68. Ulinzi wa Mungu

Mwenyezi Mungu anasema: “Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya Mungu, au kushughulikiwa, kufunzwa nidhamu, na kupogolewa na maneno Yake. Ni baada ya hapo tu ndipo wanaweza kutimiza utiifu na ibada kwa Mungu, na wasijaribu tena kumdanganya Yeye na kumshughulikia kwa uzembe. Ni kupitia kwa usafishaji wa maneno ya Mungu ndio watu hupata mabadiliko katika tabia. Ni wale tu wanaopitia mfichuo, hukumu, kufundishwa nidhamu, na kushughulikiwa kwa maneno Yake ambao hawatathubutu tena kufanya mambo kwa kutojali, na watakuwa watulivu na makini. Jambo muhimu sana ni kwamba wanaweza kutii neno la sasa la Mungu na kutii kazi ya Mungu, na hata kama hayalingani na fikira za binadamu, wanaweza kuweka kando fikira hizi na kutii kwa hiari(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu). Niliposoma maneno ya Mungu awali, “Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya Mungu, au kushughulikiwa, kufunzwa nidhamu, na kupogolewa na maneno Yake. Ni baada ya hapo tu ndipo wanaweza kutimiza utiifu na ibada kwa Mungu, na wasijaribu tena kumdanganya Yeye na kumshughulikia kwa uzembe.” sikuweza kuelewa kabisa kwa nini watu hawakuweza kubadilisha tabia zao wenyewe. Nilisoma maneno ya Mungu kwa bidii kila siku, kila mara nilihudhuria mikutano kwa wakati, na nilitii wajibu wowote niliopewa na kanisa. Nilifikiria kwamba mradi sikufanya dhambi, nilifanya wajibu wangu vizuri, nilikuwa muumini kwa miaka mingi, na nilisoma maneno ya Mungu sana, basi hakika tabia yangu potovu ingebadilika. Kwa nini bado ilibidi nihukumiwe na kuadibiwa, na kupogolewa na kushughulikiwa na Mungu? Kamwe sikuyaelewa kweli maneno haya ya Mungu niliyokuwa nimesoma mpaka baada ya mimi kupogolewa na kushughulikiwa vikali mara chache, na nikatafakari kujihusu. Ni hapo tu ndipo niliona jinsi nilivyokuwa nimepotoshwa sana na Shetani, kwamba asili yangu ya kishetani yenye kiburi na majivuno ilikuwa imekita mizizi sana ndani yangu, na bila kuhukumiwa na kuadibiwa, na kupogolewa na kushughulikiwa na Mungu, sikuwa nimejijua, sembuse kutakaswa au kubadilishwa.

Mnamo mwanzoni mwa 2016 nilikuwa nikifanya wajibu wa kiongozi wa kanisa. Nilipoanza mwanzoni, nilihisi nilipungiwa na mengi sana, kwa hivyo nilimwomba Mungu kila wakati na kumtegemea katika wajibu wangu. Nilitafuta na kufanya ushirika na na wafanyakazi wenzangu nilipokumbana na suala ambalo sikuelewa, na niliweza kukubali maoni ya watu wengine. Nilikuwa mnyenyekevu sana. Baada ya zaidi ya miezi sita ya kutenda nilikuwa na ufahamu wa baadhi ya kanuni na niliweza kusaidia kutatua shida za baadhi ya kina ndugu kwa kushiriki juu ya ukweli. Nilianza kuwa mwenye kuridhika mno, nikiwaza, “Hata ingawa sijawahi kuwa kiongozi wa kanisa awali. Nina ubora mzuri wa tabia na ninayaelewa maneno ya Mungu haraka. Baada ya utendaji zaidi nina uhakika nitakua bora hata zaidi.” Baadaye nilipewa jukumu la wajibu muhimu na nikajisikia hata zaidi. Nilikuwa mwenye umri mdogo kabisa kati ya wafanyakazi wenzangu na nilikuwa katika imani kwa muda mchache, lakini nilihisi kwamba ili kuweza kufanya kitu muhimu sana kama hicho, lazima nina talanta kweli! Kwa muda mfupi, niliiamini sana hata nilipokuwa nikitembea, nikihisi kana kwamba nilikuwa na wajibu muhimu zaidi kati ya kila mtu, kana kwamba hakuna mtu angelingana nami. Baada ya muda, nilikuwa mwenye kiburi zaidi. Katika majadiliano juu ya kazi ya kanisa, wakati wafanyakazi wenzangu walitoa maoni, nilishikilia maoni yangu mwenyewe, nikiwaza, “Je, ni vile unavyoifanya ionekane kweli? Nimeshughulikia mambo kama haya hapo awali, kwa hivyo si mimi nina ufahamu bora wa kanuni? Najua njia bora ya kushughulikia suala hili.” Wakati mwingine dada niliyefanya naye kazi alipochukulia kitu kwa uzito sana, nilikosa kuwa mvumilivu, nikifikiri kwamba jambo rahisi kama hilo lilikuwa rahisi kushughulikia na hakukuwa na haja ya kufanya ushirika na kutafuta tena na tena. Wakati mwingine katika mikutano ya wafanyakazi wenza, niliona maoni yake hayakukubaliwa na ndugu wengine, na nilianza kumdharau. Niliwaza, “Hata ingawa umekuwa kiongozi kwa muda mrefu kuniliko, huwezi kulinganishwa nami hata kidogo.” Wakati mmoja aliniambia kwamba nilifanya wajibu wangu polepole, kwamba maendeleo yangu yalikuwa ya polepole. Sikuweza kustahimili hilo na nikafoka, “Siwezi kukubali ushirika huu kutoka kwako. Je, huhusiki katika kazi hii pia? Si wewe huiwajibikii pia? Unawezaje kukosa kujitambua sana na unisukumie kila kitu?” Aliposema hilo, nilinyanyuka tu na kutoka nje. Kiongozi baadaye alijua kuhusu tabia yangu na akanishughulikia, akisema nilikuwa mwenye kiburi sana. Nilikubali tu kwa maneno, nikisema, “Nina kiburi sana, na sikubali ukweli.” Sikutafakari juu ya asili na kiini changu au kujaribu kuvielewa, lakini katika wajibu wangu niliendelea kuzungukazunguka, nikifanya mambo ninavyotaka. Kulikuwa na wafanyakazi wenzangu wakati huo ambao walibadilishwa kwa sababu walipungukiwa katika ubora wa tabia na hawakuweza kufanya kazi ya vitendo. Lakini sikuwahi kuwa na wasiwasi kuhusu kubadilishwa. Niliwaza, “Nina talanta halisi kanisani sasa na ninawajibika majukumu kadhaa. Bila mimi, wataweza kupata mtu mwingine anayefaa katika kipindi kifupi?” Wakati tu nilikuwa najivuna kupindukia, nilipogolewa na kushughulikiwa kwa ukali sana.

Wakati mmoja, nilisoma makala ya uzoefu na ushuhuda yaliyoandikwa na kina ndugu ambayo nilihisi yalikuwa ya juu juu sana. Niliyakataa bila hata kujadili suala hilo na mtu yeyote. Kiongozi alikasirika sana alipogundua hili. Aliniuliza, “Kwa nini ukatae makala mazuri kama hayo? Je, hata ulijadili hilo na wafanyakazi wenzako?” Nilisema, “Hapana, wakati huo nilihisi tu kuwa yalikuwa ya juu juu kwa namna fulani.” Punde niliposema haya, kiongozi alinishughulikia vikali, akisema, “Ingawa makala haya yanaweza kuwa ya juu juu, uzoefu wao ni wa kweli na wanaonyesha ufahamu wa vitendo. Makala haya ni yanawaadilisha watu. Hiyo ndiyo inajumuisha ushuhuda mzuri wa matukio ya mtu binafsi. Hutafuti ukweli katika wajibu wako, na wewe ni mkaidi na mwenye kiburi. Huelewi ukweli au kujadili mambo na wengine. Kukataa tu makala mazuri, kuzuia ushuhuda wa kupitia kazi ya Mungu, je, si huo si upumbavu? Hicho si kitu ambacho Shetani angefanya? Wewe unasumbua tu!” Nilikuwa nimepogolewa na kushughulikiwa hapo awali, lakini kamwe si kwa ukali hivyo. Maneno “pumbavu,” “Shetani,” “usumbufu,” “mkaidi na mwenye kiburi” yalijirudiarudia kichwani mwangu, na sikuweza kuzuia machozi. Nilihisi kana kwamba nilishindwa kupumua. Lakini bado nilihisi kukosewa. Hata ingawa sikuwa nimelijadili na wafanyakazi wenzangu wakati huo, si nilikuwa nimewaambia kuhusu jambo hilo baadaye? Kwa kweli Mungu huona ndani ya mioyo yetu. Wakati tu nilikuwa nikifikiria visingizio, kiongozi aliendelea kwa ukali, “Katika matendo yako, hufuati sheria na masharti yaliyowekwa. Unaweza kuuliza wakati huelewi kitu au ukijadili na wengine, lakini hata hufanyi hivyo. Wewe ni mwenye kiburi sana na huna moyo unaomcha Mungu kabisa!” Aliposema hili, nilinyenyekea shingo upande. Kama kweli ningekuwa na moyo unaomcha Mungu kidogo, ningetafuta kiasi kabla ya kuchukua hatua, lakini badala yake nilifanya tu vitu jinsi nilivyotaka bila kuuliza maoni ya wengine. Kwa kweli nilikuwa mwenye kiburi na mwenye kujidai.

Kiongozi alifanya uchunguzi kunihusu na akagundua kwamba nilikuwa mwenye kiburi mno, kwamba sikuelewa ukweli, na kwamba sikustahili kufanya wajibu muhimu kama huo, na kwa hivyo nilibadilishwa. Kwa kweli niliingia katika hali ya uhasi. Nilihisi kwamba kiongozi huyo alikuwa amenibaini katika suala hili na akaona kwamba sikuwa mtu aliyefuatilia ukweli, ya kwamba nilikuwa mwenye kiburi mno, na hata sikustahili kukuzwa. Nilidhani sikuwa na matarajio yoyote katika nyumba ya Mungu tena. Nilizidi kuwa hasi, na nilijawa na suitafahamu. Nilihisi kama kwamba nilikuwa nimekuwa Shetani. Ningewezaje hata kuokolewa? Nilifikiria kina ndugu walidhani hakika sikuwa mtu anayestahili, kwa hivyo ingesaidia nini kuendelea kufuatilia? Wakati huo, ingawa nilionekana kufanya baadhi ya wajibu shingo upande, sikutaka kufuatilia ukweli. Mtu husika alishiriki nami juu ya mapenzi ya Mungu mara kadhaa, lakini sikubadilika. Kisha alinipogoa na kunishughulikia, akisema kwamba nilikuwa mgumu kwa makusudi katika wajibu wangu, nilikuwa hasi kila wakati, kwamba nilikuwa nikimpinga Mungu, na kama singefanya mabadiliko, ningeondolewa na Mungu siku moja. Kusikia hili kulinitia hofu, na nikagundua uzito wa hali hiyo. Niliharakisha kuja mbele za Mungu kuomba na kutafuta, na kujitafakari. Katika miezi hiyo sita, kwa nini sikuweza kuchukulia kupogolewa na kushughulikiwa vizuri? Nilipokuwa nikitafakari, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Watu wengine wanakuwa wa kutoonyesha hisia baada ya kupogolewa na kushughulikiwa; wanapoteza nguvu zote kutekeleza wajibu wao, na wanaishia kupoteza uaminifu wao vile vile. Kwa nini hivi? Kwa kiasi ni kwa ajili ya kukosa kwao ufahamu kuhusu kiini cha matendo yao, na hili husababisha wao kutoweza kutii kupogolewa na kushughulikiwa. Hili linaamuliwa na asili yao ambayo ni ya kiburi na majivuno, na ambayo haipendi ukweli. Pia kwa kiasi ni kwa ajili ya kutoweza kwao bado kuelewa umuhimu wa kupogolewa na kushughulikiwa ni upi. Watu wote huamini kwamba kupogolewa na kushughulikiwa kunamaanisha kwama matokeo yao yameamuliwa tayari. Kwa sababu hiyo, wao huamini kimakosa kuwa wakiwa na uaminifu kiasi kwa Mungu, basi hawafai kushughulikiwa na kupogolewa; na wakishughulikiwa, basi hili haliashirii upendo na Haki ya Mungu. Suitafahamu kama hiyo huwasababisha watu wengi kutothubutu kuwa “waaminifu” kwa Mungu. Kwa kweli, baada ya yote, ni kwa sababu ni waongo kupindukia; hawataki kupitia ugumu. Wanataka tu kupata baraka kwa njia rahisi. Watu hawana ufahamu wa haki ya Mungu. Si kwamba Hajafanya lolote la haki au kwamba Hafanyi chochote cha haki; ni tu kwamba watu daima hawaamini kwamba kile Afanyacho Mungu ni haki. Machoni pa wanadamu, kama kazi ya Mungu haipatani na matamanio yao ya kibinadamu, ama kama hailingani na matarajio yao, basi lazima Yeye si mwenye haki. Hata hivyo, watu kamwe hawajui kwamba matendo yao ni yasiyofaa na kwamba hayaambatani na ukweli, wala hawatambui kamwe kwamba matendo yao yanampinga Mungu(“Maana Ndani ya Mungu Kuamua Matokeo ya Watu Kupitia Utendaji Wao” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma ufunuo huu katika maneno ya Mungu mwishowe nilielewa kwamba kuwa kwangu hasi sana kulikuwa kwa sababu nilikuwa mwenye kiburi na majivuno sana na sikugundua asili ya tabia yangu mwenyewe. Nilidhani nilikuwa nimefanya kosa tu, kwamba kunishughulikia namna hivyo kulikuwa kumekithiri. Hiyo ndiyo maana nilisalia katika uhasi, kumwelewa Mungu visivyo na kujilinda. Nikisoma maneno ya Mungu nilijiuliza kama kweli nilikuwa nimepogolewa na kushughulikiwa vikali sana kwa ajili ya kosa moja tu. Kuna kanuni ya jinsi nyumba ya Mungu inavyowashughulika na watu. Zote zinategemezwa kwa asili na kiini cha watu, na tabia yao kwa jumla. Kiongozi hakunishughulikia bila sababu nzuri. Kwa hivyo basi, ni matatizo yapi kweli yaliyokuwa ndani yangu yaliyosababisha nipogolewe na kushughulikiwa vikali sana?

Baadaye nilisoma maneno haya ya Mungu: “Kama kwa kweli una ukweli ndani yako, njia unayotembea kiasili itakuwa njia sahihi. Bila ukweli, ni rahisi kufanya uovu na hutakuwa na budi kuufanya. Kwa mfano, kama ungekuwa na kiburi na majivuno, ungeona kwamba haiwezekani kuepuka kumwasi Mungu; ungehisi kulazimishwa kumwasi. Hutafanya hivyo kimakusudi; utafanya hivyo chini ya utawala wa asili yako ya kiburi na majivuno. Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu na kumwona kuwa asiye na maana; vitakufanya ujiinue, vitakufanya kujiweka kila wakati kwenye maonyesho na mwishowe vitakufanya ukae katika nafasi ya Mungu na kujitolea ushuhuda mwenyewe. Mwishowe utafanya mawazo yako mwenyewe, fikira zako mwenyewe na dhana zako yawe ukweli wa kuabudiwa. Tazama ni kiasi gani cha uovu kinafanywa na watu chini ya utawala wa asili yao ya kiburi na majivuno! Kutatua matendo yao maovu, lazima kwanza watatue matatizo ya asili yao. Bila mabadiliko katika tabia, haitawezekana kuleta suluhu ya kimsingi kwa shida hii(“Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kuna pia mahubiri ambayo yanataja kwamba watu wengine wanapokuwa na kipaji kimoja au kingine, au wanapokuwa na ubora fulani wa tabia, wanawadharau wengine. Hawataki kumsikiliza mtu mwingine yeyote, wakidhani kwamba wao ni bora kuliko kila mtu mwingine. Mtu wa aina hiyo ni mwenye kiburi, mbinafsi, na mwenye kujidai. Nilifikiria kuhusu jinsi tangu nikuwe muumini, sikuwa nimelenga kufuatilia ukweli, lakini nilikuwa nimefanya wajibu wangu kwa kutegemea ubora wangu wa tabia na tabia yangu ya kiburi. Nilihisi kwamba nilizungumza vizuri na nilikuwa na mafanikio madogo kiasi katika wajibu wangu, kwa hivyo kiongozi alinithamini sana. Nilidhani kwamba nilikuwa mzuri na mwenye uwezo katika kazi, zaidi kuwaliko wengine, kwa hivyo sikufikiria sana kuhusu ndugu niliofanya nao kazi. Nilisisitiza kufanya mambo kwa njia yangu mwenyewe, na tabia yangu ya kiburi ilizidi kua. Baadaye, nilikuza mtazamo wa uzembe sana kwa kazi ya kanisa. Sikuwahi kutafuta kanuni za ukweli au kwenda kutafuta au kufanya ushirika na wengine. Badala yake, nilifanya mambo kiholela, jinsi nilivyotaka, na nikaishia kuivuruga kazi ya kanisa. Nilihisi daima kwamba nilikuwa mwenye ubora mzuri wa tabia na kwamba nilielewa ukweli fulani, lakini ni baada tu ya kufunuliwa ndipo mwishowe niliona kwamba kile nilichoelewa kilikuwa tu mafundisho kidogo, kwamba sikuwa na chembe ya uhalisi wa ukweli, wala sikuweza kushiriki kuhusu ukweli ili kutatua masuala ya vitendo. Licha ya haya, nilikuwa bado mwenye kiburi sana na nilitenda pekee yangu katika kila kitu. Nilikuwa mwenye kiburi kiasi kwamba nilipoteza mantiki yote na nilikosa kumwona Mungu. Tatizo langu lilifunuliwa tu kiongozi alipokuja kukagua kazi yangu. Nilifikiria kuhusu jinsi ambavyo nilikuwa nikifanya wajibu wangu siku zote. Mbali na kutowasaidia au kuwanufaisha ndugu zangu, pia nilifichua tabia nyingi potovu zilizowazuia. Sikuwa nikifanya wajibu wangu, nilikuwa nikifanya uovu tu! Kadiri nilivyofikiria zaidi kuhusu hilo, ndivyo nilivyoogopa zaidi. Nilijua kwamba mtu anapotenda kutokana na kiburi, haiwezekani kwake kujizuia kumpinga Mungu na kutenda maovu. Niliwafikiria ndugu wengine ambao walionekana kuwa wenye ubora wa chini wa tabia kuniliko, lakini walikuwa waangalifu na wasikivu katika wajibu wao. Walijua jinsi ya kutafuta ukweli na kukubali maoni ya wengine, wakati ambapo nilikuwa mwenye kiburi sana kiasi kwamba nilikosa kujitambua kabisa. Sikuwa na ufahamu wa jinsi ya kutafuta ukweli kabisa. Kadiri nilivyotafakari zaidi, ndivyo nilivyohisi njia yangu haikuwa ile ya kufuatilia ukweli. Nilikuwa mwenye kiburi sana na sikumfikiria Mungu hata kidogo, kwa hivyo nilipopogolewa na kushughulikiwa, na kufukuzwa kutoka katika wajibu wangu, kweli ni Mungu aliyekuwa Akinilinda na kuniokoa. Bila hiyo, sijui ningetenda maovu zaidi kiasi gani. Hata ningefikia hatua ambapo singeweza kubadilika na kukabiliwa na kufukuzwa. Kisha ningekuwa nimechelewa sana kujuta. Baada ya kuelewa nia njema za Mungu, nilijawa na majuto. Nilihisi kwamba kwa miezi sita iliyopita, nilikuwa nikimwelewa vibaya na kumlaumu Mungu, nilikuwa hasi na kuzembea kazini. Sikukubali kuambiwa chochote! Kuanzia wakati huo na kuendelea, nilitaka tu kutekeleza wajibu wangu vizuri ili kulipia makosa yangu ya zamani.

Miezi sita baadaye, nilichaguliwa kama kiongozi wa timu. Wakati huo, niliogopa sana kwamba ningejikwaa na nishindwe tena kwa sababu ya asili yangu ya kiburi. Masuala yalipoibuka katika wajibu wangu nilikuwa mwenye kutahadhari sana, na mara nyingi nilifanya majadiliano na kufanya ushirika na kina ndugu niliofanya nao kazi, tukitafuta ukweli ili kusuluhisha shida ndani ya kanisa. Nilihisi utulivu zaidi nilipokuwa nikifanya wajibu wangu kwa njia hiyo na nilikuwa na uhusiano mzuri zaidi na kina ndugu. Miezi michache baadaye niliona mafanikio kiasi katika wajibu wangu na nilianza kujisikia raha tena kwa siri, nikifikiri kuwa lazima nina talanta halisi, na kwamba bila kujali ni wajibu upi niliokuwa nikifanya, ningeweza kufanya mambo yaende haraka. Baada ya muda, tabia yangu ya kiburi ilianza kuonekana tena. Wakati mwingine ndugu walipokuwa na masuala ambayo walitaka kutafuta kuhusu na kiongozi, nilikosa kuwa mvumilivu kwao. Niliwaza, “Je, hatujatafuta kuhusu jambo hili hapo awali? Kwa nini unahitaji kutafuta zaidi? Ninajua kanuni, kwa hivyo ushirika wangu unapaswa kutosha.” Bila kuyafikiria mambo, nilishiriki ufahamu wangu na kina ndugu na kuwataka waukubali, lakini walihisi wasiwasi na kisha kutafuta kuhusu jambo hilo na kiongozi. Baadaye kiongozi alishiriki nasi juu ya kanuni za utendaji, ambazo zilikuwa tofauti na yale niliyoelewa hapo awali. Nilishangaa, na nikawaza, “Asante kwa kutafuta, la sivyo wajibu wetu ungeathirika.” Lakini baada ya tukio hilo, sikujifikiria au kujaribu kujijua mwenyewe. Nilisalia mwenye kiburi na asiye na busara. Nilipoona makosa katika wajibu wa kina ndugu, niliwakaripia kwa kuwaamrisha, nikiwaza, “Kama huwezi hata kufanya vizuri hiki kitu kidogo, unaweza kufanya nini? Sidhani kwamba unafanya hili kwa moyo wako wote.” Kwa muda, wale wengine walianza kuhisi kuzuiliwa na mimi na wakaanza kuwa mbali nami. Nilimzuia dada mmoja kiasi kwamba hakutaka hata kufanya wajibu wake tena. Nilijua kwamba nilikuwa mwenye makosa, lakini wakati wowote jambo lilipotokea, sikuweza kujizuia kufichua tabia yangu ya majivuno. Nikifikiria jinsi nilivyojikwaa na kushindwa hapo awali, nilihisi hofu kidogo, lakini wakati huo sikutafuta ukweli ili nitatue tatizo hilo.

Baadaye nilifanya uamuzi pekee yangu wa kumwambia dada achukue wajibu muhimu. Ndugu mmoja alinionya ya kwamba dada huyo alikuwa mdanganyifu, kwamba hakufaa sana kufanya wajibu muhimu. Niliwaza, “Ana matatizo kidogo, lakini si mabaya kama unavyosema. Ni nani asiye na upotovu na dosari?” Sikuchukua maoni ya ndugu huyu kwa uzito hata kidogo, lakini nilimtafuta tu dada huyo ili tufanye ushirika na nikamkumbusha kuhusu dosari zake. Nilishtuka alipoishia kuwa mnafiki kabisa na mzembe katika wajibu wake. Hili lilisababisha hasara kubwa kwa kazi ya nyumba ya Mungu. Kiongozi alipogundua kuhusu hili, alinishughulikia vikali sana, akisema: “Wewe ulifanya mambo yako mwenyewe tu, ukampandisha mtu mdanganyifu cheo. Ndugu alikuonya, lakini hukumsikiliza au ulichunguze mwenyewe. Na sasa imekuwa na athari mbaya sana na kusababisha usumbufu mkubwa sana. Hii ni kwa sababu ya wewe kukosa kuwajibikia wajibu wako. Huelewi ukweli na wewe ni mwenye kiburi. Lazima ubadilishwe!” Kupogolewa na kushughulikiwa vikali sana kulinitia uchungu. Nilifukuzwa kutoka katika wajibu wangu mbele ya ndugu wengine wengi sana, na kiongozi alisisitiza nilikuwa nimesababisha vurugu kubwa mno na kwamba ilibidi nibadilishwe. Nilihisi kwamba singeweza kustahimili tena, kwamba hakika ningeondolewa, na kufuatilia hilo zaidi hakungesaidia kazi. Nilikuwa hasi sana baada ya kubadilishwa. Nilifikiria juu ya kile kilichotokea nikiwa kitandani kila usiku na kuanza kulia. Nilihisi aibu sana kumwona mtu mwingine yeyote kwa muda mrefu sana. Niliona kwamba ndugu wote walikuwa wakifanya wajibu wao kwa furaha na nilihisi kwamba singelinganishwa na wao kwa sababu ya asili yangu ya kiburi. Bila kujadili na mtu yeyote au kusikiliza ushauri, nilimpandisha mtu mdanganyifu cheo, na kuivuruga sana kazi ya kanisa. Je, bado ningeweza kuokolewa na Mungu? Sikuwahi kufikiria kwamba njia yangu ya imani ingeweza kufika mwisho katika umri mdogo vile. Hata nilianza kushuku kwamba wakati Mungu alisema kupogolewa na kushughulikiwa vilikuwa wokovu, sio kuondolewa, hilo halikuwa hivyo kwangu. Moyo wangu ulikuwa umejaa suitafahamu. Wakati mmoja kiongozi alipokuja kushiriki na sisi nilijificha kwenye kona ya mbali kabisa. Nilishangaa sana wakati ghafla aliliita jina langu na kuniuliza nilikuwa nimefanya maendeleo gani karibuni. Aliuliza pia iwapo nilikuwa hasi baada ya kupogolewa na kushughulikiwa, na kisha akafanya ushirika nami kwa dhati na kunisihi, akisema “Wewe bado ni mchanga. Unapaswa kufuatilia ukweli na ulenge mabadiliko katika tabia.” Kusikia maneno haya ya dhati kutoka kwa kiongozi yalinifariji na kunitia moyo sana kiasi kwamba sikuweza kuacha kulia. Nilikuwa mwenye kiburi na majivuno, nisiyewajibika na hobelahobela katika wajibu wangu, na nilikuwa nimeidhuru kazi ya kanisa. Kiongozi alikuwa sahihi kunibadilisha na kunipogoa na kunishughulikia, lakini sikuwahi kufikiria angeweza kunitia moyo pia. Nilimshukuru Mungu kwa dhati kwa sababu ya rehema Zake. Usiku huo, nilimwomba Mungu nikilia machozi na nikaamua kujitafakari mwenyewe kwa kweli, na kutafuta ukweli ili nitatue tabia yangu ya kiburi.

Baadaye nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Kiburi ndicho chanzo cha upotovu wa mwanadamu. Kadiri watu wanavyozidi kuwa na kiburi, ndivyo wanavyozidi kuwa na uelekeo wa kumpinga Mungu. Tatizo hili ni kubwa kiasi gani? Siyo tu kwamba watu wenye tabia ya kiburi humfikiria kila mtu mwingine kuwa duni kuwaliko, lakini lililo baya zaidi, wao hata huwa na mtazamo wa udhalilishaji kwa Mungu. Hata ingawa, kwa nje, watu wengine wanaweza kuonekana kana kwamba wanamwamini Mungu na kumfuata, hawamchukulii kama Mungu hata kidogo. Wao huhisi sikuzote kuwa wanamiliki ukweli na wanajipenda mno. Hiki ndicho kiini na chanzo cha tabia ya kiburi, na hutoka kwa Shetani. Kwa hivyo, tatizo la kiburi lazima litatuliwe. Kuhisi kuwa wewe ni bora kuliko wengine—hilo ni jambo dogo. Suala la muhimu ni kwamba tabia ya kiburi ya mtu humzuia mtu kumtii Mungu, sheria Yake, na mipango Yake; mtu kama huyo daima huhisi kuwa na uelekeo wa kushindana na Mungu kuwatawala wengine. Mtu wa aina hii hamchi Mungu hata kidogo, sembuse kumpenda Mungu au kumtii. Watu ambao ni wenye kiburi na wenye majivuno, hasa wale ambao ni wenye kiburi mno hadi kiwango cha kupoteza akili zao, hawawezi kumtii Mungu katika imani yao Kwake, na hata hujiinua na kujishuhudia wenyewe. Watu kama hao ndio humpinga Mungu zaidi. Kama watu wanataka kufikia mahali ambapo wanamcha Mungu, basi lazima kwanza watatue tabia zao za kiburi. Kadiri unavyotatua tabia yako ya kiburi kikamilifu, ndivyo utakavyokuwa na uchaji zaidi kwa Mungu, na ni hapo tu ndipo utakapoweza kumtii Yeye na uweze kupata ukweli na kumjua(Ushirika wa Mungu). Ni kupitia ufunuo wa maneno ya Mungu tu ndiyo niliona kwamba kutenda kulingana na asili yangu ya kiburi halikuwa tu suala la kufichua upotovu kidogo, lakini kwa kiwango kikubwa kulinifanya niwadharau wengine kabisa na hata kumdharau Mungu. Kulinifanya nimwasi na kumpinga Mungu, bila mimi mwenyewe kutaka. Nikikumbuka wakati nilipokuwa nikifanya wajibu wangu, kila wakati nilihisi kama mtu mwerevu na mwenye ubora mzuri wa tabia, kwa hivyo nilitegemea vipaji na ubora wangu wa tabia kufanya wajibu wangu. Nilijiamini sana kiasi kwamba nilimwomba Mungu au kutafuta kanuni za ukweli kwa nadra sana. Hakukuwa na nafasi ya Mungu moyoni mwangu. Wakati wajibu wangu haukuzaa matunda nilikuwa na tabia njema, lakini punde nilipoelewa kanuni kidogo na nilikuwa na mafanikio kidogo, nilitumia hilo kama mtaji wangu. Nilihisi kwamba chochote nilichofanya kitakuwa sawa, ningeweza kufanya chochote, kwamba ningeweza kuwakadiria watu na hali, bila shida, na kwa hivyo nikawa mwenye kiburi zaidi, mbinafsi na mwenye kujidai, nikifanya vitu kwa njia yangu mwenyewe katika kila kitu, nikiwa dikteta. Hata niliwazuia kina ndugu kutafuta ukweli na kiongozi na nikiwalazimishia fikira zangu, kana kwamba zilikuwa ukweli, nikiwafanya wazikubali na kuzitii. Ukweli ulinionyesha kwamba nilikuwa nikitenda kulingana na asili yangu ya kiburi, kwamba niliwazuia na kuwadhuru tu kina ndugu, na kuivuruga kazi ya kanisa vibaya. Nilikuwa hata nimechukua nafasi ya mtumishi wa Shetani. Kiongozi kunishughulikia, kukemea vurugu hii kubwa, kulikuwa sahihi kabisa. Kufukuzwa kutoka katika wajibu wangu ilikuwa haki ya Mungu kabisa. Mwishowe niliona jinsi aina hiyo ya asili ya kiburi ilivyo ya kutisha na hatari. Ikiachwa bila kusuluhishwa, ningekuwa katika hatari ya kufanya uovu na kumpinga Mungu wakati wowote, na ningeivuruga kazi ya nyumba ya Mungu, kuikosea tabia ya Mungu, na kuondolewa na kuadhibiwa. Baada ya kubadilishwa matatizo mengine katika wajibu wangu yaliibuka. Nikikabiliwa na kusuta kwa kina ndugu, na matatizo yaliyofunuliwa katika wajibu wangu, nilijuta sana na kujilaumu. Nilijichukia kweli. Kwa nini nilikuwa mwenye kiburi sana? Nilihisi daima kwamba nilikuwa na talanta, kwamba chochote nilichofanya kilikuwa sawa, lakini nilikuwa nimefanya hata vitu vichache vilivyomridhisha Mungu? Wajibu nililokuwa nimefanya haukuwa mzuri, na nilikuwa tu msumbufu. Kama ningekuwa na uchaji kiasi kidogo tu kwa Mungu, kama ningeomba au kutafuta zaidi, au kama ningefanya ushirika na kujadili mambo na wengine, kama ningekuwa mwangalifu zaidi kidogo, singefikia hatua ya mimi kufanya mambo mengi ya kumwasi Mungu.

Katika juhudi yangu ya kutatua asili yangu ya kiburi, baadaye nilisoma baadhi ya maneno ya Mungu, na ushirika fulani. “Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya Mungu, au kushughulikiwa, kufunzwa nidhamu, na kupogolewa na maneno Yake. Ni baada ya hapo tu ndipo wanaweza kutimiza utiifu na ibada kwa Mungu, na wasijaribu tena kumdanganya Yeye na kumshughulikia kwa uzembe. Ni kupitia kwa usafishaji wa maneno ya Mungu ndio watu hupata mabadiliko katika tabia. Ni wale tu wanaopitia mfichuo, hukumu, kufundishwa nidhamu, na kushughulikiwa kwa maneno Yake ambao hawatathubutu tena kufanya mambo kwa kutojali, na watakuwa watulivu na makini. Jambo muhimu sana ni kwamba wanaweza kutii neno la sasa la Mungu na kutii kazi ya Mungu, na hata kama hayalingani na fikira za binadamu, wanaweza kuweka kando fikira hizi na kutii kwa hiari(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu). Ninaposoma kifungu hiki tena, ninashukuru sana kwamba njia pekee ya kutatua asili ya kiburi ya mtu ni kukubali kuhukumiwa, kuadibiwa, kupogolewa, na kushughulikiwa na Mungu. Kupotoshwa kwetu na Shetani ni kwa kina sana, kwa hivyo tukitegemea tu kusoma maneno ya Mungu na tafakari ya kibinafsi, ufahamu wetu kujihusu utakuwa wa juujuu na tabia zetu potovu hazitabadilika. Bila Mungu kunifunua, kunipogoa na kunishughulikia muda baada ya muda, bado ningekuwa najiamini kupita kiasi na nifikiri kwamba nilikuwa mtu wa maana sana. Singejijua hata kidogo. Kwa kweli singejua jinsi nilivyokuwa mwenye kiburi au jinsi tabia yangu ya kishetani ilivyokuwa mbaya sana. Sasa, ninapokumbuka kila kitu nilichofanya, ninahisi aibu na majuto sana. Mimi hujikunyata ninapoyafikiria na siwezi hata kuinua kichwa changu. Lakini ni funzo hilo chungu ambalo liliniruhusu kupata ufahamu kidogo wa asili yangu ya kiburi, na kujua ni wapi nilipokuwa na uwezekano wa kujikwaa na kushindwa. Pia ilinifanya niwe na uchaji kiasi kwa Mungu. Niliona pia kwamba nilikosa uhalisi wa ukweli na moyo unaotafuta ukweli katika wajibu wangu. Nilikuwa fidhuli, dikteta na msumbufu. Nikilinganishwa na wale ndugu waliokuwa na ubora wa tabia wa kiwango cha wastani, lakini waliofanya wajibu wao kwa uangalifu, sikuwa kitu. Kiburi changu hakikuwa na msingi. Baada ya kugundua haya yote, nilikuwa mnyenyekevu zaidi katika wajibu wangu na sikujiamaini kupita kiasi tena. Nilijizoeza kujiweka kando kwa kujua na kujikana, nilitafuta kanuni za ukweli zaidi na nikawasikiza kina ndugu zaidi. Nilianza kuwa na majadiliano ya wazi kutatua matatizo yoyote kanisani. Wakati mwingine nilipoonyesha kiburi changu tena, au nikakiuka kanuni katika wajibu wangu, nilitenda kujiweka kando, na kukubali kupogolewa na kushughulikiwa, na vile vile mwongozo na usaidizi wa wengine. Baada ya muda, nilihisi kwamba kutenda kwa njia hiyo kulikuwa na manufaa sana. Kwa kuwa ufahamu wangu wa ukweli ulikuwa wa juu juu na sikuwa na utambuzi katika mambo mengi, kwa kufanya kazi na kina ndugu na kuyalinganisha maoni ya kila mtu, niliweza kupata ufahamu zaidi wa mambo. Kwa kufanya wajibu wangu kwa njia hiyo, kabla ya kujua, nilikuwa nimepata ulinzi wa Mungu. Sikufanya tena makosa makubwa wala kuwa na shida kubwa, na chini ya usimamizi wa kina ndugu, asili yangu ya kiburi ilipunguka kidogo. Kuweka haya katika vitendo kulinipa hisia ya amani na utulivu, na polepole, nilipunguza kutenda kutokana na kiburi zaidi na zaidi. Wakati mmoja, dada aliyefanya kazi pamoja nami alisema, “Nimekujua kwa karibu miaka miwili sasa. Zamani ulikuwa mwenye kiburi sana na kila wakati watu wengine walihisi kuzuiliwa na wewe, lakini sasa umebadilika kweli.” Wakati huo nilihisi kama kwamba nilikuwa karibu kulia. Nilikuwa mwenye kiburi sana. Kubadilika hata kidogo hivi hakukufanyika kwa urahisi. Nikikumbuka miaka michache iliyopita, nyakati hizo mbili zisizosahaulika za kupogolewa na kushughulikiwa ndizo zilizonisaidia sana na kuninufaisha sana. Kama singepitia hayo, nina uhakika kwamba hata singekuwa na ubinadamu sahihi, kwamba singemfikiria Mungu hata kidogo. Ningekuwa kwenye eneo la hatari, ukingoni mwa kumpinga Mungu wakati wowote. Sasa ninajua kwa kweli kwamba kupogolewa na kushughulikiwa ni ulinzi na wokovu wa Mungu kwangu.

Iliyotangulia: 67. Kuishi kwa Kudhihirisha Mfano Kidogo wa Mwanadamu Hakika Ni Vizuri

Inayofuata: 69. Kurudi kwenye Njia Sahihi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

61. Ukweli Umenionyesha Njia

Na Shizai, JapaniMwenyezi Mungu anasema, “Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe...

62. Kuinuka licha ya kushindwa

Na Fenqi, Korea ya KusiniKabla ya kumwamini Mungu, nilifundishwa na CCP, na sikufikiria chochote ila jinsi ya kufaulu kutokana na juhudi...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp