Sura ya 34
Mwenyezi Mungu ndiye Mungu wa kweli mweza yote, anayefanikisha yote, na mkamilifu! Yeye si kwamba anashika tu zile nyota saba, amejaliwa Roho saba, ana macho saba, anafungua mihuri saba, na kufungua hati iliyokunjwa, lakini zaidi ya hayo, Yeye anasimamia mapigo saba na mabakuli saba, na kufunua ngurumo saba. Zamani sana, pia, Alipiga tarumbeta saba! Vitu vyote Alivyoviumba na kuvifanya kuwa timilifu vinapaswa kumsifu Yeye, kumpa Yeye utukufu, na kukitukuza kiti Chake cha enzi. Ee, Mwenyezi Mungu! Wewe ndiye kila kitu. Wewe umefanikisha kila kitu, na Kwako, yote ni kamili, yenye kung’aa, yaliyowekwa huru, huru, thabiti, na yenye nguvu! Hakuna chochote kilichofichwa au kusitiriwa; Kwako, siri zote zimefunuliwa. Zaidi ya hayo, Wewe umehukumu halaiki ya maadui Wako, Wewe unadhihirisha uadhama Wako, unadhihirisha moto Wako ulao, Wewe unaonyesha ghadhabu Yako, na, hata zaidi, Wewe unaonyesha utukufu Wako wote usio na kifani, wa milele, usio na kikomo! Watu wateule wa Mungu wasiohesabika wanapaswa kuamka na kushangilia na kuimba bila kujizuia, wakimsifu Mungu huyu wa kweli mtukufu, ambaye ni mweza yote, halisi kabisa, aliye hai kabisa, mwenye utele, na wa kutoka milele hata milele. Kiti Chake cha enzi kinapaswa kutukuzwa daima, na jina Lake takatifu litangazwe kwa shangwe na kutukuzwa daima. Hii ndiyo nia Yangu—ya Mungu—ya milele, na ni baraka isiyo na mipaka ambayo Yeye anadhihirisha kwetu na kutupa! Ni nani miongoni mwetu asiyerithi baraka hiyo? Ili kurithi baraka ya Mungu, mtu lazima alitukuze jina Lake takatifu na kuja kuzunguka kiti Chake cha enzi katika ibada. Wale wote wanaoenda mbele Zake wakiwa na makusudi mengine na nia zingine watayeyushwa na moto Wake ulao. Leo ndiyo siku ambayo maadui Wake watahukumiwa, na pia ndiyo siku watakayoangamia. Zaidi ya hayo, ndiyo siku pia ambayo Mimi, Mwenyezi Mungu, nitafunuliwa na ambayo nitapata utukufu na heshima. Ee, watu wote! Inukeni upesi kumsifu na kumkaribisha Mwenyezi Mungu ambaye, tangu zamani za kale hata milele, anatutumia fadhili, anatoa wokovu na kutupa baraka, anawafanya wanawe kuwa kamili, na kuufanikisha ufalme Wake! Hili ni tendo la ajabu la Mungu! Huku ni kuamua kabla na mpango wa Mungu wa milele—kwamba Yeye Mwenyewe amekuja kutuokoa, kutufanya kuwa kamili, na kutuleta katika utukufu.
Wale wote wasioinuka na kutoa ushuhuda ni wahenga wa vipofu na wafalme wa upumbavu. Watakuwa wapumbavu wa milele, watu waliokanganyika vichwa wa milele, wafu vipofu wa milele. Ni kwa sababu hii ndiyo roho zetu zinapaswa kuamka! Watu wote wateule wa Mungu wanapaswa kuinuka! Shangilieni, sifuni, na mtangaze kwa shangwe bila mwisho Mfalme wa utukufu, Baba wa rehema, Mwana wa ukombozi, Roho saba tele, Mwenyezi Mungu anayeleta uadhama na moto ulao, haki na hukumu, na ambaye ni mwingi kabisa, anayetosha, mwenye utele, mweza yote, na kamili. Kiti Chake cha enzi kitatukuzwa milele! Watu wote wateule wa Mungu wanapaswa kuona kwamba hii ndiyo hekima ya Mungu, njia Yake ya ajabu ya wokovu, na utimizaji wa mapenzi Yake yenye utukufu. Ikiwa bado tunashindwa kuinuka na kutoa ushuhuda, basi punde tu wakati huu utakapopita, hakutakuwa na kurudi nyuma. Iwapo tutapata baraka au kukumbwa na ole kunaamuliwa kulingana na kile tunachofanya, kile tunachofikiri, na kile tunachoishi kwa kudhihirisha katika kipindi hiki—katika sehemu hii ya safari. Ninyi mnapaswa kutendaje? Toeni ushuhuda kwa ajili ya Mungu na kumtukuza milele; mtukuzeni Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho—Mungu mmoja wa kweli wa milele!
Kuanzia sasa, mnapaswa kuona wazi kwamba wale ambao hawatoi ushuhuda kwa ajili ya Mungu—ambao hawatoi ushuhuda kwa ajili ya Mungu huyu mmoja wa kweli—na wale walio na mashaka juu Yake, wote ni wagonjwa, wafu, na wale wanaompinga Mungu! Maneno ya Mungu tayari yamethibitisha tangu zamani za kale kwamba wale wote wasiokusanyika pamoja Nami hutawanyika, na wale wasiopatana Nami wako kinyume Changu—huu ni ukweli usiopingika na usiobadilika milele! Wale ambao hawatoi ushuhuda kwa ajili ya Mungu ni watumishi wa Shetani. Watu hawa wamekuja kusumbua na kuwapotosha watoto wa Mungu, na kuvuruga usimamizi Wake; lazima washughulikiwe kwa kutumia upanga mkali! Yeyote anayewaonyesha huruma anajiletea maangamizi mwenyewe. Mnapaswa kuyasikiliza na kuyaamini maneno ya Roho wa Mungu, kutembea katika njia ya Roho wa Mungu, na kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Roho wa Mungu. Hata zaidi, mnapaswa kukitukuza kiti cha enzi cha mwenyezi Mungu hadi mwisho wa wakati!
Mwenyezi Mungu ni Mungu wa Roho saba! Yule wa macho saba na nyota saba ni Yeye, pia; Yeye anafungua mihuri saba, na hati iliyokunjwa imekunjuliwa kabisa na Yeye! Amepiga tarumbeta saba, na mabakuli saba na mapigo saba yako mkononi Mwake, ili yaachiliwe kwa mapenzi Yake. Ee, ngurumo saba ambazo zimekuwa zimefungwa daima! Wakati wa kuzifunua umefika! Yeye anayefunua ngurumo saba tayari ameonekana mbele ya macho yetu!
Mwenyezi Mungu! Kwako, yote yamewekwa huru na ni huru; hakuna matatizo, na yote yanatiririka kwa urahisi! Hakuna kinachothubutu kukuzuia au kukukwamisha Wewe, na yote yanatii mbele Yako. Chochote kisichotii kitakufa!
Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye macho saba! Yote ni wazi kabisa, yote ni yenye kung’aa na hayajasitiriwa, na yote yanadhihirishwa na kuwekwa wazi. Kwake, yote ni angavu kama fuwele, na si Mungu Mwenyewe tu aliye hivi, bali wana Wake wako hivi, pia. Hakuna mtu, hakuna kitu, na hakuna tukio linaloweza kusitiriwa mbele Yake na mbele ya wana Wake!
Nyota saba za Mwenyezi Mungu ni zenye kung’aa! Kanisa limekamilishwa na Yeye; Yeye anawaamuru wajumbe wa kanisa Lake, na kanisa lote liko ndani ya utoaji Wake. Mihuri saba imefunguliwa kikamilifu na Yeye, na mpango Wake wa usimamizi na mapenzi Yake yanakamilishwa kikamilifu na Yeye. Hati iliyokunjwa ni lugha ya kiroho ya siri ya usimamizi Wake, na imekunjuliwa na kudhihirishwa na Yeye!
Watu wote wanapaswa kusikiliza tarumbeta Zake saba zenye kishindo. Kwake, yote yanawekwa wazi, hayatafichwa tena kamwe, na hakuna huzuni tena. Yote yanadhihirishwa, na yote ni yenye ushindi!
Tarumbeta saba za Mwenyezi Mungu ni tarumbeta zilizo wazi, zenye utukufu, na za ushindi! Pia ni tarumbeta zinazowahukumu maadui Wake! Katikati ya ushindi Wake, pembe Yake inatukuzwa! Yeye anatawala ulimwengu wote!
Ametayarisha mabakuli saba ya mapigo, maadui Wake wanalengwa, na yanamwagwa kikamilifu, kwa kiwango cha juu kabisa, na maadui hao watateketezwa na moto Wake ulao. Mamlaka ya Mwenyezi Mungu yanaonyesha uweza Wake, na maadui Wake wote wanaangamizwa. Ngurumo saba za mwisho hazifungwi tena mbele ya Mwenyezi Mungu; zote zimefunuliwa! Zote zimefunuliwa! Yeye anawapiga chini maadui Wake kwa ngurumo saba, akiimarisha dunia na kuifanya itoe huduma Kwake, ili isiwe tena ukiwa!
Mwenyezi Mungu mwenye haki! Sisi tunakusifu milele! Wewe unastahili sifa zisizo na mwisho, na shangwe na kuinuliwa kusiko na mwisho! Ngurumo Zako saba si kwa ajili ya hukumu Yako tu, bali hata zaidi kwa ajili ya utukufu na mamlaka Yako, na kwa ajili ya ukamilisho wa vitu vyote!
Watu wateule wa Mungu wasiohesabika wanasherehekea mbele ya kiti cha enzi, wakimsifu na kumhimidi Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho! Sauti zao zinatikisa ulimwengu wote kama ngurumo! Hakika vitu vyote vipo kwa sababu Yake na hutokana na Yeye. Ni nani asiyethubutu kumpa utukufu wote, heshima yote, mamlaka yote, hekima yote, utakatifu wote, ushindi wote, na ufunuo wote kikamilifu Kwake? Huku ndiko kutimizwa kwa mapenzi Yake, na ni ukamilisho wa mwisho wa ujenzi wa usimamizi Wake!