Sura ya 35

Ngurumo saba zinatoka katika kiti cha enzi, zinautikisa ulimwengu, zinazipindua mbingu na dunia, na zinaenea kote angani! Sauti hiyo inapenya sana kiasi kwamba watu hawawezi kuepuka wala kujificha kutoka kwayo. Nuru za umeme na ngurumo zinatolewa, mbingu na nchi zinabadilishwa mara moja, na watu wako karibu kufa. Kisha, dhoruba kali sana ya mvua inaufagilia mbali ulimwengu wote kwa haraka sana, ikinyesha kutoka angani! Katika pembe za mwisho kabisa za dunia, kama mvua inayopita katika kila pembe, hakuna waa hata moja linalobaki, na inapofagia vitu vyote toka utosini hadi kidoleni, hakuna kitu kinachofichwa kutoka kwayo wala hakuna mtu yeyote anayeweza kuiepuka. Kama kiasi kidogo chenye baridi cha nuru za umeme, ngurumo zinawafanya watu kutetemeka kwa hofu! Upanga mkali wa kukata kuwili unawaangamiza wana wa uasi, naye adui anakabiliwa na janga, pasipo na popote pa kujificha; wanachanganyikiwa wanapokumbwa na upepo na mvua mkali, na huku wakishtushwa na pigo, wanakufa mara moja ndani ya maji yanayotiririka na kufagiliwa na maji. Wanakufa tu bila namna yoyote ya kuyaokoa maisha yao. Ngurumo saba zinatoka Kwangu nazo zinawasilisha nia Yangu, ambayo ni kuwaangamiza wana wakubwa wa Misri, kuwaadhibu waovu na kuyasafisha makanisa Yangu, ili wote wapendane sana, wafikirie na kutenda kwa njia sawa, na wawe na nia moja nami, na ili makanisa yote katika ulimwengu yaweze kujengwa na kuwa kanisa moja. Hili ni kusudi Langu.

Ngurumo inaposikika, sauti za kuomboleza zinatokea ghafla. Wengine wanaamka kutoka katika usingizi wao, na, wakiwa wameshtuka sana, wao wanachunguza nafsi zao na kukimbia mara moja mbele ya kiti cha enzi. Wanakoma kufanya hila na kudanganya na kufanya uhalifu, nami Sijachelewa sana kuwaamsha watu kama hao. Naangalia kutoka katika kiti cha enzi. Natazama ndani ya mioyo ya watu. Nawaokoa wale ambao wanitamani sana kwa dhati na kwa ari, nami Ninawahurumia. Nitawaokoa milele wale wanaonipenda mioyoni mwao zaidi ya vingine vyote, wale wanaoyaelewa mapenzi Yangu, na ambao wananifuata hadi mwisho. Mkono Wangu utawashikilia salama ili wasiweze kukabiliana na mandhari haya na hawatapatwa na madhara yoyote. Baadhi, wanapouona umeme huu wenye nuru, wana taabu isiyoelezeka mioyoni mwao na wanajuta kupindukia. Wakiendelea kutenda kwa njia hii, watakuwa wamechelewa sana kusaidika. Ee, yote na kila kitu! Yote yatafanyika. Hii pia ni moja ya njia Zangu za wokovu. Nawaokoa wale wanaonipenda na kuwaangamiza waovu. Kwa hiyo ufalme Wangu utakuwa thabiti na imara duniani na mataifa yote na watu wote, wote ulimwenguni na katika miisho ya dunia, wanajua kwamba Mimi ni uadhama, Mimi ni moto wenye ghadhabu, Mimi ni Mungu anayeutafuta moyo wa ndani kabisa wa kila mtu. Kutoka wakati huu na kuendelea, hukumu ya kiti cha enzi cheupe kikuu imefunuliwa waziwazi kwa raia na imetangazwa kwa watu wote kuwa hukumu imeanza! Bila shaka, wote ambao hawaneni yaliyo mioyoni mwao, wale wanaohisi kuwa na wasiwasi na hawathubutu kuwa na hakika, wale ambao hupoteza wakati, ambao wanayaelewa mapenzi Yangu lakini hawako radhi kuyatenda, sharti wahukumiwe. Lazima mchunguze kwa makini makusudi na nia zenu wenyewe, na mchukue nafasi yenu inayofaa, fanyieni mazoezi kabisa kile Ninachosema, kazieni umuhimu uzoefu wenu wa maisha, msitende kwa shauku kwa nje, lakini yafanyeni maisha yenu yakue, yakomae, yawe imara na yenye uzoefu, na kwa njia hiyo tu ndipo mtaupendeza moyo Wangu.

Wakane vikaragosi wa Shetani na pepo wabaya ambao wanavuruga na kuharibu yale ambayo Ninaunda fursa za kutumia vitu kwa manufaa yao. Lazima wakomeshwe na kuzuiwa kwa ukali na wanaweza tu kushughulikiwa kupitia matumizi ya mapanga makali. Wale walio wabaya zaidi lazima waangamizwe mara moja ili wasiwe tishio katika siku zijazo. Nalo kanisa litakamilishwa, litaondolewa ulemavu wote, nalo litakuwa na afya nzuri, lililojaa uhai na nguvu. Baada ya umeme wenye nuru, radi zinavuma. Hampaswi kupuuza, hampaswi kukata tamaa lakini mfanye kila mwezalo ili mfikie, na hakika mtaweza kuona kile mkono Wangu unachofanya, kile Ninachopata, kile Ninachoacha, kile Ninachokamilisha, kile Ninachoondoa kabisa, kile Ninachoangamiza. Yote haya yatatokea mbele ya macho yenu ili mweze kuona wazi kabisa uweza Wangu.

Kutoka katika kiti cha enzi hadi ulimwengu na miisho ya dunia, ngurumo saba zinasikika. Kikundi kikubwa cha watu kitaokolewa na kutii mbele ya kiti Changu cha enzi. Baada ya huu mwanga wa uzima, watu wanatafuta njia ya kuishi nao hawana budi kuja Kwangu, kupiga magoti katika ibada, midomo yao inaliita jina la Mwenyezi Mungu wa kweli, na kueleza kusihi kwao. Lakini kwa wale wanaonipinga Mimi, watu wanaoishupaza mioyo yao, radi inavuma masikioni mwao na bila shaka sharti waangamie. Haya hasa ni matokeo ya mwisho kwao. Wana Wangu wapendwa ambao ni washindi watakaa Sayuni na watu wote wataona kile watakachokipata, na utukufu mkubwa utatokea mbele yenu. Kwa kweli, hii ni baraka kubwa sana, na ni uzuri ambao ni mgumu kusimulia.

Wakati ambapo sauti za ngurumo saba zinatoka, kuna wokovu wa wale wanaonipenda Mimi, wanaonitamani kwa mioyo ya kweli. Wale wote ambao ni Wangu na ambao Nimewajaalia na kuwachagua wanaweza kuja chini ya jina Langu. Wanaweza kusikia sauti Yangu, ambayo ni wito wa Mungu. Acha wale walio katika miisho ya dunia waone kwamba Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ni upendo, Mimi ni huruma, Mimi ni uadhama, Mimi ni moto wenye ghadhabu, na hatimaye Mimi ni hukumu isiyo na huruma.

Acha wote ulimwenguni waone kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe halisi na kamili. Watu wote wanaamini kabisa na hakuna mtu anayethubutu kunipinga tena, kunihukumu au kunikashifu tena. Vinginevyo, watakumbana na laana mara moja na msiba utawafika. Watalia na kusaga meno yao tu na watasababisha uharibifu wao wenyewe.

Wacha watu wote wajue, wacha ijulikane katika ulimwengu mzima na katika miisho ya dunia, katika kila nyumba na kwa watu wote: Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja wa kweli. Kila mmoja atapiga magoti ili kumwabudu Yeye na hata watoto ambao wamejifunza tu kuzungumza wataita “Mwenyezi Mungu”! Maofisa hao wenye mamlaka watamwona kwa macho yao wenyewe Mungu wa kweli akiwa mbele yao na pia watasujudu katika ibada, wakiomba huruma na msamaha, lakini kweli wamechelewa sana kusaidika, kwani muda wao wa kufa umefika. Wanaweza tu kuangamizwa na kuhukumiwa kuelekea kwenye lindi la kina kirefu sana. Nitaikomesha enzi yote, na kuimarisha ufalme Wangu zaidi. Mataifa na watu wote watatii mbele Yangu milele yote!

Iliyotangulia: Sura ya 34

Inayofuata: Sura ya 36

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp