Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari

Watu wote wamepitia usafishaji kwa sababu ya maneno ya Mungu. Kama sio Mungu mwenye mwili wanadamu bila shaka hawangebarikiwa kuteseka hivyo. Inaweza pia kusemwa hivi—wale wanaoweza kukubali majaribio ya maneno ya Mungu ni watu waliobarikiwa. Kulingana na ubora wa akili wa watu wa asili, mwenendo wao, mitazamo yao kwa Mungu, hawastahili kupokea aina hii ya usafishaji. Ni kwa sababu wameinuliwa na Mungu ndio wamefurahia baraka hii. Watu walikuwa wakisema kwamba hawakustahili kuuona uso wa Mungu au kusikia maneno Yake. Leo ni kwa sababu tu ya kutiwa moyo na Mungu na fadhili Zake ndio watu wamepokea usafishaji wa maneno Yake. Hii ni baraka ya kila mtu ambaye anazaliwa katika siku za mwisho—je, nyinyi binafsi mmepitia haya? Ni katika hali zipi watu wanapaswa kuteseka na kuwa na vipingamizi imekusudiwa na Mungu, na haitegemei mahitaji ya watu wenyewe. Hii ni kweli kamili. Kila muumini anapaswa kuwa na uwezo wa kupitia majaribio ya maneno ya Mungu na kuteseka ndani ya maneno Yake. Je, hili ni jambo mnaloweza kuliona dhahiri? Kwa hiyo kuteseka ulikopitia kumebadilishana na baraka za leo; ikiwa hutateseka kwa ajili ya Mungu, huwezi kupata sifa Zake. Labda umelalamika hapo awali, lakini haijalishi umelalamika kiasi gani Mungu hakumbuki hayo kukuhusu wewe. Leo imekuja na hakuna haja ya kuchunguza masuala ya jana.

Watu wengine husema kwamba wao hujaribu kumpenda Mungu lakini hawawezi, na wanaposikia kwamba Mungu yuko karibu kuondoka basi wanakuwa na upendo Kwake. Watu wengine kwa jumla huwa hawaweki ukweli katika matendo, na wanaposikia kwamba Mungu yuko karibu kuondoka kwa hasira wao huja mbele Yake na kuomba. “Ee Mungu! Tafadhali usiende. Nipe nafasi! Mungu! Sijakuridhisha hapo awali; nimekuwa mdeni Wako na kukupinga Wewe. Leo niko radhi kuutoa mwili na moyo wangu kikamilifu ili hatimaye nikuridhishe na kukupenda Wewe. Sitakuwa na nafasi hiyo tena.” Umefanya aina hiyo ya ombi? Mtu anapoomba kwa njia hii ni kwa kuwa dhamiri yake imeamshwa na maneno ya Mungu. Binadamu wote ni wazito na wenye akili goigoi. Ni wenye kupatwa mara kwa mara na kuadibu na usafishaji ilhali hawajui kile ambacho Mungu anatimiza. Mungu asingefanya kazi hivi, watu bado wangechanganyikiwa; hakuna ambaye angetia msukumo hisia za kiroho ndani ya mioyo ya watu. Ni maneno ya Mungu ya hukumu na kuwafichua watu tu ndiyo yanaweza kuzaa tunda hilo. Kwa hiyo, mambo yote yanafanikishwa na kutimizwa kwa sababu ya maneno ya Mungu, na ni kwa ajili tu ya maneno Yake ndio upendo wa wanadamu kwa Mungu umeamshwa. Ikiwa watu wangempenda tu Mungu kutegemea dhamiri zao hawangeona matokeo yoyote. Watu hawakutegemeza upendo wao kwa Mungu juu ya dhamiri yao hapo awali? Kulikuwa na mtu mmoja ambaye alianza kumpenda Mungu? Ilikuwa tu kupitia kwa himizo la maneno ya Mungu ndio walimpenda Mungu. Watu wengine husema: “Nimemfuata Mungu kwa miaka mingi sana na kufurahia kiasi kikubwa cha neema Yake, baraka nyingi sana. Nimepatwa mara kwa mara na usafishaji na hukumu kutoka kwa maneno Yake. Kwa hiyo nimekuja kuelewa mengi, na nimeona upendo wa Mungu. Lazima nimshukuru Yeye, lazima nilipe neema Yake. Nitamridhisha Mungu na kifo, na nitategemeza upendo wangu Kwake juu ya dhamiri yangu.” Watu wakitegemea tu hisia za dhamiri zao, hawawezi kuhisi kupendeza kwa Mungu; wakitegemea tu dhamiri zao, upendo wao kwa Mungu utakuwa dhaifu. Ukizungumza tu kuhusu kulipa neema na upendo wa Mungu, hutakuwa na msukumo wowote katika upendo wako Kwake; kumpenda Yeye kwa kutegemea hisia za dhamiri yako ni mtazamo baridi. Ni kwa nini Nasema kwamba ni mtazamo baridi? Hili ni suala la utendaji. Huu ni upendo wa aina gani? Huku si kujaribu kumdanganya Mungu na kufanya kitu kwa namna isiyo ya dhati tu kwa ajili Yake? Watu wengi sana huamini kwamba hakuna tuzo la kumpenda Mungu, na mtu ataadhibiwa hata hivyo kwa kutompenda Yeye, kwa hiyo kwa jumla kutotenda dhambi tu kunatosha. Kwa hiyo kumpenda Mungu na kulipa upendo Wake kwa kutegemeza hisia za dhamiri ya mtu ni mtazamo baridi, na si upendo kwa Mungu unaokuja kwa hiari kutoka moyoni mwa mtu. Upendo kwa Mungu unapaswa kuwa hisia halisi kutoka katika kina cha moyo wa mtu. Watu wengine husema: “Mimi mwenyewe niko radhi kumfuatilia Mungu na kumfuata Yeye. Sasa Mungu anataka kuniacha lakini bado nataka kumfuata Yeye. Iwapo Ananitaka au la, bado nitampenda Yeye, na mwishowe lazima nimpate Yeye. Ninatoa moyo wangu kwa Mungu, na haijalishi kile Yeye hufanya, nitamfuata Yeye kwa maisha yangu yote. Lolote litokealo, lazima nimpende Mungu na lazima nimpate Yeye; sitapumzika mpaka nimpate Yeye.” Una aina hii ya nia?

Njia ya kuamini katika Mungu ni njia ya kumpenda Yeye. Ikiwa unaamini katika Yeye lazima umpende Yeye; kwa hali yoyote, kumpenda Yeye hakuhusu tu kulipa upendo Wake au kumpenda kwa kutegemea hisia za dhamiri—ni pendo safi kwa Mungu. Kuna nyakati ambazo watu hutegemea tu dhamiri zao na hawawezi kuhisi upendo wa Mungu. Kwa nini kila mara Nilisema: “Roho wa Mungu asisimue roho zetu”? Kwa nini Sikuzungumzia kusisimua dhamiri za watu kumpenda Mungu? Ni kwa sababu dhamiri za watu haziwezi kuhisi kupendeza kwa Mungu. Ikiwa hujaridhishwa na maneno hayo, huenda ukatumia dhamiri yako kuhisi upendo Wake, na utakuwa na msukumo fulani wakati huo lakini baadaye utatoweka. Ukitumia tu dhamiri yako kuhisi kupendeza kwa Mungu, una msukumo unapoomba, lakini baadaye unaondoka tu, unatoweka. Hilo linahusu nini? Ukitumia tu dhamiri yako hutaweza kuamsha upendo wako kwa Mungu; unapohisi kweli kupendeza Kwake ndani ya moyo wako roho yako itasisimuliwa na Yeye, na ni wakati huo tu ndio dhamiri yako itaweza kufanya kazi yake ya asili. Hiyo ni kusema kwamba watu wakishasisimuliwa na Mungu katika roho zao na wakati roho zao zimepata maarifa na himizo, yaani, baada ya wao kupata uzoefu, ndipo tu wataweza kumpenda Mungu kwa kufaa na dhamiri zao. Kumpenda Mungu na dhamiri yako si vibaya—hiki ni kiwango cha chini sana cha kumpenda Mungu. Njia ya wanadamu ya upendo ya kufanya haki kwa shida tu kwa neema ya Mungu bila shaka haiwezi kuchochea kuingia kwao kiutendaji. Watu wanapopata baadhi ya kazi ya Roho Mtakatifu, yaani, wanapoona na kuonja upendo wa Mungu katika uzoefu wao wa vitendo, wakiwa na maarifa fulani ya Mungu na kuona kweli kwamba Mungu anastahili sana upendo wa wanadamu na jinsi Alivyo mzuri, ni wakati huo tu ndio watu wanaweza kumpenda Mungu kwa uhalisi.

Watu wanapowasiliana na Mungu na mioyo yao, mioyo yao inapoweza kumgeukia Yeye kikamilifu, hii ni hatua ya kwanza ya upendo wa wanadamu kwa Mungu. Ikiwa unataka kumpenda Mungu, lazima kwanza uweze kugeuza moyo wako Kwake. Kugeuza moyo wako kwa Mungu ni nini? Ni wakati ambapo kila kitu unachofuatilia ndani ya moyo wako ni kwa ajili ya kumpenda na kumpata Mungu, na hii inaonyesha kwamba umeugeuza moyo wako kikamilifu kwa Mungu. Bali na Mungu na maneno Yake, hakuna takriban kitu chochote kingine ndani ya moyo wako (familia, mali, mume, mke, watoto au vitu vingine). Hata kama vipo, haviwezi kuumiliki moyo wako, na hufikirii juu ya matazamio yako ya baadaye lakini unafuatilia tu kumpenda Mungu. Wakati huo utakuwa umegeuza moyo wako kwa Mungu kabisa. Ikiwa bado unajitengenezea mipango ndani ya moyo wako na kila mara unafuatilia manufaa yako binafsi, na kila mara unafikiri: “Ni lini ninaweza kumwomba Mungu ombi ndogo? Familia yangu itakuwa tajiri lini? Ninawezaje kupata mavazi kadhaa mazuri? …” Ikiwa unaishi katika hali hiyo inaonyesha kwamba moyo wako haujamgeukia Mungu kwa ukamilifu. Ikiwa una maneno ya Mungu tu moyoni mwako na unaweza kumwomba Mungu na kuwa karibu naye nyakati zote, kana kwamba Yeye yu karibu sana nawe, kana kwamba Mungu yu ndani yako nawe u ndani Yake, ikiwa uko katika hali ya aina hiyo, inamaanisha kwamba moyo wako umekuwa katika uwepo wa Mungu. Ukimwomba Mungu na kula na kunywa maneno Yake kila siku, unafikiria kila mara kuhusu kazi ya kanisa, ukifikiria juu ya mapenzi ya Mungu, ukitumia moyo wako kumpenda Yeye kwa uhalisi na kuridhisha moyo Wake, basi moyo wako utakuwa wa Mungu. Ikiwa moyo wako unamilikiwa na vitu vingine vingi, basi bado unamilikiwa na Shetani na haujamrudia Mungu kweli. Wakati moyo wa mtu umemrudia Mungu kweli, atakuwa na upendo halisi, wa hiari Kwake na ataweza kufikiria kazi ya Mungu. Ingawa bado atakuwa na hali za kipumbavu na zisizo na akili, ataweza kuwa na fikira kwa ajili ya maslahi ya nyumba ya Mungu, ya kazi Yake, na ya mabadiliko katika tabia yake. Moyo wake utakuwa sahihi kabisa. Watu wengine kila mara hupeperusha bendera ya kanisa haijalishi wanachofanya; kweli ni kwamba hii ni kwa manufaa yao. Mtu wa aina hiyo hana aina nzuri ya nia. Yeye ni mhalifu na mdanganyifu na mambo mengi sana anayofanya ni ya kutafuta manufaa yake mwenyewe. Mtu wa aina hiyo hafuatilii kumpenda Mungu; moyo wake bado ni wa Shetani na hauwezi kumgeukia Mungu. Mungu hana njia ya kumpata mtu wa aina hiyo.

Hatua ya kwanza ya kumpenda Mungu kweli na kupatwa na Yeye ni kuurudisha moyo wako kwa ukamilifu kwa Mungu. Katika kila jambo ufanyalo, jichunguze na uulize: “Ninafanya hiki kulingana na moyo wa upendo kwa Mungu? Kuna nia yoyote ya kibinafsi ndani yake? Lengo langu halisi la kufanya hili ni lipi?” Ikiwa unataka kumpa Mungu moyo wako lazima kwanza uuhini moyo wako, uachane na nia zako zote, na ufikie kiwango cha kuwa wa Mungu kwa ukamilifu. Hii ni njia ya kufanya mazoezi ya kumpa Mungu moyo wako. Kuuhini moyo wa mtu kunahusu nini? Ni kuachana na tamaa za kupita kiasi za mwili wa mtu, kutotamani baraka za cheo au kutamani starehe, kufanya kila kitu kumridhisha Mungu, na kwamba moyo wa mtu unaweza kuwa Wake kwa ukamilifu, sio kwa ajili ya mtu mwenyewe. Hivyo ndivyo ilivyo.

Upendo halisi kwa Mungu hutoka ndani ya kina cha moyo; ni upendo uliopo tu kwa msingi wa wanadamu kumfahamu Mungu. Moyo wa mtu unapomgeukia Mungu kwa ukamilifu basi ana upendo kwa Mungu, lakini upendo huo sio lazima uwe takatifu na sio lazima uwe kamili. Hii ni kwa sababu kuna umbali fulani kati ya moyo wa mtu kumgeukia Mungu kwa ukamilifu na mtu huyo kuwa na ufahamu halisi wa Mungu na kuabudu kihalisi Kwake. Njia ya mtu kutimiza upendo wa kweli kwa Mungu na kujua tabia ya Mungu ni kuurudisha moyo wake kwa Mungu. Baada ya kutoa moyo wao wa kweli kwa Mungu, wataanza kuingia katika uzoefu wa maisha, na hivyo tabia yao itaanza kubadilika, upendo wao kwa Mungu utakua polepole, na ufahamu wao wa Mungu utaongezeka pia polepole. Kwa hivyo kuurudisha moyo wa mtu kwa Mungu ni sharti la mwanzo la kuingia katika njia sahihi ya uzoefu wa maisha. Watu wanapoweka mioyo yao mbele ya Mungu, wao huwa tu na moyo wa kumtamani Yeye lakini sio wa kumpenda Yeye, kwa sababu hawana ufahamu kumhusu Yeye. Hata ingawa katika hali hii wana upendo fulani Kwake, si wa hiari na si halisi. Hii ni kwa sababu chochote kitokacho kwa mwili wa mwanadamu ni athari ya kihisia na hakitoki kwa ufahamu halisi. Ni msukumo wa muda mfupi tu na hakiwezi kuwa ibada ya kudumu. Watu wasipokuwa na ufahamu wa Mungu wanaweza tu kumpenda Yeye kulingana na upendeleo wao wenyewe na fikira zao binafsi; aina hiyo ya upendo haiwezi kuitwa upendo wa hiari, wala haiwezi kuitwa upendo halisi. Moyo wa mtu ukimrudia Mungu kwa uhalisi, anaweza kufikiria juu ya maslahi ya Mungu katika kila kitu, lakini ikiwa hana ufahamu wowote wa Mungu, hana uwezo wa kuwa na upendo wa hiari kwa uhalisi. Yote anayoweza kufanya ni kutimiza kazi fulani za kanisa na kutekeleza wajibu wake mdogo, lakini hauna msingi. Mtu wa aina hiyo ana tabia ambayo ni ngumu kubadilisha; wao wote ni watu ambao ama hawaufuatilii ukweli, au hawauelewi. Hata mtu akiurudisha kabisa moyo wake kwa Mungu haimaanishi kwamba moyo wake wa upendo kwa Mungu ni safi kabisa, kwa sababu wale walio na Mungu ndani ya mioyo yao sio lazima kwamba wanao upendo ndani ya mioyo yao kwa Mungu. Hili linahusu utofautishaji kati ya mtu anayefuatilia au asiyefuatilia ufahamu wa Mungu. Mara tu mtu anapokuwa na ufahamu wa Yeye, inaonyesha kwamba moyo wake umemrudia Mungu kwa ukamilifu, inaonyesha kwamba upendo wake halisi kwa Mungu ndani ya moyo wake ni wa hiari. Mtu wa aina hiyo pekee ndiye ana Mungu ndani ya moyo wake. Kugeuza moyo wa mtu kwa Mungu ni sharti la mwanzo la yeye kuingia katika njia sahihi, la kumfahamu Mungu, na la kutimiza upendo wa Mungu. Siyo alama ya kukamilisha wajibu wake ya kumpenda Mungu, wala siyo alama ya kuwa na upendo halisi Kwake. Njia ya pekee ya mtu kutimiza upendo halisi kwa Mungu ni kuurudisha moyo wake kwa Mungu, ambacho pia ni kitu cha kwanza mmoja wa uumbaji Wake anapaswa kufanya. Wale wanaompenda Mungu wote ni watu wanaotafuta uzima, yaani, watu wanaofuatilia ukweli na watu wanaomtaka Mungu kweli; wote wana nuru ya Roho Mtakatifu na wamesisimuliwa n na Yeye. Wote wanaweza kuongozwa na Mungu.

Mtu anapoweza kuhisi kwamba ni mdeni wa Mungu ni kwa sababu amesisimuliwa na Roho; akihisi hivyo basi ataelekea kuwa na moyo wa kutamani na ataweza kufuatilia kuingia katika maisha. Lakini ukiachia katika hatua fulani, hutaweza kuingia ndani zaidi; bado kuna hatari kubwa ya kukwama katika wavu wa Shetani, na ikifikia kiwango fulani utatekwa nyara na Shetani. Mwangaza wa Mungu huwaruhusu watu kujijua na baadaye kuhisi kuwa kwao na deni kwa Mungu pamoja na kuwa radhi kushirikiana naye na kutupilia mbali mambo yasiyomfurahisha Yeye. Hii ni kanuni ya kazi ya Mungu. Nyote mko radhi kufuatilia kukua katika maisha yenu na kumpenda Mungu, kwa hiyo umejiondolea njia zako za kubabiababia? Ukijiondolea njia hizo tu na usisababishe vurugu yoyote au kujionyesha, hiyo kweli ni kufuatilia kukua katika maisha yako? Ikiwa huna mienendo yoyote ya juujuu lakini huingii katika maneno ya Mungu, inamaanisha kwamba wewe ni mtu asiye na maendeleo yoyote ya utendaji. Ni nini mzizi wa kutwaa mwenendo wa juujuu? Je, matendo yako ni kwa ajili ya kukua katika maisha yako? Unafuatilia kustahili kuwa mmoja wa watu wa Mungu? Chochote kile unacholenga ndicho utakachoishi kwa kudhihirisha; ukilenga njia za juujuu basi moyo wako unalenga nje, na hutakuwa na njia ya kufuatilia kukua katika maisha yako. Mungu anataka mabadiliko katika tabia, lakini kila mara unafuatilia mambo ya nje; mtu wa aina hii hatakuwa na njia ya kubadilisha tabia yake! Kila mtu ana njia fulani kabla ya kukomaa katika maisha yake, ambayo ni kuwa lazima akubali hukumu, kuadibu, na kukamilishwa kwa maneno ya Mungu. Ikiwa huna maneno ya Mungu lakini unategemea tu kujiamini kwako na nia, kila kitu ufanyacho kinategemea ari. Yaani, ikiwa unataka ukuaji katika maisha yako lazima ule na kunywa, na ufahamu zaidi maneno ya Mungu. Wote wanaofanywa wakamilifu na maneno Yake wanaweza kuishi kwa kuyadhihirisha; wale wasiopitia usafishaji wa maneno Yake, wasiopitia hukumu ya maneno Yake hawawezi kufaa kwa matumizi Yake. Kwa hiyo mnaishi kwa kudhihirisha maneno Yake kwa kiwango gani? Mkila na kunywa tu maneno ya Mungu na muweze kuyalinganisha kwa hali yenu ya maisha, na kupata njia ya kutenda kwa kuzingatia masuala ninayotaja ndipo kutenda kwenu kutakuwa sahihi. Pia kutakuwa kwa kuupendeza moyo wa Mungu. Mtu aliye na aina hii ya kutenda pekee ndiye aliye na nia ya kumpenda Mungu.

Iliyotangulia: Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu

Inayofuata: Kuhusu Desturi ya Sala

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp