61. Ukweli Umenionyesha Njia

Na Shizai, Japani

Mwenyezi Mungu anasema, “Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe kumhudumia Mungu. Kama tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa na neno la Mungu, basi tabia yako bado inamwakilisha Shetani. Hii inatosha kuthibitisha kwamba huduma yako kwa Mungu ni kutokana na nia yako nzuri wewe binafsi. Ni huduma inayotokana na asili yako ya kishetani. Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya binadamu ya kuishi katika dunia. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hakika watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo na wapinga Kristo watakaowadanganya watu katika siku za mwisho. Makristo wa uwongo na wapinga Kristo waliozungumziwa watainuka kutoka miongoni mwa watu kama hawa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku). Kusoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu kunanikumbusha tukio nililopitia miaka mitano ya nyuma.

Nilikuwa tu nimechaguliwa kama kiongozi wa kanisa. Kwa kweli nilikuwa na shauku na nilichukulia wajibu wangu kwa uzito. Nilikuwa nimeazimia kuishughulikia kazi ya kanisa vizuri. Nilipoanza kufanya tathmini ya kazi ya timu zote, niligundua kuwa baadhi ya washirika hawakustahili kufanya kazi hiyo, na viongozi wa timu hawakuwa wakirekebisha hili. Baadhi hawakuwa na ufahamu wa kanuni na viongozi wao hawakuwa wakitoa ushirika na msaada haraka vya kutosha, ambayo iliathiri kazi a kanisa. Hili kwa kweli lilinisikitisha, na niliwaza, “Shida za wazi kama hizi zinaachwa bila kusuluhishwa. Kwa dhahiri hawawajibiki katika kazi zao. Kwa kweli lazima niwakaripie kwenye mkutano ujao na nihakikishe kabisa wanajua pale wanapokosea” Katika mkutano uliofuata, niliwauliza kwa kurudia viongozi hao wa timu hizo kuhusu kazi zao na nilielezea makosa na masuala ambayo nilikuwa nimeyaona. Hata ingawa walijua hawakuwa wakifanya kazi ya utendaji na walikuwa tayari kubadilika, Bado sikuridhika. Niliwaza kwamba nisingekuwa mkali, hakika kuichambua na kuwashughulikia, hakuna lolote litakalotokea. Kwa sauti ya kukemea, nilisema walikuwa wa purukushani katika wajibu wao na hawakuweza kutatua shida zao za utendaji, hii ilikuwa inavuruga kazi ya kanisa, na kadhalika. Baada ya kumaliza, sikuwauliza jinsi walivyohisi, lakini nilijisifu tu, nikifikiri kuwa nilikuwa nimepata shida na kuzisuluhisha. Lakini siku chache baadaye, mfanyakazi mwenzangu aliniambia, “Kiongozi wa timu alisema anaogopa kukuona, kwamba anafikiria utamshughulikia ikiwa utaona masuala katika kazi yake.” Kusikia hili kulinikasirisha kidogo, lakini niliwaza mara moja kuwa nilikuwa nimefanya tu kile kilichohitajika, kwamba ilikuwa kugundua shida na kisha kuzitatua, na kuwashughulikia ilikuwa ili kwamba waweze kupata funzo. Sikuona kama lilikuwa jambo kubwa. Katika mkutano uliofuata pamoja na viongozi wa timu, niliendelea kuuliza kwa ukali kuhusu kazi zao, kisha nikawashughulikia na kuchambua mambo nilipogundua suala. Pia nilisema kwa kujiamini, “Baadhi ya kina ndugu wanaogopa kuulizwa juu ya kazi zao. Kuna nini cha kuogopa iwapo unafanya kazi ya utendaji? Ni kwa kujifunza juu ya kazi yako tu ndiyo shida zinaweza kupatikana na kusahihishwa kwa wakati” Baada ya mkutano niliskia kiongozi wa timu akisema, “Bado ninajifunza jinsi ya kufanya wajibu wangu na nina ugumu mwingi. Nilitaka yasuluhishwe kupitia ushirika katika mkutano wetu lakini badala yake, nina mfadhaiko tu.” Kusikia hili kulinikasirisha kidogo na nilihisi kwamba lilikuwa kosa langu kwamba mkutano haukuzaa matunda. Lakini nilidhani labda ilikuwa kwa sababu ya kimo changu kidogo, kwamba ushirika wangu haukuwa wazi, na ilikuwa kawaida kwa kiongozi mpya wa timu kuhisi shinikizo nyingi. Nilifoka tu, “Msongo ni wa kutia moyo. Haingekuwa sawa ikiwa hungehisi vile.” Mfanyakazi mwenzangu baadaye aligundua kuwa viongozi wa timu waliogopa kuniona na kushughulikiwa na mimi na kuonywa, “Kuwashughulikia watu kwa njia ile kunafanywa kutokana na hasira. Sio kwa kuadilisha kwa kina ndugu. Tunapaswa kushiriki ukweli zaidi ili kusuluhisha masuala na shida zao.” Bado sikufikiria chochote kuhusu hilo, nikiamini kwamba nia zangu zilikuwa sahihi na kwamba hata kama nilikuwa mkali kiasi, nilikuwa nikiwajibikia kazi yangu. Kwa hivyo licha ya maonyo yanayorudiwa kutoka kwa wafanyikazi wenzangu, Sikuwahi kuja mbele za Mungu kujitafakari. Polepole nilikuja kuhisi giza likikua ndani ya roho yangu, na singeweza kutambua kazi ya Roho Mtakatifu. Nilikuwa nikiteseka na mwenye maumivu. Ni hapo tu ndipo nilikuja mbele za Mungu na kujitafakari: “Kwa nini sijafanikisha kitu chochote katika wajibu wangu, lakini nilikuwa nikigonga mwamba kila wakati? Kwa nini ndugu daima husema wamezuiwa na mimi? Je, ni kweli vile kwamba wafanyikazi wenzangu wanavyosema, kwamba mimi huwashughulikia watu kutokana na hasira? Lakini, mimi husema vitu kwa ukali ili kazi ya kanisa ifanyike vizuri. Nisingefanya hivyo, je, kina ndugu wangegundua jinsi masuala haya ni mazito kweli?” Hata kupitia katika mateso haya, nilikuwa najaribu kujihalalisha. Nilikuwa nikiteseka sana.

Baada ya kuomba, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Kama viongozi na wafanyakazi kanisani, ikiwa mnataka kuwaongoza watu wateule wa Mungu kuingia katika uhalisi wa ukweli na watumikie kama mashahidi wa Mungu, la muhimu zaidi, lazima uwe na ufahamu wa kina wa lengo la Mungu katika kuwaokoa watu na kusudi la kazi Yake. Lazima uyaelewe mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake mbalimbali ya watu. Unapaswa kuwa mwenye utendaji katika juhudi zenu; tenda tu kiasi unachoelewa na kuwasiliana tu kuhusu kile unachokijua. Usijisifu, usitie chumvi, na usiseme maneno yasiyopaswa. Ukitia chumvi, watu watakuchukia na utahisi mwenye kushutumiwa baadaye; hili ni jambo lisilofaa kabisa. Unapotoa ukweli kwa wengine, si lazima uwashughulikie na kuwakaripia ili wao waweze kuupata ukweli. Ikiwa wewe mwenyewe huna ukweli, na unawashughulikia na kuwakaripia wengine tu, watakuogopa, lakini hiyo haimaanishi kuwa wanauelewa ukweli. Katika kazi fulani za utawala, ni vizuri kwako kuwashughulikia na kuwapogoa wengine na kuwaadhibu kwa kiwango fulani. Lakini ikiwa huwezi kuutoa ukweli na unajua tu jinsi ya kuwa mwenye kuwalazimisha na kuwakaripia wengine, upotovu na uovu wako utafunuliwa. Muda unavyopita, kama vile watu hawawezi kupata ruzuku ya uzima au mambo ya utendaji kutoka kwako, watakuja kukuchukia na kuhisi karaha kwako. Wale ambao hawana utambuzi watajifunza mambo mabaya kutoka kwako; watajifunza kushughulikia na kuwapogoa wengine, kuwa na hasira, na kukasirika. Je, hiyo si sawa na kuwaelekeza wengine kwenye njia ya Paulo, kwenye njia ya kuelekea kuangamia kabisa? Je, huo sio utenda uovu? Kazi yako inapaswa kulenga kuwasiliana ukweli na kutoa maisha kwa wengine. Ikiwa yote unayofanya ni kuwashughulikia na kuwahubiria wengine bila kufikiri, watawezaje kuuelewa ukweli daima? Wakati unapoendelea, watu watakuona jinsi wewe ulivyo kwa kweli, nao watakuacha. Unawezaje kutarajia kuwaleta wengine mbele ya Mungu kwa njia hii? Huku kunakuwaje kufanya kazi? Utampoteza kila mtu ukiendelea kufanya kazi kwa njia hii. Je, unatumaini kutimiza kazi gani hata hivyo? Viongozi wengine hawawezi kuwasilisha ukweli ili kutatua matatizo. Badala yake, wao huwashughulika wengine tu bila kufikiri na kuonyesha mamlaka yao ili wengine wapate kuwaogopa na kuwatii—watu kama hao ni wa aina ya viongozi wa uwongo na wapinga Kristo. Wale ambao tabia yao haijabadilika hawawezi kutekeleza kazi ya kanisa, na hawawezi kumtumikia Mungu(“Ni Wale wenye Uhalisi wa Ukweli Pekee Ndio Wanaoweza Kuongoza” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalifunua kabisa hali yangu mwenyewe. Hivyo ndivyo nilivyokuwa nikifanya wajibu wangu hasa. Badala ya kuzingatia ushirika juu ya ukweli ili kutatua shida, Nilikuwa mwenye hasira, nikiwashughulikia, kuwakemea, na kuwakaripia wengine. Kwa sababu hiyo, walilazimishwa, waliniogopa, na waliniepuka. Pia nilimchukiza Mungu kwa sababu nilikuwa nikiishi katika tabia yangu potovu. Nilikuwa nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na nikazama kwenye giza. Nikikumbuka wakati huo, wakati nilipata shida katika wajibu wa kina ndugu, nilitafuta ukweli kwa nadra sana au kupata maneno ya Mungu kwa ajili ya ushirika maalum, na kwa kweli sikuwaelekeza kwenye njia ya kutenda. Nilikuwa nikiwakemea na kuwakaripia na tabia yangu ya ujeuri. Nilipoona kwamba walihisi nimewazuia, bado sikujitafakari. Nilifikiri nilikuwa nikiwajibika katika kazi yangu, kwamba nilikuwa mwenye kujali mapenzi ya Mungu na kusuluhisha shida za kiutendaji. Mungu alinitahadharisha kupitia kwa wafanyakazi wenzangu nisiwashughulikie watu kidikteta kutokana na hasira lakini nilipuuza hilo. Kama matokeo, baadhi ya ndugu waligeuka kuwa hasi. Waliniogopa na kuniepuka. Pia, kazi ya kanisa haikuwa ikiendelea vizuri, Ni wazi kwamba Mungu anahitaji viongozi na wafanyakazi wafanye kazi yao kimsingi kupitia katika ushirika na ukweli. Ndugu wanafaa kufahamu ukweli kabla waweze kugundua tabia zao potovu na ukweli wa upotovu wao, na hapo tu ndipo wanaelekezwa kutenda maneno ya Mungu na kufanya wajibu wao vizuri. Lakini bado nilifikiri nilifaa niwe mkali katika kazi yangu, kwamba wakati nilipogundua masuala nilifaa kulazimika kuwakemea na kuwakaripia, na hiyo ingekuwa tu njia ya pekee kwao kuona shida zao na kuzirekebisha. Nilifikiri hiyo ndiyo ilikuwa njia ya pekee ya kupata matokeo. Niliona basi jinsi mtazamo ule ulivyokuwa wa kipumbavu kweli! Kwa kufanya kazi vile, nilikuwa nikiichukulia faida nafasi yangu na kuwakemea na kuwazuia watu kwa kiburi. Sikuwa nikisuluhisha shida za wengine kupitia katika ushirika juu ya ukweli. Mungu anahitaji kwamba viongozi watumie ushirika juu ya ukweli kusuluhisha shida za kina ndugu, kwamba wawe kwenye kiwango sawa na kila mtu, kwamba washiriki juu ya maneno ya Mungu kulingana na ugumu halisi wa watu, na kufanya ushirika juu ya uzoefu wao na ufahamu ili kuwaelekeza na kuwasaidia wengine. Wakimshughulikia au kumfunua mtu, lazima iwe ni juu ya msingi wa ushirika juu ya ukweli, kuonyesha kiini na vidokezo muhimu vya shida ili watu waelewe kile ambacho Mungu anahitaji, ili waweze kuona kwa uwazi shida zao, asili ya shida zao, athari hatari za shida zao, na ili waweze kujua kitu cha kufanya ili kulingana na ukweli na jinsi ya kufanya wajibu wao kama vile Mungu anavyohitaji. Lakini sikuwa nimefanya wajibu wangu kama vile Mungu alivyotaka. Sikusikiliza kumbusho za wafanyakazi wenzangu, sembuse kutafakari juu ya asili na athari mimi kuwakaripia watu kulingana na tabia yangu ya kishetani katika wajibu wangu. Nilijidhibitishia, nikisema kuwa ilikuwa kwa manufaa yao wenyewe, na kwa ajili ya kazi ya kanisa. Sikuwa kwenye njia sahihi katika wajibu wangu, na siyo tu kwamba sikuwa nikiwanufaisha wengine hata kidogo, lakini kwa kweli nilikuwa nikiwalazimisha, wote walikuwa wenye taabu na walizuiwa. Je, sikuwa nikiwadhuru? Nilikuwa nikifanya uovu! Sikuwahi kufikiria kwamba kufanya wajibu wangu kwa msingi wa tabia yangu ya kishetani kungekuwa na athari kubwa kama hizi. Kwa kweli nilijuta kuwashughulikia na kuwakemea kwa njia hiyo. Nilikuja haraka mbele za Mungu katika maombi na kutafuta, na nikawaza: Ni nini hasa kilinifanya nifanye uovu bila hata kujua?

Baada ya hapo, nilisoma haya katika maneno ya Mungu: “Kama kwa kweli una ukweli ndani yako, njia unayotembea kiasili itakuwa njia sahihi. Bila ukweli, ni rahisi kufanya uovu na hutakuwa na budi kuufanya. Kwa mfano, kama kiburi na majivuno, vingekuwa ndani yako, ungeona kwamba haiwezekani kuepuka kumwasi Mungu; ungehisi kulazimishwa kumwasi. Hutafanya hivyo kimakusudi; utafanya hivyo chini ya utawala wa asili yako ya kiburi na majivuno. Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu na kumwona kuwa asiye na maana; vitakufanya ujiinue, vitakufanya kujiweka kila wakati kwenye maonyesho, na mwishowe vitakufanya ukae katika nafasi ya Mungu na kujitolea ushuhuda mwenyewe. Mwishowe utayabadilisha mawazo yako mwenyewe, fikira zako mwenyewe na dhana zako yawe ukweli wa kuabudiwa. Tazama ni kiasi gani cha uovu kinafanywa na watu chini ya utawala wa asili yao ya kiburi na majivuno!(“Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalifichua matendo yangu maovu: Nilikuwa nikidhibitiwa na asili yangu ya kiburi na majivuno. Kwa sababu ya asili ya kiburi na majivuno, nilidhani siku zote kwamba nilikuwa mwaminifu zaidi kuwashinda wengine, kwa hivyo niliwatawala kimwinyi. Wakati ambapo kulikuwa na makosa au hitilafu katika kazi ya kina ndugu, niliwadharau na nilitumia cheo changu kuwakaripia na kuwashughulikia. Sikuelewa hisia za wengine au kuwa na huruma. Kwa sababu ya kudhibitiwa na asili hii ya kiburi, pia nilijiamini kabisa, nikifikiri kwamba njia ya pekee ya kusuluhisha matatizo ilikuwa kuwashughulikia watu vikali. Niliwasilisha fikira na mawazo yangu mwenyewe kama kwamba yalikuwa ukweli. Hata nilipoona kwamba namna nilivyofanya kazi iliwazuia wengine, bado sikubadilika na sikutaka kuwasikiliza kina ndugu. Hata wafanyakazi wenzangu waliponionya, bado sikutafakari juu yangu mwenyewe. Nilidhani nilikuwa tu nimetumia sauti ya ukali, na hawakuweza kuvumilia kushughulikiwa. Nilikuwa nikifanya wajibu wangu kulingana na tabia yangu ya majivuno na ya kishetani, nikiwadhuru kina ndugu na kuchelewesha kazi ya kanisa. Yote niliyokuwa nimefanya yalikuwa uovu wa kumpinga Mungu!

Baadaye nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya binadamu ya kuishi katika dunia. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hakika watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo na wapinga Kristo watakaowadanganya watu katika siku za mwisho. Makristo wa uwongo na wapinga Kristo waliozungumziwa watainuka kutoka miongoni mwa watu kama hawa. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi wamo katika hatari ya kutupwa nje wakati wowote. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kuwasomea na kuwadhibiti, kujiinua wao wenyewe—na wale katu hawatubu, katu hawakiri dhambi zao, katu hawakatai manufaa ya cheo—watu hawa wataanguka mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno ya vyeo vyao na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku). Nilihuzunika niliposoma maneno haya, na niliweza kuhisi kwamba tabia ya Mungu haivumilii kosa lolote. Niliona kwamba katika miaka yangu ya imani, sikuwa nimelenga kutafuta kanuni za ukweli, bali nilikuwa nikifanya tu wajibu wangu jinsi nilivyotaka. Tabia yangu ya kiburi haikudhibitika, na niliwakaripia na kuwazuia watu kutokana na cheo changu cha kazi na niliishia kuwazuia ndugu zangu. Walikuwa wamezuia na walikuwa na maumivu. Sikuwa na ubinadamu kabisa. Mbali na kushindwa kusuluhisha matatizo ya kiutendaji ya kina ndugu, pia nilikuwa nimezuia kuingia kwao katika uzima na kuchelewesha kazi ya kanisa. Huko kulikuwaje kufanya wajibu wangu? Je, sikuwa nikitenda kama mtumishi wa Shetani? Nilikuwa nikifikiri daima kwamba nia zangu zilikuwa mwafaka, kwamba nilijali kazi ya kanisa, lakini hata hivyo, niliona kwamba kuwa na shauku kidogo na kujua mafundisho kidogo hakukutosha kumridhisha Mungu kwa wajibu wangu. Bila kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, tabia yangu ya kishetani isingebadilika, na kisha wajibu wangu usingekubaliana na mapenzi ya Mungu. Ningetenda tu uovu na kumpinga Mungu bila kutaka. Niliwakumbuka viongozi wa uwongo na wapinga Kristo ambao walikuwa wameondolewa. Hawakukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu au kutenda ukweli, bali walifanya wajibu wao kwa tabia zao za kishetani, huku wakiwa wenye kiburi, majivuno na maringo sana, na wakiwashughulikia na kuwakaripia watu, wakijiona kuwa wa juu zaidi na wakiwa wakatili. Athari yao kwa wengine ilikuwa tu ya kudhuru, na hawakufanya lingine ila kuharibu na kuvuruga kazi ya kanisa. Kazi yao ilikuwa tu kufanya uovu na kumpinga Mungu! Ni kama Bwana Yesu alivyosema: “Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina lako? Na kutoa mapepo kupitia jina lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina lako? Na hapo ndipo nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu(Mathayo 7:22-23). Hii iliniacha nikihisi hofu kidogo. Iwapo ningeendelea kufanya wajibu wangu nikitegemea tabia yangu ya kishetani, basi ningekatiza tu kazi ya kanisa na ningelaaniwa na kuondolewa na Mungu, kama tu wale waovu wengine ambao walimpinga Mungu. Kisha nikagundua kwamba kutokuwa na mafanikio katika maisha ya kanisa na wajibu wangu kulikuwa Mungu kunifunua na kwamba nilipaswa kuja mbele za Mungu kutafakari juu yangu mwenyewe na kutubu Kwake. Nilipofikiria juu ya asili ya kiburi ambayo nilikuwa nayo, kamwe nisingetii bila hukumu na mfichuo wa maneno ya Mungu na yale ambayo ukweli ulifunua. Kamwe nisingeona athari za hatari za kufanya wajibu wangu kulingana na tabia yangu ya kishetani. Niliguswa sana wakati huo huo na nilihisi kwamba sikupaswa kuendelea hivyo. Sikuwa na budi kutafuta ukweli ili kutatua upotovu wangu.

Kisha nilisoma haya katika maneno ya Mungu: “Wakati jambo linakukumba, ni lazima kuwa mtulivu, na mtazamo unaofaa, na ni lazima kufanya chaguo. Unapaswa kujifunza kuutumia ukweli kutatua jambo lile.Katika wati wa kawaida, kuna maana gani ya wewe kuelewa ukweli fulani? Haiko hapo tu ili kujaza tumbo lako, na sio tu hapo kukupa kitu cha kusema, wala hauko hapo kwa ajili ya kutatua shida za wengine. Lililo muhimu zaidi, matumizi yake ni kutatua matatizo yako mwenyewe, shida zako mwenyewe—ni baada tu ya kutatua shida zako binafsi ndipo utaweza kutatua shida za wengine(“Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Lazima uwe na ufahamu wa watu ambao huwa na ushirika nao na ushirika kuhusu masuala ya kiroho katika maisha, ni hapo tu unapoweza kuruzuku maisha kwa wengine na kufidia mapungufu yao. Hupaswi kuchukua sauti ya kuhubiri nao, ambao kimsingi ni msimamo mbaya kuwa nao. Katika ushirika ni lazima uwe na ufahamu wa mambo ya kiroho. Lazima uwe na hekima na kuwa na uwezo wa kuelewa ni nini kilicho katika mioyo ya watu wengine. Lazima uwe mtu mwafaka kama utawatumikia wengine na lazima ufanye ushirika na kile ulicho nacho(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 13). Kupitia maneno ya Mungu nilielewa kwamba ili kusuluhisha matatizo ya watu wengine, sharti tutende na tuingie katika maneno ya Mungu kwanza. Lazima tutafute ukweli na tutatue upotovu wetu wenyewe. Hilo ndilo jambo la muhimu zaidi. Ni muhimu kuwa na utambuzi juu ya tabia yetu potovu, ili mtu mwingine atakapoonyesha upotovu wa aina hiyo, tutajua jinsi ya kumsaidia, jinsi ya kufanya ushirika juu ya uzoefu wetu na ufahamu wetu wenyewe ili kumwonyesha njia ya utendaji. Tutaweza pia kuwakabili wengine kwa usahihi na kuona kwamba tuna upotovu ule ule tunaouona kwa wengine na kwamba ni sawa kabisa. Kweli kabisa. Kisha hatutafikiri kwamba sisi ni bora kuwazidi wengine, bali tutaweza kufanya ushirika kwa usawa. Hiyo pekee ndiyo njia ya kufanya ushirika utakaowanufaisha wengine. Lakini nilikuwa nikifanya nini badala yake? Sikuwa nikizingatia kuingia kwangu au kutafakari matatizo yangu katika wajibu wangu. Badala yake, nilikuwa nikifanya kazi tu kwa ajili ya kufanya kazi, kana kwamba sikuwa na upotovu. Nilijishughulisha na kutatua matatizo ya watu wengine, na wakati ambapo ushirika wangu haukusaidia, niliwakemea kwa kuwadhalilisha. Sikuwa nikiishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu. Nilikuwa kama pepo. Nilimchukiza na kumtia Mungu kinyongo na niliwachukiza watu wengine. Ukweli ni kwamba ndugu wale walitaka kutekeleza wajibu wao vizuri, lakini hawakujua jinsi ya kufanya hivyo kwa sababu hawakuelewa kanuni kikamilifu. Kunapokuwa na makosa au hitilafu katika kazi, tunapaswa kuwa wenye kuelewa na kusamehe, tunapaswa kuongoza na kusaidia kwa njia chanya zaidi, ili tuweze kutafuta ukweli na kusuluhisha mambo pamoja. Tunapaswa tu kuwakaripia na kuwaonya watu ambao ni wazembe kwa makusudi katika wajibu wao, lakini hiyo haifai kuwa kawaida. Moyo wangu ulichangamka baada ya kuelewa haya na nilijua jinsi nilivyopaswa kufanya wajibu wangu kuanzia wakati huo.

Muda mfupi baadaye, nilisikia kwamba kulikuwa na kiongozi wa timu ambaye alikuwa na ubora mzuri wa tabia na mwenye ufahamu safi juu ya ukweli, ambaye aliweza kutatua matatizo ya kiutendaji kwa njia ya ushirika juu ya ukweli, lakini alikuwa akihisi dhaifu, na alijiondoa wakati wa matatizo na dhiki. Nilikuwa na wahaka tena pindi niliposikia juu ya haya, nikifikiria kwamba hakuwa akichukua wajibu wake kwa makini, na ilibidi nimshughulikie vikali. Niligundua ghafla kwamba nilikuwa nikitenda kulingana na tabia yangu ya kiburi tena bila kufikiria. Nilimwomba Mungu upesi na nikaazimia kutenda kulingana na maneno Yake wakati huu. Nilimtafuta kiongozi huyo wa timu baadaye na nilizungumza naye kwa dhati ili niweze kuelewa hali yake na matatizo yake. Nilitafuta maneno husika kutoka kwa Mungu na nilitumia uzoefu wangu wa kibinafsi katika ushirika wangu. Aligundua kwamba hakuwa mwaminifu katika agizo la Mungu, na alitaka kubadilika. Niliguswa sana nilipomwona dada yangu akiweza kutafakari juu yake mwenyewe na kuwa tayari kubadilika. Nilikuja kutambua vyema kwamba kiongozi wa kanisa lazima azingatie ushirika juu ya ukweli ili awaadilishe wengine kwa kweli. Hiyo ndiyo njia ya pekee ya kuyanufaisha maisha ya watu.

Iliyotangulia: 57. Kuripoti Au Kutoripoti

Inayofuata: 62. Kuinuka licha ya kushindwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

62. Kuinuka licha ya kushindwa

Na Fenqi, Korea ya KusiniKabla ya kumwamini Mungu, nilifundishwa na CCP, na sikufikiria chochote ila jinsi ya kufaulu kutokana na juhudi...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp