54. Vita vya Kiroho

Na Yang Zhi, Marekani

Mwenyezi Mungu anasema, “Tangu watu waanze kumwamini Mungu, wamekuwa na nia ambazo si sahihi. Wakati ambapo huweki ukweli katika vitendo, unahisi kuwa motisha zako ni sahihi, lakini jambo likikutokea, utaona kuwa kuna motisha nyingi ndani zisizo sahihi. Hivyo, Mungu akiwafanya watu kuwa wakamilifu, Anawafanya kugundua kuwa kuna dhana nyingi ndani yao ambazo zinawazuia kumfahamu Mungu. Ukitambua kuwa motisha zako zina makosa, kama unaweza kuacha kutenda kulingana na motisha na dhana zako, na unaweza kuwa na ushuhuda wa Mungu na kusimama imara katika msimamo wako kwa kila lifanyikalo kwako, hili linathibitisha kuwa umeuasi mwili wako. Ukiasi dhidi ya mwili wako, bila shaka kutakuwa na vita ndani yako. Shetani atajaribu kufanya watu kuifuata, atajaribu kuwafanya wafuate dhana za kimwili na kutekeleza maslahi ya kimwili—ila maneno ya Mungu yatawapa nuru watu na kuwaangazia kwa ndani, na wakati huu itakuwa juu yako ikiwa utamfuata Mungu au utamfuata Shetani. Mungu anawataka watu kuweka ukweli katika matendo kimsingi kushughulikia mambo yaliyo ndani yao, kushughulikiwa fikira zao, na dhana zao ambazo haziufuati moyo wa Mungu. Roho Mtakatifu huwagusa watu ndani ya mioyo yao, na kuwapa nuru na mwangaza. Kwa hivyo katika tukio lolote katika vita: Kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, huwa kuna vita vikali, na japokuwa mambo yanaweza kuonekana shwari katika miili yao, ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona—na ni baada tu ya hivi vita vikali, baada ya kutafakari kwa kina, ndipo ushindi au kushindwa kunaweza kuamuliwa. Mtu anashindwa kujua ama acheke au alie. Kwa sababu motisha nyingi ndani ya watu zina makosa, ama kwa sababu kazi kubwa ya Mungu inakinzana na dhana zao, watu wakiuweka ukweli katika vitendo vita vikali huzuka kisirisiri. Baada ya kuuweka huu ukweli katika vitendo, kisirisiri watu watakuwa wamemwaga machozi mengi sana ya huzuni kabla ya kuamua kumridhisha Mungu. Ni kwa sababu ya vita hivi watu huvumilia shida na usafishaji; huku ni kuteseka kwa kweli. Vita vikikukabili, kama unaweza kusimama kweli upande wa Mungu, utaweza kumridhisha Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli). Baada ya kusoma maneno ya Mungu, nilihisi moyoni kwamba kutenda ukweli si jambo rahisi hata kidogo, na vita vya kiroho ni vya lazima kabisa. Miaka kadhaa iliyopita, shemeji yangu alifichuliwa kuwa mwovu. Kanisa lilikusudia kumfukuza, lakini nilizuiwa na hisia zangu na sikuweza kutenda ukweli. Moyoni mwangu, nilihangaika moyoni sana, na nilitaabika sana. Mwishowe, kupitia hukumu na ufunuo wa neno la Mungu, niliona waziwazi hatari na athari za kutenda kutokana na mihemuko yangu. Ni wakati huo tu ndipo niliweza kuukana mwili wangu, kuachana na hisia zangu, kumfunua na kumkataa mwovu yule. na mwishowe nikafurahia amani na usalama ulioletwa na kutenda ukweli.

Ilikuwa mnamo 2017 niliporudi kuchukua wajibu wa uongozi katika kanisa langu la mtaa. Kwenye mkutano mmoja, kina ndugu waliniambia kwamba shemeji yangu Han Bing, wakati wa kufanya wajibu wake kama kiongozi wa kanisa, alipokuwa akishiriki katika mikutano, alijionyesha kwa kunena maneno na mafundisho ya juujuu. Kila mahali alipokwenda, alizungumza juu ya wajibu aliotekeleza na jinsi alivyoteseka ili kuwafanya wengine wamwabudu na kumsikiliza. Baada ya kina ndugu kuzungumza naye kuhusu matatizo kadhaa yaliyokuwapo katika wajibu wao, alikataa kushiriki kuhusu ukweli ili kusuluhisha matatizo haya, na aliwakaripia wengine kwa kujishaua. Makaripio yake yalisababisha baadhi ya kina ndugu waishi katika hali ya uhasi na kupoteza shauku yote katika wajibu wao. Baadaye, nafasi yake Han Bing ilichukuliwa. Baada ya hapo, alikataa kutafakari juu yake na kuja kujielewa, na bado alisababisha uchokozi na ugomvi miongoni mwa kina ndugu na hivyo kuvuruga maisha ya kanisa. Viongozi wa kanisa walishiriki naye mara kadhaa, na pia wakamshughulikia na kumkosoa, lakini alikataa kukubali yote hayo. Alisalia mwenye kutotii na kutoridhika, na akaendelea kueneza uhasi, na hivyo kusababisha vurugu kali katika maisha ya kanisa … Niliposikia kwamba Han Bing alikuwa akitenda kwa njia hii, nilikasirika. Nilikumbuka maneno ya Mungu: “Wale walio kanisani ambao wanaeneza matamshi yao yenye sumu, wale miongoni mwa ndugu ambao wanasambaza uvumi, kuchochea utengano na kufanya magenge wanapaswa kufukuzwa kutoka kanisani. Lakini watu hawa wamezuiwa kwa kuwa sasa ni enzi tofauti ya kazi ya Mungu, kwa sababu wamehukumiwa kuwa vyombo vya kuondolewa. Wale waliopotoshwa na Shetani wote wana tabia iliyopotoka. Hata hivyo, baadhi ya watu wana tabia potovu tu, huku kuna wengine walio tofauti: Si tu kwamba wana tabia potovu za kishetani, lakini asili zao pia ni mbovu kupita kiasi. Si tu kwamba maneno yao na vitendo vyao vinafichua tabia zao potovu za kishetani; watu hawa, aidha ndio Shetani wa kweli. Tabia yao inakatiza na kuvuruga kazi ya Mungu, inaharibu uingiaji wa kina ndugu katika uzima, na kuharibu maisha ya kawaida ya kanisa. Mbwa mwitu hawa waliovalia ngozi ya kondoo lazima waondolewe nje siku moja , na mtu lazima awe na mtazamo usiojizuia kwa vibaraka hawa wa Shetani; mtu lazima awe na mtazamo wa kuachwa kwao. Ni katika kufanya hili pekee ndipo mtu ataweza kusimama upande wa Mungu na wale wasioweza kufanya hili wako katika ushirika na Shetani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli). Nilipokumbuka kifungu hiki cha maneno ya Mungu, nilielewa waziwazi Kwamba asili na kiini cha Han Bing vinapopimwa kwa kutumia maneno ya Mungu, hakika vilikuwa vya mwovu. Viongozi wa kanisa na wafanyakazi wenza walichambua tabia yake dhidi ya maneno ya Mungu, na wakasema kwamba hata ingawa aliweza kujikana na kujitumia, na alikuwa na uwezo wa kuteseka na kulipa gharama wakati wa kutekeleza wajibu wake, alikuwa mwenye kiburi na majivuno, hakukubali ukweli hata kidogo, alikuwa dikteta na hakuwa na subira, alivuruga maisha ya kanisa, na alikataa kurekebisha makosa yake hata baada ya kuambiwa afanye hivyo. Haya yalimfanya awe mwovu. Kulingana na kanuni za mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu, watu kama hao lazima wafukuzwe. Baada ya kuwasikia ndugu wengi wakisema kwamba alipaswa kufukuzwa kanisani, nilihisi kukanganyikiwa kabisa: Kutokana na kuangalia tabia zake, niliweza kuona kwamba kwa kweli alikuwa mwovu, na alipaswa kufukuzwa, lakini alikuwa dada mdogo wa mke wangu, na wakwe zangu walinitendea vizuri na waliijali sana familia yangu. Ikiwa wangepata habari kwamba nilikuwa nimepiga kura ya kumfukuza Han Bing, basi si wangefikiri kuwa sikuwa na huruma, shukrani, na sikufurahia familia? Je, ningewezaje kuwakabili wakwe zangu baada ya kufanya kitu kama hicho? Lakini kama kiongozi wa kanisa, iwapo singetenda kulingana na kanuni, nikijua vyema kabisa kuwa kulikuwa na mwovu katika kanisa lakini bado sikumfukuza, na iwapo ningeendelea kumruhusu mwovu huyu avuruge maisha ya kanisa na kuwadhuru watu wateule wa Mungu, je, hiyo hangenifanya niwe mshiriki wa mwovu na adui wa Mungu? Naam. Niliogopa kufikiria hilo zaidi. Wakati huo, nilihisi kwamba nilinaswa katika hali ngumu. Sikujua la kufanya. Dada Zhou aliona kwamba nilionekana kuwa na wasiwasi na akaniambia, “Ndugu Liang, Han Bing amevuruga maisha ya kanisa mara kwa mara, na haonyeshi ishara ya toba hata kidogo. Kwa msingi wa kanuni, anapaswa kufukuzwa kanisani. Huku ni kulinda kazi ya kanisa. Hilo ndilo jambo la muhimu zaidi! Tunahitaji kuzingatia mapenzi ya Mungu, wala si kutenda kulingana na mihemuko na hisia zetu za kibinafsi.” Baada ya kumsikiliza, nilihisi kukanganyikiwa.

Wakati huo huo, baadhi ya ndugu walishauri, “Han Bing amemwamini Mungu kwa miaka mingi sana, ameiacha familia na kazi yake ili kutimiza wajibu wake, na amepitia mateso mengi. Tunapendekeza apewe nafasi nyingine ya kutubu.” nilijua waziwazi kuwa kina ndugu hawa walisema hayo tu kwa sababu walidanganywa na sura ya nje ya Han Bing ya kufanya vitendo vizuri, na kwamba nilipaswa kushiriki juu ya ukweli pamoja nao ili kuchambua tabia ya Han Bing ili waweze kutambua asili na kiini chake. Lakini kisha nikawaza, Han Bing ni kipenzi cha wakwe zangu, mama mkwe wangu amekanganyikiwa katika imani yake katika Mungu, na hana utambuzi, na huyu mke wangu ana mihemuko kupita kiasi. Nikiamua kumfukuza Han Bing na kuwafunulia na kuwachambulia ndugu zangu tabia yake mbaya, basi si nitakuwa nikiikosea familia ya mke wangu waziwazi? Nikisema maneno machache mazuri juu ya Han Bing mbele ya kina ndugu, na kisha nishiriki naye ili kumwomba atubu na asisababishe vurugu zaidi, basi kuna uwezekano kusiwe na haja ya yeye kufukuzwa kanisani, na hivyo, sitalazimika kuikosea familia ya mke wangu. Wazo hili lilipunguza wasiwasi ambao nilikuwa nikihisi, hivyo niliwaambia ndugu zangu, “Han Bing hakika ametenda vitendo viovu na ametenda dhambi. lakini ni mapenzi ya Mungu kuwaokoa watu kwa kiwango kikubwa kadiri iwezekanavyo, kwa hivyo tunapaswa kumpa nafasi nyingine ya kutubu. Akitenda uovu tena, hatutakuwa tumechelewa sana kumfukuza wakati huo, na tutaweza kumfanya akubali hilo kwa moyo wote.” Dada Zhou aliponisikia nikisema maneno haya mazuri ya juujuu tu, alionekana kutaka kusema jambo, lakini mwishowe alikaa kimya. Hakuna mtu mwingine aliyesema chochote zaidi, na nilihisi wasiwasi kidogo uliokuwa moyoni mwangu ukitulia. Mwishowe niliwaza moyoni, sikuhitaji kuwa na wasiwasi tena juu ya kuwachukiza wakwe zangu. Lakini siku mbili baadaye, nilipata vidonda vya kinywa ghafula—vidonda vitatu. Nilihisi kana kwamba kinywa changu kilikuwa kikiungua; kiliwasha kupindukia. Wakati mwingine kilikuwa kichungu sana kiasi kwamba sikuweza kuzungumza au kula, na maumivu yalizidi kuwa mabaya kiasi kwamba yaliniamsha usiku. Katika uchungu wangu, niliweza tu kumwomba Mungu: “Mungu, najua kuwa vidonda hivi vya kutesa sana vilivyo kinywani mwangu na kwenye ulimi wangu havikutokea tu kwa utukizi; ni Wewe unayenirudi na kunifundisha nidhamu. Ee Mungu! Natamani kutubu Kwako.”

Baadaye, wakati wa ibada zangu, niliona kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Mungu daima yumo mioyoni mwa wale wanaomwamini Mungu kwa kweli na daima wana moyo wa kumcha Mungu, moyo wa kumpenda Mungu. Wale wanaomwamini Mungu lazima wayafanye mambo kwa moyo wa uangalifu na wenye busara, na yote wanayoyafanya yanapasa kulingana na matakwa ya Mungu na yaweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Hawapaswi kuwa wabishi, wakifanya watakavyo, hayo hayafai katika utaratibu mtakatifu. Watu hawawezi kuipunga bendera ya Mungu kwa madaha na kucharuka kila mahali, wakienda kwa mikogo na kutapeli kotekote; kutenda haya ni tendo la uasi la juu zaidi. Familia zina masharti zao na mataifa yana sheria zao; je, hali sio hivi hata zaidi katika nyumba ya Mungu? Je, matarajio sio makali hata zaidi? Je, hakuna amri nyingi hata zaidi za utawala? Watu wana uhuru wa kutenda watakayo, lakini amri za usimamizi za Mungu haziwezi kubadilishwa kwa hiari. Mungu ni Mungu asiyewaruhusu watu kumkosea; Yeye ni Mungu anayewaua watu. Je, watu kweli hawajui hili tayari?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli). Maneno ya Mungu yaliniacha nikitetemeka kwa woga. Niliona kwamba tabia Yake ni takatifu, ni ya haki na haivumilii kosa lolote. Katika nyumba ya Mungu, Kristo ana mamlaka na ukweli una mamlaka. Mtazamo wa Mungu kwa waovu wanaokatiza na kuvuruga kazi ya kanisa ni chuki na maudhi. Na kwa wale wenye utambuzi lakini wanaendelea kusimama upande wa waovu na kuwatetea, mtazamo wa Mungu ni maudhi na hasira kali. Han Bing, kama mtu aliyekataa kutenda ukweli, aliyesababisha uchokozi na ugomvi, na aliyevuruga na kukatiza kazi ya kanisa, alikuwa hasa aina ya mwovu aliyefunuliwa na kazi ya Mungu, na alikuwa mtu ambaye alistahili kufukuzwa. Lakini ili kulinda uhusiano wangu na familia ya mke wangu, nilitenda kinyume cha dhamiri yangu kwa kusaliti kanuni za ukweli waziwazi. Nilimlinda na kumtolea udhuru mtu mwovu. Nilimtetea mwovu, na nikamlinda. Je, jambo hilo halikunifanya niwe msaidizi na mshiriki wa mwovu? Mungu aliniheshimu kwa kunipa wajibu wa uongozi, lakini sikumcha hata kidogo. Nilielewa ukweli waziwazi, lakini sikuutenda, badala yake nilijihusisha na udanganyifu wa kimakusudi ili kumlinda mwovu kanisani, ambapo alivuruga maisha ya kanisa na kuwadhuru kina ndugu. Nilikuwa nikiikosea tabia ya Mungu kwa kujua na kimakusudi! Matendo yangu huenda yaliwadanganya watu wengine, lakini hayakuweza kumdanganya Mungu. Mungu huona yaliyo mioyoni mwetu. Je, Angewezaje kumvumilia mtu kama mimi, ambaye alitenda kiholela na bila subira? Tayari nilitenda dhambi, na nilijua kwamba kama singetubu, Mungu angeniondoa. Kwa hivyo nilimwomba Mungu upesi ili kutubu. Baada ya kujadili na wafanyakazi wenzangu kadhaa, tulikusanya orodha ya vitendo viovu vya Han Bing na tukaomba afukuzwe kanisani. Baada ya kupata nia ya kumgeukia Mungu, vidonda vilivyokuwa kinywani mwangu viliponywa kimuujiza.

Siku mbili baadaye, nilienda nyumbani kwa mama mkwe wangu kufanya jambo fulani, na Han Bing alikuwepo. Aliponiona, alinikazia macho kisha akageuka na kuondoka. Mama mkwe aliniambia kwa hasira, “Shemeji yako amemwamini Mungu kwa miaka mingi sana, na amepitia mengi sana ili kueneza injili. Je, ni nani asiye na tabia potovu? Kanisa likimfukuza, basi, je, hatapoteza nafasi ya kupata wokovu wa Mungu? Wewe umekuwa mkatili sana kwake!” Mke wangu pia aliingilia mazungumzo hayo kwa niaba ya Han Bing. Nilipoona jinsi walivyokuwa na mhemuko, na kwamba walikuwa na utambuzi mdogo sana kuhusu Han Bing, nilishiriki nao juu ya tabia yake mbovu. Lakini mama mkwe wangu hakusikiza hata kidogo. Badala yake, alinipigia kelele kwa hasira huku machozi yakitiririka kutoka machoni. Mke wangu alipoona hasira yake, yeye pia alisimama pale akinikemea. Nilipoona haya yote, nilihisi dhaifu na mwenye taabu sana kiasi kwamba sikuweza hata kula. Usiku huo, nilipolala kitandani, niligaagaa na kugeuka, nikishindwa kulala bila kujali nilijaribu kiasi gani. Kwa upande mmoja, nililazimika kumfukuza mwovu yule ili kulinda kazi ya kanisa, lakini kwa upande mwingine, kulikuwa na tuhuma za mke na mama mkwe wangu. Nilipaswa kufanya nini? Iwapo ningemfukuza shemeji yangu, ningeikosea familia ya mama mkwe wangu, jambo ambalo lingeathiri uhusiano wangu na mke wangu na labda lingesababisha kuvunjika kwa familia yangu. Lakini kumruhusu mwovu huyu abaki kanisani kungehatarisha maisha ya kanisa na kudhuru maisha ya ndugu zangu. Kufikiria haya yote kuliniacha nikihisi kutaabika sana na kuchanganyikiwa. Nilichoweza tu kufanya kilikuwa kumwomba Mungu kwa dhati: “Mungu, nahisi dhaifu sana. Kuhusiana na kumfukuza Han Bing, sitaki kukukosea, lakini ninazuiwa na mihemuko yangu na ninashindwa kutia ukweli katika vitendo. Nakusihi Unipe nguvu na Uniongoze nishinde nguvu za giza ili niweze kusimama kidete na kukushuhudia.”

Baada ya kuomba, nilisoma maneno mengine zaidi ya Mungu: “Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli). “Wote wamesema kwamba wangeweza kuudhukuru mzigo wa Mungu na kutetea ushuhuda wa kanisa. Ni nani ambaye kweli amefikiri kwa makini kuhusu mzigo wa Mungu? Jiulize: Je, wewe ni mtu ambaye ameonyesha nadhari kwa mzigo wa Mungu? Je, unaweza kutenda haki kwa ajili ya Mungu? Je, unaweza kusimama na kuzungumza kwa ajili Yangu? Je, unaweza bila kusita kuweka ukweli katika vitendo? Je, wewe ni jasiri vya kutosha kupambana dhidi ya matendo yote ya Shetani? Je, unaweza kuwa na uwezo wa kuweka hisia zako kando na kufichua Shetani kwa sababu ya ukweli Wangu? Je, unaweza kuyaruhusu mapenzi Yangu yatimizwe ndani yako? Je, umejitolea moyo wako wakati muhimu unapowadia? Je, wewe ni mtu ambaye hufanya mapenzi Yangu? Jiulize na kufikiri juu yake mara kwa mara(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 13). Kila swali la kushutumu la maneno ya Mungu liliupenya moyo wangu kwa maumivu na taabu. Nilihisi ndani ya maneno Yake, uaminifu uliobana wa mapenzi na matakwa Yake. Mungu alitarajia kwamba nitashughulikia suala la kumfukuza mwovu yule bila kutegemea mihemuko yangu au hisia zangu za kibinafsi, na kwamba nitasimama upande wa Mungu bila kuyumbayumba na kutenda ukweli ili kuridhisha matakwa Yake. Nilimfikiria Ayubu wakati wa majaribio yake, na jinsi ambavyo, ijapokuwa kwa juujuu utajiri wake uliondolewa, watoto wake walikufa, watumishi wake waliuawa, na mkewe na marafiki watatu wakamshambulia, katika hayo yote palikuwapo upinzani wa Shetani dhidi ya Mungu. Ni majaribu ya Shetani yaliyompata Ayubu. Mwishowe, Ayubu aliweza kusimama upande wa Mungu kwa sababu ya imani na uchaji wake kwa Mungu. Alimfanya Shetani aaibishwe na kushindwa kabisa, na alitoa ushuhuda wenye nguvu na mkubwa sana kwa Mungu. Kile kilichoonekana kwa nje kuwa shinikizo la ziada lililowekwa juu yangu na mama mkwe wangu kilikuwa vita katika ulimwengu wa kiroho kwa kweli, Huo ulikuwa ujanja wa Shetani. Lilikuwa jaribio lake la kunizuia kutenda ukweli kwa kutumia upendo wangu wa kihisia, ili mwovu yule aweze kusalia na kundelea kuvuruga na kuharibu kazi ya kanisa. Lakini pia Mungu alikuwa Akitumia jambo hili kunijaribu, ili kuona ikiwa ningemtii Shetani kwa sababu ya vizuizi vya mke wangu na mama mkwe wangu, au kama ningetetea haki badala yake, kutenda ukweli, na kutenda kulingana na kanuni. Ikiwa ningechagua kuuridhisha mwili wangu na kusimama upande wa Shetani, si hiyo ingemaanisha kuwa nilidanganywa na ujanja wa Shetani? Kama ningefanya hivyo, ningepoteza ushuhuda mbele za Mungu.

Nilipofikiria hayo yote, nilianza kutafakari juu yangu: Wakati huu wote, nilipokabiliwa na chaguo hili, kwa nini nilihisi kunaswa katika hali ngumu na nilitaabika sana? Nilielewa waziwazi haja ya kulinda kazi ya kanisa, lakini kwa nini niliendelea kutenda kulingana na hisia zangu, na niliona kuwa ilikuwa vigumu kutenda ukweli na kutenda kwa mujibu wa kanuni? Baadaye, nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu, na nikapata chanzo cha tatizo hilo: “Kwa sababu ya kuzaliwa katika nchi ya uchafu vile, mwanadamu ameangamizwa kabisa na jamii, amekuwa akishawishiwa na maadili ya kikabaila, na amefundisha katika ‘taasisi za elimu ya juu.’ Fikra zilizo nyuma kimaendeleo, maadili potovu, mtazamo mbaya juu ya maisha, falsafa za kudharauliwa za kuishi, uwepo usio na thamani, na hali potovu za maisha na desturi—mambo yote haya yameuingilia moyo wa mwanadamu, na kudhoofisha na kushambuliwa dhamiri yake pakubwa. Matokeo yake, mwanadamu kamwe yuko mbali kutoka kwa Mungu, na kila mara anampinga. Tabia ya mwanadamu inakuwa matata zaidi kila siku, na hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari yake atatoa chochote kwa ajili ya Mungu, hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari atamtii Mungu, wala, zaidi ya hayo, mwanadamu mmoja ambaye kwa hiari yake atatafuta uso wa Mungu. Badala yake, chini ya umiliki wa shetani, mwanadamu hafanyi kitu ila kukimbiza anasa, kujitoa mwenyewe kwa upotovu wa mwili katika nchi ya matope(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu). Kutokana na neno la Mungu, nilikuja kuelewa kwamba nilikuwa nikiishi ndani ya mihemuko yangu, nikishindwa kutenda ukweli na katika hali ya kumwasi na kumpinga Mungu, kwa sababu tu nilipotoshwa na Shetani. Shetani, mfalme wa ibilisi, alitumia utiaji kasumba na jamii na elimu niliyoipata shuleni kunitia moyoni falsafa za kishetani kama vile “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake,” “Damu ni nzito kuliko maji,” na, “Mwanadamu si mfu, anawezaje kukosa hisia?” ili kunifanya nione hisia zangu kwa watu wengine kuwa ndilo jambo la muhimu zaidi maishani, kunifanya nifikirie kuwa kulinda uhusiano na kuwa mwepesi wa kuathirwa na hisia za watu ndivyo jinsi watu walivyo, na kunifanya niamini kuwa kutofanya hivyo kungekuwa ukatili na na kutokuwa na imani, na kwamba ningelaumiwa na wengine juu ya hilo. Nilichukulia falsafa hizi za kishetani kuwa vitu chanya, na nikazichukulia kuwa kanuni za kuishi kwa kufuata, na katika kuishi maisha yangu kulingana na hizi falsafa na sheria za kishetani, nilianza kuwa mpotovu na sikutofatuisha mema na mabaya, nilikuwa mbinafsi kupindukia, mwenye kustahili dharau, mjanja, na mdanganyifu. Katika suala la kumfukuza Han Bing, niliogopa kwamba jamaa zangu wangesema kwamba sikuwa na shukrani na huruma, na kwamba hilo lingevunja familia yangu; jambo hili lilinifanya nipuuze kazi ya kanisa na maisha ya ndugu zangu. Kwa kweli nilikuwa mbinafsi na mwenye kustahili dharau. Kwa kutenda kwa njia hii, sikuwa na shukrani na huruma kwa kweli. Tukifikiria ni kwa nini jamii yetu ni yenye uovu na mbaya, na kwa nini hakuna usawa au haki, ni kwa sababu watu wote wanaishi maisha yao kulingana na hizi falsafa na sheria za kishetani. Katika kikundi chochote cha watu, watu wanajali tu uhusiano wa mihemuko ya mwili. Watu huwatetea tu watu ambao ni wandani wao wa karibu sana. Hata wanapofanya kinyume cha sheria au kufanya uhalifu, watu hufikiria njia za kuwalinda na kuwasaidia, na hushindwa kutofautisha mema na mabaya wanapowatetea. Ni wakati huo tu ndipo niliona waziwazi kwamba hizi falsafa na sheria za kishetani zinaonekana kuwa zenye mantiki na maadili na kukubaliana na fikira za wanadamu, lakini kwa kweli ni uwongo wa upuuzi ambao Shetani hutumia kuwadanganya na kuwapotosha watu. Ni adui wa ukweli na wa Mungu. Tunapoishi kulingana na vitu hivi, tunaweza kumuasi na kumpinga Mungu, kuwaumiza wengine, na kuishi kwa kudhihirisha asili ya pepo. Hapo zamani, nilikuwa nikiishi kulingana na falsafa na sheria za kishetani, nilimlinda mwovu, na nikashiriki katika maovu yake. Lakini Mungu hakunichukia kwa sababu ya makosa yangu ya zamani, na bado Alinipa nafasi ya kutubu, na namshukuru sana Mungu kwa sababu ya hilo. Kwa hivyo, nilimwomba Mungu kimyakimya na nikaapa: Mungu, sitamani tena kutenda kulingana na mihemuko yangu. Natamani tu kupenda kile Unachopenda na kuchukia kile Unachochukia kulingana na maneno Yako, kutetea kanuni za ukweli, na kuwafukuza waovu kanisani papohapo.

Siku iliyofuata, katika mkutano wa wafanyakazi wenza, nilisikia kutoka kwa wafanyakazi wenzangu kuwa Han Bing bado hakujielewa au kuonyesha toba yoyote, na kwamba bado alikuwa akisababisha uchokozi, akichochea ugomvi, na kujaribu kuunda vikundi. Niliposikia haya, nilijilaumu hata zaidi. Nilijichukia kwa kutenda kulingana na hisia zangu na kwa kutomfukuza mapema, nikimruhusu avuruge maisha ya kanisa. Baadaye, wakati wa mkutano uliofuata, nilianza kutumia maneno ya Mungu kwa makini ili kuchambua na kutambua kila moja ya tabia mbovu ya Han Bing, na kupitia ushirika, kina ndugu ambao walikuwa wamedanganywa naye pia walipata utambuzi na wakaanza kumkataa. Baada ya mke wangu kupata ufahamu kuhusu ukweli, pia alikuja kupata utambuzi kuhusu asili na kiini cha Han Bing, na hakubisha tena kuwa hakutendewa kwa haki. Baada ya Han Bing kufukuzwa kanisani, kanisa halikuwa tena likivurugwa na mwovu, kwa hivyo kina ndugu waliweza kuhudhuria mikutano na kutekeleza wajibu wao kwa kawaida tena. Sote tulimsifu Mungu kwa ajili ya haki Yake! Tukio hili lilinifanya nione kwamba katika nyumba ya Mungu, maneno Yake na ukweli vina mamlaka, kwamba vitu vyote hushughulikiwa kulingana na kanuni za ukweli. na kwamba wasioamini, waovu, na wapinga Kristo hawawezi kujidumisha katika nyumba ya Mungu. Pia nilijionea kuwa kuishi kulingana na falsafa na sheria za kishetani kunaweza tu kutuletea uchungu. Hakutuletei au kumletea mtu mwingine yeyote faida. Ni kwa kuishi kulingana na maneno ya Mungu pekee ndiyo tunaweza kwa kweli kuhisi usalama na amani. Kwamba leo siishi tena kulingana na falsafa na sheria za kishetani, na kwamba nimeshinda vizuizi vya mihemuko yangu, naweza kutenda ukweli kiasi, na ninaweza kuishi nikiwa na haki kidogo—yote haya ni kwa sababu ya wokovu wa Mungu, na ni matokeo yaliyofanikishwa na hukumu na kuadibu vilivyo katika maneno ya Mungu.

Iliyotangulia: 53. Kulegeza Uhusiano Unaowafunga Watu Pamoja

Inayofuata: 55. Kuondokana na Minyororo ya Utumwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

29. Toba ya Afisa

Na Zhenxin, UchinaMwenyezi Mungu anasema, “Tangu uumbaji wa dunia hadi sasa, yote ambayo Mungu amefanya katika kazi Yake ni upendo, bila...

62. Kuinuka licha ya kushindwa

Na Fenqi, Korea ya KusiniKabla ya kumwamini Mungu, nilifundishwa na CCP, na sikufikiria chochote ila jinsi ya kufaulu kutokana na juhudi...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp