Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ndiko Kuwa na Uhalisi
Kuwa na uwezo wa kuyaeleza maneno ya Mungu kwa uwazi haimaanishi kwamba wewe unaumiliki uhalisi—mambo si rahisi kama ulivyoweza kufikiria. Ikiwa unaumiliki uhalisi au la haina msingi kwa kile unachokisema, badala yake, inatokana na kile unachoishi kwa kudhihirisha. Wakati maneno ya Mungu yanakuwa maisha yako na kujionyesha kwako kwa asili, hili tu ndilo linalochukuliwa kama uhalisi, na hili tu ndilo linachukuliwa kama wewe kumiliki uelewa na kimo cha kweli. Lazima uwe na uwezo wa kuhimili uchunguzi kwa muda mrefu, na lazima uwe na uwezo wa kuishi kwa kuidhihirisha sura ambayo inahitajika kwako na Mungu; isiwe mkao tu, lakini ni lazima ibubujike kwa kawaida kutoka ndani mwako. Hapo tu ndipo basi utakapokuwa na uhalisi kikweli, na ndipo tu basi utakapopata maisha. Wacha Nitumie mfano wa jaribio la watendaji huduma ambao kila mtu ana uzoefu nao. Mtu yeyote anaweza kuzungumzia nadharia zenye fahari sana kuhusu watendaji huduma, na kila mtu ana ufahamu unaofaa wa mada hii; wanazungumza juu yake na kila usemi unazidi ule wa awali, kana kwamba kuna mashindano. Hata hivyo, kama mwanadamu hajapitia jaribio kubwa, ni vigumu kusema ana ushahidi mzuri. Kwa ufupi, kuishi kwa kudhihirisha kwa mwanadamu bado kuna upungufu mwingi, na hii inatofautiana na uelewa wake. Kwa hiyo, bado hakijakuwa kimo halisi cha mwanadamu, na bado hayajakuwa maisha ya mwanadamu. Kwa sababu uelewa wa mwanadamu haujaletwa katika uhalisi, kimo chake bado ni kama ngome iliyojengwa kwenye mchanga, ikiyumbayumba na ikiwa karibu kuanguka. Mwanadamu anao uhalisi kidogo mno—ni vigumu kuupata uhalisi wowote katika mwanadamu. Kunao uhalisi kidogo mno unaobubujika kwa asili kutoka kwa mwanadamu na uhalisi wote katika maisha yake umelazimishwa, ndiyo maana nasema kwamba mwanadamu hamiliki uhalisi wowote. Usiweke hisa nyingi sana katika wanadamu wakisema kwamba upendo wao wa Mungu haubadiliki kamwe—hiki tu ndicho kile wao husema kabla ya kukabiliwa na majaribu. Mara tu wanapokabiliwa na majaribu kwa ghafla, mambo ambayo wao hunena kwa mara nyingine tena hayalingani na uhalisi, na kwa mara nyingine yatathibitisha kwamba wanadamu hawana uhalisi. Inaweza kusemwa kwamba wakati wowote unapokumbana na mambo ambayo hayalingani na dhana zako nayo yanakuhitaji kujiweka kando, haya ni majaribu yako. Kabla mapenzi ya Mungu kufichuliwa, kuna mtihani mkali kwa kila mwanadamu, jaribio kubwa kwa kila mtu—je, waweza kuliona wazi jambo hili? Wakati Mungu anapotaka kuwajaribu wanadamu, Yeye daima huwaacha kufanya maamuzi yao kabla ya ukweli wa uhalisi kufichuliwa. Yaani wakati Mungu anamweka mwanadamu katika majaribu, kamwe Yeye hatakwambia ukweli, na hivyo ndivyo wanadamu wanaweza kufichuliwa. Hii ni njia mojawapo ambayo Mungu huifanya kazi yake, ili kuona kama unamwelewa Mungu wa leo, na ili kuona kama unaumiliki uhalisi wowote. Je, kweli wewe huna shaka yoyote kuhusu kazi ya Mungu? Je, utaweza kusimama imara wakati jaribio kuu linakujia? Ni nani anayethubutu kusema maneno kama vile “Nahakikisha hakutakuwa na matatizo”? Nani anayethubutu kusema maneno kama vile “Wengine wanaweza kuwa na mashaka, lakini Mimi sitakuwa na shaka kamwe”? Kama vile nyakati Petro alipitia majaribu—alikuwa siku zote akizungumza maneno makubwa kabla ukweli haujafichuliwa. Huu sio udhaifu wa kibinafsi wa kipekee kwa Petro; hii ni shida kubwa zaidi inayomkabili kila mwanadamu sasa. Kama ningetembelea maeneo kadhaa, au kama ningewatembelea ndugu na dada kadhaa, kuuangalia uelewa wenu wa kazi ya Mungu ya leo, hakika mngeweza kweli kuzungumza kuhusu mengi ya uelewa wenu, nayo ingeonekana kwamba ninyi hamna mashaka yoyote. Kama ningewauliza: “Je, kweli waweza kutabainisha kwamba kazi ya leo inatekelezwa na Mungu Mwenyewe? Bila shaka yoyote”? ungejibu bila shaka: “Bila shaka yoyote, ni kazi inayotekelezwa na Roho wa Mungu.” Mara tu unapojibu kwa namna hiyo, kwa hakika usingekuwa hata na chembe cha shaka na unaweza hata kuhisi starehe kubwa—unaweza kuhisi kuwa umepata uhalisi kiasi kidogo. Wale ambao mara nyingi huelewa mambo kwa njia hii ni wale ambao wanamiliki uhalisi kidogo zaidi; kadri mtu anavyodhani kwamba amelipata, ndivyo atakavyokosa uwezo wa kusimama imara katika majaribio. Ole wao walio na kiburi na wenye maringo, na ole wao wasio na maarifa ya wao wenyewe. Watu kama hawa ni hodari katika kuzungumza ilhali huendelea vibaya zaidi katika matendo yao. Wakati kuna dalili ndogo zaidi ya matatizo, watu hawa wataanza kuwa na mashaka na mawazo ya kukata tamaa huingia akilini mwao. Hawana umiliki wa uhalisi wowote; yote waliyo nayo ni nadharia zenye fahari zaidi kuliko zile za dini, bila ya hali halisi ambazo Mungu anadai sasa. Nachukizwa zaidi na wale wanaosema kuhusu nadharia tu nao hawana uhalisi. Wao kufanya kilio kikubwa zaidi wanapoitenda kazi yao, lakini wao husambaratika punde tu wanapokabiliwa na uhalisi. Je, si inaonyesha kwamba watu hawa hawana uhalisi? Haijalishi jinsi upepo na mawimbi yalivyo kali, kama unaweza kubaki umesimama bila hata dalili ya shaka kuingia mawazoni mwako, na unaweza kusimama imara na usiwe kati hali ya kukana hata kama hakuna mtu mwingine aliyebaki, basi hili linachukuliwa kama wewe kuwa na uelewa wa kweli na wewe kuwa na umiliki wa uhalisi. Ukifuata njia yoyote ambayo upepo unavuma, ukiwafuata walio wengi na kujifunza kusema yale ambayo wengine wanasema, haijalishi jinsi gani unavyosema mambo hayo vizuri, sio thibitisho kwamba unao umiliki wa uhalisi. Kwa hiyo, napendekeza kwamba usiwe na haraka ya kupiga kelele kwa maneno matupu. Je, unaijua kazi ambayo Mungu ataitekeleza? Usitende kama Petro mwingine usije ukajiletea aibu na usiweze tena kutembea bila haya—hii haimfaidi mtu yeyote. Wanadamu wengi hawana kimo cha kweli. Mungu ametekeleza kazi kubwa sana lakini hajafanya uhalisi kuwajia watu; kwa kuwa sahihi zaidi, Mungu hajawahi kumwadibu yeyote binafsi. Baadhi ya watu wamefichuliwa na majaribio kama haya, na minyiri yao ya dhambi ikitambaa nje zaidi na zaidi, wakifikiri kwamba ni rahisi kumhadaa Mungu, wanaweza kumchukulia Mungu kwa kutojali, na kufanya chochote wanachotaka. Kwa kuwa hawawezi hata kustahimili majaribu ya aina hii, kadri majaribio yenye changamoto yasivyowezekana, na uhalisi pia hauwezekani. Je, si hii ni kujaribu kumpumbaza Mungu? Kuwa na uhalisi si kitu ambacho kinaweza kubuniwa, na wala si kitu ambacho unaweza kukipata kutokana na maarifa yako kukihusu. Unalingana na kimo chako cha ukweli, na unalingana na kama unao uwezo wa kuhimili majaribu yote. Je, unaelewa sasa?
Masharti ya Mungu kwa wanadamu siyo tu kuweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Je, si hiyo itakuwa rahisi sana? Kwa nini basi Mungu anazungumza kuhusu kuingia katika maisha? Kwa nini Anaongea kuhusu mabadiliko? Kama mtu ana uwezo wa mazungumzo matupu tu kuhusu uhalisi, mabadiliko katika tabia yangeweza kupatikana? Kulifunza kundi la wanajeshi wazuri wa ufalme sio sawa na kuwafunza wanadamu ambao wanaweza tu kuongea kuhusu uhalisi au watu ambao hujigamba tu, bali ni kuwafunza wanadamu ambao wanajivunia tu, lakini wanadamu ambao wanaweza kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu wakati wote, ambao ni wagumu bila kujali vikwazo wanavyokumbana navyo, na wanaoishi kwa mujibu wa maneno ya Mungu wakati wote, na hawarudi kwa ulimwengu. Huu ndio uhalisi ambao Mungu anauzungumzia, nayo ni matakwa ya Mungu kwa binadamu. Kwa hiyo, usiuone uhalisi ulionenwa na Mungu kama rahisi sana. Kupata nuru tu kwa Roho Mtakatifu sio sawa na kuumiliki uhalisi: Hiki sicho kimo cha wanadamu, lakini neema ya Mungu, nayo haihusishi mafanikio yoyote ya wanadamu. Kila mwanadamu ni lazima ayavumilie mateso ya Petro, na hata zaidi aumiliki utukufu wa Petro, ambao ndio watu huishi kwa kudhihirisha baada ya kupata kazi ya Mungu. Hii tu ndiyo inaweza kuitwa uhalisi. Usidhani kwamba utamiliki uhalisi kwa sababu unaweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Huu ni uongo, huu haulingani na mapenzi ya Mungu, na hauna maana halisi. Usiseme mambo kama haya katika siku zijazo—komesha misemo kama hii! Wale wote walio na uelewa wa uongo wa maneno ya Mungu ni makafiri. Hawana maarifa yoyote halisi, sembuse kimo chochote halisi; wao ni watu wenye kujigamba bila ya uhalisi. Hiyo ni, wale wote wanaoishi nje ya dutu ya maneno ya Mungu ni makafiri. Wale wanaoonekana kuwa makafiri na wanadamu ni wanyama mbele za Mungu, na wale wanaoonekana kuwa makafiri na Mungu ni wale ambao hawana maneno ya Mungu kama maisha yao. Kwa hiyo, wale ambao hawana uhalisi wa maneno ya Mungu nao wanashindwa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ni makafiri. Nia ya Mungu ni kufanya iwe kwamba kila mmoja anaishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu. Sio tu kwamba kila mtu anaweza kuzungumza kuhusu uhalisi, lakini muhimu zaidi, kwamba kila mmoja anaweza kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu. Uhalisi ambao mwanadamu anautambua ni wa juu juu sana, hauna thamani, hauwezi kutimiza mapenzi ya Mungu, ni duni sana, hata haustahili kutajwa, una upungufu sana, na uko mbali sana na kiwango cha mahitaji ya Mungu. Kila mmoja wenu atapitia ukaguzi mkuu ili kuona ni nani kati yenu anayejua tu kuzungumza kuhusu uelewa wake lakini hawezi kuonyesha njia, na kuona ni nani kati yenu ni taka bure. Kumbuka hili katika siku zijazo! Usizungumze kuhusu uelewa mtupu—zungumza tu kuhusu njia ya utendaji, na kuhusu uhalisi. Geuka kutoka maarifa halisi hadi kwenye vitendo halisi, na kisha geuka kutoka kutenda hadi kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. Usiwahutubie wengine, na usizungumze kuhusu maarifa ya ukweli. Kama uelewa wako ni njia, basi unaweza kuuachilia; kama si njia, basi tafadhali nyamaza, na uache kuongea. Kile unachosema ni bure. Ni baadhi tu ya maneno ya uelewa ya kumpumbaza Mungu na kuwafanya wengine wakuonee wivu. Si hilo ni lengo lako? Je, hii si kuwachezea wengine kimakusudi? Je, kunayo thamani yoyote katika hili? Zungumza tu kuhusu uelewa baada ya kuwa na uzoefu kuuhusu, na kisha hutakuwa unajisifu tena. La sivyo wewe ni mtu tu ambaye anasema maneno yenye kiburi. Huwezi hata kuyashinda mambo mengi au kuasi dhidi ya mwili wako wenyewe katika uzoefu wako halisi, siku zote ukifanya chochote unachoelekezwa kukifanya kwa tamaa zako, sio kwa kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, lakini bado unayo nyongo ya kuzungumzia uelewa wa kinadharia—huna haya! Bado unayo nyongo ya kuzungumza kuhusu uelewa wako wa maneno ya Mungu—wewe ni fidhuli jinsi gani! Kuhutubu na kujisifu kumekuwa asili yako, na umekuwa na desturi ya kufanya hili. Unalijua sana kila wakati unapotaka kuzungumza, unalifanya kwa ustadi na bila kufikiria, nawe unajiingiza katika mapambo inapokuja wakati wa kutenda. Je, si hii ni kuwapumbaza wengine? Unaweza kuwapumbaza wanadamu, lakini Mungu hawezi kupumbazwa. Wanadamu hawajui na hawana utambuzi, lakini Mungu anatilia maanani masuala hayo, naye hatakusaza. Ndugu na dada zako wanaweza kukutetea, wakiusifu uelewa wako, wakipendezwa nawe, lakini ikiwa huna uhalisi, Roho Mtakatifu hatakusaza. Pengine Mungu wa matendo hatazikaripia dosari zako, lakini Roho wa Mungu hataweka makini yoyote kwako, na hiyo itatosha wewe kuvumilia. Je, unaamini hili? Zungumza zaidi kuhusu uhalisi wa utendaji; Je, umeshasahau tayari? Zungumza zaidi kuhusu njia za kiutendaji; Je, ushasahau tayari? “Zungumza kwa uchache kuhusu nadharia za fahari au mazungumzo mazuri yasiyo na maana, na ni bora kuanza mazoezi kuanzia sasa.” Je, umesahau maneno haya? Je, huelewi yoyote haya? Je, hauna uelewa wa mapenzi ya Mungu?