Unajua Nini Kuhusu Imani?

Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binadamu huelewa kidogo sana, na binadamu mwenyewe amepungukiwa sana; yeye anakuwa tu na imani ndani Yangu bila kujali na bila kujua. Ingawa hajui imani ni nini wala ni kwa nini anayo imani ndani Yangu, anaendelea kufanya hivyo kwa shauku mno. Kile Ninachomwomba binadamu, si tu yeye kuniita Mimi kwa shauku kwa njia hii au kuniamini Mimi kwa mtindo huu wa kukosa mwelekeo. Kwani kazi Ninayoifanya ni yake binadamu kunijia Mimi na kunijia Mimi, wala si kwa binadamu kuvutiwa na kuniangalia Mimi kwa njia mpya kwa sababu ya kazi Yangu. Awali Nilijionyesha katika ishara na maajabu mengi na kufanya miujiza mingi. Waisraeli wakati huo waliniangalia Mimi kwa tamanio kuu na walistahi pakubwa uwezo Wangu wa kipekee wa kuponya wagonjwa na kupunga mapepo. Wakati huo, Wayahudi walifikiri nguvu Zangu za uponyaji zilikuwa za kistadi na zisizo za kawaida. Kwa matendo Yangu mengi kama hayo, wote walinichukulia Mimi kwa heshima; waliweza kuhisi tamanio kuu katika nguvu Zangu zote. Kwa hiyo yeyote aliyeniona Mimi nikifanya miujiza alinifuatilia Mimi kwa karibu kiasi kwamba maelfu ya watu walinizunguka ili kunitazama nikiwaponya wagonjwa. Nilionyesha ishara na maajabu mengi, ilhali binadamu alinichukulia Mimi kama daktari stadi; Niliongea maneno mengi ya mafunzo kwa watu hao wakati huo, ilhali wote walinichukulia Mimi tu kama mwalimu aliyekuwa na mamlaka zaidi kwa wanafunzi wake! Hadi siku ya leo, baada ya binadamu kuona rekodi za kihistoria za kazi Yangu, ufasiri wao unaendelea kuwa kwamba Mimi ni daktari mkuu anayeponya wagonjwa na mwalimu kwa wasiojua. Na wameniita Mimi Bwana Yesu Kristo Mwenye huruma. Wale wanaofasiri maandiko huenda walizidi mbinu Zangu katika uponyaji, au huenda pengine wakawa wanafunzi ambao tayari wamempita mwalimu wao, ilhali binadamu kama hao wanaofahamika sana ambao majina yao yanajulikana kote ulimwenguni wananichukulia Mimi kwa kiwango cha chini sana cha kuwa daktari tu! Matendo Yangu ni mengi zaidi kwa kuhesabiwa kuliko chembechembe za changarawe kwenye ufuo na hekima Yangu kubwa zaidi kuliko ile ya watoto wote wa kiume wa Suleimani, ilhali binadamu wanafikiria kwamba Mimi ni daktari tu asiye na mengi kumhusu na mwalimu wa binadamu asiyejulikana! Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze tu kupata uponyaji? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu niweze kutumia nguvu Zangu kupunga roho chafu kutoka kwenye miili yao? Na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili tu waweze kupokea amani na furaha kutoka Kwangu? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili kuhitaji kutoka Kwangu utajiri mwingi zaidi wa dunia, na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuishi maisha hayo kwa usalama na kuwa salama salimini katika maisha yajayo? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuepuka tu mateso ya kuzimu na kupokea baraka za mbinguni? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili wapate tulizo lakini hawatafuti kupata chochote kutoka kwa ulimwengu ujao? Niliposhushia hasira Zangu binadamu na kuchukua furaha na amani yote aliyokuwa nayo mwanzo, binadamu akaanza kuwa na shaka. Nilipomkabidhi binadamu mateso ya kuzimu na kuchukua tena baraka za mbinguni, aibu ya binadamu iligeuka na kuwa hasira. Wakati binadamu aliponiomba Mimi kumponya, bado Sikumsikiza na aidha nilimchukia pakubwa, binadamu alienda mbali sana na Mimi na akatafuta njia za dawa ovu na uchawi. Nilipochukua kila kitu ambacho binadamu walitaka kutoka Kwangu, walitoweka bila kuonekana tena. Kwa hivyo, Ninasema kwamba mwnadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata. Wayahudi waliniamini Mimi kwa neema Yangu, na wakanifuata Mimi popote Nilipoenda. Binadamu hawa wasiojua wenye maarifa na uzoefu finyu walitafuta tu kuona ishara na maajabu ambayo nilionyesha. Walinichukulia Mimi kuwa mkuu wa nyumba ya Wayahudi ambaye angeweza kutekeleza miujiza mikubwa zaidi. Kwa hivyo, Nilipopunga mapepo kutoka kwa binadamu walijizungumzia miongoni mwao kwa mkanganyo mkubwa wakisema Mimi ni Eliya, kwamba Mimi ni Musa, kwamba Mimi ndimi nabii wa kale zaidi kati ya wote, kwamba Mimi ndimi daktari mkuu zaidi kuliko wote. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Mimi ndimi maisha, njia na ukweli, hakuna yeyote angejua uwepo Wangu au utambulisho Wangu. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba mbingu ndipo ambapo Baba Yangu anapoishi, hakuna aliyejua kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu, na tena Mungu Mwenyewe. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Nitaleta ukombozi kwa wanadamu wote na kulipia mwanadamu fidia, hakuna aliyejua Mimi ni Mkombozi wa mwanadamu; binadamu alinijua tu Mimi kama mtu mkarimu na mwenye huruma. Na mbali na Mimi Mwenyewe kuweza kufafanua kila kitu kuhusu Mimi, hakuna aliyeweza kunitambua Mimi, hakuna aliyeamini kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu aliye hai. Binadamu pia anayo imani kama hii Kwangu Mimi, na ananidanganya Mimi kwa njia hii. Binadamu anawezaje kunitolea Mimi ushuhuda wakati anayo mitazamo kama hii kunihusu Mimi?

Binadamu anayo imani Kwangu Mimi lakini hawezi kunitolea ushuhuda Mimi; kabla ya Mimi Mwenyewe kujitambulisha, binadamu hawezi kunitolea ushuhuda Mimi. Binadamu anaona tu kwamba Mimi ninazidi viumbe na binadamu wote wengine watakatifu, na anaona kwamba kazi ninayofanya haiwezi kufanywa na binadamu wengine. Kwa hivyo, kuanzia kwa Wayahudi hadi kwa binadamu wa siku ya leo, yeyote ambaye ameyaona matendo Yangu yenye utukufu anajawa tu na uchu wa kudadisi mengi kuhusu Mimi, ilhali hakuna kinywa cha kiumbe kimoja ambacho kingeweza kunitolea ushuhuda. Baba Yangu tu ndiye Aliyenitolea ushuhuda Mimi; Alinitengenezea njia Mimi miongoni mwa viumbe vyote. Kwani, haijalishi ni namna gani Nilivyofanya kazi, binadamu asingewahi kujua Mimi ndimi Bwana wa viumbe, binadamu anajua tu kuchukua, na hajui kuwa na imani ndani Yangu Mimi kwa sababu ya kazi Yangu Mimi. Binadamu ananijua Mimi tu kwa sababu Mimi sina hatia wala si mtenda dhambi kwa vyovyote vile, kwa sababu Ninaweza kufafanua mafumbo mengi, kwa sababu Mimi niko juu ya wengine wote, au kwa sababu binadamu amefaidi pakubwa kutoka Kwangu. Ilhali wachache ndio wanaoamini kwamba Mimi ndimi Bwana wa viumbe. Hii ndiyo maana Ninasema ya kwamba binadamu hajui ni kwa nini anayo imani Kwangu mimi; hajui kusudio au umuhimu wa kuwa na imani Kwangu mimi. Uhalisia wa binadamu umekosekana, kiasi cha kwamba karibu hana thamani tena ya kuweza kunitolea ushuhuda Mimi. Unayo imani ya kweli ndogo sana na umefaidi kidogo sana, kwa hivyo una ushuhuda mdogo. Aidha, unaelewa mambo machache sana na unapungukiwa na mambo mengi sana kiasi kwamba hufai kushuhudia matendo Yangu. Azimio lako kwa hakika linaeleweka, lakini je una hakika kwamba utaweza kunitolea ushuhuda kwa ufanisi kuhusu hali halisi ya Mungu? Kile ambacho umepitia na kuona kinazidi kile ambacho watakatifu na manabii wengine wa awali walivyoshuhudia, lakini je unaweza kutoa ushuhuda mkubwa zaidi kuliko maneno ya hawa watakatifu na manabii waliotangulia? Kile Ninachokupa wewe sasa kinazidi kile Nilichompa Musa na ni kikubwa zaidi kuliko kile nilichompa Daudi, kwa hivyo vilevile Ninakuomba ushuhuda wako uzidi ule wa Musa na kwamba maneno yako yawe makubwa zaidi kuliko yale ya Daudi. Ninakupa vyote hivi mara mia moja, kwa hivyo vilevile ninakuomba nawe unilipe tena vivyo hivyo. Lazima ujue kwamba Mimi Ndimi ninayempa maisha mwanadamu, na kwamba wewe ndiwe unayepokea maisha kutoka Kwangu na lazima unitolee ushuhuda Mimi. Huu ndio wajibu wako, ambao Ninashusha kwako na ambao unastahili kunifanyia Mimi. Nimekupa utukufu Wangu wote, na kukupatia maisha ambayo watu wateule, Waisraeli, hawakuwahi kupokea. Bila kukosea, unastahili kunitolea ushuhuda, na kuutoa ujana wako kwa ajili Yangu na kuyatoa maisha yako. Yeyote yule ninayempa Mimi utukufu Wangu ataweza kunitolea Mimi ushuhuda na kunipatia maisha yake. Haya yote yametabiriwa mapema. Ni utajiri wako wewe ambao Ninawekea utukufu Wangu kwako wewe na wajibu wako ni kuutolea ushuhuda utukufu Wangu. Kama unaniamini tu Mimi ili kupata utajiri, basi kazi Yangu haitakuwa yenye umuhimu, na hutakuwa unatimiza wajibu wako. Waisraeli waliona tu huruma Yangu, upendo Wangu na ukubwa Wangu nao Wayahudi walitoa tu ushuhuda wa subira Yangu na ukombozi Wangu. Waliona kazi kidogo sana ya Roho Yangu; huenda ikawa kwamba kiwango chao cha uelewa kilikuwa sehemu ndogo sana ya ile ambayo wewe umesikia na kuona. Kile ulichoona kinazidi hata kile ambacho makuhani wakuu waliona miongoni mwao. Siku hii, ukweli ambao umeelewa umezidi wao; kile ambacho umeona siku hii kinazidi kile kilichoonwa kwenye Enzi ya Sheria pamoja na Enzi ya Neema na kile ambacho umepitia kinazidi hata kile ambacho Musa na Eliya walipitia. Kile ambacho Waisraeli walielewa kilikuwa tu sheria ya Yehova na kile ambacho waliona kilikuwa tu ni mgongo wake Yehova; kile ambacho Wayahudi walielewa kilikuwa tu ukombozi wa Yesu, kile walichopokea kilikuwa neema waliyowekewa na Yesu, na kile walichoona kilikuwa ni taswira ya Yesu ndani ya nyumba ya Wayahudi. Kile utakachoona siku hii ni utukufu wa Yehova, ukombozi wa Yesu na matendo Yangu yote ya siku hii. Umesikia pia maneno ya Roho Yangu, hekima Yangu teule, na ukaja kujua kuhusu maajabu Yangu, na umeweza kujifunza kuhusu tabia Yangu. Nimeweza pia kukuambia kuhusu mpango Wangu wa usimamizi. Kile ambacho umeona si tu Mungu mwenye upendo na huruma, lakini yule aliyejawa na haki. Umeiona kazi Yangu ya maajabu na kujua kwamba Nimejawa na hasira na adhama. Aidha, umejua kwamba Niliwahi kuzishusha hasira Zangu katika nyumba ya Israeli, na kwamba leo hii, umeshushiwa wewe. Umeelewa zaidi kuhusu mafumbo Yangu kule mbinguni kuliko vile alivyoelewa Isaya pamoja na Yohana; unajua zaidi kuhusu uzuri Wangu na kustahiwa Kwangu kuliko watakatifu wote wa vizazi vilivyotangulia. Kile ulichopokea si ukweli Wangu tu, njia Yangu, maisha Yangu, lakini maono na ufunuo ambavyo ni vikubwa zaidi kuliko vile vya Yohana. Umeelewa mafumbo mengine mengi zaidi na pia umeona sura Yangu kamili; umekubali mengi kuhusu hukumu Yangu na tabia Yangu ya haki. Kwa hivyo, ingawaje ulizaliwa kwenye siku za mwisho, uelewa wako ni ule wa siku za awali na za kale; umeweza pia kupitia ni nini kilichomo kwenye siku hii, na kile kilichotimizwa na mkono Wangu. Kile Ninachokuomba kinawezekana, kwani kile Nilichokupa ni kingi mno na ni mengi ambayo umeona Kwangu mimi. Kwa hivyo, Ninakuomba kunishuhudia Mimi kama vile watakatifu wa awali walivyofanya na hili ndilo tamanio tu la moyo Wangu.

Ni Baba Yangu ambaye amekuwa akinishuhudia Mimi, lakini Natafuta kupokea utukufu mkubwa zaidi na kwa maneno ya ushuhuda kutoka kwenye vinywa vya viumbe. Kwa hiyo Ninakupa kila kitu chote Changu kwa kusudi la wewe kuweza kutimiza wajibu wako, kukamilisha kazi Yangu miongoni mwa binadamu. Unastahili kuelewa ni kwa nini una imani Kwangu Mimi. Ukinifuata Mimi tu ili uwe mwanafunzi Wangu au mgonjwa Wangu, au kuwa mojawapo wa watakatifu Wangu mbinguni, basi kunifuata kwako hakutakuwa na maana. Kunifuata Mimi kwa njia kama hiyo ni sawa tu na kuharibu jitihada zako; kuwa na imani kama hiyo Kwangu mimi ni kuishi tu ukiharibu siku zako na kutomakinikia ujana wako. Na mwisho hutapokea chochote. Huku si ni kufanya kazi bure? Ni muda mrefu tangu Nimetoka miongoni mwa Wayahudi na mimi si daktari tena wa binadamu au dawa ya binadamu. Mimi si mnyama tena wa kumbebea mizigo binadamu ili aniendeshe au kunichinja akipenda; badala yake Nimekuja miongoni mwa binadamu ili kuhukumu na kuadibu binadamu, na kwa binadamu kunijua Mimi. Unafaa kujua kwamba Niliwahi kufanya kazi ya ukombozi; Niliwahi kuwa Yesu, lakini Nisingebakia kuwa Yesu milele, licha ya kwamba Niliwahi kuwa Yehova lakini baadaye nikawa Yesu. Mimi ndimi Mungu wa mwanadamu, Bwana wa viumbe, lakini Siwezi kubakia Yesu milele au kubakia Yehova milele. Nimekuwa kile ambacho binadamu aliona ni daktari, lakini haiwezi kusemekana kwamba Mungu ni daktari tu wa mwanadamu. Kwa hiyo kama utakuwa na mtazamo huo wa kale katika imani yako Kwangu mimi, basi hutapata chochote. Haijalishi ni vipi utakavyonisifu siku hii: “Tazama Mungu alivyo na upendo kwa binadamu; Ananiponya mimi na kunipa baraka, amani na furaha. Ni vipi ambavyo Mungu atakavyokuwa mzuri kwa binadamu; kama tutakuwa na imani tu Kwake Yeye, basi hatutahitajika kuwa na wasiwasi wa pesa na utajiri…,” Siwezi bado kutatiza kazi Yangu asilia. Kama utaniamini Mimi siku hii, utapokea tu utukufu Wangu na kustahili kunitolea ushuhuda, na kila kitu kingine kitafuata. Hili lazima ulijue wazi.

Sasa unajua kweli ni kwa nini unaniamini Mimi? Kweli unajua kusudi na umuhimu wa kazi Yangu? Kweli unajua wajibu wako? Kweli unaujua ushuhuda Wangu? Kama unaniamini Mimi tu, ilhali si utukufu Wangu wala ushuhuda Wangu vinaweza kuonekana ndani yako, basi Nimekutupa nje kitambo kirefu. Kwa wale wanaoona wanajua kila kitu, wao ni miiba zaidi katika macho Yangu, na katika nyumba Yangu, wao ni vizuizi tu Kwangu. Wao ndio magugu yanayopaswa kupepetwa kabisa na kuondolewa kwenye kazi Yangu, bila ya jitihada hata kidogo na bila ya uzito wowote; Nimevichukia kitambo kirefu. Na kwa wale bila ya ushuhuda, hasira Yangu siku zote iko juu yao, na kiboko Changu hakijawahi kutoka kwao. Kitambo kirefu Nimewakabidhi kwenye mikono ya yule mwovu, na hawana tena baraka Zangu zozote. Na siku hiyo ikifika, adhabu yao itakuwa mbaya zaidi kuliko ile ya wanawake wajinga. Sasa hivi Ninafanya kazi ile ambayo ndiyo wajibu Wangu kufanya; Nitakusanya pamoja ngano yote, pamoja na magugu. Hii ndiyo kazi Yangu sasa. Magugu haya yataweza kupepetwa na kuondolewa wakati wa kupepeta Kwangu, kisha nafaka za ngano zitakusanywa kwenye ghala, na magugu ambayo yatakuwa yamepepetwa yatawekwa motoni na kuchomwa hadi kugeuka jivu. Kazi Yangu sasa ni kuwaweka tu binadamu wote kwa pamoja, yaani, kuweza kuwashinda wote kabisa. Kisha Nitaanza upepetaji wa kufichua mwisho wa binadamu wote. Kwa hiyo unastahili kujua namna ya kunitosheleza Mimi sasa na namna unavyostahili kuwa kwenye njia iliyo sawa katika imani yako Kwangu. Kile Ninachotafuta ni uaminifu na utiifu wako sasa, upendo wako na ushuhuda wako sasa. Hata kama hujui kwa wakati huu kile ambacho ushuhuda unamaanisha au kile ambacho upendo unamaanisha, unafaa kuniletea kila kitu, na kunikabidhi mimi hazina za pekee ulizonazo: uaminifu na utiifu wako. Unafaa kujua, agano la kushinda Kwangu Shetani limo ndani ya uaminifu na utiifu wa binadamu, sawa tu na vile ilivyo katika agano la kumshinda kabisa binadamu. Wajibu wa imani Yako Kwangu mimi ni kunishuhudia Mimi, kuwa mwaminifu Kwangu mimi na si mwingine yeyote, na kuwa mtiifu hadi mwisho. Kabla Sijaanza hatua inayofuata ya kazi Yangu, utawezaje kunishuhudia Mimi? Utawezaje kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi? Je, unajitolea uaminifu wako wote katika utendakazi au utakata tamaa tu? Au afadhali unyenyekee katika kila mpangilio Wangu (uwe wa kifo au wa kuangamiza) au kutoroka hapo katikati ili kuepuka kuadibiwa? Ninakuadibu ili uweze kunishuhudia Mimi, na kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi. Pia, kuadibu huku kwa sasa kunalenga katika kufichua hatua inayofuata ya kazi Yangu na kuruhusu kazi hiyo kuendelea bila kutatizwa. Hivyo basi Nakushawishi wewe kuwa mwenye hekima na kutochukulia maisha yako au umuhimu wa kuwepo kwako kuwa ule ambao hauna manufaa kamwe. Unaweza kujua haswa kazi Yangu ijayo itakuwa ipi? Je, unajua namna Nitakavyofanya kazi katika siku zijazo na namna ambavyo kazi Yangu itakavyobadilika? Unafaa kujua umuhimu wa kile ambacho umepitia katika kazi Yangu, na zaidi, umuhimu wa imani yako Kwangu mimi. Nimefanya mengi kweli; iweje Nikate tamaa Nikiwa katikati kama unavyofikiria? Nimefanya kazi kubwa kweli; ninawezaje kuiharibu? Kwa hakika, Nimekuja kuhitimisha enzi hii. Hii ni kweli, lakini zaidi, lazima ujue kwamba Ninafaa kuanzisha enzi mpya, kuanzisha kazi mpya, na, zaidi ya yote, kueneza injili ya ufalme. Kwa hivyo unafaa kujua kwamba kazi ya sasa inalenga katika kuanzisha tu enzi mpya, na kuweka msingi wa kueneza injili katika wakati ujao na kuihitimisha enzi ya sasa katika wakati ujao. Kazi Yangu si rahisi sana kama unavyofikiria, wala si kwamba haina manufaa au maana kama unavyoweza kutaka kuamini. Kwa hivyo, lazima bado Nikuambie: Unastahili kujitolea maisha Yako katika kazi Yangu, na zaidi, unastahili kujitolea wewe mwenyewe katika utukufu Wangu. Aidha, wewe kunishuhudia ndicho kile kitu ambacho Nimetamani kwa muda mrefu, na kingine ambacho Nimetamani hata zaidi ni wewe kueneza injili Yangu. Unastahili kuelewa kile kilichomo ndani ya moyo Wangu.

Iliyotangulia: Maana ya Kuwa Mtu Halisi

Inayofuata: Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp