Hitimisho
Ingawa maneno haya si maonyesho yote ya Mungu, yanatosha kwa watu kufikia malengo ya kumjua Mungu na mabadiliko ya tabia. Labda kuna wengine ambao wanafikiri kuwa kwa sababu kazi ya Mungu katika bara la China imekwisha, hili linathibitisha kuwa Amemaliza kutamka maneno yote ambayo Anapaswa kutamka, na kwamba hawezi kamwe kuwa na matamshi mapya kwani haya ndiyo maneno ambayo Mungu anaweza kunena. Zaidi ya hayo, kuna watu wanaoamini kuwa Neno Laonekana katika Mwili linajumuisha maonyesho yote ya Mungu katika Enzi ya Ufalme, na kwamba kupokea kitabu hiki ni sawa na kupokea kila kilicho cha Mungu, au kwamba kitabu hiki kitawaongoza wanadamu katika siku za usoni kama ilivyofanya Biblia. Ninaamini kwamba watu wanaoshikilia mitazamo hii si wachache, kwa kuwa watu daima wanapenda kumwekea Mungu mipaka. Ingawa wote wanatangaza kwamba Mungu ni muweza wa yote na anajumuisha yote, asili ya watu bado inawafanya iwe rahisi kwao kumwekea Mungu mipaka ndani ya mawanda fulani. Wakati huo huo ambapo kila mtu anapata kumjua Mungu, wao pia wanampinga na kumwekea mipaka.
Kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme ndiyo tu imeanza. Matamshi yote ya Mungu katika kitabu hiki yalilengwa tu kwa wale waliomfuata wakati huo, na ni sehemu tu ya maonyesho ya Mungu katika kupata mwili Kwake kwa sasa, na hayawakilishi kila kitu cha Mungu. Zaidi ya hayo, haiwezi kusemwa kuwa inajumuisha kazi yote ambayo Mungu atafanya akiwa katika mwili huu wa sasa. Mungu atayalenga maneno Yake kwa watu wa makabila na asili tofauti, na Atawashinda wanadamu wote na kuitamatisha enzi ya zamani, hivyo basi Angekamilisha vipi baada ya kuonyesha sehemu ndogo kama hiyo ya maneno Yake? Ni kwamba tu kazi ya Mungu imegawanywa katika vipindi tofauti tofauti vya wakati na hatua tofauti tofauti. Anafanya kazi kulingana na mpango Wake na kuonyesha maneno Yake kulingana na hatua Zake. Ni vipi mwanadamu angeweza kuelewa kudura na busara za Mungu? Ukweli Ninaoufafanua hapa ni huu: Kile Mungu alicho na anacho milele hakiishi wala hakina mipaka. Mungu ni chanzo cha uhai na vitu vyote. Mungu hawezi kueleweka na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Mwishowe, ni lazima bado Nimkumbushe kila mtu: Msimwekee Mungu mipaka katika vitabu, maneno, au tena katika matamshi Yake yaliyopita. Kuna neno moja tu kwa sifa ya kazi ya Mungu—mpya. Hapendi kuchukua njia za zamani au kurudia kazi Yake, na zaidi ya hayo Hapendi watu kumwabudu kwa kumwekea mipaka katika upeo fulani. Hii ndiyo tabia ya Mungu.