69. Kurudi kwenye Njia Sahihi

Chen Guang, Marekani

Mwenyezi Mungu anasema, “Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe kumhudumia Mungu. Kama tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa na neno la Mungu, basi tabia yako bado inamwakilisha Shetani. Hii inatosha kuthibitisha kwamba huduma yako kwa Mungu ni kutokana na nia yako nzuri wewe binafsi. Ni huduma inayotokana na asili yako ya kishetani. Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya binadamu ya kuishi katika dunia. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hakika watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo na wapinga Kristo watakaowadanganya watu katika siku za mwisho(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku). Ninaposoma kifungu hiki, “Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe kumhudumia Mungu. Kama tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa na neno la Mungu, basi tabia yako bado inamwakilisha Shetani.” naguswa sana. Nimepiata kushindwa hapo zamani. Nilitekeleza wajibu wangu kulingana na tabia ya kiburi, na nilijigamba sana. Nilijionyesha, huku nikihubiri maneno ya kawaida na mafundisho ili kuwafanya watu waniheshimu na kunipenda sana, na bila hata kujua, nilitembea kwenye njia ya kumpinga Mungu. Ilikuwa tu baadaye, kupitia hukumu na ufunuo wa maneno ya Mungu, nilipokuja kugundua chanzo cha upinzani wangu kwa Mungu na asili yangu ya kishetani, na nikaanza kutubu kwa Mungu.

Ilikuwa mwaka wa 2013 nilipochaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa. Wakati huo nilikuwa na shauku sana. Kila nilipowaona ndugu zangu wakiwa mashakani, nilishiriki nao juu ya maneno ya Mungu ili kuwasaidia kutatua matatizo yao. Mara baada ya shida za kila mtu kutatuliwa, waliweza kutekeleza wajibu wao kama kawaida. Baada ya miezi michache, kiongozi wangu aliniambia, “Kuna kanisa ambalo lina idadi kubwa ya kina ndugu waliojiunga hivi karibuni, na wafanyakazi wenzako wote wamependekeza kwamba uende huko kuhudumu kama kiongozi.” Nilikubali huku nikiwa nimejiamini kabisa. Nilifikiri tu kwamba nilipaswa kufanya kazi ya kuwanyunyizia wale kina ndugu vizuri ili waweze kuelewa ukweli haraka iwezekanavyo na kuweka misingi kwenye njia ya kweli. Baada ya kufika kanisani, nilipata kuelewa hali ya jumla ya mahali pale, na pia niliandika maelezo juu ya matatizo na shida za kina ndugu, na kupanga kutafuta vifungu husika vya maneno ya Mungu baadaye ili kushiriki na kusuluhisha matatizo yao. Nilihisi kwamba kwa sababu nilikuwa mgeni kule, ndugu wengi hawakunijua, na kwa hivyo ilinibidi nitie bidii na kukusanyika pamoja nao ili kufanya ushirika zaidi. Iwapo ningefanya kazi ya kanisa vizuri kwa muda mfupi, basi ndugu hawa bila shaka wangehisi kwamba nilikuwa na uhalisi wa ukweli, na nilikuwa hodari katika kazi yangu— na kama hilo lingefanyika, basi viongozi wangu pia wangeniheshimu. Baadaye kanisa lilitoa taarifa kuhusu ukweli ambao tulipaswa kuingia ndani yake katika hatua hiyo, na kwamba tulipaswa kutafuta vifungu husika vya maneno ya Mungu vya kushiriki kuhusu. Nilifurahi sana kwa sababu hii ilikuwa nafasi nzuri ya kujionyesha. Kwa hivyo nilitafuta matamshi kadhaa ya Mungu ambayo yalihusiana na vipengele hivi vyote vya ukweli, na kisha nikayapanga kwa makini zaidi, wakati wote nikifikiri, “Imetukia tu kwamba mkutano wa wafanyakazi wenza utafanyika kesho. Wafanyakazi wenzangu wataona kwamba nilikaa macho usiku kucha nikitafuta maneno haya ya Mungu, na hakika watasema kwamba mimi ni mwangalifu na mwaminifu katika wajibu wangu.” Na kwa hivyo, ilikuwa karibu mapambazuko kabla ya mimi kumaliza kuandaa. Kwa hakika, wakati wa mkutano, baada ya wafanyakazi wenzangu kuona maneno ya Mungu niliyokuwa nimetafuta, wote walinstahi. Wengine walisema, “Mwangalieni Ndugu Chen! Yeye ni mwangalifu sana. Alikaa macho usiku kucha akitafuta vifungu hivi vyote vya maneno ya Mungu.” Wengine walisema, “Ni kweli kabisa! Inaonekana kwamba Ndugu Chen husoma maneno ya Mungu sana.” Ndugu aliyekuwa mwenyeji alisema kwa wasiwasi, “Ndugu Chen, ulilazimika kukaa hadi saa ngapi ndipo upate vifungu hivi vyote vya maneno ya Mungu?” Kusikia haya yote kulinifanya nijawe na furaha. Kukaa kwangu macho hadi alfajiri hakukuwa bure, na ndugu zangu waliweza kuona jinsi nilivyotia bidii. Huku nikificha msisimko niliohisi ndani, nilisema, “Ilikuwa karibu alfajiri nilipomaliza kuvitafuta. Mimi hukaa usiku kucha ili kutimiza wajibu wangu, kama inavyopasa. Si kitu cha kujivunia. Ilinibidi nihakikishe kwamba ndugu zangu hawatazuiwa kushiriki kwenye mikutano.” Ndugu mwenyeji kisha alisema kwamba nilikuwa mwangalifu katika wajibu wangu, na kwamba niliweza kukaa macho usiku kucha na kuvumilia dhiki. Moyo wangu ulijaa furaha tele. Ilinibidi niendelee kufanya kazi kwa bidii ili ndugu zangu wote waseme kwamba mimi ni kiongozi hodari.

Baadaye, kazi ya kueneza injili ilipokuwa ikiendelea, tulianzisha makanisa mengine machache. Kila siku, nilifanya kazi kuanzia alfajiri hadi jioni, nikizunguka katika kila kanisa ili kuwanyunyizia ndugu zangu. Nilimsomea mtu yeyote aliyekuwa na tatizo maneno ya Mungu, na kufanya ushirika kwa uvumilivu ili kutatua matatizo yake, na watu wakazidi kuniheshimu. Wakati mmoja, ndugu wachache walikabiliwa na tatizo walipokuwa wakieneza injili na hawakuweza kulisuluhisha. Walianza kuwa hasi na dhaifu, kwa hivyo walinijia ili kufanya ushirikia kulihusu. Nilishiriki nao niliyoyapitia nikieneza injili hapo zamani. Nilisema, “Watu niliokuwa nikiwaenezea injili walikuwa na maoni na hawakuikubali. Baadhi yao walinifukuza nyumbani kwao. Wakati huo, pia nilidhani ilikuwa vigumu sana, kwa hivyo nilimwomba Mungu kila wakati. Nilikaa macho usiku kucha nikitafuta vifungu husika vya maneno Yake, na mara kwa mara nilienda kufanya ushirika na watu hao ili kutatua matatizo yao. Nilifanya hivyo ili waweze kusikia sauti ya Mungu na kupewa wokovu Wake katika siku za mwisho. Bila kujali nilifedheheshwa au kukabiliwa na dhiki kiasi gani, nilikataa kukata tamaa. Mwishowe, niliwaleta wote zizini….” Nilipomaliza kuongea, ndugu mmoja alisema kwa kusifu, “Hebu mwangalieni ndugu yetu Chen. Anajua sana jinsi ya kuvumilia dhiki. Yeye kweli hubeba mzigo.” Wengine walisema, “Sote tunapaswa kueneza injili kama ambavyo Ndugu Chen hufanya.” Nilipoona jinsi kina ndugu hawa walivyoniheshimu, nilihisi furaha mno. Baadaye, wengine waliokabiliwa na matatizo katika wajibu wao walikuja kunitafuta wakinuia kupata msaada, na wachache sana walimwendea ndugu niliyefanya kazi naye. Kina ndugu walipokuwa wakitimiza wajibu wao, walifanya kwa bidii chochote nilichowaambia. Nilipoona jinsi walivyoniheshimu sana, nilianza kujithamini zaidi na zaidi; nilihisi kama kwamba nilikuwa nguzo ya kanisa.

Wakati wa mkutano mmoja, nilizungumza kirefu juu ya jinsi nilivyoteseka na gharama nilizolipa katika wajibu wangu, na matokeo niliyokuwa nimefanikisha. Dada mmoja aliniambia ghafla, “Ndugu Chen, mimi husikia ukisema sanasana juu ya jinsi ulivyoteseka na kujitumia ulipokuwa ukitimiza wajibu wako, lakini hujazungumza kuhusu udhaifu uliokuwa nao ulipokabiliwa na dhiki au tabia potovu ulizofichua, au maarifa uliyojipatia, au jinsi ulivyotafuta ukweli ili kutatua shida zako. Hilo linafanya ionekane kana kwamba huna upotovu wowote hata kidogo….” Alipomaliza kusema hayo, wengine wote walinitazama tu. Nilishtuka. Nilihisi kwamba nilifedheheshwa, na uso wangu ukawa mwekundu. Niliwaza moyoni, “Kunizungumzia kwa njia hiyo kumenifanya nionekane mpumbavu mbele ya ndugu hawa wote. Watanionaje?” Ili kujaribu kupata tena heshima, nilisema upesi, “Dada, kile ambacho umeshiriki ni sahihi, na naweza kukikubali. Hata hivyo, ndugu zetu wanakabiliwa na shida katika wajibu wao, na wanaanza kua hasi na dhaifu. Hatupaswi kuongea tu juu ya upotovu wetu. Hatuna budi kushiriki zaidi juu ya utendaji unaosaidia; hivi pekee ndivyo kina ndugu zetu wanaweza kuwa na njia ya kusonga mbele na kupata imani yao….” Baadaye, kina ndugu wengine waliniambia kwamba nilipozungumza juu ya uzoefu na maarifa yangu, sikuzungumza juu ya upotovu mwingi uliofichuliwa ndani yangu, na kwamba kwa kuwa nilisema mengi sana juu ya jinsi nilivyoteseka, gharama niliyolipa, na jinsi nilivyoukana mwili wangu katika wajibu wangu, ilinifanya nionekane kana kwamba nilikuwa hodari kabisa katika kutenda ukweli. Nikiwa nimekabiliwa na maonyo haya kutoka kwa ndugu zangu, niliona aibu kidogo. Je, mambo haya niliyokuwa nikiyashiriki kweli hayakufaa? Wakati mwingine nilifanya ushirika juu ya jinsi nilivyokuwa na kiburi na ubinafsi. Aidha, nilipata matokeo mazuri katika wajibu wangu kila wakati, na sikuzuia kazi ya kanisa. Kwa hivyo hiyo ilimaanisha kwamba hakukupaswa kuwa na kosa lolote katika jinsi tulivyokuwa tukishiriki, siyo? Na kwa hivyo, sikutafakari juu yangu kwa dhati. Kwa hivyo uligunduaje mambo haya baadaye?

Baadaye, nilihamishiwa katika kanisa lingine ili kuendelea na kazi yangu kwa sababu wajibu wangu ulihitaji hivyo. Wakati wa mkutano wa wafanyakazi wenzangu, Ndugu Zhang aliniambia kwa sauti ya mashaka, “Ndugu Chen, tangu ulipoondoka katika kanisa hilo lingine, ndugu wengine kule wamepoteza hamu ya kufanya wajibu wao. Kila wanapokabiliwa na tatizo fulani, hawasomi maneno ya Mungu wala kutafuta ukweli; wanataka tu wewe utatue matatizo yao. Wengine hata wameacha kutaka kuhudhuria mikutano. Hii inaonyesha kuwa hujakuwa ukimtukuza Mungu au kumshuhudia katika wajibu wako. Umekuwa tu ukijionyesha ili wengine wakuheshimu na kukupenda sana. Hiki ni kitendo kiovu, na unahitaji kutafakari juu yako mwenyewe!” Baada ya kusikia kile alichosema, nilishangazwa sana. Je, hili lilitokeaje? Ndugu zangu wote walinipenda sana? Hili lilikuwa tatizo kubwa! Nilijawa na hofu sana. Baada ya hapo, sikusikia lolote lililosemwa wakati wa mkutano huo; nilikanganyikiwa. Sikujua nilipaswa kufaulu vipi katika hali hii. Baada ya kufika nyumbani, niliendelea kufikiria maneno ya Ndugu Zhang. Mwanzoni, nilidhani kwamba wajibu wangu ulikuwa umepata matokeo kiasi tu na kwamba niliweza kufanya ushirika juu ya ukweli ili kutatua baadhi ya matatizo. Sikufikiri hata kidogo kwamba kutakuwa na matokeo ya aina hii. Kwa kweli, jambo hili lilinifadhaisha mno. Katika kutojiweza kwangu, nilimwomba Mungu. Nilisema, “Mungu, tafadhali nipe nuru ili niweze kupata chanzo cha tatizo langu na niweze kujielewa kwa kweli.”

Baadaye, niliona baadhi ya maneno ya Mungu, “Wote wanaoanguka wanajikuza na kujitolea ushuhuda wao wenyewe. Wao huenda wakijisifu na kujitwalia zaidi, na hawajamweka Mungu moyoni hata kidogo. Je, mmepitia chochote Ninachozungumza kuhusu? Watu wengi wanajitolea ushuhuda bila kukoma: ‘Nimeteseka kwa njia hii na ile; nimefanya kazi hii na ile; Mungu amenitendea kwa njia hii na ile; Aliniuliza nifanye hiki na kile; Ananifikiria kwa heshima hasa; sasa niko namna hii na ile.’ Wanazungumza kwa sauti fulani kwa makusudi na kuchukua msimamo fulani. Hatimaye, watu wengine huishia kufikiri kwamba watu hawa ni Mungu. Punde wanapofikia hatua hiyo, Roho Mtakatifu atakuwa amewaacha muda mrefu uliopita. Ingawa, kwa sasa, wanapuuzwa, na hawatimuliwi, hatima yao imewekwa, na kile wanachoweza kufanya ni kusubiri adhabu yao tu(“Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Huku wengine wakiweza kutumia vyeo vyao kushuhudia mara kwa mara kuhusu wao wenyewe, kujiongezea zaidi umaarufu wao, na kushindana na Mungu kwa ajili ya watu na hadhi. Wanatumia mbinu na njia mbalimbali kuwafanya watu kuwaabudu, kujaribu mara kwa mara kuwa na ufuasi mkubwa wa watu na kutaka kuwadhibiti watu hao. Baadhi hata hupotosha kimakusudi watu na kuwafanya kufikiria kwamba wao ni Mungu ili waweze kuchukuliwa kama Mungu. Hawawezi katu kuwaambia watu kwamba wamepotoshwa, kwamba pia wao wamepotoka na wana kiburi, na hivyo basi hawafai kuwaabudu, na kwamba haijalishi watafanya vyema kiasi kipi, haya yote ni kutokana na utukuzaji wa Mungu na kile wanachostahili kufanya kwa kweli. Kwa nini hawasemi mambo haya? Kwa sababu wana hofu kuu ya kupoteza nafasi yao ndani ya mioyo ya watu. Hii ndiyo maana watu kama hao hawamtukuzi Mungu katu na katu hawamshuhudii Mungu(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I). Baada ya kusoma maneno ya Mungu, nilifadhaika sana. Ni baada tu ya kutafakari juu yangu ndipo niliona kwamba ingawa kwa nje nilikuwa nimeonekana kuteseka na kulipa gharama, na nilishiriki na ndugu zangu juu ya maneno ya Mungu ili kutatua matatizo yao, nilikuwa kwa kweli nikifanya hivyo ili nijitokeze na kujionyesha ili wengine waniheshimu na kunipenda sana. Nikikumbuka wakati ambapo wafanyakazi wenzangu walipendekeza niwe kiongozi katika kanisa lililokuwa na washiriki wapya, niligundua kuwa nilifikiria tu jinsi ambavyo ningepata mafanikio ambayo yangewafanya kina ndugu na kiongozi wangu waniheshimu. Kwa hivyo, nilifanya kazi ya ovataimu, nikikaa usiku kucha ili kutafuta vifungu husika vya maneno ya Mungu na kuandaa kile nitakachoshiriki kuhusu mikutanoni. Ndugu zangu walipokabiliwa na shida wakati wa kueneza injili, sikufanya ushirika nao juu ya mapenzi ya Mungu ili kuwaongoza katika kanuni za ukweli, lakini badala yake nilijigamba na kuonyesha jinsi nilivyokuwa nimeteseka na gharama niliyolipa wakati wa kueneza injili. Kazi yangu ilipoanza kufanya vizuri zaidi, ndugu zangu walinisifu. Nilikuwa nimefurahia hayo, na kujisifu kwa kazi iliyofanikishwa na Roho Mtakatifu, na kuringa bila aibu kana kwamba yalikuwa mafanikio yangu. Nipokuwa nikishiriki kwenye mikutano, nilijionyesha mara kwa mara mbele ya watu, huku nikishiriki tu utendaji chanya na kuepuka kutaja tabia zozote potovu ambazo nilikuwa nimefichua. Mada hiyo ilipotokea, sikueleza kinaganaga. Kuhusiana na nia zangu za aibu za kutekeleza wajibu wangu, nilisita hata zaidi kuzichambua au kuzifichua. Mara kwa mara, Mungu alikuwa amewatumia ndugu zangu kutaja matatizo yangu, lakini ili kulinda cheo na picha yangu, nilisema tu kwa maneno kwamba nilikubali maoni yao, lakini kwa kweli sikutafakari kujihusu hata kidogo. Wakati wa ushirika niliendelea tu kunena kwa mbwembwe ili kuwadanganya ndugu zangu. Kwa njia hiyo, nilikuja kuamini kwamba nilikuwa mwaminifu katika wajibu wangu na ningeweza kuvumilia dhiki na kulipa gharama. Tatizo au shida yoyote ambayo kanisa lilikuwa nayo, au hali yoyote ambayo ndugu zangu walikuwamo, sikusita, lakini niliwasaidia kupata suluhisho kila wakati. Nilipofunuliwa na ukweli, niliona kwamba nilipokuwa nikifanya wajibu wangu, sikuwa nikitenda ukweli hata kidogo, wala sikuzingatia mapenzi ya Mungu. Nilikuwa nimetumia fursa iliyotolewa na kutimiza wajibu wangu kujionyesha ili wengine waniheshimu, na hivyo kuridhisha tamaa yangu ya umaarufu na cheo. Kwa kufanya hivi, sikuwaleta ndugu zangu mbele za Mungu; badala yake, niliwafanya waniabudu. Hii ilimaanisha kwamba nilikuwa nikishindana na Mungu kwa ajili ya watu na cheo. Wakati huo tu ndipo nilijua ukweli kwamba nilikuwa tayari nimetembea kwenye njia ya kumpinga Mungu na kutenda dhambi kubwa. Niliogopa na nilihisi mwenye hatia sana. Kisha nikajiuliza: Je, nimeingiaje katika njia ya kumpinga Mungu bila kujua?

Baadaye, nilisoma kifungu fulani cha maneno ya Mungu: “Kwa kuwa wanadamu walipotoshwa na Shetani, asili yao ilianza kubadilika na polepole wakapoteza mantiki ya watu wa kawaida. Sasa hawatendi tena kama wanadamu katika nafasi ya mwanadamu; badala yake, wanataka kuipita hadhi ya mwanadamu, na wanatamani sana kuwa na kitu cha juu zaidi na zaidi. Na hiki kitu cha juu zaidi ni kipi? Wanatamani kumpita Mungu, kuzipita mbingu, na kuvipita vingine vyote. Je, chanzo cha sababu ya watu kuwa hivi ni kipi? Hatimaye, asili ya mwanadamu ni ya kiburi kupindukia. … Punde watu wanapokuwa wenye kiburi katika asili na kiini, wanakuwa na uwezo wa kufanya vitu ambavyo vinamkaidi na kumpinga Mungu, vitu ambavyo haviyatii maneno Yake, vitu vinavyoibua maoni kumhusu, vitu vinavyomwasi, na vitu vinavyowatukuza na kuwashuhudia wenyewe. Wewe unasema kwamba huna kiburi, lakini tuseme upewe makanisa kadhaa na uruhusiwe kuyaongoza; tuseme Sikukushughulikia, na kwamba hakuna yeyote katika familia ya Mungu aliyekupogoa: Baada ya kuwaongoza kwa muda, utawaelekeza miguuni pako na uwafanye watii mbele yako. Na kwa nini ufanye hivyo? Hili litaamuliwa na asili yako; litakuwa ufichuzi wa kiasili tu. Huhitaji kufanya bidii sana ili kujifunza hili, wala sio lazima upate wengine wakufunze kuhusu hili. Huhitaji kufanya lolote kati ya haya kwa makusudi; hali ya aina hii hukujia kwa kawaida: Unawafanya watu watii mbele yako, wakuabudu, wakutukuze, washuhudie kukuhusu, na wakusikilize katika kila jambo, na huwaruhusu wazidi mamlaka yako. Chini ya uongozi wako, hali kama hizi zinatokea kwa kawaida. Na hali hizi hutokea vipi? Zinaamuliwa na asili ya mwanadamu yenye kiburi(“Asili yenye Majivuno ya Mwanadamu Ndiyo Chanzo cha Upinzani Wake kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kusoma maneno ya Mungu kulinifanya nielewe ni kwa nini nilitaka kumridhisha Mungu katika wajibu wangu lakini nilikuwa nimeanza kutembea kwenye njia ya kumpinga bila kukusudia. Chanzo cha hilo kilikuwa asili ya kishetani ya kiburi iliyokuwa ndani yangu. Chini ya udhibiti wa asili yangu ya kiburi, nilijiheshimu sana, na mara nyingi nilijaribu kujionyesha katika usemi na vitendo ili wengine waniheshimu na kunipenda sana. Ndugu zangu walipopata shida wakati wa kutekeleza wajibu wao, sikushiriki kuhusu kanuni za ukweli ili kuwafanya waelewe ukweli na wawe na njia ya kutenda, lakini nilisema tu maneno na mafundisho ya juujuu ili nionekane kuwa mzuri, na hata nilitumia uzoefu wangu wa kuteseka na kufanya kazi kama mtaji wa kutumia kujionyesha. Hii iliwafanya ndugu zangu waniheshimu na waamini kuwa nilielewa ukweli na ningeweza kutatua shida zao. Kila walipokabiliwa na shida yoyote, walinijia kila mara, bila kujua kwamba walipaswa kumtegemea Mungu na kutafuta ukweli ili kusuluhisha matatizo yao. Hawakuwa na mahali pa Mungu mioyoni mwao. Ilifika hata wakati ambapo baada ya mimi kuhamishwa, kina ndugu wengine hawakutaka kuhudhuria mikutano tena. Je, huko kungewezaje kuitwa kutimiza wajibu wangu? Nilikuwa tu nikifanya uovu na kumpinga Mungu! Mimi kuweza kutenda uovu kama huo kulitokana kabisa na kiburi na majivuno yangu. Nilitaka tu kutawala watu kimwinyi huku nikilinda hadhi na picha yangu, na kuwafanya ndugu zangu wote waniabudu na wawe na matumaini juu yangu. Nilitamani sana baraka ya hadhi yangu. Niliweza kuona kwamba ndani yangu kabisa, sikumcha Mungu hata kidogo. Unapoishi kuishi kwa kutegemea asili ya kiburi, kumpinga Mungu hufanyika bila hiari. Ni hatari mno. Nilifikiria wachungaji na wazee katika ulimwengu wa kidini. Hawamtukuzi Mungu au kumshuhudia, wala hawawaongozi waumini katika kutia maneno ya Bwana katika vitendo. Badala yake, wao hufasili maarifa ya kibiblia na nadharia ya kitheolojia kwa upofu ili kuwadanganya waumini, na kuonyesha jinsi ambavyo wameteseka, uzuri ambao umetokana na injili waliyoeneza, na idadi ya makanisa ambayo wameanzisha. Hii husababisha waumini wawaabudu, wawaheshimu, na kufanya chochote wanachosema. Wengine wamesoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kusikia sauti ya Mungu, lakini hata hivyo, wanaenda kuwauliza wachungaji na wazee na kuyachunguza pamoja nao. Bila idhini ya wachungaji, hawathubutu kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu hata kama wanajua ni njia ya kweli. Wachungaji na wazee wa ulimwengu wa dini huwadhibiti kikamilifu. Wanatembea kwenye njia ya mpinga Kristo ya kumpinga Mungu, na wanajaribu kuunda ufalme wa kujitegemea! Nilijaribu mara nyingi kujionyesha katika wajibu wangu ili watu waniheshimu na kunistahi. Je, nilikuwa na tofauti gani na hao wachungaji na wazee? Niliwafikiria wale kina ndugu waliokuwa katika kanisa hilo lililokuwa na washiriki wapya: Walikuwa wamekubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho hivi karibuni, na bado kulikuwa na ukweli mwingi ambao hawakuwa wameelewa. Mungu alikuwa ameniinua ili nitimize wajibu wa kuliongoza kanisa, kwa hivyo nilipaswa kushiriki nao juu ya maneno ya Mungu na kushuhudia kazi Yake zaidi ili waweze kuelewa ukweli na kupata maarifa juu ya Mungu, na kuweka misingi kwenye njia ya kweli. Mm. Lakini nilifanya nini? Je, matokeo ya jaribio langu la kutimiza wajibu huo yalikuwa gani? Nilimfanya kila mtu aniabudu, na nikawazuia kuwa na maarifa yoyote juu ya Mungu. Kwa kufanya hivyo, niliwadhuru ndugu zangu, na nikaingilia kati na kuvuruga kazi ya kanisa. Nilikuwa nikitembea kwenye njia ya mpinga Kristo ya kumpinga Mungu! Kadiri nilivyozidi kufikiria hayo, ndivyo nilivyozidi kuwa na wasiwasi na kufadhaika. Niliweza kuona jinsi nilivyokuwa na kiburi, jinsi nilivyokosa kabisa kumcha Mungu, na matendo yangu yalikuwa yakiikosea tabia Yake kwa muda mrefu sana. Asingewatumia ndugu zangu kunipogoa na kunishughulikia kwa njia hiyo, nisingejua kutafakari juu ya matendo yangu. Kama ningeendelea kutembea kwenye njia hiyo, sijui ningetenda uovu kiasi gani kiasi cha kulaaniwa na kuadhibiwa na Mungu. Huku nikihisi woga usiotoweka, nilisujudu mbele ya Mungu na kuomba. Nilisema, “Mungu! Nimekuwa na kiburi sana. Mimi hujionyesha katika wajibu wangu kila wakati na hii imesababisha ndugu zangu wanipende sana na wasiwe na nafasi Yako mioyoni mwao. Nimetenda uovu na kukupinga. Nastahili adhabu Yako. Mungu! Natamani kutubu mbele Yako, kufuatilia ukweli kwa dhati, na kuanza upya.”

Baadaye, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa wajibu kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Naye binadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni ya kuchukiza Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkubwa, au wa kipekee, au zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I). “Haijalishi ni nini ambacho wanadamu wanatafuta au kile wanachotamani, ni wale tu wanaorudi mbele ya Muumba na kutimiza na kukamilisha kile wanachostahili kufanya, na kile walichoaminiwa nacho kwa utiifu, ndio watakaoishi na dhamiri ya amani na kwa njia ambayo ni sahihi na inayofaa, bila mateso yoyote. Hii ndiyo maana na thamani ya kuishi(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma maneno ya Mungu, nilielewa kwamba Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na ni sawa na sahihi—ni jambo la kawaida tu— kwamba wanadamu wanapaswa kumwabudu na kumtii Yeye. Aidha, nilijua kuwa nilikuwa kiumbe mdogo tu na mwanadamu mpotovu. Nilijawa na tabia za kishetani—nilikuwa mwenye kiburi, mdanganyifu, mbinafsi, na aliyestahili dharau. Hata hivyo, nilikuwa daima nikijaribu kujionyesha na kuchukua nafasi yangu mioyoni mwa watu. Sikuwa na aibu hata kidogo na nilikuwa na kiburi kupita kiasi! Kadiri nilivyozidi kufikiria hilo, ndivyo nilivyozidi kuaibika. Nilijichukia kwa kuwa kipofu na kutomjua Mungu. Sikujua nilikuwa nani. Mimi kuweza kuwa hapa leo kutekeleza wajibu wangu ni kwa sababu ya neema na kuinuliwa na Mungu. Napaswa kuchukua mahali pangu panapofaa kama kiumbe, na kuwa mtu mkweli na mnyofu ambaye huzingatia kufuata ukweli, kumtukuza Mungu na kumshuhudia, na kutekeleza wajibu vizuri— kwa maana wakati huo tu ndipo nitaweza kuwa na dhamiri na busara ambayo kiumbe anapaswa kuwa nayo.

Baadaye, nilitafuta njia ya kutenda na kuingia kupitia maneno ya Mungu. Nilisoma baadhi ya maneno ya Mungu ambayo yalisema, “Mnapokuwa na ushuhuda wa, mnapaswa kuzungumza hasa kuhusu jinsi Mungu anavyowahukumu na kuwaadibu watu, ni majaribio yapi anayoyatumia kuwasafisha wanadamu na kubadilisha tabia zao. Mnapaswa pia kuzungumza kuhusu kiwango cha upotovu ambacho kimefichuliwa katika uzoefu wenu, kiasi ambacho mmestahimili na jinsi ambavyo hatimaye mlishindwa na Mungu; kiasi cha maarifa ya kweli ya kazi ya Mungu mlicho nacho, na jinsi mnavyopaswa kumshuhudia Mungu na kumlipiza kwa ajili ya upendo Wake. Mnapaswa kuweka umuhimu katika lugha ya aina hii, huku mkiisema kwa njia rahisi. Msizungumze juu ya nadharia tupu. Zungumzeni mambo halisi zaidi, zungumzeni kwa dhati. Hivi ndivyo jinsi mnavyopaswa kupitia. Msijiandae kwa nadharia zinazoonekana kuu, zilizo tupu katika juhudi la kujionyesha; kufanya hivyo kunawafanya muonekane wenye majivuno sana na msio na maana. Mnapaswa kuzungumza zaidi kuhusu mambo ya kweli na halisi kutoka kwa uzoefu wenu ambayo ni ya kweli na ya dhati; hili ndilo la manufaa zaidi kwa wengine, na ndilo linalowafaa zaidi kuona(“Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma maneno ya Mungu, nilielewa kidogo juu ya jinsi ninavyopaswa kutenda kumtukuza Mungu na kumshuhudia katika wajibu wangu. Katika kumshuhudia Mungu, ninapaswa kusema zaidi kuhusu jinsi nilivyopitia kazi Yake, ni tabia zipi potovu zilizofunuliwa ndani yangu, jinsi nilivyomwasi na kumpinga, jinsi nilivyotafakari juu yangu na kujijua kwa kujilinganisha na maneno Yake, na jinsi nilivyotubu na kubadilika. Kupitia kushiriki juu ya ukweli, ninapaswa kuwasaidia watu waelewe mapenzi ya Mungu na matakwa Yake, kuwasaidia waelewe kazi ambayo Yeye hufanya ili kuwaokoa watu, na pia tabia Yake, na kuweza kumcha na kumtii Mungu na kutekeleza wajibu wa viumbe. Ni kwa kufanya hivyo tu ndiyo ninaweza kumtukuza Mungu kwa kweli na kumshuhudia. Nilikumbuka nilipokuwa nikishiriki na ndugu zangu. Wakati mwingi nilizungumza tu juu ya jinsi nilivyoteseka na gharama niliyolipa, na jinsi nilivyoshuhudia matendo ya Mungu na kupewa baraka za Mungu. Ilipofikia ni tabia zipi potovu zilizokuwa zimefichuliwa ndani yangu au nia mbaya nilizokuwa nazo, nilizificha kila wakati na hata nilizitaja kwa nadra sana. Niliogopa kwamba iwapo ndugu zangu wangeona upotovu wangu, maoni yao juu yangu yangeathirika. Kweli nilikuwa na asili ya udanganyifu kabisa. Baada ya kutambua mambo haya, nilimtafuta Ndugu Zhang na kumweleza juu ya matendo yangu maovu ya kujionyesha ili kuwadanganya watu. Pia nilimsihi Ndugu Zhang aende katika kanisa ambalo nilikuwa nikihudumia hapo awali na aichambue tabia yangu na kina ndugu huko, na hivyo kumruhusu kila mtu awe na utambuzi zaidi. Wakati wa mkutano, pia niliwaambia ndugu zangu kuhusu tabia yangu mbaya, nikaishuhudia tabia ya Mungu yenye haki, na nikamwambia kila mtu anitumie kama mfano ili ajifunze kile kisichostahili kufanywa ili asitembee kwenye njia ya kumpinga Mungu kama nilivyofanya.

Baadaye, nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, nilianza kuwa mnyenyekevu zaidi, na nilipata kumcha Mungu kidogo. Nakumbuka wakati mmoja, wakati wa mkutano, kulikuwa na ndugu mgeni ambaye alikuwa amekabiliwa na shida fulani, na nilishiriki naye juu ya maneno ya Mungu ili nimsaidie kutatua tatizo lake. Baada ya kunisikiliza, ndugu huyo alisema kwa furaha, “Ndugu Chen, ushirika wako ni mzuri sana. Tatizo hili limekuwa likinisumbua kwa muda mrefu, na sijawahi kuweza kulitatua. Kwa kweli unaelewa ukweli! Lazima uje hapa kufanya ushirika katika mkutano wetu mara nyingi zaidi katika siku zijazo.” Ndugu mwingine alisema jambo hilo hilo. Wakati huo, nilifurahi sana, lakini nikatambua mara moja kuwa kosa langu la zamani la kujionyesha lilikuwa karibu kujitokeza tena, kwa hivyo nilimwomba Mungu upesi na nikajikana. Baadaye, nilimshuhudia Mungu na kuwaleta ndugu zangu mbele Zake. Nilisema, “Kila mtu anaweza kujifunza kutoka kwa yale ambayo tumeshiriki katila mkutano wa leo. Haya yote ni Roho Mtakatifu anayetuongoza na kutupa nuru. Sote tunapaswa kusoma maneno ya Mungu zaidi, na tunapokabiliwa na matatizo, tunapaswa kutafuta ukweli katika maneno Yake zaidi, na Roho Mtakatifu atatupa nuru na kutuangazia. Kwa kufanya hivi, tutaelewa hata zaidi.” Baada ya kusema hayo, nilihisi amani kuu ndani yangu. Kwangu mimi kuweza kupitia mabadiliko haya madogo, na kujua jinsi ya kutenda kumtukuza Mungu na kumshuhudia katika wajibu wangu, ni kwa ajili tu ya hukumu ya maneno ya Mungu na kuadibu Kwake.

Iliyotangulia: 68. Ulinzi wa Mungu

Inayofuata: 73. Wokovu wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

1. Nimebahatika Kumhudumia Mungu

Na Gensui, Korea ya KusiniMwenyezi Mungu anasema, “Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp