Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

`

Tamko la Ishirini na Nne

Kuadibu kwangu kunawajia watu wote, lakini pia kunakaa mbali na watu wote. Maisha yote ya kila mtu yamejaa upendo na pia chuki Kwangu, na hakuna mtu ambaye amewahi kunijua na kwa hivyo mtazamo wa mwanadamu Kwangu ni wa sitasita, na hauna uwezo wa kuwa kawaida. Lakini Nimekuwa Nikimlea na kumchunga mwanadamu na ni kwa sababu ya upumbavu wake ndiyo maana hana uwezo wa kuona matendo Yangu yote na kuelewa nia Zangu. Mimi Ndiye Ninayeongoza katika mataifa yote, na ndiye Mkubwa Zaidi kwa watu wote; kwa ufupi ni kwamba mwanadamu hanijui Mimi. Kwa miaka mingi Nimeishi na mwanadamu na kujionea Maisha katika dunia ya mwanadamu, lakini amekuwa Akinipuuza na kunichukulia kama kiumbe kutoka ulimwengu wa nje ya dunia. Kwa sababu hii, kutokana na tofauti za tabia na lugha, watu Hunichukulia Mimi kama mgeni barabarani. Nguo Zangu, huenda ikawa, pia ni za kipekee, hata kumfanya mwanadamu kukosa imani ya kunikaribia. Ni wakati huo ndio naona upweke wa maisha ya mwanadamu, na wakati huo tu ndio Ninapata ufafanuzi wa dhuluma katika dunia ya mwanadamu. Ninatembea katikati ya wapita njia, Nikiangalia nyuso zao zote. Ni kama kwamba wanaishi ndani ya maradhi, ambayo yanajaza nyuso zao na huzuni, na miongoni mwa adhabu, inayozuia kuachiliwa kwao. Mwanadamu hujitia pingu mwenyewe na kujifedhehesha mwenyewe. Watu wengi hujenga hisia za uwongo juu yao mbele Yangu ili Niwaunge mkono, watu wengi hujifanya makusudi kuwa wa kuhuzunisha mbele Yangu ili waweze kupata usaidizi Wangu. Nyuma Yangu, watu wote hunidanganya na kuniasi. Je, Mimi sio wa kweli? Je, huu si mkakati wa mwanadamu ili aweze kuishi? Ni nani ambaye ameweza kuishi kulingana na mfano Wangu maishani mwake? Nani ambaye ameweza kunitukuza miongoni mwa wengine? Nani amewahi kuwajibika mbele ya Roho? Nani ambaye amesimama imara kwa ushuhuda wake Kwangu mbele ya Shetani? Ni nani ameweza kuongezea ukweli kwa uaminifu wake Kwangu? Ni nani amewahi kuangamizwa na joka kubwa jekundu kwa sababu Yangu? Watu wametupa kura zao kwa shetani, wamekuwa wataalam kwa Kunipinga, na wamekuwa waanzilishi wa upinzani kuja Kwangu, na wamehitimu katika kunifanyia Mimi mzaha. Kwa ajili ya hatima yake mwenyewe, mwanadamu anatafuta hapa na pale duniani; Ninapomwita, anabaki bila fahamu ya thamani Yangu kubwa na anaendelea kuwa na Imani katika kujitegemea, asiwe mzigo kwa wengine. Matarajio ya mwanadamu ni ya thamani, lakini hakujawahi kuwa na matarajio ya yeyote ambayo yametimiza alama zote. Yote yanabomoka mbele Yangu, na kuporomoka bila sauti.

Kila siku Ninaongea, na kila siku Nafanya mambo mapya pia. Ikiwa mwanadamu hawezi kutumia nguvu zake zote, basi atakuwa na ugumu kusikia sauti Yangu na atapata ugumu kuona uso wangu. Mpendwa Anaweza kuwa sawa, na mazungumzo Yake kuwa ya upole, lakini mwanadamu hana uwezo wa kutazama kwa urahisi sura Yake tukufu na kusikia sauti Yake. Katika miaka yote, hakuna ambaye amewahi kuweza kutazama sura Yangu kwa urahisi. Niliwahi kuongea na Petro na Nikajitokeza kwa Paulo, na hakuna mwingine—isipokuwa Waisraeli—ambaye kweli amewahi kuona uso Wangu. Leo, nimekuja Mimi Mwenyewe kati ya mwanadamu kuishi pamoja na yeye. Je, hiki hakihisi kuwa kitu nadra na cha thamani kwenu? Je, hamtamani kufanya matumizi bora ya muda wenu? Je, mnataka jambo hili liwapite kwa njia hii? Inawezekana muda usimamishwe ghafula katika mawazo ya watu? Au inawezekana muda urudishwe nyuma? Au inawezekana mwanadamu awe kijana tena? Inawezekana maisha ya leo yenye baraka kuja tena? Simpatii mwanadamu "zawadi" sahihi kwa "ubadhirifu" wake. Mimi huendelea kufanya kazi Yangu tu, nimejitenga na mengine yote na sisimamishi mtiririko wa masaa kwa sababu mwanadamu ana shughuli, au kwa sababu ya sauti ya vilio vyake. Kwa miaka elfu kadhaa, hakuna ambaye ameweza kugawa nguvu Yangu, na hakuna ambaye ameweza kuharibu mpango Wangu wa asili. Nitavuka anga, na kuzunguka miaka, na kuanzisha kiini cha Mpango Wangu mzima juu na miongoni mwa vitu vyote. Hakuna ambaye ameweza kupokea utunzaji maalum kutoka Kwangu, hakuna aliyeweza kupata "tuzo" iliyo mikononi Mwangu. Na hata kama watu wamefungua vinywa vyao na kuomba Kwangu, na hata kama, bila kujali mambo mengine yote, wamenyosha mikono yao ya kufanya madai Kwangu, hakuna madai yoyote ambayo yameniathiri, na wao wote wamesukumwa nyuma na sauti Yangu "isiyo na utu." Watu wengi bado wanaamini kuwa wao ni "wachanga sana," na hivyo wanasubiri Niwaonyeshe rehema kubwa, kuwa na huruma kwao kwa mara ya pili, na wanauliza Niwaruhusu kuchukua mlango wa nyuma. Hata hivyo ni jinsi gani Mimi Nitaufanyia mpango Wangu mzaha? Je, Ninaweza kusimasisha dunia isizunguke kwa ajili ya ujana wa mwanadamu, ili aweze kuishi miaka zaidi duniani? Akili ya mwanadamu ni tata, lakini inaonekana kwamba pia kuna vitu ambavyo inakosa. Kwa sababu hii, katika akili ya mwanadamu mara nyingi huonekana "njia za ajabu" za kupinga kazi Yangu kwa makusudi.

Ingawa ni mara nyingi Nimesamehe dhambi za mwanadamu, na kumwonyesha upendeleo wa pekee kwa sababu ya udhaifu wake, mara nyingi

Iliyotangulia:Tamko la Ishirini na Tatu

Inayofuata:Tamko la Ishirini na Tano

Unaweza Pia Kupenda