Kiambatisho 4: Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kama wale mamia ya mamilioni ya wengine wanaomfuata Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa pia wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri kwamba sisi pia tunajiamini kuwa kwenye njia ya kufanya mapenzi ya Baba aliye mbinguni. Tunatamani kurudi kwake Bwana Yesu, kushuka Kwake kwa utukufu, mwisho wa maisha yetu hapa duniani, kuonekana kwa ufalme, na kila kitu kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo: Bwana anafika, Analeta maafa, Anawazawadia walio wema na kuwaadhibu walio waovu, na Anawachukua wale wote wanaomfuata na kukaribisha kurudi Kwake juu kumlaki angani. Wakati wowote tunapowaza kuhusu haya, hatuwezi ila kujawa na hisia na kujawa na shukrani kwa kuwa tulizaliwa siku za mwisho na tuna bahati nzuri ya kushuhudia kuja kwake Bwana. Ingawa tumepitia mateso, tumepata badala yake “utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.” Baraka gani hii! Hamu hii yote, na neema inayopewa na Bwana hutufanya kuingia kwenye maombi kwa kawaida, na hutufanya waangalifu zaidi katika kukusanyika pamoja. Labda mwaka ujao, labda kesho, na tena, labda kwa muda mfupi zaidi kuliko binadamu anavyoweza kung’amua, Bwana ghafla atashuka, akionekana kati ya kundi la watu ambao wamekuwa wakimsubiri kwa faragha ya hamu. Tunaharakisha ili tuwe mbele ya wenzetu, hakuna anayetaka kubaki nyuma, yote kwa ajili ya kuwa kundi la kwanza la kutazama kuonekana kwa Bwana, ya kuwa miongoni mwa wale watakaonyakuliwa kwenda mbinguni. Tumetoa kila kitu, bila kujali gharama, kwa ajili ya kuwadia kwa siku hii, wengine wakiacha kazi zao, wengine wakiacha familia zao, wengine wakikana ndoa zao, na baadhi hata wakipeana akiba zao zote. Ni vitendo vya upendo usio na ubinafsi kweli! Uaminifu na utiifu kama huu bila shaka hata unashinda ule wa watakatifu wa nyakati za zamani! Kwa kuwa Bwana anampa neema yeyote yule ambaye Yeye anataka, na kumwonyesha huruma yeyote ambaye Yeye anataka, vitendo vyetu vya kujitolea na vya kutumia, tunaamini, vimetazamika machoni Pake kitambo. Kwa hivyo, pia, sala zetu za dhati zimefikia masikio Yake, na tunaamini kuwa Bwana atatulipa kwa ajili ya kujitolea kwetu. Aidha, Mungu alikuwa mwenye neema kwetu kabla hajauumba ulimwengu, na baraka na ahadi Ambazo ametupa hakuna anayeweza kuziondoa. Sote tunapanga kwa ajili ya siku za usoni, na bila shaka tumefanya kujitolea na kutumia kwetu kuwa vitu vya madai au raslimali ya kubadilishana kwa ajili ya kunyakuliwa kupatana na Bwana hewani. Kuongezea, bila kusita hata kidogo, sisi tumejiweka kwenye kiti cha enzi cha siku za baadaye, ili tutawale mataifa na watu wote kwa jumla, ama kutawala kama wafalme. Yote haya, sisi huchukulia kama jambo la lazima, kama kitu cha kutarajiwa.

Tunadharau wale wote walio kinyume na Bwana Yesu; wote wataishia kuangamizwa. Nani aliwaambia wasiamini kwamba Bwana Yesu ni Mwokozi? Bila shaka, kuna nyakati ambapo tunaiga Bwana Yesu katika kuwa na huruma kwa watu wa dunia, kwa kuwa hawaelewi, na ni sahihi kwamba tuwe wavumilivu na kuwasamehe. Kila kitu tufanyacho ni kwa mujibu wa maneno ya Biblia, kwani kila kitu ambacho hakifuatani na Biblia ni chenye kufuata imani tofauti na ni uzushi, Imani ya aina hii imekita mizizi katika akili ya kila mmoja wetu. Bwana wetu yumo katika Biblia, na tusipoondoka kwenye Biblia basi hatutaondoka kwa Bwana; tukitii kanuni hii, tutapata wokovu. Sisi huhimizana, kila akisaidia mwingine, na kila wakati tunapokusanyika pamoja ni matumaini yetu kwamba kila kitu tunachosema na kutenda kinaambatana na matakwa ya Bwana na kuwa kitabaliwa na Bwana. Licha ya uhasama mkali ulioko kwenye mazingira yetu, mioyo yetu imejaa furaha. Tunapowaza kuhusu baraka hizi tunazoweza kupata kwa urahisi, je, kuna kitu ambacho hatuwezi kukitenga kando? Je, kuna kitu ambacho hatuko tayari kuachana nacho? Yote haya hayapingwi, na haya yote yako chini ya macho angalifu ya Mungu. Sisi, walio wachache wa maskini ambao tumeinuliwa kutoka jaani, ni sawa tu na wafuasi wote wa Bwana Yesu wa kawaida tukiota kuhusu kunyakuliwa, na kubarikiwa, na kutawala mataifa yote. Upotovu wetu umeanikwa peupe machoni pa Mungu, na tamaa zetu na uchoyo zimehukumiwa machoni pa Mungu. Hata hivyo, yote haya hutokea bila ajabu kabisa, na tena yenye mantiki sana, na hakuna hata mmoja kati yetu ambaye hushangaa kama hamu zetu ni za haki, sembuse yeyote kati yetu ambaye anashuku usahihi wa yote yale ambayo sisi hushikilia. Nani anayeweza kujua mapenzi ya Mungu? Njia hii hasa ni gani ambayo binadamu hutembelea, hatujui jinsi ya kutafuta, au kuchunguza, sembuse kujishughulisha nayo. Kwa maana sisi hujali tu kuhusu kama tutaweza kunyakuliwa, kama tunaweza kubarikiwa, kama kuna pahali tumetengewa katika ufalme wa mbinguni, na kama sisi tutaweza kupata mgawo wa maji ya mto wa uzima na matunda ya mti wa uzima. Je, si ni kwa ajili ya kupata vitu hivi ndiyo tunamwamini Bwana na kuwa wafuasi Wake? Dhambi zetu zimesamehewa, tumetubu dhambi zetu, tumekunywa kikombe cha mvinyo ambao ni mchungu, na tumeuweka msalaba migongoni mwetu. Nani anayeweza kusema kuwa Bwana hatafurahi kukubali gharama ambayo tumelipia? Nani anayeweza kusema kuwa hatujatayarisha mafuta yanayotosha? Hatungependa kuwa wale mabikira wapumbavu, ama mmoja wa wale ambao wameachwa. Aidha, tunaomba mara kwa mara, tukimwomba Bwana atuepushe kutokana na kudanganywa na Kristo wa uongo, kwa maana imeandikwa kwenye Biblia: “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi” (Mathayo 24:23-24). Sisi sote tumeweka mistari hii ya Biblia kwenye kumbukumbu, tunaijua vyema sana, na tunaiona kama hazina ya thamani, kama hati ya muamana ambayo inaamua ikiwa tunaweza kuokolewa au kunyakuliwa …

Kwa maelfu ya miaka, wanaoishi wamefariki, wakichukua tamaa zao na ndoto zao, lakini kuhusu iwapo wameenda kwa ufalme wa mbinguni, hakuna ajuaye hakika. Wafu wanarudi, wakiwa wamesahau hadithi zote zilizowahi kutokea wakati mmoja, na bado wanafuata mafundisho na njia za babu zetu. Na kwa njia hii, miaka inavyopita na siku zinavyosonga, hakuna anayejua iwapo Bwana Yesu, Mungu wetu, kwa kweli hukubali yote tunayoyafanya. Yote tuwezayo kufanya ni kutarajia tu kuwa na matokeo na kubashiri kuhusu yale yote ambayo yatakuja kutokea. Bado Mungu yu kimya siku zote, kamwe asionekane kwetu, kamwe asiseme nasi. Na kwa hivyo, kwa kufuata Biblia na kulingana na ishara tunahukumu mapenzi na tabia ya Mungu kwa hiari yetu. Sisi tumezoea kimya cha Mungu; tumekuwa na mazoea ya kupima usahihi na makosa ya mwenendo wetu kwa kutumia njia zetu wenyewe za mawazo: tumekuwa na mazoea ya kutegemea elimu yetu, dhana, na maadili yetu badala ya matakwa anazotutolea Mungu; tumekuwa na mazoea ya kufurahia neema ya Mungu; tumekuwa na mazoea ya Mungu kutoa msaada wakati sisi tunahitaji msaada huo; tumekuwa na mazoea ya kunyosha mikono yetu kwa Mungu ili tupate mambo yote, na kumuagiza Mungu; na pia tumekuwa na mazoea ya kufuata kanuni, kutotilia maanani jinsi Roho Mtakatifu hutuongoza; na, hata zaidi, tumekuwa na mazoea ya siku ambazo sisi ni bwana zetu wenyewe. Tunamwamini Mungu wa namna hii, ambaye hatujawahi kukutana naye uso kwa uso. Maswali kama namna tabia Yake ilivyo, kile Anacho na Alicho, mfano Wake ulivyo, kama tutamjua ama hatutamjua wakati Atakaporudi, na kadhalika—haya yote hayana umuhimu. Jambo muhimu ni kuwa Yeye yumo mioyoni mwetu na kuwa tunamsubiri, na inatosha kuwa tunaweza kufikiria kwamba Yuko jinsi hii au jinsi ile. Tunathamini imani yetu, na kuthamini hali yetu ya kiroho. Tunaona kila kitu kikiwa kama samadi, na kukanyaga vitu vyote kwa nyayo zetu. Kwa sababu sisi ni wafuasi wa Bwana mwenye utukufu, bila kujali jinsi safari yetu ilivyo ndefu na ngumu, bila kujali shida na hatari zinazotukumba, hakuna kitu kitakachosimamisha nyayo zetu tunapomfuata Bwana. “Mto safi wa maji ya uhai, ung’aao kama kioo, uliondoka katika kiti cha Mungu cha enzi na cha Mwanakondoo. Na katika kila upande wa ule mto, ulikuwapo ule mti wa uhai unaozaa matunda ya jinsi kumi na mbili, na kuyatoa hayo matunda yake kila mwezi: na majani yake mti huu yalikuwa ya ajili ya kuyaponya mataifa. Na laana haitakuwepo tena: ila kiti cha Mungu cha enzi na cha Mwanakondoo kitakuwa ndani yake; na watumishi Wake watamhudumia: Na wao wataona uso Wake; nayo mapaji ya nyuso zao yatakuwa na jina Lake. Na hakutakuwa na usiku pale; wala hawahitaji mshumaa, wala mwanga wa jua; kwa sababu Bwana Mungu huwapa mwanga: na wao watatawala daima na milele” (Ufunuo 22:1-5). Kila wakati sisi hukariri maneno hayo, mioyo yetu hujawa na furaha isiyo na mipaka na maridhio, na machozi hutiririka kutoka machoni mwetu. Shukrani ni kwa Bwana kwa kutuchagua, shukrani ni kwa Bwana kwa neema Yake. Ametupa mara mia katika maisha haya, Yeye ametupa uzima wa milele kwa ulimwengu ujao. Kama Angetuomba tufe sasa, tungetii hiyo bila kusita hata kidogo. Ee Bwana! Tafadhali njoo hivi karibuni! Kwa kuwa sisi tunakutamani sana, na tumeacha kila kitu kwa ajili Yako, usikawie hata dakika moja, sekunde moja tena.

Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimama. Yeye huangalia dunia nzima, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Yeye huendesha usimamizi Wake kwa hatua zilizopimwa na kulingana na mpango Wake kwa kimya, na bila madhara ya kutia shauku, ilhali nyayo Zake hukaribia, moja baada ya nyingine, daima hukaribia binadamu, na kiti Chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, na baada yake kiti Chake cha enzi mara moja hushuka kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, tukio hilo ni mandhari ya adhimu na yenye taadhima! Kama njiwa, na kama simba anayenguruma, Roho huja kati yetu. Yeye ni hekima, Yeye ni haki na uadhama, na Yeye huja kwa ukimya kati yetu, akiwa na mamlaka na akiwa amejawa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuwasili Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote ambacho yuko karibu kufanya. Maisha ya mwanadamu yanaendelea kama awali moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu huishi kati yetu, mwanadamu kama watu wengine, kama mmoja wa wafuasi wasio na maana kabisa na kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na zaidi ya hayo, Ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila mipaka au kuogopa, kwa kuwa katika macho yetu, Yeye ni muumini asiye wa maana tu. Yeye huona matukio yetu yote, na fikra na mawazo yetu yote yanawekwa wazi mbele Yake. Hakuna mtu ambaye huwaza chochote kuhusu kazi Yake na isitoshe, hakuna aliye na shuku hata kidogo kuhusu kitambulisho Chake. Chote tunachofanya ni kuendelea na shughuli zetu, kana kwamba Yeye hahusiani nasi …

