sasa hivi, kumaanisha leo, wangapi wanaweza kupata aina hii ya kimo? Daima Nayaonyesha mapenzi yangu kwako na hisia za maisha daima zinakimbia ndani yako, hivyo kwa nini usitende kulingana na Roho? Je, una hofu ya kufanya makosa? Hivyo basi kwa nini usizingatie mazoezi kabisa? Nakwambia, huwezi kufahamu mapenzi Yangu kwa kujaribu mara moja au mbili; lazima kuwe na mchakato. Nimesema hivi mara nyingi, hivyo kwa nini usiiweke katika vitendo? Je, hufikiri unakuwa mkaidi? Unataka kumaliza kila kitu mara moja, huko radhi kamwe kufanya juhudi yoyote au kutumia muda wowote kwa kitu chochote. U mpumbavu jinsi gani na hata zaidi u mjinga!

Je, hamfahamu kwamba daima Mimi huzungumzia mambo bila kuyaficha maneno Yangu? Kwa nini daima ninyi ni wapumbavu, wenye kutojali na wagumu kuelewa? Mnapaswa kujichunguza zaidi, na mnapaswa kuja mbele Zangu mara nyingi zaidi ikiwa kunacho kitu chochote msich0kielewa. Nasema kwako, Nazungumza kwa njia hizi mbalimbali ili kuwaelekeza mbele Zangu; kwa nini, baada ya muda mrefu sana, bado hamtambui hili? Je, ni kwa sababu maneno Yangu yamewafanya nyote kuchanganyikiwa? Au ni kuwa bado hamjashughulikia kila moja ya maneno Yangu kwa uzito? Mnapoona maneno Yangu mnakuwa na ufahamu mzuri kujihusu wenyewe, na mnasema kuwa mnanidai au kwamba hamuwezi kuyafahamu mapenzi Yangu. Na baada ya hayo? Ni kama hamjakuwa na lolote la kufanya na vitu hivi, kana kwamba wewe si mtu tu ambaye anaamini katika Mungu. Je, si wewe tu unapokea tu habari kwa haraka bila kujipa muda wa kuiwaza? Wakati unayafurahia maneno Yangu, ni kama kutazama maua kwa haraka ukiwa kwenye mgongo wa farasi, bila kujaribu kamwe kufahamu mapenzi Yangu ndani ya maneno Yangu. Hivi ndivyo watu walivyo: Mara zote wao hupenda kuonekana wanyenyekevu, na aina hii ya mtu ni mwenye kuchukiza zaidi. Wanapokuwa pamoja na wengine kushiriki, siku zote hupenda kusambaza ufahamu wao kujihusu mbele ya watu wengine, na kuwafanya wengine waone kwamba wao ni mtu ambaye anaonyesha kuufikiria mzigo Wangu, wakati kwa kweli wao ni wajinga zaidi. (Hawashiriki umaizi wao ama ufahamu wao kweli kunihusu Mimi na ndugu zao, lakini badala yake wanajiweka wenyewe tu katika maonyesho na kujionyesha mbele ya watu wengine, Nawachukia watu hawa kabisa, kwa kuwa wao hunikashifu na kuniumbua.)

Mara kwa mara Mimi huifanya wazi miujiza yangu mikubwa zaidi kwenu—hamuwezi kuiona? Kile kinachoitwa ukweli kinaishi kwa kudhihirishwa na wale ambao wananipenda kwa dhati—hamjaiona? Si hili ni thibitisho bora ambalo mnaweza kunijua? Je, hili halishuhudii bora Kwangu? Lakini hamlitambui hilo. Niambieni, nani anaweza kuishi kwa kudhihirisha hali halisi katika dunia hii iliyochangamana ambayo ni chafu, yenye taka, na iliyopotoshwa na Shetani? Si watu wote ni waovu na watupu? Hata hivyo, maneno Yangu yamefikia kilele chake; hakuna maneno ambayo yanaweza kueleweka kwa urahisi zaidi kuliko haya. Hata mpumbavu mkubwa anaweza kuyasoma maneno Yangu na kuyaelewa, hivyo si kwamba ninyi tu hamjafanya jitihada yoyote?

Iliyotangulia: Sura ya 62

Inayofuata: Sura ya 64

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp