55. Kuondokana na Minyororo ya Utumwa

Na Zhou Yuan, Uchina

Mwenyezi Mungu anasema, “Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, bali si hatua ambapo nilianza kumfinyanga mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo ya kila mtu katika kitabu Changu, moja baada ya lingine, njia ambayo kwayo wameitumia kunifuata, sifa zao asilia, na hatimaye jinsi ambavyo wamejistahi. Kwa njia hii, haijalishi ni mtu wa aina gani, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu, na wote watakuwa pamoja na wa aina yake kama Nilivyopanga(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako). “Matokeo ya kila mtu yanaamuliwa kulingana na asili inayotoka kwa mwenendo wao, na daima yanaamuliwa inavyofaa. Hakuna awezaye kubeba dhambi za mwingine; hata zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kupokea adhabu badala ya mwingine. Hii ni thabiti. Malezi ya upendo ya mzazi kwa watoto wake hayamaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya watoto wake, wala upendo wenye utiifu wa mtoto kwa wazazi wake haumaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya wazazi wake. Hiyo ndiyo maana ya kweli ya maneno haya, ‘Basi kutakuwa na watu wawili shambani; mmoja wao atachukuliwa, na mwingine kuachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga katika kisiagi; mmoja atachukuliwa, na mwingine kuachwa.’ Hakuna anayeweza kuwaingiza watoto wake watenda maovu rahani kwa msingi wa upendo wao wa kina kwa watoto wao, wala hakuna anayeweza kumwingiza mke wake (ama mume) rahani kwa sababu ya mwenendo wao wa haki. Hii ni kanuni ya utawala; hakuwezi kuwa na ubaguzi kwa mtu yeyote. Wanaotenda haki ni wanaotenda haki, na watenda maovu ni watenda maovu. Watenda haki watasalimika, na watenda maovu wataangamizwa. Watakatifu ni watakatifu; wao si wachafu. Wachafu ni wachafu, na hawana sehemu yoyote takatifu. Watu wote waovu wataangamizwa, na watu wote wa haki watasalimika, hata kama watoto wa watenda maovu wanafanya matendo ya haki, na hata kama wazazi wa mtu wa haki wanafanya matendo maovu. Hakuna uhusiano kati ya mume anayeamini na mke asiyeamini, na hakuna uhusiano kati ya watoto wanaoamini na wazazi wasioamini. Ni aina mbili zisizolingana. Kabla ya kuingia rahani, mtu ana jamaa wa kimwili, lakini baada ya mtu kuingia rahani, mtu hana jamaa wa kimwili tena wa kuzungumzia(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja). Maneno ya Mungu yanatuambia kuwa kazi Yake katika siku za mwisho ni kuainisha watu kulingana na aina yao. Anaamua matokeo na hatima ya kila mtu kulingana na tabia zake, na asili na kiini chake. Ni kitu ambacho hakuna mtu anayeweza kubadilisha, na kinaamuliwa na tabia ya Mungu ya haki. Mungu anataka tuwatendee wengine kulingana na maneno Yake na kanuni za ukweli. Hatuwezi kumlinda au kumpendelea yeyote kulingana na mhemuko, hata awe ni mpendwa wetu.. Kufanya hivyo ni kinyume na ukweli na ni kuikosea tabia ya Mungu.

Wakati mmoja, kama miaka mitatu iliyopita, mkutano ulipokuwa ukimalizika, kiongozi mmoja aliniambia: “Baba yako huzua migogoro kati ya kina ndugu kila mara, akivuruga maisha ya kanisa. Tumefanya ushirika naye, tukachambua hili, na tukamwonya, lakini hatubu. Kina ndugu wameripoti kwamba alifanya jambo hilo hilo katika wajibu wake katika maeneo mengine hapo awali. Tutakusanya ukweli juu ya matendo yake maovu.” Moyo wangu ulipapa niliposikia hayo na nikajiuliza, “Je, hali hii kweli ni mbaya hivyo?” Lakini baadaye nilifikiri jinsi ambavyo, nilipohudhuria mikusanyiko na babangu, alivuruga sana maisha ya kanisa na hakukubali ukweli. Katika mikutano hakutaka kushiriki kuhusu maneno ya Mungu, lakini kila mara alizungumza juu ya vitu ambavyo havikuhusiana na ukweli, akiwachochea watu ili wasiweze kutafakari maneno ya Mungu kwa utulivu. Nilimtajia hilo lakini hakutaka kusikiza hata kidogo. Alinijibu kwa kunipa tu visingizio chungu nzima. Nilimwambia kiongozi wa kanisa kuhusu hali hiyo, ambaye kisha alifanya ushirika na babangu, na kumsaidia mara kadhaa, na akamweleza kiini na matokeo ya tabia yake. Lakini babangu alikataa kukubali hayo. Aliendelea tu kutoa visingizio na kubishana. Hakuwa mwenye kutubu hata kidogo. Lazima hali ilizidi kuwa mbaya kwani kina ndugu walikuwa wakiripoti hili sasa. Nilikumbuka kulikuwa na watu kadhaa kanisani ambao walionekana kuwa waovu na walifukuzwa kwa kuwa hawakutenda ukweli, lakini walivuruga maisha ya kanisa kila mara na hawakutubu. Iwapo babangu kweli alikuwa hivyo, je, si yeye pia angefukuzwa? Hilo kwa kweli likitokea, njia yake ya imani itafika kikomo. Je, bado atakuwa na nafasi ya kupata wokovu? Hofu yangu ilizidi kukua nilipokuwa nikifiria hayo, na nilihisi kama kwamba nilichanganyikiwa.

Usiku huo niligaagaa na kugeuka, sikuweza kulala, nikifikiria yale ambayo wengine walisema kumhusu babangu. Nilijua walikuwa tu wakijaribu kulinda maisha ya kanisa kutokana na vurugu, kutokana na kuzingatia kuingia kwa kina ndugu katika uzima, na hilo lilikubaliana na mapenzi ya Mungu. Nilijua kuhusu tabia ya babangu na nilijiuliza ikiwa nilipaswa kumwambia kiongozi kuihusu. Nilifikiria jinsi babangu alivyokuwa mwenye upendo nilipokuwa mdogo. Kila mimi na kaka yangu tulipopigana. alinilinda iwe nilikuwa mwenye makosa au la; kulipokuwa baridi na shule yangu haikuwa na malazi ya joto, aliendesha baiskeli yake zaidi ya maili 60 ili kuniletea mfarishi. Mama yangu aliondoka zake kufanya wajibu wake mara nyingi, kwa hivyo babangu kwa kawaida ndiye aliyekuwa akinipikia na kunitunza. Nilipoendelea kufikiria hayo, sikuweza kuzuia machozi yangu. Niliwaza, “Babangu ndiye aliyenilea. Nikimfunua na agundue hilo, je, hatasema kwamba sina dhamiri na kwamba sina huruma? Nitawezaje kumkabili kule nyumbani baada ya hilo?” Nilianza kuandika mambo kadhaa kuhusu tabia ya babangu kwa kusitasita, lakini sikuweza kuendelea. Nilikuwa nikiwaza, "Je, itakuwaje nikiandika kila kitu ninachojua na afukuzwe? La. Sifai kuandika.” Nilitaka kuwa na usingizi mzuri wa pono ili uniondoe kutoka katika hali halisi, lakini sikuweza kulala hata kidogo. Nilihisi wasiwasi na hatia. Tabia yake kwa kweli haikuwa nzuri hivi karibuni, na nilijua machache kuhusu matendo yake ya zamani. Nikinyamaza, je, sitakuwa nikificha ukweli? Nilikuwa na mapambano halisi ya ndani. Ilibidi nije mbele za Mungu kumwomba. Niliomba, "Ee Mungu, najua kuhusu baadhi ya maovu ambayo babangu ametenda, na najua lazima nitetee kazi ya kanisa na kusema ukweli kuhusu kile ninachojua, lakini sitaki kufanya hivyo kwani ninaogopa kwamba atafukuzwa. Mungu, tafadhali niongoze ili niweze kutenda ukweli, niwe mtu mwaminifu, na nitetee kazi ya kanisa.” Nilihisi mtulivu kiasi baada ya sala hii. Kisha nikasoma maneno haya ya Mungu: “Wote wamesema kwamba wangeweza kuudhukuru mzigo wa Mungu na kutetea ushuhuda wa kanisa. Ni nani ambaye kweli amefikiri kwa makini kuhusu mzigo wa Mungu? Jiulize: Je, wewe ni mtu ambaye ameonyesha nadhari kwa mzigo wa Mungu? Je, unaweza kutenda haki kwa ajili ya Mungu? Je, unaweza kusimama na kuzungumza kwa ajili Yangu? Je, unaweza bila kusita kuweka ukweli katika vitendo? Je, wewe ni jasiri vya kutosha kupambana dhidi ya matendo yote ya Shetani? Je, unaweza kuwa na uwezo wa kuweka hisia zako kando na kufichua Shetani kwa sababu ya ukweli Wangu? Je, unaweza kuyaruhusu mapenzi Yangu yatimizwe ndani yako? Je, umejitolea moyo wako wakati muhimu unapowadia? Je, wewe ni mtu ambaye hufanya mapenzi Yangu? Jiulize na kufikiri juu yake mara kwa mara(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 13). “Wote huishi katika hisia—na hivyo Mungu haepuki hata mmoja wao, na Hufunua siri zilizofichwa mioyoni mwa wanadamu wote. Kwa nini ni vigumu sana kwa watu kujitenga na hisia? Je, ni muhimu zaidi kuliko viwango vya dhamiri? Je, dhamiri inaweza kufanikisha mapenzi ya Mungu? Je, hisia inaweza kuwasaidia watu kupitia shida? Machoni pa Mungu, hisia ni adui Yake—hili halijanenwa wazi katika maneno ya Mungu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 28). Sikuwa na majibu ya maswali haya ya maneno ya Mungu. Nilijua vizuri kuwa babangu hakufuatilia ukweli, na kwamba alivuruga mikutano na kukatiza wengine kula na kunywa maneno ya Mungu. Hakusikiliza ushirika wa mtu yeyote, aliwachukia wengine bila sababu, aliwahukumu watu bila wao kufahamu, na alieneza ugomvi. Lakini kwa kuwa nilizuiwa na hisia, nilishindwa kutilia maanani jinsi kuingia katika uzima kwa kina ndugu kulivyokuwa kukikatizwa. Sikutaka kabisa kumwambia ukweli kiongozi ili kumlinda babangu. Sikuwa nikitia ukweli katika vitendo au kuyazingatia mapenzi ya Mungu. Nilifikiri kuhusu watu wawili waovu ambao kanisa liliwafukuza hapo awali. Kuwaona wakikataa kutenda ukweli na kuvuruga maisha ya kanisa kulinighadhabisha sana, na niliwafunua kwa haki na vikali. Hivyo kwa nini sikuweza kusema ukweli ilipofikia wakati wa kuandika kuhusu tabia ya babangu? Niliona kwamba sikuwa mtu mwaminifu, na kwamba sikuwa na ufahamu wa haki. Sikuwa nikitenda ukweli au kutetea kazi ya kanisa wakati huu muhimu. Badala yake nilikuwa nikimlinda babangu kwa sababu ya mhemuko, nikificha maovu yake na kutenda kinyume cha kanuni za ukweli. Je, huko hakukuwa kusimama upande wa Shetani na kuwa adui wa Mungu? Nilipogundua hili, nilimwomba Mungu na katubu Kwake. “Sitaki kutenda kutokana na mhemuko wangu tena. Nataka kusema ukweli kuhusu babangu.”

Baada ya ombi langu, nilikumbuka baadhi ya maonyesho yake maovu na nikayaorodhesha yote, moja moja. Alipokuwa akihudumu kama shemasi wa injili, alianza kumchukia Ndugu Zhang aliyekuwa mfanyakazi mwenza bila sababu, Alimhukumu na kumbagua mbele ya kina ndugu wengine, akimwacha Ndugu Zhang akifadhaika na akiwa katika hali hasi. Kiongozi alimpogoa na kumshughulikia babangu, lakini hakusikiza. Kina ndugu walipoonyesha matatizo yake, hakuyakubali. Kila mara alilenga kasoro za wengine na kutumia udhaifu wao na kila wakati alisema, “Nimekuwa muumini kwa miaka mingi. Naelewa haya yote!” Aliponiona nikishiriki kikamilifu katika wajibu wangu, alinihimiza nitafute pesa na vitu vya kidunia, na kila mara alisema mambo mabaya ili kufifiza shauku yangu kwa wajibu wangu. Wakati mmoja baada ya babangu kuhusika katika ajali ya gari, Ndugu Lin kutoka kanisani alikwenda kumjulia hali na kushiriki juu ya ukweli, akisema kwamba alipaswa kutafakari juu yake mwenyewe na apate funzo, lakini hakukubali hayo. Alipotosha ukweli, na akaeneza uvumi kwamba Ndugu Lin alikuwa amekuja kumdhihaki. Jambo hilo liliwafanya ndugu wengine wamchukie Ndugu Lin bila sababu. Kufikiria haya yote kulinistaajabisha na kunikasirisha sana. Nilijiuliza, “Je, huyu kweli ni babangu? Je, huyu si mtu mwovu?” Nilifikiri daima kwamba baada ya miaka mingi ya kuamini huku akifanya wajibu wake wa kazi ya injili, angeweza kuteseka na kulipa gharama. Nilidanganywa na jinsi alivyoonekana kwa nje, nikidhani kuwa alikuwa muumini wa kweli. Sikuwahi kujaribu kutambua tabia yake. Nilikuwa mpumbavu sana na kipofu. Sasa nilijilaumu kwa kutawaliwa na mhemuko, kumdekeza na kumlinda. Kisha nikasoma haya katika maneno ya Mungu: “Wale walio kanisani ambao wanaeneza matamshi yao yenye sumu, wale miongoni mwa ndugu ambao wanasambaza uvumi, kuchochea utengano na kufanya magenge wanapaswa kufukuzwa kutoka kanisani. Lakini watu hawa wamezuiwa kwa kuwa sasa ni enzi tofauti ya kazi ya Mungu, kwa sababu wamehukumiwa kuwa vyombo vya kuondolewa. Wale waliopotoshwa na Shetani wote wana tabia iliyopotoka. Hata hivyo, baadhi ya watu wana tabia potovu tu, huku kuna wengine walio tofauti: Si tu kwamba wana tabia potovu za kishetani, lakini asili zao pia ni mbovu kupita kiasi. Si tu kwamba maneno yao na vitendo vyao vinafichua tabia zao potovu za kishetani; watu hawa, aidha ndio Shetani wa kweli. Tabia yao inakatiza na kuvuruga kazi ya Mungu, inaharibu uingiaji wa kina ndugu katika uzima, na kuharibu maisha ya kawaida ya kanisa. Mbwa mwitu hawa waliovalia ngozi ya kondoo lazima waondolewe nje siku moja, na mtu lazima awe na mtazamo usiojizuia kwa vibaraka hawa wa Shetani; mtu lazima awe na mtazamo wa kuachwa kwao. Ni katika kufanya hili pekee ndipo mtu ataweza kusimama upande wa Mungu na wale wasioweza kufanya hili wako katika ushirika na Shetani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli). Nilipolinganisha tabia ya babangu dhidi ya maneno ya Mungu, niliona hii haikuwa tu tabia potovu ya kawaida ambayo alikuwa akionyesha, lakini ilikuwa asili yenye uovu. Alikuwa na shauku kubwa kwa juujuu na aliweza kuteseka kwa ajili ya wajibu wake, na aliweza kuendelea kueneza injili licha ya mateso ya CCP, lakini hakuweza kukubali ukweli. Hata alichukia ukweli. Matendo yake yalifichua asili yake yenye hila na uovu. Kimsingi alikuwa mtu mwovu ambaye alikuwa wa Shetani, na alipaswa kufukuzwa. Ingawa nilikuwa bintiye, sikufaa kufuata hisia zangu. Nilipaswa kusimama upande wa Mungu katika imani yangu, na kumfunua na kumkana Shetani. Nilifikiri juu ya kina ndugu katika kundi nililosimamia ambao hawakuwa na utambuzi juu yake. Ilinibidi nifanye ushirika nao na kufunua uovu wa babangu ili wasidanganywe naye tena. Lakini kisha nikawa na wasiwasi: “Baadhi yao waliletwa na yeye katika imani na wana uhusiano mwema naye. Nikimfunua, je, hawatasema kwamba sina dhamiri, kwamba mimi ni mkatili? Na akifukuzwa na apoteze nafasi yake katika wokovu, hilo litamuumiza sana.” Wazo hili lilinifadhaisha sana, na nilipoteza hamu yangu ya kushiriki ushirika huo. Sikuweza kulala usiku huo, nikifikiri kwamba nisipofunua uovu wa babangu na kina ndugu wadanganywe na kusimama upande wake, basi watakuwa wakishiriki katika uovu wake. Nikiwaona wakidanganywa lakini nisifanye ushirika nao, je, sitakuwa nikiwadhuru? Nilijilaumu kiasi nilipofikiria hayo, kwa hivyo nilimwomba Mungu: “Ee Mungu, nina wasiwasi mwingi sasa. Tafadhali nipe imani na nguvu, niongoze na Unielekeze katika kutenda ukweli na kumfunua mtu huyu mwovu.”

Baada ya kuomba, nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Katika maneno ya Mungu, ni kanuni ipi iliyotajwa kuhusiana na jinsi watu wanapaswa kutendeana? Kipende kile ambacho Mungu anapenda, na ukichukie kile ambacho Mungu anachukia. Yaani, watu wanaopendwa na Mungu, ambao kweli hufuatilia ukweli na kufanya mapenzi ya Mungu, ndio ambao unapaswa kuwapenda hasa. Wale wasiofanya mapenzi ya Mungu, wanaomchukia Mungu, wasiomtii, na wale Anaowachukia ndio wale ambao sisi pia tunapaswa kuwadharau na kuwakataa. Hiki ndicho neno la Mungu linahitaji. … Wakati wa Enzi ya Neema, Bwana Yesu alisema, ‘Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni nani? ... Kwa kuwa yeyote atakayetenda mapenzi ya Baba yangu wa mbinguni, yeye ndiye ndugu Yangu, na dada yangu, na mama yangu.’ Msemo huu tayari ulikuwepo zamani katika Enzi ya Neema, na sasa maneno ya Mungu ni yanayofaa zaidi: ‘Penda kile anachopenda Mungu, na uchukie kile anachochukia Mungu.’ Maneno haya ni ya moja kwa moja, lakini watu mara nyingi hushindwa kufahamu maana yake ya kweli. Mtu akilaaniwa na Mungu, lakini kwa mwonekano wote wa nje anaonekana kuwa mzuri kabisa, au yeye ni mzazi au jamaa wako, basi unaweza kujikuta unashindwa kumchukia mtu huyo, na huenda kukawa hata na urafiki mwingi na uhusiano wa karibu kati yenu wawili. Unaposikia maneno kama hayo kutoka kwa Mungu, wewe unakasirika na huwezi kuufanya moyo wako uwe mgumu kwa mtu kama huyo au kumwacha mtu kama huyo. Hii ni kwa sababu kuna fikira ya desturi hapa inayokufunga. Unafikiria kwamba ukifanya hili, utakabiliwa na ghadhabu ya Mbinguni, uadhibiwe na Mbinguni, na hata utupwe kando na jamii na uhukumiwe na maoni ya umma. Aidha, tatizo dhahiri ni kwamba litaisumbua dhamiri yako. Dhamiri hii hutokana na kile ambacho wazazi wako walikufundisha tangu utotoni, au kutokana na ushawishi na maambukizo ya tamaduni za kijamii, ambazo zimeweka mizizi na njia ya kufikiria ndani yako kiasi kwamba huwezi kutenda neno la Mungu na kupenda kile Anachopenda na kuchukia kile Anachochukia. Hata hivyo, ndani mwako kabisa, unajua kwamba unapaswa kuyachukia na kuyakataa, kwa maana maisha yako yalitoka kwa Mungu, na hukupewa na wazazi wako. Mwanadamu anapaswa kumwabudu Mungu na kujirudisha Kwake. Hata ingawa unasema na kufikiria hivyo, huwezi kabisa kubadilika na huwezi kabisa kuyaweka katika vitendo. Je, unajua kinachoendelea hapa? Ni kwamba vitu hivi vimekufunga, kwa nguvu na kwa kina. Shetani hutumia vitu hivi kufunga mawazo yako, akili yako na moyo wako kiasi kwamba huwezi kukubali maneno ya Mungu. Vitu kama hivyo vimekujaza kabisa, kufikia kiwango ambapo huna nafasi ya maneno ya Mungu. Aidha, ukijaribu kuyaweka maneno Yake katika vitendo, basi vitu hivyo vitakuathiri na kukufanya ukinzane na maneno Yake na matakwa Yake, na hivyo kukufanya usiweze kujinasua kutoka katika shida hizi na usiweze kuwa huru kutokana na utumwa huu(“Ni kwa Kutambua Maoni Yako Yaliyopotoka Tu Ndipo Unapoweza Kujijua Mwenyewe” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kisha nilielewa kwamba kanuni ambayo Mungu anataka tuwe nayo katika kuwashughulikia wengine lazima iwe kupenda kile Anachopenda na kuchukia kile Anachochukia. Watu wanaopenda ukweli na wanaoweza kufanya mapenzi ya Mungu ndio ambao tunapaswa kuwatendea kwa upendo, ilhali watu waovu wanaochukia ukweli na kumpinga Mungu ndio tunaopaswa kuwachukia. Utendaji huu pekee ndio unaokubaliana na mapenzi ya Mungu. Lakini nilizuiwa kila mara na mhemuko ilipofikia babangu. Nilimlinda na kumtetea. Sikuweza kupenda kile ambacho Mungu anapenda na kuchukia kile ambacho Mungu anachukia. Ni kwa sababu mawazo ya zamani ya Shetani ya “Damu ni nzito kuliko maji” na “Mwanadamu si mfu, anawezaje kukosa hisia?” yalitawala moyo wangu. Sikuweza kutofautisha mema na mabaya, nikifikiri kwamba kufunua tabia mbovu ya babangu kingekuwa kitendo cha kufedhehesha na kisicho cha busara. Niliogopa kukosolewa na kushutumiwa na wengine. Ili kulinda uhusiano wa familia ya kimwili, nilishindwa kulinda ukweli na kumfunua mtu mbaya bila kujali kazi ya nyumba ya Mungu na kuingia katika uzima kwa kina ndugu. Huko kwa kweli ndiko kulikuwa kukosa busara na kukosa ubinadamu. Niliona kwamba mawazo haya ya kishetani na ya zamani yalikuwa yakinizuia kutenda ukweli, yakinifanya nisimame upande wa Shetani na kumpinga Mungu, ingawa sikutaka. Kwa kweli, Mungu hajawahi kusema kwamba tunapaswa kuwa wenye busara tunapowashughulikia pepo na watu waovu, wala Yeye hajasema kwamba kuwakataa wapendwa ambao ni wa Shetani ni uovu. Katika Enzi ya Sheria, watoto wa Ayubu ambao hawakuwa na imani walikufa katika maafa, lakini Ayubu hakuwatetea watoto wake au kumlalamikia Mungu kwa ajili yao kutokana na mhemuko. Badala yake, alilisifu jina la Mungu. Naam. Katika Enzi ya Neema, wazazi wa Petro walizuia imani yake, kwa hivyo aliwaacha na kuondoka nyumbani, akiacha kila kitu ili amfuate Mungu, na hivyo akapata sifa ya Mungu. Nilipofikiria juu ya uzoefu wa Ayubu na Petro, Nilipata ufahamu kiasi kuhusu matakwa ya Mungu ya kupenda kile Anachopenda na kuchukia kile Anachochukia.

Kisha nikasoma maneno mengi zaidi ya Mungu: “Shetani ni nani, mapepo ni nani, na nani ni maadui wa Mungu kama si wapinzani wasiomwamini Mungu? Wao si watu wasiomtii Mungu? Wao si watu wanaodai kwa maneno kuamini lakini hawana ukweli? Wao si wale watu wanaofuata tu kupata kwa baraka lakini hawawezi kumshuhudia Mungu? Bado unachanganyika na wale mapepo leo na kuwa na dhamiri na mapenzi kwao, lakini kwa hali hii huenezi nia nzuri kuelekea kwa Shetani? Je, huchukuliwi kuwa unashiriki na mapepo? Kama watu siku hizi bado hawawezi kutofautisha kati ya mema na maovu, na wanaendelea kuwa wenye kupenda na kuhurumia bila kufikiri na bila nia yoyote ya kutafuta mapenzi ya Mungu au kuweza kwa njia yoyote kushikilia nia za Mungu kama zao wenyewe, basi miisho wao utakuwa dhalili zaidi. … Kama unalingana na wale Ninaowachukia na wale Nisiokubaliana nao, na bado unashikilia mapenzi na hisia za binafsi kwao, basi wewe si asiyetii? Humpingi Mungu kimakusudi? Je, mtu kama huyu anamiliki ukweli? Ikiwa watu wako na dhamiri kwa maadui, wana upendo kwa mapepo na wana huruma kwa Shetani, basi hawaikatizi kazi ya Mungu kimakusudi?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja). Kusoma haya kulinifanya nihisi huzuni na hatia sana. Nilijua kuwa babangu alichukia ukweli na alikuwa kila mara akivuruga maisha ya kanisa, na kwamba asili na kiini chake vilikuwa viovu, lakini niliendelea kuwa mzuri na mwenye upendo kwake, hata kumtetea na kumlinda. Je, Mungu hakumaanisha hivyo hasa kwa kusema “lakini kwa hali hii huenezi nia nzuri kuelekea kwa Shetani?” na “Je, huchukuliwi kuwa unashiriki na mapepo”? Je, sikuwa nikimpinga Mungu na kuvuruga kazi ya kanisa bila haya? Katika nyumba ya Mungu, ukweli na haki hutawala. Nguvu zote za Shetani, pamoja na watu wote waovu na wapinga Kristo, hawawezi kubaki. Lazima wafunuliwe na kuondolewa na Mungu, na wafukuzwe kanisani. Jambo hili limebainishwa na tabia ya Mungu ya haki. Lakini nilikuwa nikimtetea mtu mwovu, nikijaribu kumruhusu abaki ndani ya nyumba ya Mungu. Je, sikuwa nikivumilia vurugu ya mtu mwovu katika maisha ya kanisa? Je, sikuwa nikimsaidia adui mwovu na kumpinga Mungu? Kuendelea hivyo kungemaanisha kwamba Mungu ningeadhibiwa pamoja na yule mtu mwovu. Utambuzi huu uliniogofya kidogo. Niliona kwamba tabia ya Mungu ya haki haivumili kosa lolote na kumtetea mwovu kutokana na hisia za kibinafsi ni hatari sana! Sikuweza kuendelea kuongea na kutenda kulingana na hisia zangu. Hata ingawa alikuwa babangu, nilipaswa kutenda ukweli, kupenda kile ambacho Mungu anapenda, kuchukia kile ambacho Mungu anachukia, na kutetea maslahi ya nyumba ya Mungu.

Baadaye nilienda mkutanoni na kikundi changu na nikafichua ukweli wote wa tabia na vitendo viovu vya babangu. Kina ndugu ambao walikuwa wamepotoshwa naye walianza kutambua kiini chake. Baadaye kanisa lilitoa taarifa ya kufukuzwa kwa babangu. Nilikwenda nyumbani, nikamsomea taarifa hiyo, na nikazungumza juu ya tabia yake mbaya. Nilishtuka aliposema kwa dharau., “Nimejua kwa muda sasa kwamba nitafukuzwa. Nimemwamini Mungu kwa miaka mingi kwa ajili ya baraka, vinginevyo ningekuwa nimeacha kuamini zamani sana.” Nilipoona kwamba hakuwa na nia ya kutubu, nilijua waziwazi moyoni mwangu kuwa asili yake yenye uovu ilikuwa imefichuliwa kabisa. Baada ya babangu kufukuzwa hakukuwa na waovu waliovuruga mambo kanisani. Mikutanoni, kina ndugu wote waliweza kusoma maneno ya Mungu na kufanya ushirika kuhusu ukweli bila vurugu. Walifanya wajibu wao kama walivyopaswa, na maisha ya kanisa yalizaa matunda. Niliona kwamba katika nyumba ya Mungu, ukweli na haki hutawala, na tunapotenda ukweli kulingana na maneno ya Mungu, tunashuhudia uongozi na baraka Zake. Kwa mintarafu ya babangu, niliondokana na hisia zangu za kibinafsi polepole na mwishowe niliweza kutenda ukweli kidogo na kuiunga mkono kazi ya kanisa. Haya yote yalifanikishwa kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu!

Iliyotangulia: 54. Vita vya Kiroho

Inayofuata: 57. Kuripoti Au Kutoripoti

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

33. Pingu za Umaarufu na Faida

Na Jieli, UhispaniaMwenyezi Mungu anasema, “Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp