Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Ni Wale tu Wanaolenga Vitendo Ndio Wanaweza Kufanywa kuwa Watimilifu

Katika siku za mwisho, Mungu alikuwa mwili ili kufanya kazi Anayopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja binafsi kufanya kazi miongoni mwa wanadamu kwa lengo la kuwafanya watimilifu watu wale wanaopendeza roho Yake. Tangu uumbaji hadi leo Anafanya tu kazi hiyo katika siku za mwisho. Ni katika siku za mwisho tu ndipo Mungu alikuwa mwili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa kama hicho. Ingawa Anastahimili mateso ambayo watu wataona vigumu kustahimili, ingawa Yeye kama Mungu mkuu ana unyenyekevu wa kuwa binadamu wa kawaida, hakuna kipengele cha kazi Yake kimecheleweshwa, na mpango wake hauvurugwi hata kidogo. Anafanya kazi kulingana na mpango Wake asilia. Mojawapo wa kusudi la huku kupata mwili ni kuwashinda watu. Lingine ni kuwafanya watu Anaowapenda kuwa watimilifu. Anapenda kuwaona watu Anaowafanya kuwa watimilifu kwa macho Yake mwenyewe, na Anataka kujionea mwenyewe jinsi watu Anaowafanya kuwa watimilifu wanavyomtolea ushuhuda. Si mtu mmoja anayefanywa kuwa mtimilifu, na si wawili. Bali ni kundi la watu wachache sana. Kundi hili la watu linatoka sehemu mbalimbali za nchi za dunia, na kutoka mataifa mbalimbali ya dunia. Kusudi la kufanya kazi hii nyingi ni kulipata kundi hili la watu, kuupata ushuhuda ambao kundi hili la watu humtolea, na kuupata utukufu Anaoupata kupitia kundi hili la watu. Hafanyi kazi ambayo haina maana, wala Hafanyi kazi ambayo haina thamani. Inaweza kusemwa kwamba, kwa kufanya kazi nyingi sana, lengo la Mungu ni kuwafanya kuwa watimilifu wale wote ambao Anataka kufanya kuwa watimilifu. Katika muda Wake wote wa ziada nje ya hili, Atawaangamiza wale ambao ni waovu. Fahamu kuwa Hafanyi kazi hii kubwa kwa sababu ya walio waovu; hasha, Anajitolea kabisa kwa sababu ya idadi hiyo ndogo ya watu ambao wanapaswa kufanywa kuwa watimilifu na Yeye. Kazi Anayoifanya, maneno Anayoyazungumza, miujiza Anayoifichua, na hukumu Yake na kuadibu vyote ni kwa ajili ya idadi hiyo ndogo ya watu. Hakupata mwili kwa ajili ya wale ambao ni waovu, sembuse kuchochea ghadhabu ndani Yake. Anasema ukweli, na Anazungumzia kuingia, kwa sababu ya wale ambao wanapaswa kufanywa kuwa watimilifu, Alipata mwili kwa ajili yao, na ni kwa sababu yao Anatoa ahadi na baraka Zake. Ukweli, kuingia, na maisha katika ubinadamu ambayo Anayazungumzia si kwa ajili ya walio waovu. Anataka kuepuka kuzungumza na walio waovu, na kutaka kuwapa ukweli wote wale wanaopaswa kufanywa kuwa watimilifu. Lakini kazi Yake inahitaji kwamba, kwa sasa, wale ambao ni waovu waruhusiwe kufaidi baadhi ya hizi fadhila. Wale ambao hawatekelezi ukweli, wasiomridhisha Mungu, na wanaoingilia kazi Yake wote ni waovu. Hawawezi kufanywa kuwa watimilifu, na wanachukiwa na kukataliwa na Mungu. Kwa upande wa pili, watu wanaotia ukweli katika vitendo na wanaweza kumridhisha Mungu na kujitumia kikamilifu katika kazi ya Mungu ndio watu wanaopaswa kufanywa na Mungu kuwa watimilifu. Wale ambao Mungu anataka kuwakamilisha si wengine bali ni kundi hili la watu, na kazi anayoifanya Mungu ni kwa ajili ya watu hawa. Ukweli Anaouzungumzia unaelekezwa kwa watu ambao wako tayari kuuweka katika vitendo. Hazungumzi na watu ambao hawauweki ukweli katika vitendo. Kuongezeka kwa umaizi na kukua kwa utambuzi Anakozungumzia kumekusudiwa watu ambao wanaweza kutekeleza ukweli. Anapozungumza kuhusu wale ambao wanaopaswa kufanywa kuwa watimilifu huwa Anawazungumzia watu hawa. Kazi ya Roho Mtakatifu imeelekezwa kwa watu wanaoweza kutekeleza ukweli. Mambo kama kuwa na busara na kuwa na ubinadamu yanaelekezwa kwa watu ambao wako radhi kuuweka ukweli katika vitendo. Wale ambao hawatekelezi ukweli wanaweza kusikia ukweli mwingi na wanaweza kuelewa ukweli mwingi, ila kwa sababu wako miongoni mwa watu waovu, ukweli wanaoufahamu unakuwa mafundisho na maneno tu, na hauna maana katika mabadiliko yao ya tabia au kwa maisha yao. Hakuna hata mmoja wao ambaye ni mwaminifu kwa Mungu; wote ni watu ambao humwona Mungu lakini hawawezi kumpata, na wote wamelaaniwa na Mungu.

Roho Mtakatifu ana njia ya kutembea ndani ya kila mtu, na humpa kila mtu fursa za kufanywa kuwa mtimilifu. Kupitia uhasi wako unafanywa kuujua ubovu wako mwenyewe, na kisha kupitia kuutupilia mbali uhasi utapata njia ya utendaji, na huku ndiko kufanywa kwako kuwa mtimilifu. Aidha, kupitia ushauri wa siku zote na mwangaza wa baadhi ya mambo chanya yaliyo ndani yako, utatimiza kwa vitendo kazi yako na kukua katika umaizi na kupata utambuzi. Wakati hali zako ni nzuri, hasa unakuwa radhi kusoma neno la Mungu, na hasa uko radhi kumwomba Mungu, na unaweza kuhusisha mahubiri unayoyasikia na hali zako mwenyewe. Katika nyakati kama hizo Mungu anakupa nuru na kukuangazia kwa ndani, Akikufanya ugundue baadhi ya mambo ya hali chanya. Huku ni kukufanya mtimilifu katika hali chanya. Katika hali hasi, uko mnyonge na mhasi, na kuhisi kuwa huna Mungu, walakini Mungu anakuangazia, Akikusaidia upate njia ya kutenda. Kinachotokana na hili ni kupata utimilifu kwa hali hasi. Mungu anaweza kumfanya mwanadamu kuwa mtimilifu kwa hali chanya na hata hasi. Inategemea na kama unaweza kupitia, na kama unafuatilia kufanywa na Mungu kuwa mtimilifu. Kama unatafuta kwa kweli kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu, basi yale mambo mabaya hayawezi kuchukua chochote kutoka kwako, lakini yanaweza kukuletea mambo ambayo ni halisi zaidi, na yanaweza kukufanya kuweza kujua zaidi kile ambacho kinakosekana ndani yako, kukufanya kuweza kuelewa zaidi hali yako halisi, na kuhakikisha kwamba mwanadamu hana chochote, na hana thamani yoyote; kama hutapitia majaribio, huyajui haya, na siku zote utahisi kwamba unawazidi wengine na kwamba wewe ni bora zaidi ya kila mtu mwingine. Kupitia haya yote utatambua kwamba yale yote uliyoyapitia awali yalifanywa na Mungu na kulindwa na Mungu. Kuingia katika majaribu hukuwacha bila upendo au imani, unakosa maombi, na huwezi kuimba nyimbo za kuabudu—na, bila ya kutambua, katikati ya haya yote unakuja kujijua. Mungu anazo mbinu nyingi za kumfanya binadamu kuwa mtimilifu. Yeye hutumia namna zote za mazingira ili kushughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia mambo mbalimbali ya kumweka mwanadamu wazi; kwa njia moja Anamshughulikia binadamu, kwa njia nyingine Anamweka mwanadamu wazi, na kwa njia nyingine Anamfichua mwanadamu, Akichunguza na kufichua “siri” zilizomo katika kina cha moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kufichua hali zake nyingi. Mungu humfanya mwanadamu kuwa mtimilifu kupitia mbinu nyingi—kupitia kwa ufunuo, kumshughulikia, utakasaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa matendo.

Mnatafuta nini sasa? Labda ni kutaka mfanywe na Mungu kuwa watimilifu, kumjua Mungu, kumpata Mungu, au ni mtindo wa Petro wa miaka ya tisini, au ni kuwa na imani kubwa kuliko ile ya Ayubu. Mnaweza kutafuta mengi, iwe ni kutaka kuitwa wenye haki na Mungu na kufika mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, au muweze kumdhihirisha Mungu duniani na kumtolea Mungu ushuhuda mkubwa na wa nguvu. Bila kujali mnatafuta nini, kwa ujumla, ni kwa ajili ya mpango wa usimamizi wa Mungu. Haijalishi kama unataka kuwa mtu mwenye haki, au unatafuta mtindo wa Petro, au imani ya Ayubu, au kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu, chochote kile unachokitafuta, kwa jumla, yote ni kazi ya Mungu. Kwa maneno mengine, bila kujali unachokitafuta, yote ni kwa ajili ya kufanywa na Mungu kuwa mtimilifu, yote ni kwa ajili ya kupitia neno la Mungu, kuuridhisha moyo wa Mungu; yote ni kwa ajili ya kuutambua uzuri wa Mungu, yote ni kwa ajili ya kutafuta njia ya kutenda katika mapitio ya kweli kwa kusudi la kuweza kuitupilia mbali tabia yako ya uasi, kuifikia hali ya kawaida ndani yako mwenyewe, kuweza kabisa kukubaliana na mapenzi ya Mungu, kuwa mtu sahihi, na kuwa na nia njema kwa kila jambo utendalo. Sababu yako kupitia haya mambo yote ni kufika katika kumjua Mungu na kutimiza ukuaji wa maisha. Ingawa unayoyapitia ni neno la Mungu, na unayoyapitia ni matukio halisi, watu, masuala, na vitu katika mazingira yako, mwishowe unaweza kumjua Mungu na kufanywa na Mungu kuwa mtimilifu. Kutaka kutembea katika njia ya mwenye haki au kutaka kuweka neno la Mungu katika vitendo, hizi ndizo njia. Kumjua Mungu na kufanywa na Mungu kuwa mtimilifu ndizo hatima. Ikiwa unataka kufanywa na Mungu kuwa mtimilifu sasa, au kumtolea Mungu ushuhuda, kwa ujumla, ni ili mwishowe umjue Mungu; ni ili kwamba kazi Aifanyayo ndani yako isiwe bure, ili kwamba mwishoni upate kuujua ukweli wa Mungu, kuujua ukubwa Wake, na zaidi kuujua unyenyekevu na usiri wa Mungu, na kuijua kazi nyingi Aifanyayo Mungu ndani yako. Mungu amejinyenyekesha kwa kiwango fulani, kufanya kazi Yake katikati ya watu hawa wachafu na waovu, na kulifanya kuwa timilifu kundi hili la watu. Mungu hakupata tu mwili ili kuishi na kula miongoni mwa watu, kuwachunga watu, kutoa kinachohitajika na watu. La muhimu zaidi ni kuwa Anafanya kazi Yake kubwa ya wokovu na ushindi juu ya watu hawa waovu kupindukia. Alikuja kwenye kiini cha joka kuu jekundu kuwafinyanga watu hawa waovu kupindukia, ili kwamba watu wote waweze kubadilishwa na kufanywa wapya. Mateso makubwa ambayo Mungu hustahimili si tu mateso ambayo Mungu mwenye mwili hustahimili, lakini muhimu ni kwamba Roho wa Mungu anapitia fedheha kupita kiasi—Anajinyenyekesha na kujificha sana kiasi kwamba Anakuwa mwanadamu wa kawaida. Mungu alipata mwili na kuchukua umbo la mwili ili kwamba watu waone kuwa Ana maisha ya kawaida ya binadamu, na kwamba Ana mahitaji ya kawaida ya binadamu. Hili linatosha kuthibitisha kuwa Mungu amejinyenyekesha kwa kiwango fulani. Roho wa Mungu anapatikana katika mwili. Roho Wake ni wa juu na mkubwa sana, lakini Anachukua umbo la mwanadamu wa kawaida, umbo la mtu mdogo sana kufanya kazi ya Roho Wake. Ubora wa tabia, ufahamu, busara na ubinadamu wenu, na maisha ya kila mmoja wenu vinaonyesha kuwa hamfai kuikubali kazi ya Mungu ya aina hii. Hamfai kabisa kumfanya Mungu astahimili mateso hayo kwa ajili yenu. Mungu ni mkubwa sana. Yeye ni mkuu sana, na watu ni wakatili na duni, lakini bado Anafanya kazi juu yao. Hakupata mwili tu ili kuwapa watu riziki, kuzungumza na watu, vilevile hata Anaishi pamoja na watu. Mungu ni mnyenyekevu sana, ni mwenye kupendeka sana. Ikiwa mara tu upendo wa Mungu unapotajwa, mara tu neema ya Mungu inapotajwa, unadondosha machozi ukitoa sifa kuu, kama unafikia hii hali, basi una ufahamu wa kweli wa Mungu.

Kuna mkengeuko katika utafutaji wa watu siku hizi; wanataka tu kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu, lakini hawana uelewa wowote wa Mungu, na wametelekeza nuru na mwangaza wa Roho Matakatifu ndani yao. Hawana uelewa wa kweli wa Mungu kama msingi. Kwa njia hii wanapoteza nguvu kadri uzoefu wao unavyoongezeka. Wale wote wanaotafuta kuwa na ufahamu wa kweli wa Mungu, aina ya mtu ambaye zamani hakuwa katika hali nzuri, aliyeelekea kwa uhasi na udhaifu, ambaye mara kwa mara alimwaga machozi, aliishia kuvunjika moyo, na kukatishwa tamaa; watu kama hao sasa wanaongezeka kuwa katika hali bora kwa kuwa wana tajriba kubwa. Baada ya kupitia hali ya kushughulikiwa na kuvunjwa, au kupitia tukio la kutakaswa, wamepiga hatua kubwa. Hali kama hiyo haionekani kuwafika tena, tabia zao zimebadilika, na upendo wa Mungu unaishi kwa kudhihirishwa ndani yao. Kuna kanuni katika Mungu kuwafanya watu kuwa watimilifu, ambayo ni kwamba Anakupa nuru kwa kutumia sehemu yako inayopendeza hivi kwamba una njia ya kutenda na unaweza kujitenga na hali zote hasi, kusaidia roho yako kupata uhuru, na kukufanya uwe na uwezo zaidi wa kumpenda. Kwa namna hii unakuwa na uwezo wa kutupilia mbali tabia potovu ya Shetani. Wewe ni usiye na hila na uko wazi, radhi kujijua, na radhi kuweka ukweli katika vitendo. Mungu anaona kuwa uko radhi kujijua na uko radhi kuweka ukweli katika vitendo, kwa hivyo unapokuwa mnyonge na hasi, Anakupa nuru mara mbili, Akikusaidia kujijua zaidi, kuwa radhi zaidi kujitubia mwenyewe, na kuwa na uwezo zaidi wa kutenda mambo ambayo unapaswa kutenda. Ni kwa njia hii tu ndipo moyo wako unakuwa na amani na utulivu. Mtu ambaye kwa kawaida anatilia maanani kumjua Mungu, ambaye anatilia maanani kujijua yeye mwenyewe, ambaye anayatilia maanani matendo yake atakuwa na uwezo wa kupokea kazi ya Mungu mara kwa mara, kupokea mara kwa mara ushauri na nuru kutoka kwa Mungu. Hata ingawa katika hali hasi, anaweza kubadilika mara moja, iwe ni kutokana na tukio la utambuzi au kutokana na kupata nuru kutoka kwa neno la Mungu. Mabadiliko ya tabia ya mtu yanapatikana mara zote anapoijua hali yake halisi na kujua tabia na kazi ya Mungu. Mtu ambaye yuko radhi kujijua na yuko radhi kujiweka wazi ataweza kutekeleza ukweli. Mtu wa aina hii ni mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, na mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu ana ufahamu wa Mungu, uwe wa kina au wa juu juu, duni au tele. Hii ni haki ya Mungu, na ni kitu ambacho watu hupata, ni faida yao wenyewe. Mtu aliye na ufahamu wa Mungu ni ambaye ana msingi, ambaye ana maono. Mtu wa aina hii ana uhakika kuhusu mwili wa Mungu, ana uhakika kuhusu neno la Mungu, ana uhakika kuhusu kazi ya Mungu. Haijalishi Mungu anafanya kazi vipi au anazungumza vipi, au ni vipi watu wengine wanasababisha machafuko, anaweza kushikilia msimamo wake, na kumshuhudia Mungu. Kadri mtu anavyokuwa wa namna hii ndivyo anavyoweza zaidi kutekeleza ukweli anaoufahamu. Kwa sababu daima anatenda neno la Mungu, anapata ufahamu zaidi wa Mungu na anakuwa na uamuzi wa kumshuhudia Mungu milele.

Kuwa na utambuzi, kuwa na unyenyekevu, na kuwa na uwezo wa kuelewa mambo ili kwamba uwe makini katika roho ina maana kuwa maneno ya Mungu yanakuangazia na kukupa nuru ndani yako punde tu unapokabiliana na jambo. Huku ni kuwa makini katika roho. Kila kitu Anachokifanya Mungu ni kwa ajili ya kufufua roho za watu. Je, kwa nini Mungu husema kila wakati kuwa watu ni wenye ganzi na ni wapumbavu? Ni kwa sababu roho za watu zimekufa, na wamekuwa wenye ganzi kiasi kwamba hawana fahamu ya mambo ya kiroho. Kazi ya Mungu ni kufanya maisha ya watu yaendelee na ni kusaidia roho za watu kuchangamka, ili ziweze kuelewa mambo ya kiroho, na kuwa na uwezo wa kumpenda Mungu, kumridhisha Mungu. Kwa Kufikia hapa inaonyesha kuwa roho ya mtu imehuishwa, na wakati mwingine atakapokabiliana na kitu chochote, anaweza kujibu papo hapo. Anaitikia miito, na kuzishughulikia hali kwa hima. Huku ndiko kuwa na umakini wa kiroho. Wapo watu wengi ambao wanajibu haraka tukio la nje, lakini punde tu kuingia katika uhalisia au mambo yenye maelezo ya kina katika roho yanapotajwa, wanakosa kujali na kuwa wapumbavu. Wanaelewa jambo kama tu lipo usoni mwao. Hizi zote ni dalili za kuwa mzito kiroho na mpumbavu, za kuwa na uzoefu mdogo wa vitu vya kiroho. Watu wengine ni makini kiroho na wana utambuzi. Punde tu wanasikia kitu kimeelekezwa kwa hali zao hawapotezi muda wowote katika kukiandika chini. Wanakitumia katika uzoefu wao unaofuata, na kujibadilisha wao wenyewe. Huyu ni mtu mwenye umakini kiroho. Na ni kwa nini ana uwezo wa kujibu haraka namna hiyo? Kwa sababu anaangazia hali hizi katika maisha ya kila siku, na mara tu mojawapo ya hizi hali zinapotajwa, inatokea kulingana na hali yake ya ndani, na anaweza kuipokea mara moja. Ni sawa na kumpa chakula mtu aliye na njaa; anaweza kula mara moja. Ukimpa chakula mtu asiye na njaa, hakichangamkii mara moja. Unaomba kwa Mungu mara kwa mara, na unaweza kukabiliana mara moja unapokabiliana na jambo lolote: anachokihitaji Mungu katika hili jambo, na jinsi unavyofaa kutenda. Mungu alikuelekeza katika jambo hili wakati uliopita; unapokabiliana na jambo kama hili leo unajua jinsi ya kulikabili, kuuridhisha moyo wa Mungu. Kama unatenda kwa njia hii kila wakati na kupitia njia hii kila wakati, upo wakati utakuwa na ujuzi wa jambo hilo. Unaposoma neno la Mungu unajua ni mtu wa aina gani Mungu anarejelea, unafahamu ni hali zipi za kiroho Anazozizungumzia, na una uwezo wa kushika jambo lililo muhimu na kuliweka katika matendo; hii inaonyesha kwamba una uwezo wa kupitia. Ni kwa nini watu wengi wanapungukiwa katika jambo hili? Ni kwa sababu hawaweki juhudi nyingi sana katika hali ya matendo. Ingawa wako tayari kuweka ukweli katika matendo, hawana ufahamu wa kweli wa maelezo ya huduma, wa maelezo ya ukweli katika maisha yao. Wanachanganyikiwa wakati kitu kinafanyika. Kwa njia hii, unaweza kupotoshwa wakati unapatana na nabii wa uongo au mtume wa uongo. Haikubaliki kupuuza utambuzi. Ni lazima daima utilie maanani vitu vya kiroho: jinsi Mungu anavyofanya kazi, anachokizungumza Mungu, ni yapi mahitaji ya Mungu kwa watu, ni aina gani ya watu unapaswa kuwasiliana nao, na ni aina gani ya watu unapaswa kuepuka. Ni lazima utilie mkazo mambo haya unapokula na kunywa neno la Mungu na wakati wa kupitia uzoefu. Ikiwa unapitia mambo kwa njia hii kila mara, utaelewa kikamilifu mambo mengi, na utakuwa na utambuzi pia. Ni nini kufundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu, ni nini lawama itokanayo na kusudi la mwanadamu, ni nini mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini mpango wa mazingira, maneno ya Mungu yanatia nini nuru ndani, kama huko dhahiri kuhusu mambo haya, hutakuwa na utambuzi. Unapaswa kujua kinachotoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini tabia ya uasi, jinsi ya kutii neno la Mungu, na jinsi ya kuacha uasi wa kibinafsi wa mtu; unapaswa kuelewa maelezo ya ukweli huu wote, ndipo jambo likifanyika, uwe una ukweli wa kufaa wa kulilinganishia, una maono ya kufaa kama msingi, una msimamo katika kila jambo na uwe na uwezo wa kutenda kulingana na ukweli. Wakati huo maisha yako yatakuwa yamejaa nuru ya Mungu, yamejaa baraka za Mungu. Mungu hatamtesa mtu yeyote anayemtafuta kwa dhati. Hatamtesa mtu yeyote ambaye anaishi kwa kumdhihirisha na kumtolea ushuhuda na hatamlaani mtu yeyote anayetamani ukweli. Kama, utakapokuwa unakula na kunywa maneno ya Mungu, unaweza kuzingatia hali yako mwenyewe ya kweli, kuzingatia matendo yako mwenyewe, na kuzingatia uelewa wako mwenyewe, basi, unapokumbana na tatizo, utapokea nuru na utapata uelewa wa kimatendo. Hivyo basi utakuwa na njia ya matendo na kuwa na utambuzi wa kila jambo. Mtu ambaye ana ukweli ni vigumu kudanganyika, na ni vigumu kuwa na tabia inayovuruga au kutenda kwa ziada. Amelindwa kwa sababu ya ukweli, na pia kwa sababu ya ukweli anapata uelewa zaidi. Kwa sababu ya ukweli ana njia nyingi za kutenda, na hupata nafasi zaidi za Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yake, na nafasi zaidi za kufanywa kuwa mtimilifu.

Iliyotangulia:Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake

Inayofuata:Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani

Unaweza Pia Kupenda