Sura ya 36

Kila kitu kinapangwa kwa mkono Wangu. Nani anathubutu kufanya anavyopenda? Nani anayeweza kukibadilisha kwa urahisi? Watu huelea hewani, wakienda mbele kama vumbi linavyokwenda, nyuso zao zikiwa zimejaa uchafu, kuwafanya wasivutie kutoka utosini hadi wayoni. Mimi huangalia kutoka miongoni mwa mawingu kwa moyo mzito: Kwa nini mwanadamu, ambaye wakati mmoja alijaa uhai, alibadilika na kuwa sura hii? Na kwa nini hajui jambo hili, na kutohisi jambo hili? Kwa nini "anajiachilia" na kujiruhusu kufunikwa kwa uchafu? Huo ndio ukosefu wa kujipenda na kujiheshimu. Kwa nini mwanadamu daima huepuka Ninachouliza? Je, Mimi ni mkatili na mnyama kwake kweli? Je, Mimi kweli ni dhalimu na Asiye na huruma? Hivyo kwa nini watu daima hunitazama kwa macho makali? Kwa nini daima wao hunichukia? Je, Nimewaleta mpaka ukingoni? Mwanadamu hajawahi kugundua chochote katika kuadibu Kwangu, kwani hafanyi chochote ila kushika nira inayolizunguka shingo lake kwa mikono miwili, macho yake mawili yakiwa yamekodolewa Kwangu, kana kwamba anamwangalia adui kwa makini—na wakati huu tu ndio Nahisi vile amedhoofishwa. Ni kwa sababu ya hili ndio Nasema hakuna yeyote aliyewahi kusimama imara katikati ya majaribio. Je, kimo cha mwanadamu hakiko hivyo kabisa? Je, ananihitaji Nimwambie tarakimu za "vipimo" vyake? "Urefu" wa mwanadamu sio mkubwa zaidi kuliko ule wa mnyoo mdogo anayejinyonganyonga juu ya ardhi, na "kifua" chake kina upana sawa tu na wa nyoka. Katika hili, mimi Simdunishi mwanadamu—je, hizi sizo tarakimu kamili za kimo chake? Je, Nimemshusha daraja mwanadamu? Mwanadamu ni kama mtoto anayechezacheza. Kuna hata nyakati ambapo anacheza na wanyama, lakini bado anabaki na furaha; na yeye ni kama paka, akiishi maisha bila kujali au wasiwasi. Labda ni kwa sababu ya mwelekeo wa Roho, au jukumu la Mungu mbinguni, ndio Najisikia mchovu sana kuhusu maisha ya ubadhirifu ya watu duniani. Kwa sababu ya maisha ya mwanadamu—ambayo ni kama ya kimelea—"Shauku" Yangu katika maneno "maisha ya binadamu" imeongezeka kwa kiasi fulani, na hivyo Nimekuwa "mwingi wa heshima" zaidi kidogo kwa maisha ya binadamu. Kwa maana inaonekana kwamba mwanadamu pekee ndiye anaweza kuunda maisha ambayo yana maana, wakati ambapo Siwezi kufanya hivi. Kwa hivyo Naweza tu kwenda kwenye "milima," kwa maana Siwezi kupitia na kuchunguza shida miongoni mwa wanadamu. Lakini mwanadamu ananishurutisha—Sina budi! Ninaweza tu kutii mipango ya mwanadamu, kufupisha uzoefu pamoja naye na kupitia maisha ya binadamu pamoja naye. Mbinguni, wakati mmoja Nilitalii jiji lote, na chini ya mbingu, wakati mmoja Nilitalii nchi zote. Lakini hakuna mtu aliyewahi kunitambua, walisikia tu sauti ya mwendo Wangu Nilipokuwa Nikitembea kote. Machoni pa watu, Mimi huja na kwenda Nisionekane tena. Ni kana kwamba Nimekuwa sanamu isiyoonekana ndani ya mioyo yao, lakini watu hawaamini hivyo. Yawezekana kuwa yote haya si ukweli uliokiriwa na kinywa cha mwanadamu? Wakati huu, ni nani asiyekubali kwamba anapaswa kuadibiwa? Je, watu bado wangejiamini kabla ya ushahidi thabiti?

Nafanya mapatano ya biashara miongoni mwa wanadamu, Naufuta uchafu na udhalimu wake wote, na hivyo "Namtengeneza" ili apate kuupendeza moyo Wangu. Lakini ushirikiano wa mwanadamu ni wa lazima kwa hatua hii ya kazi, kwa sababu yeye daima huchupa na kuruka kote kama samaki ambaye amevuliwa hivi sasa. Kwa hiyo, ili kuzuia ajali zozote, Niliwaua samaki wote waliokuwa wamevuliwa, baada ya hilo samaki hao wakawa watiifu, na hawakuwa na malalamiko hata kidogo. Ninapomhitaji mwanadamu, daima huwa amejificha. Ni kana kwamba hajawahi kuona mandhari ya kustaajabisha, kana kwamba alizaliwa mashambani na hajui chochote kuhusu mambo ya mjini. Naongeza hekima Yangu kwa sehemu za mwanadamu ambazo zina upungufu, na kumfanya anijue Mimi; kwa sababu mwanadamu ni maskini sana, Mimi binafsi huja miongoni mwa wanadamu na kumpa "njia ya kupata utajiri," na kumfanya afumbue macho yake. Katika hili, je, Simwokoi? Je, hii si huruma Yangu kwa mwanadamu? Je, upendo ni kutoa bila masharti? Je, kuadibu ni chuki tu? Nimemwelezea mwanadamu kutoka kwa taswira tofauti, lakini analichukulia hili kama maneno na kanuni tu. Ni kana kwamba maneno Yangu ni bidhaa za daraja la pili, ambazo huuzwa kama vitu visivyo na thamani tena katika mikono ya mwanadamu. Hivyo, wakati Ninapowaambia watu kuwa dhoruba kubwa inakuja kumeza kijiji cha mlima, hakuna mtu anayefikiri chochote juu yake, ni wachache tu wanaohamia nyumba zingine, mioyo yao ikiwa na shaka. Wengine hawahami, kana kwamba hawajali, kana kwamba Mimi ni mbayuwayu kutoka angani—hawaelewi chochote kati ya yale Nisemayo. Ni wakati ambapo tu milima hupinduliwa na dunia kutenganishwa mbalimbali ndipo watu hufikiria kuhusu maneno Yangu, wakati huo tu ndio wao huamshwa kutoka kwa ndoto zao, lakini wakati umefika tayari, wamemezwa katika mafuriko makuu, maiti yao ikielea juu ya maji. Nionapo taabu ulimwenguni, Nashusha pumzi kwa msiba wa mwanadamu. Nilitumia muda mwingi, na kulipa gharama kubwa, kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu. Katika mawazo ya watu, Sina michirizi ya machozi—lakini Mimi, "dubwasha" huyu asiye na michirizi ya machozi, Nimelia machozi mengi kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu, hata hivyo, hajui lolote kuhusu hili, anacheza tu na vidude vya kuchezea watoto mikononi mwake duniani, kana kwamba Siishi. Hivyo, katika hali za leo, watu hubakia sugu na wajinga, bado "wameganda" katika sehemu za nyumba zilizo chini ya ardhi, kana kwamba bado wanalala pangoni. Nionapo vitendo vya mwanadamu, chaguo Langu la pekee ni kuondoka ...

Machoni pa watu, Nimefanya mengi ambayo ni mazuri kwa mwanadamu, na hivyo wananitazama kama mfano mwema wa enzi ya sasa. Lakini hawajawahi kunifikiria kama Mtawala wa majaliwa ya mwanadamu na Muumba wa vitu vyote. Ni kana kwamba hawanielewi. Ingawa wakati fulani watu walitangaza "Ufahamu udumu,' hakuna yeyote ambaye ametumia muda mwingi kuchambua neno ‘ufahamu,’ kuonyesha kwamba watu hawana hamu ya kunipenda. Katika nyakati za leo, watu hawajawahi kunithamini, Sina nafasi ndani ya mioyo yao. Je, wataweza kuonyesha upendo wa kweli Kwangu katika siku zijazo za mateso? Haki ya mwanadamu inabaki kitu bila umbo, kitu ambacho hakiwezi kuonekana wala kuguswa. Nitakacho ni moyo wa mwanadamu, kwa kuwa katika mwili wa mwanadamu moyo ndio wa thamani sana. Je, matendo Yangu hayafai kulipwa kwa moyo wa mwanadamu? Kwa nini watu hawanipi mioyo yao? Kwa nini daima huikumbatia kwa vifua vyao wenyewe, wasitake kuiwacha? Je, moyo wa mwanadamu unaweza kuhakikisha amani na furaha katika maisha yote ya watu? Kwa nini, wakati Ninapotaka vitu kutoka kwa watu, wao daima hunyakua kiasi kidogo cha vumbi kutoka ardhini na kulirusha Kwangu? Je, huu ni mpango wa hila wa mwanadamu? Ni kana kwamba anajaribu kumdanganya mpita njia ambaye hana mahali popote pa kwenda, akimshawishi arudi nyumbani kwake, ambapo anageuka na kuwa mbaya na kumuua. Watu wametaka pia kufanya mambo kama hayo Kwangu. Ni kana kwamba yeye ni chakari ambaye atamuua mtu bila kujali, kana kwamba yeye ni mfalme wa pepo, ambaye asili yake ya pili ni kuwaua watu. Lakini sasa watu huja mbele Yangu, bado wakitaka kutumia njia hizo—lakini wana mipango yao, nami Nina mipango Yangu ya kupinga. Ingawa watu hawanipendi, Ningewezaje kukosa kuifanya mipango yangu ya kupinga wazi kwa mwanadamu wakati huu? Nina ujuzi usio na kikomo, usiopimika katika kumshughulikia mwanadamu; kila sehemu yake hushughulikiwa binafsi na Mimi, na kutengenezwa na Mimi binafsi. Hatimaye, Nitamfanya mwanadamu avumilie maumivu ya kujitenga na kile anachopenda, na kumfanya atii mipango Yangu, na wakati huo, watu watalalamikia nini? Je, yote Nifanyayo si kwa ajili ya mwanadamu? Katika nyakati zilizopita, Sikuwahi kumwambia mwanadamu hatua za kazi Yangu—lakini leo, katika wakati usiofanana na uliopita, kwa sababu maudhui ya kazi Yangu ni tofauti, Nimewaambia watu juu ya kazi Yangu mapema ili kuwazuia kuanguka chini kutokana na hili. Je, hii siyo chanjo ambayo Nimeidunga sindano ndani ya mwanadamu? Kwa sababu yoyote ile, watu hawajawahi kuzingatia maneno Yangu kwa makini; ni kana kwamba kuna njaa ndani ya matumbo yao na hawachagui kile wanachokula, ambacho kimefanya matumbo yao kuwa dhaifu. Lakini watu huchukua "gimba yao bora" kuwa rasilimali na hawatambui maonyo ya "daktari." Ninapoona ukaidi wao, Najikuta Nikisikitika kwa ajili ya mwanadamu. Kwa sababu watu ni wadogo sana, na bado hawana uzoefu wa maisha ya binadamu, hawana hofu; mioyoni mwao, maneno "maisha ya binadamu" hayapo, hawayajali, na hudharau maneno Yangu tu, kana kwamba Nimekuwa mwanamke mzee mwenye kuparaganyaparaganya. Kwa jumla, kwa vyovyote vile, Natumaini kwamba watu wanaweza kuuelewa moyo Wangu, kwa maana Mimi Sina hamu ya kumtuma mwanadamu katika nchi ya kifo. Natumaini kwamba mwanadamu anaweza kuelewa hisia Zangu ni zipi kwa wakati huu, na kuujali mzigo Ninaobeba hasa wakati huu.

Aprili 26, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 35

Inayofuata: Sura ya 37

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Njia …(6)

Tumeletwa hadi siku ya leo kwa sababu ya kazi ya Mungu, na kwa hiyo sisi ndio waliosalia katika mpango wa Mungu wa usimamizi. Kwamba...

Utangulizi

“Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima” ni sehemu ya pili ya matamshi yaliyoonyeshwa na Kristo. Ndani ya sehemu hii, Kristo Anatumia...

Hitimisho

Ijapokuwa maneno haya yote si maonyesho ya Mungu, yanatosha kwa ajili ya watu kutimiza makusudi ya kumjua Mungu na badiliko katika tabia....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki