Sura ya 28

Unaona kwamba muda ni mfupi sana na kazi ya Roho Mtakatifu inavurumisha mbele, ikikusababisha kupata baraka kubwa hivi, kumpokea Mfalme wa ulimwengu, Mwenyezi Mungu, ambaye ni Jua ling’aalo, Mfalme wa ufalme—hii yote ni neema na huruma Yangu. Kuna nini kinachoweza kuwepo kinachoweza kukutoa kwa upendo Wangu? Tafakari kwa makini, usijaribu kuepa, subiri kwa ustahamilivu mbele Yangu kila wakati na usiwe ukizurura nje daima. Moyo wako lazima ukae karibu na moyo Wangu, na bila kujali kile kinachoweza kukufikia usifanye vitu bila kufikiri au kiholela. Lazima utazame mapenzi Yangu, ufanye chochote Ninachokitaka na kudhamiria kuacha kile ambacho Sikitaki. Ni lazima usitende hisia zako, ila badala yake utende haki kama Mimi; haikubaliki kuwa na hisi za moyoni hata kwa mama na baba yako. Ni lazima uache yote yasiyokubaliana na ukweli na lazima ujitolee na kujitumia kwa ajili Yangu kwa moyo safi unaonipenda Mimi. Usikubali udhibiti wa mtu yeyote, jambo au kitu; alimuradi linapatana na mapenzi Yangu basi lifanye kwa mujibu wa maneno Yangu. Usiogope, kwa kuwa mikono Yangu hukusaidia, na kwa hakika Nitakukinga dhidi ya watu wote wabaya. Unapaswa kuulinda moyo wako, kuwa ndani Yangu nyakati zote, kwa kuwa maisha yako yanaishiwa kwa kutegemea maisha Yangu; ukiniacha basi utanyauka mara moja.

Unapaswa kujua kwamba ni siku za mwisho sasa. Shetani ibilisi, kama simba ambaye ananguruma, anatembea huku na kule, akitafuta watu wa kuwameza. Kila aina ya mapigo yanatokea sasa na kuna aina nyingi tofauti za roho wabaya. Mimi pekee ndiye Mungu wa kweli; Mimi pekee ndiye kimbilio lako. Unaweza tu kujificha sasa katika mahali Pangu pa siri, ndani Yangu tu, na maafa hayatakufika na hakuna janga litakalokuja karibu na hema lako. Ni lazima unikaribie zaidi, ushiriki na Mimi katika mahali pa siri; usishiriki kiholela na watu wengine. Ni lazima uelewe maana katika maneno Yangu—Sisemi kwamba huruhusiwi kushiriki, ni kwamba tu bado sasa huna utambuzi. Katika kipindi hiki, kazi inayofanywa na roho wabaya inaenea kwa haraka. Wanakupa ushirika kupitia kila aina ya watu. Maneno yao yanasikika kuwa mazuri sana, lakini kuna sumu ndani yayo. Ni risasi za kuvutia na kabla ujue yataweka sumu yayo ndani yako. Unapaswa kujua kwamba watu wengi leo si thabiti, kana kwamba wamelewa. Unapokuwa na ugumu na ushiriki na wengine, wanachokuambia ni amri na mafundisho tu, na si kizuri kama kushiriki moja kwa moja na Mimi. Kuja mbele Yangu na umwage kabisa mambo mazee yaliyo ndani yako, fungua moyo wako Kwangu na moyo Wangu hakika utafichuliwa kwako. Moyo wako lazima uwe mwangalifu mbele Yangu. Usiwe mzembe, ila badala yake lazima unikaribie mara kwa mara; hii ni njia ya haraka kabisa ya maisha yako kukua. Ni lazima uishi ndani Yangu na Nitaishi ndani yako na pia Nitatawala kama Mfalme ndani yako, Nikikuongoza katika vitu vyote, na utakuwa na mgao wa ufalme.

Usijidunishe kwa sababu wewe ni mdogo; unapaswa kujitoa Kwangu. Sioni watu wako vipi juu juu au ni wa umri upi. Naona tu iwapo wananipenda kwa kweli au la, na iwapo wanafuata njia Yangu na kutenda ukweli wakipuuza mambo mengine yote. Usijali kuhusu jinsi kesho itakuwa au jinsi siku za baadaye zitakuwa. Alimradi unitegemee kuishi kila siku, basi hakika Nitakuongoza. Usikae kwa fikira kwamba “Maisha yangu ni machanga sana, sielewi chochote,” ambayo ni fikira iliyotumwa na Shetani. Tumia tu moyo wako kunikaribia daima na ufuate nyayo Zangu hadi mwisho wa njia. Unapoyasikia maneno Yangu ya lawama na onyo na kuzinduka, lazima ukimbie mbele mara moja; usiache kunikaribia, kuwa kasi sawa na nyayo za wanakondoo na endelea kuangalia mbele. Mbele Yangu, ni lazima umpende Mungu wako kwa moyo na nafsi yako yote. Jaribu kuyaelewa maneno yangu zaidi katika njia ya kuhudumu. Katika kutenda ukweli lazima usiwe mwenye moyo dhaifu, ila uwe na moyo wenye nguvu, uwe na azimio na ujasiri wa mtoto wa kiume, na kuwa na moyo mgumu. Ikiwa unataka kunipenda, basi lazima uniridhishe na mambo yote Ninayotaka kutimiza ndani yako. Ikiwa unataka kunifuata, basi lazima utelekeze vyote ulivyo navyo, vyote uvipendavyo, utii kwa unyenyekevu mbele Yangu, kuwa na akili ya kawaida na usijishughulishe kutafiti au kufikiria vitu bila mpango maalum; lazima uwe kasi sawa na kazi ya Roho Mtakatifu daima.

Hapa Nakupa ushauri: Ni lazima ushikilie kwa uthabiti na kutenda yote ambayo Nimetia nuru ndani yako!

Iliyotangulia: Sura ya 27

Inayofuata: Sura ya 29

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp