Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Tendeni Ukweli Mara Mnapouelewa

Kazi na neno la Mungu vina maana ya kuleta mabadiliko katika tabia zenu; lengo Lake si kuwafanya tu kulielewa au kulitambua na kufanya hilo kuwa mwisho wa jambo hilo. Kama mmoja wa uwezo wa kupokea, hampaswi kuwa na ugumu katika kuelewa neno la Mungu, kwa kuwa wingi wa neno la Mungu limeandikwa kwa lugha ya kibinadamu ambayo ni rahisi sana tu kuelewa. Kwa mfano, mnaweza kujua ni nini Mungu anataka muelewe na kutenda; hili ni jambo ambalo mtu wa kufaa ambaye ana uwezo wa uelewa anapaswa kuwa na uwezo wa kufanya. Maneno ya Mungu sasa ni hasa wazi na bayana, na Mungu husema mambo mengi ambayo watu hawajachukulia maanani au hali mbalimbali za mtu. Maneno yake yanajumuisha yote, angavu kama nuru ya mwezi kamili. Hivyo sasa, watu wanaelewa masuala mengi; wanachokosa ni kuweka neno Lake katika vitendo. Lazima watu wapitie vipengele vyote vya ukweli kwa kina, na kuutafiti na kuutafuta kwa undani zaidi, sio kusubiri tu kuchukua kile ambacho wamepewa bila shida; vinginevyo wanakuwa wadogo zaidi ya barakala. Wanajua neno la Mungu, lakini hawaliweki katika vitendo. Mtu wa aina hii hana upendo wa ukweli, na hatimaye ataondolewa. Kuwa na mtindo kama Petro wa miaka ya tisini inamaanisha ya kwamba kila mmoja wenu anapaswa kutenda neno la Mungu, kuwa na kuingia kwa kweli katika uzoefu wenu na kupata hata zaidi na hata nuru kubwa katika kushirikiana kwenu na Mungu, kuleta hata zaidi ya msaada Wake katika maisha yenu. Kama mmesoma sana neno la Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandishi na hamna maarifa ya kwanza ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu wa vitendo, hamtajua neno la Mungu. Ili mradi unahusika, neno la Mungu si maisha, lakini barua bila uhai. Na kama unaamini tu barua bila uhai, huwezi kufahamu kiini cha neno la Mungu, wala kuelewa mapenzi Yake. Wakati tu unapitia neno Lake katika uzoefu wako halisi ndio maana ya kiroho ya neno la Mungu itafunguka yenyewe kwako, na ni katika uzoefu tu ambapo unaweza kufahamu maana ya kiroho ya ukweli mwingi, na ni kwa kupitia tu uzoefu ndio unaweza kufungua mafumbo ya neno la Mungu. Usipoliweka katika vitendo, basi haijalishi jinsi neno Lake lilivyo wazi, jambo pekee ambalo umefahamu ukashikilia ni barua tupu na mafundisho, ambayo yamekuwa kanuni za dini kwako. Si hili ndilo Mafarisayo walifanya? Kama mtatenda na kupitia neno la Mungu, linakuwa vitendo kwenu; msipotafuta kulitenda, basi neno la Mungu kwenu ni kidogo zaidi ya hadithi ya mbingu ya tatu. Kwa kweli, mchakato wa kuamini katika Mungu ni mchakato wenu kupitia neno Lake pamoja na kupatwa na Yeye, au kuliweka wazi zaidi, kuamini katika Mungu ni kuwa na maarifa na ufahamu wa neno Lake na kupitia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake; huo ndio ukweli wa imani yenu katika Mungu. Kama mnaamini katika Mungu na mna matumani ya uzima wa milele bila kutafuta kutenda neno la Mungu kama kitu mlicho nacho ndani yenu, basi nyinyi ni wapumbavu; ni kama kwenda karamuni tu kuangalia yaliyo huko ya kula bila kweli kuyajaribu. Si mtu kama huyo ni mpumbavu?

Ukweli ambao mtu anahitaji kumiliki unapatikana katika neno la Mungu, ukweli ambao ni faida zaidi na manufaa kwa mtu. Ni lishe na riziki ambayo miili yenu inahitaji, kitu ambacho huwasaidia kurejesha ubinadamu wenu wa kawaida, ukweli ambao mnapaswa kujiandaa nao. Zaidi mnavyotenda neno la Mungu, kwa haraka ndivyo zaidi maisha yenu yatachanua; zaidi mnavyotenda neno la Mungu, ndio wazi ukweli unakuwa. Mnavyokua katika kimo, mtaona mambo ya ulimwengu wa kiroho wazi zaidi, na mtakuwa na nguvu zaidi ya ushindi juu ya Shetani. Sehemu kubwa ya ukweli ambao hamuelewi itakuwa wazi wakati unatenda neno la Mungu. Watu wengi wameridhika na kuelewa tu maandiko ya neno la Mungu na kuzingatia katika kujiandaa wenyewe na mafundishi bila kupitia kina chake katika vitendo; si hiyo ni njia ya Mafarisayo? Jinsi gani kirai “Neno la Mungu ni uzima” kikawa ukweli kwao, basi? Wakati tu mtu anatenda neno la Mungu ndio maisha yake yanaweza kweli kuchanua; maisha hayawezi kukua tu kwa kusoma neno Lake. Kama ni imani yako ya kwamba kuelewa neno la Mungu ni kila kinachohitajika kuwa na maisha, kuwa na kimo, basi kuelewa kwako ni potovu. Kuelea kwa kweli neno la Mungu hutokea wakati unatenda ukweli, na ni lazima uelewe ya kwamba “ni kwa kutenda tu ukweli kunaweza kueleweka siku zote.” Leo, baada ya kusoma neno la Mungu, unaweza tu kusema ya kwamba unajua neno la Mungu, lakini huwezi kusema ya kwamba unalielewa. Baadhi wanasema kuwa njia pekee ya kutenda ukweli ni kuelewa ukweli kwanza, lakini hii ni nusu tu ya haki na sio sahihi kabisa. Kabla uwe na maarifa ya ukweli, bado hujapitia ukweli huo. Kuhisi ya kwamba unaelewa unachosikia sio kitu kimoja kama kweli kuelewa. Kujiandaa mwenyewe na ukweli kama inavyoonekana katika maandishi si sawa na kuelewa maana halisi humo. Kwa sababu tu una ufahamu wa ukweli juu juu haina maana ya kwamba kweli unaelewa ukweli au kuutambu; maana halisi ya ukweli inatokana na kuwa na uzoefu wake. Ndio maana nasema ya kwamba wakati tu unapitia ukweli ndio unaweza kuuelewa, na wakati tu unapitia ukweli ndio unaweza kufahamu sehemu ya undani wake. Kuwa na uzoefu wa ukweli kwa kina ni njia pekee ya kufahamu kidokezo cha ukweli, na kuelewa kiini chake. Kwa hivyo, unaweza kwenda kila mahali na ukweli, lakini kama hakuna ukweli ndani yako, usifikirie hata kujaribu kuwashawishi watu wa kidini, kwa kiasi kidogo familia yako. Utakuwa kama kupepea kwa theluji bila ukweli, lakini kwa ukweli, unaweza kuwa na furaha na huru, ambapo hakuna awezaye kukushambulia. Haijalishi nadharia ina nguvu jinsi gani, haiwezi kushinda ukweli. Kwa ukweli, dunia yenyewe inaweza kutetemeka na milima na bahari kuhamishwa, wakati ambapo ukosefu wa ukweli unasababisha uharibifu na mabuu; huu ndio ukweli.

Cha muhimu sasa ni kujua ukweli kwanza, kisha uuweke katika vitendo, na kujiandaa wenyewe zaidi na maana halisi ya ukweli. Hilo ndio linapaswa kuwa lengo lako, sio tu watu kufanya wengine kufuata maneno yako lakini kuwafanya wafuate matendo yako, na ni katika hili tu unaweza kupata kitu cha maana. Bila kujali yanayokupata, bila kujali unayekutana naye, unaweza tu kusimama imara na ukweli. Neno la Mungu ndilo huleta maisha kwa mtu, sio kifo. Kama baada ya kusoma neno la Mungu hupati uzima, lakini bado umekufa baada ya kusoma neno Lake, basi kuna kitu kibaya na wewe. Kama baada ya muda fulani umesoma kiasi cha neno la Mungu na umesikia mahubiri mengi ya vitendo, lakini bado uko katika hali ya mauti, huu ni uthibitisho kuwa wewe si yule huthamini ukweli, wala mtu ambaye hutafuta ukweli. Kama kweli mngetafuta kumpata Mungu, hamngezingatia kujiandaa wenyewe na mafundisho ya juu na kuyatumia kuwahimiza wengine, lakini badala yake kuzingatia kupitia neno la Mungu na kuweka ukweli katika vitendo; si katika hilo ndio mnapaswa muingie ndani sasa?

Kuna muda mdogo kwa Mungu kufanya kazi Yake ndani yako, lakini kunaweza kuwa na matokeo yapi kama hushirikiani na yeye? Kwa nini daima Mungu huwataka kutenda neno Lake mara mnapolielewa? Ni kwa sababu Mungu amedhihirisha maneno Yake kwenu, na hatua yenu ifuatayo ni kweli kuyatenda, na Mungu atatekeleza kazi ya kutoa nuru na mwongozo wakati mnatenda maneno haya. Hivyo ndivyo jinsi ilivyo. Neno la Mungu linawekwa ili kuruhusu mtu kuchanuka maishani bila kusababisha kupotoka au ubaya. Unasema umesoma neno la Mungu na kulitenda, lakini hujapokea kazi yoyote ya Roho Mtakatifu—unachosema kinaweza tu kudanganya mtoto. Binadamu hajui kama nia zako ni sahihi, lakini unafikiri Mungu hawezijua? Ni jinsi gani basi wengine wanatenda neno la Mungu na wanapokea nuru ya Roho Mtakatifu, na bado kwa namna fulani unatenda neno Lake na hupokei nuru ya Roho Mtakatifu? Je, Mungu ni wa kihisia? Kama nia zako ni kweli nzuri na wewe ni mshirika, basi Roho wa Mungu atakuwa pamoja nawe. Mbona baadhi ya watu mara zote hutaka kuchukua nafasi maarufu, na bado Mungu hamruhusu kuinuka na kuongoza kanisa? Kwa nini baadhi ya watu hutimiza tu kazi yao na bila kuijua, wanapata kibali cha Mungu? Hilo linaweza kuwaje? Mungu huchunguza moyo, na watu ambao wanatafuta ukweli lazima wafanye hivyo kwa nia njema—watu ambao hawana nia njema hawawezi kusimama. Katika msingi wake, lengo lenu ni kuruhusu neno la Mungu kufanya kazi ndani yenu. Kwa maneno mengine, ni kuwa na uelewa wa kweli wa neno la Mungu katika kulitenda kwenu. Labda uwezo wenu wa kupokea neno la Mungu ni duni, lakini mnapotenda neno la Mungu, Yeye anaweza kubadilisha uwezo wenu duni kupokea, hivyo sio lazima tu mjue ukweli mingi, lakini pia ni lazima mtende huo ukweli. Hili ndilo lengo kubwa zaidi ambalo hauwezi kupuuzwa. Yesu aliteseka sana katika miaka yake 33½ kwa sababu Yeye alitenda ukweli. Kwa nini daima inasemwa katika rekodi ya kwamba Yeye aliteswa? Ni kueleza ni kiasi gani Yeye aliteseka kwa sababu Yeye alitenda ukweli na kutimiza mapenzi ya Mungu. Hangepitia mateso kama Yeye angejua ukweli bila kutenda ukweli huo. Kama Yesu angefuata mafunzo ya Wayahudi, na angefuata Mafarisayo, basi Yeye hangeteseka. Unaweza kujifunza kutoka kwa matendo ya Yesu ya kwamba ufanisi wa kazi ya Mungu juu ya mtu unatokana na ushirikiano wake, na hili ni jambo ambalo lazima mtambue. Je, Yesu angeteseka kama Yeye alivyofanya msalabani kama Yeye hangekuwa ametenda ukweli? Je, Yeye angeomba sala la huzuni kama hilo kama Yeye hangekuwa ametenda kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu? Basi hii ina maana ya kwamba hii ndio aina ya mateso mtu anapaswa kuvumilia.

Iliyotangulia:Kuhusu Mungu Kumtumia Mwanadamu

Inayofuata:Mtu Ambaye Hupata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Radhi Kutenda Ukweli