Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, bila shaka, Nimetamka mengi pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho kikamilifu. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani, bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. Kwa hivyo, Ninasonga mbele katika mpango Wangu mpya, katika kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya katika kazi Yangu ili wale ambao wanaoniona watajipiga kifuani na kuulilia na kuombolezea uwepo Wangu bila kukoma. Kwani Ninaleta mwisho wa wanadamu duniani, na baada ya hapo kuendelea, Ninaweka wazi tabia Yangu yote mbele ya wanadamu, ili wote wanijuao na wasionijua watayashibisha macho yao na kuona kwamba kweli, nimekuja ulimwenguni, nimekuja duniani ambapo vitu vyote vinazidi kuongezeka. Huu ni mpango Wangu, ni “kukiri” Kwangu kwa pekee tangu Niwaumbe wanadamu. Matilaba yangu ni kuona mnafuatilia kwa moyo wenu wote kila Ninachokifanya, maana kiboko Changu kinamkaribia wanadamu tena, karibu na wale wote wanaonipinga.

Pamoja na mbingu, Ninaanza kazi ambayo ni lazima Niifanye. Kwa hivyo Mimi husafiri kati ya misururu ya watu na kupita kati ya mbingu na ardhi, bila ya yeyote kutambua mienendo Yangu au kuyatambua maneno Yangu. Kwa hivyo, mpango Wangu bado unaendelea kwa urahisi. Ni vile tu hisia zenu zote zimekuwa nzito kiasi kwamba hamjui hatua za kazi Yangu hata kidogo. Hata hivyo, siku moja hakika mtakuja kutambua kusudio Langu. Leo hii, Ninaishi miongoni mwenu na Ninasumbuka pamoja nanyi. Kwa muda mrefu Nimeelewa mtazamo walio nao wanadamu juu Yangu. Nisingependa kueleza wazi zaidi, sembuse kutoa mifano zaidi ya kile kinachoniumiza ili kuwaaibisha. Ombi Langu la pekee ni kwamba myaweke moyoni yale yote mliyoyafanya kwa ajili ya kulinganisha maelezo yetu siku tutakapokutana tena. Nisingependa kumshutumu yeyote miongoni mwenu kwa njia isiyo ya kweli, kwa sababu daima Nimekuwa Nikifanya mambo kwa njia ya haki, bila upendeleo, na kwa heshima. Bila shaka, Ningependa pia kwamba nyinyi mngeweza kuwa wazi na wakarimu na kutofanya lolote lililo kinyume na mbingu na ardhi na dhamiri yenu. Haya pekee ndiyo Ninayowauliza. Watu wengi huhisi kusumbuka na hawana amani kwa sababu wametenda makosa mabaya, na wengi wanaona aibu kwa sababu hawajawahi kutenda tendo lolote zuri. Tena wapo pia wengi ambao, mbali na kutahayari kutokana na dhambi zao, wanakuwa wabaya zaidi, wakizitoa kabisa barakoa inayoficha sura zao mbaya—ambayo ilikuwa bado haijaonyeshwa kikamilifu—ili kujaribu tabia Yangu. Huwa Sijali wala sitilii maanani sana matendo ya mtu yeyote. Badala yake, Mimi hufanya kazi Ninayopaswa kufanya, iwe kukusanya habari, kuzungukazunguka katika nchi au kufanya lile ambalo linanipendeza. Katika nyakati muhimu, Mimi nitaendelea na kazi Yangu miongoni mwa wanadamu kama Nilivyopanga awali, bila kuchelewa au kuwa mapema hata kidogo, na kwa urahisi na kwa makini. Hata hivyo, kuna watu wengine ambao wanawekwa pembeni kwa kila hatua katika kazi Yangu, kwa sababu Ninadharau hali yao ya kujipendekeza na hali ya kujifanya wanyenyekevu. Wale wanaochukiza Kwangu hakika watatelekezwa, iwe ni kwa kupenda au kwa kutopenda. Kwa ufupi, Ninataka wale wote Ninaowadharau kuwa mbali sana Nami. Ni dhahiri kwamba, Sitawahurumia wale waovu ambao wamebaki katika makao Yangu. Kwa kuwa siku ya adhabu ya mwanadamu inakaribia, Sina haraka ya kuzitupa nje zile nyoyo zote zinazostahili dharau, kwa kuwa Nina mpango Wangu Mwenyewe.

Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, wala si hatua ambapo nilianza kumfinyanga mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo yote ya kila mtu katika kitabu Changu, moja baada ya nyingine, na vilevile njia zao katika kunifuata, sifa zao asilia, na utendakazi wao wa mwisho. Kwa njia hii, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu na kila mmoja atakuwa wa aina yake kama Nilivyowaweka. Ninaamua hatima ya kila mwanadamu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anavuta huruma, bali ni kwa kuangalia kama ana ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili tu. Ni sharti mjue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa. Huu ndio ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu. Sijafanya mabadiliko yoyote katika mpango Wangu tangu kuuanzisha. Ni vile tu, kwa binadamu, wale ambao kwao Mimi huelekeza maneno Yangu wanaonekana kupungua kwa idadi, na vile vile wale Ninaowakubali kwa kweli. Hata hivyo, Ninasisitiza kwamba mpango Wangu haujawahi kubadilika; badala yake, ni imani na upendo wa mwanadamu ambao hubadilika daima, kufifia daima, kiasi kwamba upo uwezekano wa kila mwanadamu kubadilika kutoka kujipendekeza Kwangu hadi kufikia hali ya kunidharau au hata kunitupa nje. Mtazamo Wangu kwenu hautakuwa baridi wala moto, hadi pale Nitakapohisi kuchukizwa na kuchafuliwa moyo, na hatimaye kutoa adhabu. Hata hivyo, katika siku ya adhabu yenu, bado Nitawaona lakini nyinyi hamtaweza kuniona tena. Tayari Kwa kuwa maisha miongoni mwenu yamekuwa ya kuchosha na ya taabu tayari Kwangu, kwa hivyo ni wazi kuwa, Nimechagua mazingira tofauti Yangu kuishi, ili Niepuke vizuri kuumizwa na maneno yenu mabovu na kuwa mbali na tabia zenu hafifu sana, ili msinipumbaze au kunitendea kwa namna ya uzembe. Kabla Sijawaacha, lazima bado Ninawasihi mjiepushe kufanya yale ambayo hayaambatani na ukweli. Badala yake, mnafaa kufanya yale ambayo yanawapendeza watu wote, na yale ambayo yana manufaa kwa binadamu wote, na yale yanayofaidi hatima yenu wenyewe, la sivyo, yule atakayeteseka katika maafa hatakuwa mwingine ila wewe.

Huruma Zangu zinaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wote wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, wakijipata katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra katika mamilioni ya miaka, wataishi katika hali ya kila siku ya taharuki na woga. Na wale wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu pekee watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya wanadamu na kuchukia matendo yao maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha wanadamu ambao wanafikiria kama Mimi. Sijawahi kuwasahau wale ambao hawana fikira sawa na Zangu; Nimewachukia sana moyoni Mwangu, Nikisubiri tu nafasi kutoa adhabu kwa hao na kufurahia kuona hilo. Siku Yangu hatimaye imefika na siwezi kusubiri zaidi!

Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi. tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema. Ingawa wanaoweza kunilipa ni wachache, bado Nitahitimisha safari Yangu duniani na Nianze hatua ifuatayo ya kazi Yangu inayotokea, kwa sababu kukimbia kimbia Kwangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuchukuliwa kama vinavyofaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na mlijionyesha tu kuwa wenye woga au sugu. Kuhusu hili, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya tu. Shaka Yangu inaendelea kuwa jinsi kila mmoja wenu hutenda na kujionyesha, kwa msingi ambao Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba: Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

Iliyotangulia: Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Inayofuata: Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Sura ya 6

Kwa masuala ya ndani ya roho, unapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, unapaswa kuwa msikivu kwa makini. Unapaswa kulenga...

Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Kila siku mnayoiishi sasa ni ya maana sana na muhimu sana kwa hatima yenu na majaliwa yenu, kwa hivyo mnapaswa kufurahia kila mlicho nacho...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki