Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

18. Somo la Utiifu

Na Yang Mingzhen, Kanada

Jina langu ni Yang Mingzhen, na nimemfuata Mwenyezi Mungu kwa miaka saba sasa. Miaka hii michache iliyopita, bila kujali kanisa limeniandalia wajibu gani niutekeleze au nakutana na vipingamizi vipi katika wajibu wangu, hata ikiwa unahitaji mateso, au nilipe gharama, nimeweza kushirikiana kwa shauku bila uhasi wowote au kurudi nyuma. Nilidhani kwamba kwa kuwa niliweza kufanya yote hayo, tabia yangu ya maisha ilikuwa imebadilika na kwamba nilikuwa na utiifu wa vitendo kwa Mungu. Lakini Mungu anajua kasoro yangu na kile ninachohitaji kwa ukuaji katika maisha yangu, kwa hivyo Alipanga kwa uangalifu mazingira halisi niyapitie. Ilikuwa tu kupitia ufunuo wa Mungu ndiyo niliona waziwazi kimo changu cha kweli.

Mnamo Machi 2016, nilitoroka kwenda nchi nyingine ili kuepuka kukamatwa na kuteswa na serikali ya CCP na kumwamini Mungu na kumwabudu kwa uhuru. Nilipofika, nilikaa na dada wachache na wadogo zaidi. Dada hao walikwenda kila siku kueneza injili, na kuwanyunyizia na kuwasaidia waumini wapya. Walipokuja nyumbani jioni, walishiriki kwa furaha na kila mmoja kuhusu uzoefu wao na kile walichopata kutokana na kutekeleza wajibu wao. Nilipoona hili, niliwastahi sana. Niliwaza: Kama ningeweza kuwa kama wao, kama ningeweza pia kufanya kazi ya kuwanyunyizia na kuwasaidia ndugu zetu wapya, hilo lingekuwa jambo zuri sana! Siku moja, Dada Zhang alikuja kujadili nasi kazi ya kanisa. Aliniuliza: “Je, uko tayari kusaidia kuwafadhili ndugu zetu wapya?” Nilisema ndiyo kwa furaha, na nikawaza: Marafiki na jamaa yangu, na ndugu ambao wananijua watakapogundua kuwa ninaweza kutekeleza wajibu wa aina hii ughaibuni, hakika watanistahi na kuniheshimu. Hilo litakuwa jambo la kuvutia sana! Katika siku zilizofuata, nilikuwa na hamu ya kuanza wajibu wangu wa kuwanyunyizia waumini wapya.

Wakati tu ambapo moyo wangu ulikuwa umejaa matarajio, kiongozi wa kanisa alinijia na kuniuliza kama ningewakaribisha wageni. Moyo wangu ulipinduka papo hapo: “Nilidhani kwamba kanisa litanifanyia mpango niwanyunyizie na kuwasaidia ndugu wapya, hivyo sasa kwa nini nimeandaliwa kutenda kama mwenyeji? Si nitakuwa tu nikishughulika na vyombo vya nyumbani siku nzima? Sio tu kuwa ni kazi ngumu, lakini pia ni kitu kinachonivunjia heshima! Nilipokuwa ulimwenguni nilikuwa mfanyabiashara, na niliendesha kiwanda. Marafiki na jamaa zangu wote wamesema kuwa mimi ni mwanamke hodari sana. Huko nyumbani, niliajiri mtu wa kufua, kupikia, na kusafisha kila mara. Lakini sasa, inaonekana kwamba mimi ndiye ninawapikia. Sitaki kutenda wajibu wa aina hii!” Mawazo haya yote yalinijia akilini, lakini ili kuepuka aibu nilihisi aibu sana kukataa moja kwa moja. Nilitoa kisingizio cha busara, nikisema kwamba nilikuwa nimefika tu katika nchi hii, sikujua mazingira yangu, na sikuweza kuzungumza lugha ya mahali pale. Sikujua hata jinsi ya kununua mboga, kwa hivyo singeweza kutekeleza wajibu wa mwenyeji vizuri. Dada Zhang aliniambia nisiwe na wasiwasi, kwamba kila mtu atanisaidia wakati wowote nitakapohitaji msaada. Baada ya kusema hivyo, sikuweza kutoa kisingizio chochote zaidi, lakini moyoni mwangu, sikutaka kabisa kuufanya. Kama ningekubali, labda singepata fursa nyingine ya kufanya wajibu wa kunyunyizia, na je, si matumaini yangu yote yangekosa kufanikiwa? Lakini kama singekubali, si dada huyo angesema kuwa mimi si mtiifu kwa kuchagua wajibu wangu? Baada ya kufikiria tena jambo hilo, nilijilazimisha kukubali wajibu huo.

Kwa siku chache zilizofuata, ingawa nilitekeleza wajibu wangu wa kuwakaribisha wageni, moyo wangu ulikuwa ukigeuka kila wakati, na nikaanza kuwa na shaka. Niliwaza: Je, yawezekana dada huyu haoni kama nina uwezo wa kutekeleza wajibu wa kunyunyizia? Vinginevyo, kwa nini anipangie mimi kuwa mwenyeji? Ndugu ambao wananijua wakigundua kuhusu hili, si watafikiria kuwa nimepangiwa kutekeleza wajibu wa mwenyeji kutokana na ukosefu wangu wa uhalisi wa ukweli? Je, si watanidharau? Wazo hilo lilinifanya nihisi vibaya zaidi. Wakati huo huo, uamuzi niliokuwa nimefanya mbele ya Mungu ulinijia akilini: Bila kujali kile ninachokutana nacho, almradi ni cha manufaa kwa kazi ya kanisa, nitafanya kila niwezalo kushirikiana. Bila kujali halikubaliani na mawazo yangu kwa kiasi kipi, lazima niwe mtiifu na nimridhishe Mungu. Lakini nilipoombwa kuwa mwenyeji, kwa nini nilikosa utiifu? Nilimwomba Mungu kwa utulivu: “Ee Mungu! Ninajua ya kuwa sheria Yako na mipango Yako inanijia katika wajibu huu, lakini kila mara kuna uasi moyoni mwangu, na siwezi kwa kweli kuwa mtiifu Kwako. Ninajua kuwa hali yangu si sawa. Nakuomba Unipe nuru na Uniongoze ili niweze kuelewa mapenzi Yako na kuweza kutii kile ambacho Umeandaa na kupanga.” Baada ya kuomba, nilifikiria kuhusu maneno ya Mungu: “Wale wote ambao hawatafuti utii kwa Mungu kwa imani yao wanampinga Mungu. Mungu anaomba kwamba watu watafute ukweli, kwamba wawe na kiu ya neno la Mungu, na wanakula na kunywa maneno ya Mungu, na kuyaweka katika matendo, ili waweze kupata utii kwa Mungu. Kama motisha zako ni hizo kweli, basi Mungu atakuinua juu hakika, na hakika Atakuwa mwenye neema kwako. Hakuna anayeweza kutilia shaka hili, na hakuna anayeweza kulibadilisha. Ikiwa motisha zako sio kwa ajili ya utii kwa Mungu, na una malengo mengine, basi yote ambayo unasema na kufanya—maombi yako mbele ya Mungu, na hata kila tendo lako—litakuwa linampinga Mungu. Unaweza kuwa unaongea kwa upole na mwenye tabia ya upole, kila tendo lako na yale unayoyaonyesha yanaweza kuonekana ni sahihi, unaweza kuonekana kuwa mtu anayetii, lakini linapofikia suala la motisha zako na mitazamo yako juu ya imani kwa Mungu, kila kitu unachofanya kipo kinyume cha Mungu, na ni uovu” (“Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Baada ya kwenda nyumbani, nilisoma katika ushirika: “Katika kutekeleza wajibu wao, watu wengine hulenga tu majisifu na heshima yao wenyewe. 'Nitatekeleza wajibu wowote utakaoniruhusu nijionyeshe. Ikiwa wajibu unahitaji nijitahidi na kufanya kazi kwa bidii, ikiwa hakuna mtu atauona na sitaweza kujionyesha, ikiwa utafichika na nitakuwa tu shujaa asiye na jina, basi sitaufanya. Nitafanya kazi ambayo inanifanya nivutie, kazi inayopendeza majivuno yangu.' Wao hutaka tu kupendeza mbele ya wengine, na mara tu wanapoweza kufanya hivyo, wao husisimka. Watateseka kwa kiwango chochote, watatia bidii kiasi chochote. Wao hutafuta kila wakati kutosheleza majivuno yao. Mtu wa aina hiyo hapendi ukweli. Lazima uyadhukuru mapenzi ya Mungu na utii mipango Yake. Mipango katika nyumba ya Mungu huruhusiwa na Mungu, kwa hivyo lazima uwe mtiifu kwa makusudi. Ikiwa unaweza kutii mipango ya nyumba ya Mungu, hiyo inamaanisha kuwa unaweza kumtii Mungu. Ikiwa huwezi, basi utiifu wako kwa Mungu sio chochote ila maneno matupu, kwa sababu Mungu kamwe hawezi kukuamuru ufanye kitu, uso kwa uso. Leo, nyumba ya Mungu imekupangia utekeleze wajibu huu, kutekeleza wajibu huo kulingana na mahitaji yetu ya sasa ya kazi. Unasema: ‘Nina chaguo. Nitafanya yoyote niitakayo. Kama siupendi, sitaufanya.’ Je, kutekeleza wajibu wako kwa namna hiyo ni kuwa mtiifu kwa Mungu? Je, mtu wa aina hiyo ni mtu anayependa ukweli? Je, anaweza kufikia ufahamu kumhusu Mungu? Sio mtu anayemcha Mungu. Kuchagua wajibu wako, kuwa hasi na kuzembea—mtu wa aina hiyo hana uhalisi wa ukweli hata kidogo. Hana utiifu wa kweli, lakini yeye hutegemea kabisa upendeleo wake katika wajibu wake. Mungu hampendi mtu kama huyo” (“Mahubiri na Ushirika Kuhusu Neno la Mungu ‘Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu’ (I)” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha X).

Maneno ya Mungu na ushirika viliuumiza moyo wangu, na nilihisi aibu. Hata zaidi niligundua sababu yangu ya kuwa mwasi katika wajibu wa kuwakaribisha wageni. Nilipofikiria nyuma wakati ambapo niliwajibikia kikundi kidogo kanisani, kila mara kiongozi angejadiliana nami kwanza kuhusu kazi ya kanisa, halafu ningejadili na ndugu na kuitekeleza. Wakati huo nilihisi kuwa kiongozi huyo wa kanisa aliniheshimu sana, na ndugu zangu pia waliniheshimu. Nilijawa sana na nguvu katika wajibu wangu, na nilifurahia kuufanya bila kujali ulikuwa ngumu kiasi gani au ulichosha kiasi gani. Lakini sasa kwa kuwa ninatarajiwa kuwa mwenyeji, nina uhasi na sina nguvu, nikifikiri kuwa kuandaa chakula ni kazi duni, kushughulika tu na vyombo vya jikoni siku nzima na hakuna mtu atakayejua bila kujali natia bidii kiasi gani. Wajibu wa aina hiyo unavunja moyo, kwa hivyo ninaupinga, na sitaki kuukubali. Sina utiifu wowote wa vitendo kwa Mungu. Ni wakati huo tu ndipo niliona kwamba hapo zamani, kazi yangu isiyochosha katika wajibu wangu haikufanywa kwa utiifu wa kweli, lakini yote ni kwa ajili ya kujionyesha na kupata heshima na taadhima kubwa ya wengine, na kwamba sikuwa nikifanya wajibu wangu kama kiumbe wa Mungu. Mara tu wajibu wangu ulipokosa kutimiza malengo na tamaa yangu ya kupata umaarufu na hadhi, nilifikiria kila njia inayowezekana ya kutoa visingizio, na sikuwa tayari kuukubali na kuwa mtiifu. Kusema waziwazi, nilikuwa tu nikipeperusha bendera ya kutekeleza wajibu wangu huku nikitafuta umaarufu na hadhi yangu binafsi ili kukidhi majivuno yangu. Sikuwa nikiyadhukuru mapenzi ya Mungu hata kidogo, au kuendeleza kazi ya kanisa. Kwa kweli mimi ni mbinafsi na mwenye kustahili kudharauliwa! Nimekuwa kwa kawaida nikifanya wajibu wangu kwa upendeleo wangu na chaguo langu mwenyewe, kila mara nikifanya njama kwa sababu za mwili. Nawezaje kuwa mtu anayefuatilia ukweli na aliye mtiifu kwa Mungu? Kisha, nikasoma maneno zaidi ya Mungu: “Wale ambao wanaweza kutia ukweli katika vitendo wanaweza kukubali uchunguzi makini wa Mungu katika matendo yao. Unapokubali uchunguzi makini wa Mungu, moyo wako unawekwa kuwa sawa. Ikiwa daima unafanya tu mambo kwa ajili ya wengine kuona na hukubali uchunguzi makini wa Mungu, je, una Mungu moyoni mwako? Watu kama hawa hawana moyo unaomcha Mungu. Usifanye mambo kwa ajili yako daima, usifikirie maslahi yako mwenyewe daima, na usifikirie hadhi yako mwenyewe, heshima au sifa daima. Lazima kwanza ufikirie maslahi ya nyumba ya Mungu na kuyapa hayo kipaumbele; unapaswa kuyafikiria mapenzi ya Mungu, utafakari kuhusu iwapo unafikiria kazi ya nyumba ya Mungu au la na kuhusu iwapo umetimiza wajibu wako vizuri au la. Wakati unapofikiria kazi ya nyumba ya Mungu moyoni mwako daima na kufikiria kuhusu kuingia kwa maisha kwa ndugu zako, basi utaweza kutimiza wajibu wako vizuri” (“Unaweza Kupata Ukweli Baada ya Kumkabidhi Mungu Moyo Wako Halisi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nilipokuwa nikiwaza juu ya maneno ya Mungu, nilielewa mapenzi Yake, na nilijua cha kufanya ili kumridhisha. Nilimwomba Mungu na kufanya uamuzi wangu: “Ee Mungu! Niko tayari kukubali uchunguzi Wako makini, kuweka kando majivuno na heshima yangu, na kutofuatilia tena umaarufu au hadhi. Niko radhi kutii mipango Yako na kutekeleza wajibu wangu kwa dhati ili kukuridhisha!” Baada ya kuomba, moyo wangu ulikuwa mtulivu zaidi, na nikakubali wajibu huu kutoka moyoni mwangu.

Katika siku zilizofuata, kwa kuwa dada zangu walijua kuwa nilikuwa nimefika hapa tu muda mfupi na sikuyajua mazingira yangu, kwa hivyo kununua mboga kungekuwa kugumu, walitenga muda kwenda nami kununua vyakula na mahitaji ya kila siku. Mimi nawazidi kwa umri, na mimi si hodari sana katika kutumia kompyuta, kwa hivyo dada zangu walinifundisha kwa ukarimu na uvumilivu. Wakati mwingine, nilipokutana na shida, nilikuwa katika hali ya uhasi na udhaifu, na walitafuta vifungu husika vya maneno ya Mungu vya kushiriki nami katika ushirika. Walinisaidia kwa upendo, na kutatua shida zangu za utendaji. Hata ingawa dada zangu walikuwa na shughuli nyingi sana za wajibu wao, wakati wowote walipokuwa na muda walinisaidia na kazi ya nyumbani, kusafisha, na kadhalika. Hakuna hata mmoja wao aliyenidharau au kutonithamini kwa sababu nilikuwa mwenyeji. Kila mtu alifanya tu kila awezalo katika wajibu wake. Nilihisi kuwa kati ya ndugu, hakukuwa na tofauti kati ya kile kilichokuwa duni na kile kilichokuwa cha hali ya juu. Tulikuwa wandani hata zaidi, wenye urafiki wa karibu sana kuliko familia. Kila siku ilijaa shughuli, na nilihisi mtulivu na mwenye amani. Ninamshukuru Mungu kwa kweli! Baada ya kupitia hukumu hiyo na kuadibu kwa maneno ya Mungu, nilihisi kwamba nilikuwa nimepata kuingia kiasi katika ukweli wa kumtii Mungu, na nikawa mtiifu zaidi katika wajibu wangu. Lakini Mungu alijua vizuri kuwa asili yangu ya kishetani ya kutafutilia umaarufu na hadhi ilikuwa madhubuti kabisa, hivyo Aliandaa mazingira mengine ya kunitakasa na kuniokoa.

Siku moja, kiongozi wa kanisa alinipigia simu na akasema kwamba mmoja wa akina dada alikuwa akishughulika sana za wajibu wake na hakuwa na mtu wa kumchungia mwanawe wakati wa Jumamosi alasiri, akiniuliza ikiwa ningeweza kupata wakati wa kumsaidia kwa nusu siku kila wiki. Niliposikia kwamba ningemlinda mtoto, nilihisi kukosewa kidogo. Je, kumchunga mtoto kunachukuliwa kama kutekeleza wajibu wangu? Aidha, miaka hii yote nimekuwa nikifanya shughuli za biashara, na sikuhitaji kuwalinda wajukuu wangu. Kazi yote niliyoifanya ilikuwa kitu ambacho kilinifanya nivutie, na machoni pa jamaa na marafiki nilikuwa mwanamke hodari. Kufanya wajibu wa mwenyeji tayari ni duni sana kwangu, kwa hivyo zaidi ya hayo nikimlinda mtoto wa mtu, si nimekuwa tu yaya? Siwezi kujipatia sifa njema au kupata hadhi kwa kumwangalia mtoto, kwa hivyo sitaki kufanya hivyo. Hivyo, nilitoa kisingizio: Naandaa vyakula vya akina dada sasa, na sina budi kutunza nyumba, ndugu huja mara nyingi, kwa hivyo siwezi kuondoka. Nilipokuwa tu nikitoa visingizio na kukwepa, kiongozi yule alinisihi kwanza nimwombe Mungu, nitafute na kisha nifanye uamuzi. Baada ya kukata simu, sikuweza kupata amani moyoni mwangu, na kadiri nilivyozidi kufikiri juu ya jambo hilo ndivyo nilivyozidi kuhisi vibaya. Niliwaza: Kwa nini kiongozi asimtafute mtu mwingine? Kwa nini sharti iwe mimi? Siwezi kujipatia sifa au kupata hadhi kwa kumwangalia mtoto Ndugu zangu wangenionaje kama wangejua? Ningeonekanaje hadharani kwao? Lakini nisipofanya hivyo, si ndugu zangu watasema sina upendo moyoni mwangu? Niliwaza na kuwazua, na mwishowe nikaamua kwenda kujaribu kufanya hivyo.

Nilikwenda nyumbani kwa Dada Zhou Jumamosi alasiri na nikaona kwamba mtoto huyo mchanga na mchangamfu alikuwa maasumu na wa kupendeka mno, lakini sikuweza tu kuhisi furaha yoyote. Moyo wangu ulikuwa na wasiwasi. Nilijitahidi sana hadi ilipofika saa 11 jioni wakati ambapo msichana huyo mdogo alianza kumlilia mamake, na sikuweza kumtuliza bila kujali nilichofanya. Dada Zhou alikuwa karibu kufika nyumbani, lakini msichana huyo hangeacha tu kulia. Nilifadhaika. Niliwaza: Akirudi na kumwona binti yake akilia, atanifikiria vipi? Atafikiria kuwa katika umri wangu, siwezi hata kumtunza mtoto mdogo? Katika msukosuko huo, yote ambayo ningefanya ilikuwa kumshawishi kwa makumbwe matamu, kumsimulia hadithi, na kumwekea filamu za katuni. Aliacha kulia polepole, kisha Dada Zhou akarudi kutoka kutekeleza wajibu wake. Nilifaulu kumaliza alasiri moja kwa namna hiyo. Nilipokuwa njiani nikirudi nyumbani, nilitembea muda wote na nikawaza: Kumtunza mtoto si kazi rahisi. Mbali na kuchoka, kuna mengi ya kuhangaikia. Kama jambo fulani lingetokea, singeweza kulishughulikia. Na kuna watu wengi sana kanisani, hivyo kwa nini sharti wanitake mimi nimwangalie mtoto? Kadiri nilivyozidi kufikiria kuhusu jambo hilo, ndivyo nilivyozidi kuchanganyikiwa. Jioni hiyo, niligaagaa na kugeuka kitandani, na sikuweza kulala. Nililazimika kuja mbele za Mungu na kuomba: “Mungu! Ninahisi vibaya sasa hivi. Najua kuwa kumsaidia dada huyu kumtunza bintiye ni ili kwamba shughuli za familia yake zisikatize wajibu wake, na ninapaswa kuukubali kama wajibu wangu. Lakini mimi huhisi kukosewa kila wakati na ninajitahidi kutii. Ee Mungu! Ninakuomba Unipe nuru na Uniongoze ili niweze kuelewa mapenzi Yako, na nitaweza kutoka katika hali hii mbaya.” Baada ya kuomba, sikuhisi vibaya kama nilivyohisi hapo awali. Nilifungua kitabu cha maneno ya Mungu, na kusoma haya: “Kutii kwa dhati ni nini? Wakati wowote ambapo mambo yanakuendea vizuri na kukufanya utokezee, unga’e, na kuwa na heshima kiasi, unahisi kuwa kila kitu ni cha kuridhisha na cha kufaa. Unamshukuru Mungu na unaweza kutii utaratibu na mipango Yake. Hata hivyo, kila unapotengwa, kutoweza kutokezea, na unapuuzwa kila wakati na wengine, basi unaacha kuhisi furaha. … Kutii wakati hali zinafaa kwa kawaida huwa rahisi. Ikiwa unaweza pia kutii katika hali ngumu—zile ambazo mambo hayakwendei vizuri na unasononeshwa, ambazo hukufanya uwe dhaifu, ambazo zinakufanya uteseke kimwili na sifa yako iharibike, ambazo haziwezi kuridhisha majivuno na majisifu yako, na zinazokufanya uteseke kisaikolojia—basi umekomaa kweli. Je, hili si lengo mnalopaswa kuwa mnafuatilia? Ikiwa mna azimio kama hilo, lengo kama hilo, basi kuna tumaini” (Umetoholewa kutoka kwa ushirika wa Mungu).

Tabia potovu ya mwanadamu hujificha ndani ya kila wazo na fikira yake, ndani ya nia za kila kitendo chake; inajificha ndani ya kila maoni, ufahamu, fikira na tamaa aliyo nayo katika mtazamo wake kwa yote ambayo Mungu hufanya. Na, je, Mungu huyachukuliaje mambo haya ya mwanadamu? Yeye hupanga mazingira ili kukufichua. Hatakufichua tu, lakini pia Atakuhukumu. Unapoonyesha tabia yako potovu, unapokuwa na mawazo na maoni ambayo yanamkaidi Mungu, unapokuwa na hali na maoni ambayo yanashindana na Mungu, unapokuwa na hali ambapo unamwelewa Mungu visivyo, au kumkataa na kumpinga, Mungu atakukemea, kukuhukumu na kukuadibu, na wakati mwingine hata Atakuadhibu na kukufundisha nidhamu. … Mungu anakutaka utambue tabia zako potovu na kiini cha kishetani, uweze kuwa mtiifu kwa mazingira ambayo Mungu amekupangia na hatimaye, uweze kutenda kile Anachohitaji kutoka kwako kulingana na mapenzi Yake, na kuweza kutimiza kusudi Lake” (“Kuwa Mtiifu Kwa Kweli Pekee Ndiyo Imani ya Kweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo).

Huku nikikabiliwa na maneno ya Mungu ya kufichua ya hukumu, nilihisi kwamba sikuwa na mahali pa kujificha. Nilipoona maneno haya ya Mungu “Tabia potovu ya mwanadamu hujificha ndani ya kila wazo na fikira yake, ndani ya nia za kila kitendo chake; inajificha ndani ya kila maoni, ufahamu, fikira na tamaa aliyo nayo katika mtazamo wake kwa yote ambayo Mungu hufanya.” Sikuwa na budi ila kujichunguza: Kwa nini sikuweza kutii mazingira ambayo Mungu alikuwa ameniandalia? Kwa nini sikutaka kumsaidia dada huyo katika utunzaji wa mtoto? Niliamini kwamba kuwatunza watoto lilikuwa jambo ambalo watu wa hadhi ya chini walifanya, na kwamba ilikuwa upotezaji wa hadhi, kwamba wengine wangelichukia. Nilidhani kwamba kutekeleza tu wajibu ambao ningejionyesha na kufanya kitu kizuri, ambao wengine wangevutiwa nao na kuheshimu ndiko kulikuwa na thamani, na kungesifiwa na Mungu. Ikiwa wajibu wangu ni duni na wengine hawauoni, hauna thamani yoyote. Nilifikiri kuhusu mawazo na fikira hizi zilizokuwa ndani yangu na wakati huo tu ndipo nikagundua kuwa nilikuwa bado chini ya udhibiti wa tamaa ya umaarufu na hadhi. Malengo, mtazamo juu ya maisha, na maadili ambayo nilifuatilia katika imani yangu katika Mungu yalikuwa sawa na ya watu wa ulimwengu, kama vile “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” “Watu daima wanapaswa kujitahidi kuwa bora kuliko watu wao wa hirimu,” “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” “Mtu hujitahidi kwenda juu; maji hububujika kwenda chini,” nk. Sumu za kishetani na sheria hizi za mantiki zote zilikuwa zimekita mizizi moyoni mwangu na kuwa tegemeo langu, yakinifanya niwe na kiburi mno, na kunifanya nipende umaarufu na hadhi. Hii ilinisababisha kila siku nihesabu faida na hasara zangu za umaarufu na hadhi katika wajibu wangu, na kutoweza kumtii Mungu kwa kweli.

Kisha nikatafakari maneno ya Mungu tena na nikaja kuelewa kuwa ingawa mazingira ambayo Mungu alikuwa amenipangia yalikuwa kinyume cha mawazo yangu, yalikuwa na nia njema za Mungu. Alitaka kunifunua kupitia mazingira hayo ili niweze kupata ufahamu wa kina kuhusu tabia yangu potovu na kuona wazi kuwa nilikuwa nikitembea kwenye njia mbaya, Akiniruhusu nitubu na kugeuka mapema, kuingia kwenye njia sahihi ya kufuatilia ukweli. Sasa, wengine wakiona wajibu ninaoutekeleza kuwa mkubwa au mdogo, yote ni sheria na mpango wa Mungu na ni jukumu na wajibu ambao lazima nichukue. Lazima tu niukubali na kuutii bila bahatisho au majadiliano; siwezi kufikiri au kuupinga. Sifai kuchagua—huu pekee ndio utiifu wa kweli!

Nilipokuwa nikifanya ibada yangu ya kiroho siku iliyofuata, nilisoma maneno zaidi ya Mungu: “Usipotekeleza wajibu wako vizuri, lakini kila wakati unatafuta heshima na kushindania cheo, heshima, sifa, na masilahi yako mwenyewe, basi wakati unapoishi katika hali kama hii, unataka kufanya huduma? Unaweza kutumikia iwapo unataka, lakini inawezekana kwamba utafunuliwa kabla ya huduma yako kumalizika. Kukufichua hufanyika ghafla. Mara tu unapofunuliwa, suala tena si iwapo hali yako inaweza kuboreshwa; badala yake, inawezekana kwamba matokeo yako yatakuwa tayari yameamuliwa—na hilo litakuwa tatizo kwako” (“Unaweza Kupata Ukweli Baada ya Kumkabidhi Mungu Moyo Wako Halisi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo).

Wale ambao hawafuatilii maisha hawawezi kubadilishwa; wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na kuingia ndani; daima wewe hulenga tamaa zile badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kufika karibu na Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?” (“Mbona Huko Tayari Kuwa Foili” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Hili liliuchoma moyo wangu, neno kwa neno. Niliona tabia takatifu ya Mungu na ya haki ambayo haitavumilia makosa ya wanadamu, na sikuwa na budi ila kuogopa njia ambayo nilikuwa nimeitembea. Niligundua kuwa nilikuwa nimemwamini Mungu kwa miaka mingi lakini bado sikuwa nimefuatilia ukweli—nilikuwa nimefuatilia umaarufu na hadhi siku zote. Nilikuwa nimelenga vitu ambavyo ningeweza kufanya mbele ya wengine ili waniheshimu na kuniunga mkono. Nilifungwa na kuzuiliwa na tamaa hizi za kupita kiasi, na sikuweza kutii mipango wa Mungu. Sikuweza hasa kabisa kumtii au kumpenda Mungu. Kama ningeendelea kumfuata Mungu kwa njia hii hadi mwisho, tabia yangu ya maisha haingebadilika kamwe. Ningeendelea kuteseka kutokana na udhibiti wa asili hii ya kishetani, na kumwasi na kumpinga Mungu. Basi ningeokolewaje na Mungu? Hata ingawa nilifunua kiasi kidogo cha upotovu kupitia marekebisho haya katika wajibu wangu, nilikuja kuelewa kwamba katika imani yangu katika Mungu, ni kwa kufuatilia tu ukweli, na kukubali hukumu, kuadibu, kupogolewa, na kushughulikiwa na maneno ya Mungu ndiyo ninaweza kuelewa kiini cha asili yangu ya kishetani, na kuona waziwazi ukweli wa upotovu wangu wa kumwasi na kumpinga Mungu. Hii inaweza kunisababisha nijichukie, kuuacha mwili, na kufikia badiliko la tabia ya maisha, na hivyo kuwa mtu anayemtii Mungu kwa kweli na kupata sifa Yake. Nilipoelewa hili, nilihisi kuwa ilikuwa muhimu sana kujifunza kutii kwa imani katika Mungu. Wakati huo huo, niliamua: Bila kujali ni wajibu upi nitakaoandaliwa na kanisa, niko tayari kabisa kuyatii yale ambayo Mungu ameniandalia. Sitajaribu kuingiza uwazaji wangu wa kimantiki, na sitaangalia faida au hasara yangu mwenyewe. Nataka tu kutimiza wajibu wangu kama kiumbe wa Mungu na kumridhisha Mungu kwa uthabiti!

Katika siku zilizofuata, kila wakati ndugu zangu walipokuwa na shughuli nyingi za wajibu wao na walinihitaji niwasaidie kuwatunza watoto, nilikubali kutoka moyoni mwangu na kutii mazingira ambayo Mungu alikuwa ameniandalia. Nilifanya wajibu wangu kwa bidii, na nilihisi utulivu, na nilikuwa na amani akilini. Niliona pia mwongozo na baraka nyingi za Mungu. Wakati mwingine mtoto alipoasi au kughadhabika, nilikuwa karibu kukasirika. Lakini mara moja niliweza kugundua kuwa nilikuwa nikifunua upotovu wangu kwa mara nyingine tena, kwa hivyo ningekimbia na kurudi kwa Mungu na kujitafakari, na kuona kuwa mbele za Mungu, nilikuwa tu kama mtoto mchanga ambaye mara nyingi alimwasi na kumpinga Mungu, na singefanya yale Aliyosema. Sikuhisi kufadhaika sana, na niliweza kumwelewa zaidi na kumsamehe mtoto yule. Wakati mwingine nilikuwa na tofauti ndogo za mawazo nao, kwa hivyo nilijaribu kuvua joho la mtu mzima na kusikiliza walichokuwa nacho cha kusema, na kukubali mapendekezo yao yoyote ambayo yalikuwa sahihi. Pia nilijifunza jinsi ya kuwa na mazungumzo ya kirafiki na mtoto na kuelewa hisia zake kwa kweli. Walipokuwa na jambo akilini mwao, walikuwa na mazoea ya kuzungumza nami juu ya jambo hilo, na hakukuwa tena na kutozoeana kati yetu. Pia tuliyasoma maneno ya Mungu mara kwa mara pamoja na kusikiliza nyimbo. Nilishiriki ushirika juu ya hatua tatu za kazi ya Mungu, na jinsi ya kumwomba Mungu na kumtegemea tulipopatwa na matatizo katika maisha. Wao pia walinifundisha Kiingereza— tulisaidiana. Nilipoona kuwa watoto walizidi kuwa watiifu zaidi na zaidi, na kwamba walijifunza jinsi ya kumwomba Mungu na kumtegemea walipokuwa na dhiki, nilifurahi sana. Sikuwa na budi ila kutoa shukrani na sifa kwa Mungu kutoka moyoni mwangu! Kupitia uzoefu wangu wa hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, niliacha hamu yangu ya kutafuta umaarufu na hadhi polepole. Sikutaka tena kutekeleza wajibu ambao ungenipa umaarufu, na sikulenga tena jinsi wengine walivyoniona. Badala yake, niliweza kutii mipango ya Mungu na kumkabili Mungu kwa uthabiti na kutimiza wajibu wangu. Ninahisi kuwa kuishi kwa njia hii kunapumzisha, kunaweka huru, na ni ufunguliaji. Pia nimepata uzoefu wa kina kwamba katika nyumba ya Mungu, hakuna wajibu ambao ni mkubwa au mdogo, na hakukuwa na tofauti kati ya kile kilichokuwa cha hali ya chini na cha kifahari. Bila kujali natekeleza wajibu wa aina gani, una somo ambalo lazima nijifunze na ukweli ambao lazima niweke kwenye vitendo na kuingia ndani yake. Almradi nitende maneno ya Mungu na kumtii nitaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu na kuelewa ukweli, na kupokea baraka Zake wakati wa kutekeleza wajibu wangu. Hii inaniruhusu nione jinsi Alivyo mwenye haki, na kwamba Yeye hamtendei mtu yeyote bila haki!

Mungu anasema: “Mungu analipa gharama—gharama kubwa sana ya kujitahidi—kwa kila mmoja, na kila mmoja ana mapenzi Yake. Mungu analipa gharama ya kujitahidi kwa ajili ya kila mtu. Anaweka mapenzi Yake kwa kila mtu, kwa matarajio na tumaini kwa wote. Kwa kupenda Anawalipia watu hao gharama ya kujitahidi kwa mapenzi Yake, na kwa hiari humtolea kila mtu maisha Yake na ukweli. Kwa hivyo Mungu anaridhika ikiwa kuna mtu anayeweza kuelewa hili kusudi Lake. Ikiwa unaweza kukubali na kutii vitu Anavyofanya, na ikiwa unaweza kupokea yote kutoka kwa Mungu, basi anahisi kuwa gharama ya kujitahidi haijalipwa bure. Hii inamaanisha kuwa, ikiwa umeridhisha utunzaji na kujali ambako Mungu amewekeza ndani yako, umepata thawabu katika kila mazingira, na hujasikitisha tumaini la Mungu ndani yako, na ikiwa kile ambacho Mungu amekufanyia kimekuwa na matoke yanayotarajiwa na kimefikia lengo linalotarajiwa, basi moyo wa Mungu umeridhika” (“Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nimeelewa kutoka katika maneno ya Mungu kwamba watu, matukio, vitu, na mazingira yote ambayo mimi hukutana nayo kila siku yana mapenzi ya Mungu na juhudi Zake. Mungu ana agizo kwa ajili yangu na hasa ameweka tumaini Lake kwangu. Ameniokoa kutoka kwa ulimwengu mkubwa. Mapenzi ya Mungu ni kwamba nifanye wajibu wangu mwenyewe katika mpango Wake wa usimamizi. Kama mmoja wa kiumbe cha Mungu, wajibu wangu ni kutii anayoyasema Mungu, kutii mipango Yake, kufanya kile Alichoniaminia kwa makini, na kutekeleza majukumu yangu. Huu ni wajibu wangu na misheni yangu ambayo siwezi kukwepa. Kwa hivyo ninaazimia kukubali na kutii vitu vyote vitokavyo kwa Mungu, na katika watu, matukio na vitu vyote vilivyowekwa na Mungu, kutafuta ukweli, kujaribu kuelewa mapenzi ya Mungu, na kutenda kulingana na matakwa ya Mungu. Katika siku zijazo, bila kujali ni aina gani ya mazingira au ni wajibu gani ambao unanijia, bila kujali uko mbali na maoni yangu kiasi gani, nitakuwa tayari kukubali na kutii. Nitajitoa moyo, roho, na akili kutekeleza wajibu wangu. Nitafuatilia kuwa mtu anayemtii Mungu kwa kweli na kupata sifa Zake!

Iliyotangulia:Kuishi Mbele za Mungu

Inayofuata:Toba ya Afisa

Maudhui Yanayohusiana

 • Buriani, Mtu Mwenye Kujipendekeza

  Kwa mintarafu ya watu ambao hujipendekeza, nilidhani kuwa walikua wazuri sana kabla ya kumwamini Mungu. Walikuwa na tabia za upole, hawakuwahi kubisha…

 • Maneno ya Mungu Yanaoongoza Njia

  Na Xiaocheng, Shaanxi Maneno ya Mungu yanasema: “Kusudi la Mungu katika kuwafunua watu sio kuwaondoa, bali ni kuwafanya wakue” (“Ni kwa Kuyatenda Mane…

 • Situmii Ubora Duni wa Tabia Kama Kisingizio Tena

  Na Lin Ran, Mkoa wa Henan Hapo zamani, kila wakati nilipokabiliwa na shida fulani wakati wa kutekeleza wajibu wangu, au nilifanya kazi yangu vibaya, n…

 • Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo

  Petro alikamilishwa kwa sababu alimpenda Mungu kweli na kwa sababu alikuwa na hiari na uvumilivu wa kutafuta ukweli. Ingawa niko mbali na hilo, sitaishi kwa namna ya kuchukiza na isiyovutia tena ili kujihifadhi; niko tayari kufanya kumpenda Mungu kuwa lengo langu katika kutafuta na nitatumia juhudi zote na kulipa gharama katika kutimiza wajibu wangu. Kweli nitaubeba mzigo wa majukumu yangu na kutia ukweli katika vitendo wakati ninatimiza wajibu na kuingia katika uhalisi wa kumpenda Mungu.