Kwa bahati, Roho Mtakatifu huonyesha kifungu cha maneno “kupitia” Kwake, na hata ingawa inaonekana ni jambo lisilotarajiwa sana, tunalitambua hata hivyo kama tamko kutoka kwaa Mungu, na tunaukubali kwa urahisi kutoka kwa Mungu. Hii ni kwa sababu, bila kujali ni nani anayeonyesha maneno haya, ilimradi yanatoka kwa Roho Mtakatifu tunapaswa kuyakubali, na hatufai kuyakana. Tamko linalofuata linaweza kuja kupitia mimi, au wewe, ama kupitia yeye. Yeyote yule, yote ni neema ya Mungu. Ilhali bila kujali mtu huyo ni nani, hatufai kumwabudu mtu huyu, kwa kuwa bila kujali chochote, mtu huyu hawezi kuwa Mungu, wala hatuwezi kwa njia yoyote ile kumchagua mtu wa kawaida kama huyu kuwa ndiye Mungu wetu. Mungu wetu ni mkubwa na mwenye kuheshimika sana; mtu asiye na maana kama huyu anawezaje kusimama katika nafasi Yake? Zaidi ya hayo, tunamsubiri Mungu aje na kuturudisha kwa ufalme wa mbinguni, na kwa hivyo mwanadamu asiye na umuhimu hivyo anawezaje kuwa na sifa zinazostahili kufanya kazi ngumu na muhimu kama hiyo? Bwana akirudi tena, ni lazima iwe juu ya wingu jeupe, ambalo halaiki ya watu wanaweza kuliona. Huo utakuwa wa adhimu namna gani! Itawezekanaje kwamba Anaweza kujificha kwa siri kati ya kundi la watu wa kawaida?

Na bado ni huyu mtu wa kawaida, aliyefichika kati ya watu, ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hatupi maelezo yoyote, wala Hatuambii kwa nini amerudi, lakini Yeye anafanya tu kazi anayotarajia kufanya kwa hatua zilizopimwa, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole na laini mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—lakini hakuna inayompa mwanadamu huruma na kumtia hofu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa tumejaa aibu isiyovumilika, tusijue pa kujificha. Tunaanza kutafakari iwapo Mungu Aliye katika roho ya huyu mtu kweli anatupenda, na nini hasa Anafanya. Labda tunaweza tu kunyakuliwa baada ya kuvumilia mateso haya? Vichwani mwetu tunafanya hesabu … kuhusu hatima inayokuja na kuhusu majaliwa yetu ya baadaye. Bado, kama awali, hakuna hata mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu amechukua mwili tayari ili kutenda kazi kati yetu. Japokuwa Ametuandama kwa muda mrefu sana, ingawa tayari Yeye amesema maneno mengi uso kwa uso nasi, bado tunabaki bila hiari ya kumkubali mtu aliye wa kawaida kiasi hicho awe Mungu wa mustakabali wetu, na bado hatuna nia ya kumwaminisha mtu huyu asiye na maana udhibiti wa mustakabali na majaliwa yetu. Kutoka Kwake, tunafurahia ugavi usioisha wa maji ya uhai, na kupitia Kwake tunaishi uso kwa uso na Mungu. Lakini tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Bado, kama awali Yeye kwa unyenyekevu, hufanya kazi Yake akiwa amefichwa ndani ya mwili, akipeana maonyesho a moyo Wake wa ndani zaidi, kana kwamba hafahamu kukataliwa Kwake na binadamu, kana kwamba yeye milele husamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele huvumilia mtazamo wa mwanadamu Kwake usioheshimu.

Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua moja baada ya nyingine ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, kuvumilia kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunapata kujua kuhusu tabia ya Mungu ya haki na uadhama, kufurahia, pia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua tabia na kiini cha Mungu, kufahamu mapenzi ya Mungu, kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno Yake hutufanya sisi “tufe,” na tena hutufanya “kuzaliwa upya”; maneno Yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno Yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa sana. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa mikononi Mwake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho Yake na kufurahia upendo Wake wenye upole; wakati mwingine sisi ni kama adui Yake, na chini ya macho Yake tunageuzwa majivu na ghadhabu Yake. Sisi ni jamii ya wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni Pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao, usiku na mchana, Yeye hunuia kuwapata. Yeye ni mwenye huruma kwetu, hutudharau, Yeye hutuinua, Yeye hutufariji na kutuhimiza, Yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Usiku na mchana, Yeye hakomi kamwe kuwa na wasiwasi nasi na hutulinda na kututunza usiku na mchana, Asiwache upande wetu kamwe, bali humwaga damu ya moyo Wake kwa ajili yetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa matamshi ya mwili huu mdogo na wa kawaida wa nyama, tumefurahia ukamilifu wa Mungu na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. Licha ya haya, majivuno bado yanazua rabsha mioyoni mwetu, na sisi bado hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu. Ingawa Yeye ametupa mana nyingi sana, nyingi sana ya kufurahia, hamna kati ya haya ambalo linaweza kuchukua nafasi ya Bwana katika mioyo yetu. Tunaheshimu utambulisho maalum na hadhi ya huyu mwanadamu kwa kusita sana. Bora hafungui mdomo Wake kututaka tukiri kwamba Yeye ni Mungu, sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni Mungu ambaye yuko karibu kuja na ilhali amekuwa akifanya kazi kati yetu kwa muda mrefu sana.

Mungu huendelea na matamshi Yake, akitumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya kuhusu kile tunachofaa kufanya na wakati uo huo akipea moyo Wake sauti. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na hisia za ndani kabisa za mwanadamu huyu asiye wa ajabu. Yeye hutema damu ya moyo Wake kwa niaba yetu, hupoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na uasi wetu na kufa ganzi kwetu kunatoa machozi na damu kutoka kwa moyo Wake. Njia hii ya kuwa na kumiliki si ya mtu wa kawaida, wala haiwezi kumilikiwa au kufikiwa na mtu yeyote aliyepotoka. Anaonyesha uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake si kitu ambacho kiumbe chochote kimepewa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu. Yeye huonyesha moyo wa ndani zaidi wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na kuleta mbingu na nchi mpya na kazi mpya, na ametuletea matumaini, akimaliza maisha ambayo tuliishi katika hali isiyo dhahiri, na kuwezesha nafsi yetu nzima kuona njia ya wokovu kwa udhahiri kamili. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zimepata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, huyu si ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, tukiwa tumeamka au kuota, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu! Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ametuwezesha kuishi tena na kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele. Wakati huu, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye ni nani tena, hatupingi tena kazi Yake na neno Lake, na tunasujudu, mbele Yake. Hakuna tunachotaka zaidi yakufuata nyayo za Mungu maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila Yake, na kulipa upendo Wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio Yake, na kushirikiana na kazi Yake, na kufanya kila kitu tunachoweza ili kukamilisha kile Anachotuaminia.

Kushindwa na Mungu ni kama mashindano ya kareti.

Kila neno la Mungu hugonga eneo letu moja la kufisha, likituwacha na uchungu na kujawa na hofu Yeye hufichua dhana zetu, mawazo yetu, na tabia zetu potovu. Kutoka kwa yale yote sisi husema na kutenda, hadi kwa kila wazo na fikra zetu, asili na kiini chetu kinafichuliwa katika maneno Yake, yakituweka katika hali ya hofu na kutetemeka na bila mahali pa kuficha aibu yetu. Mmoja baada ya mwingine, Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua sisi wenyewe, na kutufanya tuhisi kwamba tumewekwa wazi katika dosari zetu mbaya na hata zaidi kushindwa kikamilifu. Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba, machoni Pake, hatuna sifa hata moja inayoweza kutuokoa, kwamba sisi ndio Shetani anayeishi. Matumaini yetu yanavunjika, na hatuthubutu tena kumpa madai yoyote yasiyo na busara au kuendeleza matumaini yoyote ya Yeye, na hata ndoto zetu hupotelea mara moja. Huu ni ukweli ambao hakuna kati yetu anaweza kufikiria, na ambao hakuna yeyote kati yetu anayeweza kukubali. Katika muda mfupi, tunapoteza usawa wetu wa ndani, na hatujui jinsi ya kuendelea kwa njia iliyo mbele wala jinsi ya kuendelea katika imani zetu. Inaonekana kana kwamba imani yetu imerudi kama ilivyokuwa mwanzoni, na tena ya kana kwamba hatujawahi kukutana na Bwana Yesu au kupata kumjua. Kila kitu machoni petu hutujaza na mkanganyo, na kutufanya kuyumba kwa shaka. Tunasikitishwa, tunahuzunika, na ndani ya mioyo yetu kuna ghadhabu isiyozuilika na aibu. Tunajaribu kujieleza, kupata suluhisho, na, aidha, sisi huendelea kumsubiri Mwokozi Yesu, ili tuweze kujieleza kwa dhati Kwake. Ingawa kuna nyakati zingine ambazo sisi huonekana hatuyumbiyumbi kwa kutazamwa nje, tusio wenye kiburi wala wanyenyekevu, mioyoni mwetu tunateseka na hisia ya hasara kuliko ile tumewahi kuwa nayo. Ingawa wakati mwingine tunaweza kuonekana ni kama tuna utulivu kwa kutazamwa nje, akili zetu zinasokoteka kwa mateso kama bahari yenye dhoruba. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimechukua matumaini na ndoto zetu zote, kukomesha tamaa zetu kuu na kutuacha tusitake kuamini kuwa Yeye ndiye Mwokozi wetu na anayeweza kutuokoa. Hukumu Yake na kuadibu zimefungua ghuba kati yetu na Yeye, ghuba kubwa kiasi kwamba hakuna aliye tayari hata kujaribu kuivuka. Hukumu na kuadibu Kwake ni mara ya kwanza ambapo sisi tumepitia pingamizi kubwa hivi, udhalilishaji kiasi kikubwa hivyo maishani mwetu. Hukumu na kuadibu Kwake kwa kweli zimetusababisha kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia Kwake kosa la binadamu, ambazo tukilinganishwa nazo, sisi ni waovu sana, wachafu sana. Hukumu Yake na kuadibu zimetufanya sisi kutambua kwa mara ya kwanza jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hataweza kulingana na Mungu, ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya tutumaini kutoishi tena katika tabia potovu hivi, kujiondoa asili na kiini hiki haraka iwezekanavyo, na kuwacha kuwa waovu na wa kuchukiwa na Yeye. Hukumu na kuadibu Kwake zimetufanya tufurahie kutii maneno Yake, na tusiasi matayarisho na mipangilio Yake tena. Hukumu na kuadibu Kwake kwa mara nyingine zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa ya kuendelea kuwepo na zilituwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi wetu…. Sisi tumetoka nje ya kazi ya ushindi, nje yaa kuzimu, tumetoka nje ya bonde la uvuli wa mauti…. Mwenyezi Mungu ametupata, kundi hili la watu! Ameshinda dhidi ya Shetani, na kuwashinda adui Zake wengi!

Sisi ni kundi la watu wa kawaida tu, waliomilikiwa na tabia potovu ya kishetani, wale waliochaguliwa na Mungu kabla ya enzi, na wale maskini ambao Mungu ameinua kutoka jaani. Kuna wakati tulipomkataa na kumshutumu Mungu, lakini sasa tumeshindwa na Yeye. Kutoka kwa Mungu tumepokea uzima, njia ya uzima wa milele. Licha ya mahali ambapo tunaweza kuwa duniani, licha ya mateso na dhiki tunazovumilia, hatuwezi kuwa mbali na wokovu wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Yeye ndiye Muumba wetu, na ukombozi wetu pekee!

Upendo wa Mungu unaenea mbele kama maji ya chemichemi, na unapewa wewe, na mimi pia, na kwake, na kwa wale wote ambao wanatafuta ukweli kwa kweli na kungoja kuonekana kwa Mungu.

Kama vile tu mwezi hufuata jua kwa kubadilishana bila mwisho, vile vile ndivyo kazi ya Mungu haikomi kamwe, na inatekelezwa kwako, kwangu, kwake, na kwa wale wote ambao hufuata nyayo za Mungu na kukubali hukumu Yake na kuadibu Kwake.

Machi 23, 2010

Haya yaliandikwa na Mungu kama dibaji ya “Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu.”

Iliyotangulia: Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Inayofuata: Hitimisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp