Utangulizi

Sehemu hii ya maneno ya Mungu ina jumla ya vifungu vinne; vilionyeshwa na Kristo kati ya Juni ya 1992 na Septemba ya 2005. Nyingi zao zimetegemezwa kwa rekodi za mahubiri na ushirika wa Kristo alipokuwa Akitembea miongoni mwa makanisa. Hazijabadilishwa kwa namna yoyote, wala hazijageuzwa baadaye na Kristo. Sehemu zilizobaki ziliandikwa na Kristo binafsi (Kristo anapoandika, Anafanya hivyo katika kikao kimoja, bila kusita ili kufikiria ama kufanya uhariri wowote, na maneno Yake ni maonyesho ya Roho Mtakatifu kikamilifu—hili ni jambo la hakika). Badala ya kutenganisha hizi aina mbili za matamshi, tumeziwasilisha pamoja, tukitumia mpangilio wa asili ambao ulitumiwa kuzionyesha; hili linatuwezesha kuona hatua za kazi ya Mungu kutoka kwa matamshi Yake yote, na kuelewa jinsi Anavyofanya kazi wakati wa kila awamu, jambo ambalo linafaidi ufahamu wa watu wa hatua za kazi ya Mungu na maarifa ya Mungu.

Sura nane za kwanza za “Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani I”—zinazojulikana kwa jumla kama “Njia”—ni sehemu ndogo ya maneno yaliyonenwa na Kristo alipokuwa sawa na mwanadamu. Licha ya jinsi zinavyoonekana kukosa ladha, zimejaa upendo na kujali kwa Mungu kuhusu wanadamu. Kabla ya hili, Mungu alizungumza kutoka kwa mtazamo wa mbingu ya tatu, jambo lililosababisha utengano mkubwa kati Yake na mwanadamu, na kuwafanya watu waogope kumkaribia Mungu, sembuse kumwomba Ayaruzuku maisha yao. Kwa hivyo, katika “Njia”, Mungu alimzungumzia mwanadamu kama aliyelingana naye na kuonyesha mwelekeo wa njia, hivyo kurejesha uhusiano wa mwanadamu na Mungu katika hali yake ya asili; watu hawakushuku tena iwapo Mungu bado alikuwa akitumia mbinu ya kuzungumza, na hawakusumbuliwa tena na hofu kuu ya jaribio la kifo. Mungu alishuka kutoka mbingu ya tatu hadi duniani, watu wakaja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kutoka katika ziwa la moto na kiberiti, wakatupilia mbali kivuli cha “watendaji huduma,” na kama ndama waliozaliwa karibuni, wakakubali kirasmi ubatizo wa maneno ya Mungu. Ni hapo tu ndipo Mungu aliweza kuzungumza nao waziwazi na kufanya kazi zaidi ya kuwapa uzima. Lengo la Mungu kujinyenyekeza kama mtu lilikuwa ili Awakaribie watu zaidi, hivyo kupunguza utengano kati yao na Yeye, na kumwezesha Apate utambuzi na imani ya watu, na kuwatia watu moyo wasadiki kufuatilia uzima na kumfuata Mungu. Sura nane za “Njia” zinaweza kufupishwa kama funguo ambazo Mungu hutumia kufungua milango ya mioyo ya watu, na kwa pamoja zinaunda tembe inayovutia ambayo Anampa mwanadamu. Mungu anapofanya hili tu ndipo watu wanaweza kutilia maanani mafundisho na makaripio ambayo Yeye hurudiarudia. Inaweza kusemekana kwamba ilikuwa tu baada ya hapa ndiyo Mungu alianza kirasmi kazi ya kutoa uzima na kuonyesha ukweli katika hatua hii ya sasa ya kazi, Alipokuwa akiendelea kuzungumza: “Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini” na “Kwenye Hatua za Kazi ya Mungu”…. Je, mbinu kama hii haionyeshi maarifa ya Mungu na makusudi Yake ya ari? Huu ndio mwanzo kabisa wa Mungu kutoa uzima, kwa hiyo ukweli huu ni wa juujuu kiasi kuliko sehemu zinazofuata. Kanuni ya hili ni rahisi sana: Mungu hufanya kazi kulingana na mahitaji ya wanadamu. Hatendi wala kuzungumza bila kufikiri; ni Mungu pekee anayeelewa mahitaji ya wanadamu kikamilifu, na hakuna mwingine anayempenda na kumfahamu mwanadamu zaidi.

Katika tamko la kwanza hadi tamko la kumi katika “Kazi na Kuingia,” maneno ya Mungu yanaingia katika awamu mpya. Matokeo yake ni kwamba matamshi haya yanawekwa mwanzoni. Kisha, “Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani II” ilitokea. Wakati wa awamu hii, Mungu aliwatolea wafuasi Wake matakwa ya utondoti zaidi, matakwa yaliyojumuisha ufahamu kuhusu mitindo ya maisha ya watu, kinachohitajika kutoka kwa ubora wao wa tabia, na kadhalika. Kwa sababu watu hawa walikuwa wameazimia kumfuata Mungu, na hawakuwa tena na shaka kuhusu utambulisho na asili ya Mungu, Mungu pia alianza kirasmi kuwachukulia kama washirika wa familia Yake mwenyewe, Akishiriki ukweli wa ndani wa kazi ya Mungu kutoka wakati wa uumbaji hadi leo, Akifichua ukweli wa Biblia, na kuwafunza maana ya kweli ya Mungu kupata mwili. Matamshi ya Mungu katika sehemu hii yaliwapa watu ufahamu mzuri zaidi wa asili ya Mungu na asili ya kazi Yake, na yakawawezesha kutambua vyema kwamba kile walichopata kutoka kwa wokovu wa Mungu kilipita kile ambacho manabii na mitume walipata katika enzi zote zilizopita. Kutoka kwa kila mstari wa maneno ya Mungu, unaweza kuona busara Yake yote, na vilevile upendo mwadilifu na kumjali Kwake mwanadamu. Kando na kuonyesha maneno hayo, moja baada ya nyingine Mungu alifichua hadharani fikira na makosa ya awali ya mwanadamu na mambo ambayo watu hawakuwa wamewahi kufikiri, na pia njia ambayo watu walipaswa kuitembea baadaye. Huenda hili hasa ndilo “upendo” mdogo ambao mwanadamu anaweza kupitia! Hata hivyo, Mungu alikuwa amewapa watu yote waliyohitaji, na alikuwa amewapa kile walichotaka, bila kuzuia chochote ama kutaka kulipwa.

Sura kadhaa maalumu katika fungu hili zinazungumzia Biblia. Biblia imekuwa sehemu ya historia ya binadamu kwa miaka mingi. Zaidi ya hayo, watu huichukulia kuwa Mungu, kufikia kiwango ambapo katika siku za mwisho, imechukua nafasi ya Mungu, jambo ambalo linamchukiza Mungu. Hivyo, muda uliporuhusu, Mungu alihisi kulazimishwa kubainisha maelezo ya ndani na vyanzo vya Biblia; Asingefanya hivi, Biblia ingeendelea kushikilia nafasi ya Mungu mioyoni mwa watu, na watu wangetumia maneno ya Biblia kupima na kushutumu matendo ya Mungu. Kwa kuelezea asili, muundo na dosari za Biblia, Mungu hakuwa akikana kuwepo kwa Biblia hata kidogo, wala Hakuwa anaishutumu; badala yake, Alikuwa akitoa maelezo yaliyofaa na kustahili yaliyorejesha picha asilia ya Biblia, Akazungumzia suitafahamu za watu kuhusu Biblia, na kuwapa maoni sahihi ya Biblia, ili wasiiabudu Biblia tena, na wasipotee tena; yaani, ili wasichanganye tena imani yao pofu ya Biblia kuwa imani katika Mungu na ibada ya Mungu, wakihofia hata kukabili usuli na dosari zake za kweli. Mara tu watu wanapopata ufahamu wa Biblia usiochanganywa na mambo duni, wanaweza kuiweka kando bila majuto na kuyakubali maneno mapya ya Mungu kwa ujasiri. Hili ndilo lengo la Mungu katika sura hizi kadhaa. Ukweli ambao Mungu angetaka kuwaambia watu hapa ni kwamba hakuna nadharia ama ukweli ambao unaweza kuchukua nafasi ya kazi na maneno ya Mungu ya leo, na kwamba hakuna kitu kinachoweza kuwa mbadala wa Mungu. Ikiwa watu hawawezi kuepuka mtego wa Biblia, hawatawahi kuweza kuja mbele za Mungu. Ikiwa wanataka kuja mbele za Mungu, lazima kwanza waitakase mioyo yao na kuondoa chochote kinachoweza kuchukua nafasi Yake; kisha watamridhisha Mungu. Ingawa Mungu anaifafanua Biblia pekee hapa, usisahau kwamba kuna mambo mengi yenye makosa ambayo watu wanayaabudu kwa kweli kando na Biblia; mambo wasiyoyaabudu ni yale yanayotoka kwa Mungu kwa kweli pekee. Mungu anatumia tu Biblia kama mfano kuwakumbusha watu wasichukue njia mbaya, na wasivuke mipaka tena na kukanganyikiwa wanapomwamini Mungu na kukubali maneno Yake.

Maneno ambayo Mungu anampa mwanadamu yanageuka kutoka kuwa ya juujuu hadi kuwa ya kina. Mada za matamshi Yake husonga kutoka kwa tabia na matendo ya nje ya watu kuelekea tabia zao potovu, ambapo Mungu hutumia lugha Yake kulenga vina vya nafsi za watu: asili yao. Katika kipindi ambapo “Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani III” yalinenwa, matamshi ya Mungu yanasisitiza Asili na Utambulisho wa Mwanadamu, na maana ya kuwa mtu halisi—ukweli huu wa kina na maswali muhimu kuhusu watu kuingia katika uzima. Bila shaka, tukikumbuka ukweli ambao Mungu humpa mwanadamu katika “Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani I,” kwa kulinganishwa maudhui ya “Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani III,” ni ya kina sana. Maneno katika sehemu hii yanagusia njia ya watu ya baadaye na jinsi wanavyoweza kukamilishwa; pia yanagusia hatima ya baadaye ya wanadamu, na jinsi Mungu na mwanadamu wataingia pumzikoni pamoja. (Inaweza kusemekana kwamba hadi wa leo, haya ndiyo maneno ambayo Mungu amenena kwa watu kuhusu asili, misheni na hatima yao ambavyo ndivyo rahisi zaidi kuelewa.) Ni tumaini la Mungu kwamba watu wanaosoma maneno haya ni wale waliojitenga na fikira na mawazo ya binadamu, wanaoweza kufahamu vyema kila neno la Mungu kwa dhati. Aidha, Anatumai kwamba wale wote wanaoyasoma maneno haya wanaweza kuyachukulia maneno Yake kuwa ukweli, njia na uzima, na kwamba wasimtendee Mungu bila umakini ama kumrairai. Watu wakiyasoma maneno haya kwa mtazamo wa kumchunguza ama kumwangalia Mungu kwa makini, basi matamshi haya yatakuwa kama fumbo kwao. Ni wale tu wanaofuatilia ukweli, wanaodhamiria kumfuata Mungu, na wasio na shaka hata kidogo kumhusu ndio wanaostahili kuyakubali maneno haya.

“Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani IV” ni aina nyingine ya tamko takatifu inayofuata “Sehemu ya Pili Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima.” Sehemu hii inajumuisha ushawishi, mafundisho na ufunuo wa Mungu kwa watu katika madhehebu ya Kikristo, kama vile: “Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia,” “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu.” Pia inajumuisha mahitaji maalum zaidi ya Mungu kwa wanadamu, kama vile: “Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako,” “Maonyo Matatu,” “Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu.” Vipengele vingi vimezungumziwa, kama vile ufunuo na hukumu ya watu wa aina zote na maneno kuhusu jinsi ya kumjua Mungu. Inaweza kusemekana kwamba fungu hili ndilo kiini cha Mungu kuwahukumu wanadamu. Sehemu isiyoweza kusahaulika kabisa ya fungu hili la matamshi ya Mungu ni kwamba, Mungu alipokuwa karibu kukamilisha kazi Yake, Alifichua kile kilicho katika asili ya watu: usaliti. Madhumuni Yake ni watu wajue ukweli ufuatao mwishowe kabisa, na kuacha ukite mizizi mioyoni mwao: Haijalishi umekuwa mfuasi wa Mungu kwa muda upi—asili yako bado ni kumsaliti Mungu. Yaani, ni asili ya mwanadamu kumsaliti Mungu, kwa sababu watu hawawezi kupevuka kabisa maishani mwao, na kunaweza tu kuwa na mabadiliko madogo katika tabia zao. Ingawa sura hizi mbili, “Usaliti (1)” na “Usaliti (2),” zinawashtua watu, kweli ni maonyo halisi na karimu zaidi ya Mungu kwa watu. Angalau kabisa, wakati watu wameridhika mno na ni wenye majivuno, baada ya kuzisoma sura hizi mbili, uovu wao wenyewe utazuiwa na watatulia. Kupitia sura hizi mbili, Mungu anawakumbusha watu wote kwamba bila kujali jinsi maisha yako yalivyopevuka, jinsi uzoefu wako ulivyo wa kina, jinsi ujasiri wako ulivyo mkuu, bila kujali ulikozaliwa na unakoenda, asili yako ya kumsaliti Mungu inaweza kujifichua wakati wowote na mahali popote. Mungu anataka kumwambia kila mtu jambo hili: Ni asili ya kuzaliwa ya kila mtu kumsaliti Mungu. Bila shaka, nia ya Mungu ya kueleza sura hizi mbili si kupata sababu za kuwaondoa ama kuwashutumu wanadamu, ila ni kuwafanya watu wafahamu zaidi asili ya mwanadamu, ili waweze kuishi kwa uangalifu mbele za Mungu nyakati zote kupokea mwongozo Wake, jambo litakalowazuia kupoteza uwepo wa Mungu na kuingia kwenye njia mbaya. Hizi sura mbili ni onyo kwa wale wote wanaomfuata Mungu. Matumaini ni kwamba watu wataelewa nia za ari za Mungu; kwani maneno haya yote ni ukweli usiopingika—kwa hivyo mwanadamu ana haja gani ya kubishana kuhusu ni lini ama ni namna gani zilinenwa na Mungu? Ikiwa Mungu angejiwekea haya mambo yote, na Asubiri hadi watu walipoona wakati ulifaa wa Yeye kuzinena, muda haungekuwa umepita sana? Wakati huo unaofaa zaidi ungekuwa upi?

Mungu hutumia mbinu na mitazamo mingi katika hizi sehemu nne. Kwa mfano, wakati mwingine Anatumia tashtiti, na wakati mwingine Anatumia mbinu ya ruzuku na mafundisho ya moja kwa moja; wakati mwingine Anatumia mifano, na wakati mwingine Anatumia makaripio makali. Kwa jumla, kuna mbinu tofauti za kila aina, na lengo la mbinu hizi ni kuridhisha hali na mapendeleo mbalimbali ya watu. Mtazamo Anaotumia kuzungumza unabadilika kulingana na mbinu na maudhui tofauti ya matamshi Yake. Kwa mfano, wakati mwingine Anasema “Mimi”; yaani, Anawazungumzia watu kutoka kwa mtazamo wa Mungu Mwenyewe. Wakati mwingine Anazungumza kutoka kwa nafsi ya tatu, Akisema “Mungu” ni hili ama lile, na kuna nyakati nyingine Anapozungumza kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu. Bila kujali mtazamo Anaozungumza kutoka, asili Yake haibadiliki, kwani haijalishi Anavyozungumza, kila kitu Anachonena ni asili ya Mungu Mwenyewe—yote ni ukweli, na ndiyo ambayo wanadamu wanahitaji.

Iliyotangulia: Sura ya 46

Inayofuata: Njia … (1)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp