Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake
Sasa, mnatakiwa kufuatilia kugeuka kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kote katika njia sahihi. Kuwa watu wa Mungu kuna maana ya kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza rasmi kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa goigoi na hobelahobela kama yalivyokuwa awali; maisha hayo ni yasiyoweza kufikia viwango vinavyotakiwa na Mungu. Kama huhisi umuhimu wowote, basi hili huonyesha kwamba huna hamu ya kujiendeleza mwenyewe, kwamba ukimbizaji wako umekanganywa na kuchanganywa, na wewe ni usiyeweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Kuingia katika mafunzo ya ufalme kuna maana ya kuanza maisha ya watu wa Mungu—uko radhi kuyakubali mafunzo hayo? Uko radhi kuhisi kuthamini kwa umuhimu? Uko radhi kuishi chini ya nidhamu ya Mungu? Uko radhi kuishi chini ya kuadibu kwa Mungu? Wakati ambapo maneno ya Mungu yatakujia na kukujaribu, utafanyaje? Na utafanya nini wakati ambapo utakabiliwa na aina yote ya ukweli? Zamani, kulenga kwako hakukuwa juu ya maisha; leo, lazima uingie katika uhalisi wa maisha, na kufuatilia mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Hili ndilo lazima litimizwe na watu wa ufalme. Wale wote ambao ni watu wa Mungu lazima wawe na uzima, lazima wakubali mafunzo ya ufalme, na kufuatilia mabadiliko katika tabia ya maisha yao. Hili ndilo Mungu huwashurutisha watu wa ufalme.
Masharti ya Mungu kwa watu wa ufalme ni kama yafuatayo:
1. Lazima wakubali maagizo ya Mungu, ambalo ni kusema, lazima wakubali maneno yote yaliyonenwa katika kazi ya Mungu ya siku za mwisho.
2. Lazima waingie katika mafunzo ya ufalme.
3. Lazima wafuatilie kufanya mioyo yao iguswe na Mungu. Wakati ambapo moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na una maisha ya kiroho ya kawaida, utaishi katika eneo la uhuru, ambalo lina maana kuwa utaishi chini ya utunzaji na ulinzi wa upendo wa Mungu. Ukiishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu tu ndipo utakuwa wa Mungu.
4. Lazima wapatwe na Mungu.
5. Lazima wawe dhihirisho la utukufu wa Mungu duniani.
Haya mawazo makuu matano ni maagizo Yangu kwenu. Maneno Yangu yananenwa kwa watu wa Mungu, na kama hutaki kuyakubali maagizo haya, Sitakulazimisha—lakini ukiyakubali kwa kweli, basi utaweza kuyafanya mapenzi ya Mungu. Leo, anzeni kuyakubali maagizo ya Mungu, na kufuatilia kuwa watu wa ufalme na kufikia viwango vinavyohitajika kuwa watu wa ufalme. Hii ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia. Kama ungependa kufanya mapenzi ya Mungu kwa ukamilifu, basi lazima uyakubali maagizo haya matano, na kama unaweza kuyatimiza, utaupendeza moyo wa Mungu na kwa hakika utatumiwa sana na Mungu. Kilicho cha maana sana leo ni kuingia katika mafunzo ya ufalme. Kuingia katika mafunzo ya ufalme kunahusisha maisha ya kiroho. Awali, hakukuwa na mazungumzo ya maisha ya kiroho, lakini leo, unapoanza kuingia katika mafunzo ya ufalme, unaingia rasmi katika maisha ya kiroho.
Maisha ya kiroho ni maisha ya aina gani? Maisha ya kiroho ni yale ambayo kwayo moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na unaweza kuwa mzingatifu wa upendo wa Mungu. Ni yale ambayo kwayo unaishi katika maneno ya Mungu, na hakuna kingine kinachoushughulisha moyo wako, na unaweza kuyafahamu mapenzi ya Mungu leo, na unaongozwa na nuru ya Roho Mtakatifu leo ili kutimiza wajibu wako. Maisha kama hayo kati ya mwanadamu na Mungu ndiyo maisha ya kiroho. Kama huwezi kuifuata nuru ya leo, basi umbali umefunguka katika uhusiano wako na Mungu—huenda hata ukawa umevunjwa—na huna maisha ya kiroho ya kawaida. Uhusiano wa kawaida na Mungu hujengwa juu ya msingi wa kukubali maneno ya Mungu leo. Je, una maisha ya kiroho ya kawaida? Je, una uhusiano wa kawaida na Mungu? Wewe ni mtu anayeifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama unaweza kufuata nuru ya Roho Mtakatifu leo, na unaweza kufahamu mapenzi ya Mungu ndani ya maneno Yake, na kuingia katika maneno haya, basi wewe ni mtu ambaye hufuata mkondo wa Roho Mtakatifu. Kama hufuati mkondo wa Roho Mtakatifu, basi wewe bila shaka ni mtu asiyefuatilia ukweli. Roho Mtakatifu hana nafasi ya kufanya kazi ndani ya wale ambao hawana hamu ya kujiendeleza wenyewe, na kutokana na hayo, watu hao hawawezi kamwe kukusanya nguvu zao, na kila mara wao huwa baridi. Leo, wewe hufuata mkondo wa Roho Mtakatifu? Wewe uko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu? Je, umeibuka kutoka kwa hali baridi? Wale wote ambao huamini katika maneno ya Mungu, ambao huchukulia kazi ya Mungu kama msingi, na hufuata nuru ya Roho Mtakatifu leo—wao wote wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Kama wewe huamini kwamba maneno ya Mungu ni kweli na sahihi kwa dhahiri, na kama wewe huamini maneno ya Mungu bila kujali kile Yeye husema, basi wewe ni mtu ambaye hufuatilia kuingia katika kazi ya Mungu, na kwa njia hii utatimiza mapenzi ya Mungu.
Ili kuingia katika mkondo wa Roho Mtakatifu lazima uwe na uhusiano wa kawaida na Mungu, na lazima kwanza ujiondoshe kwa hali yako baridi. Watu wengine kila mara hufuata walio wengi, na mioyo yao imetangatanga mbali sana na Mungu; watu hao hawana hamu ya kujiendeleza wenyewe, na viwango ambavyo wao hufuatilia ni vya chini sana. Ukimbizaji wa kumpenda Mungu tu na kupatwa na Mungu ndiyo mapenzi ya Mungu. Kuna watu ambao hutumia tu dhamiri yao kulipa mapenzi ya Mungu, lakini hili haliwezi kuridhisha mapenzi ya Mungu; kadri viwango unavyofuatilia vilivyo juu zaidi, ndivyo vitakavyokuwa vinawiana na mapenzi ya Mungu. Kama mtu aliye wa kawaida, na ambaye hufuatilia upendo wa Mungu, kuingia katika ufalme kuwa mmoja wa watu wa Mungu ni siku za usoni zenu za kweli, na maisha ambayo ni yenye thamani na maana sana; hakuna aliyebarikiwa kuliko ninyi. Mbona Nasema hili? Kwa sababu wale wasiomwamini Mungu huishi kwa ajili ya mwili, na wao huishi kwa ajili ya Shetani, lakini leo ninyi huishi kwa ajili ya Mungu, na huishi kufanya mapenzi ya Mungu. Ndiyo maana Nasema maisha yenu ni yenye maana sana. Ni kundi hili tu la watu, ambao wameteuliwa na Mungu, wanaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana sana: Hakuna mwingine duniani anaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya thamani na maana hivyo. Kwa sababu mmeteuliwa na Mungu, na mmekuzwa na Mungu, na, aidha, kwa sababu ya upendo wa Mungu kwenu, mmefahamu uzima wa kweli, na mnajua namna ya kuishi maisha yenye thamani sana. Hili si kwa sababu ukimbizaji wenu ni mzuri, lakini kwa sababu ya neema ya Mungu; ni Mungu aliyefungua macho ya roho zenu, na ni Roho wa Mungu aliyegusa mioyo yenu, kuwapa ninyi bahati nzuri ya kuja mbele Yake. Kama Roho wa Mungu hangekuwa amekupa nuru, basi hungekuwa na uwezo wa kuona kilicho cha kupendeza kuhusu Mungu, wala haingewezekana kwa wewe kumpenda Mungu. Ni kwa sababu kabisa Roho wa Mungu amegusa mioyo ya watu ndiyo mioyo yao imeelekea kwa Mungu. Mara nyingine, wakati ambapo unafurahia maneno ya Mungu, roho yako huguswa, na wewe huhisi kwamba huna budi kumpenda Mungu, kwamba kuna nguvu nyingi ndani yako, na kwamba hakuna chochote usichoweza kuweka kando. Kama wewe unahisi hivi, basi umeguswa na Roho wa Mungu, na moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na utamwomba Mungu na kusema: “Ee Mungu! Sisi kweli tumejaaliwa na kuteuliwa na Wewe. Utukufu Wako hunipa fahari, na inaonekana ya kuleta sifa kuu kwa mimi kuwa mmoja wa watu Wako. Nitatumia chochote na kutoa chochote ili kufanya mapenzi Yako, na nitayatoa maisha yangu yote, na juhudi za maisha yangu yote, Kwako.” Unapoomba hivi, kutakuwa na upendo usioisha na utiifu wa kweli kwa Mungu ndani ya moyo wako. Je, umewahi kuwa na tukio kama hili? Kama watu huguswa mara kwa mara na Roho wa Mungu, basi wako radhi hasa kujitolea wenyewe kwa Mungu katika maombi yao: “Ee Mungu! Ningependa kutazama siku Yako ya utukufu, na ningependa kuishi kwa ajili Yako—hakuna kilicho cha thamani au maana zaidi kuliko kuishi kwa ajili Yako, na sina hamu hata kidogo ya kuishi kwa ajili ya Shetani na mwili. Wewe huniinua kwa kuniwezesha mimi kuishi kwa ajili Yako leo.” Wakati ambapo umeomba kwa njia hii, utahisi kwamba huna budi ila kutoa moyo wako kwa Mungu, kwamba lazima umpate Mungu, na kwamba ungechukia kufa bila kumpata Mungu wakati ambapo uko hai. Baada ya kunena ombi hilo, kutakuwa na nguvu isiyoisha ndani yako, na hutajua hiyo hutoka wapi; ndani ya moyo wako kutakuwa na nguvu bila kikomo, na utakuwa na hisi kwamba Mungu ni wa kupendeza sana, na kwamba Anastahili kupendwa. Huu ndio wakati ambapo utakuwa umeguswa na Mungu. Wale wote ambao wamekuwa na tukio hilo wameguswa na Mungu. Kwa wale ambao mara kwa mara huguswa na Mungu, mabadiliko hutokea ndani ya maisha yao, wao huweza kufanya azimio lao na wako radhi kumpata Mungu kabisa, upendo kwa Mungu ndani yao ni thabiti zaidi, mioyo yao imeelekea kwa Mungu kabisa, wao huwa hawastahi familia, ulimwengu, matatizo, au siku zao za baadaye, na wao huwa radhi kutoa juhudi za maisha yote kwa Mungu. Wale wote ambao wameguswa na Roho wa Mungu ni watu wanaofuatilia ukweli, na ambao huwa na tumaini la kufanywa wakamilifu na Mungu.
Je, umeelekeza moyo wako kwa Mungu? Moyo wako umeguswa na Roho wa Mungu? Kama hujawahi kuwa na tukio kama hilo, na kama hujawahi kuomba kwa njia kama hiyo, basi hili linaonyesha kwamba Mungu hana nafasi ndani ya moyo wako. Wale wote ambao huongozwa na Roho wa Mungu na ambao wameguswa na Roho wa Mungu huwa na kazi ya Mungu, ambalo linaonyesha kwamba maneno ya Mungu na upendo wa Mungu vimekita mizizi ndani yao. Watu wengine husema: “Mimi si mwenye ari kama wewe katika maombi yangu, wala siguswi sana na Mungu: mara nyingine—wakati ambapo mimi hutafakari na kuomba—mimi huhisi kwamba Mungu ni wa kupendeza, na moyo wangu huguswa na Mungu.” Hakuna kilicho muhimu zaidi kuliko moyo wa mwanadamu. Wakati ambapo moyo wako umeelekea kwa Mungu, nafsi yako yote itakuwa imeelekea kwa Mungu, na wakati huo moyo wako utakuwa umeguswa na Roho wa Mungu. Wengi sana miongoni mwenu wamekuwa na tukio kama hilo—ni kwamba tu vina vya matukio yenu si sawa. Watu wengine husema: “Mimi huwa sisemi maneno mengi ya maombi, mimi husikiliza tu mawasiliano ya wengine na nguvu huongezeka ndani yangu.” Hili huonyesha kwamba umeguswa na Mungu ndani. Watu ambao wameguswa na Mungu ndani hutiwa moyo wakati ambapo wao husikia mawasiliano ya wengine; kama moyo wa mtu hubaki bila kuathirika kabisa wanaposikia maneno ya kutia moyo, basi hili huthibitisha kwamba kazi ya Roho Mtakatifu haiko ndani yao. Hakuna shauku ndani yao, ambalo huthibitisha kwamba hawana azimio, na hivyo hawana kazi ya Roho Mtakatifu. Kama mtu ameguswa na Mungu, atakuwa na athari anaposikia maneno ya Mungu; kama hajaguswa na Mungu, basi hajajishughulisha na maneno ya Mungu, hayana uhusiano naye, na hana uwezo wa kupata nuru. Wale ambao wamesikia maneno ya Mungu na hawakuwa na athari ni watu ambao hawajaguswa na Mungu—ni watu ambao hawana kazi ya Roho Mtakatifu. Wale wote ambao wanaweza kukubali nuru mpya huguswa, na huwa na kazi ya Roho Mtakatifu.
Jitathmini mwenyewe:
1. Je, uko katikati ya kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu?
2. Moyo wako umeelekea kwa Mungu? Umeguswa na Mungu?
3. Maneno ya Mungu yamekita mizizi ndani yako?
4. Je, utendaji wako umejengwa juu ya msingi wa masharti ya Mungu?
5. Wewe huishi chini ya uongozi wa nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu?
6. Moyo wako hutawaliwa na dhana za zamani, au hutawaliwa na maneno ya Mungu leo?
Ukiyasikia maneno haya, athari iliyo ndani yenu ni gani? Baada ya kuamini kwa miaka hii yote, una maneno ya Mungu kama uzima wako? Je, kumekuwa na mabadiliko katika tabia yako potovu ya awali? Wewe, kwa mujibu wa maneno ya Mungu leo, unajua ni nini maana ya kuwa na uzima, na nini maana ya kutokuwa na uzima? Je, hili linaeleweka kwenu? Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno ya Mungu leo: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno ya Mungu leo. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno ya Mungu leo, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Kile ambacho Mungu hutaka ni watu ambao huzifuata nyayo Zake. Haijalishi vile ulichoelewa awali ni cha ajabu na safi, Mungu hakitaki, na kama huwezi kuweka kando vitu hivyo, basi vitakuwa kizuizi kikubwa mno kwa kuingia kwako katika siku za baadaye. Wale wote ambao wanaweza kufuata nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Watu wa enzi zilizopita pia walifuata nyayo za Mungu, ilhali hawangeweza kufuata mpaka leo; hii ndiyo baraka ya watu wa siku za mwisho. Wale ambao wanaweza kufuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, na ambao wanaweza kuzifuata nyayo za Mungu, kiasi kwamba wamfuate Mungu popote Awaongozapo—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu. Leo, wale wote ambao hufuata maneno ya sasa ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno ya leo ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu. Huduma ambayo imetenganishwa na matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu ni huduma ambayo ni ya mwili, na ya dhana, na haiwezi kuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kama watu huishi miongoni mwa dhana za kidini, basi hawawezi kufanya lolote lenye kustahili kwa mapenzi ya Mungu, na hata ingawa wao humhudumia Mungu, wao huhudumu katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kuhudumu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Wale ambao hawawezi kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi mapenzi ya Mungu, na wale ambao hawaelewi mapenzi ya Mungu hawawezi kumhudumia Mungu. Mungu hutaka huduma inayoupendeza moyo Wake mwenyewe; Hataki huduma ambayo ni ya dhana na mwili. Kama watu hawawezi kuzifuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wao huishi katikati ya dhana. Huduma ya watu hao hukatiza na huvuruga, na huduma ya aina hii huenda kinyume na Mungu. Hivyo wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu hawawezi kumhudumia Mungu; wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu humpinga Mungu bila shaka, na ni wasioweza kulingana na Mungu. “Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu” kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli. Wale ambao huondoshwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni watu wasioweza kufuata kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na ambao huasi dhidi ya kazi ya karibuni zaidi ya Mungu. Kwamba watu hao humpinga Mungu waziwazi ni kwa sababu Mungu amefanya kazi mpya, na kwa sababu picha ya Mungu si sawa na ile iliyo ndani ya dhana zao—kutokana na hilo wao humpinga Mungu waziwazi na kumhukumu Mungu, kusababisha wao kuchukiwa na kukataliwa na Mungu. Kuwa na ufahamu wa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu si jambo rahisi, lakini kama watu wana nia ya kutii kazi ya Mungu kwa kudhamiria na kuitafuta kazi ya Mungu, basi watakuwa na nafasi ya kumwona Mungu, na watakuwa na nafasi ya kupata uongozi mpya zaidi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao hupinga kazi ya Mungu kwa kudhamiria hawawezi kupata nuru ya Roho mtakatifu au uongozi wa Mungu. Hivyo, kama watu wanaweza kupokea kazi ya karibuni zaidi ya Mungu au la hutegemea neema ya Mungu, hutegemea ukimbizaji wao, na hutegemea makusudi yao.
Wale wote ambao huweza kutii matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Haijalishi vile walikuwa, au vile Roho Mtakatifu alikuwa akifanya kazi ndani yao—wale ambao wamepata kazi ya karibuni zaidi ni waliobarikiwa zaidi, na wale ambao hawawezi kufuata kazi ya karibuni zaidi huondoshwa. Mungu anataka wale wanaoweza kukubali nuru mpya, na Anataka wale ambao hukubali na kujua kazi Yake ya karibuni zaidi. Kwa nini husemwa kwamba lazima uwe mwanamwali safi? Mwanamwali safi anaweza kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu na kuelewa mambo mapya, na zaidi ya hayo, kuweza kuweka kando dhana za zamani, na kutii kazi ya Mungu leo. Kundi hili la watu, ambao hukubali kazi mpya zaidi ya leo, walijaaliwa na Mungu kabla ya enzi, na ni ambao wamebarikiwa zaidi ya watu wote. Ninyi huisikia sauti ya Mungu moja kwa moja, na kutazama kuonekana kwa Mungu, na hivyo, kotekote mbinguni na duniani, na kotekote katika enzi, hakuna waliobarikiwa kuliko ninyi, hili kundi la watu. Haya yote ni kwa sababu ya kazi ya Mungu, kwa sababu ya majaaliwa na uteuzi wa Mungu, na kwa sababu ya neema ya Mungu; kama Mungu hangeongea na kutamka maneno Yake, hali zenu zingekuwa kama zilivyo leo? Vivi hivi, utukufu wote na sifa ziwe kwa Mungu, kwani haya yote ni kwa sababu Mungu huwainua ninyi. Na mambo haya yakiwa akilini, bado ungeweza kuwa baridi? Nguvu zako bado hazingeweza kuongezeka?
Kwamba wewe huweza kukubali hukumu, kuadibu, kuangamiza, na usafishaji wa maneno ya Mungu, na, aidha, unaweza kukubali maagizo ya Mungu, lilijaaliwa na Mungu mwanzoni mwa wakati, na hivyo lazima usihuzunishwe sana wakati ambapo wewe huadibiwa. Hakuna anayeweza kuondoa kazi ambayo imefanywa ndani yenu, na baraka ambazo zimetolewa ndani yenu, na hakuna anayeweza kuondoa yote ambayo mmepewa ninyi. Watu wa dini hawastahimili mlingano na ninyi. Ninyi hamna ubingwa mkuu katika Biblia, na hamjajizatiti na nadharia za kidini, lakini kwa sababu Mungu amefanya kazi ndani yenu, mmepata zaidi ya yeyote kotekote katika enzi—na kwa hiyo hii ni baraka yenu kuu zaidi. Kwa sababu ya hili, lazima mjitolee hata zaidi kwa Mungu, na hata waaminifu zaidi kwa Mungu. Kwa sababu Mungu hukuinua, lazima utegemeze juhudi zako, na lazima utayarishe kimo chako kukubali maagizo ya Mungu. Lazima usimame imara mahali ambapo Mungu amekupa, ufuatilie kuwa mmoja wa watu wa Mungu, ukubali mafunzo ya ufalme, upatwe na Mungu na hatimaye kuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Je, wewe una maazimio haya? Kama una maazimio hayo, basi hatimaye una hakika ya kupatwa na Mungu, na utakuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Unapaswa kuelewa kwamba agizo kuu ni kupatwa na Mungu na kugeuka kuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Haya ni mapenzi ya Mungu.
Maneno ya Roho Mtakatifu leo ni nguvu za kazi ya Roho Mtakatifu, na kuendelea kwa Roho Mtakatifu kumpa nuru mwanadamu wakati wa kipindi hiki ni mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu. Na mwelekeo ni upi katika kazi ya Roho Mtakatifu leo? Ni uongozi wa watu ndani ya kazi ya Mungu leo, na ndani ya maisha ya kiroho ya kawaida. Kuna hatua kadhaa za kuingia katika maisha ya kiroho ya kawaida:
1. Kwanza, lazima uumimine moyo wako ndani ya maneno ya Mungu. Lazima usiyafuatilie maneno ya Mungu katika siku za zamani, na lazima usiyasome wala kuyafananisha na maneno ya sasa. Badala yake, lazima uumimine moyo wako kabisa katika maneno ya sasa ya Mungu. Kama kuna watu ambao bado wangependa kuyasoma maneno ya Mungu, vitabu vya kiroho, au maelezo mengine ya mahubiri kutoka kwa siku za zamani, ambao hawafuati maneno ya Roho Mtakatifu leo, basi wao ni wapumbavu zaidi ya watu wote; Mungu huchukia sana watu kama hao. Kama uko radhi kukubali nuru ya Roho Mtakatifu leo, basi mimina moyo wako kabisa katika matamshi ya Mungu leo. Hili ni jambo la kwanza ambalo lazima utimize.
2. Lazima uombe juu ya msingi wa maneno yaliyonenwa na Mungu leo, uingie ndani ya maneno ya Mungu na uwasiliane kwa karibu na Mungu, na ufanye maazimio yako mbele ya Mungu, ni viwango vipi ambavyo ungependa kufuatilia ufanikishaji wake.
3. Lazima ufuatilie kuingia kwa maana sana ndani ya ukweli juu ya msingi wa kazi ya Roho Mtakatifu leo. Usishikilie matamshi na nadharia zilizopitwa na wakati kutoka zamani.
4. Lazima utafute kuguswa na Roho Mtakatifu, na kuingia katika maneno ya Mungu.
5. Lazima ufuatilie kuingia katika njia ambayo Roho Mtakatifu anatembea leo.
Na ni vipi ambavyo wewe hutafuta kuguswa na Roho Mtakatifu? Kilicho muhimu ni kuishi ndani ya maneno ya sasa ya Mungu, na kuomba juu ya msingi wa masharti ya Mungu. Baada ya kuomba kwa njia hii, Roho Mtakatifu kwa kweli atakugusa. Kama hutafuti kwa kutegemea msingi wa maneno yaliyonenwa na Mungu leo, basi hili ni bure. Unapaswa kuomba, na kusema: “Ee Mungu! Mimi hukupinga Wewe, na unanidai Mimi mengi sana; mimi ni mkaidi sana, na siwezi kamwe kukuridhisha Wewe. Ee Mungu, natamani Wewe uniokoe, natamani kukupa Wewe huduma hadi mwisho kabisa, natamani kufa kwa ajili Yako. Wewe hunihukumu na kuniadibu, na sina malalamiko; mimi hukupinga Wewe na nastahili kufa, ili watu wote waweze kutazama tabia Yako yenye haki katika kifo changu.” Wakati ambapo wewe huomba kutoka moyoni mwako kwa njia hii, Mungu atakusikia, na atakuongoza; kama huombi juu ya msingi wa maneno ya Roho Mtakatifu leo, basi hakuna uwezekano wa Roho Mtakatifu kukugusa wewe. Kama wewe huomba kwa kadri ya mapenzi ya Mungu, na kwa kadri ya kile ambacho Mungu hutaka kufanya leo, utasema: “Ee Mungu! Nataka kukubali maagizo Yako na kuwa mwaminifu kwa maagizo Yako, na niko radhi kuyatoa maisha yangu yote kwa utukufu Wako, ili yote nifanyayo yaweze kufikia kiwango cha watu wa Mungu. Moyo wangu na uweze kuguswa na Wewe. Nataka Roho Wako anipe nuru wakati wowote, kusababisha yote nifanyayo yalete aibu kwa Shetani, ili hatimaye nipatwe na Wewe.” Kama wewe huomba kwa njia hii, ukilenga mapenzi ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako bila kuzuilika. Haijalishi maneno ya maombi yako ni mangapi—kilicho muhimu ni kama unaelewa mapenzi ya Mungu au la. Huenda ninyi nyote mmekuwa na tukio lifuatalo: Wakati mwingine, ukiwa unaomba katika kusanyiko, nguvu za kazi ya Roho Mtakatifu hufikia kilele chake, kusababisha nguvu za kila mtu kuongezeka. Watu wengine hulia kwa uchungu na kutoa machozi huku wakiomba, kwa kulemewa na majuto mbele ya Mungu, na watu wengine huonyesha azimio lao, na kuweka nadhiri. Hiyo ndiyo athari ya kutimizwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Leo, ni ya muhimu sana kwamba watu wote wamimine mioyo yao kabisa ndani ya maneno ya Mungu. Usisisitize kwa maneno yaliyonenwa awali; kama bado unashikilia kilichokuja awali, basi Roho Mtakatifu hatafanya kazi ndani yako. Je, waona vile hili ni muhimu?
Je, mnajua njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea leo? Mawazo makuu kadhaa hapo juu ni kile kitakachotimizwa na Roho Mtakatifu leo na katika siku za baadaye; ni njia inayofuatwa na Roho Mtakatifu, na kuingia ambako kunapaswa kufuatiliwa na mwanadamu. Katika kuingia kwako maishani, kwa kiasi kidogo sana lazima umimine moyo wako ndani ya maneno ya Mungu, na uweze kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu; moyo wako lazima uwe na shauku kwa Mungu, lazima ufuatilie kuingia kwa maana sana katika ukweli, na malengo ambayo Mungu hutaka. Wakati ambapo unakuwa na nguvu hizi, basi hilo huonyesha kuwa umeguswa na Mungu, na moyo wako umeanza kuelekea kwa Mungu.
Hatua ya kwanza ya kuingia katika uzima ni kuumimina moyo wako kabisa ndani ya maneno ya Mungu, na hatua ya pili ni kukubali kuguswa na Roho Mtakatifu. Ni nini athari ya kutimizwa kwa kukubali kuguswa na Roho Mtakatifu? Kuweza kuwa na shauku ya, kutafuta, na kuchunguza ukweli wa maana sana, na kuwa na uwezo wa kushirikiana na Mungu katika njia nzuri. Leo, wewe hushirikiana na Mungu, ambalo ni kusema kuna lengo kwa ukimbizaji wako, kwa maombi yako, na kwa mawasiliano yako ya maneno ya Mungu, na wewe hutekeleza wajibu wako kwa mujibu wa masharti ya Mungu—huku pekee ndiko kushirikiana na Mungu. Ukizungumza tu kuhusu kumwacha Mungu atende, lakini usichukue hatua yoyote, wala kuomba au kutafuta, basi hili lingeweza kuitwa ushirikiano? Kama huna chochote kuhusu ushirikiano ndani yako, na umeondolewa mafunzo ya kuingia ambayo yana lengo, basi wewe hushirikiani? Watu wengine husema: “Kila kitu hutegemea majaaliwa ya Mungu, yote hufanywa na Mungu mwenyewe: kama Mungu hangelifanya, basi mwanadamu angewezaje?” Kazi ya Mungu ni ya kawaida, na siyo ya rohoni hata kidogo, na ni kupitia tu kwa utafutaji wako wa utendaji ndiyo Roho Mtakatifu hufanya kazi, kwani Mungu hamlazimishi mwanadamu—lazima umpe Mungu nafasi ya kufanya kazi, na kama hufuatilii au kuingia, na kama hakuna shauku hata kidogo ndani ya moyo wako, basi Mungu hana nafasi ya kufanya kazi. Ni kwa njia ipi ndio unaweza kutafuta kuguswa na Mungu? Kupitia maombi, na kuja karibu na Mungu. Lakini la muhimu zaidi, kumbuka, lazima iwe juu ya msingi wa maneno yanayonenwa na Mungu. Wakati ambapo unaguswa mara kwa mara na Mungu, hutawaliwi kabisa na mwili: Mume, mke, watoto, na pesa—yote ni yasiyoweza kukufunga wewe, na wewe hutamani kufuatilia tu ukweli na kuishi mbele ya Mungu. Wakati huu, utakuwa mtu anayeishi katika eneo la uhuru.