Watu Waliochaguliwa wa China Hawana Uwezo wa Kuwakilisha Kabila Lolote la Israeli
Nyumba ya Daudi ilikuwa ni familia ambayo kiasili ilipokea ahadi na urithi wa Yehova. Ilikuwa kwa asili moja ya makabila ya Israeli na ilikuwa ya watu waliochaguliwa. Wakati huo, Yehova aliamuru sheria iwepo kwa Wana wa Israeli kuwa Wayahudi wote waliokuwa wa nyumba ya Daudi, wale wote waliozaliwa katika nyumba hiyo wangepokea urithi Wake. Wangepokea sehemu mia kwa moja na kupata hadhi ya wana wa kiume wazaliwa wa kwanza. Wakati huo, wao ndio waliokuwa wameinuliwa zaidi miongoni mwa Waisraeli wote—walikuwa na cheo cha juu zaidi miongoni mwa familia zote za Israeli, na walimhudumia Yehova hekaluni moja kwa moja, kama wamevaa kanzu za ukuhani na mataji. Wakati huo, Yeye aliwaita watumishi waaminifu na watumishi watakatifu nao walipata heshima ya makabila mengine yote ya Israeli. Hivyo, wakati huo wote walitajwa kwa heshima kama mabwana—hii ilikuwa ni kazi ya Yehova katika Enzi ya Sheria. Leo bado wanamhudumia Yehova kwa njia hii katika hekalu, hivyo daima watakuwa wafalme walioteuliwa na Bwana. Hakuna yeyote anayeweza kuwanyang’anya taji lao, na hakuna yeyote anayeweza kubadilisha huduma zao kwa kuwa wao walikuwa ni wa nyumba ya Daudi tangu mwanzo; hili ndilo Yehova amewafadhilia. Sababu ya nyinyi kutokuwa wa nyumba ya Daudi ni kwa sababu nyinyi hamjatoka Israeli, lakini ni mali ya nyumba ya kutoka nje ya Israeli. Kadhalika, asili yenu si kumwabudu Yehova, lakini ni ya kumpinga Yeye, hivyo hamna utambulisho sawa na wa wale wa kutoka nyumba ya Daudi na nyinyi si mojawapo wa wale ambao watapokea urithi Wangu. Nyinyi hasa si wale watakaopokea sehemu mia kwa moja.
Katika Israeli wakati huo kulikuwa na nyumba nyingi tofauti na makabila mengi tofauti, lakini wote walikuwa watu waliochaguliwa. Hata hivyo, kilicho tofauti na nchi zingine ni kwamba katika Israeli watu huanishwa, vyeo vyao mbele ya Yehova vinatofautishwa, na eneo la kila mtu linatandazwa kulingana na makabila yao tofauti. Katika nchi zingine bali na Israeli, hakuna anayeweza kudai kuwa wanyumba za Daudi, Yakobo, au Musa. Hili lingekuwa kinyume cha ukweli—makabila ya Israeli hayawezi kusambazwa pasi na uangalifu katika nchi zingine. Watu mara nyingi hutumia vibaya majina ya Daudi, Ibrahimu, Esau, na kadhalika, au wao husema: “Sisi sasa tumemkubali Mungu, hivyo sisi ni wa nyumba ya Yakobo” Kusema mambo haya si chochote ila kufikiri kwa binadamu kusiko na msingi na mambo haya hayaji moja kwa moja kutoka kwa Yehova, wala kuja kutoka kwa mawazo Yangu Mwenyewe. Ni upuzi wa binadamu tu! Kama mhutubu ambaye husema hadithi ndefu za uongo, bila msingi watu hujifikiria wenyewe kama wa ukoo wa Daudi au sehemu ya familia ya Yakobo, na wanaamini kuwa wao wanastahili hilo. Je, watu hawajui kwamba wale wa nyumba ya Daudi waliamuliwa zamani za kale na Yehova, na hakuwa Daudi aliyejiteua mwenyewe kama mfalme? Hata hivyo, kuna wengi ambao bila haya hudai kuwa wa ukoo wa nyumba ya Daudi—watu ni wajinga sana! Ukweli ni kwamba masuala ya Israeli hayana uhusiano na watu wa mataifa mengine—ni mambo mawili tofauti, na hayahusiani kabisa. Masuala ya Israeli yanaweza tu kuzungumziwa kwa watu wa Israeli, lakini watu wa mataifa hawahusiki kabisa, na kazi inayofanywa sasa miongoni mwa watu wa mataifa haina uhusiano na watu wa Israeli. Kinachosemwa juu watu wa mataifa mengine kinaamuliwa na kile Mimi Ninachokisema sasa, na kazi iliyofanyika Israeli haiwezi kufananishwa na maonyesho ya mbele ya kazi miongoni mwa watu wa mataifa. Je, si hiyo ingeonyesha kwamba Mungu ni wa kawaida sana? Ni wakati tu kazi inapoanza kuenea miongoni mwa watu wa Mataifa ambapo yale yanayosemwa juu yao, au matokeo yake yafichuliwe, ili maneno ya watu ya siku za nyuma, “Sisi ni wa ukoo wa Daudi,” au “Yesu ni mwana wa Daudi,” ni mambo ya upuuzi hata zaidi kuyasema. Kazi Yangu imetenganishwa. Mimi singemtaja kulungu kama farasi; badala yake, kazi hutofautishwa kulingana na utaratibu wake.