Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda wa Uzoefu Mbele ya Kiti cha Hukumu cha Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

72. Nilijifunza Jinsi ya Kuwatendea Watu Wengine Inavyostahili

Na Siyuan, Ufaransa

Siku moja, Ndugu Chen kutoka katika kanisa letu alinijia. Alisema alitaka kufanya mazoezi ya kutoa ushuhuda katika muda wake wa ziada na kutoa uwezo wake kiasi kwa ajili ya kazi ya injili. Kwa sababu ya uhusiano wangu wa zamani na Ndugu Chen, nilijua kwamba alikuwa na tabia ya kiburi sana, na kwa hivyo nilikuwa na mawazo na na maoni juu yake kabla ya kujua. Zaidi ya hayo, nilidhani kwamba wale ambao wanatoa ushuhuda lazima wawe na kiwango fulani cha ufahamu wa Bibilia. Lazima waweze kuwasilisha ukweli waziwazi na kuweza kujibu maswali yaliyoulizwa na wale tunaowahubiria injili. Nilihisi kuwa hakuwa na sifa hizi, na kwa hivyo sikukubaliana na hilo. Alipoona haya, alisema, “Kulingana na uwezo wangu, hufikiri kwamba naweza kujizoeza kutoa ushuhuda? Sitakuwa napoteza talanta yangu nisipotoa ushuhuda?” Wakati niliposikia haya, nilihisi mwenye kukerwa sana na nikawaza,” Je, unafikiri kwamba kutoa ushuhuda ni jambo rahisi kufanya? Kama huna talanta halisi, unafikiri kuwa unaweza kutimiza wajibu huu vema? Unajiona kuwa mtu wa maana sana. Huna kipimo sahihi kujihusu!” Baadaye, nilishiriki juu ya hali ya Ndugu Chen pamoja na ndugu wengine wachache ili tuweze kuwa na utambuzi kuhusu hali yake. Baada ya baadhi ya ndugu wengine kusikia kile nilichokuwa nikisema, pia walisema jinsi Ndugu Chen alivyoonyesha kiburi katika tabia zake. Hii ilinithibitishia kwamba maoni niliyokuwa nayo kumhusu Ndugu Chen yalikuwa sahihi hasa. Sikujua kamwe kuwa, wakati nilipotoa maoni juu ya Ndugu Chen kwa kawaida bila kutafuta ukweli kumwelewa kwa usahihi, kimsingi nilikuwa ninamhukumu na kula njama pamoja na wengine.

Wakati mmoja, nilikuwa nahudhuria mkutano na Ndugu Chen. Tulipokuwa tukisoma mpangilio wa kazi kuhusu jinsi ambavyo tungeweza kutazama filamu za familia ya Mungu huku tukiishi maisha ya kanisa, alisema, “Nadhani kwamba viongozi na washirika hawana uhalisi wa ukweli. Wanahubiri nyaraka na mafundisho tu katika mikutano na hawawezi kutatua matatizo ya kiutendaji ambayo ndugu zetu wanakabiliwa nayo. Ni vizuri sana kwamba tunaweza kutazama filamu kwenye mikutano yetu sasa. Hii itatusaidia kuuelewa ukweli.” Aliendelea kusema, “Wakati nilipokuwa nikitimiza wajibu huu mwanzoni, kwa sababu sikuzielewa kanuni, nilikuwa na matatizo mengi. Hata hivyo, sasa kwa kuwa nina ufahamu wa kanuni hizo, nahisi kuwa kutimiza wajibu huu kunaenda vizuri zaidi, na matokeo ninayoyapata katika kazi yangu ni mazuri hasa.….” Wakati nilipomsikia akisema hivi, chuki kubwa na upinzani viliibuka katika moyo wangu. Nilifikiria, “Wewe ni mzuri sana katika kuchukua fursa hiyo. Unatumia ushirika wa mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu kutudharau sisi viongozi na wafanyikazi wenzako. Wakati huo huo, hujasahau kujishuhudia na kujidai. Wewe ni mwenye kiburi sana na asiye na busara kweli.….” Kisha, tukaanza kujadili jinsi tutakavyofanya kazi pamoja kuhusu maswali matano ya kuwasilishwa kwenye mkutano uliofuata. Wakati huu, Ndugu Chen alijitolea kuwa msimamizi wa maswali matatu na hata alipendekeza watu watakaowajibikia maswali mawili yaliyobaki. Wakati nilipompangia kiongozi wa kikundi atakayesimamia mkutano uliofuata, alimuuliza haraka kiongozi wa kikundi kwa namna ya shaka, “Je, unafikiri kuwa unaweza kuushughulikia? Unaweza kufanya hivyo?” Kutoka kwa toni ya sauti yake, ilionekana kana kwamba alifikiria kwamba ni yeye tu ndiye angeweza kuusimamia mkutano. Nikiwa nimekabiliwa na tabia yake, nilifikiria, “Wewe huna busara kabisa. Je, unaweza kufanya hivi? Unataka tu kutumia fursa hii kama jukwaa la kujionyesha kwa ndugu. Unataka kuvuta macho yote, lakini sitaruhusu jambo hili.” Ili kumzuia kufikia lengo lake, nilitumia mamlaka yangu kuipanga tena ili asiwe msimamizi. Huku nikifikiri kuhusu tabia zote za Ndugu Chen, nilimchukia sana moyoni mwangu na chuki yangu isiyo na sababu kwake ikazidi kuwa yenye nguvu. Hasa, nilikuwa nimewasiliana naye mara kadhaa kuhusu tabia yake ya majivuno, lakini yeye alikubali tu kwa maneno na baadaye sikuona mabadiliko yoyote ya wazi. Kwa hivyo nilihisi kuwa alikuwa na kiwango cha ajabu cha majivuno. Alikuwa na kiburi kupita kiasi kufikia kiwango kwamba nilihisi hangeweza kubadilika na na hakukuwa na matumaini kabisa. Na wakati mwingine hata nilifikiri kwamba kwa kuwa alikuwa mwenye kiburi sana, kimsingi hakufaa kwa ajili ya kutekeleza wajibu wake wa sasa. Ningembadilisha tu na mtu mwingine.

Baada ya mkutano kumalizika na nikatafakari juu ya kila moja ya mawazo na maoni ambayo nilikuwa nimeyafichua wakati wa mkutano, moyo wangu ulihisi fedheha fulani na kukosa utulivu. Nilimwomba Mungu, “Ee Mungu! Nina mawazo mengi na chuki nyingi isiyo na sababu kwa Ndugu Chen. Nadhani yeye ni mwenye kiburi sana. Sasa, kila ninapomsikia akizungumza, chuki kubwa na upinzani huibuka moyoni mwangu. Hata nataka kumbadilisha. Ee Mungu! Najua kuwa niko katika hali mbaya. Hata hivyo, sielewi mapenzi Yako na sijui ni kipengele kipi cha ukweli ninachopaswa kuingia. Ee Mungu, tafadhali nipe nuru na uniongoze.” Baada ya kumaliza kuomba, nilifikiria kuhusu kifungu kutoka kwa mahubiri: “Je, mawazo ya aina hii yapo mioyoni mwenu? Unapofikiria kumhusu mtu fulani, kwanza unafikiria kuhusu udhaifu wake, na unafikiria kwanza kuhusu namna ambavyo amepotoka. Hiyo ni kweli? Ikiwa utaendelea kufikiria hivi, hutaweza kushirikiana na wengine kwa kawaida. … Lakini kwa sababu anamwamini Mungu kwa dhati na anatamani kuufuatilia ukweli, kwa hivyo haitachukua muda mrefu, kabla ya upotovu huu ulio ndani yake kuanza kubadilika na kutoweka. Hivi ndivyo tunavyopaswa kuliona suala hili, na lazima tuyaone maswala kwa maono ya ukuaji. Hatupaswi kuukazia udhaifu wa mtu, kisha tumshutumu milele, tukisema kwamba mtu huyo atakuwa hivi maisha yake yote, kwamba yeye ni mtu wa aina hii. Kufanya hivi kutakuwa kumhukumu na kumwekea mipaka! Katika kuwaokoa watu, Mungu hajazungumza kwa namna hii, Akisema kwamba binadamu amepotoka kwa kiwango hiki, na kwa hivyo hakuna maana ya kumwokoa, na kwamba huu ndio mwisho wa binadamu. Mungu halioni hivyo hata kidogo. Hivyo, sote tunaufuatilia ukweli sasa. Sote tunatamani kuufuatilia ukweli, na tunaamini kwamba, kwa kiwango cha chini zaidi, tukiendelea na ufuatiliaji wetu, basi baada ya miaka michache hakika tutaweza kubadilika kwa namna fulani, na hatimaye tutaweza kufikia mabadiliko ya tabia kabisa na kukamilishwa na Mungu. Nyote mna imani ya aina hii, sivyo? Kwa kuwa mna imani ya aina hii, kwa hivyo mnapaswa kuamini kuwa watu wengine pia wanayo imani ya aina hii” (“Jinsi ya Kuweka Uhusiano wa Kawaida Kati ya Watu Wawili” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha I). Kifungu hiki cha ushirika kilinionyesha wazi hali yangu na niliona aibu. Niliona jinsi asili yangu ilivyokuwa yenye kiburi na madharau. Nilitenda kama kwamba nilikuwa na ukweli na niliweza kumhukumu mtu kwa usahihi kwa mtazamo mmoja tu na kuelewa kiini chake kabisa. Kwa kuyahusisha maneno katika mahubiri hayo na mimi mwenyewe, niligundua: Kutokana na uhusiano wangu na Ndugu Chen, nilihisi kwamba alikuwa mchanga na mwenye kujivuna nilipomwona akionyesha tabia yake yenye kiburi katika maneno aliyokuwa akisema na mambo aliyokuwa akifanya. Nilihisi kuwa bila shaka hakuwa na ujuzi wa kibinafsi. Hata nilifanya uamuzi moyoni mwangu kuwa alikuwa mtu mwenye kiburi asiyekuwa na busara hata kidogo na hakuwa na matumaini ya kubadilika. Hiyo ndiyo sababu singeweza kamwe kumtendea kwa haki au bila ubaguzi. Mungu huwaokoa watu kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo, lakini nilikuwa nikimwekea Ndugu Chen mipaka katika kila njia. Sasa, Mungu alikuwa Amenifunua na kunifanya niweze kuona kiburi na majivuno yangu waziwazi. Nilikuwa nimechukulia mitazamo na imani yangu mwenyewe kama ukweli na kama viwango ambavyo nilitumia kuwahukumu watu—nilikuwa bila busara kabisa. Je, nilikuwa nawatazama na kuwapima wengine kwa kanuni na viwango? Je, njia yangu ya kuwatazama na kuwawekea mipaka watu ilikubaliana na ukweli? Nilikuwa chini kuliko buu. Je, nilikuwa na sifa gani za kuwahukumu na kuwalaani watu wengine? Maneno ya Mungu yanasema: “Watu ambao Mungu huwaokoa ni wale ambao wana tabia potovu kwa njia ya kupotoshwa na Shetani; sio watu safi wasio na dosari hata kidogo, wala sio watu ambao wanaishi katika utupu” (“Uingiaji Katika Maisha ni Muhimu Zaidi Katika Kumwamini Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Bado hatujakamilishwa na bado tuko katika mchakato wa kubadilika taratibu kupitia uzoefu wetu wa kazi ya Mungu. Hata ingawa tunaweza kuonyesha tabia zetu potovu au kutenda makosa fulani tunapotimiza wajibu wetu, almradi tunamwamini Mungu kwa dhati na kuufuatilia ukweli, tutaweza kubadilika. Hata hivyo, sikuwa nawaona wengine kwa mtazamo wa ukuaji. Badala yake, nilikuwa nawawekea wengine mipaka kwa mitazamo yangu mwenyewe na tabia potovu. Kwa kweli nilikuwa mwenye kiburi sana.

Kisha nikasoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Unapaswa kuwatendea washiriki wa familia ya Mungu kulingana na kanuni gani? (Mtendee kila ndugu kwa haki.) Unawatendeaje kwa haki? Kila mtu ana makosa na upungufu mdogo mdogo, pamoja na upekepeke fulani; watu wote wana kujidai, udhaifu, na sehemu ambazo wana upungufu. Unapaswa kuwasaidia kwa moyo wenye upendo, uwe mvumilivu na mstahimilivu, na usiwe mkali sana au kufuatilia kila jambo dogo. Kwa watu ambao ni vijana au ambao hawajamwamini Mungu kwa muda mrefu sana, au ambao wameanza hivi karibuni kutekeleza wajibu wao au walio na maombi fulani maalum, ukiwashika kwa lazima na usiwaachilie, basi huku ndiko kunakojulikana kama kuwa mkali. Unapuuza maovu yanayofanywa na wale viongozi wa uwongo na wapinga Kristo, lakini unapoona mapungufu na makosa madogo katika ndugu zako, unakataa kuwasaidia, badala yake ukichagua kuhangaikia vitu hivyo na kuwahukumu bila wao kujua, na hivyo kuwasababisha watu hata zaidi wawapinge, kuwaacha, na kuwatenga. Hii ni tabia ya aina gani? Huku ni kufanya mambo kulingana na upendeleo wako wa kibinafsi tu, na kutoweza kuwatendea watu kwa haki; hii inaonyesha tabia potovu ya kishetani! Haya ni makosa! Watu wafanyapo mambo, Mungu anatazama; kila ufanyacho na bila kujali unavyofikiria, Yeye huona! Ukitaka kuzifahamu kanuni, basi lazima uelewe ukweli kwanza. Mara tu ukielewa ukweli, unaweza kuelewa mapenzi ya Mungu; usipoelewa ukweli, bila shaka hutaelewa mapenzi ya Mungu. Ukweli unakueleza jinsi ya kuwatendea watu, na mara unapoelewa hili, utajua jinsi ya kuwatendea watu kulingana na mapenzi ya Mungu. Jinsi unavyopaswa kuwatendea wengine imeonyeshwa na kuelezwa wazi katika maneno ya Mungu; mtazamo ambao Mungu huchukua katika kuwatendea binadamu ndio mtazamo ambao watu wanapaswa kuwa nao katika kutendeana wao kwa wao. Je, Mungu humtendeaje kila mmoja? Watu wengine ni wenye kimo kisicho komavu, au ni wachanga, au wamemwamini Mungu kwa muda mfupi tu. Asili na kiini cha watu wengine si kibaya au kiovu; ni kwamba tu ni wajinga au wanaopungukiwa katika ubora wa tabia, au kwamba wamechafuliwa sana na jamii. Hawajaingia katika uhalisi wa ukweli, kwa hivyo ni vigumu kwao kujiepusha kufanya mambo mengine ya kijinga au kufanya vitendo kadhaa vya ujinga. Hata hivyo, kutoka katika mtazamo wa Mungu, mambo kama haya siyo muhimu; Yeye huangalia tu mioyo ya watu. Kama wameazimia kuingia katika uhalisi wa ukweli, wanaelekea katika njia sahihi, na hili ndilo kusudi lao, basi Mungu anawaangalia, kuwangojea, na kuwapa muda na fursa zinazowaruhusu kuingia. Sio kwamba Mungu anawaangusha kwa pigo moja au kuwapiga punde wanapoinua vichwa vyao; Mungu hajawahi kuwatendea watu kwa namna hii. Licha ya hayo, watu wakitendeana kwa namna hiyo, basi hili halionyeshi tabia yao potovu? Hii hasa ndiyo tabia yao potovu. Lazima uangalie jinsi Mungu anavyowatendea watu wasiojua na wapumbavu, jinsi Anavyowatendea wale wasio na kimo komavu, jinsi Anavyochukulia udhihirisho wa kawaida wa tabia potovu ya binadamu, na jinsi Anavyowatendea wale ambao ni waovu. Mungu ana njia mbali mbali za kuwatendea watu tofauti, na pia Ana njia mbali mbali za kusimamia hali nyingi tofauti za watu. Lazima uelewe ukweli wa mambo haya. Mara unapoelewa ukweli huu, unaweza basi kujua jinsi ya kuyapitia” (“Ili Kufikia Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yanaeleza waziwazi kanuni na njia ya jinsi ya kuwatendea watu. Pia yanaeleza kuwa mtazamo wa Mungu kwa wapinga Kristo na watu wabaya umejaa chuki, laana na adhabu. Na kwa wale ambao kimo chao ni kidogo, ambao ni wenye ubora duni wa tabia na wana upotovu na mapungufu ya kila aina, almradi wanamwamini Mungu kweli, wako tayari kuufuatilia ukweli, wanaweza kuukubali ukweli na wanaweza kuutenda ukweli, mtazamo wa Mungu kwao ni ule wa upendo, huruma na wokovu. Kutoka kwa maneno ya Mungu, niliona kwamba Mungu ana kanuni na viwango kuhusu jinsi Anavyomtendea kila mtu. Mungu anahitaji kwamba tuwapende wale ambao Mungu anawapenda na tuwachukie wale ambao Mungu anawachukia. Lazima tuwe wavumilivu na wenye kuwasamehe ndugu ambao wanamwamini Mungu kweli na lazima tuwape nafasi ya kutubu na kubadilika. Hatuwezi tu kuwabomoa kwa mpigo mmoja wanapoonyesha tabia yao potovu, kwa kuwa hii hailingani na kanuni na njia za Mungu za kuwatendea watu, sembuse kuwa mapenzi ya Mungu. Nilianza kufikiria jinsi Ndugu Chen alijichukulia mzigo juu ya wajibu wake, jinsi alivyokuwa na hisia ya uwajibikaji na jinsi alivyoweza kufanya kazi fulani ya vitendo. Sikuwahi kufikiria kikamilifu kuhusu uwezo wake na sifa zake. Badala yake, nilikazia macho upotovu wake na sikuacha, nami nilimhukumu na kumshutumu. Hakika asili yangu ilikuwa yenye uovu!

Kipindi hicho tu, nilifikiria kuhusu kifungu cha maneno ya Mungu: “Mwelekeo na njia ambayo Mungu alishughulikia Adamu na Hawa ni sawa na namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyoonyesha hali ya kuwajali watoto wao binafsi. Ni kama pia namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyopenda, kuangalia, na kutunza watoto wao binafsi wa kiume na kike—halisia, namna ya kuonekana, na kushikika. Badala ya kujiweka Yeye Mwenyewe katika cheo cha juu na cha utukufu, Mungu mwenyewe alitumia ngozi kutengeneza nguo za binadamu. Haijalishi kama koti hili la manyoya lilitumika kufunika uchi wao au wao kujikinga dhidi ya baridi. Kwa ufupi, nguo hii iliyotumika kuufunika mwili wa binadamu ilitengenezwa na Mungu mwenyewe kwa mikono Yake mwenyewe. Badala ya kuitengeneza tu kupitia kwa fikira au kwa mbinu za kimiujiza kama watu wanavyofikiria, Mungu alikuwa amefanya kitu cha halali kwa binadamu ambacho binadamu anafikiria Mungu hawezi na hafai kufanya. Kitu hiki kinaweza kuwa rahisi ambacho baadhi huenda hata wasifikirie kwamba kinastahili kutajwa, lakini kinawaruhusu pia wale wote wanaomfuata Mungu lakini awali walikuwa na mawazo yasiyoeleweka kuhusu Yeye kuweza kupata maono kuhusu ukweli na uzuri Wake, na kuuona uaminifu Wake na asili Yake ya unyenyekevu. Kinawafanya watu wenye kiburi kisicho na kifani wanaofikiria kwamba wako juu na wanao utukufu kuinamisha vichwa vyao kwa aibu mbele ya ukweli na unyenyekevu wa Mungu” (“Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila moja la maneno ya Mungu liliupa moyo wangu furaha. Niliweza kuhisi wasiwasi wa Mungu na huruma kwa watu na kwamba utunzaji Wake na wasiwasi wake vilikuwa vya kweli. Wakati Adamu na Hawa hawakutii amri ya Mungu na kula tunda kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya, ingawa Mungu alijificha kutoka kwao na kuwatimua kutoka katika Bustani ya Edeni, Mungu bado Aliwahurumia na Yeye binafsi Aliwafanyia mavazi kutoka kwa ngozi ili wavae. Hakika Mungu ni mzuri, na tabia Yake ni ya kupendeza na nzuri kweli. Mtazamo Wake kwa watu wapotovu na watu wanaofanya makosa ni ile ya ustahimilivu. Kwa sababu ya huruma Yake, Anaweza kusamehe ujinga, udhaifu na kutokomaa kwa mwanadamu. Yeye humpa mwanadamu muda na nafasi ya kutubu. Wakati Anasubiri, Yeye huendelea kumpa mwanadamu ukweli ili mwanadamu aingie ndani. Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu ni halisi sana. Mungu ni mwaminifu na upendo Wake kwa mwanadamu ni wa kweli, sio wa uwongo au wa kuiga hata kidogo, lakini unaogusika na kuonekana. Wakati nilipofikiria kuhusu jambo hili, machozi yalinijaa machoni mwangu na kuanza kutiririka. Nilianza kutafakari juu ya uzoefu wangu wote. Katika kazi ya kuwabadilisha viongozi na wafanyakazi, kwa kuwa sikuwa nimeingia katika kanuni, nilifanya mambo fulani ambayo yaliingilia kati na kuvuruga kazi ya kanisa. Hata hivyo, Mungu hakuniondoa au kuniadhibu. Badala yake, Alitumia ripoti ambayo ndugu zangu waliandika ili kunifanya nitafakari kujihusu mimi mwenyewe, nitubu na nibadilike ili niweze kutekeleza wajibu wangu kulingana na kanuni. Wakati nilikuwa hasi na dhaifu, Mungu alitumia maneno Yake kunifariji na kunisaidia. Pia Aliwagusa akina ndugu ambao walikuwa kando nami ili kuwasiliana mapenzi Yake nami, ambalo lilinitia nguvu sana. Wakati nilipofanya dhambi au wakati nilifanya makosa katika kazi yangu, nilipokuwa na hali ya kutokuelewana na nilipokuwa mwangalifu dhidi ya Mungu na nilipokuwa hasi na mzembe katika kazi yangu, Mungu alinielimisha na kunielekeza kwa maneno Yake ili niweze kuelewa mapenzi Yake, na niliona upendo Wake na wokovu Wake. Kisha niliweza kuacha uzembe na kutoelewana…. Je, Mungu hakuwawa Ameshafanya hili juu yangu muda mrefu uliopita? Wakati nilipouona upendo wa Mungu usio na kikomo kwangu, moyo wangu mkaidi na wenye ganzi uliyeyushwa na upendo wa dhati wa Mungu. Nilisema sala ya toba kwa Mungu, “Ee Mungu! Nimekukaidi na kukukataa Wewe mara kwa mara. Hata hivyo, bado Unanitendea kwa upendo na uvumilivu na Unaonyesha ufahamu kwa udhaifu wangu. Mara kwa mara, Ulinitumia maneno ili kunielimisha, kuniongoza, kunisaidia na kunipa lishe. Umeniongoza hatua kwa hatua hadi leo. Sistahili Wewe kutumia utunzaji na juhudi nyingi sana katika kuniokoa. Ee Mungu! Upendo Wako kwangu hauelezeki. Unapongoja kwa uvumilivu nibadilike, Unanipa pia fursa za kutubu. Ninachotamani ni kwamba, kuanzia sasa na kuendelea, nitatenda kulingana na mapenzi na matakwa Yako. Natamani kutegemea kanuni za ukweli ninapomtendea kila ndugu anayekuamini kwa kweli.”

Kisha, nilisoma kifungu kingine katika mahubiri ambacho kinasema: “Kwa mfano, wewe ni kiongozi na unapaswa kuwawajibikia akina ndugu. Tuseme kuna ndugu au dada ambaye haufuatilii ukweli na hafuati njia sahihi. Unapaswa kufanya nini? Lazima umsaidie mtu huyu. Msaada huu ni pamoja na kumpogoa na kumshughulikia. Ni pamoja na kudhibiti na kukosoa. Hii ndiyo njia ya kusaidia. Yote haya ni upendo. Je, ni lazimakumrairai au kutumia sauti ya ushauri? Si lazima. Ikiwa kuna haja ya kumpogoa na kumshughulikia, fanya hivyo. Funua kile kinachopaswa kufunuliwa. Hii ni kwa sababu wewe ni kiongozi na mfanyakazi. Ikiwa hutasaidia, ni nani atakayesaidia? Huu ndio wajibu unaopaswa kutekeleza” (“Jinsi Mtu Anavyopaswa Kupitia Kazi ya Mungu ili Apate Wokovu na Akamilishwe” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha VI). Kutoka katika ushirika huu, nilijifunza kwamba kiongozi au mfanyakazi ambaye kwa hakika ana uhakika wa ukweli huwatendea ndugu zake kwa kanuni. Anajua jukumu lake ni nini na agizo lake ni nini. Anaweza kutegemea kanuni za ukweli kuwashughulikia watu kulingana na asili na kiini chao. Anaweza kuwasaidia watu kwa vitendo kulingana na upotovu na upungufu wao. Anajua ni wakati gani anapopaswa kuwasaidia kwa moyo wenye upendo, ni wakati gani wa kuwashughulikia na kuwapogoa kwa ukali na ni wakati gani wa kuwakemea. Anaweza kutenda ipasavyo, ana kanuni, na hatawatendea ndugu ambao wameonyesha upotovu kama maadui kiholela. Nilianza kufikiria tena jinsi ninavyomtendea Ndugu Chen. Wakati nilipomwona akifichua tabia yake potovu, sikumsaidia ama kumsaidia kwa njia ya vitendo. Sikuichangua asili yake ya kiburi ili kumsaidia ajue kiini cha asili yake au kumsaidia aone wazi matokeo yenye hatari ikiwa tabia yake ya kiburi haingebadilika. Badala yake, nilihukumu, nikamtenga na kumshutumu kiholela. Hata nilieneza chuki yangu juu yake bila yeye kujua. Sikuonyesha uvumilivu au ustahimilivu wowote, sembuse kumtendea kwa moyo wenye upendo. Wakati huu, niliona kwamba sikuwa na kanuni za ukweli katika jinsi nilivyokuwa nikimtendea ndugu huyu na sikuwa nikitimiza wajibu wangu na jukumu langu. Nilielewa mapenzi ya Mungu na nikapata njia ya kutenda. Kwa hivyo, nilienda na kumtafuta Ndugu Chen. Nilizitaja shida zake na nikatoa msaada na usaidizi wangu. Wakati huo huo, nilimshughulikia na kumpogoa. Niliichangua mitazamo yake isiyo sahihi kuhusu ufuatiliaji na njia mbaya aliyokuwa akiifuata. Pia nilishiriki naye juu ya kiini kitakatifu cha Mungu na tabia Yake isiyostahimili makosa.… Namshukuru Mungu kwa mwongozo Wake. Kupitia kwa mawasiliano yangu na yeye, Ndugu Chen alipata ufahamu fulani wa hali yake ya kiburi na upotovu ambao alikuwa ameonyesha. Alisema, “Ingawa najua kuwa nina kiburi sana, mara nyingi mimi hukiri hayo kwa maneno tu. Sijawahi kuichangua asili yangu ya kiburi kwa kina, sembuse kuichukia kwa kweli. Ila tu wewe kunionyesha mambo haya leo ndiyo sasa nimegundua kuwa hali yangu mwenyewe ni mbaya sana na ni hatari. Mungu hayuko ndani ya moyo wangu na simheshimu mtu yeyote. Siku zote huwa ninahisi kuwa nina uwezo. Hasa wakati kazi inaleta matokeo, mimi siibi tu utukufu wa Mungu, nina kiburi na majivuno hata zaidi kwa sababu nahisi kuwa mimi ni mtu wa ajabu. Niko kwenye njia ya mpinga Kristo, nami nafanya matendo mabaya na kumpinga Mungu. Leo, onyo lako na msaada wako vimenipa nafasi ya kutafakari kwa binafsi, na kutubu na kubadilika.…” Nilipomsikia akisema hivi, liliugusa moyo wangu sana. Nilihisi kwa undani kwamba sikuwa nimetimiza wajibu wangu vizuri na kwamba sikuwa na moyo wa huruma. Sikuwa nimempa ndugu yangu msaada au usaidizi. Badala yake, nilikuwa nimechukua fursa ya upotovu wake na nikamhukumu. Ilikuwa ni hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu kulikoniokoa, kukanifanya nione wazi kuwa nilikuwa na kiburi na asili mbaya na nikibadilisha maoni yangu ya upuuzi. Nilisoma katika kifungu cha mahubiri ya Aliye juu: “Inaweza kusemwa kwamba wale watu wote ambao hakika wanapenda ukweli na ambao wana nia ya kufuatilia kukamilishwa wana tabia ya kiburi na ya kujidai. Almradi wanaweza kuukubali ukweli na kukubali kupogolwea na kushughulikiwa, na wanaweza kuutii ukweli kabisa bila kujali hali, basi watu kama hawa wanaweza kupata wokovu na kukamilishwa. Kwa kweli, hakuna watu ambao kwa hakika ni wenye ubora mzuri wa tabia na ambao wana nia kwa kweli wasio na kiburi. Huu ni ukweli. Lazima watu wa Mungu wateule waweze kutofautisha. Hawapaswi kumwekea mtu mipaka kuwa mtu asiye mzuri na mtu asiyeweza kuokolewa na kukamilishwa kwa sababu tu yeye ni wenye kiburi na mwenye kujidai kupindukia. Haijalishi mtu huyo ni mwenye kiburi kupindukia kiasi gani, almradi yeye ni mwenye ubora mzuri wa tabia na anayeweza kuufuatilia ukweli, yeye ni mtu Mungu anataka kumkamilisha. Vigezo vya Mungu kuwakamilisha watu hasa ni kwamba mtu ni mtu mzuri, ni mwenye ubora mzuri wa tabia na anayeufuatilia ukweli. Ikiwa ubora wa tabia ya mtu ni duni sana na hawezi kuuelewa ukweli kila wakati, basi hata kama tabia yake ni upole sana na sio mwenye kiburi hata kidogo, hana maana na hafai kukamilishwa. Katika hoja hii, mtu anahitaji kuelewa mapenzi ya Mungu. Ikiwa ubora wa tabia ya mtu ni mzuri, na ana nia na si mwenye majivuno na mwenye kujidai, basi hakika hicho ni kisingizio au unafiki, kwa kuwa hakuna mtu kama huyo. Lazima mtu ajue kwamba binadamu wapotovu wana kiburi na kwa asili ni wenye kujidai. Huu ni ukweli usiopingika” (“Ni watu tu ambao Wanakubali na Kuitii Hukumu na Kuadibu kwa Mungu kwa Kweli ndio Wanaoufuata Ukweli” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha). Ushirika huu ulinisaidia kuelewa wazi jinsi ninavyopaswa kuwashughulikia na watu ambao wana tabia ya majivuno. Nilijifunza kwamba inawezekana kwa wale ambao wana tabia ya kiburi kubadilika, na jambo la msingi ni ikiwa wanaweza kuufuatilia ukweli na kuukubali ukweli au la. Ikiwa wanaweza kuukubali ukweli, kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu na kukubali kushughulikiwa na kupogolewa, wanaweza kubadilika kabisa na kukamilishwa na Mungu. Sasa nilipoiangalia tena hali ya Ndugu Chen, niligundua kuwa kwa kuwa alikuwa mchanga, alikuwa hajamwamini Mungu kwa muda mrefu sana na alikuwa hajapitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, kuonyesha kwake tabia yenye kiburi na kujidai kulikuwa kawaida. Tumepotoshwa na Shetani na tunadhibitiwa na tabia zetu zenye kiburi, kwa hivyo tunapenda kutafuta umaarufu na kujionyesha. Hii ni tabia ya kawaida ya binadamu wapotovu. Je, mimi pia sijaonyesha kiburi na majivuno mara kwa mara? Kwa nini nahisi kuwa mimi mwenyewe naweza kubadilika lakini yeye hawezi? Kwa nini viwango ambavyo nimejiwekea ni vya chini kuliko viwango ambavyo nimemwekea? Ji, hii haimaanishi kuwa mimi ni mwenye kiburi zaidi kumliko yeye? Si njia ya haki ninavyomtendea. Nilipogundua hili, niliweza kuacha upendeleo na maoni yangu mabaya ambayo nilikuwa nayo dhidi ya Ndugu Chen. Nilihisi kwamba kiini cha asili yake hakikuwa kibaya. Alikuwa na azimio la kuufuatilia ukweli, na ilikuwa tu kwamba tabia yake yenye kiburi ilikuwa kali zaidi, nami nilielewa kwamba nilipaswa kumsaidia kwa moyo wa upendo na kutimiza jukumu langu.

Namshukuru Mungu kwa nuru na mwongozo Wake. Kutokana na tukio hili, nilijifunza kuwa wale ambao wanaishi ndani ya tabia zao potovu na hawawatendei wengine kulingana na kanuni za maneno ya Mungu na wasioweza kuchukua mtazamo sahihi kuelekea uwezo na udhaifu wa watu wengine, hawawezi kuwatendea wengine kwa njia ya haki. Hawatawaletea ndugu zao madhara ya kimwili na kiakili tu, pia watachelewesha kuingia kwao katika maisha. Wanaweza hata kuwapa wengine wakati mgumu au kuwaadhibu, wakichukua njia ya mpinga Kristo. Namshukuru Mungu kwa kazi ya hukumu na kuadibu ambayo Aliifanya kwangu wakati huu. Wakati nilikuwa nikiishi katika tabia yangu ya uasi na sikuweza kumtendea ndugu yangu kulingana na kanuni za ukweli, Mungu Alitumia hukumu na kuadibu Kwake mara moja ili Aniokoe kwa wakati unaofaa na kunifanya nitambue tabia yangu mwenyewe yenye kiburi na yenye uovu. Nilipomrudia Mungu, nikajiweka kando na kuutafuta ukweli, nilipata mwongozo na uongozi wa Mungu—nilielewa kutoka kwa maneno ya Mungu jinsi ya kuwashughulikai watu kwa kanuni. Wakati nilipomtendea Ndugu Chen kulingana na maneno ya Mungu, nilipata amani ya kiroho na utulivu kwa hakika. Aidha, niliweza kugundua na kujifunza kutoka kwa uwezo wa ndugu huyo ili kujaliza upungufu wangu mwenyewe. Nilionja utamu wa kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo. Ilikuwa ni kazi na mwongozo wa Mungu ambavyo vilinisababisha kuuelewa ukweli fulani na kupata ufahamu fulani kuhusu upotovu na upungufu wangu mwenyewe. Wakati huo huo, nilihisi kweli kwamba kuwashughulikia watu wengine kulingana na kanuni za ukweli ni muhimu sana. Natamani tu kuendelea kuliweka neno la Mungu katika vitendo wakati ninatimiza wajibu wangu, na kumtendea kila mmoja wa ndugu zangu kulingana na ukweli wa maneno ya Mungu.

Iliyotangulia:Kuulewa Moyo wa Mungu Kunaweza Kuondoa Kuelewa Visivyo

Inayofuata:Kujijua kwa Hakika kwa Kuuelewa Ukweli Tu

Maudhui Yanayohusiana

 • Ufahamu Kiasi Kuhusu Kuokolewa

  Baada ya kusoma hili, nilihisi kama kwamba nilikuwa nikiamka kutoka ndotoni. Kwa hiyo, kuokolewa na Mungu hakukuwa rahisi kama nilivyokuwa nimefikiri hata hivyo; inategemea watu kupitia kazi na maneno ya Mungu kila hatua ya njia, kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu, ushughulikiaji na upogoaji, pamoja na kupitia machungu ya kila aina ya maudhi na kero. Ili waweze kufikia ufahamu halisi wa tabia zao potovu na hatua kwa hatua kujiondolea upotovu, na hatimaye waweze kutegemea maneno ya Mungu na kutegemea ukweli kumshinda Shetani na kuvuka mipaka ya nguvu za giza katika kila aina ya mazingira. Kufikia matokeo haya tu ndio kuokolewa na Mungu kwa kweli.

 • Mateso na Majaribio—Baraka za Kufadhiliwa

  Wang Gang Mkoa wa Shandong Mimi ni mkulima na kwa sababu familia yangu ni maskini, daima ilinibidi nisafiri kwenda kote kutafuta kazi za muda ili kup…

 • Sababu ya Kweli ya Kazi Isiyofaa

  Xinyi Mji wa Xi’an, Mkoa wa Shaanxi Katika ziara zangu za karibuni kwa makanisa, mara nyingi niliwasikia viongozi na wafanyakazi wakisema kwamba watu …

 • Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri

  Xiaoxiao Jijini Xuzhou, Mkoani Jiangsu Kwa sababu ya mahitaji ya kazi ya kanisa, nilihamishwa mpaka mahali pengine ili kutimiza wajibu wangu. Wakati …