Sura ya 102

Nimeongea hadi kwa kiwango fulani na kufanya kazi hadi kwa kiwango fulani; ninyi nyote mnapaswa kuelewa mapenzi Yangu na kwa viwango tofauti muweze kuzingatia mzigo Wangu. Sasa ndicho kipindi muhimu kutoka katika mwili kuingia katika dunia ya roho, na ninyi ndio watangulizi kwa kutagaa enzi, watu wa ulimwengu wanaovuka ulimwengu na miisho ya dunia. Ninyi ni wapendwa Wangu zaidi; ninyi ndio Ninaowapenda. Inaweza kusemwa kwamba Sina wapendwa wengine ila ninyi, kwa sababu jitihada Yangu yote ya bidii imekuwa kwa ajili yenu—inaweza kuwa kwamba hamjui hilo? Kwa nini Niumbe vitu vyote? Kwa nini Nidhibiti vitu vyote ili kuwatumikia? Haya yote ni maonyesho ya upendo Wangu kwenu. Milima na vitu vyote milimani, dunia na vitu vyote duniani vinanisifu na kunitukuza kwa sababu Nimewapata ninyi. Kweli, kila kitu kimefanywa, na aidha, kila kitu kimefanyika kikamilifu. Mmekuwa na ushuhuda mkubwa sana kwa ajili Yangu na kufedhehesha ibilisi na Shetani kwa ajili Yangu. Watu, mambo, na vitu vyote nje Yangu vinatii mamlaka Yangu, na vyote, kwa sababu ya ukamilisho wa mpango Wangu wa usimamizi, vinafuata aina yao (Watu Wangu ni Wangu, na aina ya Shetani wote wanaenda kwa ziwa la moto—wanaenda kwa shimo lisilo na mwisho, ambapo watalia milele na kuangamia daima). Ninapozungumza kuhusu “kuangamia” na “kutoka wakati huo kuendelea kuchukua roho, nafsi na miili yao,” Ninarejelea kuwakabidhi kwa Shetani na kuwaruhusu kukanyagwa. Kwa maneno mengine, wote wasio wa nyumba Yangu watakuwa walengwa wa maangamizo na hawatakuwepo tena. Hili silo, kama wanavyofikiri watu, kwamba wataondoka. Na pia inaweza kusemwa kwamba kila kitu nje ya Mimi, kwa maoni Yangu, hakipo, ambayo ndiyo maana ya kweli ya kuangamia milele. Kwa macho ya wanadamu wanaonekana kuwepo bado, lakini katika maoni Yangu wamekuwa bure na wataangamia milele. (Mkazo uko kwa yeyote ambaye Sifanyii kazi tena na ambaye yuko nje ya Mimi.) Kwa wanadamu, bila kujali jinsi wanavyofikiri, hawawezi kuelewa hili, na bila kujali jinsi wanavyoona, hawawezi kulipenya. Hakuna mtu anayeweza kuelewa kwa wazi isipokuwa Nimpe nuru, Nimpe mwangaza, na kulionyesha kwa wazi. Aidha, watu wote watakuwa na wasiwasi zaidi na zaidi kulihusu, watahisi watupu hata zaidi, na watahisi kwa kuongeza kwamba hakuna njia ya kufuata—wao karibu ni kama wafu. Sasa hivi watu wengi (kumaanisha watu wote isipokuwa wazaliwa wa kwanza) wako katika hali hii. Nasema mambo haya kwa wazi sana na watu hawa hawana mjibizo mdogo na bado wanajali kuhusu raha zao za kimwili—wanakula na kisha kulala; wanalala na kisha wanakula, na hawatafakari maneno Yangu. Hata kama wamechangamshwa, itakuwa kwa muda tu, na baadaye watabaki vile vile walivyokuwa, wasibadilike kabisa, kana kwamba hawakunisikiza hata kidogo. Hawa ndio mfano hasa wa binadamu wasiojali wajibu ambao hawana mizigo—wasio na kazi dhahiri kabisa. Baadaye, Nitawatelekeza mmoja mmoja. Msijali! Nitawarudisha mmoja mmoja kwenye shimo lisilo na mwisho. Roho Mtakatifu hajawahi kuwashughulikia watu kama hawa, na kila kitu waanachokifanya kinatokana na uwezo walioupokea. Ninapozungumza kuhusu hizi nyezo, Namaanisha kwamba huyu ni mtu asiye na uzima, ambaye ni mtendaji huduma Wangu. Simtaki yeyote kati yao na Nitawaondoa (lakini sasa hivi bado ana manufaa kiasi). Ninyi ambao ni watendaji huduma, sikizeni! Usifikiri kwamba Mimi kukutumia kunamaanisha kwamba Ninakupendelea. Si rahisi hivyo. Kama unataka Nikupendelee, lazima uwe mtu Nitakayemwidhinisha na lazima uwe mtu ambaye Nitamkamilisha binafsi. Huyu ni aina ya mtu ambaye Ninampenda. Hata kama watu wanasema Nimekosea, Sitawahi kuvunja ahadi. Unajua? Wale wanaotoa huduma ni ng’ombe na farasi. Wanawezaje kuwa wazaliwa Wangu wa kwanza? Hilo halitakuwa upuuzi? Huo hautakuwa ukiukaji wa sheria za asili? Yeyote aliye na uzima Wangu, ubora Wangu, wao ndio wazaliwa Wangu wa kwanza. Hili ni jambo la busara—hakuna mtu anayeweza kulikana. Lazima liwe hivyo, vinginevyo hakungekuwa na mtu ambaye angeweza kufanya wajibu huo, hakuna mtu ambaye angeweza kuchukua nafasi yake. Hili silo jambo la kutendewa kulingana na hisia, kwa kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe mwenye haki; Mimi ndiye Mungu mtakatifu Mwenyewe; Mimi ni Mungu mwenye uadhama, asiyekosewa Mwenyewe!

Yote ambayo hayawezekani kwa wanadamu yanaenda taratibu na kwa uhuru Kwangu. Hakuna anayeweza kulikomesha na hakuna mtu anayeweza kulibadili. Dunia kubwa kama hii yote iko mikononi Mwangu, sembuse Shetani mdogo ibilisi. Isingekuwa kwa sababu ya mpango Wangu wa usimamizi, na isingekuwa kwa sababu ya wazaliwa Wangu wa kwanza, Ningekuwa nimeiharibu kitambo enzi hii nzee, ovu na zinzi ambayo imeenea harufu mbaya ya kifo. Lakini Natenda kwa utaratibu na Sizungumzi juu juu. Punde Ninapoongea litakamilishwa; hata kama hili halingekuwa hivyo, kuna kipengele cha hekima Yangu, ambacho kitakamilisha kila kitu kwa ajili Yangu na kufungulia matendo Yangu njia. Kwa kuwa maneno Yangu ni hekima Yangu; maneno Yangu ni kila kitu. Watu wanakosa kuyaelewa kimsingi na hawawezi kuyafahamu. Mara nyingi Ninarejelea “ziwa la moto.” Hili linamaanisha nini? Linatofautiana vipi na ziwa la moto na kibiriti? Ziwa la moto na kibiriti linarejelea ushawishi wa Shetani, na ziwa la moto linarejelea dunia nzima chini ya miliki ya Shetani. Kila mtu duniani ni wenye uelekeo wa kutolewa kafara katika ziwa la moto (yaani, wanazidi kuwa wapotovu na, upotovu wao unapofika kiwango fulani, wataangamizwa na Mimi mmoja mmoja, ambalo ni rahisi Kwangu kufanya kwa neno Langu moja pekee). Kadiri ghadhabu Yangu ilivyo kubwa, ndivyo moto mkali unavyokuwa mkubwa zaidi kotekote katika ziwa la moto. Hili linarejelea watu kuwa waovu zaidi na zaidi. Wakati huu ambapo ghadhabu Yangu inaripuka ndio pia utakuwa wakati ambapo ziwa la moto linalipuka; yaani, utakuwa wakati ambapo ulimwengu dunia mzima unaangamia. Siku hiyo ufalme Wangu utapatikana kikamilifu duniani na maisha mapya yataanza. Hiki ni kitu ambacho kitatimizwa karibuni. Kwa kuwa Ninazungumza, kila kitu kitatimizwa papo hapo. Huo ndio mtazamo wa binadamu wa suala hilo, lakini katika mtazamo Wangu vitu vimekamilishwa mapema kwa sababu Kwangu kila kitu ni rahisi. Nasema na kinafanywa; Nasema na kinaanzishwa.

Kila siku mnakula maneno Yangu; mnafurahia wingi ulio katika hekalu Langu; mnakunywa maji kutoka kwa mto Wangu wa uzima; mnachuma tunda kutoka mti Wangu wa uhai. Basi, wingi katika hekalu Langu ni nini? Maji ya mto Wangu wa uzima ni nini? Mti wa uzima ni nini? Tunda la mti wa uzima ni nini? Virai hivi vya kawaida havieleweki hata hivyo kwa binadamu wote, ambao wamechanganyikiwa wote, wakivisema kwa njia isiyopaswa, wakivitumia kwa kutojali, na kuvitumia bila mpango maalum. Wingi katika hekalu haumaanishi maneno ambayo Nimezungumza au neema ambayo Nimewapa. Kwa hivyo, hata hivyo, unamaanisha nini? Tangu nyakati za zamani hakujawahi kuwa na mtu yeyote ambaye ana bahati kufurahia wingi katika hekalu Langu. Ni katika siku za mwisho tu, miongoni mwa wazaliwa Wangu wa kwanza, ndipo watu wanaweza kuona wingi katika hekalu Langu ni nini. “Hekalu” linalozungumziwa katika “wingi katika hekalu Langu” ni nafsi Yangu, likirejelea Mlima Sayuni, makao Yangu. Bila ruhusa Yangu hakuna mtu anayeweza kuliingia au kuliondoka. Je, “wingi” huu unamaanisha nini? Wingi unamaanisha baraka za kutawala pamoja na Mimi katika mwili. Kuzungumza kwa jumla, hili linamaanisha baraka za wazaliwa wa kwanza kutawala na Mimi katika mwili, na hili si gumu kuelewa. Maji ya mto wa uzima una maana mbili: Kwa upande mmoja unarejelea maji hai yanayotiririka kutoka kwa nafsi Yangu ya ndani sana, yaani, kila neno linalotoka katika kinywa Changu. Kwa upande mwingine, unarejelea hekima na maarifa ya matendo Yangu, na vile vile kile Nilicho na ninacho. Katika maneno Yangu kuna siri nyingi, zilizofichwa (kwamba siri hazifichwi tena kunazungumziwa kinyume na zamani, lakini kukilinganishwa na ufunuo wa umma katika siku ijayo, bado zimefichwa. Hapa, “kufichwa” si kamili, badala yake linategemea uhusiano), ambayo ni kusema kwamba maji ya mto wa uzima yanatiririka wakati wote. Ndani Yangu kuna hekima isiyo na kikomo, na watu hawawezi kuelewa kabisa kile Nilicho na ninacho hata kidogo; yaani, maji ya mto wa uzima yanatiririka milele. Katika mtazamo wa binadamu kuna aina nyingi za miti yakinifu, lakini hakuna mtu ambaye amewahi kuona mti wa uzima. Hata hivyo, licha ya kuiona leo, watu bado hawaitambui—na bado hata wanazungumza kuhusu kula kutoka kwenye mti wa uzima. Hakika huu ni upuuzi kweli! Wangekula kwa mti huu bila mpango! Kwa nini Nasema leo watu wanauona lakini hawautambui? Kwa nini Nasema hivyo? Je, unaelewa maana ya maneno Yangu? Mungu wa vitendo Mwenyewe wa leo ni mtu Niliye, na Yeye ndiye mti wa uzima. Usitumie dhana za binadamu kunipima—kutoka nje Sifanani na mti, lakini unajua kwamba Mimi ndio mti wa uzima? Kila tendo Langu, usemi na tabia Yangu, ni tunda la mti wa uzima, na ni nafsi Yangu—hayo ndiyo ambayo wazaliwa Wangu wa kwanza wanapaswa kula, kwa hivyo hatimaye ni Mimi na wazaliwa Wangu wa kwanza pekee ndio tutakuwa sawa hasa. Wataweza kuishi kwa kunidhihirisha na wataweza kunishuhudia. (Haya ni mambo yanayofanyika baada ya sisi kuingia katika dunia ya roho. Ni katika mwili tu ndiyo tunaweza kuwa sawa kabisa; katika nyama tunaweza kuwa takribani sawa, lakini bado tuna aina zetu wenyewe).

Sionyeshi tu nguvu Yangu katika wazaliwa Wangu wa kwanza pekee, lakini pia Nitaonyesha nguvu Yangu kwa uongozi wa wazaliwa Wangu wa kwanza wa mataifa yote na watu wote. Hii ni hatua ya kazi Yangu. Sasa ndio wakati wa maana, na sasa ni kipindi muhimu hata zaidi. Wakati ambapo kila kitu kinakamilishwa, mtaona ni nini ambacho mikono Yangu inafanyia kazi, na mtaona Ninavyopanga na Ninavyosimamia, lakini hili si jambo lisilo yakini. Kulingana na elimumwendo ya kila nchi duniani, si tofauti sana; ni jambo ambalo watu hawawezi kulifikiria, na aidha, jambo ambalo hawawezi kuliona mbele. Ni lazima msiwe wazembe au wenye upurukushani hata kidogo ili msikose fursa ya kubarikiwa na kupewa zawadi. Matarajio ya ufalme yanaonekana na dunia nzima inakufa polepole. Kutoka kwa shimo lisilo na mwisho na kutoka kwa ziwa la moto na kibiriti kunatokea sauti kubwa za milio, zikiwaogofya watu na kuwafanya kuhisi kuogopa na kuaibika. Yeyote anayechaguliwa kwa jina Langu na kisha kuondolewa atakuwa katika shimo lisilo na mwisho. Kwa hivyo Nimesema nyakati nyingi, Nitarusha walengwa wa kuangamizwa ndani ya shimo lisilo na mwisho. Wakati ambapo dunia yote imeharibiwa kila kitu ambacho kimeharibiwa kitaenda katika ziwa la moto na kibiriti—yaani, kitahamishwa kutoka katika ziwa la moto hadi kwenye ziwa la moto na kibiriti. Wakati huo kila mtu atakuwa ameamuliwa kuangamizwa milele (kumaanisha wote ambao wako nje ya Mimi) au kupata uzima wa milele (kumaanisha wale wote ambao wako ndani ya Mimi). Wakati huo Mimi na wazaliwa Wangu wa kwanza tutaibuka kutoka kwa ufalme na kuingia katika uzima. Hili ni jambo ambalo litatimizwa baadaye, na hata Nikiwaambia sasa, hamtaelewa. Mnaweza tu kufuata mwongozo Wangu, mtembee katika mwanga Wangu, kuambatana nami katika upendo Wangu, kufurahia nami katika nyumba Yangu, kutawala nami katika ufalme Wangu, na kuwa na kutawala nami juu ya mataifa yote na watu wote katika mamlaka Yangu. Kile ambacho Nimesema hapo juu ni baraka zisizoisha ambazo Ninawapa.

Iliyotangulia: Sura ya 101

Inayofuata: Sura ya 103

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp