Sura ya 23
Ninapopaza sauti Yangu, macho Yangu yanapotoa moto, Ninaitazama dunia nzima, Ninauchunguza ulimwengu wote. Wanadamu wote wananiomba, wakielekeza macho yao Kwangu, wakiniomba Nikomeshe hasira Yangu, na kuapa kutoniasi tena. Lakini hii sio kama zamani tena; bali ni sasa. Ni nani awezaye kuyageuza mapenzi Yangu? Kwa kweli sio maombi katika nyoyo za watu, wala maneno katika vinywa vyao? Ni nani ambaye ameweza kuishi hadi sasa, ikiwa si kwa sababu Yangu? Ni nani anayesalia isipokuwa kwa maneno katika kinywa Changu? Ni nani asiyekaa chini ya uangalizi wa macho Yangu? Ninapotekeleza kazi Yangu mpya duniani kote, ni nani ambaye amewahi kuweza kuiepuka? Inawezekana kuwa milima imeiepuka kutokana na urefu wayo? Inawezekana kuwa maji kwa wingi na upana wake, yameweza kuizuia kazi hii? Katika mpango Wangu, Sijawahi kuachilia kitu chochote kiende kwa wepesi, hivyo basi hakuna mtu yeyote, wala kitu chochote, ambacho kimeepuka mikono Yangu. Hivi leo, jina Langu takatifu linatukuka katika uumbaji wote, na tena, maneno ya malalamiko katika ubinadamu dhidi Yangu yanachipuka, na hadithi kuhusu kuwepo Kwangu ulimwenguni zimeenea miongoni mwa binadamu. Sivumilii binadamu wanapotoa hukumu dhidi yangu, wala Sivumilii wao kuugawanya mwili Wangu, wala lugha ya machungu na matusi dhidi Yangu. Ukweli ni kuwa mwanadamu hajawahi kunifahamu Mimi, tangu awali amenikana na kuzua upinzani Kwangu, akishindwa kumpenda Roho Wangu au kuyathamini maneno ya kinywa Changu. Kwa kila tendo na hatua yake, na kwa mtazamo wake Kwangu, Nampa binadamu “tuzo” yake inayomfaa. Hivyo basi, binadamu hufanya jambo wakiwa wameweka macho kwenye tuzo yao, na wala hapana mmoja aliyefanya kazi inayohusisha kujinyima na kujitolea. Wanadamu hawana nia ya kujitoa kwa kujinyima, ila wanafurahia tuzo zinazopatikana kwa kutofanya chochote. Japo kuwa Petro alijiweka wakfu mbele Zangu, haikuwa ni kwa sababu ya malipo ya kesho, bali kwa maarifa ya leo. Ubinadamu haujawahi kuwasiliana na Mimi kwa kweli, lakini mara kwa mara umenishughulikia kwa njia ya juu juu, wakifikiri kwa hivyo bila juhudi kupata idhini Yangu. Nimeangalia kwa kina ndani ya moyo wa mwanadamu, na kuibua undani wake wa siri “mgodi wa utajiri mwingi,” kitu ambacho hata mwanadamu mwenyewe hafahamu lakini mimi Nimefahamu upya. Hivyo basi, mpaka watakapojionea kwa macho “ushahidi wa kuonekana”, hapo tu ndipo binadamu atasitisha unafiki wa kujidhalilisha mwenyewe na, mikono iliyonyooshwa watakubali hali yao ya uchafu. Miongoni mwa wanadamu, kuna mengi zaidi ambayo ni mapya na safi yanayonisubiri “kutoa” kwa ajili ya starehe ya ubinadamu wote. Mbali na kuacha kazi Yangu kwa sababu ya kutoweza kwa mwanadamu, Ninampogoa kama ilivyokuwa mpango Wangu wa awali. Binadamu ni kama mti wa matunda: bila ya kuukata na kuupogoa, mti huo hautaweza kuzaa matunda na, mwishowe, yatakayoonekana ni matawi yaliyonyauka na majani yaliyoanguka, pasipo na matunda yoyote kuanguka ardhini.
Ninapokipamba “chumba cha ndani” cha ufalme Wangu siku baada ya siku, hakuna yule ameingia katika “chumba Changu cha kazi” kwa ghafla ili kuvuruga kazi Yangu. Watu wote wanafanya wawezayo kushirikiana nami, wakiwa na hofu mno ya “kufukuzwa” na “kupoteza nafasi zao” hivyo kufikia tamati maishani mwao ambapo wanaweza kuanguka “jangwani” anakoishi Shetani. Kwa sababu ya uoga wa mwanadamu, Ninamfariji kila siku, Nikimwegemeza katika pendo kila siku na zaidi ya yote kumwelekeza na sheria kila siku ya maisha yake. Ni kana kwamba wanadamu wote ni watoto wachanga ambao wamezaliwa sasa hivi; bila ya kupewa maziwa, watatoweka duniani humu, wasipate kuonekana tena. Kati ya maombi ya unyenyekevu ya mwanadamu, Nakuja katika ulimwengu wa mwanadamu, na moja kwa moja, mwanadamu anaishi katika ulimwengu wenye mwanga, wasifungiwe tena katika “chumba” ambako wanatoa vilio vya maombi vikielekea mbinguni. Mara tu wanaponiona, binadamu kwa kusisitiza huleta mbele Yangu “maombolezo” yaliyo mioyoni mwao, wakifungua vinywa vyao mbele Yangu wakiomba kwamba chakula kiangushwe midomoni mwao. Lakini baadaye, hofu yao kutoweka na hali tulivu kurejea, na hakuna wanachohitaji kutoka Kwangu tena, mwanadamu hulala fofofo au hukana uwepo Wangu, kisha kuelekea kufanya mambo yao wenyewe. Katika ile hali ya mwanadamu “kutelekeza”, ni wazi kuwa binadamu pasi na “hisia” huendeleza “haki bila mapendeleo” Kwangu. Hivyo basi, Ninapomwangalia mwanadamu katika ile hali yake ya ukosefu wa pendo Kwangu, Mimi huondoka kwa upole pasi na kurudi tena kwa wepesi katika hali yake ya maombi ya hitaji. Bila ya mwanadamu kufahamu, shida zake zinaongezeka siku baada ya siku, hivyo, katika hali yake ya kufanya kazi kwa bidii, ndipo anapofahamu uwepo Wangu, yeye, akikataa kuchukua “la” kama jawabu, kisha anashika kwa nguvu nguo Yangu na kunikaribisha kwa ukarimu nyumbani kwake kama mgeni. Lakini, ingawa anaandaa chakula kitamu mbele Yangu ili Niweze kustarehe, hajawahi kunikubali kama mmoja wa wenzi wake, badala yake akinichukulia kama mgeni ili tu apate kitu kiasi kidogo cha usaidizi kutoka Kwangu. Hivyo basi mwanadamu kwa wakati huu anaweka wazi Kwangu hali yake ya kuhurumisha, akiwa na matumaini kuwa atapata “sahihi,” na, kama yule anayehitaji mkopo kwa ajili ya biashara yake, ananikabili kwa nguvu zake zote. Katika kila ishara na mwenendo wake, Ninapata mtazamo wa nia ya mwanadamu: ni kana kwamba, katika maoni yake, Mimi sijui jinsi ya kusoma tafsiri zilizofichwa katika uso wa mwanadamu au zilizofichwa nyuma ya maneno anayotamka, ama jinsi ya kuangalia kwa kina katika moyo wa mwanadamu. Kwa hiyo mwanadamu huachilia ujasiri wake Kwangu katika kila uzoefu wa kila tukio alilowahi kupitia, bila ya kuacha au kusahau jambo lolote, na baada ya hayo anayaleta madai yake Kwangu. Ninachukia na kudharau kila tendo la mwanadamu. Miongoni mwa wanadamu, hakujawahi kamwe kuwepo na yeyote yule aliyefanya tendo linalonipendeza, ni kana kwamba wanadamu wanafanya makusudi ili kuniudhi Mimi, na kwa kudhamiria wanaikaribisha ghadhabu Yangu: Wote wanakwenda nyuma na mbele mbele Yangu, wakitenda yaliyo mapenzi yao wenyewe mbele za macho Yangu. Hakuna yeyote kati ya binadamu anayeishi kwa ajili Yangu, hivyo basi kuwepo kwa viumbe vyote kunakosa maana na wanadamu wanaishi kwa utupu mkuu. Hata hivyo, binadamu bado wanakataa kutoka katika hali ile ya uzinifu wakiendelea na uasi wao Kwangu wakisisitiza kukaa katika ubatili.
Katika majaribu yote ambayo wamepitia, wanadamu hawajawahi kunifurahisha hata mara moja. Kwa sababu ya uovu wao wa kikatili, wanadamu hawalengi kulishuhudia jina Langu; badala yake, “anakimbia njia nyingine” huku akinitegemea kumpa riziki ya kila siku. Moyo wa mwanadamu haunigeukii kabisa, na kwa hivyo Shetani humnyanyasa mpaka awe na wingi wa majeraha, mwili wake kufunikwa na uchafu. Lakini mwanadamu bado hatambui jinsi uso wake ulivyo na mbaya: Wakati wote ameendelea kumwabudu Shetani nyuma ya mgongo Wangu. Kwa sababu hii, kwa ghadhabu Nitamtupa mwanadamu ndani ya shimo lisilo na mwisho, asiloweza kujikomboa mwenyewe. Hata hivyo, katikati ya kilio chake cha kusikitisha, mwanadamu bado anakataa kurekebisha mawazo yake, akidhamiria kunipinga hadi mwisho mchungu, na akitumaini kwa makusudi kuchochea ghadhabu Yangu. Kwa ajili ya yale aliyoyatenda, Ninamtendea kama mwenye dhambi na kumnyima joto la kumbatio Langu. Tokea mwanzo, malaika wamenihudumia na kuniheshimu bila ya kubadili mienendo, lakini mwanadamu kila mara akifanya kinyume, kana kwamba hakutoka Kwangu, ila kazaliwa na Shetani. Malaika katika maeneo yao hunipa ibada kamili; hawatikiswi na nguvu za kishetani, na wanatimiza tu wajibu wao. Wakiwa wamelishwa na malaika, halaiki za Wanangu na watu Wangu wote hukua kwa nguvu na wenye afya, hakuna kati yao yeyote yule aliyedhoofika kiafya. Hii ni kazi ya mikono Yangu, muujiza Wangu. Kama vile vigelegele baada ya vigelegele vya moto wa kanuni huzindua uanzilishi wa ufalme Wangu, malaika, wakiwa wanatembea katika usawa wa kifuasi, huja mbele ya jukwaa Langu kujiwasilisha kwa ukaguzi, Wangu, kwa sababu mioyo yao haina uchafu na haiabudu miungu mingine, hivyo hawaepuki ukaguzi Wangu.
Upepo mkali unapovuma kwa mayowe, mbingu hushuka ghafla, na kufanya wanadamu kukosa hewa hivyo basi hawawezi tena kuliita jina Langu jinsi wapendavyo. Bila ya kujua, ubinadamu wote umeanguka. Miti huyumba mbele na nyuma katika upepo, mara kwa mara matawi husikika yakitoa sauti ya kuvunjika, na majani yote yaliyonyauka hubebwa na upepo. Dunia hujaa kiza na ukiwa mara moja, na watu wakikumbatiana kwa pamoja, wakingoja maafa yanayofuata majira ya kupukutika kwa majani kuwapata wakati wowote. Ndege juu ya vilima huruka huku na huko, kana kwamba wanamlilia mtu huzuni yao; katika mapango ya milimani, simba hunguruma, wakitisha watu kwa sauti hiyo, wakiganda uboho wao na kufanya nywele zao zisimame, na ni kana kwamba kuna hisia ya kutisha inayotabiri mwisho wa mwanadamu. Bila kungojea furaha ya nia Yangu ya kuwaangamiza, binadamu wote huomba kimoyomoyo kwa Bwana Mkuu aliye mbinguni. Lakini itawezekanaje upepo mkubwa kuzuiliwa na kelele za maji yakitiririka kwenye kijito? Itawezekanaje upepo huu usimamishwe kwa sauti za sala za binadamu? Itawezekanaje hasira moyoni mwa radi kutulizwa sababu ya woga wa mwanadamu? Mwanadamu huyumba nyuma na mbele katika upepo; anakimbia huku na huko ili kujificha na mvua; na chini ya ghadhabu Yangu, wanadamu hutingisika na kutetemeka, wakiogopa sana kwamba Nitaweka mkono Wangu juu ya miili yao, kana kwamba Mimi ni ncha ya bunduki iliyoelekezwa kila wakati kwenye kifua cha mwanadamu, na tena, kana kwamba yeye ni adui Yangu, na bado ni rafiki yangu. Mwanadamu hajawahi kwa kweli kufahamu nia Yangu kwake, hajawahi hata siku moja kufahamu makusudi Yangu ya kweli hivyo basi bila ya kujua, hukosea dhidi Yangu, bila ya kujua, hunipinga, ilhali, bila kutaka, ameona kiasi cha upendo Wangu. Ni vigumu binadamu kuona uso Wangu wakati wa ghadhabu Yangu. Nimejificha nyuma ya mawingu ya hasira Yangu na Ninasimama, kati ya mingurumo ya radi, juu ya ulimwengu wote na kutuma huruma Zangu chini kwa mwanadamu. Kwa sababu ya mwanadamu kukosa maarifa kunihusu, Simwadibu kwa kukosa kujua nia Yangu kwake. Mbele ya macho ya binadamu, Mimi huweka wazi ghadhabu Yangu mara kwa mara, Ninatabasamu mara kwa mara, lakini hata anaponiona, mwanadamu kweli hajawahi kuona ukamilifu wa tabia Yangu, na bado hana uwezo wa kusikia kelele za furaha na uwazi, kwa sababu amejaa upumbavu na ujinga. Ni kana kwamba umbo Langu linakaa katika kumbukumbu ya mwanadamu, na nafsi Yangu katika mawazo yake. Hata hivyo, hapana Yule ambaye amewahi kuniona kwa kweli kati ya ukuaji wa wanadamu wote, kwa sababu akili za binadamu zina upungufu wa hali ya juu. Kwa yote ambayo mwanadamu “amenichambua”, sayansi ya jamii ya mwanadamu haina mizizi na, kufikia sasa, utafiti wake wa kisayansi haujaibua matokeo kamilifu. Na hivyo basi, mada ya “umbo Langu” imekuwa daima tupu pasiwe na yeyote wa kuijaza, hakuna wa kuivunja rekodi ya dunia kwa sababu ili mwanadamu aweze kuweka mguu wake imara katika ulimwengu wa sasa ni kifuta machozi kisichokadirika katika matukio makuu yenye majonzi.
Machi 23, 1992