Sura ya 18

Kujenga kanisa si kitu rahisi cha kufanya! Niliweka moyo Wangu wote katika kulijenga na Shetani angefanya kila kitu ingeweza kuibomoa. Kama unataka kujengwa lazima uwe na maono; lazima uishi maisha kwa Mimi, kuwa shahidi wa Kristo, shikilia Kristo juu kwa juu, na kuwa mwaminifu Kwangu. Hupaswi kutoa visingizio, lakini badala yake kutii bila ya sharti; lazima uvumilie majaribu yoyote, na kukubali yote yanayotoka kwa Mimi. Lazima ufuate chochote Roho Mtakatifu hufanya ili Akuongoze wewe. Lazima uwe na roho hodari na uwezo wa kutofautisha mambo. Ni lazima uelewe watu na usifuate wengine kwa upofu, weka macho yako ya kiroho nga’vu na umiliki elimu kamilifu ya mambo. Watu ambao ni wa akili sawa na Mimi lazima wawe shahidi Kwangu Mimi na kupigana vita vya kuamua dhidi ya Shetani. Lazima uwe umejengwa na kupigana vita. Mimi nipo miongoni mwenu, Ninawasaidia na Mimi ndiye kimbilio lenu.

Shughuli ya kwanza ni kujitakasa, kuwa mtu aliyebadilika, na kuwa na mwenendo imara. Lazima uishi kwa Mimi katika mazingira mazuri na mabaya, na kama uko nyumbani au katika sehemu zingine, usisite kwa sababu ya mtu mwingine, au kwa sababu ya baadhi ya tukio au kitu. Na lazima usimame imara na, kama kawaida, ishi kwa kudhihirisha Kristo na kumdhihirisha Mungu Mwenyewe. Lazima ufanye shughuli zako na kutimiza wajibu wako kama kawaida; hii haitendeki yote mara moja, lakini lazima iendelezwe. Lazima uchukue Moyo Wangu kama moyo wako, dhamira Zangu lazima ziwe mawazo yako, lazima ufikirie hali yote kwa ujumla, ruhusu Kristo Aanzie kwako, na utumikie kwa kushirikiana na wengine. Lazima uende kwa kasi sawa na kazi ya Roho Mtakatifu na ujiegemeze katika mbinu ya wokovu wa Roho Mtakatifu. Lazima ujifanye tupu na kuwa mtu asiye na hatia na mtu aliye wazi. Lazima ushiriki kwa kawaida pamoja na ndugu na dada zako, muwe na uwezo wa kufanya mambo katika roho, wapende, ruhusu nguvu zao kusawazisha udhaifu wako, tafuta kujengwa katika kanisa. Ni wakati huo tu ambapo utakuwa na sehemu katika ufalme.

Iliyotangulia: Sura ya 17

Inayofuata: Sura ya 19

Maudhui Yanayohusiana

Kuhusu Desturi ya Sala

Nyinyi hamtilii maanani sala katika maisha yenu ya kila siku. Watu daima wamepuuza sala. Hapo awali sala zilikuwa za uzembe, huku...

Kazi na Kuingia (4)

Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya...

Njia … (1)

Katika maisha yake, hakuna mtu anayejua ni aina gani ya vipingamizi atakavyoenda kukutana navyo, wala hajui ni aina gani ya kusafishwa...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki