Sura ya 8

Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa Roho, sauti Yake huelekezwa kwa wanadamu wote. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa mwanadamu, sauti Yake huelekezwa kwa wote wafuatao uongozi wa Roho Wake. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu (kile ambacho watu hutaja kama mtazamaji), Anaonyesha neno Lake moja kwa moja kwa watu ili watu wamwone kama mtoa maoni, na huonekana kwamba kutoka kinywani Mwake hutoka mambo yasiyo na kikomo ambayo mwanadamu hayajui, mambo ambayo mwanadamu hawezi kuelewa. Je, hilo si sahihi? Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa Roho hilo huwashangaza binadamu wote. “Upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo mno na imani yake Kwangu ni ndogo ajabu. Kama sehemu kubwa ya maneno Yangu haingeelekezwa kwa udhaifu wa mwanadamu, angejigamba na kutia mambo chumvi, na angehubiri na kubuni nadharia zenye kuvutia, ni kama aliye na maarifa yote na anayejua yote kuhusu masuala duniani.” Maneno haya hayafichui tu tabia halisi ya mtu na kufichua nafasi ya Mungu ndani ya mioyo ya watu, bali pia hufichua maisha yote ya wanadamu. Kila mtu huamini kwamba yeye ni wa ajabu na hata hajui kwa kweli kuna neno linaloitwa “Mungu” kwa hiyo yeye hubuni nadharia nyingi za kuvutia. Hata hivyo, huku “kubuni nadharia nyingi za kuvutia” si “kunena” kwa hali ambayo watu wanaielewa. Badala yake, ina maana kwamba binadamu wamepotoshwa na Shetani kiasi kwamba kila kitu wafanyacho humkaidi Mungu na humpinga Mungu wazi, na kwamba kiini hasa cha kile mwanadamu hufanya hutoka kwa Shetani na kiko katika upinzani kwa Mungu, ni kitendo cha kujitegemea, na huenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Hii ndiyo maana Mungu husema kwamba watu wote hubuni nadharia nyingi za kuvutia. Kwa nini Mungu asema kwamba sehemu kubwa ya maneno Yake huelekezwa kwa udhaifu wa mwanadamu? Kwa sababu kwa mujibu wa kusudi la Mungu, kama Hangefichua mambo yaliyofichwa katika ulimwengu wa ndani wa moyo wa mwanadamu, basi hakuna mtu ambaye angetii, na kwa hivyo hangejielewa, na hangemcha Mungu. Hii ni kusema kwamba makusudi ya mwanadamu yasipofichuliwa, basi mwanadamu atathubutu kufanya chochote, labda hata kuelekeza laana kwa Mbingu au kwa Mungu. Huu ni udhaifu binadamu. Hivyo basi Mungu ananena hivi: “Nasafiri hadi katika pembe zote za ulimwengu katika hali ya kutafuta kwa kudumu wale wanaolingana na nia Yangu na wanaostahili kwa matumizi Yangu.” Kauli hii, ikiunganishwa na kile kinachosemwa baadaye kuhusu maamkizi ya ufalme yanayovuma kwa urasmi, inatumika kuonyesha kwamba Roho wa Mungu anajishughulisha na kazi mpya duniani; ni kwamba tu wanadamu hawawezi kuona kwa macho yao ya kimwili. Kwa vile inasemwa kwamba Roho yuko duniani Akifanya kazi mpya, ulimwengu wote pia hupitia mabadiliko ya maana sana: Wana wa Mungu na watu wa Mungu hawaanzi tu kukubali ushuhudiaji wa kupata mwili kwa Mungu, zaidi ya hayo, kila dini, kila dhehebu, kila tabaka, na kila mahali, kwa viwango mbalimbali, huukubali pia. Ni badiliko kubwa la ulimwengu katika ulimwengu wa kiroho. Huo hutetemesha ulimwengu wote wa dini kabisa, ambalo ni sehemu ya maana ya “zilizala” iliyotajwa zamani. Inayofuata, malaika wanaanza kazi yao rasmi na Waisraeli wanarudi katika nchi yao ya asili, wasiwahi kupotea tena, na wale wote waliojumuishwa huanza kukubali uchungaji. Kinyume, Wamisri wanaanza kujitoa kwa eneo la wokovu Wangu, yaani, kupokea kuadibu Kwangu (lakini hilo bado halianzi kwa urasmi). Kwa hiyo ni katika wakati huu wa mabadiliko haya makubwa ya kutokea wakati mmoja duniani ndio maamkizi ya ufalme yanavuma kwa urasmi, Hiki ndicho watu wameita, “wakati ambapo Roho aliyeongezwa nguvu mara saba Huanza kufanya kazi.” Kila wakati ambapo Mungu hufanya kazi ya kupata tena, katika awamu hizi (au katika nyakati hizi za mpito), hakuna anayeweza kuhisi kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa hivyo, maneno ya Mungu kwamba “Mwanadamu anapokata tamaa” huonekana kuwa kweli. Aidha, katika kila awamu hizi za mpito wakati ambapo wanadamu hukata tamaa, au wanapohisi mkondo huu si sahihi, Mungu huanza upya na huchukua hatua inayofuata ya kazi Yake. Tangu wakati wa uumbaji mpaka sasa, Mungu kufanya kazi ya kupata tena na kubadilisha mbinu ambazo Yeye hufanyia kazi kunafanana kwa njia hii. Ingawaje watu wengi zaidi, kwa viwango tofautitofauti, wanaweza kuelewa vipengele vyake vingine, mwishowe hata hivyo wao huondolewa kwa mbubujiko wa maji kwa sababu kimo chao ni kidogo sana; hawawezi kuelewa hatua za kazi ya Mungu na hivyo wao huondolewa. Hata hivyo, hii pia ni mbinu ya Mungu ya kuwatakasa watu, na hii ni hukumu ya Mungu kwa fikira za zamani za wanadamu. Kadri watu wanavyokuwa na msingi zaidi, ndivyo fikira zao za kidini kuhusu Mungu huwa kubwa zaidi, ambazo ni ngumu wao kuzipuuza; wao hushikilia mambo ya zamani na ni vigumu wao kukubali nuru mpya. Kwa upande mwingine, kama mtu anasimama, mtu lazima awe na msingi fulani, lakini watu wengi sana huwa na tatizo la kuweka kando fikira zao. Hii ni kweli hasa kwa fikira zao kuhusu Mungu mwenye mwili wa leo, ambalo ni wazi na rahisi kuona.

Katika tamko la siku hii, Mungu alizungumza mengi kuhusu maono, na hakuna haja ya kueleza kinaga ubaga. Mungu anazungumza kimsingi kuhusu jinsi ujenzi wa kanisa unaweka msingi wa ujenzi wa ufalme. Hasa, wakati kanisa lilikuwa likijengwa, lengo kuu lilikuwa kuwashawishi watu moyoni na kwa neno, ingawa hawajamjua Mungu mwenye mwili kwa macho yao wenyewe. Ingawaje walikuwa na imani ndani ya mioyo yao, hawakumjua Mungu mwenye mwili kwa sababu katika hatua hiyo Hangetofautishika na mtu. Katika Enzi ya Ufalme, wote lazima waonyeshe kusadiki sana ndani ya mioyo yao, kunena kwao, na macho yao. Kutoka hapa, ni wazi kwamba ili wote waonyeshe kusadiki sana ndani ya mioyo yao, kunena kwao, na macho yao, lazima waruhusiwe kumjua Mungu aishiye katika mwili kwa macho yao ya mwili. Hili haliwezi kufanikishwa katika hali ambayo watu wanalazimishwa kufanya jambo kwa sababu hawana hiari nyingine au ambayo watu wana imani isiyo ya kudumu. Badala yake, watu wataridhishwa moyoni na kwa neno kupitia ufahamu. Kwa hivyo, katika hatua hii ya ujenzi hakuna kupiga au kuua. Badala yake, inawaruhusu watu kupata nuru kupitia neno la Mungu, na kupitia hili waweze kufuatilia na kuchunguza ili kwa kufichika akilini watakuja kumjua Mungu mwenye mwili. Kwa hiyo kumhusu Mungu, hatua hii ya kazi ni rahisi zaidi, huacha maisha yaendelee katika hali yake ya asili na haiendi kinyume na wanadamu. Hiyo, mwishowe, itamruhusu mwanadamu kuja kumjua Mungu kwa kawaida, kwa hiyo usiwe mwenye wahaka au kuwa na wasiwasi. Mungu aliposema, “vita vya ulimwengu wa kiroho vimewekwa wazi miongoni mwa watu Wangu wote,” Alimaanisha kwamba watu wanapoingia katika njia sahihi na kuanza kumjua Mungu, sio pamoja tu na kila mtu kujaribiwa ndani na Shetani, bali pia waweze kujaribiwa na Shetani ndani ya kanisa lenyewe. Hata hivyo, hii ndiyo njia ambayo kila mtu anafaa kuifuata, kwa hivyo mtu yeyote asishtuke. Majaribu ya Shetani yanaweza kuja kwa aina kadhaa. Mtu anaweza kudharau au kutelekeza asemacho Mungu, na anaweza kusema mambo hasi ili kufifiza matumaini wa watu wengine, hata hivyo, yeye kwa kawaida hawashawishi watu wengine wajiunge ndani; mambo haya ni magumu kwa watu kutambua. Sababu kuu ya hili ni: Huenda bado akawa mtendaji katika kuhudhuria mikutano, lakini haelewi kuhusu maono. Kama kanisa halihadhari naye, basi kanisa lote lingeweza kushawishiwa na uhasi wake katika kumwitikia Mungu kwa uvuguvugu, hivyo kutozingatia neno la Mungu na hii ingekuwa kuanguka ndani kabisa ya majaribu ya shetani. Huenda asimuasi Mungu moja kwa moja, lakini kwa vile hawezi kuelewa neno la Mungu na hamjui Mungu, huenda akalalamika au kuwa na chuki ndani ya moyo wake. Huenda akasema kwamba Mungu amemtelekeza kwa hiyo hawezi kupata nuru na mwangaza. Huenda akataka kuondoka, lakini hisia tulivu ya woga hukaa ndani yake na huenda akasema kwamba kazi ya Mungu haitoki kwa Mungu lakini badala yake ni kazi ya pepo waovu.

Mbona Mungu humtaja Petro mara kwa mara sana? Na mbona Asema kwamba hata Ayubu hakukaribia kuwa sawa na yeye. Kusema hili hakusababishi tu kutilia maanani matendo ya Petro, bali pia inawalazimu kuweka kando mifano yote waliyonayo ndani ya mioyo yao, na hata mfano wa Ayubu—aliyekuwa na imani kuu zaidi—unapaswa kuwekwa kando pia. Ni kupitia hili tu ndio kunaweza kuwa na matokeo bora ambapo watu wanaweza kuachana na kila kitu ili kumwiga Petro, na hivyo kusonga hatua moja karibu zaidi katika kumjua Mungu. Mungu aliwaleta watu kwa njia ya utendaji ambayo Petro alifuata kumjua Mungu, ambalo lengo lake lilikuwa ni kuwapa watu jambo la rejelea. Kisha Mungu anaendelea kutabiri mojawapo ya njia ambazo Shetani atawajaribu watu Anaposema, “Lakini kama wewe huna hisia na hujali kuhusu maneno Yangu, basi bila shaka unanipinga Mimi. Hii ni kweli.” Ndani ya maneno haya, Mungu anatabiri hila za ujanja ambazo Shetani atajaribu kutumia na Anawatahadharisha watu kulizingatia kuwa onyo. Hata kama sio kila mtu atadharau neno la Mungu, hata hivyo watu wengine watatekwa na majaribu haya, kwa hiyo mwishowe Mungu asema tena kwa msisitizo, “Iwapo hamyajui maneno Yangu, hamyakubali, na wala hamyaweki katika matendo, basi bila shaka mtakuwa chombo cha kuadibu Kwangu! Nyinyi kwa hakika mtakuwa waathirika wa Shetani!” Huu ni ushauri wa Mungu kwa wanadamu, lakini mwishowe, kama alivyotabiri Mungu, sehemu ya watu watakuwa waathiriwa wa Shetani.

Iliyotangulia: Kuhusu Maisha ya Petro

Inayofuata: Sura ya 9

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp