Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli
Katika matendo, kushika amri zapaswa kuunganishwa na matendo ya ukweli. Wakati unapozishika amri, mtu anapaswa kutenda ukweli. Wakati anapotenda ukweli, mtu hapaswi kukiuka kanuni za amri au kwenda kinyume na amri. Fanya yale ambayo Mungu anahitaji uyafanye. Kuzishika amri na kuutenda ukweli vinahusiana, bali havikinzani. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo unavyoweza kutilia maanani zaidi kiini cha amri. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo utakavyoweza kulielewa zaidi neno la Mungu kama ilivyoonyeshwa katika amri. Kutenda ukweli na kuzishika amri sio vitendo vinavyopingana, lakini badala yake vinahusiana. Mwanzoni, ni kwa kuzishika tu amri ndipo mwanadamu anaweza kuutenda ukweli na kufikia kuipata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Lakini hii sio nia ya awali ya Mungu. Mungu inakuhitaji umwabudu Mungu kwa moyo, sio tu kutenda tabia nzuri. Lakini lazima uzishike amri angalau hivi hivi. Hatua kwa hatua, kupitia uzoefu, mwanadamu hupata ufahamu wa wazi zaidi wa Mungu. Yeye huacha kumwasi na kumpinga Mungu, naye anaacha kuitilia shaka kazi ya Mungu. Kwa njia hii mtu anaweza kuzingatia kiini cha amri. Kwa hiyo, kuzishika tu amri bila kutenda ukweli ni hafifu nako hakufanyizi ibada ya kweli ya Mungu kwa sababu bado hujafikia kimo cha kweli. Ukizishika amri bila ukweli, hii ni sawa na kuzingatia tu sheria bila kushawishika. Katika kufanya hivyo, amri zinakuwa sheria yako, ambayo haitakusaidia kukua katika maisha. Badala yake, zitakuwa mzigo wako, nazo zitakufunga imara kama sheria ya Agano la Kale, zikusababishe kuupoteza uwepo wa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, ni kwa kuutenda ukweli tu ndipo utakapoweza kuzishika amri kwa ufanisi. Mtu huzishika amri ili autende ukweli. Unautenda hata ukweli zaidi kwa kuzishika amri. Unapata hata uelewa zaidi wa maana halisi ya amri kwa kuutenda ukweli. Kusudi na maana ya sharti la Mungu ni kwamba lazima mwanadamu azishike amri sio kuzifuata sheria kama mwanadamu anavyoweza kufikiria, lakini inahusiana na mwanadamu kuingia katika maisha. Zaidi unavyokua katika maisha, ndivyo unapata kiwango kibukwa zaidi ambacho utaweza kutii amri. Ingawa amri ni za mwanadamu kuzishika, asili ya amri inakuwa tu dhahiri kupitia kwa uzoefu wa maisha ya mwanadamu. Watu wengi wanadhani kwamba kuzishika amri vizuri inamaanisha “kila kitu kiko tayari, kile kimebaki ni kuchukuliwa juu.” Huku ni kufikiria badhirifu nako sio mapenzi ya Mungu. Wale wanaosema mambo kama haya hawataki kufanya maendeleo nao wanayo tamaa ya mwili. Hili halina maana! Hili haliambatani na uhalisi! Siyo mapenzi ya Mungu kutenda ukweli tu bila kushika amri kwa kweli. Wale wanaofanya hivi ni vilema; wao ni kama watu wasio na mguu mmoja. Wakifuata tu amri kana kwamba wanafuata masharti, lakini hawana ukweli—huku si kuridhisha mapenzi ya Mungu, pia; kama kama wale wasio na jicho moja, watu wanaofanya hivi pia, wanateseka kwa ajili ya aina fulani ya ulemavu. Inaweza kusemwa kwamba ukizishika amri vizuri na kupata uelewa wa wazi wa Mungu wa vitendo, basi utakuwa na ukweli. Kutokana na mtazamo wa uhusiano, utakuwa umepata kimo cha kweli. Unatenda ukweli unaopaswa kutenda na kuzishika amri kwa wakati mmoja bila migogoro ya pande zote. Kuutenda ukweli na kuzishika amri ni mifumo miwili, yote ambayo ni sehemu muhimu ya uzoefu wa maisha ya mtu. Uzoefu wa mtu lazima uafikiane na muungano wa kuzishika amri kwa kuutenda ukweli, sio kugawanya. Hata hivyo, kunazo tofauti na uhusiano kati ya mambo haya mawili.
Kutangazwa rasmi kwa amri katika enzi mpya ni ushahidi wa ukweli kwamba wanadamu wote katika mkondo huu na wale ambao husikia sauti ya Mungu leo wameingia katika enzi mpya. Huu ni mwanzo mpya kwa ajili ya kazi ya Mungu nao ni mwanzo wa sehemu ya mwisho ya kazi katika mpango wa usimamizi wa Mungu katika kipindi cha miaka elfu sita. Amri za enzi mpya zinaashiria kuwa Mungu na binadamu wameingia katika eneo la mbingu mpya na nchi mpya, na kwamba Mungu, kama vile Yehova alifanya kazi miongoni mwa Waisraeli naye Yesu alifanya kazi miongoni mwa Wayahudi, Ataifanya kazi zaidi ya vitendo na kuifanya kazi zaidi na kubwa zaidi duniani. Pia zinaashiria kwamba kundi hili la watu watapokea agizo zaidi na kubwa zaidi kutoka kwa Mungu, nao watapokea ugavi wa vitendo, malisho, msaada, huduma na ulinzi kutoka kwa Mungu. Zaidi ya hayo watafanywa kupitia katika mazoezi zaidi ya vitendo, na pia kushughulikiwa, kuvunjwa na kusafishwa kwa neno la Mungu. Maana ya amri za enzi mpya ni kubwa sana. Zinaonyesha kwamba Mungu kweli ataonekana kwenye ardhi naye Mungu ataushinda ulimwengu mzima juu ya nchi, akiuonyesha utukufu Wake wote katika mwili. Pia zinaonyesha kwamba Mungu wa vitendo anaenda kuifanya kazi zaidi ya vitendo duniani ili akamilishe yote ambayo Amechagua. Zaidi ya hayo, Mungu atatimiza kila kitu kwa maneno duniani na kufanya wazi amri kwamba “Mungu mwenye mwili huinuka juu zaidi naye ametukuzwa, nao watu wote na mataifa yote hupiga magoti kumwabudu Mungu—ambaye ni mkuu.” Ingawa amri za enzi mpya ni za mwanadamu kuzishika, na ingawa kufanya hivyo ni wajibu wa mwanadamu na jukumu lake, maana ambazo zinawakilisha ni ya kina sana kuweza kuonyeshwa kikamilifu katika neno moja au mawili. Amri za enzi mpya zinachukua nafasi ya sheria za Agano la Kale na maagizo ya Agano Jipya kama zilivyotangazwa rasmi na Yehova na Yesu. Hili ni somo la ndani zaidi, sio jambo rahisi kama mtu anavyoweza kufikiria. Amri za enzi mpya zinazo kipengele cha maana ya vitendo: Zinatumika kama kipengee kinachojitokeza kati ya Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme. Amri za enzi mpya zinahitimisha mazoea yote na maagizo yote ya enzi ya zamani na pia zinahitimisha mazoea yote ya enzi ya Yesu na zile kabla yake. Zinamleta mwanadamu katika uwepo wa Mungu wa vitendo zaidi na kumruhusu mtu kuanza kuupokea ukamilifu wa binafsi wa Mungu, ambazo ni mwanzo wa njia ya kukamilika. Kwa hiyo, ninyi mtamiliki mtazamo sahihi kuelekea amri za enzi mpya na wala hamtazifuata ovyo wala kuzidharau. Amri za enzi mpya zinasisitiza hoja moja: kwamba mwanadamu atamwabudu Mungu wa vitendo Mwenyewe wa leo, ambayo ni kutii kiini cha Roho katika matendo zaidi. Pia zinasisitiza kanuni ambayo Mungu atamhukumu mwanadamu kuwa na hatia au haki Atakapoonekana kama Jua la haki. Amri zinaeleweka kwa urahisi kuliko kutendwa. Hivyo, kama Mungu anataka kumkamilisha mwanadamu, lazima Atafanya hivyo kupitia kwa maneno Yake mwenyewe na mwongozo, mwanadamu hawezi kufikia ukamilifu kupitia asili ya akili yake peke yake. Ikiwa mwanadamu anaweza kuzishika amri za enzi mpya au la inahusiana na maarifa ya mwanadamu ya Mungu wa vitendo. Kwa hiyo, kama unaweza kuzishika amri au la sio swali litakalotatuliwa katika siku chache. Hili ni somo la kina.
Kuutenda ukweli ni njia ambayo kwayo maisha ya mwanadamu yanaweza kukua. Msipotenda ukweli, mtaachwa na nadharia tu nanyi hamtakuwa na maisha ya kweli. Ukweli ni ishara ya kimo cha mwanadamu. Ikiwa hauutendi ukweli au la inahusiana na kufikia kimo cha kweli. Kama hauutendi ukweli, hutendi kwa haki, au unashawishiwa na hisia na kuujali mwili, basi uko mbali na kuzishika amri. Hili ni somo la kina zaidi. Kunazo kweli nyingi kwa mwanadamu kuingia na mwanadamu kuelewa katika kila enzi. Lakini kunazo amri mbalimbali zinazoambatana na ukweli katika kila enzi. Ukweli ambao mwanadamu huutenda unahusiana na enzi na amri zinazowekwa na mwanadamu pia huhusiana na enzi. Kila enzi inazo kweli zake ambazo lazima zitendwe na amri za kuhifadhiwa. Hata hivyo, kulingana na amri mbalimbali ambazo zimetangazwa rasmi na Mungu, ambayo ni, kulingana na enzi tofauti, lengo na athari ya kuutenda ukweli kwa mwanadamu vinatofautiana kwa kadri iliyo sawa. Inaweza kusemwa kwamba amri huutumikisha ukweli nao ukweli huwepo kuzidumisha amri. Kama kunao ukweli tu, hakutakuwa na mabadiliko katika kazi ya Mungu kuyataja. Hata hivyo, kwa kuzirejelea amri, mwanadamu anaweza kutambua ukubwa wenye nguvu wa kazi iliyofanywa na Roho Mtakatifu naye mwanadamu anaweza kujua enzi ambayo Mungu hufanya kazi. Katika dini, kunao watu wengi ambao wanaweza kutenda ukweli unaotendwa na mwanadamu wa Enzi ya Sheria. Hata hivyo, hawana amri za enzi mpya nao hawawezi kuzishika amri za enzi mpya. Wao huifuata njia ya zamani nao hubaki kama binadamu wa asili. Hawaambatani na namna mpya ya kazi nao hawawezi kuziona amri ya enzi mpya. Kimsingi, kazi ya Mungu haipo. Wao ni kama mtu aliyeshika ganda tupu la yai: Hakuna roho kama hakuna kifaranga ndani mwake. Tukizungumza kwa udhahiri, hakuna maisha. Watu kama hawa hawajaingia katika enzi mpya nao wamekawia nyuma kwa hatua nyingi. Kwa hiyo, ni bure kama watu wanao ukweli wa enzi ya miaka ya zamani lakini hawana amri za enzi mpya. Wengi wenu mnautenda ukweli wa wakati huu lakini hamzishiki amri za wakati huu. Hamtapata chochote, ukweli mnaoutenda utakuwa bure na bila maana naye Mungu hatausifu. Kuutenda ukweli lazima ufanyike kwa njia ambayo Roho Mtakatifu hufanya kazi leo; ni lazima ufanyike kwa kufuata sauti ya Mungu wa vitendo leo. Bila hii, kila kitu ni bure—kama vile kuchota maji na kikapu cha mianzi. Hii ndiyo maana halisi ya kutangazwa rasmi kwa amri za enzi mpya. Ikiwa watu wanapaswa kutii amri hizo, angalau kabisa wanafaa kumjua Mungu mwenye vitendo anayeonekana katika mwili bila kukanganyikiwa. Yaani, watu wanapaswa kuelewa kanuni za kutii sheria. Kutii sheria hakumaanishi kuzifuata kiholela ama bila mpangilio, bali kuzitii ukiwa na msingi, na lengo, na kanuni. Kitu cha kwanza cha kufanikishwa ni maono yako kuwa dhahiri. Ikiwa unao uelewa wa kina wa kazi ya Roho Mtakatifu katika wakati wa sasa nawe uingie namna ya kazi ya leo, kwa kawaida utaona kiini cha kuziweka amri. Kama siku itakuja utakapoona kiini cha amri za enzi mpya nawe utaweza kuzishika amri, basi wakati huo utakuwa umekamilika. Hii ndiyo maana ya kweli ya kuutenda ukweli na kuzishika amri. Ikiwa unaweza kuutenda ukweli au la inategemea jinsi unavyotambua kiini cha amri ya enzi mpya. Kazi ya Roho Mtakatifu itaonekana daima kwa mwanadamu naye Mungu itahitaji zaidi na zaidi kutoka kwa mwanadamu. Kwa hiyo, kweli ambazo mwanadamu huzitenda kwa kweli zitakuwa zaidi na kubwa zaidi nayo madhara ya kuzishika amri yatakuwa ya kushangaza zaidi. Kwa hiyo, ninyi mtautenda ukweli na kuzishika amri kwa wakati mmoja. Hakuna mtu atakayepuuza jambo hili. Hebu ukweli mpya na amri mpya zianze kwa wakati mmoja katika enzi hii mpya.