65. Mfano wa Binadamu Unafikiwa kwa Kutatua Kiburi

Na Zhenxin, Marekani

Hadithi yangu inaanza mnamo Machi 2017. Nilianza kufanya kazi ya kulibunia kanisa picha hasa za mabango ya sinema na vijipicha vya video. Mwanzoni sikujua mengi kuhusu upande wa kiufundi, kwa hivyo nilikuwa nikijifunza kila wakati kanuni na maarifa ya kiufundi. Kwa unyenyekevu niliomba msaada wa kina ndugu na nilikuwa mwangalifu nikichukua ushauri wa wengine katika miundo yangu. Baada ya muda nilianza kuelewa vyema maarifa ya kiufundi niliyohitaji kwa wajibu huo. Vijipicha vyangu viliwekwa mtandaoni na kiwango cha ubonyezaji ulikuwa wa juu. Kulikuwa na bango moja hasa la filamu ya hali halisi ambayo kina ndugu wengi waliisifu. Wengine walikuwa wakishauriana nami kuhusu masuala mengi ya kiufundi waliyokumbana nayo kwa hivyo nilihisi kama nilikuwa na talanta halisi katika eneo la usanifu wa picha. Nikawa mwenye kiburi bila kufahamu.

Baadaye, nilipokuwa nikitengeneza vijipicha ambavyo vilikuwa rahisi kuliko mabango ya sinema, nilihisi kama nilikuwa na ujuzi wa kutosha kuvikamilisha haraka sana. Kwa hivyo ningevifanya kulingana na ustadi niliokuwa nao bila kufikiria kwa makini au kutafuta kanuni. Kama matokeo ya njia mtazamo huu, nilipata maoni fulani yakisema kuwa mwangaza na rangi ya muundo haikulingana na mada. Sikuzingatia maoni yao au hata kujaribu kuyakubali, lakini niliwaza, “Je, huna ufahamu ladha yoyote? Huu ni ubunifu wa ujasiri. Nimezingatia haya yote na si shida. Unapendekeza vitu bil kujua.” Nilishikilia sana maoni yangu na hasira yangu hata iliwaka. Nilikataa kufanya mabadiliko yoyote. Kama matokeo, baadhi ya vijipicha vyangu vilikataliwa kwa sababu ya matatizo na picha hizo. Nilisikia baadaye kwamba dada mmoja alihisi kushurutishwa sana na mimi na aliogopa kunipa maoni zaidi. Nilihisi vibaya kiasi niliposikia hili lakini sikujitafakari kulingana na kile kilichotokea.

Nilifanya kazi kwenye muundo wa bango lingine la sinema kabla ya muda. Sinema ilikuwa juu ya muumini ambaye alipotoshwa na kudhibitiwa na wachungaji na wazee na kuzuiliwa na maoni ya kidini, na hivyo hakukubali kazi mpya ya Mungu. Mwishowe alikubali kazi ya Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho baada ya kutafuta ukweli na akaja kuishi katika nuru ya Mungu. Nilizingatia mada hii na kufikiria mwenyewe, “Bango bila shaka lazima lififie kutoka gizani hadi kwenye nuru—hakuna wazo bora kuliko hili.” Nilitumia miaka mingi nikitafuta bango kama hilo la sinema nitumie kama kirejeleo. Nilipomaliza bango, nilifikiri lilikuwa zuri sana, lilionekana kama bango la filamu kubwa zaidi. Kwa kweli nilikuwa nikijisifu. Kisha dada mmoja aliona bango langu na akaniambia: “Ni, mmmh, yenye giza sana hapa. Hakuna maelezo na si changamfu sana.” Kisha dada mwingine alipendekeza: “Kwa jumla ni yenye giza sana, haionekani vizuri. Inaonekana yenye kuchusha. Sinema hii inamshuhudia Mungu, kwa hivyo picha haipaswi kuwa nyeusi sana.” Nilihisi upinzani sana kwa maoni yao, kwa kile walichokuwa wakisema. Niliwaza, “Nadhani hii inaonekana nzuri sana. Hujui kuhusu uwekaji rangi lakini unaniambia jinsi ya kufanya. Si wewe ni mtu wa kutafuta mambo madogo madogo tu?” Nikasema: “Je, hii si rangi sahihi hata hivyo? Lazima kuwe na tofauti ya nuru na giza. Mbali na hilo, ni kwa bango la sinema, kwa hivyo hoja ni kufanya kazi kwenye utiaji rangi. Hivyo ndivyo mabango ya sinema nyingine hutengenezwa. Hakuna tatizo na hilo.” Kisha nikamtumia nakala ya bango la sinema nililotumia kama kirejeleo. Na kisha lililonishangaza, alisema kulikuwa na nafasi nyeusi sana kwenye bango langu na haikuonekana kuwa nzuri kama ile nyingine. Nilikasirika na kushikwa na hasira waliposema hivyo, kisha nikawaza, “Usisahau jinsi wewe huniuliza ushauri kila wakati kuhusu rangi. Huna hata maarifa ya kimsingi kuhusu hili, lakini unaniambia jinsi ya kufanya. Kwa nini unamfundisha samaki kuogelea?” Ili kumwathibitishia nilikuwa sahihi, niliwatumia kina ndugu wengine picha niliyokuwa nimebuni, lakini pia waliniambia ilikuwa yenye giza sana. Ilinibidi tu nijikaze kisabuni na niibadilishe. Bado nilifikiri nilikuwa na wazo sahihi hata hivyo na kwamba nilifanya bango hilo ilivyopasa kwa hivyo nilifanya mabadiliko madogo, lakini bado halikukubaliwa. Kwa sababu ya hilo, nilikuwa nikiifanyia kazi picha iliyopasa kuchukua wiki karibu mwezi. Hatimaye ilitupwa kwa sababu ya masuala. Hiyo ilikuwa kama, kofi usoni kwangu. Nilihisi nimevunjika moyo na kukata tamaa na sikutaka kuzungumza katika ushirika na wale wengine. Nilikuwa mahali pa giza, na pa uchungu. Kisha kiongozi wa timu akanikumbusha kwamba hakuna miundo yangu ya hivi karibuni iliyofanikiwa na kwamba nilihitaji kutafakari juu yangu mwenyewe mbele za Mungu mara moja. Hapo tu ndipo nilipokuja mbele za Mungu kwa tafakari na nikapata maneno husika ya Mungu.

Nilisoma haya katika ibada yangu siku moja: “Masuala yanapokupata, hupaswi kuwa mwenye kujidai, ukifikiri, ‘Naelewa kanuni, nina kauli ya mwisho. Hamna sifa ya kuzungumza. Ninyi mnajua nini? Ninyi hamwelewi; mimi ninaelewa!’ Huku ni kuwa mwenye kujidai. Kuwa mwenye kujidai ni tabia potovu, ya kishetani; si kitu kilicho ndani ya ubinadamu wa kawaida.” “Ikiwa daima wewe ni mwenye kujidai na unasisitiza kufuata njia zako mwenyewe, ukisema, “Sitamsikiliza mtu yeyote. Hata nikisikiliza, itakuwa kwa ajili ya kuonekana tu—sitabadilika. Nitafanya mambo kwa njia yangu; ninahisi niko sawa na nimethibitishwa kabisa,” ni nini kitakachotokea? Huenda kuwa umethibitishwa na huenda kusiwe na kosa katika kile ufanyacho; huenda hujafanya makosa yoyote, na huenda ukawa na ufahamu bora wa kipengele cha ustadi kuhusu jambo zaidi kuliko wengine, lakini, mara unapofanya na kutenda kwa njia hii, wengine wataona na watasema: ‘Tabia ya mtu huyu si nzuri! Anapokabiliwa na masuala, hakubali kitu chochote ambacho mtu mwingine yeyote anasema, kiwe sahihi au kibaya. Yeye hupinga tu. Mtu huyu huwa hakubali ukweli.’ Na watu wakisema kwamba wewe hukubali ukweli, Mungu atalazimika kufikiri nini? Je, Mungu anaweza kuona maonyesho haya yako? Mungu anaweza kuyaona vizuri kabisa. Mungu hachunguzi tu chokomeani mwa moyo wa mwanadamu, bali pia huangalia kila kitu usemacho na kufanya wakati wote, mahali pote. Na, Anapoona mambo haya, Yeye hufanya nini? Yeye husema: ‘Wewe umefanywa mgumu. Uko namna hii katika hali ambapo wewe uko sahihi, na wewe uko namna hii pia katika hali ambapo umekosea.Katika hali zote, ufichuzi na maonyesho yako yote ni kinyume na yenye kupingana na kukinzana. Hukubali chochote kuhusu maoni au mawazo ya wengine. Yote ndani ya moyo wako ni kupingana, kufungwa, na kukataa. Wewe ni mgumu sana!’(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Mungu huona ndani ya mioyo na akili zetu. Hii ilifunua hali yangu kabisa. Nilikuwa nikifichua tabia ya kishetani ya kiburi. Zamani wakati mabango yangu yalikubaliwa na kusifiwa na kina ndugu nilidhani hiyo ilikuwa kwa sababu ya ustadi wangu mwenyewe na kwamba hakuna mtu mwingine angeweza kulingana na muundo na maarifa yangu. Wakati watu wengine walinipa maoni nilikataa kuyakubali, nikidhani hawakuelewa. Hata wakati watu wengi walitoa maoni sawa, nilikuwa mkaidi kweli. Nilijifanya kukubali kile walichosema lakini kwa kweli nilishikilia mawazo yangu mwenyewe. Nilibadilisha tu kile kilichofaa mawazo yangu na kukataa kubadilisha kile ambacho sikukubaliana nacho. Nilipata visingizio vya kila aina vya kubishana na watu. Nilimzuia dada mmoja kwa sababu ya hiyo. Niligundua nilikuwa na kiburi kupita kiasi. Sikuwa na busara kabisa! Nilikuwa na kiburi na kujidai sana kwa kupuuza maoni. Si tu kwamba nilihitaji kuhariri kila wakati, ambayo ilichelewesha kazi yetu, lakini hali yangu mwenyewe ilizorota. Bila kukabiliwa na kushindwa huko singewahi kuja mbele za Mungu kutafakari na kujijua. Kama singegeuka, lakini niendelee tu kuishi kwa kufuata tabia yangu ya kiburi, wengine wangenikataa na Mungu angechukizwa. Nilijawa na majuto haya na niliogopa. Nilikuja mara moja mbele za Mungu kuomba ili nitubu.

Baadaye, niliwaambia akina dada katika timu hiyo kuhusu upotovu niliokuwa nimefichua na kuwaambia nilikuwa tayari kupokea maoni yoyote na kushughulikiwa. Katika wajibu wangu langu kutoka hapo, kina ndugu walinipa maoni kadhaa na mwanzoni ilikuwa vigumu kwangu kuyakubali. Lakini nilipokumbuka jinsi nilivyopata shida za hivi karibuni, niliomba na kujiweka kando kutafakari. Niliwaza ni kwa nini walitoa maoni hayo, ni nini kilichopatikana kwa kuyafuata, na tatizo lilikuwa wapi. Kisha niliyazingatia kulingana na kanuni. Kwa njia hii mpya ilikuwa rahisi kuelewa na kukubali maoni ya wengine na marekebisho yangu yalipokelewa vizuri zaidi na kila mtu. Niliona pia jinsi kutenda ukweli ni jambo zuri. Lakini tabia yangu ya kiburi ilikuwa imekita mizizi ndani yangu, kwa hivyo sikuweza kuing'oa kwa tukio moja la kutofaulu.

Niliingia tena katika kiburi muda kidogo baadaye. Kuna wakati mmoja nilitengeneza kijipicha cha hizo nyimbo zote za kanisa. Nilifikiria kweli kwamba kuwa ni kina ndugu wakionyesha sifa kwa Mungu baada ya kupitia kazi Yake inapaswa kuwa yenye ukunjufu, kimapenzi, na yenye hisia nzuri. Nilifikiri kuhusu nadharia fulani ya rangi niliyokuwa nimejifunza iliyosema zambarau ilikuwa mfano halisi wa hisia ya aina hiyo, na ilikuwa na maana ya heshima. Nilihisi kwamba singekosea kutumia zambarau kama rangi ya msingi. Nilipomaliza mradi wangu, kina ndugu wengine walisema walipenda kile nilichobuni na rangi hizo zilikuwa nzuri. Nilifurahishwa sana na yale niliyokuwa nimefanya na kufikiri nilikuwa na ubora fulani wa tabia na uwezo wa kubuni. Nilishangaa wakati ambapo dada mmoja ambaye alikuwa ameanza tu kazi ya kubuni alinitumia maoni, akisema “Nyimbo za kanisa ni matukio halisi na mafunzo kutoka kwa waumini. Matumizi ya rangi ya zambarau ni kama ndoto na haifai kabisa. Ni ngumu kiasi ikitazamwa. Ningeshauri kuibadilisha.” Nilisoma maoni yake lakini nilihisi upinzani wa ndani. Niliwaza, “Nimesoma hati nyingi za mafunzo ambazo zinasema kwamba zambarau hutoa hisia zenye joto. Mbali na hilo, kuna miundo mingi ambayo hutumia zambarau kwa njia hii. Kwa nini unasema kuwa ni ngumu ikitazamwa? Juu ya hayo umeanza tu na hili na hujaunda chochote wewe mwenyewe, lakini unanipa maoni. Hujui mipaka yako mwenyewe.” Lakini bado sikuhisi raha kumpinga moja kwa moja, kwa hivyo nikampuuzilia mbali, nikisema nitawauliza watu wengine watoe maoni. Sikuwahi kwenda kuuliza maoni ya mtu mwingine baada ya hapo, nilipuuzilia tu mbali jambo hilo.

Siku chache baadaye dada mwingine alinipa maoni sawa akasema rangi niliyokuwa nikitumia ilikuwa ya kukatisha tamaa, akipendekeza niibadilishe. Wakati huo tu, kiongozi wa timu alinikumbusha nisiwe mkaidi hata kidogo na kwamba nilipaswa kufanya mabadiliko kwa ukaguzi zaidi. Sikuthubutu kushikilia simamo wangu kwa hivyo nilijaribu kufanya mabadiliko. Lakini sikuwa tayari kuachilia muundo huo wa zambarau. Kisha nikawaza, “Ubuni wangu na rangi hii hauwezi kuwa mbaya. Baadhi ya wale wengine waliupenda sana, hivyo kwa nini lazima nibadilishe?” Lakini nilijitahidi kuibadilisha nilipofikiria kulihusu kwa njia hiyo. Haukuonekani vizuri baada ya majaribio machache. Kisha kosa lilionekana katika mojawapo ya mabadiliko niliyofanya ambayo nilitumia masaa mengi kufanya lakini sikupata njia ya kurekebisha. Nilikatishwa tamaa sana, nisijue la kufanya na hata nilitaka kukata tamaa. Nilifikiri kuhusu jinsi nilivyotumia mwezi mzima kwenye picha hiyo moja nikiiariri mara sita, na jinsi wengine walikuwa wamenipa maoni mengi. Bado sikuwa nimeimaliza na ilikuwa ikiichelewesha kazi yetu. Nilikasirika sana. Nilikumbuka jinsi nilivyokuwa nimeichelewesha kazi yetu kwa sababu nilikuwa na kiburi na sikuweza kuchukua maoni. Sasa nilikuwa mwenye kiburi tena na kukataa mapendekezo. Je, hiyo haikuwa shida ile ile ya zamani? Nilikuja haraka mbele za Mungu katika maombi, nikisema, “Ee Mungu, tabia yangu ya kiburi ni mbaya sana. Siwezi kutii katika hali hii. Tafadhali nipe nuru na uniongoze, nielewe mapenzi Yako, nijitambue na nitoke katika hali hii.”

Baadaye nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Kiburi ndicho chanzo cha upotovu wa mwanadamu. Kadiri watu wanavyozidi kuwa na kiburi, ndivyo wanavyozidi kuwa na uelekeo wa kumpinga Mungu. Tatizo hili ni kubwa kiasi gani? Siyo tu kwamba watu wenye tabia ya kiburi humfikiria kila mtu mwingine kuwa duni kuwaliko, lakini lililo baya zaidi, wao hata huwa na mtazamo wa udhalilishaji kwa Mungu. Hata ingawa, kwa nje, watu wengine wanaweza kuonekana kana kwamba wanamwamini Mungu na kumfuata, hawamchukulii kama Mungu hata kidogo. Wao huhisi sikuzote kuwa wanamiliki ukweli na wanajipenda mno. Hiki ndicho kiini na chanzo cha tabia ya kiburi, na hutoka kwa Shetani. Kwa hivyo, tatizo la kiburi lazima litatuliwe. Kuhisi kuwa wewe ni bora kuliko wengine—hilo ni jambo dogo. Suala la muhimu ni kwamba tabia ya kiburi ya mtu humzuia mtu kumtii Mungu, sheria Yake, na mipango Yake; mtu kama huyo daima huhisi kuwa na uelekeo wa kushindana na Mungu kuwatawala wengine. Mtu wa aina hii hamchi Mungu hata kidogo, sembuse kumpenda Mungu au kumtii. Watu ambao ni wenye kiburi na wenye majivuno, hasa wale ambao ni wenye kiburi mno hadi kiwango cha kupoteza akili zao, hawawezi kumtii Mungu katika imani yao Kwake, na hata hujiinua na kujishuhudia wenyewe. Watu kama hao ndio humpinga Mungu zaidi. Kama watu wanataka kufikia mahali ambapo wanamcha Mungu, basi lazima kwanza watatue tabia zao za kiburi. Kadiri unavyotatua tabia yako ya kiburi kikamilifu, ndivyo utakavyokuwa na uchaji zaidi kwa Mungu, na ni hapo tu ndipo utakapoweza kumtii Yeye na uweze kupata ukweli na kumjua(Ushirika wa Mungu). Hili lilinisaidia kuelewa kuwa kiburi ni chanzo cha kumpinga Mungu. Kudhibitiwa na tabia yangu ya kiburi, nilifikiri siku zote kwamba nilikuwa sahihi kana kwamba mitazamo yangu pekee ndiyo ilikuwa ukweli, kana kwamba ilikuwa chanzo cha mamlaka. Sikuwa na hamu yoyote ya kutafuta ukweli na kumtii Mungu. Sikuweza tu kuchukua maoni ya mtu yeyote. Hasa wakati ambapo mtu hakuwa na ujuzi kama mimi au hakuelewa mambo fulani ya kiufundi, na bado alinipa maoni yake, Kwa kweli nilikuwa mpinzani. Nilitenda kama niliyeyakubali, lakini kwa kweli sikuchukua maoni yao kwa uzito. Mungu alinikumbusha mara nyingi kupitia wengine kuweka mapenzi yangu kando, kuzingatia kazi ya kanisa, kutafuta, na kujaribu, na kutoa toleo bora. Lakini nilikuwa mkaidi na mwenye kiburi kupindukia. Nilichukua maoni na uzoefu wangu mwenyewe kama ukweli na nilishikilia msimamo wangu wakati ambapo maoni ya wengine hayakuwa na maana kwangu. Yote haya yalivuruga kazi ya nyumba ya Mungu. Kisha, mwishowe nikaanza kuelewa maneno haya ya Mungu: “Siyo tu kwamba watu wenye tabia ya kiburi humfikiria kila mtu mwingine kuwa duni kuwaliko, lakini lililo baya zaidi, wao hata huwa na mtazamo wa udhalilishaji kwa Mungu.” “Kadiri watu wanavyozidi kuwa na kiburi, ndivyo wanavyozidi kuwa na uelekeo wa kumpinga Mungu.” Nilishawishiwa kabisa kutoka kwa maneno haya ya Mungu. Nilihisi pia hofu kidogo. Ilinikumbusha wapinga Kristo kanisani. Kwa kweli walikuwa wenye kiburi na madikteta, na kamwe hawakusikiliza maoni ya wengine kamwe. Hata waliwashutumu na kuwatenga watu, ambayo ilivuruga kazi ya nyumba ya Mungu na kuikosea tabia ya Mungu. Vyote viliondolewa na Mungu. Sikuwa nimefanya aina ya uovu ambao wapinga Kristo walikuwa wamefanya, lakini tabia yangu ilikuwa tofauti vipi na yao? Ni hapo ndipo niligundua jinsi athari zitakavyokuwa mbaya nisingerekebisha tabia hiyo. Nilikuja mbele za Mungu katika maombi mara moja, nikiwa tayari kutubu.

Baadaye, nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Unapoangalia jambo hili sasa, je, ni vigumu mtu kutimiza wajibu wake kiasi cha kutosha? Kwa kweli, si vigumu; watu lazima waweze kabisa kuchukua msimamo wa unyenyekevu, wawe na busara kidogo na wachukue msimamo unaofaa. Bila kujali unafikiri kwamba wewe ni msomi jinsi gani, umeshinda zawadi gani, au umepata mafanikio kiasi gani, na bila kujali unaamini kwamba una ubora wa juu wa tabia na cheo cha juu kiasi gani, lazima uanze kwa kuacha mambo haya yote kwa sababu hayana maana. Katika nyumba ya Mungu, bila kujali mambo haya ni makubwa na mazuri jinsi gani, hayawezi kuwa ya muhimu zaidi kuliko ukweli; mambo hayo siyo ukweli, na hayawezi kuchukua nafasi ya ukweli. Hii ndiyo sababu Nasema kwamba lazima uwe na kitu hiki kiitwacho busara. Ukisema, ‘Nina kipaji sana, nina akili sana, mimi hujibu haraka, mimi hujifunza mambo haraka na nina kumbukumbu nzuri sana,’ na wewe hutumia mambo haya kama mtaji, basi jambo hili litasababisha tatizo. Ukiona mambo haya kama kwamba ni ukweli au ni ya muhimu zaidi kuliko ukweli, basi itakuwa vigumu kwako kukubali ukweli na kuutia katika vitendo. Watu wenye kiburi na majivuno ambao siku zote hutenda kama wa cheo cha juu hushindwa kabisa kuukubali ukweli na wana uelekeo wa kuanguka. Iwapo mtu anaweza kutatua tatizo la kiburi chake, basi kutia ukweli katika vitendo kutakuwa rahisi. Kwa hivyo, lazima kwanza uache na ukane mambo yanayoonekana kijuujuu kuwa mema na ya kifahari na yanayowasababisha watu wengine waone wivu. Mambo hayo siyo ukweli; badala yake, yanaweza kukuzuia kuingia katika ukweli(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya hapo nilielewa kwamba ilibidi nijiweke kando na nijikane ili nisuluhishe tabia yangu ya kiburi. Ujuzi, uwezo, uzoefu, na vipawa vya binadamu si ukweli, hata viwe vizuri jinsi gani. Ni zana tu za kutusaidia kufanya wajibu wetu. Hatupaswi kuzitegemea. Kujaribu kutafuta ukweli, kufanya vitu kwa kufuata kanuni, kufanya kazi vizuri na wengine, na kujifunza kutoka kwa wengine yote ni muhimu sana. Hiyo ndiyo njia pekee ya kufanya wajibu wetu vizuri. Kisha niliangalia baadhi ya mabango bora niliyokuwa nimetengeneza hapo awali na kugundua kuwa kulikuwa na shida dhahiri kama vile, za dhana, za rangi, kiwango cha rangi, na muundo zote zilipatikana katika picha zangu za asili. Lakini baada ya kuzihariri kulingana na maoni yaliyotolewa na kina ndugu zilikuwa ziliimarika sana, na nyingine zilipitia mabadiliko kamili. Kwa kweli niliaibika kuona hili. Nilidhani kuwa nilikuwa nimepata mafanikio ya aina fulani katika kazi yangu na kwamba nilikuwa nimepokea sifa kutoka kwa wengine kwa sababu nilikuwa na maarifa zaidi ya kiufundi na uzoefu zaidi kuwaliko. Nilitumia, nikikataa katakata kumsikiliza mtu yeyote. Lakini ukweli ulikuwa kwama miundo yangu ilifanikiwa kwa sababu nilifuata kanuni za ukweli na nikakubali maoni ya watu wengine. Ilifanywa kwa mwongozo na nuru ya Mungu na kwa kufanya kazi kwa upatanifu na unyenyekevu pamoja na kina ndugu. Wakati ambapo yote niliyofanya yalitegemea maarifa ya kiufundi bila kutafuta kanuni za ukweli au kukubali maoni ya wengine, picha zangu hazikuwa nzuri hata kidogo, na hili lilizuia kazi ya kanisa kweli. Niliaibika sana nilipokumbuka wakati nilikuwa mwenye kiburi na kujidai sana katika njia yangu. Kwa wazi sikuwa kitu chochote maalum. Nilikuwa tu nimeanza kuingia katika uwanja wa ubunifu na nilikuwa mbali sana kuwa mtaalamu wa kweli. Lakini bado nilikuwa mwenye kujiamini na mwenye kiburi sana. Nilikuwa mkaidi sana. Nilipotambua hili, nilisali na kuachalia maoni yangu. Nilifuata maoni ya wengine, na kwa kweli nilifikiri kuhusu jinsi ya kufanya marekebisho ili kupata matokeo bora. Si tu kwamba suala kuu lilisuluhishwa lakini pia nilipata rangi bora ya kutumia. Niliihariri picha hiyo haraka sana na kina ndugu walisema ilionekana nzuri zaidi baada ya mabadiliko hayo. Niliaibika sana kuona na kutambua hili. Tulikuwa tumepitia marekebisho mengi ya picha hiyo yote kwa sababu ya kiburi changu mwenyewe, nikipoteza wakati wa thamani sana na kuwasumbua wengine. Iliivuruga sana kazi ya nyumba ya Mungu. Si tu kwamba ujuzi wangu ulituama, lakini kuingia kwangu katika uzima kulipata pigo. Niliona kwamba kuishi kwa kufuata tabia yangu ya kiburi kulinisababishia madhara tu. Nilijuta sana na niliamua kimyakimya: “Haijalishi nitapata maoni gani nitajifunza kujiweka kando, nitafute ukweli, na kuweka masilahi ya nyumba ya Mungu mbele. Siwezi kuendelea kuishi kwa kiburi.”

Hivi majuzi nilibuni kijipicha cha video ya usomaji wa maneno ya Mungu na nilipowaonyesha kina ndugu rasimu yangu ya kwanza walisema picha ya ulimwengu ilikuwa kubwa sana na ilionekana kujaa katikati, kwa hivyo mtazamo haukuwa wazi vya kutosha. Walinitumia picha kadhaa kama marejeleo kunisaidia kuboresha. Nilianza kuwaza, “Ulimwengu lazima uwe mkubwa hivyo ili uwe na athari nzuri na huna uzoefu wa kitaalam wa usanifu wa picha au mafunzo yoyote ya vitendo. Nina ujuzi zaidi katika uwanja huu. Hakuna chochote ninachopata kutoka kwa maoni yako.” Kwa hivyo nilichunguza tu maoni yake kwa juu juu na nilizingatia maoni yangu tu. Wakati huo niligundua kwamba nilikuwa nikionyesha kiburi changu tena, kwamba sikuwa nimezingatia maoni ya utulivu au matokeo ya mwisho. Nilikuwa nikitoa tu maamuzi bila kufikiri na hilo lilikinzana na mapenzi ya Mungu. Nilisali mara moja nikimwomba Mungu autulize moyo wangu ili niweze kutenda ukweli na kuuacha mwili wangu. Nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu baada ya hapo: “Lazima kwanza uwe na mtazamo wa unyenyekevu, upuuze kile unachoamini kuwa ni sahihi, na umwache kila mtu awe na ushirika. Hata kama unaamini kwamba njia yako ni sahihi, hupaswi kuendelea kuisisitiza. Kwanza kabisa, hayo ni maendeleo ya aina fulani; inaonyesha mtazamo wa kutafuta ukweli, wa kujinyima, na wa kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Unapokuwa na mtazamo huu, wakati huo huo ambapo hushikilii maoni yako, unaomba. Kwa kuwa hujui kutofautisha mema na mabaya, unamruhusu Mungu afichue na kukuambia jambo bora na linalofaa kufanywa ni lipi. Kila mtu anapojiunga katika ushirika, Roho Mtakatifu anawaletea nyote nuru. Mungu huwapa watu nuru kulingana na mchakato fulani, ambao wakati mwingine hukadiria tu mtazamo wako. Iwapo mtazamo wako ni wa msimamo mkali wa kujionyesha haki, Mungu atakufichia uso Wake na Atajitenga nawe; Atakufunua na kuhakikishia kwamba utashindwa. Iwapo kwa upande mwingine, mtazamo wako ni muwafaka, hausisitizi kufuata njia yako mwenyewe wala si wa kujidai, si dhalimu wala usio na subira, bali ni mtazamo wa kutafuta na kukubali ukweli, basi utakapofanya ushirika pamoja na kikundi na Roho Mtakatifu afanye kazi miongoni mwenu, pengine Atakuongoza katika kuelewa kwa njia ya maneno ya mtu(Ushirika wa Mungu). Baada ya hapo nilielewa, kwamba wakati nikikutana na maoni tofauti kutoka kwa wengine katika wajibu wangu, hicho kilikuwa kitu ambacho Mungu aliruhusu. Mungu huangalia kila fikira na tendo letu, kwa hivyo napaswa kuwa nikitenda ukweli na kukubali uchunguzi wa Mungu. Sikupaswa kuchukua vitu jinsi vilivyo tu na kuhukumu hisia za watu wengine za taaluma. Hata ikiwa nilikuwa na ujuzi zaidi, bila kujali nilifikiri wazo langu lilikuwa la busara vipi, nilipaswa kujinyenyekeza, niweke kando mawazo yangu mwenyewe, nitafute kanuni za ukweli, na nifanye chochote kilicho chenye matokeo bora zaidi. Hata nikitukia kuwa sahihi mwishowe, angalau nitakuwa nimetafuta na kutenda ukweli kama vile Mungu anavyotaka. Hilo ni jambo la thamani sana. Mungu alichukia tabia zangu za kishetani ambazo zilikuwa katika uadui na Yeye, kwa hivyo kuonyesha kiburi changu lilikuwa jambo baya zaidi kuliko kufanya makosa. Nilifikiria kuhusu jinsi kiburi changu kilikuwa kimeivuruga kazi ya nyumba ya Mungu na sikupenda hilo na nilihisi kweli kuwa sikupaswa kuwa mkaidi hivyo. Ilinibidi niyachukulie maoni ya marekebisho kwa utulivu na kujitahidi kuifanya picha iwe bora. Baada ya hapo, nilianza kuchukua maoni ya wengine kwa uzito na nikapata picha ya kumbukumbu ambayo ilikuwa maridadi sana ambayo ningeweza kujifunza kutoka kwayo. Niliijadili na washiriki wengine wa timu wakati huu na kila mtu alikubali kwamba marekebisho lazima yafanywe kama ilivyopendekezwa. Nilishughulikia upya mpangilio na vipengele vingine na vilifanyika ghafla bin vu Nilihisi kwamba haya yote yalikuwa yametimizwa kupitia nuru na mwongozo wa Mungu. Ingawa nilipokea maoni kadhaa zaidi, niliyashughulikia ipasavyo na sikuhisi mpinzani sana. Nilifurahi kuibadilisha mara nyingi ilivyohitajika ili niwe shahidi kwa Mungu. Baada ya marekebisho machache, kila mtu alisema ilikuwa nzuri na hakuwa na maoni yoyote zaidi. Niliona jinsi ilivyokuwa vizuri kufanya wajibu wangu kwa njia hiyo.

Baada ya kufundishwa nidhamu na kwa kusoma maneno ya Mungu Hatimaye nilielewa na kuchukia tabia yangu ya kishetani ya kiburi. Niliona jinsi ilivyo muhimu kutafuta na kukubali ukweli. Sina kiburi jinsi nilivyokuwa zamani na ninaweza kukubali maoni kutoka kwa wengine. Nimebadilika namna hii kabisa kwa sababu ya hukumu, kuadibu na kufundishwa nidhamu na Mungu.

Iliyotangulia: 64. Kiburi Huja Kabla ya Kuanguka

Inayofuata: 67. Kuishi kwa Kudhihirisha Mfano Kidogo wa Mwanadamu Hakika Ni Vizuri

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

3. Jaribu la Foili

Na Xingdao, Korea ya Kusini“Ee Mungu! Kama nina hadhi au la, sasa ninajielewa mwenyewe. Hadhi yangu ikiwa juu ni kwa sababu ya kuinuliwa na...

45. Kuishi Mbele za Mungu

Na Yongsui, Korea ya KusiniMwenyezi Mungu anasema, “Ili kuingia katika uhalisi, mtu lazima apindue vitu vyote kuelekea maisha halisi. Iwapo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp