Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu

Je, ushawishi wa giza ni nini? “Ushawishi wa giza” ni ushawishi wa Shetani kuwadanganya, kuwapotosha kuwafunga na kuwatawala watu; ushawishi wa shetani ni ushawishi ambao una hali ya kifo. Wale wote ambao wanaishi chini ya miliki ya shetani wamehukumiwa kuangamia. Unawezaje kuepuka ushawishi wa giza baada ya kupata imani katika Mungu? Baada ya kumwomba Mungu kwa dhati, unaelekeza moyo wako Kwake kikamilifu. Katika hatua hii, moyo wako unasongezwa na Roho wa Mungu, uko tayari kujitoa mwenyewe kikamilifu, na katika wakati huu, umeepuka ushawishi wa giza. Kama yote ambayo mtu anafanya yanampendeza Mungu na anapatana na matakwa Yake, basi yeye ni mtu ambaye anaishi ndani ya maneno ya Mungu, yeye ni mtu anayeishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu. Kama watu hawawezi kutenda maneno ya Mungu, daima wakimpumbaza na kutenda katika namna ya uzembe na Yeye, na hawaamini katika uwepo Wake, watu kama hao wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Watu ambao hawajapokea wokovu wa Mungu wote wamemilikiwa na Shetani, yaani, hao wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wale ambao hawamwamini Mungu wamemilikiwa na Shetani. Hata wale ambao wanaamini katika kuwepo kwa Mungu huenda si lazima wawe wanaishi katika nuru ya Mungu, kwa sababu wale ambao wanamwamini huenda si lazima wawe wanaishi ndani ya maneno ya Mungu, na huenda si lazima wawe watu ambao wanaweza kumtii Mungu. Mtu anamwamini tu Mungu, na kwa sababu ya kushindwa kwake kumjua Mungu, bado anaishi ndani ya sheria za zamani, anaishi ndani ya maneno yaliyokufa, anaishi katika maisha ambayo ni giza na si ya hakika, hajatakaswa kikamilifu na Mungu au kupatwa kikamilifu na Mungu. Kwa hivyo, ni dhahiri ya kwamba wale wasiomwamini Mungu wanaishi chini ya ushawishi wa giza, hata wale ambao wanamwamini Mungu huenda wakawa bado wanaishi chini ya ushawishi wake, kwa ajili Roho Mtakatifu hajatekeleza kazi juu yao. Wale ambao hawajapokea neema ya Mungu au rehema ya Mungu, na wale ambao hawawezi kuona kazi ya Roho Mtakatifu, wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza; wale ambao wanafurahia tu neema ya Mungu na bado hawamjui pia wanaishi chini ya ushawishi wa giza wakati mwingi. Kama mtu anamwamini Mungu na bado anatumia wakati mwingi wa maisha yake akiishi chini ya ushawishi wa giza, basi kuwepo kwa mtu huyu kumepoteza maana yake, bila kutaja wale ambao hawaamini katika uwepo wa Mungu.

Wale wote ambao hawawezi kukubali kazi ya Mungu au wanaokubali kazi ya Mungu lakini hawawezi kukidhi matakwa Yake wanaishi chini ya ushawishi wa giza; wale tu wanaofuatilia ukweli na wana uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu watapokea baraka kutoka Kwake, na ni wao tu wataepuka ushawishi wa giza. Watu ambao hawajafunguliwa, ambao siku zote wamedhibitiwa na mambo fulani na ambao hawawezi kutoa mioyo yao kwa Mungu, ni watu ambao wako chini ya utumwa wa Shetani, na wanaoishi chini ya hali ya kifo. Wale wasio waaminifu kwa wajibu wao wenyewe, wasio waaminifu kwa agizo la Mungu na wale ambao hawatekelezi jukumu lao kanisani wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wale ambao husumbua maisha ya kanisa kimakusudi, wale ambao huharibu mahusiano kati ya akina ndugu na kimakusudi, au kuweka pamoja magenge yao wenyewe, wanaishi hata zaidi chini ya ushawishi wa giza; wao wanaishi ndani ya utumwa wa Shetani. Wale walio na uhusiano usio sahihi na Mungu, walio na tamaa za kifahari daima, ambao daima wanataka kupata faida, na ambao kamwe hawatafuti mabadiliko katika tabia yao ni watu ambao wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wale ambao hawako imara daima, ambao hawajatilia maanani utendaji wao wa ukweli, na ambao hawatafuti kukidhi matakwa ya Mungu ila kuridhisha tu miili yao wenyewe ni watu ambao pia wanaishi chini ya ushawishi wa giza na kufunikwa katika kifo. Wale ambao hujihusisha na hila na udanganyifu wakati wa kutekeleza kazi ya Mungu, ambao wanashughulikia Mungu katika njia ya kizembe, wanamdanganya Mungu, na ambao daima hujifikiria, ni watu wanaoishi chini ya ushawishi wa giza. Wale wote ambao hawawezi kumpenda Mungu kwa dhati, ambao hawafuatilii ukweli, na wasiozingatia kubadilisha tabia yao, wanaishi chini ya ushawishi wa giza.

Kama unataka kusifiwa na Mungu, lazima kwanza uepuke ushawishi wa giza wa Shetani, ufungue moyo wako kwa Mungu, na uuelekeze kwa Mungu kikamilifu. Je, mambo ambayo unafanya kwa sasa yanasifiwa na Mungu? Umeelekeza moyo wako kwa Mungu? Je, mambo ambayo umeyafanya ni yale ambayo Mungu ametaka kutoka kwako? Je, yanaingiana na ukweli? Lazima ujichunguze kila wakati, uzingatie kula na kunywa maneno ya Mungu, uweke moyo wako wazi mbele Yake, umpende kwa uwazi, na ujitumie kwa bidii kwa ajili ya Mungu. Watu kama hao hakika watapokea sifa ya Mungu. Wote ambao humwamini Mungu ilhali hawafuatilii ukweli hawana namna ya kuepuka ushawishi wa shetani. Wale wote ambao hawaishi maisha yao kwa uaminifu, wanaotenda kwa njia moja mbele ya wengine na njia nyingine kwa siri, wanaotoa mwonekano wa unyenyekevu, uvumilivu, na upendo ilhali katika kiini ni wenye kudhuru kwa siri, wana hila, na hawana uaminifu kwa Mungu—watu hawa ni mfano halisi wa wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza. Wao ni wa kizazi cha nyoka. Wale ambao imani yao katika Mungu daima ni kwa ajili ya faida zao wenyewe, ambao ni wa kujidai na wenye maringo, ambao hujigamba, na hulinda hadhi zao wenyewe ni wale wanaompenda Shetani na kuupinga ukweli. Wao wanapinga Mungu na ni wa Shetani kikamilifu. Wale ambao hawako makini kwa mizigo ya Mungu, ambao hawamtumikii Mungu kwa moyo wote, ambao daima wanajali maslahi yao wenyewe na maslahi ya familia zao, ambao hawawezi kuacha kila kitu ili wajitumie kwa ajili ya Mungu, na ambao kamwe hawaishi kulingana na maneno Yake wanaishi nje ya maneno ya Mungu. Watu kama hawa hawawezi kupokea sifa ya Mungu.

Wakati Mungu aliumba watu, ilikuwa ili kuwafanya wafurahie utajiri Wake na wampende kwa kweli; katika njia hii, watu wangeishi katika nuru Yake. Leo, wote ambao hawawezi kumpenda Mungu, ambao hawako makini kwa mizigo Yake, ambao hawawezi kutoa mioyo yao kikamilifu kwa Mungu, ambao hawawezi kuchukua moyo wa Mungu kama wao wenyewe, ambao hawawezi kubeba mizigo ya Mungu kama yao wenyewe—nuru ya Mungu haiangazi juu ya watu wowote kama hawa, kwa hivyo, wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wako kwenye njia ambayo huenda kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu, na yote wanayoyafanya hayana hata chembe ya ukweli. Wanazamia katika matatizo na Shetani na ni wale ambao wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Kama unaweza daima kula na kunywa maneno ya Mungu na pia kuwa makini na mapenzi Yake na kutenda maneno Yake, basi wewe ni wa Mungu, na wewe ni mtu anayeishi ndani ya maneno ya Mungu. Je, uko tayari kuepuka kumilikiwa na Shetani na kuishi katika nuru ya Mungu? Kama unaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atakuwa na nafasi ya kutenda kazi Yake; kama unaishi chini ya ushawishi wa Shetani, basi Roho Mtakatifu hatakuwa na nafasi ya kutenda kazi yoyote. Kazi ambayo Roho Mtakatifu hutenda kwa watu, nuru ambayo Yeye huangaza kwa watu, na imani ambayo Yeye hutoa kwa watu hukaa kwa muda tu; kama hawako makini na hawampi kipaumbele, kazi iliyotendwa na Roho Mtakatifu itawapita. Kama watu wanaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atakuwa pamoja nao na kutenda kazi juu yao; kama watu hawaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi wanaishi ndani ya utumwa wa Shetani. Watu wanaoishi katika tabia ya kiufisadi hawana uwepo wala kazi ya Roho Mtakatifu. Kama unaishi ndani ya nyanja ya maneno ya Mungu, kama unaishi katika hali inayohitajika na Mungu, basi wewe ni Wake na kazi Yake itatendwa juu yako; kama huishi ndani ya nyanja ya matakwa ya Mungu lakini badala yake unamilikiwa na Shetani, basi hakika wewe unaishi chini ya upotovu wa Shetani. Ni kwa kuishi ndani ya maneno ya Mungu tu na kutoa moyo wako Kwake, ndipo unaweza kukidhi matakwa Yake; lazima ufanye asemavyo Mungu, lazima ufanye maneno ya Mungu msingi wa kuwepo kwako na hali halisi ya maisha yako, na ni hapo tu ndipo utakuwa wa Mungu. Kama kwa dhati unatenda kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, Atatenda kazi juu yako na kisha utaishi chini ya baraka za Mungu, uishi katika nuru ya uso wa Mungu, kufahamu kazi ambayo Roho Mtakatifu hutenda, na pia kuhisi furaha ya uwepo wa Mungu.

Kuepuka ushawishi wa giza, lazima kwanza uwe mwaminifu kwa Mungu na kuwa na hamu ya kufuatilia ukweli—ni hapo tu ndipo utakuwa na hali sahihi. Kuishi katika hali sahihi ndilo sharti la mwanzo la kuepuka ushawishi wa giza. Kukosa hali sahihi ina maana kwamba wewe si mwaminifu kwa Mungu na ya kwamba huna hamu ya kutafuta ukweli. Basi, kuepuka ushawishi wa giza hakutawezekana. Mtu kuepuka ushawishi wa giza ni kwa msingi wa maneno Yangu, na kama mtu hawezi kutenda kwa mujibu wa maneno Yangu, hataepuka utumwa wa ushawishi wa giza. Kuishi katika hali sahihi ni kuishi chini ya uongozi wa maneno ya Mungu, kuishi katika hali ya kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuishi katika hali ya kutafuta ukweli, kuishi katika uhalisi wa kugharamia rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa dhati, kuishi katika hali ya kumpenda Mungu kwa kweli. Wale ambao wanaishi katika hali hizi na ndani ya hali halisi hii watabadilika hatua kwa hatua wanapoingia ndani zaidi katika ukweli, nao watabadilika kwa kuongezeka kwa kazi, mpaka hatimaye hakika watapatwa na Mungu, na watakuja kwa kweli kumpenda Mungu. Wale ambao wameepuka ushawishi wa giza wataweza kufahamu mapenzi ya Mungu hatua kwa hatua, wataelewa mapenzi ya Mungu hatua kwa hatua, na hatimaye kuwa wasiri wa Mungu. Hawatakosa dhana kumhusu Mungu tu, na kukosa uasi dhidi Yake, lakini watakuja kuchukia hata zaidi dhana na uasi ambao walikuwa nao kabla, kusababisha upendo wa kweli kwa Mungu mioyoni mwao. Wale ambao hawawezi kuepuka ushawishi wa giza wanashughulika na miili yao, na wamejaa uasi; mioyo yao imejazwa dhana za kibinadamu na falsafa za kuishi, pamoja na nia zao na majadiliano. Mungu anataka upendo mmoja wa mtu, naye humhitaji mtu amilikiwe na maneno Yake na upendo wa mtu Kwake. Kuishi ndani ya maneno ya Mungu, kugundua kile ambacho mtu anapaswa kutafuta kutoka ndani ya maneno Yake, kumpenda Mungu kama matokeo ya maneno Yake, kukimbiakimbia kwa ajili ya maneno ya Mungu, kuishi kwa ajili ya maneno ya Mungu—haya yote ni mambo ambayo mtu anapaswa kufikia. Kila kitu lazima kijengwe kulingana na maneno ya Mungu, na hapo tu ndipo mtu ataweza kukidhi matakwa ya Mungu. Kama mwanadamu hajatayarishwa na maneno ya Mungu, basi yeye ni funza tu ambaye amemilikiwa na Shetani. Yapime moyoni mwako mwenyewe—ni maneno mangapi ya Mungu ambayo umekita mizizi yake ndani yako? Ni katika mambo gani unaishi kulingana na maneno Yake? Ni katika mambo gani ndiyo hujakuwa ukiishi kulingana nayo? Kama maneno ya Mungu hayajakumiliki kikamilifu, basi ni nini hasa kilicho moyoni mwako? Katika maisha yako ya kila siku, je, unadhibitiwa na Shetani, au unamilikiwa na maneno ya Mungu? Je, maombi yako yameanzishwa kutoka kwa maneno Yake? Je, umeondoka katika hali yako mbaya kupitia nuru ya maneno ya Mungu? Kuchukua maneno ya Mungu kama msingi wa kuwepo kwako, hili ndio jambo kila mtu anapaswa kuingia ndani. Kama maneno ya Mungu hayapo katika maisha yako, basi unaishi chini ya ushawishi wa giza, wewe ni muasi dhidi ya Mungu, unampinga Mungu, na huheshimu jina Lake—imani ya watu kama hao katika Mungu ni uharibifu na usumbufu kabisa. Je, ni kiasi gani cha maisha yako kimeishiwa kwa mujibu wa maneno Yake? Ni kiasi gani cha maisha yako hakijaishiwa kwa mujibu wa maneno Yake? Je, ni kiasi gani cha kile ambacho maneno ya Mungu yamehitaji kwako kimetimizwa ndani yako? Ni mangapi yamepotea ndani yako? Je, umechunguza mambo kama hayo kwa karibu?

Kuepuka ushawishi wa giza, kipengele kimoja ni kwamba kunahitaji kazi ya Roho Mtakatifu, na kipengele kingine ni kwamba kunahitaji ushirikiano wa kujitolea kutoka kwa mtu. Mbona Nasema ya kwamba mtu hayuko kwenye njia sahihi? Kwanza, kama mtu yuko kwenye njia sahihi, ataweza kutoa moyo wake kwa Mungu, ambayo ni jukumu linalohitaji muda mrefu kuingia ndani kwa sababu mwanadamu daima amekuwa akiishi chini ya ushawishi wa giza na amekuwa chini ya utumwa wa Shetani kwa maelfu ya miaka. Kwa hivyo, kuingia huku hakuwezi kupatikana katika siku moja au mbili. Nilileta suala hili leo ili watu waweze kuwa na ufahamu wa hali yao wenyewe; kuhusu ushawishi wa giza ni nini na kuishi ndani ya nuru ni nini, kuingia kunawezekana wakati mtu ana uwezo wa kutambua mambo haya. Hii ni kwa sababu ni lazima ujue ushawishi wa Shetani ni nini kabla uuepuke, na hapo tu ndipo utakuwa na njia ya kuuepuka hatua kwa hatua mwenyewe. Kuhusu ni nini cha kufanya baada ya hapo, hilo ni suala la wanadamu wenyewe. Lazima daima uingie kutoka mtazamo mwema na hupaswi kusubiri kamwe kwa utulivu. Ni kwa njia hii tu ndiyo unaweza kupatwa na Mungu.

Iliyotangulia: Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu

Inayofuata: Katika Imani, Mtu Lazima Alenge Ukweli—Kujihusisha na Kaida za Dini Sio Imani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp