Sura ya 12

Ikiwa una tabia ambayo si thabiti, nyepesi kuhamaki kama upepo au mvua, kama huwezi kuendelea kusonga mbele, basi fimbo Yangu haitakuwa mbali na wewe. Unaposhughulikiwa, kadiri hali ilivyo mbaya zaidi, na kadiri unavyoteswa zaidi, ndivyo upendo wako kwa Mungu unavyoongezeka, na unaacha kushikilia dunia. Bila njia nyingine, unakuja Kwangu, na unapata tena nguvu na imani yako. Ilhali, katika hali rahisi, ungeboronga. Ni lazima uingie ndani kwa mtazamo chanya, uwe mwenye vitendo na si baridi. Hutatingisika na yeyote na chochote katika hali yoyote, na huwezi kushawishiwa na maneno ya yeyote. Ni lazima uwe na tabia thabiti, na bila kujali kile watu wanachoweza kusema, utatenda kile unachojua kuwa ukweli mara moja. Lazima daima uwe na maneno Yangu yakifanya kazi ndani yako, bila kujali ni nani unayemkabili; lazima uweze kusimama imara katika ushuhuda wako Kwangu na ufikirie mizigo Yangu. Hupaswi kuchanganyikiwa, ukikubaliana na watu bila kufikiri na bila kuwa na mawazo yako mwenyewe, ila badala yake lazima uwe na ujasiri wa kusimama na kupinga vitu visivyotoka Kwangu. Ukijua kwa dhahiri kwamba jambo si sahihi, ilhali unyamaze, basi wewe si mtu anayetenda ukweli. Ukijua kwamba jambo si sahihi na kisha ugeuze mada, lakini Shetani azuie njia yako—unazungumza bila athari yoyote na huwezi kuvumilia hadi mwisho—basi bado unabeba woga moyoni mwako, na moyo wako bado haujazwi na fikira kutoka kwa Shetani?

Mshindi ni nini? Wanajeshi wazuri wa Kristo lazima wawe jasiri na kunitegemea kuwa wenye nguvu kiroho; lazima wapigane kuwa wapiganaji na wapambane na Shetani hadi kufa. Lazima daima ukae macho, na hii ndiyo maana Nakuomba ushirikiane kwa vitendo na Mimi kila wakati na kujifunza kuja karibu nami. Ikiwa katika wakati wowote na katika hali yoyote, unaweza kubaki kimya mbele Yangu, ukisikiza usemi Wangu na kuzingatia maneno Yangu na matendo, basi hutashawishiwa na kupoteza msimamo wako. Chochote unachopata kutoka ndani Yangu kinaweza kutendwa. Kila neno Langu linaelekezwa kwa hali yako. Yanachoma moyo wako, na hata ukiyakana na kinywa chako, huwezi kuyakana na moyo wako, na ukichunguza maneno Yangu, utahukumiwa. Kwa maneno mengine, maneno Yangu ni ukweli, uhai, njia; hayo ni upanga mkali, ukatao kuwili na yanaweza kumshinda Shetani. Wale wanaoelewa na wana njia ya kutenda maneno Yangu wamebarikiwa, na wale wasioyatenda watahukumiwa pasipo shaka; hili ni jambo la busara sana. Sasa, kadiri ya wale Ninaowahukumu imepanuka. Sitahukumu tu mbele Yangu wale wanaonijua, ila wale wasioniamini na wanaojaribu kadiri wawezavyo kupinga na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu pia watahukumiwa. Wale wote wanaofuata nyayo Zangu mbele Yangu wataona kwamba Mungu ni moto mkali sana! Mungu ni uadhama! Anafanya hukumu Yake, na kuwahukumu kifo. Wale walio kanisani wasiozingatia kufuata kazi ya Roho Mtakatifu, wanaoingilia kazi ya Roho Mtakatifu, wanaojionyesha, walio na nia na malengo yasiyo sahihi, wasioweka jitihada yao katika kula na kunywa maneno ya Mungu, waliokanganyikiwa na wenye shaka, wanaochunguza kazi ya Roho Mtakatifu—maneno ya hukumu yatawajia wakati wowote. Matendo yote ya watu yatafichuliwa. Roho Mtakatifu huchunguza vina vya mioyo ya watu, hivyo usiwe asiyejali; kuwa mwangalifu na utahadhari, usitende bila kufikiri wewe binafsi. Ikiwa matendo yako hayafuati maneno Yangu, basi utahukumiwa. Hakuna haja ya kuiga, ya kuwa mwenye kujifanya, au ya kutoelewa kweli; lazima uje mbele Yangu na kuwasiliana kwa karibu na Mimi mara nyingi.

Chochote utakachochukua kutoka ndani Yangu, kitakupa njia ya kutenda, na utaandamana na nguvu Zangu, utakuwa na uwepo Wangu, na daima utembee katika maneno Yangu, utazidi kila kitu duniani, na kuwa na nguvu ya ufufuo. Ikiwa maneno yako, tabia yako na matendo yako hayana maneno Yangu na uwepo Wangu, ukijitenga kutoka Kwangu na kuishi ndani yako, uishi katika dhana za akili, uishi katika mafundisho na amri, basi hiyo ni ithibati kwamba umeweka akili yako kwa dhambi. Kwa maneno mengine, unaendelea kushikilia nafsi yako nzee na huachi wengine wadhuru nafsi yako kidogo au kuharibu nafsi yako; mtu kama huyu ana ubora duni sana wa tabia na ni mpuuzi sana, na hawezi kuona neema ya Mungu au kutambua baraka za Mungu. Utaweza kuacha Nifanye kazi ndani yako lini ukiendelea kunikwepa! Wakati Nimemaliza kuzungumza, unasikiza lakini hukumbuki, na unakuwa mnyonge hasa shida zako zinapoonyeshwa kweli; hiki ni kimo cha aina gani! Ninaweza kukufanya uwe kamili lini ikiwa daima unahitaji kubembelezwa! Ikiwa unaogopa uvimbe na mikwaruzo, basi unapaswa kuharakisha kuwaonya wengine, “Sitamwacha yeyote anishughulikie, ninaweza kuondoa tabia yangu ya asili na nzee mimi mwenyewe.” Hivyo hakuna mtu atakukosoa au kukugusa, na uko huru kuamini njia yoyote unayotaka bila mtu yeyote kukujali. Je, unaweza kufuata nyayo Zangu hivi? Ni maneno matupu kusema kwamba una hakika kwamba mimi ni Mungu wako na Bwana wako. Ikiwa kweli huna shaka, mambo haya hayatakuwa shida, na utaamini kwamba ni upendo wa Mungu na baraka za Mungu juu yako. Ninapozungumza, ni kwa wana Wangu, na inapaswa kukabiliwa na shukrani na sifa.

Iliyotangulia: Sura ya 11

Inayofuata: Sura ya 13

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp