43. Kwa Kuacha Ubinafsi, Nimekombolewa

Na Xiaowei, Uchina

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika tabia za watu wa kawaida hakuna uhalifu au udanganyifu, watu wana uhusiano wa kawaida kati yao, hawafanyi mambo pekee yao, na maisha yao si duni wala ya kufifia. Kwa hiyo, vilevile, Mungu huinuliwa miongoni mwa wote, maneno Yake hupenya miongoni mwa wanadamu, watu huishi katika amani kati yao na chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, dunia imejaa upatanifu, bila kuingilia kwa Shetani, na utukufu wa Mungu huwa na umuhimu mkuu sana miongoni mwa wanadamu. Watu kama hao ni kama malaika: watakatifu, wa kusisimua, wasiolalamika kamwe kuhusu Mungu, na hutoa juhudi zao zote kwa utukufu wa Mungu duniani pekee(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 16). Maneno ya Mungu yanatuonyesha kwamba tabia ya mtu wa kawaida haina upotovu, udanganyifu, ubinafsi na si yenye kustahili dharau. Kuchukulia agizo la Mungu kwa dhati, kufanya kazi kwa amani na kina ndugu na mtu kufanya kila awezalo kwa ajili ya wajibu wake ni vitu vya msingi zaidi ambavyo mtu anapaswa kuweza kufanya. Nilikuwa nikiishi kulingana na falsafa za kishetani kama vile “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake” na “Mjinga akierevuka, mwerevu huwa mashakani.” Nilikuwa mbinafsi, mwenye kustahili dharau, mpotovu, na mjanja, na nilikosa kabisa ufanani wa kibinadamu. Nilipopitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu ndipo tabia hizi zangu za kishetani zilipoanza kubadilika.

Ilikuwa mwezi wa Juni ya 2018 wakati ambapo Ndugu Zhang alijiunga na timu yetu ili kushirikiana nami katika wajibu wangu. Wakati huo niliwaza, “Nimekuwa nikifanya wajibu huu kwa muda sasa, kwa hivyo ninafahamu kanuni na nimepata matokeo kidogo. Labda wakati fulani nitaiacha timu hii na nichukue jukumu kubwa zaidi. Nahitaji kumsaidia Ndugu Zhang ailewe kazi hii haraka iwezekanavyo ili aweze kufanya kazi ndani ya timu yetu.” Nilianza kumfundisha ujuzi wa msingi ambao nilikuwa nimejifunza katika wajibu wangu. Miezi mitatu baadaye niligundua kwamba Ndugu Zhang alikuwa na ufahamu wa msingi kuhusu kila kitu na alikuwa akiendelea kwa haraka sana. Wakati huo nilianza kutishika, nikiwaza, “Ndugu Zhang amekuwa na maendeleo ya haraka sana katika wajibu wake. Haya yakiendelea, je, hatanishinda hivi karibuni? Kiongozi akigundua jinsi maendeleo yake yalivyo ya haraka, je, hatampa cheo kikubwa?” Wazo hili liliponijia akilini, niliwaza moyoni mwangu, “Hapana, nahitaji kuficha mambo. Siwezi kushiriki naye kila kitu ninachojua.” Katika kazi yetu kuanzia wakati huo, nilipogundua kwamba ujuzi wa Ndugu Zhang ulikuwa na upungufu kidogo, nilimwambia tu mambo machache ya juujuu bila kushiriki kikamilifu maarifa yangu. Nilijua kwamba kufanya hivyo hakukuwa sawa lakini hata hivyo nilifikiri kuhusu methali ya zamani isemayo, “Mjinga akierevuka, mwerevu huwa mashakani.” Yeye akiwa maarufu, ningewezaje kujionesha vizuri? Sikumruhusu anishinde. Tulipokuwa tukiendelea kufanya kazi pamoja, chochote ambacho Ndugu Zhang aliniulizia, nilimpa jibu lisilo kamilifu na kuficha habari nyingine.

Muda mfupi baadaye, kiongozi alimtafuta Ndugu Zhang ili kujadili kazi muhimu. Nilishtuka niliposikia kuhusu haya. Niliwaza, "Nimekuwa kwenye timu kwa muda mrefu zaidi kuliko Ndugu Zhang. Kwa nini kiongozi hakutaka kuzungumza nami? Je, mimi si hodari kama yeye? Mimi ndimi ninayemfundisha, lakini sasa yeye ndiye anayethaminiwa sana na ninapuuzwa. Yeye ni maarufu nami nimesahaulika. Nikiendelea kumfundisha, je, hatapata ujuzi haraka hata zaidi? Akipata cheo kikubwa, ni nani atakayenistahi?” Kwa hivyo katika kazi yetu pamoja tangu wakati huo, nilipomwona Brother Zhang akikabiliwa na matatizo, sikutaka kumsaidia. Maendeleo yetu yaliathirika kwa sababu ya mambo haya kutotatuliwa kwa wakati ufaao, na hii iliishia kuchelewesha kazi ya kanisa. Nilihisi hatia na wasiwasi kidogo, lakini sikutafakari juu yangu mwenyewe hata kidogo. Siku moja kwapa langu lilianza kuwasha ghafla, na sikuweza kukomesha mwasho huo. Hata kupaka lihamu hakukusaidia. Siku iliyofuata, mkono wangu ulianza kuuma sana kiasi kwamba sikuweza kuusogeza. Niligundua kwamba tatizo hili halikuwa utukizi, kwa hivyo nilikuja mbele za Mungu kuomba na kutafuta. Nilisema, "Ee Mungu, tatizo hili limeanza ghafla sana. Ninajua kuwa mapenzi Yako mema yamelisababisha. Lakini sijali kabisa na sijui mapenzi Yako ni yapi. Tafadhali nitie nuru na Uniongoze.”

Siku moja wakati wa ibada zangu, maneno haya ya Mungu yalinijia akilini ghafla: “Ikiwa hutaki kutoa yote uliyo nayo, ukiyaficha, iwapo wewe ni mjanja katika matendo yako….(“Ni kwa Kuwa Mtu Mwaminifu tu Ndiyo Mtu Anaweza Kuwa na Furaha Kweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno haya yalinizindua. Nilikuwa nikiishi katika hali ya kushindania sifa na faida, nikiogopa kwamba ndugu huyu angenishinda, kwa hivyo sikuwahi kuwa mkweli katika kazi yetu, na sikutaka kushiriki naye maarifa yangu. Nilitambua kwamba Mungu alikuwa Akinionya kwa kutumia tatizo hilo, ili nitafakari juu yangu. Baadaye, nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Wasioamini wana aina fulani ya tabia potovu. Wanapowafundisha watu wengine maarifa ya kitaalamu au ujuzi fulani, wanaamini dhana kwamba ‘Mjinga akierevuka, mwerevu huwa mashakani.’ Wanaamini kwamba wakiwafundisha wengine kila kitu wanachojua, basi hakuna mtu atakayewastahi tena na watakuwa wamepoteza hadhi zao. Kwa sababu hii, wao huhisi haja ya kuficha kiasi fulani cha maarifa haya, wakiwafundisha watu asilimia themanini tu ya yale wanayoyajua na kuhakikisha kwamba wanaficha maaarifa fulani watakayotumia kwa manufaa yao; wanahisi kwamba hivi pekee ndivyo wanavyoweza kuonyesha vyeo vyao kama waalimu. Kuficha habari kila wakati na kuwa na kutofichua maarifa fulani kwa manufaa yao wenyewe—je, hii ni tabia ya aina gani? Ni udanganyifu. … Usifikiri kwamba unafanya tu vizuri au kwamba hujaficha maarifa kwa kumwambia tu kila mtu mambo ya juujuu au ya msingi; hii haifai kabisa. Wakati mwingine unaweza kufundisha nadharia chache tu au vitu ambavyo watu wanaweza kuvielewa neno kwa neno, lakini wanafunzi hawawezi kabisa kutambua kiini chochote au mambo muhimu. Unatoa muhtasari tu, bila kufafanua au kueleza kwa utondoti, wakati huo wote bado ukidhani, ‘Kwa vyovyote vile, nimekwambia, na sijaficha lolote kwa makusudi. Ikiwa huelewi, ni kwa sababu ubora wako wa tabia ni duni sana, kwa hivyo usinilaumu. Itabidi tu tuone jinsi Mungu atakavyokuongoza sasa.’ Fikira kama hiyo ina udanganyifu, siyo? Je, si jambo la aibu na ubinafsi? Kwa nini huwezi kuwafundisha watu kila kitu kilichoko moyoni mwako na kila kitu unachoelewa? Kwa nini badala yake, unaficha maarifa? Hili ni tatizo la nia na tabia yako(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalifichua kabisa hali yangu mwenyewe. Sikutaka kumfundisha ujuzi ambao nilikuwa nimejifunza kwa ajili ya sifa yangu na cheo changu mwenyewe. Niliogopa kwamba angeuelewa na kunishinda, nikifikiri kwamba mwanafunzi angemnyang’anya mwalimu nafasi yake. Kwa kusita kila wakati, je, sikuwa nikidhibitiwa na asili yangu ya ubinafsi, ya kustahili dharau, potovu na ya kishetani? Nilikumbuka pia wakati ambapo Ndugu Zhang alikuwa amejiunga na timu yetu. Motisha yangu ya kumfundisha ilikuwa ili aweze kufanya kazi ya timu haraka iwezekanavyo. Kisha ningekuwa na mtu wa kumwachia wajibu wangu kwa sababu nilikuwa nikitarajia kupata cheo muhimu zaidi. Lakini nilipoona jinsi alivyoelewa mambo haraka na kwamba kiongozi alimthamini sana, nilianza kuwa na wasiwasi sana. Nilionea wasiwasi kwamba iwapo angeendelea kufanya vizuri, angenishinda siku moja na kwamba angechukua nafasi yangu. Kama matokeo, sikutaka kushiriki naye yale niliyoyajua. Wakati mwingine nilipojua kwamba alikuwa amekabiliwa na matatizo katika wajibu wake sikutaka kumsaidia, jambo ambalo liliishia kuchelewesha kazi ya kanisa. Niliona kwamba nilikuwa nikifanya kazi ili kulinda sifa yangu na cheo changu mwenyewe bila kuzingatia kazi ya nyumba ya Mungu. Kwa kweli nilikuwa mbinafsi na mdanganyifu sana. Bila nidhamu ya Mungu ya wakati ufaao iliyonifanya niwe na tatizo hilo, nisingetafakari juu yangu mwenyewe. Kisha nikasoma maneno haya ya Mungu: “Tangu ulipomwamini Mungu, umekula na kunywa maneno ya Mungu; umeikubali hukumu Yake na kuadibu Kwake na umekubali wokovu Wake. Hata hivyo, iwapo kanuni zako za kutenda na mwelekeo wako wa kufanya mambo na wa kutenda kama mwanadamu havijabadilika, ikiwa wewe ni sawa na wasioamini, je, Mungu atakutambua kama mtu anayemwamini? Hapana. Atasema kwamba bado unatembea kwenye njia ya wasioamini. Kwa hivyo, iwe unatimiza wajibu wako au kujifunza maarifa ya kitaalamu, lazima ufuate kanuni katika kila kitu unachofanya. Lazima uchukulie kila kitu unachofanya kulingana na ukweli, na utende kwa mujibu wa ukweli. Lazima utumie ukweli kusuluhisha matatizo, kutatua tabia potovu ambazo zimefichuliwa ndani yako, na kutatua njia na mawazo yako yasiyofaa. Lazima uweze kushinda haya kila wakati. Kwanza, lazima ujichunguze. Mara utakapofanya hivyo, ikiwa utagundua tabia potovu, lazima uitatue, uishinde na uiache. Mara utakapotatua matatizo haya, wakati ambapo hutafanya tena mambo kulingana na tabia zako potovu, na utakapoweza kuacha nia na maslahi yako na utende kulingana na kanuni za ukweli, wakati huo tu ndipo utakapokuwa ukifanya yale ambayo mtu anayemfuata Mungu kwa kweli anapaswa kufanya(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Lazima uchukue kiini na mambo muhimu ya maarifa hayo ya kitaalamu—mambo ambayo wengine hawajaelewa au kuyatambua—na uwaambie watu ili wote waweze kutumia uwezo wao, na kwa sababu hiyo wajue mambo mengi, ya maana, na yaliyokomaa hata zaidi. Ukichangia mambo haya yote, yatakuwa na manufaa kwa watu wanaotimiza wajibu huu na pia kwa kazi ya nyumba ya Mungu. … Watu wengi zaidi wanapojulishwa kipengele fulani cha maarifa ya kitaalamu kwa mara ya kwanza, wanaweza tu kuelewa maana yake iliyo wazi, ilhali sehemu inayojumuisha kiini na mambo muhimu huhitaji mazoezi ya kipindi fulani cha muda ili watu waielewe. Ikiwa tayari umeelewa mambo haya muhimu sana, unapaswa kuwaambia moja kwa moja; usiwafanye wazungukezunguke sana na kutumia muda mwingi sana kuyaelewa. Hili ni jukumu lako; hiki ndicho kile unachopaswa kufanya. Ukiwaambia tu yale unayoyaamini kuwa ndiyo kiini na mambo muhimu, hutakuwa ukificha chochote, na wakati huo tu ndipo hutakuwa mbinafsi(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kutoka katika maneno ya Mungu niligundua kwamba nilihitaji kuzingatia kutafakari juu yangu katika wajibu wangu na kutafuta ukweli ili kutatua asili yangu ya kishetani, ya ubinafsi na ya kustahili dharau. Nilihitaji kuacha mawazo na dhana zangu zisizofaa na niweze kufanya kazi kwa upatanifu na kina ndugu katika wajibu wangu. Niligundua kwamba kila mmoja wetu ana upungufu mwingi, iwe ni wa ukweli au katika kazi yetu, kwa hivyo kina ndugu wanahitaji kusaidiana na kuungana mikono katika wajibu wao, na kushiriki juu ya yale wanayoelewa bila kuficha lolote. Kwa kufidia upungufu wa kila mmoja kwa njia hii, tuna uwezekano mdogo zaidi wa kuchepuka. Kwa kweli, mimi kuwa mjuzi zaidi kuliko Ndugu Zhang kulitokana kabisa na wema wa Mungu. Nilipaswa kuwa mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, kuacha ubinafsi wangu na kumfundisha kila kitu nilichojua ili aweze kutimiza wajibu wake vizuri haraka iwezekanavyo. Ni hayo tu ambayo yangekuwa yanaambatana na mapenzi ya Mungu. Mara nilipogundua hayo, nilikuja mbele za Mungu upesi kuomba, nikiwa tayari kuacha mawazo yangu mwenyewe yasiyofaa na kutoishi tena kulingana na tabia zangu za kishetani, za ubinafsi na za kustahili dharau. Baadaye, nilimtafuta Ndugu Zhang ili nizungumze naye kwa dhati juu ya hali yangu na kuchambua tabia hizi zangu potovu na za kishetani. Pia, nilishiriki naye vidokezo muhimu vya ujuzi niliokuwa nao. Nilipoanza kutenda kwa njia hii: nilihisi amani zaidi, na tatizo hilo la kiafya likaondoka haraka sana.

Nilidhani kwamba, baada ya kupitia hayo, nilikuwa tayari nimebadilika, lakini tabia hizi za kishetani zilikuwa zimekita mizizi. Mara hali nzuri ilipotokea, sikuweza kujizuia kuacha sumu hizo zionekane tena.

Mnamo Machi 2019, mimi na Ndugu Zhang tulichaguliwa kwa wakati mmoja tuwe viongozi wa kanisa. Mwanzoni, tulifanya kazi vizuri sana pamoja. Iwe ni tatizo ndani ya kanisa au shida iliyotukabili, tuliweza kutafuta ukweli pamoja ili kuitatua. Lakini hata hivyo siku moja, nilimsikia mtu kanisani akisema, “Ushirika wa Ndugu Zhang juu ya ukweli ni wa vitendo sana, na yeye ni mwaminifu sana katika wajibu wake." Nilifadhaika niliposikia haya na nikawaza, “Nikishindwa na Ndugu Zhang, hivi karibuni sitakuwa na hadhi yoyote hata kidogo!” Katika majadiliano yetu yote ya kazi baada ya hapo nilionyesha tu makosa na dosari na nilificha njia za utendaji ili kuzitatua mwenyewe. Wakati mwingine aliponijia ili kutafuta, nilijikaza tu kisabuni na kumpa habari kidogo isiyo muhimu sana, nikiogopa kwamba iwapo angeelewa mambo mengi sana, angeenda tu kusuluhisha matatizo bila mimi kujionyesha. Nakumbuka kwamba kulikuwa na wakati mmoja ambapo alikuwa karibu kwenda kuwasaidia ndugu wachache waliokuwa dhaifu. Aliogopa kwamba bila ushirika uliofaa, kusingekuwa na mafanikio, kwa hivyo alikuja kutafuta ushauri wangu juu ya ukweli ambao alipaswa kuzingatia. Lakini mawazo yangu wakati huo yalikuwa kwamba kama ningemwambia kila kitu nilichojua na iwapo angeenda kushughulikia tatizo lile, bila shaka kina ndugu wangemstahi na kisha ningeshiriki nini katika ushirika wakati uliofuata? Je, hiyo isingemfanya aonekane kuwa bora kunishinda? Kwa hivyo wakati huo niliwaza, “La, lazima nifiche jambo fulani ili nilishiriki wakati ujao ili waweze kuona kwamba mimi ndimi ninayeweza kutatua matatizo.” Nilimpa Ndugu Zhang muhtasari mfupi tu lakini sikutaja habari dhahiri au jambo lolote la muhimu sana. Kwa kuwa nilikuwa na ubinafsi wangu mwenyewe na sikutaka kushiriki naye kila kitu nilichojua, nilimwepa Ndugu Zhang kimakusudi katika kazi yetu ya pamoja na tulitumia muda kidogo kujadiliana mambo kuliko vile tulivyokuwa tukifanya. Wakati mwingine nilihisi hatia sana na nikawaza, “Kwa kufanya wajibu wangu kwa njia hii, sifanyi kazi kwa upatanifu na ndugu yangu na hili si jambo ambalo Mungu anaweza kufurahishwa nalo.” Lakini hata hivyo niliwaza, “Akinishinda, kila mtu atamstahi," kwa hivyo sikutaka kutenda ukweli tena. Wakati huo, nilikuwa katika hali ngumu kila mara na tabia ya Mungu yenye haki ikanijia. Nilikanganyikiwa kila wakati. Ushirika wangu katika mikutano haukuwa na mwanga wowote na sikuwa nikifanikisha chochote katika wajibu wangu na nilisinzia na kulala mapema sana kila usiku. Nilizidi pia kuhisi wasiwasi. Wakati huo niligundua kwamba Mungu alikuwa Ameniacha na kisha nikaogopa. Nilikuja mbele za Mungu upesi na kuomba. “Ee Mungu, nimekuwa nikiishi ndani ya tabia zangu za kishetani, za ubinafsi na zinazostahili dharau. Najua kuwa jambo hili linakuchukiza lakini siwezi kujizuia. Siwezi kuondokana na tabia hizo. Mungu, tafadhali nitie nuru ili nipate ufahamu wa kweli kuhusu asili yangu na kiini changu mwenyewe.”

Baada ya maombi yangu nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Mpaka watu wawe wamepitia kazi ya Mungu na kupata ukweli, ni asili ya Shetani inayotwaa madaraka na kuwatawala kwa ndani. Ni nini, hasa, kilicho ndani ya asili hiyo? Kwa mfano, kwa nini wewe ni mchoyo? Kwa nini wewe hulinda nafasi yako mwenyewe? Kwa nini una hisia kali sana namna hiyo? Kwa nini unafurahia hivyo vitu visivyo vya haki? Kwa nini unapenda maovu hayo? Msingi wa kupenda kwako vitu hivi ni upi? Mambo haya hutoka wapi? Kwa nini unafurahia sana kuyakubali? Kufikia sasa, nyote mmekuja kuelewa kwamba sababu kuu ya mambo haya yote ni kwamba sumu ya Shetani iko ndani yenu. Kuhusu sumu ya Shetani ni nini, inaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa maneno. Kwa mfano, ukiwauliza baadhi ya watenda maovu kwa nini walitenda jinsi walivyotenda, watajibu, ‘Kwa sababu kila mwamba ngoma huvutia upande wake.’ Msemo huu mmoja unaonyesha asili ya shida. Mantiki ya Shetani imekuwa maisha ya watu. Wanaweza kutenda mambo kwa ajili ya madhumuni fulani au mengine, lakini wanajifanyia tu. Kila mtu hudhani kwamba kwa kuwa ni kila mwamba ngoma huvutia upande wake, watu wanafaa kuishi kwa sababu yake mwenyewe tu, na kufanya kila awezalo kupata wadhifa mzuri kwa ajili ya chakula na mavayi mazuri. ‘Kila mwamba ngoma huvutia upande wake’—haya ndiyo maisha na falsafa ya mwanadamu, na pia inawakilisha asili ya binadamu. Maneno haya ya Shetani ni sumu ya Shetani hasa, na watu wanapopoiweka moyoni, inakuwa asili yao. Asili ya Shetani hufunuliwa kupitia maneno haya; yanamwakilisha yeye kabisa. Sumu hii inakuwa maisha ya watu pamoja na msingi wa kuwepo kwao; na wanadamu waliopotoshwa wametawaliwa kwa uthabiti na sumu hii kwa maelfu ya miaka(“Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niliposoma maneno ya Mungu, niliona kwamba sikuweza kabisa kujizuia kuishi kulingana na tabia zangu za kishetani, za ubinafsi na za kustahili dharau kwa sababu sumu za Shetani kama vile “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake” na “Mjinga akierevuka, mwerevu huwa mashakani.” zilikuwa tegemeo langu kuu. Nilikuwa nimezichukulia kama mambo ya kujenga, kama sheria za kufuata, nikifikiri kwamba hivyo ndivyo watu wanavyostahili kuishi na kwamba hiyo ilikuwa njia ya pekee ya kujikinga. Kama matokeo, nilizidi kuwa mbinafsi na mwenye kustahili dharau, nikijifikiria tu. Niliogopa kila wakati kwamba Ndugu Zhang atakuwa bora kunishinda katika wajibu tulioufanya pamoja, kwa hivyo kila tulipozungumza juu ya kazi, sikueleza mambo kwa dhati bali nilieleza kijuujuu bila kushiriki kila kitu nilichojua. Ndugu Zhang alipokabiliwa na matatizo katika wajibu wake na kunijia ili kutafuta, sikuonea wasiwasi kazi ya nyumba ya Mungu, bali nilionea wasiwasi kwamba kama ningemfundisha kila kitu, nisingepata tena nafasi ya kung’aa kanisani. Hata nilipojua vizuri kwamba haikuwa njia iliyofaa, bado sikutaka kumsaidia. Niliweza kuona kwamba sikuwa nikifanya wajibu wangu kutokana na kuzingatia mapenzi ya Mungu au kutetea kazi ya nyumba ya Mungu, bali kwamba nilikuwa nikifanya hivyo ili kufuatilia sifa na hadhi ya kibinafsi. Kwa kweli nilikuwa mbinafsi na mjanja sana. Kwa kutegemea tabia hizo za kishetani katika wajibu wangu, ningewezaje kupata mwongozo na baraka za Mungu? Nilidhani kwamba kwa kutomfundisha mtu mwingine yeyote yale niliyoyajua ningekuwa bora kanisani na kuheshimiwa na kila mtu, lakini kwa kweli ilitokea kwamba kadiri nilivyozidi kuficha mambo, ndivyo roho yangu ilivyozidi kuwa na giza na ndivyo nilivyozidi kutokuwa na mwongozo wa Mungu. Ilifika wakati ambapo sikuweza hata kufanya kile ambacho niliweza kufanya hapo awali. Maneno haya kutoka kwa Bwana Yesu yalinijia akilini: “Kwa kuwa yeyote aliye na kitu, yeye atapewa, na yeye atakuwa na mengi zaidi: lakini yule asiye na kitu, kitachukuliwa kutoka kwake hata kile alicho nacho(Mathayo 13:12). Kupitia hayo kulinifanya nithamini sana tabia ya Mungu yenye haki. Nilipofikira hayo zaidi, nilitambua kwamba kuweza kugundua matatizo kadhaa katika wajibu wangu kulikuwa tu mwongozo na nuru ya Mungu na bila mwongozo wa maneno ya Mungu, nilikuwa kipofu, asiyeweza kuelewa chochote na asiyeweza kutatua matatizo yoyote. Lakini sikujijua hata kidogo na bila aibu, nilichukulia nuru ya Roho Mtakatifu kama uwezo wangu mwenyewe. Je, sikuwa nikijaribu kumwibia Mungu utukufu Wake? Mungu anaweza kuona ndani ya mioyo na akili za watu. Nilijua kwamba kama ningeendelea kutekeleza wajibu wangu kwa kutegemea tabia hizo za kishetani, bila shaka ningedharauliwa na kuondolewa na Mungu. Baada ya kufikiria hayo nilikuja mbele za Mungu upesi kuomba, nikisema, “Mungu, sitakuwa tena mbinafsi sana wala mwenye kustahili dharau katika wajibu wangu. Nataka sana kufanya kazi vizuri pamoja na Ndugu Zhang na kufanya wajibu wangu vizuri.”

Baada ya hapo, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Usifanye mambo kwa ajili yako daima na usiyafikirie masilahi, hadhi na sifa yako mwenyewe kila wakati. Pia usiyafikirie masilahi ya mwanadamu. Lazima kwanza uyafikirie masilahi ya nyumba ya Mungu, na uyape kipaumbele. Unapaswa kuyafikiria mapenzi ya Mungu na uanze kwa kutafakari kama umekuwa mwenye najisi katika utimizaji wa wajibu wako au la, kama umefanya kila uwezalo kuwa mwaminifu, kama umefanya kila uwezalo kutimiza majukumu yako, na kufanya kadiri uwezavyo au la, na vile vile kama umefikiria wajibu wako na kazi ya nyumba ya Mungu kwa moyo wote au la. Lazima uyazingatie mambo haya. Yafikirie mara kwa mara, na itakuwa rahisi kwako kutekeleza wajibu wako(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Unapojidhihirisha kuwa mbinafsi na mtu wa aibu, na unapogundua haya, unapaswa kutafuta ukweli: Je, ninapaswa kufanya nini ili nilingane na mapenzi ya Mungu? Je, ninapaswa kutenda jinsi gani ili imfaidi kila mtu? Yaani, lazima uanze kwa kupuuza masilahi yako mwenyewe na kuyaacha polepole kulingana na kimo chako, kidogo kidogo. Baada ya kupitia haya mara chache, utakuwa umeyapuuza kabisa, na utakapokuwa ukifanya hivyo, utazidi kuwa thabiti. Kadiri utakavyozidi kuyapuuza masilahi yako, ndivyo utakavyozidi kuhisi kwamba kama binadamu, unapaswa kuwa na dhamiri na mantiki. Utahisi kwamba bila nia zenye ubinafsi, wewe ni mtu mwaminifu, mwadilifu na unafanya mambo ili kumridhisha Mungu tu. Utahisi kuwa tabia kama hii hukufanya ustahili kuitwa ‘mwanadamu,’ na kwamba katika kuishi duniani kwa njia hii, wewe ni mkweli na mwaminifu, wewe ni mtu halisi, una dhamiri safi, na unastahili mambo yote uliyopewa na Mungu. Kadiri utakavyozidi kuishi kwa njia hii, ndivyo utakavyozidi kuwa thabiti na mchangamfu. Kwa hivyo, je, hutakuwa umetembea kwenye njia ifaayo?(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma haya, nilielewa kwamba kama nilitaka kutekeleza wajibu wangu vizuri, kwanza ilibidi nifikirie jinsi ya kuitetea kazi ya nyumba ya Mungu, jinsi ya kutia juhudi zote katika wajibu wangu na jinsi ya kuufanya kwa uaminifu mkubwa zaidi. Mungu hulenga mtazamo wetu katika wajibu wetu. Matumaini Yake ni kwamba tumkabili kwa moyo wa dhati, kwamba tutie juhudi zetu zote katika kutekeleza wajibu wetu vizuri, na kwamba tuwe watu wenye dhamiri na ubinadamu. Mara nilipofahamu mapenzi Yake, nilimwomba Mungu ndani ya moyo wangu, nikimwambia kuwa nilikuwa tayari kuacha ubinafsi wangu na kuacha kuyafikiria masilahi yangu ya kibinafsi na kwamba nitafanya tu chochote ambacho kitalifaidi kanisa na maisha ya kina ndugu. Baada ya hapo, nilienda kuzungumza na Ndugu Zhang, nikimwambia juu ya tabia zangu za kishetani, za ubinafsi na za kustahili dharau na nia zangu za udanganyifu. Pia, tulitafuta pamoja ukweli juu ya matatizo na dosari zilizokuwa katika kazi yetu ili kuzitatua, na nilifanya ushirika juu ya kila kitu nilichojua bila kusita. Nilipotenda kwa njia hiyo, nilipata hisia ya amani. Nilihisi jinsi ilivyo vizuri kuwa mtu wa aina hiyo, kuwa mwaminifu na mkweli. Hali yangu ilianza kuboreka polepole na nilianza kuona matokeo kidogo katika wajibu wangu. Hata ingawa nyakati nyingine bado nilionyesha tabia zangu za kishetani za ubinafsi na za kustahili dharau, pindi nilipofikiria jinsi ambavyo hayo yalimchukiza Mungu, nilikuja mbele za Mungu kuomba, nikayaacha mawazo yangu yasiyo sahihi, na kutamani kutenda kulingana na maneno Yake.

Baada ya kupitia tukio la aina hiyo, nilihisi kwa kweli kwamba kufanya wajibu wetu kwa kutegemea tabia za kishetani na sumu za Shetani kunaweza tu kutufanya tuzidi kuwa wabinafsi, wenye kustahili dharau, na wenye kujitafutia makuu. Tutapoteza ufanani wote wa binadamu, na mbali na kujisababishia maumivu, pia hatutaweza kufanya kazi na wengine vizuri. Aidha, kufanya hivyo huharibu tu kazi ya nyumba ya Mungu. Nilipotenda ukweli kama mtu mwaminifu kulingana na maneno ya Mungu, na sikupanga tena njama kwa ajili ya maslahi yangu mwenyewe, nilikuwa na nuru na mwongozo wa Roho Mtakatifu katika wajibu wangu, na nilihisi Amani ya rohoni. Shukrani kwa Mungu! Ni hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu ambavyo vilinipa ufahamu kidogo kuhusu tabia zangu za kishetani za ubinafsi na udanganyifu, na mwishowe niliweza kutenda ukweli kidogo na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu.

Iliyotangulia: 40. Tiba ya Wivu

Inayofuata: 44. Mwishowe, Naona Ukweli Kujihusu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

2. Katikati ya Jaribu la Kifo

Na Xingdao, Korea ya KusiniMwenyezi Mungu anasema, “Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp